Saturday 16 May 2009

BINGWA KAPATIKANA ILA KIMBEMBE NANI ANASHUSHWA DARAJA?

Wakati leo Manchester United amenyakua Ubingwa wa LIGI KUU England, Hull City kajichomoa toka eneo la hatari la kushuka Daraja na kumrudisha Newcastle katika eneo hilo, Middlesbrough ndio anachungulia kushushwa pamoja na West Bromwich!

Hull City akicheza ugenini Reebok Stadium ametoka suluhu na Bolton ya bao 1-1 na anaweza kupona kwenye mechi yake ya mwisho atakapowakaribisha Mabingwa Manchester United kwake KC Stadium kwenye mechi ya mwisho ya ligi.

Middlesbrough yuko kwenye mashaka makubwa baada ya kutoka sare 1-1 na Aston Villa na bado wako nafasi ya pili toka mkiani na hata wakishinda mechi yao ya mwisho bado wanahitaji wengine wawasaidie ili wapone.

Newcastle wakiwa nyumbani walifungwa 1-0 na Fulham na sasa wameporoka kwenda nafasi ya 18. Mechi yao ya mwisho ni ya ugenini watakapocheza na Aston Villa.

Msimamo kwa Timu za chini ni: [TIMU ZILIZO NAFASI YA 18 HADI 20 NDIZO HUSHUSHWA]

-Nafasi ya 13: Bolton pointi 41

-Nafasi ya 14: Blackburn pointi 40

-Nafasi ya 15: Portsmouth pointi 38

-Nafasi ya 16: Sunderland pointi 36

-Nafasi ya 17: Hull City pointi 35

-Nafasi ya 18: Newcastle pointi 34

-Nafasi ya 19: Middlesbrough pointi 32

-Nafasi ya 20: West Brom pointi 31

MANCHESTER UNITED BINGWA kwa mara nyingine tena!!!!!!
WATWAA LIGI KUU ENGLAND KWA MARA YA 11!!!!


  • WAIFIKIA REKODI YA LIVERPOOL YA KUWA BINGWA MARA 18!!!!
  • NI TIMU YA KWANZA KUTWAA LIGI KUU MARA 3 MFULULIZO!!!!
Mabingwa Watetezi wa LIGI KUU England, Manchester United, leo nyumbani kwao Old Trafford wametoka suluhu na Arsenal kwa bao 0-0 na kutwaa Ubingwa wa LIGI KUU kwa msimu wa mwaka 2008/9 huku wakiwa na mechi moja mkononi.
Manchester United, wakicheza chini ya kiwango, wamefikisha pointi 87 ambazo haziwezi kufikiwa na Timu yeyote ingawa ligi inamalizika wiki ijayo tarehe 24 mei 2009.
Vikosi vilikuwa:
Man Utd: Van der Sar, O'Shea, Vidic, Evans, Evra, Ronaldo, Fletcher, Carrick, Giggs, Rooney (Anderson 90), Tevez (Park 67).
Akiba hawakucheza: Kuszczak, Neville, Berbatov, Scholes, Rafael Da Silva.
Arsenal: Fabianski, Sagna, Toure, Song Billong, Gibbs (Eboue 76), Nasri (Bendtner 69), Denilson, Diaby, Fabregas, Arshavin (Walcott 69), van Persie.
Akiba hawakucheza: Mannone, Vela, Ramsey, Silvestre.
Kadi: van Persie, Arshavin, Fabregas, Nasri, Song Billong.
Watazamaji: 75,468
Refa: Mike Dean

MECHI ZA MOTO: Timu zenye balaa ya kushushwa Daraja!!!

Kumebaki mechi 2 kwa kila Timu na mbali ya vita ya kupata Bingwa kati ya Manchester United na Liverpool ambayo Mabingwa Watetezi Man U wanahitaji pointi moja tu kutwaa Ubingwa huo kwa mara ya 3 mfululizo katika mechi yao ya leo Old Trafford na Arsenal, vita kubwa ipo kwenye Timu zinazopigana kujinusuru kushushwa Daraja.

Msimamo kwa Timu za chini ambazo zinapigana kupona kushushwa daraja ni: [TIMU ZILIZO NAFASI YA 18 HADI 20 NDIZO HUSHUSHWA]

-Nafasi ya 13: Bolton pointi 40
-Nafasi ya 14: Blackburn pointi 40
-Nafasi ya 15: Portsmouth pointi 38
-Nafasi ya 16: Sunderland pointi 34
-Nafasi ya 17: Newcastle pointi 34
-Nafasi ya 18: Hull City pointi 34
-Nafasi ya 19: Middlesbrough pointi 31
-Nafasi ya 20: West Brom pointi 31

