Saturday, 9 October 2010


WADAU: TUNAHAMIA MTAA WA PILI!!!!
UKITAKA HABARI MOTOMOTOZ NJOO:
http://www.sokainbongo.com/

WWW.SOKAINBONGO.COM

Ureno, Spain, Germany zapeta EURO 2012
Katika mechi za Makundi za EURO 2012, Germany ilipata ushindi mzuri wa 3-0 dhidi ya Uturuki huko Berlin na Urusi ilipata mshimshike huko Dublin, Republic of Ireland na hatimaye kushinda 3-2.
Ureno, iliyokuwa ikisuasua, ilizinduka na kuichapa Timu ngumu Denmark mabao 3-1 na Spain iliichapa Lithuania 3-1 ugenini.
Katika mechi ya Germany, Miroslav Klose aliifungia Germany mabao mawili na Mesut Oezil alifunga bao moja lakini hakushangilia bao hilo hata chembe kwani Uturuki ndiko wanakotoka Wazazi wake.
Belgium iliishinda Kazakhstan mabao mawili ugenini na bao zote zilipachikwa na Ogunjimi ambae awali aliamua kuichezea Nigeria anakotoka Baba yake lakini baadae akageuza mawazo na kuichezea Belgium alikozaliwa.
Katika mechi ya Ureno na Denmark, Nani wa Manchester United alifunga bao mbili ndani ya dakika mbili kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili Beki wa Ureno, Ricardo Carvalho, alijifunga mwenyewe na kuifanya mechi iwe 2-1.
Ronaldo aliwakikishia Ureno ushindi alipofunga bao la 3 dakika ya 85 na kuifanya Denmark ilale 3-1.
Katika Kundi C, Ireland ya Kaskazini ikicheza nyumbani Mjini Belfast iliibana mbavu Italy na kwenda nao sare 0-0.
Mabingwa wa Dunia, Spain, wakiwa ugenini, waliichapa Lithuania 3-1 kwa mabao mawili ya Fernando Llorente na David Silva.
Boa la Lithuania lilifungwa na Davydas Sernas.
Leo, kutakuwa na mechi mbili, France v Romania na Israel v Croatia.
Jumanne kutakuwa na lundo la mechi za Euro 2012 ikiwemo ile ya England v Montenegro.
EURO 2012:
Ratiba
Jumamosi, 9 Oktoba 2010
France v Romania
Israel v Croatia
Matokeo
Ijumaa, 8 Octoba 2010
Armenia 3 Slovakia 1
Kazakhstan 0 Belgium 2
Andorra 0 FYR Macedonia 2
Georgia 1 Malta 0
Hungary 8 San Marino 0
Cyprus 1 Norway 2
Czech Republic 1 Scotland 0
Luxembourg 0 Belarus 0
Albania 1 Bosnia-Hercegovina 1
Austria 3 Azerbaijan 0
Moldova 0 Netherlands 1
Montenegro 1 Switzerland 0
Serbia 1 Estonia 3
Wales 0 Bulgaria 1
Germany 3 Turkey 0
Greece v Latvia
Northern Ireland 0 Italy 0
Rep of Ireland 2 Russia 3
Slovenia 5 Faroe Islands 1
Portugal 3 Denmark 1
Spain 3 Lithuania 1
Nigeria yafunguliwa kwa muda
FIFA leo imetangaza kuwa imeondoa kwa muda amri ya kuifungia Nigeria kushiriki Mashindano ya Kimataifa baada ya kuridhika na mwelekeo thabiti wa kufuta kesi iliyokuwa Mahakamani kuwapinga Viongozi wa NFF, Chama cha Soka Nigeria, na pia kurudishwa madarakani kwa Katibu Mkuu wa NFF.
Taarifa rasmi iliyotolewa leo huko Zurich, Uswisi, Makao Makuu ya FIFA, ilisema: “Baada ya Mdai katika kesi iliyokuwa Mahakamani kutangaza waziwazi kuifuta kesi hiyo, Kaimu Katibu Mkuu wa NFF kurudishwa madarakani tangu Oktoba 5 na Ligi ya Nigeria kuachiwa NFF kuiendesha, kusimamishwa kwa Nigeria kunafutwa kwa muda hadi Oktoba 26 tutakapojua hatma ya kesi iliyopo Mahakamani itakayosikilizwa Oktoba 25. Endapo kesi hiyo itaendelea Mahakamani na ikiwa NFF itaendelea kuingiliwa, kusimamishwa kwa Nigeria kutaanza mara moja hadi matatizo yote yatakapokwisha.”
Jumapili Nigeria wanatakiwa wacheze mechi ya Kundi lao kwenye Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika huko Conakry dhidi ya Guinea.
Mancini alikoka bifu na Fergie
Roberto Mancini wa Manchester City ameiponda Manchester United kwa kudai Chelsea na Arsenal ndio Timu zenye ufundi wa hali ya juu na hilo huenda likasababisha Sir Alex Ferguson wa Manchester United kukerwa na kuchochea zaidi uhasama kati ya Mahasimu hao wa Jijini Manchester.
Akiongea huko kwao Italia ambako alienda kumuuguza Baba yake, Mancini alisema: “Chelsea ndio Timu ngumu Ligi Kuu. Arsenal wako sawa nao kiufundi lakini wanazidiwa miguvu na Chelsea.”
Ingawa Man City iliifunga Chelsea 1-0 kwenye Ligi Kuu, Mancini anaamini Chelsea chini ya Mtaliana mwenzake Carlo Ancelotti itatwaa tena Ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara pili mfululizo.
Mancini aliongeza: “Baada ya mechi na Chelsea nilimwambia Carlo Ancelotti ‘Nimekufunga lakini mtashinda Ligi Kuu’! Nadhani Chelsea watachukua Ubingwa!”
Baada ya mechi 7, Chelsea wanaongoza Ligi wakifuatiwa na Man City, Man United na Arsenal na hii ni mara ya kwanza kwa Man City, kwenye hatua hii, kuwa mbele ya Man United katika Miaka 20.
Hata hivyo, Mancini anasema yeye na Wamiliki wa Klabu lengo lao ni kumaliza katika nafasi 4 za juu ili wacheze UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu wa 2011/12.
Mancini pia alisema amekuwa haongei na Mtaliana mwenzake Fabio Capello ambae ni Kocha wa England licha ya Man City kuwa na Wachezaji wengi Timu ya England.

