Wednesday 24 December 2008

Ferguson: 'Sinunui Mchezaji Januari!'

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema hawana haja ya kununua Mchezaji yeyote wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa Januari 2009.
Msimu ulipoanza, Manchester United ilinunua Mchezaji mmoja tu ambae ni Dimitar Berbatov waliemnunua kutoka Tottenham kwa Pauni Milioni 30 mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.
Ferguson ametamka: 'Tulichukuwa Wachezaji 23 kwenda Japan na tumetwaa Ubingwa wa Dunia! Sina wasiwasi kumchezesha yeyote kati ya hao wakati wowote!'

Mourinho anatamani kurudi LIGI KUU ENGLAND!

Aliekuwa Meneja machachari na mwenye vituko wa Chelsea, Jose Mourinho, amekiri ana hamu sana ya kurudi England ili aongoze Klabu ya LIGI KUU.
Mourinho kwa sasa yuko Italia na Timu ya Inter Milan ambayo ndio kinara wa Ligi huko iitwayo Serie A na ambao watakutana na Mabingwa Watetezi wa Ulaya Man U kwenye Raundi ya Mtoano ya UEFA Champions League mwezi Februari mwakani.
Akihojiwa, Mourinho: 'Sifichi. Naipenda LIGI KUU England. Lazima siku moja nirudi huko!'

Scolari ashangazwa na Kadi Nyekundu aliyopewa Nahodha wake John Terry!!

Meneja wa Chelsea Luis Felipe Scolari amesema ameshangazwa na Mwamuzi Phil Dowd kumpa John Terry Kadi Nyekundu.
Terry alipewa kadi hiyo siku ya Jumatatu usiku wakati Chelsea ilipocheza na Everton na Terry kumchezea vibaya Leon Osman kwenye dakika ya 35.
Mara baada ya mechi hiyo Scolari aligoma kufanya mahojiano na Waandishi wa Habari na vilevile alikataza mtu yeyote wa Klabu kuhojiwa.

Fabregas kuepuka kisu!!

Nahodha wa Arsenal Cesc Fabregas alieumizwa goti kwenye mechi kati ya Arsenal na Liverpool amethibitisha kuwa Daktari Bingwa wa mjini Barcelona, Spain ameridhia asifanyiwe upasuaji na badala yake apumzike tu ingawa muda unaokadiriwa goti lake kupona ni miezi minne.

Tuesday 23 December 2008

IMETHIBITISHWA: Fabregas nje miezi minne!

Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, amethibitisha kuwa Nahodha wake Cesc Fabregas atakuwa nje ya uwanja hadi mwezi Aprili mwakani baada ya Madaktari kugundua ameumia vibaya ndani ya goti lake.

Cesc Fabregas hatihati kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Kiungo mahiri wa Arsenal ambae pia ndie Nahodha, Cesc Fabregas, huenda akawa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuumia goti kwenye mechi ya Arsenal na Liverpool.
Fagregas aliumia baada ya kupigana kibuyu na Xavi Alonso wa Liverpool katika kipindi cha kwanza na kutolewa nje ya uwanja hapohapo na nafasi yake kuchukuliwa na Vassiriki Diaby.
Hatma yake itajulikana leo baada ya kuchunguzwa na wataalam.

LIGI KUU ENGLAND inaingia patamu!

LIGI KUU ENGLAND sasa inaingia kwenye mechi ngumu na za mfululizo zitakazochezwa kipindi cha Sikukuu ya Krismas siku ya Boxing Day tarehe 26 Desemba 2008 na kufuatiwa na mechi nyingine baada ya mapumziko ya siku moja tu kwa baadhi ya timu.
Kihistoria kipindi hiki ndio hutoa mwanga Timu zipi zitapata mafanikio na zipi zitakumbwa na vita ya kupuruchuka kushushwa daraja.

Kimsimamo, kwa Timu za juu hali iko hivi:

-Liverpool: mechi 18 pointi 39

-Chelsea: mechi 18 pointi 38

-Aston Villa: mechi 18 pointi 34

-Man U: mechi 16 pointi 32

-Arsenal: mechi 18 pointi 31

Ijumaa, 26 Decemba 2008
[saa 9 dak 45 mchana]


Stoke v Man U

[saa 10 jioni]

Liverpool v Bolton
Portsmouth v West Ham
Chelsea v West Brom
Tottenham v Fulham

[saa 12 jioni]

Man City v Hull
Middlesbrough v Everton
Sunderland v Blackburn
Wigan v Newcastle

[saa 2 na robo usiku]

Aston Villa v Arsenal

Jumapili, 28 Decemba 2008
[saa 9 mchana]

Newcastle v Liverpool

[saa 11 jioni]

Arsenal v Portsmouth
Bolton v Wigan
Everton v Sunderland
Fulham v Chelsea
West Brom v Tottenham
West Ham v Stoke
[saa 1 na robo usiku]
Blackburn v Man City

Jumatatu, 29 Decemba 2008
[saa 5 usiku]

Man U v Middlesbrough

Jumanne, 30 Decemba 2008
[saa 5 usiku]

Hull v Aston Villa


LIGI KUU ENGLAND: Nahodha John Terry ala NYEKUNDU!

Everton 0 Chelsea 0

Nahodha wa Chelsea John Terry alitandikwa KADI NYEKUNDU na Refa Phil Dowd baada ya kumchezea rafu mbaya Winga wa Everton Leon Osman kwenye dakika ya 36 ya mechi lakini Chelsea wakajikongoja na kupata suluhu.

Monday 22 December 2008

LIGI KUU ENGLAND: Msimu huu Mameneja 6 washabwagwa!! Nani atafuata?

LIGI KUU ENGLAND inasifika ndio ligi bora duniani lakini imeshaanza kurithi mwenendo mbaya ambao zamani ulikuwa ukionekana kwenye ligi za nchi za Italy, Spain na hasa nchi za Marekani ya Kusini tu!
Mwendo huu mbovu ambao umeleta wasiwasi mkubwa kwa baadhi ya wadau wa soka la England ni ile tabia ya kuwatimua au kulazimisha Mameneja wa Klabu za Soka kujiuzulu.
Tangu msimu huu uanze hapo mwezi Agosti tayari Mameneja kadhaa wa Klabu za LIGI KUU ENGLAND hawana kazi!
Ukichukulia kwamba LIGI KUU ina Klabu 20, hivyo wapo Mameneja 20, basi hiyo idadi ni kubwa mno na inatisha na kuleta mtikiso mkubwa sana ndani ya soka ya Uingereza.

Mpaka sasa mabadiliko ya Mameneja ni:

-Paul Ince: Blackburn Rovers-aliondolewa Desemba 16.

-Roy Keane: Sunderland-aliondoka 4 Desemba.

-Harry Redknapp: Portsmouth-yeye alihamia Tottenham 25 Oktoba.

-Juande Ramos: Tottenham-kafukuzwa 25 Oktoba.

-Kevin Keagan: Newcastle-mwenyewe alibwaga manyanga 4 Septemba.

-Alan Curbishley: West Ham-aliachishwa 3 Septemba.

Sasa, kwenye anga za soka, upo mdahalo mkubwa sana wa nani ataingia kwenye listi hiyo?
Wanaotarajiwa kujumuika kwenye listi hiyo ni pamoja na, amini usiamini, Luis Felipe Scolari, Meneja Mbrazil wa Klabu ya Chelsea.
Yeye anahusishwa sana hasa kwa dhana kwamba Chelsea haichezi soka la kuvutia na matokeo mengi ya mechi zake ni kama tombola kitu ambacho kinahisiwa kumkera mmiliki wa Klabu hiyo, tajiri aliekubuhu toka Urusi Roman Abramovich, ambae amwekeza mabilioni ya pesa.
Mwingine anaeingizwa kwenye listi hii ni Mark Hughes wa Manchester City.
Huyu alitolewa timu ya Blackburn Rovers na kuingizwa Manchester City na aliekuwa Waziri Mkuu wa Thailand Shinawatra Thanksin ambae alikuwa ndie mmiliki wa Klabu hiyo.
Wakati Mark Hughes anatua tu hapo Manchester City, Shinawatra, pengine kufuatia matatizo yake ya kisiasa huko kwao Thailand ambako alikimbia baada ya kuandamwa na kashfa za rushwa na kuburuzwa Mahakamani, aliamua kuiuza Klabu hiyo kwa Koo ya Kifalme tajiri sana kutoka Abu Dhabi, Falme ya Nchi za Kiarabu.
Matajiri hao wa Kiarabu, mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu, siku hiyo hiyo walipotangazwa kuwa ndio wamiliki wapya wa Manchester City na ikiwa ndio siku ya mwisho kwa dirisha la uhamisho la kuhama Wachezaji kufungwa, walikufuru kwa kumnyotoa Staa toka Brazil Robinho aliekuwa akichezea Real Madrid kwa dau la Pauni Milioni 32 ambalo ndio rekodi ya bei ghali kwa kununuliwa Mchezaji England na kumleta Manchester City!
Leo, miezi minne baadae, Manchester City wako nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi wakiwa timu ya 3 toka chini na hilo ndio eneo la timu zinazoporomoshwa daraja mwishoni mwa msimu!
Hilo ndio janga linalomkabili Mark Hughes wakati akiwa Meneja wa Klabu inayokejeliwa kuwa ndio tajiri duniani!
England kuna Chama cha Mameneja wa Ligi kiitwacho LEAGUE MANAGERS ASSOCIATION [LMA] na siku zote kimepinga maamuzi ya kuwatimua Mameneja bila ya kupewa nafasi, muda na mtaji wa kuongoza timu.
LMA siku zote imekuwa ikitoa mifano ya Sir Alex Ferguson wa Manchester United na Arsene Wenger wa Arsenal kwamba ukimpa Meneja nafasi, muda na mtaji basi lazima Klabu itakuwa na mafanikio!
Sir Alex Ferguson yuko Manchester United tangu tarehe 6 Novemba 1986 na katika miaka 22 aliyokuwa hapo ameshaweka historia ya kuwa Meneja Bora katika historia ya soka Uingereza.
Yeye ameshatwaa Makombe, Ubingwa na Tuzo ambazo listi yake ni ndefu kupita urefu wa makala hii!
Siku chache zilizopita, Sir Alex Ferguson ameiwezesha Manchester United kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Duniani hili likiwa Kombe lake kubwa la tatu mwaka huu baada ya kuutwaa Ubingwa wa LIGI KUU ENGLAND na Kombe la Klabu Bingwa Ulaya mwezi Mei.
Arsene Wenger yuko Arsenal kwa miaka 12 tangu alipojiunga tarehe 1 Oktoba 1996 na yeye ndie mwenye sifa ya kuwa Meneja Bora na mwenye mafanikio bora katika historia ya miaka 100 ya Klabu ya Arsenal, klabu iliyoanzishwa mwaka 1886!
Katika LIGI KUU ENGLAND, Arsene Wenger ndie mwenye rekodi pekee ya kuwa Meneja pekee ambae Klabu yake haikufungwa msimu mzima!
Huo ulikuwa msimu wa mwaka 2004!
Sasa, fanananisha na Paul Ince aliepewa madaraka Mwezi Agosti mwaka huu na wakati anaingia tu hapo Klabuni wamiliki wanauza Wachezaji bora wa timu na hapewi mtaji wala Mchezaji yeyote mpya!
Baada ya Mechi 17 za LIGI KUU, Paul Ince akiwa madarakani na kushinda mechi 3 tu, anatimuliwa!
Jambo hili limewakera wengi na Sir Alex Ferguson ashatamka: 'Kwa sasa ni vigumu kwa Mameneja wapya! Klabu zinatawaliwa na Wamiliki na Bodi zenye uroho wa pesa tu! Klabu sasa zimekuwa si mali ya Mashabiki na wapenzi-ni mali za mabwanyenye waroho wa utajiri wasiojua utu hata chembe! Inasikitisha sana!'
Wenger alinena: 'Ni upumbavu! Huwezi kumpa mtu miezi miwili ukategemea maajabu! Hii si soka sasa, hii ni kampuni za watu wenye pesa wasiojua soka!'
Inasikitisha na inaondoa ile ladha ya ushindani ndani ya kandanda!
MABINGWA WA ENGLAND, MABINGWA WA ULAYA na sasa MABINGWA WA DUNIA: Hata Sepp Blatter wa FIFA arukaruka kwa furaha!!!
Baada ya kukabidhiwa Kombe lao na kutawazwa rasmi kuwa wao ndio MABINGWA WA DUNIA, Mabingwa wa England ambao pia ndio Mabingwa wa Ulaya, Manchester United, wakiongozwa na Nahodha wa mechi hiyo, Beki Rio Ferdinand alieshikilia Kombe hilo, waliimba, kupiga kelele, vifijo, nderemo na rapu za kila lugha maana kundi la Wachezaji wa sasa wa Man U wanatoka kila kona ya Dunia!!
Hata Rais wa FIFA Sepp Blatter aliingia uwanjani kwa furaha [pichani juu] maana NI KWELI MAN U NI TIMU YA DUNIA!
Hebu tizama baadhi tu ya Wachezaji: Park ni Mkorea, Vidic anatoka Serbia, Evra ni Mfaransa, Ronaldo na Nani ni Wareno, na ingawa Anderson na Rafael wanatoka Brazil, hawa wawili wanaweza kuongea Kireno pamoja na akina Ronaldo na Nani!
Yupo Tevez toka Argentina, Berbatov wa Bulgaria na usiwasahau Waingereza wenyewe akina Rio, Neville, Carrick, Rooney, Scholes wakisaidiwa na Wajomba zao toka Ireland O'Shea na Evans, na Giggs kutoka Wales!
Alikuwepo chipukizi Danny Welbeck ambae ingawa Mwingereza asili yake ni Ghana!
Na, yupo Manucho toka Angola! Huyu nae anaweza kuteta Kireno na kundi la Ronaldo!
Aaah, yupo Kipa stadi toka Uholanzi Edwin van der Sar, akisaidiwa na Tomasz Kuszczak toka Poland na Chipukizi Ben Amos toka Uingereza!
Juu ya wote, wapo viongozi na hao ni Sir Alex Ferguson anaetoka Scotland na Sir Bobby Charlton ambae ni Mwingereza halisi!
Mbali ya wote, ukiacha kundi la Mashabiki wachache waliotoka Uingereza kuja kuishangilia Man U, ZAIDI YA ASILIMIA 90 YA WATAZAMAJI HAPO UWANJANI YOKOHAMA, JAPAN WALIOKUWA WAKIISHANGILIA MANCHESTER UNITED WALIKUWA NI WAJAPANI HALISI!
Wakati Rooney azawadiwa gari huko Japan, Mashabiki wa Quito walia huko Ecuador!!

