Friday 27 March 2009

Uchambuzi wa Mechi za Mchujo za wiki hii Kombe la Dunia za Mataifa ya Ulaya, Marekani ya Kusini na Afrika.

ULAYA:
Wakati LIGI KUU England iko mapumzikoni wikiendi hii, Timu za Mataifa ya Ulaya zitaingia uwanjani kutafuta wawakilishi watakaokwenda Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Mataifa hayo ya Ulaya yamegawanywa kwenye Makundi 9 na ufuatao ni uchambuzi wa kila Kundi:
KUNDI 1
Inaelekea aliekuwa Meneja Msaidizi wa Manchester United, Carlos Queiroz, ambae sasa ni Meneja wa Timu ya Taifa ya Nchi yake Ureno yuko kwenye hali ngumu na hatari kubwa ya kukosa kibarua.
Katika Kundi hili, Ureno imeshinda mechi moja tu dhidi ya wadhaifu Malta na kufungwa na Denmark, kutoka suluhu na Sweden pamoja na Albania, na sasa wako nafasi ya nne kwenye Kundi.
Jumamosi, Ureno wataivaa Sweden huku wanaoongoza Kundi hili Denmark watakuwa wageni wa wadhaifu Malta.
KUNDI 2
Greece ndio wanaoongoza Kundi hili ingawa walipigwa 2-1 na Switzerland mechi iliyopita.
Mechi za Jumamosi ni Luxemborg v Latvia, Moldova v Switzerland, Israel v Greece.
Jumatano, Aprili 1 ni Latvia v Luxemborg, Switzerland v Moldova, Greece v Israel.
KUNDI 3
Slovakia wanaongoza Kundi hili lakini hawachezi Jumamosi na badala yake wana mechi ya kirafiki siku hiyo dhidi ya England huko Wembley.
Timu nyingine Kundini ni Northern Ireland, Poland, Slovenia, Czech Republic na San Marino.
KUNDI 4
Germany wanaongoza wakifuatiwa na Russia, Wales, Finland, Azerbaijan na Liechstenstein.
Mechi za Jumamosi ni Wales v Finland, Russia v Azerbaijan, Germany v Liechstenstein.
Jumatano ni Liechstenstein v Russia na Wales v Germany.
KUNDI 5
Spain ndiyo Timu Bora Duniani katika msimamo wa FIFA na ndio wanaoongoza Kundi hili likiwa na Timu za Turkey, Belgium, Armenia, Estonia na Bosnia-Herzegovina.
KUNDI 6
England ni vinara Kundini baada ya kushinda mechi zao zote za mwanzo.
Kwa sababu isiyojulikana, Kundi hili halina mechi Jumamosi na badala yake wanacheza Jumatano ijayo wakati England atacheza na Ukraine, Kazakhstan v Belarus, Andorra v Croatia.
KUNDI 7
Serbia na Lithuania zimefungana kileleni wakiwa na pointi 9 na kucheza mechi 4 kila mmoja huku Austria akiwa wa tatu akiwa na pointi 4 kwa mechi 4.
France na Romania, zote zimecheza mechi 3, wanafuata wakiwa na pointi 3 kila mmoja.
Jumamosi ni Lithuania v France na Romania v Serbia wakati Jumatano ni France v Lithuania na Austria v Romania.