Friday, 8 October 2010

CHEKI KITU MPYA: www.sokainbongo.com


Morocco kuwakamia Mastaa wa Taifa Stars
Morocco, maarufu kama Simba wa Atlas, wamesema wanawatambua Wachezaji wazuri na hatari wa Taifa Stars na washabuni mbinu za kuwadhibiti kwenye mechi ya Kundi lao kuwania kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mwaka 2012 itakayochezwa hapo kesho Jumamosi Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Morocco imesema Wachezaji hao ni Kiungo Nizar Khalfan na Nahodha Shadrack Nsajigwa.
Timu kwenye Kundi D ni Algeria, Tanzania, Morocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Katika mechi za kwanza, Algeria na Tanzania zilitoka sare 1-1 huko Algiers na Morocco, ikiwa nyumbani ilitoka 0-0 na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Msemaji wa Msafara wa Morocco uliokuwa na Watu 40 amesema wameridhishwa na mapokezi yao tangu wawasili Dar es Salaam Jumatano usiku.
Msemaji huyo alitamka: “Tumefurahi. Tulipokuwa tukiingia Uwanja wa Taifa kwa mazoezi Mashabiki watushangilia na kutupungia mikono huku wakitaja majina ya Wachezaji wetu!”
Wengi wa Mashabiki hao walikuwa wakimtaja Straika wa Arsenal, Marouane Chamakh, ambae yupo kwenye Kikosi hicho.
Nae Kocha wa Morocco, Dominic Cuperly, amekisifia kiwanja cha kuchezea cha Uwanja wa Taifa na kusema ni moja ya viwanja bora Barani Afrika.
Wakati huo huo, Timu ya watu 26 ya Kituo cha TV maarufu cha Michezo Barani Afrika, Supersport, kimetua Dar es Salaam tayari kwa kulirusha moja kwa moja pambano hilo la Tanzania na Morocco kwenye Chaneli maarufu ya Soka Supersport 3, SS3.
Macheda amtaka radhi Rooney
Baada ya kukaririwa na Gazeti moja huko Italia akimsema Mchezaji mwenzake wa Manchester United, Wayne Rooney, kuwa ni mtu mzuri alietoka familia ya kimasikini na hana elimu lakini sasa anatamba kwa utajiri, Chipukizi Kiko Macheda imebidi aombe radhi kwa maneno hayo.
Inasemekana Macheda alimbembeleza Rio Ferdinand amwombee msamaha kwa Rooney .
Hata hivyo, marafiki wa Macheda, mwenye umri wa Miaka 19, wamedai Macheda mwenyewe ni kama Rooney tu kwa vile nae ametoka familia ya kimaskini na hana elimu.
Mmoja wa hao marafiki wa Macheda alisema: “Baba yake Macheda ni deiwaka! Mama yake ni mfagiaji! Macheda ni kama Rooney tu!”