Wakati Wayne Rooney, nyota wa Mabingwa wapya wa Dunia Manchester United, akizawadiwa gari mpya aina ya Toyota na kukabidhiwa UFUNGUO MKUBWA WA DHAHABU baada ya kuiwezesha timu yake kunyakua Kombe la Klabu Bingwa Duniani huko Yokohama, Japan baada ya kuiua Liga de Quito kwa bao 1-0, Mashabiki wa Quito waliangua vilio waziwazi huko kwao walipokuwa wakiangalia pambano hilo moja kwa moja toka kwenye TV kubwa zilizowekwa hadharani kwenye mitaa maarufu huko nchini kwao Ecuador!!
Rooney ndie aliechaguliwa Mchezaji Bora wa mechi ya Fainali na pia Mchezaji Bora wa Mashindano hayo yote na vilevile Mfungaji Bora na hivyo kushinda Mpira wa Dhahabu.
Cristiano Ronaldo alizawadiwa Mpira wa Fedha.
Wayne Rooney alifunga jumla ya mabao matatu kwenye Mashindano hayo mawili yakiwa kwenye Nusu Fainali dhidi ya Gamba Osaka ya Japan mechi ambayo Man U walishinda 5-3.

Sunday 21 December 2008

MAN U NI MABINGWA WA DUNIA! Rooney awapa ushindi!!

Mabingwa wa England na Ulaya, Manchester United, wamejiongezea taji lingine na sasa ni Klabu Bingwa Duniani baada ya kuipachika Liga de Quito ya Ecuador, Mabingwa wa Marekani Kusini, bao 1-0 kwa bao tamu la Wayne Rooney katika mechi ya Fainali ya Klabu Bingwa Duniani iliyochezwa Yokohama, Japan.
Wakiwa wametawala kipindi chote cha kwanza na kukosa mabao mengi, Manchester United walipata pigo pale Beki wao Nemanja Vidic alipotolewa nje kwa Kadi Nyekundu dakika ya 49 ya mchezo baada ya kumpiga kipepsi Mchezaji wa Quito Claudio Bieler.
Ikabidi Man U wamtoe Fowadi Carlos Tevez na kumwingiza Mlinzi Johnny Evans kuziba pengo la Vidic.
Hata hivyo pengo la kucheza watu 10 halikuonekana kwani Man U waliendelea kutawala na kushambulia.
Ilipofika dakika ya 73, kazi nzuri ya Cristiano Ronaldo ilimkuta Wayne Roonel aliefunga bao safi la ushindi.
Meneja Sir Alex Ferguson alikipongeza kikosi chake kwa kucheza kitimu na juhudi hasa walipokuwa 10 tu.
Nae Mchezaji aliewapa Kombe, Wayne Rooney, alietangazwa ndie Mchezaji Bora wa Mashindano, alijigamba: 'Sisi ndio bora duniani! Ushindi huu ni muhimu kwa klabu!'

LIGI KUU ENGLAND: Arsenal 1 Liverpool 1

Vinara wa LIGI KUU ya England, Liverpool walilazimisha sare ya 1-1 na Arsenal katika mechi iliyochezwa nyumbani kwa Arsenal uwanja wa Emirates.
Arsenal walipata bao lao kwenye dakika ya 24 baada ya Robin Van Persie kufunga bao la kifundi sana baada ya kupokea pasi safi toka kwa Samir Nasri.
Liverpool, wakicheza bila ya kuwa na Meneja wao Rafa Benitez aliefanyiwa operesheni kuondolewa vijiwe kwenye figo, walisawazisha kwa bao zuri pia kupitia Robbie Keane aliefumua shuti kali dakika ya 42.
Mshambuliaji nyota wa Arsenal Emmanuel Adebayor alipewa Kadi Nyekundu dakika ya 62 baada ya kupata Kadi 2 za Njano.

Matokeo mechi nyingine za LIGI KUU:

Newcastle 2 Tottenham 1

West Brom 2 Manchester City 1

MECHI INAYOFUATA: Jumatatu, 22 Desemba 2008: Everton v Chelsea

Endapo Chelsea ataifunga Everton kwenye mechi hii, basi Chelsea atachukua uongozi wa LIGI KUU.

Mpaka sasa msimamo kwa Timu 5 za juu ni kama ufuatavywo:

-Liverpool: mechi 18 pointi 39

-Chelsea: mechi 17 pointi 37

-Aston Villa: mechi 18 pointi 34

-Manchester United: mechi 16 pointi 32

-Arsenal: mechi 18 pointi 31
KLABU BINGWA DUNIANI: Leo Fainali!!!

Liqa de Quito v Manchester United

Leo saa 7 na nusu mchana saa za kibongo, Mabingwa wa Ulaya Manchester United watakutana na Mabingwa wa Marekani ya Kusini Liga de Quito, klabu kutoka Ecuador, katika Fainali ya FIFA CLUB WORLD CUP mechi itakayochezwa Yokohama International Stadium mjini Yokohama huko Japan.
Manchester United iliwahi kuchukua Kombe linalofanana na hili mwaka 1999 pale ilipoifunga Palmeiras ya Brazil iliyokuwa ikiongozwa na Meneja wa sasa wa Chelsea, Luis Felipe Scolari, kwa bao 1-0.
Wakati huo mechi zilikuwa zinashindaniwa na Klabu mbili tu, moja ikiwa Bingwa wa Ulaya na nyingine Bingwa wa Marekani ya Kusini.
Siku hizi mfumo wa Klabu Bingwa Duniani umebadilika na kila Bara la Dunia linawakilishwa na Bingwa wake.
Safari hii, Afrika iliwakilishwa na Al Ahly ya Misri.
Kocha wa Liga de Quito, Edgardo Bauza amesema mechi hii itakuwa ngumu sana lakini watacheza kufa na kupona.
Nae Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson amesema Quito wanacheza kandanda la aina ile ile ya Timu za Marekani ya Kusini na hivyo ni timu ngumu.
Nae Mchezaji Bora wa Ulaya, Cristiano Ronaldo, ametamka; 'Hakika si mechi rahisi lakini nataka kushinda kwa ajili ya timu yangu na mashabiki wa England. Hii itatupa morali tena kushinda Ligi Kuu na Klabu Bingwa Ulaya!'
LIGI KUU ENGLAND: Meneja Sam Allardyce aanza vyema utawala Blackburn!!

Meneja mpya wa Blackburn Sam Allardyce ameanza vyema utawala wake baada ya kuwakung'uta Stoke City mabao 3-0 uwanja wa nyumbani Ewood Park.
Mabao ya Blackburn yalifungwa ndani ya nusu saa ya kwanza ya mchezo wafungaji wakiwa McCarthy, dakika ya 9 kwa penalti, Roberts dakika ya 18 na Benni McCarthy akafunga tena dakika ya 27.

Katika mechi nyingine zilizochezwa jana, matokeo ni:

Bolton 2 Portsmouth 1

Fulham 3 Middlesbrough 0

Hull City 1 Sunderland 4

West Ham 0 Aston Villa 1

MECHI ZA LEO NA KESHO:

JUMAPILI, 21 Desemba 2008
[saa 10 na nusu jioni]


West Brom v Man City

[saa 12 jioni]

Newcastle v Tottenham

[saa 1 usiku]

Arsenal v Liverpool

JUMATATU, 22 Desemba 2008
[saa 5 usiku]

Everton v Chelsea

Friday 19 December 2008

JOSE MOURINHO: 'Ni furaha kukutanishwa na Timu Bora!!'