KUNDI 8
Italy na Republic of Ireland ndio vinara wa pamoja wakiwa wote sawa kwa kuwa na pointi 10 lakini Italy yuko mbele kwa kuwa na tofauti ya magoli bora.
Wanafuatia Bulgaria wenye pointi 3, Montenegro na Georgia pointi 2 na mkiani ni Cyprus wenye pointi moja tu.
Jumamosi ni Ireland v Bulgaria, Cyprus v Georgia, Montenegro v Italy.
Jumatano ni Italy v Ireland, Bulgaria v Cyprus, Georgia v Montenegro.
KUNDI 9
Holland ni vinara baada ya kushinda mechi zao zote 3 wakifuatiwa na Scotland wenye pointi 4.
Jumamosi ni Holland v Scotland na Jumatano ni Scotland v Iceland, Holland v Macedonia.
AFRIKA:
Hii ni Raundi ya Tatu katika mchujo wa Mataifa ya Afrika kupata wawakilishi watano watakaojumuika na Mwenyeji Afrika Kusini Fainali za Kombe la Dunia 2010.
Raundi hii, Nchi zimegawanywa kwenye Makundi Matano ya Nchi nne kila moja na atakaemaliza Kinara kila Kundi atafuzu kuingia Fainali Kombe la Dunia.
Makundi na mechi zake zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili hii ni kama ifuatavyo :
KUNDI A: Togo, Cameroun, Morocco, Gabon
Togo v Cameroun na Morocco v Gabon
KUNDI B: Mozambique, Nigeria, Kenya, Tunisia
Kenya v Tunisia na Mozambique v Nigeria
KUNDI C: Rwanda, Algeria, Egypt, Zambia
Rwanda v Algeria na Egypt v Zambia
KUNDI D: Ghana, Benin, Sudan, Mali
Ghana v Benin na Sudan v Mali
KUNDI E: Ivory Coast, Malawi, Burkina Faso, Guinea
Ivory Coast v Malawi na Burkina Faso v Guinea
MAREKANI KUSINI:
Marekani Kusini kuna Kundi moja tu lenye Nchi 10 na Timu nne za kwanza zitaingia moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia 2010 huku Timu iliyo nafasi ya 5 itakwenda kucheza na Timu kutoka Kundi la Marekani ya Kati ili kupata mshindi atakaesonga mbele.
Hadi sasa baada ya kila Nchi kucheza mechi 10, Paraguay ndio vinara wakiwa na pointi 23, Brazil ni nafasi ya pili akiwa na pointi 17, Argentina na Chile ni nafasi ya tatu wote wakiwa na pointi 16 kila mmoja, nafasi ya nne ni Uruguay pointi 13, Ecuador pointi 12, Colombia pointi 11, Venezuela 10, Bolivia 9 na wa mwisho ni Peru akiwa na pointi 7 tu.
Mechi zinazofuata ni:
Jumamosi: Uruguay v Paraguay, Argentina v Venezuela na Colombia v Bolivia.
Jumapili: Ecuador v Brazil na Peru v Chile
Jumanne: Venezuela v Colombia
Jumatano: Bolivia v Argentina, Ecuador v Paraguay, Chile v Uruguay na Brazil v Peru
Mama Mzazi na Mama Mkwe wa John Terry waonywa na Polisi kwa 'udokozi' Madukani!!!!!