Mechi muhimu sana katika vita hiyo ni:
-Bolton v Hull City [REEBOK STADIUM]
Bolton wako 'salama' kwenye nafasi ya 13 na pointi 40 na Hull City wamekalia kuti kavu kwenye nafasi ya 18 wakiwa na pointi 34.
Lakini leo Hull City watashushwa Daraja ikiwa watafungwa na Bolton, Newcastle akiwafunga Fulham na Sunderland akitoka suluhu na Portsmouth siku ya Jumatatu usiku.
-Middlesbrough v Aston Villa [RIVERSIDE STADIUM]
Middlesbrough atashushwa Daraja wakishindwa kuifunga Aston Villa na mechi za Newcastle v Fulham na ile ya Bolton v Hull City zikaisha suluhu.
-Newcastle v Fulham [ST JAMES PARK]
Hatima ya Newcastle iko mikononi mwao. Wakishinda mechi zao 2 zilizosalia watanusurika kushushwa. Lakini kama hawashindi leo na Hull City wakiwafunga Bolton leo basi wataporomoshwa hadi nafasi ya 18 na hilo ni eneo hatari la kuporomoshwa Daraja.
-Portsmouth v Sunderland [Jumatatu usiku, FRATTON PARK]
Inawezekana ikifika hiyo Jumatatu Portsmouth atakuwa ameshanusurika hata bila ya kucheza mechi ikiwa Hull City au Newcastle wakifungwa.
Ikiwa Newcastle na Hull City wakishinda leo Sunderland ndio atavutwa shati hadi lile eneo hatari la kushushwa Daraja.
-West Bromwich v Liverpool [Jumapili, HAWTHORNS STADIUM]
West Brom hana njia mbili. Ni lazima ashinde mechi hii na aombe matokeo mengine yamsaidie yeye.

Friday 15 May 2009

RATIBA LIGI KUU ENGLAND:

Jumamosi, 16 Mei 2009
[saa 8 dak 45 mchana]
Man U v Arsenal
[saa 11 jioni]
Bolton v Hull
Everton v West Ham
Middlesbrough v Aston Villa
Newcastle v Fulham
Stoke v Wigan
Tottenham v Man City
Jumapili, 17 Mei 2009
[saa 9 na nusu mchana]
West Brom v Liverpool
[saa 12 jioni]
Chelsea v Blackburn
Jumatatu, 18 Mei 2009
[saa 4 usiku]
Portsmouth v Sunderland

Wenger awaomba Mashabiki kuwa wavumilivu!
Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, amewataka wadau wa Arsenal kuvumilia wakati akiijenga Timu mpya na amekubali kuwajibika ikiwa katika mwaka mmoja au miwili ijayo mikakati yake haifanikiwi.
Arsenal tangu mwaka 2005 walipoifunga Manchester United kwa matuta na kuchukua FA CUP hawajachukua Kombe lolote jingine.
Wenger alipata wakati mgumu sana alipokutana na Wadau wa Arsenal ambao walimshambulia kwa maswali kadha wa kadhaa. Lakini, kama alivyobatizwa 'Profesa' aliyapanchi vizuri na kusisitiza ana kikosi cha chipukizi na ataongeza nguvu pale panapo hitajika.
NAHODHA WA ASTON VILLA LAURSEN ASTAAFU SOKA!!

Nahodha wa Klabu ya Aston Villa Martin Laursen kutoka Denmark amelazimika kustaafu kucheza soka baada ya kuumia goti.
Lursen, miaka 31, amekuwa akipata matatizo ya mara kwa mara ya goti na mara ya mwisho aliumia mwezi Desemba.

Thursday 14 May 2009

UBINGWA UNANUKIA MAN U: Ferguson baridiiii, Benitez atoa visingizio!!!!!!
Endapo Man U watatwaa Ubingwa mbele ya Arsenal Jumamosi itakuwa ni mara ya 2 tu kuutwaa kwao OLD TRAFFORD!!!!
Wakati Manchester United wanahitaji pointi moja tu kunyakua Ubingwa wa LIGI KUU msimu huu huku wakiwa wamebakiwa na mechi 2 huku Meneja wao Sir Alex Ferguson akiionya Timu yake iache mzaha na kuwa makini, Meneja wa Liverpool Rafa Benitez, bila shaka, akijua fika Timu yake ishaukosa Ubingwa ameanza visingizio.
Benitez, akikaririwa na Tovuti ya Liverpool, amesema laiti kama Nahodha wake Steven Gerrard na Mshambuliaji hatari Fernando Torres wasingekuwa majeruhi mara kwa mara basi lazima wangekuwa Mabingwa!!!
Lakini Wadau wanashangaa mbona Manchester United hawasemi lolote kuhusu kukosa Mastaa wake kwani mwanzoni mwa msimu kwa kipindi kirefu walimkosa Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, alieumia enka na kufanyiwa operesheni, walimkosa Mchezaji Bora Uingereza, Wayne Rooney, kwa vipindi kadhaa, wamewakosa pia mara kadhaa Mabeki Bora Vidic na Ferdinand, kwa aidha kufungiwa au kuwa majeruhi!!
Msimu wote, Manchester United wamekuwa wakipanga Kikosi kinachobadilika mechi hadi mechi na kwenye baadhi ya mechi zaidi ya nusu ya Timu ilikuwa tofauti ya ile iliyocheza mechi iliyopita.
Huu ni ushahidi fika kuwa Man U wamekuwa hawamtegemei Mchezaji mmoja au wawili bali siku zote wamekuwa wakiitegemea Timu kamili!!
Mechi zilizobaki za Manchester United ni ile ya nyumbani Old Trafford Jumamosi na Arsenal na ya mwisho ni ya ugenini na Hull City.
Akionyesha hajabweteka, Sir Alex Ferguson ameonya: 'Mechi ijayo na Arsenal lazima tuwe makini! Tuna kazi ya kufanya! Arsenal ni Timu nzuri!!! Usisikilize kinachosemwa wao ni wazuri sana!!'
Pengine kitu cha ajabu mno ni kuwa tangu LIGI KUU ianzishwe msimu wa mwaka 1992/3 na Manchester United kuchukua Ubingwa mara 10 ni mara moja tu Mabingwa hawa wameweza kutwaa Ubingwa mbele ya Mashabiki zao nyumbani Old Trafford na hiyo ilikuwa siku ya mwisho ya mechi za ligi msimu wa mwaka 1998/9, msimu ambao walinyakua Vikombe vitatu yaani LIGI KUU, FA CUP na Klabu Bingwa Ulaya, wakati walipoifunga Tottenham Hotspurs.
Hiyo ilikuwa ni enzi ya kina Dwight Yorke, Andy Cole, Teddy Sheringham nk.