-Aikandya ARSENAL!!!

Jose Mourinho, aliekuwa Meneja wa Chelsea na kwa sasa yuko Italia akiiongoza Inter Milan timu ambayo haijachukua Ubingwa wa Ulaya tangu 1965, ametamka ana furaha timu yake kukutana na Mabingwa wa Ulaya Manchester United kwenye Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwa sababu ndio timu bora.
Mourinho alisema: 'Nimeridhika! Nilitaka timu bora nimeipata! Pengine baada ya siku mbili watakuwa Mabingwa wa Dunia! Wana Mchezaji Bora Ulaya, Ronaldo, Meneja Bora, Ferguson na Kiwanja Bora, Old Trafford!'
Mbali ya Liverpool, watakaopambana na Real Madrid, Timu zote 3 nyingine za England zitapambana na Klabu za Italia kuwania Ubingwa huo wa Klabu za Ulaya.
Chelsea na Juventus, Arsenal na AS Roma, Manchester United na Inter Milan.
Nae Jose Mourinho, kama alivyokuwa Chelsea, hakuacha kukandya!
Alisema: 'Mechi zote 3 kwa Timu za Italia ni fifte fifte lakini AS Roma wanaurahisi kidogo kwa sababu Arsenal sio Chelsea au Manchester United!'


RATIBA:

Jumanne, 24 Februari 2009

Arsenal v AS Roma

Atletico Madrid v FC Porto

Inter Milan v Man U

Lyon v Barcelona

Jumatano, 25 Februari 2009

Chelsea v Juventus

Real Madrid v Liverpool

Sporting v Bayern Munich

Villarreal v Panathinaikos

Jumanne, 10 Machi 2009

Bayern Munich v Sporting

Juventus v Chelsea

Liverpool v Real Madrid

Panathinaikos v Villarreal

Jumatano, 11 Machi 2009

Barcelona v Lyon

FC Porto v Atletico Madrid

Man U v Inter Milan

Roma v Arsenal
DRO YA RAUNDI YA MTOANO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE YAFANYWA!!

Mabingwa Watetezi wa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya Manchester United wamepangiwa kukutana na Timu inayoongozwa na aliekuwa Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, ambae kwa sasa yuko Italia akiwa na Inter Milan.
Mechi ya kwanza kati ya Inter Milan na Manchester United itachezwa nyumbani kwa Inter Milan kati ya Februari 24 au 25, 2009 na mechi ya marudiano ni kati ya Machi 10 au 11, 2009 uwanjani Old Trafford.
Timu nyingine za Uingereza zilizo kwenye raundi hii ni Chelsea watakaocheza na Juventus, Liverpool atakumbana na Real Madrid na Arsenal atapambana na Roma.
Washindi wa Raundi hii wataingia Robo Fainali.

RATIBA KAMILI NI: [Timu inayotajwa kwanza ipo nyumbani]
-Mechi za kwanza ni 24 na 25 Februari na marudiano ni 10 na 11 Machi 2009.

Chelsea v Juventus

Villareal v Panathinaikos

Sporting Lisbon v Bayern Munich

Atletico Madrid v FC Porto

Lyon v Barcelona

Real Madrid v Liverpool

Arsenal v Roma

Inter Milan v Manchester United

DRO YA UEFA CUP:

Sambamba na Dro ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, vilevile ilifanyika Dro ya Kombe la UEFA ambayo ilijumuisha jumla ya Timu 32 zikiwemo Timu 8 zilizokuwa Washindi wa tatu kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Washindi wa mechi hizo zitakazochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini wataingia RAUNDI YA Timu 16 za mwisho ambayo pia Dro yake ilifanywa.
Uingereza inawakilishwa na Timu za Aston Villa, Tottenham na Manchester City.
Kwenye RAUNDI YA TIMU 32, Aston Villa anacheza na CSKA Moscow, Tottenham v Shakhtar Donetsk na Manchester City v FC Copenhagen.
Lakini kwenye RAUNDI YA TIMU 16, Aston Villa na Tottenham huenda wakapambana endapo watashinda mechi zao za RAUNDI YA TIMU 32.

RATIBA KAMILI NI:

MECHI ZA RAUNDI YA TIMU 32 (Mechi ya kwanza 18-19 Feb na mechi ya marudiano 26 Feb 2009):

Paris Saint-Germain v Wolfsburg

FC Copenhagen v MANCHESTER CITY

NEC Nijmegen v Hamburg

Sampdoria v Metalist Kharkiv

Braga v Standard Liege

ASTON VILLA v CSKA Moscow

Lech Poznan v Udinese

Olympiakos v Saint-Etienne

Fiorentina v Ajax

Aalborg v Deportivo La Coruna

Werder Bremen v AC Milan

Bordeaux v Galatasaray Dynamo Kiev v Valencia

Zenit St. Petersburg v Stuttgart

Marseille v FC Twente

Shakhtar Donetsk v TOTTENHAM

MECHI ZA RAUNDI YA TIMU 16 (Mechi ya kwanza 12 Mar na marudiano 18-19 Mar 2009):

Werder Bremen AU AC Milan v Olympiakos AU Saint-Etienne

ASTON VILLA AU CSKA Moscow v Shakhtar Donetsk AU TOTTENHAM

Lech Poznan AU Udinese v Zenit St Petersburg AU Stuttgart

Paris Saint-Germain AU Wolfsburg v Braga AU Standard Liege

Dynamo Kiev AU Valencia v Sampdoria AU Metalist Kharkiv

Copenhagen AU MANCHESTER CITY v Aalborg AU Deportivo

Marseille AU FC Twente v Fiorentina AU Ajax

NEC Nijmegen AU Hamburg v Bordeaux AU Galatasaray

Thursday 18 December 2008

KOMBE LA DUNIA LA KLABU: MAN U watinga Fainali!!!!

Mabingwa wa Ulaya Manchester United leo wamewachakaza wenyeji wa mashindano Gamba Osaka ya Japan ambao pia ni Mabingwa wa Asia kwa mabao 5-3 na hivyo kuingia Fainali ya Kombe la Dunia ya Klabu na sasa watavaana na Liga de Quito ya Ecuador siku ya Jumapili tarehe 21.
Timu zilikuwa:

Gamba Osaka: Fujigaya, Kaji, Nakazawa, Yamaguchi, Endo, Michihiro Yasuda, Myojin, Hashimoto, Bando (Terada 85), Lucas, Yamazaki.
Akiba hawakucheza: Matsuyo, Shimohira, Futagawa, Kurata, Takei, Roneliton.
Kadi: Yamaguchi.
Magoli: Yamazaki 74, Endo 85 pen, Hashimoto 90.
Man Utd: Van der Sar, Neville, Ferdinand, Vidic (Evans 69), Evra, Nani, Anderson, Scholes (Fletcher 67), Ronaldo, Giggs, Tevez (Rooney 73).
Akiba hawakucheza: Kuszczak, Rafael Da Silva, O'Shea, Carrick, Gibson, Park, Welbeck, Amos.
Kadi: Rooney.
Magoli: Vidic 28, Ronaldo 45, Rooney 75, Fletcher 78, Rooney 79.
Watazamaji: 67,618
Refa: Benito Archundia Tellez (Mexico).

Wednesday 17 December 2008

Allardyce atua Blackburn Rovers!

Sam Allardyce ametangazwa kuwa Meneja mpya wa Blackburn Rovers kuchukua nafasi ya Paul Ince aliefukuzwa.
Allardyce alikuwa Meneja wa Bolton na baadae Newcastle.
Liga de Quito yatinga FAINALI!

Klabu ya Liga de Quito ya Ecuador ambao ndio Mabingwa wa Marekani Kusini wametinga Fainali ya KLABU BINGWA DUNIANI baada ya kuipiga Pachuca bao 2-0 na watakutana na mshindi kati ya Gamba Osaka na Manchester United wanaocheza kesho.
Mabao ya Claudio Bieler dakika ya 4 na Luis Alberto Bolanos dakika ya 25 ndio yaliwaua Pachuca.
Sasa Liga de Quito wako FAINALI itakayochezwa JUMAPILI tarehe 21 DESEMBA 2008 mjini Yokohama, Japan.

Tuesday 16 December 2008

MAN U haikati rufaa kupinga adhabu ya EVRA!!!

Manchester United imeamua kutokata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa mechi 4 na faini ya Pauni 15,000 ya Mchezaji wao Patrice Evra aliyopewa na FA baada ya kupatikana na hatia ya kupigana na Mfanyakazi mkata nyasi wa Uwanja wa Chelsea, Stamford Bridge, aitwae Sam Bethell, ugomvi uliotokea mara baada ya mechi kati ya Chelsea na Man U msimu uliopita.
Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson alistushwa na kukasirishwa na adhabu hiyo aliyoiita 'ni uamuzi mbovu ambao sijawahi kuuona!'.
Katika taarifa yake, Klabu ya Manchester United imesisitiza kwamba adhabu hiyo haikustahili, ina kasoro nyingi na kuikatia rufaa ni kupoteza muda hasa wakati klabu inaingia awamu ya pili ya LIGI KUU.
Vilevile, Man U wamesema kumfungia Mchezaji mechi 4 ambae hajawahi kupewa Kadi Nyekundu hata moja wakati wale wanaocheza rafu mbaya sana na wale wanaolipiza kwa kuwarushia Watazamaji vitu walivyorushiwa kufungiwa mechi 3 tu, ni ukiukwaji mkubwa wa haki.
Evra, ambae kwa sasa yuko Japan pamoja na kikosi kamili cha Man U kitakachoshiriki Mashindano ya Klabu Bingwa Duniani, atazikosa mechi za LIGI KUU za Man U watakapocheza na Stoke na Middlesbrough, Kombe la FA dhidi ya Southampton hapo tarehe 3 Januari 2009 na pambano la kwanza la Nusu Fainali ya Kombe la Carling dhidi ya Derby litakalochezwa siku nne baadae.
Mechi yake ya kwanza anayoweza kurudi uwanjani itakuwa ni pambano la kukata na shoka la LIGI KUU litakalofanyika Old Trafford dhidi ya klabu iliyomtia matatizoni, Chelsea, hapo tarehe 11 Januari 2009.
LIGI KUU ENGLAND: Kipindi kigumu kinaingia!!!

Inasemekana, hakika inaaminika hasa kwa wafuatiliaji wazuri wa historia ya LIGI KUU ENGLAND, mechi zinazochezwa mwezi Desemba hasa wakati wa kipindi cha Sikukuu ya Krismas ambako kunakuwa mechi za 'kubanana' na zinazoendelea mfululizo hadi Januari, ndizo zinazotoa mwelekeo wa nani anaweza kuwa Bingwa.
Wakati tunaelekea kipindi hicho, msimamo wa ligi mpaka sasa kwa Timu 5 za juu ni kama ifuatavyo:

-Liverpool mechi 17 pointi 38

-Chelsea mechi 17 pointi 37

-Man U mechi 16 pointi 32

-Aston Villa mechi 17 pointi 31

-Arsenal mechi 17 pointi 30

Mabingwa Watetezi Manchester United wamecheza mechi moja pungufu kwa sababu walienda kucheza mechi ya UEFA SUPER CUP na mechi yao dhidi ya Fulham ikaahirishwa.
Mechi hii sasa imepangwa kuchezwa tarehe 17 Februari 2009.