Familia ya Nahodha wa Chelsea na Timu ya Taifa ya England, John Terry, imekumbwa na fedheha pale Polisi walipothibitisha kuwa Bibi Sue Terry [50], ambae ni Mama Mzazi wa John Terry na Bibi Sue Poole [54], Mama Mkwe wa Mchezaji huyo, wamepewa onyo baada ya kukiri tuhuma za udokozi kwenye Maduka mawili makubwa ya Marks & Spencer na la Tesco yaliyopo Weybridge, Surrey.
Inasemekana John Terry amewanunulia kina Mama hao Nyumba huko Surrey na yeye mwenyewe na Mkewe wanaishi pia maeneo hayo.
Lakini, Mwanasheria wa John Terry amedai kina Mama hao walikubali kosa la udokozi huo huko Polisi kimakosa na yeye sasa yuko kwenye harakati za kusafisha majina yao.

Refa afyatua Kadi Nyekundu 18 katika Mechi moja!!!!!

Huko Argentina, kwenye mechi ya Primera C, yaani mechi ya Timu za Daraja la 3, kati ya wenyeji Barracas Bolivar na wageni General Lamadrid, Refa alitoa Kadi Nyekundu 18 katikati ya kipindi cha pili cha mechi baada ya kutokea fujo na ngumi uwanjani.
Huku wenyeji Barracas Bolivar wakiongoza 3-0, mashabiki wa timu hiyo walikuwa wakiwazomea na kuwakejeli General Lamadrid, ndipo Wachezaji watatu wa Lamadrid na Watu wanne wa benchi la ufundi wakaanza kuzozana na mashabiki hao.
Mzozo huo ukazua ngumi na mapigano makali kati ya Wachezaji wote 11 wa Lamadrid wakisaidiwa na Wachezaji 7 wa akiba.
Fujo hizo zilisimama pale tu Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia walipoingilia na ndipo Refa wa mechi hiyo akawalamba Wachezaji wote 11 wa General Lamadrid Kadi Nyekundu na kuongeza Kadi nyingine Nyekundu 7 kwa Wachezaji wote wa Akiba wa timu hiyo.
Sasa itabidi Klabu ya General Lamadrid ichezeshe Wachezaji wa Akiba na Timu ya Vijana kwenye mechi ifuatayo ya Ligi.

Beckham asema kuvunja rekodi si kusudio lake, kuipeleka England Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini 2010 ndio lengo lake!!!!!

David Beckham, ambae yeye na Mchezaji wa zamani Bobby Moore, ndio wanashikilia rekodi ya kuchezea England mechi nyingi kwa kucheza mechi 108 kwa Wachezaji wa mbele [Rekodi ya mechi nyingi inashikiliwa na Kipa Peter Shilton aliechezea mechi 125], amesema yeye anachotaka ni kuiona England Fainali Kombe la Dunia mwaka 2010 huko Afrika Kusini.
Beckham ambae yumo kwenye Kikosi cha England kinachofanya mazoezi kwa mechi ya kirafiki ya Jumamosi dhidi ya Slovakia na ile ya mchujo Kombe la Dunia hapo Jumatano dhidi ya Ukraine atafikisha mechi 109 akicheza Jumamosi na hivyo kumpita Sir Bobby Moore.

Thursday 26 March 2009

Meneja wa England, Fabio Capello, amwita Rooney mwehu!!!

Kwenye kambi ya mazoezi ya Kikosi cha Timu ya England kinachojitayarisha kwa mechi ya kirafiki ya Jumamosi watakapocheza na Slovakia na ile ya mchujo wa Kombe la Dunia dhidi ya Ukraine ya Jumatano, Fabio Capello alimwita kwa mzaha Rooney: 'Kwa nini ulipiga ngumi kibendera cha kona? Wewe ni mwehu, ni mtu mwehu!!'
Capello anadaiwa kusema maneno hayo akimaanisha kitendo cha Rooney alichokifanya mara baada ya kupewa Kadi Nyekundu na Refa Phil Dowd kwenye mechi ambayo Man U ilifungwa 2-0 na Fulham.
Inasemekana vilevile, Capello alifanya mazungumza ya undani na Ashley Cole wa Chelsea na Steven Gerrard wa Liverpool ambao wote walikwaruzana na Polisi huku Cole akipata onyo kwa ulevi na ubishi toka kwa Polisi lakini Gerrard mpaka sasa yuko Mahakamani akikabiliwa na kesi dhidi yake.
Inaelekea nia ya Capello ni kutaka kudumisha nidhamu kwa Wachezaji wake Mastaa tegemezi ili wahakikishe England inafuzu Fainali za Kombe la Dunia 2010 huko Afrika Kusini.
England mpaka sasa ni kinara kwenye Kundi lake la mchujo akiwa juu ya Croatia, Ukraine, Belarus, Kazakhstan na Andorra akiwa na pointi 12 kwa mechi nne huku Croatia na Ukraine ambao wamefungana nafasi ya pili wana pointi 7.

Marefa England wataka ufafanuzi kwanini Kadi zao Nyekundu zinafutwa na FA!!!

Bodi ya Marefa wa Kulipwa wa England (PGMO) kimeitaka FA England itoe ufafanuzi ni sababu gani na vipengele vipi vimeifanya kufuta baadhi ya Kadi Nyekundu zinazotolewa kwenye mechi za LIGI KUU England.
Hivi juzi Kadi Nyekundu walizotwangwa Kipa Brad Friedel wa Aston Villa na Mlinzi wa Sunderland George McCartney zilifutwa na FA baada ya rufaa ya klabu zao.

Man U kucheza AUDI CUP huko Ujerumani!!