Mara nyingine zote 9 walishinda Ubingwa wakiwa nje ya Old Trafford.
Ingawa Ferguson hajazungumza lolote kuhusu furaha atakayoisikia ikiwa Manchester United watachukua Ubingwa Old Trafford mbele ya Arsenal, Washabiki wanakumbuka kwa uchungu sana ile siku ya mwaka 2002 wakati Arsenal walipotwaa Ubingwa Old Trafford kwa kuifunga Manchester United kwa bao 1-0 bao alilofunga Sylvain Wiltord!!
Wakati huo, Sir Alex Ferguson alizungumzia tukio hilo la Arsenal kuwafunga Old Trafford na kuchukua Ubingwa na akalifananisha na kama vile kuwa nje ya nyumba yako huku uso wako umeugandamiza kwenye kioo cha dirisha na kushuhudia watu wakiwa ndani ya hiyo nyumba yako wakiselebuka kwenye bonge la pati!!!!
Pengine, Mchezaji Nyota wa Manchester United, Wayne Rooney, akihojiwa jana, ndie anaetoa msimamo wa Mashabiki wengi wa Man U, kwani alisema: 'Pointi moja tu itatupa Ubingwa! Labda tutaipata Jumamosi na itakuwa ni kitu kizuri sana kushinda Old Trafford mbele ya Mashabiki wetu na tena dhidi ya Arsenal ambayo ni Timu nzuri sana!! Mashabiki wa Arsenal siku zote wakija Old Trafford utawasikia wakiimba tumeshachukua Ubingwa Old Trafford, sasa itakuwa poa tukiwashinda wao Arsenal na kuwa bingwa!! Hiyo ni spesho!!'
Rooney alimaliza: 'Tunataka tushinde mbele ya Mashabiki wetu!! Nadhani Meneja wetu Ferguson amesema ni mara moja tu katika miaka 17 tumechukua Ubingwa Old Trafford!!! Na kuwa Mabingwa mara 3 mfululizo ni kitu cha ajabu sana!!!!'

Manchester United wala Kiporo, sasa pointi moja tu kuwa Bingwa!!! Je Arsenal kuwapa Ubingwa Old Trafford Jumamosi??

Mabingwa Watetezi wa LIGI KUU England, Manchester United, jana wakiwa wageni wa Wigan ndani ya JJB Stadium kwenye mechi yao kiporo walilazimika kucheza kwa ziada na nguvu zote ili kwanza kuishinda hali ngumu ya mchezo kwani mvua kubwa ilikuwa ikinyesha na Wachezaji kuteleza ovyo na pili kupigana kuwamudu na kuwashinda Wapinzani wao Wigan waliochachamaa vilivyo.

Baada ya kuwa nyuma kwa bao moja mpaka hafutaimu kwa bao lililofungwa na Mshambuliaji wa Wigan Hugo Rodallega kutoka Colombia dakika ya 28 baada ya Vidic kuteleza ndani ya boksi na Rodallega kufumua shuti pembeni wavuni, Man U waliibuka kipindi cha pili na kufunga bao 2. Tevez, alieingizwa dakika ya 58 kumbadilisha Anderson alipachika bao tamu kwa kisigino dakika ya 61 lililomhadaa Kipa Kingson kutoka Ghana kufuatia shuti la Carrick. Huku zikiwa zimesalia dakika 4 mechi kwisha Carrick akafunga bao murua baada ya muvu nzuri sana iliyowahusisha Ronaldo na O'Shea upande wa kulia.