Ratiba ya mechi za 'VIGOGO' hao wa LIGI KUU katika kipindi hiki ambacho kawaida hutoa fununu wa nani anaunusa ubingwa ni kama ifuatavyo:

[Timu inayotajwa kwanza iko nyumbani]

MANCHESTER UNITED:

-Stoke v Man U [26 Desemba]
-Man U v Middlesbrough [29 Desemba]
-Man U v Chelsea [11 Januari]
-Man U v Wigan [14 Januari] [Hiki ni kiporo.
Mechi hii ilitakiwa ichezwe Desemba 21 lakini Man U watakuwa Japan kwenye Kombe la Dunia la Klabu]

CHELSEA

-Everton v Chelsea [22 Desemba]
-Chelsea v West Brom [26 Desemba]
-Fulham v Chelsea [28 Desemba]
-Man U v Chelsea [11 Januari]

ARSENAL

-Arsenal v Liverpool [21 Desemba]
-Aston Villa v Arsenal [26 Desemba]
-Arsenal v Portsmouth [28 Desemba]
-Arsenal v Bolton [10 Januari]

LIVERPOOL

-Arsenal v Liverpool [21 Desemba]
-Liverpool v Bolton [26 Desemba]
-Newcastle v Liverpool [28 Desemba]
-Stoke v Liverpool [10 Januari]

Hebu tusubiri tuone nani atavuka hivi vigingi na kuibuka kidedea.
PAUL INCE ATIMULIWA BLACKBURN!!

Klabu ya Blackburn Rovers imemfukuza kazi Meneja wake Paul Ince kufuatia matokeo mabaya kwenye LIGI KUU.
Ince alijiunga Blackburn mwezi Juni akitoka MK Dons na kuiongoza timu hiyo kwenye mechi 17 za LIGI KUU lakini wameshinda mechi 3 tu kati ya hizo na ushindi wao wa mwisho ulitokea Septemba 27 walipoifunga Newcastle.
Kwa sasa Blackburn ipo nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi yaani timu ya pili toka mwisho.
Mwenyekiti wa Blacburn John Williams akitangaza uamuzi huo wa kumtimua alisema: 'Ushindi wa mechi 3 katika 17 kwa timu iliyomaliza ligi nafasi ya 7 msimu uliopita na kutufanya sasa tuwe wa 19 kati ya timu 20 haukubaliki!'
Paul Ince ameweka historia ya kuwa Meneja wa kwanza mweusi kuongoza klabu iliyo LIGI KUU.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Benitez alazwa hospitali jana, augua ugonjwa uleule uliomlaza Scolari juzi!!!
Klabu ya Liverpool imethibisha Meneja wao Rafa Benitez alikimbizwa hospitali Jumatatu usiku na inabidi afanyiwe operesheni ndogo baadae wiki hii kwa kuwa anasumbuliwa na vijiwe kwenye figo.
Taarifa hizi zimekuja masaa 24 tu tangu Meneja wa Chelsea Luis Felipe Scolari alazwe hospitali kwa usiku mmoja kwa tatizo la aina hiyohiyo.
Katika msimamo wa LIGI KUU, Liverpool ndio inaongoza ikifuatiwa na Chelsea walio pointi moja nyuma.
Rooney, Ronaldo wanusurika adhabu

Nyota wa Manchester United, Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo, wamenusurika kubandikwa adhabu na UEFA na FA baada ya kutuhumiwa kutenda makosa katika mechi na makosa hayo kutoonwa na Marefa wa mechi hizo.
Rooney alituhumiwa kumkanyaga Mlinzi wa Aalborg ya Denmark Kasper Risgard kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kati ya Man U na Aaalborg iliyochezwa Old Trafford Jumatano iliyopita.
Baada ya UEFA kupitia mkanda wa video wameamua hakuna hatua zozote zinastahili kuchukuliwa.
Baada ya mechi hiyo, Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, aliwapandishia Waandishi wa Habari kwa kulivalia njuga tukio ambalo halikustahili chochote.
Nae Ronaldo alituhumiwa kumpiga teke Mlinzi wa Tottenham Michael Dawson kwenye mechi ya Tottenham na Manchester United siku ya Jumamosi.
FA ilimtaka Refa wa pambano hilo Mike Dean kulitazama tena tukio hilo kwenye video na kuamua kama angeliliona angechukua hatua gani lakini Dean alithibitisha hata kama angeliona asingempa Ronaldo Kadi Nyekundu.

Monday 15 December 2008

Mabingwa Man U watua Tokyo, Japan kucheza KOMBE LA KLABU BINGWA DUNIANI

Kikosi cha Wachezaji 23 wa Mabingwa wa Ulaya Manchester United kikiongozwa na Meneja wao Sir Alex Ferguson leo asubuhi kimetua Uwanja wa Ndege wa Narita mjini Tokyo [pichani] ili kupambana kwenye Nusu Fainali ya FIFA CLUB WORLD CUP na Gamba Osaka ya Japan ambao ndio Mabingwa wa Asia.
Jana Gamba Osaka iliifunga Adelaide United ya Australia bao 1-0 na kuingia Nusu Fainali.
Mechi hii itachezwa siku ya Alhamisi tarehe 18 Desemba 2008 saa 7 na nusu mchana kwa saa za bongo.
Kikosi cha Man U kilichopo Japan ni:
MAKIPA: Van der Sar, Kuszczak, Amos; WALINZI: Neville, Evra, Ferdinand, Vidic, O'Shea, Evans, Rafael; VIUNGO: Ronaldo, Anderson, Giggs, Park, Carrick, Nani, Scholes, Fletcher, Gibson; WASHAMBULIAJI: Berbatov, Rooney, Tevez, Welbeck.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Harry Redknapp: 'Bingwa ni Man U au Chelsea!'
Meneja wa Tottenham Harry Redknapp amesema Bingwa wa England msimu huu atakuwa Chelsea au Watetezi Man U na hadhani kama Liverpool ana ubavu wa kuhimili mikikimikiki ya muda mrefu.
Redknapp, ambae Timu yake Tottenham ililazimisha sare ya 0-0 ilipocheza na Mabingwa Man U juzi, alisema: 'Mmoja kati ya Chelsea au Man U atashinda. Arsenal wamepoteza pointi nyingi na siwaoni kama wanaweza kurudi kwenye kinyang'anyiro! Nao Liverpool wanawategemea sana Steve Gerrard na Fernando Torres! Sijui kiktokea kitu kwa hao wawili watafanya nini na hivyo wana mapungufu ukilinganisha na vikosi vya Chelsea na Man U!'
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND: MECHI ZA WIKIENDI [saa ni za bongo]
JUMAMOSI, 20 Desemba 2008
[saa 12 jioni]

Blackburn v Stoke

Bolton v Portsmouth

Fulham v Middlesbrough

Hull v Sunderland

[saa 2 na nusu usiku]

West Ham v Aston Villa

JUMAPILI, 21 Desemba 2008

[saa 10 na nusu jioni]

West Brom v Man City

[saa 12 jioni]

Newcastle v Tottenham

[saa 1 usiku]

Arsenal v Liverpool

JUMATATU, 22 Desemba 2008
[saa 5 usiku]

Everton v Chelsea

Sunday 14 December 2008

LIGI KUU ENGLAND: Nao Chelsea wakwama!!!

Chelsea leo wameshindwa kuchukua mwanya wa Liverpool kutoka suluhu ya bao 2-2 na Hull City hapo jana na wao kushinda leo ili wachukue uongozi wa ligi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na West Ham wakiwa nyumbani kwao Stamford Bridge.
West Ham, wakiongozwa na Meneja wao Gianfranco Zola ambae alikuwa Mchezaji nyota hapo Chelsea, walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Craig Bellamy aliefunga dakika ya 33.
Nicholas Anelka aliisawazishia Chelsea dakika ya 51.
Matokeo hayo yanawafanya Liverpool waendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 38 kwa mechi 17, Chelsea wanafuata pointi 37 kwa mechi 17, kisha Mabingwa Man U pointi 32 mechi 16, Aston Villa pointi 31 mechi 17 na Arsenal ni wa 5 wakiwa na pointi 30 kwa mechi 17.

Portsmouth 0 Newcastle 3

Katika mechi ya awali ya LIGI KUU leo, Newcastle, ikiwa ugenini, iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Portsmouth huo ukiwa wa ushindi wao wa kwanza wa mechi za ugenini msimu huu ambao umewafanya kuchupa hadi nafasi ya 14 kutoka nafasi ya 18.
Hadi mapumziko mechi ilikuwa 0-0 na kipindi cha pili mabao ya Nahodha wao Michael Owens dakika ya 52, Obafemi Martins dakika ya 77 na la Guthrie dakika ya 89 yaliwapa ushindi.
GAMBA OSAKA yatinga Nusu Fainali, kuikwaa MAN U Alhamisi!

Leo, Mabingwa wa Asia, Gamba Osaka ya Japan, imeipachika Adelaide United ya Australia, timu iliyoshika nafasi ya pili katika Ubingwa wa Asia. bao 1-0 na kuingia Nusu Fainali watakakopambana na Mabingwa wa Ulaya Manchester United siku ya Alhamisi tarehe 18 Desemba 2008.
Katika mechi iliyochezwa Toyota Stadium mjini Tokyo, Japan, Mchezaji wa Gamba Osaka Yasuhito Endo alipachika bao la ushindi dakika ya 23.
Timu hizi, Gamba Osaka na Adelaide United, zilikutana wiki kadhaa nyuma kwenye Fainali ya Klabu Bingwa Asia na Gamba Osaka waliibuka kidedea baada ya kuichabanga Adelaide United katika mechi zote mbili jumla ya Mabao 5-0 ikiwa 3-0 mechi iliyochezwa Japan na 2-0 mechi iliyochezwa Australia.
LIGI KUU ENGLAND: Liverpool, Arsenal na Man U wabanwa mbavu! Chelsea leo!