Mabingwa wa England, Ulaya na Dunia, Manchester United, wamealikwa na Kampuni ya Magari aina ya Audi ya Ujerumani kucheza kwenye Kombe lao majira ya joto yajayo na wataungana na Klabu machachari ya zamani ya Diego Maradona, Boca Juniors ya Argentina, AC Milan ya Italy na Bayern Munich ya Ujerumani.
Man U watapambana na Boca Juniors tarehe 29 Julai 2009 na siku hiyo hiyo Bayern Munich itaikwaa AC Milan.
Washindi wa mechi hizo watacheza Fainali tarehe 30 Julai 2009 huku mechi hiyo ikitanguliwa na waliofungwa mechi za utangulizi ili kupata Mshindi wa Tatu.

Wednesday 25 March 2009

Ledley King ajitoa Kikosi cha Timu ya England


Nahodha wa Tottenham Hotspurs, Ledley King, amejiondoa kweye Kikosi cha England ambacho kiko kambini kwa matayarisho ya mechi ya kirafiki na Slovakia hapo Jumamosi na ile ya mchujo wa Kombe la Dunia 2010 ya Jumatano dhidi ya Ukraine.
Kuteuliwa kwa Ledley King kulimkera sana Meneja wa Tottenham, Harry Redknapp, ambae amesema King ana ubovu wa goti na hivyo huwa hawezi kucheza mechi mbili kwa wiki na wao kama Klabu humpa mazoezi na mapumziko maalum ili angalau aweze kucheza moja kwa wiki.


FA England yafuta Kadi Nyekundu kwa Friedel na McCartney lakini Rooney atatumikia kifungo cha mechi moja!!!!


Kipa wa Aston Villa, Brad Friedel, na Mlinzi wa Sunderland, George McCartney, wamefutiwa Kadi Nyekundu zao baada ya FA kuona hamna uhalali baada ya Klabu zao kukata rufaa.
Brad Friedel alipewa Kadi Nyekundu wakati Timu yake Aston Villa ilipopewa kipigo cha 5-0 na Liverpool na kama ingesimama hivyohivyo basi angeikosa mechi na Manchester United hapo Aprili 5.
George McCartney aliikumba Kadi yake kwenye mechi Sunderland aliyofungwa 1-0 na Manchester City.
Na FA imethibitisha Wayne Rooney hatochukuliwa hatua yeyote zaidi ya kuikosa mechi na Aston Villa hapo Aprili 5 baada ya kulambwa Kadi 2 za Njano na hivyo kupewa Kadi Nyekundu walipofungwa bao 2-0 na Fulham mechi iliyopita.

Tuesday 24 March 2009

MECHI ZA KIMATAIFA ZENYE MVUTO ZA KOMBE LA DUNIA 2010 JUMAMOSI NA JUMATANO!!!

Wikiendi hii na Jumatano ijayo ni siku za mechi za Kimataifa kuwania nafasi za kuingia Fainali Kombe la Dunia 2010 huko Afrika Kusini.
Hivyo LIGI KUU England itasimama kupisha mechi hizo na ligi hii itarudi tena Jumamosi tarehe 4 Aprili 2009.
Timu ya Taifa ya England Jumamosi hii itacheza mechi ya kirafiki na Timu ya Slovakia Uwanjani Wembley na Jumatano hapohapo Wembley itachuana na Ukraine kwenye michujo ya Kombe la Dunia.
Baadhi ya mechi zenye mvuto za vigogo wa Ulaya ni:
Jumamosi, Machi 28
Holland v Scotland
Lithuania v France
Germany v Liechtenstein
Montenegro v Italy
Portugal v Sweden
Spain v Turkey
Jumatano, Aprili 1
Denmark v Albania
England v Ukraine
France v Lithuania
Holland v Macedonia
Turkey v Spain
Wales v Germany
HUKO MAREKANI KUSINI, Mechi za vigogo Brazil na Argentina:
Jumamosi, Machi 28
Argentina v Venezuela
Ecuador v Brazil
Jumatano, Aprili 1
Bolivia v Argentina
Brazil v Peru
NAYO LIGU KUU England itaibuka tena tarehe 4 Aprili 2009 kwa mechi zifuatazo:
Jumamosi, Aprili 4
Arsenal v Man City
Blackburn v Tottenham
Bolton v Middlesbrough
Fulham v Liverpool
Hull v Portsmouth
Newcastle v Chelsea
West Brom v Stoke
West Ham v Sunderland
Jumapili, April 5
Everton v Wigan
Man U v Aston Villa