Kwa ushindi huo, huku kukiwa kumesalia mechi 2 tu kwa kila Timu ili kumaliza LIGI KUU, Manchester United yuko kileleni kwa pointi 6 mbele akiwa na poiniti 86, Liverpool wa pili pointi 80, Chelsea nafasi ya 3 pointi 77 na Arsenal ni wa 4 pointi 68.

Ili kutwaa Ubingwa kwa mara ya 3 mfululizo, Man U anahitaji poiniti moja tu katika mechi mbili zilizosalia na Jumamosi yuko nyumbani Old Trafford akipambana na Arsenal.

Vikosi vilikuwa;
Wigan: Kingson, Melchiot, Boyce, Bramble, Figueroa, Valencia, Cattermole, Scharner, Brown, N'Zogbia (Mido 82), Rodallega.
Akiba hawakucheza: Pollitt, Edman, Watson, Koumas, De Ridder, Kapo.
Man Utd: Van der Sar, O'Shea, Vidic, Evans, Evra, Carrick, Scholes (Giggs 75), Anderson (Tevez 58), Ronaldo, Berbatov (Park 89), Rooney.
Akiba hawakucheza: Kuszczak, Neville, Nani, Rafael Da Silva.
Watazamaji: 21,286
Refa: Rob Styles
Barcelona washinda Kombe la Mfalme 'COPA DEL REY' na huko Italy Lazio wanyakua Kombe la Italy kwa matuta!
Barcelona jana usiku walikaza kamba kipindi cha pili na kuwabamiza Athletic de Bilbao mabao 4-1 na kutwaaa Kombe la Mfalme wa Spain [pichani] baada ya kuwa suluhu 1-1 na Athletic Bilbao hadi mapumziko.
Bilbao ndio waliotangulia kupata bao lakini Yaya Toure akaisawazishia Barcelona na kipindi cha pili mabao ya Lionel Messi, Bojan Krkic na Xavi yaliwafanya Barcelona kuwa kidedea.
Huko Italy, baada ya mechi kuwa 1-1, penalti zikapigwa na Lazio wakaibuka washindi dhidi ya Sampdoria baada ya kushinda penalti 6-5 na hivyo kutwaa Kombe la Italia.
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora ya Waandishi!!!!
Chama cha Waandishi wa Habari wa Soka cha England kimemtunukia Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard Tuzo ya Mchezaji Bora kwa mwaka 2009.
Gerrard amewapiku Wachezaji wa Manchester United Ryan Giggs na Wayne Rooney kutwaa Tuzo ya mwaka huu.
Tuzo hii ilianza kutolewa mwaka 1948 na Gerrard atakabidhiwa Tuzo yake hapo Mei 29 katika Hoteli ya Royal Lancaster mjini London.
Bayern Munich yapata Meneja mpya baada ya kumtimua Klinsmann!!
Vigogo wa Ujerumani, Bayern Munich, ambao hivi karibuni walimtimua Staa wa zamani wa Ujerumani Jurgen Klinsmann kama Meneja wao, wamemteua Mholanzi Louis van Gaal aliewahi kuwa Bosi wa Ajax, Barcelona na Timu ya Taifa ya Holland, kuwa Meneja wao mpya.
Louis van Gaal, miaka 57, kwa sasa ni Meneja wa Klabu ya AZ Alkmaar ya Holland na ndio kwanza tu ameiwezesha Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Uholanzi msimu huu. Akiwa na Ajax, Van Gaal aliweza kutwaa UEFA CUP mwaka 1992 na UEFA CHAMPIONS LEGUE mwaka 1995 na alipokuwa na Barcelona aliiwezesha Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Spain mara 2.
Meneja huyu mpya ataanza kazi yake rasmi tarehe 1 Julai 2009.
Bayern Munich msimu uliopita walishinda Ubingwa wa Ujerumani na Kombe la Ujerumani lakini msimu huu wanasuasua na mpaka sasa kukiwa na mechi 2 tu zimebakia kumalizika kwa Bundesliga, Bayern wamefungana na Wolfsburg kwa pointi kileleni.

Wednesday 13 May 2009

LIGI KUU ENGLAND: JE LEO MAN U KULA KIPORO CHAKE NA KUONGOZA LIGI KWA POINTI 6 HUKU MECHI ZIMESALIA 2?