Vigogo Man U, Liverpool na Arsenal jana walitoka suluhu katika mechi zao za LIGI KUU na sasa nafasi iko wazi kwa Chelsea kuchukua uongozi wa ligi hiyo toka mikononi mwa Liverpool endapo watawafunga West Ham kwenye mechi yao ya leo itakayochezwa Stamford Bridge saa 1 usiku saa za bongo.
Liverpool, akiwa kwake Anfield, alijikuta yuko nyuma kwa bao 2-0 walipocheza na Hull ndani ya dakika 22 za kwanza kwa mabao yaliyofungwa na McShane dakika ya 12 na Beki wa Liverpool Carragher akajifunga mwenyewe dakika ya 22.
Nahodha wa Liverpool Steve Gerrard akaokoa jahazi kwa kurudisha mabao yote kwenye dakika za 24 na 32.
Arsenal waliocheza ugenini uwanjani Riverside dhidi ya Middlesbrough, walipata bao dakika ya 17 kupitia Adebayor lakini Boro wakasawazisha kupitia Mchezaji wao ambae zamani alikuwa Arsenal Aliadiere dakika ya 29.
Nao Mabingwa Man U wakicheza ugenini White Hart Lane nyumbani kwa Tottenham, walilazimishwa sare ya 0-0 huku Kipa wa Spurs Gomez akiibuka nyota kwa kuokoa mipira mingi ya hatari ya Wachezaji wa Man U.
Ronaldo alifanikiwa kupachika bao lakini Mwamuzi Mike Dean alilikataa kwa kudai aliunawa kabla ya kufunga.

MATOKEO MECHI NYINGINE:

Aston Villa 4 Bolton 2

Man City 0 Everton 1

Stoke o Fulham 0

Sunderland 4 West Brom 0

Wigan 3 Blackburn 0

MECHI ZA LEO:

Portsmouth v Newcastle [saa 10 na nusu mchana]

Chelsea v West Ham [saa 1 usiku]

LA LIGA: Barcelona 2 Real Madrid 0

Magoli yaliyofungwa na Samuel Etoo dakika ya 80 na Lionel Messi kwenye dakika za majeruhi yamewaua Mahasimu Real Madrid na kuwafanya Barcelona waendelee kuongoza Ligi ya Spain na kuwa pointi 12 mbele ya Real Madrid.

FIFA CLUB WORLD CUP:

Leo ni mechi kati ya Mabingwa wa Asia, Gamba Osaka ya Japan na Adelaide United ya Australia ambao ni Washindi wa pili wa Klabu Bingwa Asia.
Katika mechi ya awali, Adelaide United waliifunga Waitakere United ya New Zealand 2-0.
Mshindi wa mechi hii atapambana na Mabingwa wa Ulaya Manchester United siku ya Alhamisi Desemba 18 katika Nusu ya pili.

Saturday 13 December 2008

MCHEZAJI BORA DUNIANI KUJULIKANI JANUARI 12: Listi yapunguzwa hadi Wagombea Watano!!!

Winga wa Manchester United, Cristiano Ronaldo na Straika wa Liverpool, Fernando Torres, wamo katika listi ya mwisho ya Wachezaji watano wanaogombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia inayotolewa na FIFA.
Uteuzi huo wa Wachezaji hao watano umefanywa na Makocha na Manahodha wa Timu za Taifa za Nchi kutoka duniani kote.
Wachezaji wengine watatu ni Kaka wa AC Milan, nyota wa Barcelona Lionel Messi na Xavi wa Barcelona.
Ronaldo, ambae alipata Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya [Ballon D'Or] siku ya Jumapili, alimaliza nafasi ya 3 kwenye Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia wa FIFA mwaka uliopita nyuma ya Messi na Mshindi Kaka.
Mshindi atakabidhiwa Tuzo yake huko Zurich, Uswisi kwenye Jumba la Opera la Zurich Januari 12, 2009.
Kwa upande wa wanawake mshindi atakuwa kati ya Nadine Angerer, Cristiane, Marta, Birgit Prinz au Kelly Smith.
Kwa kina mama, Marta wa Brazil [pichani] ndie Mshindi mwaka uliopita na anapewa nafasi kubwa kushinda tena.
Mabingwa wa Afrika Al Ahly yatolewa nje KLABU BINGWA DUNIANI!
Wabandikwa 4-2 na Pachuca!!!

Leo Jumamosi tarehe 13 Desemba 2008, Mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri, waliingia dimbani National Stadium, Tokyo, Japan kucheza na Pachuca ya Mexico ambao ni Mabingwa wa CONCACAF [Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean].
Al Ahly walikuwa wakiongoza mabao 2-0 huku la kwanza Pachuca wakijifunga wenyewe kupitia Fausto Pinto na la pili akafunga Mshambuliaji wa Al Ahly kutoka Angola Amado Flavio.
Pachuca wakasawazisha kupitia Luis Montez na Christian Gimenez dakika ya 47 na 73.
Mpaka dakika 90 kumalizika mabao yalibaki 2-2 na dakika 30 za nyongeza zikachezwa.
Pachuca wakatoka kifua mbele kwa mabao ya Damian Alavarez dakika ya 98 na Gimenez akaongeza la 4 dakika ya 110.
Pachuca sasa watapambana na Liga de Quito ya Ecuador, Mabingwa wa Nchi za Marekani ya Kusini kwenye Nusu Fainali ya kwanza itakayochezwa Jumatano tarehe 17 Desemba 2008 .
Kesho ni mechi kati ya Mabingwa wa Asia, Gamba Osaka ya Japan na Adelaide United ya Australia ambao ni Washindi wa pili wa Klabu Bingwa Asia.
Mshindi wa mechi hii atapambana na Mabingwa wa Ulaya Manchester United siku ya Alhamisi Desemba 18 katika Nusu ya pili.
Ronaldo ajiunga na Corinthians

Aliekuwa nyota wa Brazil Ronaldo de Lima ambae aliumia vibaya goti lililomlazimu kuiacha klabu ya Italia AC Milan mwezi Juni ametangazwa kujiunga na klabu ya Sao Paulo, Brazil iitwayo Corinthians.
Ronaldo aliumia goti hilo mwezi Februari na mkataba wake na AC Milan uliisha Juni.


Kipa Van der Sar aongeza mkataba

Golikipa wa Mabingwa Manchester United, Edwin van der Sar [38], ameongeza mwaka mmoja katika mkataba wake na sasa atabaki klabuni hapo hadi mwaka 2010.
Van der Sar alijiunga Man U Juni 2005 akitokea klabu ya Fulham. Awali alichezea klabu za Ajax na Juventus.


Barcelona v Real Madrid leo Nou Camp!

Timu inayosuasua kwenye Ligi ya Spain, La Liga, na ambayo siku ya Jumannne ilimtimua Meneja wake Bernd Schuster na kumchukua Juande Ramos ambae nae alietimuliwa Tottenham, Real Madrid, leo inaingia myumbani kwa mahasimu wao na vinara wa ligi, Barcelona, uwanjani Nou Camp.
Mpaka sasa Real Madrid wako nafasi ya 5 wakiwa pointi 9 nyuma ya viongozi wa La Liga Barcelona.
Juande Ramos amepewa mkataba wa miezi 6 tu kuwa Meneja wa Real Madrid na kumfanya awe Meneja wa 8 wa klabu hiyo katika miaka 6 iliyopita.

Mechi ya leo itachezwa saa 6 usiku saa za bongo.

Thursday 11 December 2008

Baada ya Miaka 40 Tuzo ya 'BALLON d'OR' yarudi OLD TRAFFORD!!!

Kabla ya kuanza mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE iliyochezwa Jumatano kati ya Manchester United na Aalborg uwanjani Old Trafford, Cristiano Ronaldo alietunukiwa 'Ballon d'Or' [KOMBE LA DHAHABU] kudhihirisha yeye ndie MCHEZAJI BORA ULAYA mwaka huu, alitambulishwa rasmi na kukabidhiwa tena Kombe hilo uwanjani hapo huku akiwa amesindikizwa na Wachezaji wa zamani wa Manchester United Dennis Law, alieshinda tuzo hiyo mwaka 1964 na Sir Bobby Charlton alieipata 1966.
Mchezaji wa mwisho wa Manchester United kushinda Tuzo hiyo ni George Best alietunukiwa mwaka 1968.
George Best ni marehemu.

LIGI KUU UINGEREZA: Kitimtim cha Wikiendi

Jumamosi, 13 Decemba 2008

[saa 8 dak 45]
Middlesbrough v Arsenal

[saa 12 jioni]
Aston Villa v Bolton

Liverpool v Hull

Man City v Everton

Stoke v Fulham

Sunderland v West Brom

Wigan v Blackburn

[saa 2 na nusu]
Tottenham v Man U

Jumapili, 14 Decemba 2008
[saa 10 na nusu jioni]
Portsmouth v Newcastle

[saa 1 usiku]
Chelsea v West Ham
FIFA CLUB WORLD CUP JAPAN 2008 yaanza!!!

Mabingwa wa Afrika Al Ahly kucheza Jumamosi, Man United dimbani wiki ijayo!!!!!

Leo mashindano ya kugombea 'KOMBE LA KLABU BINGWA YA DUNIA' yajulikanayo kama 'FIFA CLUB WORLD CUP JAPAN 2008' yameanza rasmi huko Tokyo, Japan kwa mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa kati ya Adelaide United, Washindi wa Pili wa Klabu Bingwa Asia wanaotoka Australia, na Waitakere United ya New Zealand, ambayo inawakilisha Timu kutoka Nchi za Oceania.
Katika mechi hiyo ya ufunguzi, Adelaide United ilibwaga Waitakere United kwa mabao 2-1 wafungaji wakiwa ni Daniel Mullen na Travis Dodd kwa Adelaide kwenye dakika ya 38 na 83.
Paul Seaman aliifungia Waitakere dakika ya 34.
Sasa Adelaide United wanasonga mbele na watakutana na Gamba Osaka ya Japan ambao ndio Mabingwa wa Bara la Asia mchezo ambao utachezwa Toyota Stadium, mjini Tokyo, Japan siku ya Jumapili tarehe 14 Desemba 2008.
Kesho ni mapumziko na siku ya Jumamosi tarehe 13 Desemba 2008, Mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri, inashuka dimbani National Stadium, Tokyo, Japan kucheza na Pachuca ya Mexico ambao ni Mabingwa wa CONCACAF [Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean].
Mshindi wa mechi hii atapambana na Liga de Quito ya Ecuador, Mabingwa wa Nchi za Marekani ya Kusini kwenye Nusu Fainali ya kwanza.
Mabingwa wa Ulaya, Manchester United, wao wameingizwa moja kwa moja Nusu Fainali ya pili na watapambana na mshindi wa mechi kati Adelaide United na Gamba Osaka hapo Alhamisi tarehe 18 Desemba 2008 mjini Yokohama, Japan.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: DRO YA RAUNDI YA MTOANO KUFANYIKA DESEMBA 19: Vigogo Man U, Chelsea, Arsenal na Liverpool kukutana na nani?

Wakati tayari Timu 16 zilizoingia Raundi ya Mtoano ambayo huchezwa kwa mtindo wa mechi za nyumbani na ugenini ili kupata Timu 8 zitakazoingia Robo Fainali zimeshapatikana, Dro ya kuamua nani anacheza na nani itafanyika tarehe 19 Desemba 2009.
Timu 16 zilizoingia kwenye Dro hiyo ni:
WALIOSHINDA KILA KUNDI: Roma, Panathinaikos, Barcelona, Liverpool, Man U, Bayern Munich, FC Porto, Juventus.
WASHINDI WA PILI: Chelsea, Inter Milan, Sporting, Atletico Madrid, Villareal, Lyon, Arsenal, Real Madrid.
KANUNI ZINAZOTAWALA DRO:
-Timu toka Nchi moja haziwezi kukutana.
-Mshindi wa Kundi na Mshindi wa Pili wa Kundi hilohilo hawawezi kukutana.
-Washindi wa Makundi hawawezi kukutanishwa.
-Washindi wa Pili wa Makundi hawawezi kukutanishwa.
-Washindi wa Pili wa kila Kundi watacheza mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano nyumbani kwao.

