Sunday 6 July 2008

KAKAYE YOBO ATEKWA KWAO NIGERIA!
Kaka mkubwa wa Mchezaji wa Taifa wa Nigeria na Everton ya Uingereza Joseph Yobo ametekwa nyara na watu wenye silaha nje ya hoteli moja mjini Port Harcourt, Nigeria.
Hakuna kikundi chochote au mtu yeyote aliejitokeza kudai kuhusika au kudai fedha ili Norum Yobo aachiwe huru.
Klabu yake Joseph Yobo, Everton, imesema itafanya kila iwezalo ili kumsaidia mchezaji wake ambae kwa sasa yuko mapumzikoni mjini Lagos, Nigeria.

Utekaji nyara katika upande huo wa Nigeria, ambao ni tajiri kwa uchimbaji mafuta ingawa wananchi wake ni masikini, ni kitu cha kawaida lakini hasa huhusisha wafanyakazi raia wa kigeni waliojiriwa na kampuni za mafuta.
Powered By Blogger