Mabingwa Watetezi Manchester United leo wanaingia uwanjani nyumbani kwa Wigan kucheza ile mechi yao kiporo ya muda mrefu na hivyo kufikisha mechi 36 kama Timu nyingine zilivyocheza na kubakisha mechi 2 ili ligi kumalizika hapo Mei 24. Mpaka sasa Manchester United anaongoza akiwa na pointi 83, ingawa amecheza mechi pungufu moja, Liverpool ana pointi 80, Chelsea ni wa 3 pointi 77 na Arsenal ni wa 4 pointi 68.
Ili Manchester United kutwaa Ubingwa kwa mara ya 3 mfululizo na kwa mara ya 11 tangu mfumo huu wa LIGI KUU England uanzishwe mwaka 1992/3 na pia kwa jumla ya mara 18 tangu ligi ianzishwe huko England ikiwa ni rekodi hiyohiyo ya mechi 18 inayoshikiliwa na Liverpool, Man U wanahitaji pointi 4 tu katika mechi zao 3 walizobakisha.
Mechi hizo 3 za Man U ni ya leo anayocheza ugenini na Wigan, Jumamosi yuko kwake Old Trafford atacheza na Arsenal na anamaliza ligi hapo tarehe 24 Mei kwa kucheza na Hull City ugenini.
Burnley aingia Fainali sasa kucheza na Sheffield United kuwania kuungana na Wolves na Birmingham kucheza LIGI KUU msimu ujao!!!!!!
Timu ya Burnley, iliyoshinda nyumbani mechi ya kwanza 1-0, jana iliwaua Reading nyumbani kwake kwa mabao 2-0 na kuwatoa nje ya kuwania nafasi ya kupanda Daraja kwenda LIGI KUU msimu ujao.
Sasa Burnley, hapo Mei 25 Uwanjani Wembley, London, atapambana Fainali na Sheffield United iliyoibwaga Preston kwa jumla ya mabao 2-1 katika mechi mbili, ili kupata Timu moja itakayoungana na Wolverhamton Wanderers na Birmingham kucheza LIGI KUU England msimu ujao.
APEWA MEDALI YAKE YA DHAHABU MIAKA 43 BAADA YA ENGLAND KUTWAA KOMBE LA DUNIA!!!!
Mtangazaji wa Michezo wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, Jimmy Armfield, miaka 73, atapewa na FIFA Medali ya Dhahabu miaka 43 baada ya England kunyakua Kombe la Dunia.
Jimmy Armfield, aliekuwa Mchezaji wa Blackpool na pia kuwemo kwenye Kikosi cha England kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1966 pale England ilipoifunga Ujerumani mabao 4-2 kwenye Fainali iliyochezwa Wenbley, hakucheza Fainali hiyo lakini alikuwa kama mmoja wa Wachezaji wa Akiba kwenye mechi hiyo.
Kabla ya Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1974, Wachezaji waliocheza mechi ya Fainali tu ndio walikuwa wakipewa Medali na wale wa Akiba walikuwa hawaambulii kitu.
FIFA imetamka Medali 14 za nyongeza zitapatiwa Nchi zote zizlizoshinda Kombe la Dunia kuanzia mwaka 1930 hadi 1970.
Jimmy Armfield, aliposikia habari za kupata Medali ya Dhahabu, amesema: 'Ni kitu kizuri!! Lakini siwezi kusema kama nilikereka miaka yote hii nilipokuwa sinayo. Siki hizi Medali zinatolewa hovyo tu-Msimamia Jezi, Mwendesha Basi wote wanapata!!!'
Meneja wa Tottenham Redknapp kupiga marufuku Wagidaji Timu yake!!!!
Meneja wa Tottenham, Harry Redknapp, ametangaza kuwa kuanzia msimu ujao hairuhusiwi kwa Mchezaji wa Timu yake kunywa pombe na hii imefuatia baada ya kukamatwa kwa Nahodha wake Ledley King alfajiri ya Jumapili iliyopita nje ya Naiti Klabu huko Soho, London kwa kumjeruhi mtu.
King alihojiwa na Polisi na kisha kuachiwa kwa dhamana hadi katikati ya Julai. King ameomba radhi kwa tukio hilo.
Lakini Redknapp amekerwa na mkasa huo na ameaapa kwa kusema: 'Msimu ujao tutakuwa na sheria ya kupiga marufuku pombe. Wanasoka hawatakiwi kunywa!! Huwezi gari la thamani kama Ferrari ukalipa mafuta ya Dizeli!! Hawa wanalipwa vizuri sana!!! Hawa wanatakiwa wawe mfano kwa Watoto!!

Tuesday 12 May 2009

MECHI KUBWA ULAYA KESHO: Huko Spain Fainali ya Kombe la Mfalme- Barcelona v Athletic de Bilbao na Italia ni Fainali Kombe la Italia- SS Lazio v Sampdoria!!!!!

Huko Spain na Italy kesho ni Fainali ya Vikombe sawa na kile FA CUP cha England wakati Barcelona atakapokumbana na Athletic de Bilbao saa 4 usiku saa za bongo kugombea SPAIN COPA DEL REY, yaani Kombe la Mfalme.

Na huko Italia ni mechi ya Fainali ya Kombe la Italia kati ya SS Lazio na Sampdoria pambano litakaloanza saa 3 dakika 45 usiku saa za bongo.

VIOJA VYA SOKA!!!!!
Duniani kuna vituko na mikasa mingi na hata Dunia ya Soka haikosi vibweka vyake!!!

Angalia kushoto ni bango la tahadhari ambalo kawaida huwekwa wakati sakafu inapigwa deki ili kumtahadharisha mtu asiteleze lakini Mdau mmoja amelibadilisha na kutoa tahadhari jinsi Wachezaji wa Italia walivyo Mabingwa kwa kujidondosha makusudi!!!!