Kufuatana na Kanuni hizi, Timu za England, Man U, Chelsea, Arsenal na Liverpool, haziwezi kukutana zenyewe.

Hivyo basi, tumechambua ni Timu zipi ambazo Vigogo hao wa England wanaweza kupambanishwa nao:

MANCHESTER UNITED: Inter Milan, Sporting Lisbon, Atletico Madrid, Lyon, Real Madrid.

ARSENAL: Bayern Munich, Juventus, AS Roma, Panathinaikos, Barcelona.

CHELSEA: Panathinaikos, Barcelona, Bayern Munich, FC Porto, Juventus.

LIVERPOOL: Inter Milan, Sporting Lisbon, Villareal, Lyon, Real Madrid.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Arsenal apigwa, Man U sare!!!

Timu zote 16 zitakazocheza Raundi ya Mtoano zilikuwa zishajulikana na mechi za Jumatano zilikuwa ni kuamua msimamo wa kila Kundi.

Baada ya mechi hizo hali ni kama ifuatavywo:

KUNDI E
Celtic 2 v Villarreal 0,
Man U 2 v AaB 2,

Msimamo:
1 Man U 10 pts
2 Villareal 9 pts
3 Aab Aalborg 6 pts
4 Celtic 5 pts

KUNDI F
Steaua Bucharest 0 v Fiorentina 1,
Lyon 2 v Bayern Munich 3,
Msimamo:

1 Bayern Munich 14 pts
2 Lyon 11 pts
3 Fiorentina 6 pts
4 Steau Bucharest 1 pts

KUNDI G
Dynamo Kiev 1 v Fenerbahce 0,
FC Porto 2 v Arsenal 0,

Msimamo:
1 FC Porto 12 pts
2 Arsenal 11 pts
3 Dynamo Kiev 8 pts
4 Fenerbahce 2 pts

KUNDI H
Juventus 0 v BATE 0
Real Madrid 3 v Zenit St Petersburg 0

Msimamo:
1 Juventus 12 pts
2 Real Madrid 12 pts
3 Zenit St Petersburg 5 pts
4 BATE Borisov 3 pts

MECHI ZA JUMANNE:
WALIOSHINDA KILA KUNDI: Roma, Panathinaikos, Barcelona, Liverpool.
WASHINDI WA PILI: Chelsea, Inter Milan, Sporting, Atletico Madrid.
MECHI ZA JUMATANO:
WALIOSHINDA KILA KUNDI: Man U, Bayern Munich, FC Porto, Juventus
WASHINDI WA PILI: Villareal, Lyon, Arsenal, Real Madrid

Wednesday 10 December 2008

UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
TIMU 16 ZINAZOINGIA RAUNDI YA MTOANO ZAPATIKANA!!

Mechi za jana za UEFA CHAMPIONS LEAGUE zimetoa Timu 3 zilizobaki ili kufanya idadi ya timu kuwa 16 zitakazocheza Raundi inayofuata ya Mtoano.
Dro ya kuamua timu ipi inakutana na ipi kwa mechi za nyumbani na ugenini ili kupata timu 8 zitakazoingia Robo Fainali itafanyika tarehe 19 Desemba 2008.
Mechi za Raundi hii ya Mtoano zitachezwa tarehe 24 na 25 Februari 2009 na marudiano ni tarehe 10 na 11 Machi 2009.
Katika Timu hizo 16 zilizofuzu 4 zinatoka England, nazo ni Manchester United, Chelsea, Liverpool na Arsenal na 4 nyingine zinatoka Spain ambazo ni Real Madrid, Barcelona, Villareal na Atletico Madrid.
Timu zilizobaki ni AS Roma, Inter Milan, Panathinaikos, Sporting Lisbon, Lyon, Bayern Munich, FC Porto na Juventus.
Katika hiyo Dro ya Raundi ya Mtoano Timu kutoka nchi moja na zile zilizokuwa Kundi moja haziruhusiwi kukutana.
Pia Timu iliyoongoza Kundi itapambanishwa na Timu iliyokuwa ya pili toka Kundi jingine.
Timu amabazo jana zilipata nafasi ya tatu katika msimamo wa Makundi na ambazo sasa zitaingizwa UEFA CUP ni: Bordeaux, Werder Bremen, Shakhtar Donetsk na Marseille.

MATOKEO MECHI ZA Jumanne, 9 Decemba 2008

KUNDI A
Chelsea 2 v CFR 1,
Roma 2 v Bordeaux 0,
Msimamo:
1 Roma 12 pts
2 Chelsea 11 pts
3 Bordeaux 7 pts
4 CFR Cluj 4 pts

KUNDI B
Werder Bremen 2 v Inter Milan 1,
Panathinaikos 1 v Anorthosis Famagusta 0,
Msimamo:
1 Panathinaikos 10 pts
2 Inter Milan 8 pts
3 Werder Bremen 7 pts
4 Anorthosis 6 pts

KUNDI C
Barcelona 2 v Shakhtar Donetsk 3,
Basle 0 v Sporting 1,
Msimamo:
1 Barcelona 13 pts
2 Sporting Lisbon 12 pts
3 Shakhtar Donetsk 9 pts
4 Basle 1 pt

KUNDI D
Marseille 0 v Atletico Madrid 0,
PSV 1 v Liverpool 3,
Msimamo:
1 Liverpool 14 pts
2 Atletico Madrid 12 pts
3 Marseille 4 pts
4 PSV 3 pts

MECHI ZA LEO: Jumatano, 10 Decemba 2008

Ingawa Timu zote 16 zitakazocheza Raundi ya Mtoano zimepatikana, umuhimu wa mechi za leo ni kuamua nani ataongoza kwenye Kundi na nani atacheza UEFA.

KUNDI E
Celtic v Villarreal,
Man U v AaB,

KUNDI F
Steaua Bucuresti v Fiorentina
Lyon v Bayern Munich

KUNDI G
Dynamo Kiev v Fenerbahce,
FC Porto vArsenal,

KUNDI H
Juventus v BATE
Real Madrid v Zenit St Petersburg

Monday 8 December 2008

STRAIKA EDUARDO KARIBUNI KUSHUKA DIMBANI!!

Mshambuliaji wa Arsenal Eduardo ambae aliumizwa vibaya mwezi Februari mwaka huu huko Birmingham wakati Arsenal wakicheza mechi ya LIGI KUU na Birmingham City yupo karibu kuonekana tena uwanjani.
Eduardo [25] alivunjwa enka na Mchezaji wa Birmingham City Martin Taylor [tizama picha] na tangu wakati huo alikuwa akijiuguza lakini kwa sasa yupo mazoezini na hucheza hata mechi kamili za mazoezi.
Meneja Arsene Wenger wa Arsenal amethibitisha: 'Ndio yupo mazoezini na atacheza hivi karibuni.'
Eduardo ni mzawa wa Brazil ingawa anaichezea Croatia.

Wenger amtetea Mchezaji wake Eboue aliekasirishwa kubadilishwa kwenye mechi.

Kwenye mechi ya Jumamosi iliyopita ya LIGI KUU ambayo Arsenal wakiwa kwao Emirates Stadium waliifunga Wigan bao 1-0 kwa bao la Adebayor, Eboue alianza mechi hii akiwa benchi la akiba kama resevu.
Eboue alipata nafasi ya kuingizwa kucheza dakika ya 32 baada ya Samir Nasri kuumia.
Lakini, hiyo itakuwa ni mechi ambayo hatopenda kuikumbuka kwani mara baada ya kuingizwa akawa akicheza kosa baada ya kosa mojawapo likiwa kumnyang'anya mpira mwenzake Kolo Toure na kumpasia adui!
Washabiki wa Arsenal wakaanza kumzomea!
Alipozidi kuzodolewa na kuendelea kufanya makosa huku timu yake Arsenal ikiwa imebanwa sana na Wigan ambao walionekana wanaweza kurudisha, Meneja Arsene Wenger akalazimika kumbadilisha na kumwingiza Mlinzi Mikael Silvestre.
Wakati Eboue akitoka uwanjani, Washabiki wa Arsenal walimshangilia kwa kejeli kubwa na yeye akakasirika na akasusa kwenda benchi la akiba na badala yake akaingia moja kwa kwa moja vyumba vya kubadilishia jezi Wachezaji.
'Ulikuwa uamuzi mgumu lakini alishapoteza morali na imani yake' Wenger alisema. 'Alikuwa hawezi tena kumiliki mpira na ilikuwa hatari kwetu! Mashabiki wetu wamenisikitisha sana! Atarudi tu ni mchezaji mzuri na mashabiki haohao watamshangilia!'

DWIGHT YORKE ALIA KUONDOKA ROY KEANE SUNDERLAND!!!

Dwight Yorke[37] amekaririwa akinung'unika kuhusu kung'oka kwa aliekuwa Mchezaji mwenzake huko Manchester United, Roy Keane, kama Meneja wake wa Sunderland: 'Nilishtuka, nilishangaa na nimesikitishwa!'
Yorke aliongeza: 'Yeye ndie alienileta Sunderland! Namshkuru sana! Naamini sana angeendelea hapa lazima timu ingefanya vizuri tu!'
Roy Keane alimleta Dwight Yorke kuichezea Sunderland mwaka 2006 wakati timu ikiwa Daraja la Chini ya LIGI KUU na wote wakaipandisha LIGI KUU msimu huo huo.
LEO LIGI KUU: West Ham v Tottenham

West Ham wakiwa nyumbani uwanjani Upton Park leo wanawakaribisha wenzao wa jijini London Tottenham kwenye mechi pekee ya LIGI KUU itakayochezwa saa 5 usiku saa za kibongo.
Timu zote mbili zikiwa zimecheza idadi sawa ya mechi 15 kila mmoja, West Ham yuko juu ya Tottenham kwa pointi 3. West Ham yuko nafasi ya 15 akiwa na pointi 18 na Tottenham yuko wa 17 akiwa na pointi 17.
Meneja wa West Ham Gianfranco Zola amesisitiza umuhimu wa mechi hii wakati yule wa Tottenham Harry Redknapp amekiri Upton Park ni mahali pagumu sana kupata ushindi.
VIKOSI VITATATOKANA NA:
West Ham: Green, Neill, Collins, Upson, Ilunga, Faubert, Boa Morte, Parker, Mullins, Behrami, Bellamy, Cole, Noble, Lastuvka, Tristan, Davenport, Collison, Di Michele, Bowyer.
Tottenham: Gomes, Cesar, Alnwick, Bale, Gunter, Dawson, Assou-Ekotto, Woodgate, King, Corluka, Zokora, Bentley, Huddlestone, Jenas, O'Hara, Bostock, Lennon, Jenas, Boateng, Bent, Campbell, Pavlyuchenko, Modric.
REFA: CHRIS FOY
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Mechi za mwisho za MAKUNDI!!!