Monday 23 March 2009

MECHI ZA KIMATAIFA Jumamosi na Jumatano ijayo

Wikiendi hii, LIGI KUU England itasimama kuzipisha mechi za Kimataifa za Kirafiki na pia mechi za Mtoano kuwania kuingia Fainali Kombe la Dunia 2010.
England Jumamosi Uwanja wa Wembley watacheza na Slovakia katika mechi ya kirafiki na Jumatano ijayo watamenyena na Ukraine kwenye mechi ya Kombe la Dunia.
Meneja wa England, Fabio Capello, ameteua Kikosi cha England kama kinavyoonyeshwa hapo chini.

Kikosi cha England:
Makipa: David James (Portsmouth), Robert Green (West Ham United), Ben Foster (Manchester United)
Walinzi: Leighton Baines (Everton), Phil Jagielka (Everton), Joleon Lescott (Everton), Ashley Cole (Chelsea), John Terry (Chelsea), Rio Ferdinand (Manchester United), Glen Johnson (Portsmouth), Matthew Upson (West Ham United), Ledley King (Tottenham Hotspur).
Viungo: Gareth Barry (Aston Villa), Michael Carrick (Manchester United), Frank Lampard (Chelsea), Stewart Downing (Middlesbrough), David Beckham (AC Milan), Shaun Wright-Phillips (Manchester City), Aaron Lennon (Tottenham Hotspur), Steven Gerrad (Liverpool).
Washambuliaji: Carlton Cole (West Ham United), Peter Crouch (Portsmouth), Emile Heskey (Aston Villa), Wayne Rooney (Manchester United).

Sunday 22 March 2009

Liverpool 5 Villa 0!!!

Ndani ya Anfield, leo Liverpool wamewanyemelea Manchester United na kuwa pointi moja tu nyuma yao ingawa Mabingwa hao wana mechi moja mkononi, baada ya kuwashindilia Aston Villa bao 5-0.

MATOKEO MECHI NYINGINE ZA LEO:

Manchester City 1 Sunderland 0

Wigan 1 Hull City 0
Ferguson ajuta kuteleza, akiri ukifungwa mechi Machi na Aprili ni balaa kwako. Hodgson wa Fulham atabiri Man U Bingwa!
Wenger kwake kibarua milele!!!


Sir Alex Ferguson, baada ya kupigwa mara mbili mfululizo na Liverpool 4-1 na Fulham 2-0, amesema ukifungwa kwenye Ligi mwezi Machi na Aprili ni balaa na unakuwa kwenye hatihati ya kupoteza matumaini ya kunyakua Ubingwa.
Ingawa Manchester United wako pointi 4 mbele ya Chelsea huku wakiwa na mechi moja mkononi, leo Liverpool anacheza na Aston Villa na wakishinda watakuwa pointi moja tu nyuma yao.
Wakati Ferguson akilalama kuhusu Refa Phil Dowd kuwabamiza Paul Scholes na Wayne Rooney Kadi Nyekundu, Meneja wa Fulham, Roy Hodgson, amesisisitiza: 'Tumezifungua upya mbio za Ubingwa! Lakini ukiniuliza, ni Manchester United ndio watatwaa Ubingwa!!!'
Bosi mpya wa Arsenal, Mkurugenzi Mtendaji, Ivan Gazidis, alietwaa hatamu siku chache zilopita, amesisitiza Meneja Arsene Wenger kibarua chake ni cha kudumu milele.
Tamko hilo limekuja ili kuwapa moyo Arsenal ambao hawajashinda Kombe lolote tangu Mei 2005 waliponyakua FA CUP.
Gazidis amesisitiza: 'Nataka Wenger adumu! Ni Meneja bora na anajenga timu bora!'
Powered By Blogger