Mdau hana Wapinzani wa kusakata nao kabumbu lakini Ng'ombe anao!!!! Akajikita Kiwanjani kuwapiga chenga Ng'ombe zake!!!
Yote ni starehe na burudani ya Soka!!!!


Wadau hawana Kiwanja cha Mpira lakini hawakukata tamaaaa!!!!! Wakaenda kando ya Ziwa kwenye kilima na kujitengenezea 'NESHNO STEDIUMU' yao burudani huku imepambwa na 'pori' la mimea mikubwa!!!!
Bila shaka Timu yenye Kiwanja hiki 'spesho' wakiingia kwenye Viwanja vya kawaida vilivyo tambarare basi soka lao litakuwa la kutisha sana maana mazoezi wanayoyapata kwenye Kiwanja hiki kilicho chini juu ni magumu sana na bora sana!!!!
Wachezaji wakilala yombo ovyo basi wanaishia Ziwani!!!!

Newcastle wajikwamua toka Timu 3 za mwisho: Newcastle 3 Middlesbrough 1


Newcastle, waliokuwa nafasi ya 18 ikiwa ni nafasi ya 3 toka chini ambalo ndilo eneo la Timu zinazoshushwa Daraja huanzia, jana ilijikwamua toka nafasi hiyo na kupanda hadi nafasi ya 17 baada ya kuifunga Middlesbrough mabao 3-1 Uwanjani St James Park, nyumbani kwa Newcastle. Kwa kipigo hicho,huku zimesalia mechi 2 ligi kumalizika, Middlesbrough wameendelea kujichimbia hatarini huku wakiwa nafasi ya 19 ikiwa ni nafasi moja tu toka mkiani ambako yuko West Bromwich Albion. Kwa kupanda hadi nafasi ya 17, Newcastle imeishusha Hull City hadi nafasi ya 18 kwa ubora wa tofauti ya magoli kwani wote wana pointi 34 na hivyo kuiingiza kwenye kundi la Timu 3 za mwisho zilizo hatarini kuporomoka Daraja.

Msimamo kwa Timu za chini ambazo zinapigana kupona kushushwa Daraja huku kukiwa kumesalia mechi 2 tu ni: [TIMU ZILIZO NAFASI YA 18 HADI 20 NDIZO HUSHUSHWA]

-Nafasi ya 13: Bolton pointi 40
-Nafasi ya 14: Blackburn pointi 40
-Nafasi ya 15: Portsmouth pointi 38
-Nafasi ya 16: Sunderland pointi 34
-Nafasi ya 17: Newcastle pointi 34
-Nafasi ya 18: Hull City pointi 34
-Nafasi ya 19: Middlesbrough pointi 31
-Nafasi ya 20: West Brom pointi 31

Vikosi vya mechi ya Newcastle v Middlesbrough:
Newcastle: Harper, Beye, Steven Taylor, Bassong, Duff, Guthrie, Butt, Nolan, Gutierrez (Lovenkrands 65), Owen (Martins 70), Viduka (Carroll 87).
AKIBA: Krul, Coloccini, Ryan Taylor, LuaLua.
KADI: Butt, Duff, Nolan.
MAGOLI: Steven Taylor 9, Martins 71, Lovenkrands 86.
Middlesbrough: Jones, Hoyte, Bates, Huth, Taylor (Adam Johnson 76), Downing, O'Neil, Shawky (Aliadiere 69), Sanli, Emnes, Alves (King 36).
AKIBA: Turnbull, Arca, McMahon, Grounds.
KADI: Bates.
GOLI: Beye [Kajifunga mwenyewe dakika ya 3]

WATAZAMAJI: 51,252

REFA: Mike Dean


UEFA yathibitisha: Fletcher wa MAN U na Abidal na Alvez wa Barcelona kukosa FAINALI ya ULAYA!!

UEFA jana ilithibitisha kuwa Kiungo wa Manchester United, Darren Fletcher, na Wachezaji wa Barcelona, Eric Abidal na Dani Alvez, wataikosa Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huko Rome, Italy Mei 27 ambayo itazikutanisha Man U na Barcelona baada ya kutupilia mbali Rufaa zao.

Fletcher alipewa Kadi Nyekundu kwenye Nusu Fainali Man U waliyocheza na Arsenal.

Eric Abidal alipataka Kadi Nyekundu kwenye Nusu Fainali kati ya Chelsea na Barcelona na kwenye mechi hiyo hiyo Dani Alvez alipata Kadi ya Njano ikiwa ni Kadi yake ya pili.

Sheffield United yatinga Fainali kuwania kuingia LIGI KUU England!!!!


Jana Sheffield United imeifunga Preston bao 1-0 kwenye mechi ya marudiano baada ya Timu hizi kutoka sare 1-1 kwenye mechi ya awali na hivyo sasa Sheffield United wameingia Fainali na wanamsubiri mshindi wa wa marudiano ya Nusu Fainali nyingine inayochezwa leo kati ya Reading na Burnley.