Jumanne tarehe 9 Desemba 2008 na Jumatano mechi za mwisho za Makundi ya kugombea Klabu Bingwa Ulaya 2008/9, yaani UEFA CHAMPIONS LEAGUE, zitamalizika.
Awamu hii iligawiwa kwenye Makundi manane yenye timu 4 kila moja huku mbili za juu zikisonga mbele kuingia Raundi inayofuata ya Mtoano itakayokuwa na jumla ya timu 16.
Timu zitakazokuwa nafasi ya 3 toka kila Kundi zitaingizwa kwenye Kapu la Dro yenye Timu 32 kugombea Kombe la UEFA.
Mpaka sasa Timu 13 kati ya 16 tayari zimeshafuzu kuingia Raundi hiyo ya Mtoano.
Timu hizo 13 ni pamoja na Mabingwa Watetezi wa Kombe hili Manchester United, Liverpool, Inter Milan, Atletico Madrid, Villareal , Barcelona, Sporting Lisbon, Lyon, Bayern Munich, Arsenal, FC Porto, Juventus na Real Madrid.
Timu 3 zilizobaki zitakazokamilisha idadi ya Timu 16 moja itatoka Kundi B, ambako tayari Inter Milan kashafuzu, hivyo nafasi hiyo moja itaamuliwa kwenye mechi ya mwisho ya Jumanne kati ya Panathinaikos na Anorthosis Famagusta na mshindi ndie ataendelea.
Nafasi mbili za mwisho kukamilisha jumla ya Timu 16 ni za Timu za Kundi A ambamo kukiwa kumesalia mechi moja kwa kila Timu, AS Roma, anaongoza Kundi hili akiwa na pointi 9, Chelsea, ni wa pili akiwa na pointi 8 na Bordeaux wa tatu akiwa na pointi 7 huku CFR Cluj wa mwisho akiwa na pointi 4.Katika mechi za mwisho, AS Roma anamkaribisha Bordeaux na Chelsea atakuwa nyumbani Stamford Bridge kupambana na CFR Cluj. Timu mbili za juu toka Kundi hili zitaendelea.
Vilevile, mechi hizi za mwisho kwa baadhi ya Makundi zitaamua nani atashika nafasi ya uongozi na nani wa pili kitu ambacho ni muhimu sana kwenye upigaji kura timu zipi zinakutana kwenye Raundi hiyo ya Mtoano yenye jumla ya timu 16 zitakazopangwa kucheza nyumbani na ugenini kuanzia tarehe 24 na 25 Februari 2009.
Umuhimu huo unakuja kutokana na Timu iliyoshika uongozi kupangiwa kukutana na mshindi wa pili toka kundi jingine na kwamba timu zilizokuwa Kundi moja kwenye awamu ya Makundi na zile zinazotoka Nchi moja haziwezi kupangwa kukutana kwenye Raundi hiyo ya Mtoano.
Hivyo, kwenye Raundi ijayo, Man U, Arsenal, Liverpool na Chelsea haziwezi kukutana kwani zote zinatoka England.
Dro ya kuamua nani wanakutana kwenye Mtoano itafanyika tarehe 19 Desemba 2008.
KUNDI A
Kundi hili ndilo lenye kasheshe kubwa.
Mahesabu yake ni kwamba ni CFR Cluj pekee ndio imeshatolewa nje na ina uhakika wa kumaliza nafasi ya mwisho. Chelsea wanawakaribisha CFR Cluj hapo Jumanne.
Chelsea wanahitaji ushindi ili wasonge mbele ingawa wanaweza kusonga mbele hata wakifungwa endapo tu Bordeaux hawatowafunga AS Roma timu inayoongoza Kundi hili kwenye mechi itakayochezwa Rome, Italia.
Nao AS Roma wanaweza kusonga mbele hata kama wakifungwa ikiwa Chelsea atafungwa.
Bordeau hana ujanja. Lazima amfunge AS Roma ili asonge mbele.
KUNDI B
Inter Milan, ambao washafuzu, watashika uongozi Kundi hili wakiifunga Werder Bremen walio nafasi ya mwisho na ambao wanahitaji ushindi angalau wamalize wa tatu na kucheza Kombe la UEFA. Na hata huo ushindi unaweza usitosheleze kwa Werder Bremen kwani ikiwa Anorthosis Famagusta ya Cyprus ikiifunga Panathinaikos ya Ugiriki hukohuko Ugiriki basi Anorthosis Famagusta watasonga mbele na Panathinaikos watacheza UEFA.
Lakini droo kwa Panathinaikos ni vilevile nzuri kuwafanya wasonge mbele ingawa ushindi unaweza kuwapa nafasi ya kuongoza Kundi.
KUNDI C
Kila kitu kimekamilika toka Kundi hili huku Barcelona wako wa kwanza na Sporting Lisbon wako wa pili na ndio timu zinazosonga mbele.
Timu toka Ukraine Shakhtar Donetsk iko ya 3 na itacheza UEFA.
FC Basel ya Uswisi wako mkiani na nje ya mashindano na wanacheza mechi ya mwisho na Sporting Lisbon kukamilisha ratiba tu.
KUNDI D
Atletico Madrid na Liverpool wameshafuzu lakini nani ndie wa kwanza ndio kitaamuliwa kwenye mechi zao za Jumanne. Timu zote hizi zina pointi 11 lakini Atletico Madrid wanaongoza kwa tofauti ya magoli.
Atletico Madrid atacheza ugenini na Olympique de Marseille ambao wanahitaji ushindi ili wacheze UEFA.
Liverpool watakuwa wageni wa PSV Eindhoven ambao nao wanahitaji ushindi wa nguvu ili kuwapiku Marseille kucheza UEFA.
KUNDI E
Mabingwa Watetezi wa Kombe hili Manchester United wanaoongoza ingawa wako pointi sawa na Villareal, wote wakiwa wameshapita, wanawakaribisha Aaalborg ya Demark ambao nao washaingia UEFA CUP.
Man U wanajua wazi wakishinda mechi hii basi watashika uongozi Kundi hili labda Villareal aifunge Celtic magoli mawili zaidi ya yale Man U watawafunga Aalborg.
Celtic ya Scotland, timu iliyotupwa nje, itaikaribisha Villareal.
KUNDI F
Lyon wanawakaribisha Bayern Munich katika mechi itakayoamua nani anachukua hatamu za Kundi hili kwani timu zote zimeshafuzu.
Ushindi kwa Lyon au suluhu ya bila magoli itawapa uongozi Lyon.
Ili wacheze UEFA, wenyeji Steau Bucharest lazima wawafunge Fiorentina na matokeo mengine yeyote Fiorentina ataonja UEFA.
KUNDI G
Arsenal wanasafiri hadi Ureno kupambana na FC Porto na ingawa timu zote zimefuzu ni pambano ambalo litaamua nani ataongoza Kundi hili huku Arsenal anahitaji suluhu tu ili aongoze.
Nao Fenerbahce watasafiri hadi nyumbani kwa Dynamo Kiev na inabidi washinde ili wacheze UEFA.
KUNDI H
Juventus wanaongoza Kundi hili na wakicheza nyumbani wanahitaji sare tu katika mechi na timu iliyotupwa nje ya FC Bate.
Real Madrid, nao washafuzu ingawa wakishinda na Juventus akifungwa basi wao watashika hatamu.
Real anacheza na timu ya FC Zenit St Petersburg ambao sasa watacheza UEFA baada ya kukosa nafasi kusonga mbele na hii ni nafasi nzuri kwao kutetea Taji lao la UEFA kwani wao ndio Mabingwa wa UEFA CUP msimu uliopita.
RATIBA KAMILI NI:
Jumanne, 9 Decemba 2008
KUNDI A
Chelsea v CFR
Roma v Bordeaux,
KUNDI B
Werder Bremen v Inter Milan,
Panathinaikos v Anorthosis Famagusta,
KUNDI C
Barcelona v Shakhtar Donetsk,
Basle v Sporting,
KUNDI D
Marseille v Atletico Madrid,
PSV vLiverpool,
Jumatano, 10 Decemba 2008
KUNDI E
Celtic v Villarreal,
Man U v AaB,
KUNDI F
Steaua Bucuresti v Fiorentina
Lyon v Bayern Munich
KUNDI G
Dynamo Kiev v Fenerbahce,
FC Porto vArsenal,
KUNDI H
Juventus v BATE
Real Madrid v Zenit St Petersburg

Sunday 7 December 2008

RONALDO AKABIDHIWA TUZO YA 'Ballon d'Or'

Leo, mjini Paris, Ufaransa, nyota wa Mabingwa wa Uingereza na Ulaya, Manchester United, Cristiano Ronaldo, amekabidhiwa Tuzo inayotukuka ya Ballon d'Or, yaani 'MPIRA WA DHAHABU' inayoashiria yeye kwa sasa ndie MCHEZAJI BORA ULAYA.
Ronaldo, ambae vilevile ndie anaetegemewa sana kushinda Tuzo ya MCHEZAJI BORA WA DUNIA inayotolewa na FIFA, ameshashinda Tuzo ya MCHEZAJI BORA WA DUNIA YA FIFPRO ambayo hutolewa na Wachezaji wa Kulipwa.
Akipokea Tuzo hiyo, huku Mama yake Mzazi aitwae Maria na Meneja wa Klabu yake Sir Alex Ferguson wakiwepo [tizama picha] kwenye ghafla iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni, Ronaldo alitoa shukrani zake za dhati.
Sir Alex Ferguson alitoa nasaha zake kwenye ghafla hiyo kwa kusema: 'Cristiano, tunasikia fahari sana, wewe ni mfano bora kwa vijana wote duniani wanaokuja Manchester kutoka nje! Sasa endelea mazoezi ili ushinde, endeleza kipaji chako! Hongera! Endelea hivihivi!'
Nao Mameneja wa Chelsea, Felipe Scolari na wa Arsenal, Arsene Wenger, nao walipewa ruhusa ya kuongea kwa njia ya video.
Luis Felipe Scolari aliewahi kuwa Kocha wa Ronaldo kwenye Timu ya Taifa ya Ureno alisema: 'Hii ni tuzo yako ya kwanza kwa yote uliyofanya lakini sio ya mwisho. Hii itakuwa moja ya nyingi utakazopata kwenye historia yako.'
Arsene Wenger alisema wakati Ronaldo amesimama bega kwa bega na Ferguson kwenye ghafla hiyo: 'Una kipaji kikubwa sana! Nawapongeza nyote wawili kwani hii ni kazi ya pamoja.'