Thursday, 7 October 2010

Van der Sar kung’atuka mwakani
Edwin van der Sar huenda akastaafu Soka mwishoni mwa Msimu wa 2010/11 kufuatia kauli ya Kocha wa Makipa wa Manchester United, Eric Steele.
Van der Sar atatimiza Miaka 40 hapo Oktoba 29 na alihamia Manchester United Mwaka 2005 akitokea Fulham.
Eric Steele amesema anadhani Msimu huu ndio wa mwisho kwa Van der Sar na yeye, Streele, amekuwa akihaha kila kona huko Ulaya kuchunguza Makipa wanaoweza kumrithi Kipa huyo mkongwa kutoka Uholanzi.
Miongoni kwa Makipa wanaotajwa ni pamoja na Gianluigi Buffon wa Juventus na Martin Stekelenburg wa Ajax..

Wamiliki Liverpool wagomea kuuzwa!
Mmoja wa Wamiliki wa Liverpool, Tom Hicks, amesema wao hawaiuzi Liverpool kwa Pauni Milioni 300 na wamewasilisha kesi Mahakama Kuu kupinga ununuzi huo.
Bodi ya Wakurugenzi ya Liverpool, chini ya Mwenyekiti Martin Broughton, ilitangaza kukubali ofa ya Kampuni inayomiliki Timu ya Beziboli huko Marekani Boston Red Sox lakini Wamiliki wa Liverpool, Tom Hicks na George Gillett, wamedai Bodi hiyo haina mamlaka kuiuza kwa vile wao waliibadilisha.
Kina Hicks wanasemekana walitangaza kuwaondoa Wakurugenzi wawili wa Bodi, Christian Purslow na Ian Ayre, ambao wamegoma kung’olewa na Mwenyekiti wa Bodi, Martin Broughton, amesisitiza Wamiliki hao hawana mamlaka ya kubadilisha Bodi.
Alipohojiwa kuhusu mzozo huo, Tom Hicks, alitamka: “Ndio maana kuna sheria na Mahakama!”
Hicks alisisitiza wao waliibadilisha Bodi kisheria.
Mzozo huo utasikilizwa Mahakama Kuu wiki ijayo.
Kipa wa Oman kuigharimu Wigan
Kipa wa Bolton, Ali Al-Habsi, anaetoka Oman ambae yuko Wigan kwa mkopo, inabidi alipiwe dau kubwa ikiwa Wigan itataka kumchukua moja kwa moja.
Bosi wa Bolton, Owen Coyle, amesema Wigan haiwezi kumchukua Kipa huyo ambae amemng’oa Kipa namba moja, Chris Kirkland, kwa bei ya chee na ni yeye tu ndie ataamua uhamisho wa Al-Habsi.
Roberto Martinez, Meneja wa Wigan, ameridhishwa na uchezaji wa Al-Habsi na ameonyesha nia ya kumchukua kijumla.