Katika mechi ya kwanza ya Reading na Burnley, Burnley ikiwa nyumbani kwake ilishinda bao 1-0 na leo watakuwa ugenini nyumbani kwa Reading.

Mshindi wa Fainali ya mchujo huu atajumuika na Wolverhamton Wanderers na Birmingham kuingia LIGI KUU England msimu ujao.

Wolverhampton alimaliza LIGI YA COCA COLA CHAMPIONSHIP akiwa wa kwanza na Birmingham alishika nafasi ya pili na hivyo Timu hizi mbili zikapandishwa moja kwa moja.

Timu zilizomaliza nafasi ya 3 hadi ya 6 ziliingizwa kwenye mchujo maalum kupata Timu moja kuwa ya 3 itakayopanda Daraja.


LIGI YA KLABU BINGWA AFRIKA 2009: RATIBA YATOKA

Ratiba ya KLABU BINGWA AFRIKA IMETOLEWA NA CAF, Chama cha Soka Afrika, huku Timu zimegawanywa kwenye Makundi mawili ya Timu nne kila moja ambazo zitacheza kwa mtindo wa ligi wa nyumbani na ugenini.
Michuano ya Makundi itaanza Tarehe 17 Julai na kumalizika Septemba 20 na Timu mbili za juu kila Kundi zitaingia Nusu Fainali zitazochezwa Oktoba pia kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Fainali ni kati ya Tarehe 30 na Novemba 1 na marudiano ni kati ya Novemba 6 na 8.
KUNDI A:
-Al Merreikh [Sudan]
-Al Hilal [Sudan]
-Kano Pillars [Nigeria]
-Zesco United [Zambia]
KUNDI B
-Etolie du Sahel [Tunisia]
-Heartland [Nigeria]
-TP Mazembe [DR Congo]
-Monomotapa [Zimbabwe]
RATIBA LIGI KUU ENGLAND
Jumatano, 13 Mei 2009
[saa 4 usiku]
Wigan v Man U
Jumamosi, 16 Mei 2009
[saa 8 dak 45 mchana]
Man U v Arsenal
[saa 11 jioni]
Bolton v Hull
Everton v West Ham
Middlesbrough v Aston Villa
Newcastle v Fulham
Stoke v Wigan
Tottenham v Man City
Jumapili, 17 Mei 2009
[saa 9 na nusu mchana]
West Brom v Liverpool
[saa 12 jioni]
Chelsea v Blackburn
Jumatatu, 18 Mei 2009
[saa 4 usiku]
Portsmouth v Sunderland
Jumapili, 24 Mei 2009 [HIZI NDIZO MECHI ZA MWISHO LIGI KUU MSIMU HUU]
[saa 12 jioni]
Arsenal v Stoke

Aston Villa v Newcastle
Blackburn v West Brom
Fulham v Everton
Hull v Man U
Liverpool v Tottenham
Man City v Bolton
Sunderland v Chelsea
West Ham v Middlesbrough
Wigan v Portsmouth

Sunday 10 May 2009

Aaaaah masikini Arsenal, wakung'utwa 4-1 kwao Emirates na Chelsea!!!!

Baada ya kucheza mechi 21 mfululizo bila kufungwa kwenye LIGI KUU England leo Arsenal wamechapwa bao 4-1 na Chelsea kwenye mechi ya LIGI KUU hiki kikiwa kipigo cha pili kikubwa kwa Arsenal Uwanjani kwao Emirates ndani ya wiki moja.
Jumanne iliyopita, kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, walitandikwa mabao 3-1 na Manchester United.
Kitu kinachowashangaza wengi ni kuwa Arsenal wanacheza soka tamu, wanatawala na kupata nafasi nyingi sana lakini ile staili yao ya kutaka kufunga goli lisilo na 'dosari' ndicho kinawaua kwani, mwisho ya yote, hilo goli hawalipati na hii ndio, kwa mara nyingine tena, hadithi ya leo!!!
Ukweli Arsenal walitawala na kukosa MABAO YA WAZI MIA KIDOGO lakini mwishowe Arsenal 1 Chelsea 4.
Magoli ya Chelsea yalifungwa na Alex, Anelka, Toure [Wa Arsenal aliejifunga mwenyewe] na Malouda. Goli la Arsenal lilifungwa na Bendtner.
Mbali ya kipigo cha leo, Arsenal wana uhakika wa kumaliza nafasi ya 4 LIGI KUU England na hivyo kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao kwa sababu Timu zilizo nyuma yao haziwezi kufikia pointi zao.
Vikosi vilkuwa:.
Arsenal: Fabianski, Sagna, Toure, Silvestre, Gibbs, Walcott, Nasri, Song Billong, Diaby, Fabregas, Van Persie.
Akiba: Mannone, Denilson, Ramsey, Djourou, Adebayor, Bendtner, Eboue.
Chelsea: Cech, Bosingwa, Alex, Terry, Ashley Cole, Essien, Mikel, Lampard, Anelka, Drogba, Malouda.
Akiba: Hilario, Ivanovic, Di Santo, Ballack, Kalou, Belletti, Mancienne.
Refa: Phil Dowd