West Brom 1 Portsmouth 1

West Brom imefanikiwa kupata pointi moja baada ya kutoka suluhu leo na Portsmouth lakini bado ndio timu ya mwisho kwenye msimamo wa LIGI KUU ikiwa nafasi ya 20 na pointi 12 kwa mechi 16.
Nafasi ya 19 inashikwa na Blackburn ikiwa nayo imecheza mechi 16 na ina pointi 13.
Sunderland ni ya 18 kwa mechi 16 na pointi 15.
West Bromwich ilikuwa wa kwanza kupata bao wakati Nahodha wao Jonathan Greening alipofunga dakika ya 39 lakini Peter Crouch wa Portsmouth alisawazisha dakika ya 58 kwa shuti kali la mita kama 20 hivi.
Kimsimamo, Portsmouth wako nafasi ya 7 wamecheza mechi 16 na wana pointi 23.
Everton 2 Aston Villa 3
Ni mechi iliyoanza kwa bao la kwanza kupatikana sekunde 34 tu tangu mechi ianze!
Steve Sidwell, akipokea pasi kutoka kwa James Milner, alifumua mkwaju na kuipatia Aston Villa bao la kuongoza.
Dakika ya 30, wenyeji Everton wakasawazisha kupitia Beki wao John Lescott kufuatia fikikiki ya Arteta.
Kipindi cha pili dakika ya 54 Beki wa kutumainiwa wa Everton Phil Jagielka akiwa mtu wa mwisho kwenye safu ya ulinzi aligeuka na kurudisha mpira nyuma kwa Kipa wake Tim Howard bila ya kutazama kumbe alikuwa akitoa pasi murua kwa adui Winga Ashley Young ambae akaipa kilaini Aston Villa bao la pili.
Zikiwa dakika 90 zimekwisha na mechi iko kwenye dakika 3 za nyongeza, John Lescott tena akaisawazishia Everton baada ya krosi ya Jagielka kumkuta Cahill aliempasia mfungaji Lescott aliefunga goli zuri sana dakika ikiwa ya 92.
Dakika ya 93, Ashley Young akaipa bao la ushindi Aston Villa baada ya defensi ya Everton kujikoroga yenyewe.
Mabingwa Man U washinda kwa mbinde: Beki Vidic apachika bao la ushindi dakika za majeruhi!!!

Goli lililofungwa na Nemanja Vidic, Beki pacha na Rio Ferdinand, kwenye dakika ya 90 ya mchezo, liliwapa ushindi wa bao 1-0 Mabingwa Man U wakiwa nyumbani Old Trafford wakicheza na Sunderland timu ambayo haina Meneja baada ya Roy Keane kuitema na ambayo kwa sasa iko nafasi za mwisho kabisa kwenye msimamo wa LIGI KUU.
Nae Meneja wa Man U, Sir Alex Ferguson, alishuhudia mechi hii akiwa amekaa jukwaani [pichani akiwa amekaa nyuma ya Mkurugenzi na Mchezaji wa zamani wa Man U Sir Bobby Charlton] kwa Watizamaji ikiwa ni kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi 2 na hivyo kutoruhusiwa kukaa benchi la timu yake baada ya kufarakana na Refa Mike Dean wakati Man U ilipocheza na Stoke.
Hii ilikuwa mechi yake ya pili ya kifungo.
Wimbi baada ya wimbi la mashambulizi kwa dakika zote za mchezo hazikuzaa goli kwani Wachezaji karibu wote wa Sunderland walijikita mbele ya penalti boksi yao kujihami.
Wenyewe Wazungu wanaita 'Timu imepaki basi mbele ya mlango wao'.
Katika mechi nzima Man U walipiga jumla ya mashuti 23 golini na Sunderland hawakupiga hata moja.

Man U walipata kona 10 na Sunderland walipata 1 tu na ambayo ndiyo ilisababisha kifo chao.
Kona hiyo pekee waliyopata Sunderland dakika ya 89 ilizuiwa na ukuta wa Man U na huku Wachezaji wengi wa Sunderland wakiwa wamepanda golini kwa Man U ili kuongeza mashambulizi, Man U walifanya shambulizi la haraka na Kiungo Michael Carrick akiwa nje ya boksi alipiga shuti lilombabatiza Collin Edwards, kumpita Kipa, na kugonga posti chini na kurudi ndani na mpira kumkuta Beki Nemanja Vidic aliushindilia wavuni.
Man U walimiliki mpira kwa asilimia 78 na Sunderland asilimia 28 tu!

Wataalam wa LIGI KUU wameielezea mechi hii kuwa ni ya upande mmoja sana kiasi ambacho haijawahi kutokea ingawa cha kushangaza ni kukosekana lundo la magoli.
Katika mechi hii Mabingwa Man U walipata pigo pale Mchezaji wao Bora wa Ulaya Ronaldo alipoumia na ikabidi atoke nje ya uwanja kwenye dakika ya 68.
Ingawa Man U hawakupata ushindi wa kishindo lakini kupata pointi 3 kwao ni jambo bora kwani linawafanya bado wawe karibu sana na vinara wa ligi Liverpool na Chelsea.
Msimamo mpaka sasa ni:
Liverpool: mechi 16 pointi 37
Chelsea: mechi 16 pointi 36
Man U: mechi 15 pointi 31
Arsenal: mechi 16 pointi 29
MECHI ZA LEO:
Jumapili, 7 Decemba 2008
[saa 12 jioni] West Brom v Portsmouth
[saa 1 usiku]Everton v Aston Villa

Saturday 6 December 2008

LIGI KUU: Wakubwa washinda!!

Timu zinazoaminika ndio 'Wakubwa', yaani Liverpool, Chelsea na Arsenal, zote zimepata ushindi kwenye mechi zao za LIGI KUU za leo na Mabingwa wenyewe, Manchester United, watashuka uwanjani kwake Old Trafford muda si mrefu kuanzia sasa kuwakaribisha Sunderland ambao hawana Meneja baada ya Nahodha wa zamani wa Man U, Roy Keane, kubwaga manyanga.

MATOKEO YA MECHI ZA LEO NI:

Arsenal 1-0 Wigan

Blackburn 1-3 Liverpool

Bolton 0-2 Chelsea

Fulham 1-1 Man City

Hull 2-1 Middlesbrough

Newcastle 2-2 Stoke
CARLING CUP: NUSU FAINALI= Burnley v Tottenham na Derby v Man United

Dro ya Nusu Fainali ya Kombe la Carling imefanyika na Timu ya Daraja la chini ya LIGI KUU ambayo mpaka sasa imeshawatoa kwenye muchuano hiyo Timu za vigogo za LIGI KUU za Fulham, Chelsea na Arsenal wamepangiwa kigogo mwingine wa LIGI KUU Tottenham ambao pia ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo.
Nao Derby County, timu nyingine ya Daraja la chini ya LIGI KUU, itapambana na Mabingwa wa LIGI KUU Manchester United.
Nusu Fainali ya Kombe hili zitachezwa kwa mikondo miwili, nyumbani na ugenini, na mechi ya kwanza itachezwa wiki inayoanzia Januari 5, 2009 na marudiano wiki inayoanza Januari 19, 2009.
Fainali itachezwa tarehe 1 Machi 2009.
EVRA AFUNGIWA MECHI 4 NA FAINI PAUNI 15,000!!!

Beki wa pembeni kushoto wa Mabingwa Manchester United Patrice Evra amefungiwa mechi 4 na kupigwa faini ya Pauni ya 15,000 baada ya FA kumwona ana hatia ya kupigana na Mkata Majani wa Chelsea, Sam Bethell, kosa lililotendeka Stamford Bridge mara tu baada ya mechi ya Man U na Chelsea mnamo tarehe 26 Aprili 2008.
Kufuatia adhabu hii ambayo ataanza kuitumikia Desemba 22 na ambayo Klabu yake Man U wametamka bado wanaitafakari na watajua hivi karibuni nini wafanye, Evra atazikosa mechi za LIGI KUU dhidi ya Stoke, ikifuatiwa na ya Middlesbrough kisha ya Southampton kugombea Kombe la FA na ya mwisho ni mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la CARLING.

Baada ya kifungo hicho, Evra anaweza kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Chelsea kwenye LIGI KUU hapo Januari 11, 2009.
Klabu ya Chelsea nayo imepigwa faini ya Pauni 25,000 kwa kushindwa kumdhibiti mfanyakazi wao Sam Bethell.


SAKATA LA MIDO KUBAGULIWA: Wawili wabambwa na Polisi kutua kortini Jumanne!

Watu wawili wenye umri ya miaka 49 na 23 wanashikiliwa na Polisi kwa kutuhuma za kutoa matusi ya kibaguzi dhidi ya Mchezaji kutoka Misri Mido anaechezea Middlesbrough kwenye mechi dhidi ya Newcastle hapo tarehe 29 Novemba 2008 na watafikishwa Mahakamani Jumanne ijayo.
Mido alilalamika vikali kushambuliwa na Washabiki wa Newcastle kwa misimu miwili mfululizo kibaguzi bila FA kuchukua hatua yeyote.

Friday 5 December 2008

UEFA CUP: Portsmouth yatolewa nje!, Aston Villa yafungwa lakini yasonga mbele!!

Portsmouth imetwangwa mabao 3-2 na Wolfsburg ya Ujerumani na hivyo kutolewa nje ya Kombe la UEFA.
Aston Villa nao walifungwa mabao 2-1 na MSK Milina lakini wamemudu kusonga mbele kutoka kwenye Kundi lake baada ya Hamburg kuwafunga Slovakia Prague 2-0.
Aston Villa sasa wanaungana na Manchester City kuingia Raundi nyingine.

RATIBA YA LIGI KUU WIKIENDI HII:

Jumamosi, 6 Decemba 2008

[saa 9 dak 45 mchana]

Fulham v Man City

[saa 12 jioni]

Arsenal v Wigan

Blackburn v Liverpool

Bolton v Chelsea

Hull v Middlesbrough

Newcastle v Stoke

[saa 2 na nusu usiku]

Man U v Sunderland

Jumapili, 7 Decemba 2008

[saa 12 jioni]

West Brom v Portsmouth

[saa 1 usiku]

Everton v Aston Villa

Jumatatu, 8 Decemba 2008

[saa 5 usiku]

West Ham v Tottenham

Thursday 4 December 2008

ROY KEANE ANG'OKA SUNDERLAND!

Kukiwa kumebaki siku mbili tu kabla Meneja Roy Keane [37] hajaipeleka timu yake Sunderland Old Trafford kukutana na Bosi wake wa zamani Sir Alex Ferguson wa Manchester United ambako Keane alikuwa Mchezaji na Nahodha mwenye sifa za kipekee, Roy Keane ameamua kuachana na Sunderland.
Roy Keane alianza kazi ya Umeneja Sunderland Agosti 2006 na akaifanya Sunderland iwe Bingwa wa COCA COLA LIGI na kuipandisha LIGI KUU msimu uliofuatia.
Keane aliwanunua Djibril Cisse, Pascal Chimbonda, Anton Ferdinand, El-Hadji Diouf na George McCartney kwa jumla ya Pauni Milioni 30 lakini mbali ya kucheza mechi 15 za LIGI KUU timu hiyo imeshinda mechi 4 tu na wako nafasi ya 18, yaani watatu toka chini!
Powered By Blogger