Wednesday, 6 October 2010

KWA HABARI MOTOMOTOZ, TAMU NA ZENYE UTAFITI WA KINA, TEMBELEA:
www.sokainbongo.com

Liverpool yapata Mnunuzi lakini……………………..
Klabu ya Liverpool iko mbioni kuuzwa kwa Wamiliki wa Timu maarufu ya mchezo wa Beziboli huko Marekani iitwayo Boston Red Sox lakini huenda hatua hii ikakwama kufuatia kufukuta kwa mgogoro ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya Liverpool ambapo Wamiliki wa Liverpool, Wamarekani wawili, Tom Hicks na George Gillett, wanataka kuwatimua Mkurugenzi Mtendaji, Christian Purslow na Mkurugenzi wa Masoko, Ian Ayre, ambao Wamiliki hao wanawaona kama kikwazo kwa Klabu hiyo kupata Mnunuzi.
Wakurugenzi hao wawili tayari wameshatafuta hifadhi ya Kisheria ili wasitimuliwe Liverpool na hatua hii huenda ikachelewesha uuzwaji wake.
Inasemekana Wamiliki hao wa Boston Red Sox wametoa ofa ya Pauni Milioni 300 ambayo inatosha kulipia deni la Pauni Milioni 240 la Liverpool pamoja na ada za benki ya Royal Bank of Scotland waliodhamini mkopo huo na ada hiyo ni Pauni Milioni 40.
Deni hilo pamoja na ada ya Benki ni lazima zilipwe kabla ya Oktoba 15 la sivyo Klabu hiyo itatozwa faini ya Pauni Milioni 60.
Ni muda mrefu sasa Liverpool imekuwa sokoni kutafuta mnunuzi lakini Watu wamekuwa wakikwepa kuinunua na wenye mali, Hicks na Gillett, wanahisi kikwazo ni hao Wakurugenzi wawili ambao sasa wanataka kuwatimua.
Hicks na Gillett waliinunua Liverpool Mwaka 2007 kwa Pauni Milioni 174.1 na kurithi deni la Pauni Milioni 44.8 tu.
Mimiliki Mkuu wa Boston Red Sox ni John W. Henry ambae pia anamiliki Kampuni nyingine kadhaa za michezo huko Marekani.
Huddlestone apona rungu la UEFA
Kiungo wa Klabu ya Tottenham HotspurTom Huddlestone amenusurika kuadhibiwa na UEFA baada ya kudaiwa kumpiga kiwiko Mchezaji wa FC Twente Marc Janko kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Jumatano iliyopita huko White Hart Lane ambayo Spurs walishinda bao 4-1.
Janko alidai Huddlestone alikusudia kumpiga kipepsi wakati Wachezaji hao walipovaana katika tukio ambalo Refa alipiga filimbi kuashiria ni Janko ndie aliecheza faulo.
UEFA ilithibitisha kutaka kuchunguza mikanda ya tukio hilo na sasa imetamka baada ya kufanya hivyo Idara yao ya Nidhamu imeamua Huddlestone hakuwa na kesi ya kujibu na hivyo kupona kuadhibiwa.