Mabingwa Man U wahitaji pointi 4 tu katika mechi 3 zilizobaki kutetea Ubingwa wao kwa mara ya 3 mfululizo!!!!
Baada ya kukaa kileleni mwa LIGI KUU tangu jana jioni huku wakiwa pointi sawa na Man U lakini wana ubora wa magoli, leo Liverpool wameng'olewa nafasi hiyo na Mabingwa Manchester United baada ya kuwafunga Watani zao wa Jadi Manchester City kwa bao 2-0 Uwanjani Old Trafford. Sasa Man U anaongoza kwa pointi 3 mbele ya Liverpool huku akiwa amebakisha mechi 3 na Liverpool amebakisha mechi 2.
Hii ina maana Man U anahitaji pointi 4 tu katika mechi hizo 3 alobakisha ili anyakue tena Ubingwa kwa mara ya 3 mfululizo.
Jumatano Man U anacheza mechi yake ya kiporo ugenini kwa Wigan na Jumamosi ijayo tarehe 16 Mei Man U anamkaribisha Arsenal Old Trafford.
Liverpool mechi yake inayofuata ni Jumapili tarehe 17 Mei wakati atakapokuwa mgeni wa West Bromwich Timu inayopigana isishushwe Daraja na pengine mambo yakienda vizuri kwa Manchester United, kabla Liverpool hajacheza mechi hii, Man U atakuwa tayari Bingwa kwa mara nyingine tena!!
Magoli ya Man U yalifungwa na Ronaldo dakika ya 20 kwa frikiki na Tevez alipachika goli la pili baada ya pasi nzuri ya Berbatov na Tevez akaachia kigongo kilichopiga posti na kutinga ndani.
Goli hilo la Tevez liliwafanya Washabiki wa Man U waimbe kumtaka Ferguson amsaini Tevez ili abaki Old Trafford.
Baada ya mechi Sir Alex Ferguson akihojiwa kuhusu kauli ya Tevez ya kwamba hadhani atabaki Man U, Ferguson alisema Tevez ni Mchezaji wa Man U. Alipoulizwa kuhusu Ronaldo kuonekana amekasirika baada ya kubadilishwa kipindi cha pili, Ferguson alisema hakuna Mchezaji anaefurahi kutolewa hasa kama anacheza vizuri.
Man Utd: Van der Sar, Rafael Da Silva, Vidic, Evans, Evra, Ronaldo, Fletcher, Giggs, Park, Berbatov, Tevez.
Akiba: Kuszczak, Neville, Rooney, Carrick, Nani, Scholes, O'Shea.
Man City: Given, Richards, Onuoha, Dunne, Bridge, Elano, Ireland, Kompany, De Jong, Robinho, Caicedo.
Akiba: Hart, Zabaleta, Bojinov, Petrov, Fernandes, Evans, Berti.
Refa: Chris Foy

Tevez anategemea kuondoka Man U!!!!

Carlos Tevez amesema anadhani ataondoka Manchester United baada ya msimu kumalizika. Tevez amekaririwa na Gazeti moja huko Uingereza akisema: 'Inanisikitisha lakini hiki ninachosema ni kwaheri! Sidhani kama ntakuwa Mchezaji wa Manchester United msimu ujao. Nimefanya kila niwezalo lakini hawajanipa mkataba wala ofa yeyote!' Tevez alijiunga Man U mwaka 2007 kwa mkopo wa miaka 2 na mkataba wake unaisha baada ya msimu huu kumalizika. Kabla alikuwa akiichezea West Ham. Tevez ameongeza: 'Nitaisaidia Man U kuchukua LIGI KUU na Klabu Bingwa Ulaya.'

Nahodha wa Tottenham mikononi mwa Polisi!!

Ledley King, Nahodha wa Tottenham, leo alfajiri amekamatwa na Polisi baada ya kutuhumiwa kumjeruhi mtu kwa kumshambulia. King alikamatwa na Polisi baada ya mtu mmoja kusimamisha Gari la Patroli la Polisi na kuwaarifu ameumizwa. Tukio hili lilitokea kitongoji maarufu cha London chenye Majumba ya Starehe mengi kiitwacho Soho. Ledley King ameachiwa kwa dhamana muda mfupi uliopita.

Mdogo wa Mchezaji mwingine wa Tottenham auawa!!!!

Kiungo wa Tottenham kutoka Honduras, Wilson Palacios, amerudi kwao baada ya kupata taarifa mdogo wake aitwae Edwin Palacios alietekwa nyara na genge la majambazi tangu Oktoba 2007 mwili wake umeokotwa kilomita 240 toka mji mkuu wa Honduras, Tegucigalpa.

Powered By Blogger