Tuesday, 5 October 2010

PITIA TOVUTI BOMBA: www.sokainbongo.com

Newcastle yageuka mbogo, yataka De Jong aadhibiwe!
Newcastle imewaandikia FA kuwataka wamchukulie hatua Mchezaji wa Manchester City Nigel de Jong kwa kumvunja mguu Hatem Ben Arfa wa Newcastle katika mechi ya Ligi Kuu ambayo Man City walishinda 2-1 siku ya Jumapili.
Vilevile, Klabu hiyo imeitaka FA kuangalia uchezeshaji wa Refa Martin Atkinson ambae hakupiga filimbi ya faulo wakati Ben Arfa anavunjwa mifupa yote miwili ya mguuni na hivyo kutomwadhibu Mholanzi huyo.
Pia Newcastle wamedai Refa Atkinson aliwapa Man City penati ya utata ambayo Carlos Tevez aliwafungia bao la kwanza na wao kunyimwa penati ya wazi.
Kitendo cha de Jong kumvunja Ben Arfa kilimfanya Kocha wa Uholanzi, Bert van Marwijk, kutomwita Mchezaji huyo kwenye Timu yake itakayocheza mechi za EURO 2012 dhidi ya Moldova na Sweden wiki hii na ijayo.
Marwijk ameelezea tukio hilo kama ni baya na halistahili.
Romario atinga siasani, sasa ni Seneta!
Gwiji la Soka la zamani la Brazil, Romario, ameshinda uchaguzi huko Brazil kwa kupata kura zaidi ya Laki 150 na hivyo kuchaguliwa kuwa Seneta wa Bunge dogo la Shirikisho la Brazil kupitia Chama cha Kisoshalisti cha Brazil.
Romario, akigombea huku akinadi ilani yake ya kuendeleza miradi ya michezo kwa jamii masikini, alisheherekea ushindi huo kwa bonge la pati ya usiku kucha.
Romario aliwahi kuwa Mchezaji Bora wa Dunia Mwaka 1994 na ameshazichezea Klabu za Barcelona, Valencia, Flamengo na Vasco da Gama.
Mshauri wa Romario kwenye siasa, Marcio Saraiva, ametamka hapo baadae wanaweza kugombea Uraisi wa Brazil kwani hamna sababu ya kutofanya hivyo ikiwa Rais wa sasa wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, alianza kama mfua vyuma.
TEMBELEA TOVUTI YENYE SURA MPYAAAAA: www.sokainbongo.com

Tevez afarakana na Mancini
Straika wa Manchester City Carlos Tevez aligombana na Meneja wake Roberto Mancini wakati wa mapumziko wa mechi ya Ligi Kuu Jumapili ambayo Man City waliifunga Newcastle 2-1.
Inadaiwa mzozo kati yao ulianza pale Tevez, Nahodha wa Timu hiyo, alipotukana kwa lugha ya Kispanish na Mancini kusikia ndipo wakaanza kurushiana maneno.
Inasemekana Tevez alikuwa ameudhiwa na mbinu za Mancini za kulundika Wachezaji wengi kwenye Kiungo na kumuacha yeye kama Straika pekee na hivyo kukosa mipira ya kufunga.
Hii ni mara ya pili kwa Tevez na Mancini kukwaruzana mara ya kwanza ilikuwa pale Tevez aliponukuliwa na Magazeti akiponda jinsi Mancini anavyoendesha mazoezi ya Timu.
Mancini amekuwa hana uhusiano mzuri na baadhi ya Wachezaji na tayari alishakwaruzana na Craig Bellamy na kumfanya Mchezaji huyo apelekwe Cardiff City kwa mkopo.
Pia ameshagombana na Emmanuel Adebayor ambaye amekuwa hapewi namba.
Torres nje Wiki kadhaa
Fernando Torres atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa akiuguza musuli za kwenye nyonga na hiyo imemfanya asiitwe kwenye Kikosi cha Spain kitakachocheza mechi za EURO 2012 wiki hii na ijayo dhidi ya Lithuania na Scotland.
Torres, Miaka 26, alicheza dakika 10 tu za mechi ya Ligi Kuu Jumapili iliyopita ambayo Liverpool ilichapwa 2-1 Uwanjani kwao Anfield na Blackpool.
Pia kuumia huko kutamfanya Torres aikose dabi ya Liverpool na Watani zao Everton itakayochezwa Oktoba 17 huko Goodison Park.
Tangu Msimu uliokwisha Torres amekuwa akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara.
Spain yataja Kikosi cha mechi za EURO 2012
Kocha wa Spain, Vicente del Bosque, ametangaza Kikosi cha Spain kitakachocheza mechi za EURO 2012 hapo Oktoba 8 na Lithuania na Oktoba 12 na Scotland huku Mastaa kama Fernanbdo Torres wa Liverpool, Fowadi wa Barcelona Pedro na Winga wa Sevilla Jesus Navas, wakiachwa baada ya kuumia.
Badala yake Kocha del Bosque amelazimika kuchukua Wachezaji wapya, wawili kutoka Valencia, Aritz Aduriz na Pablo Hernandez, na wawili kutoka Villareal, Borja Valero na Bruno Siriano.
Kikosi kamili:
Makipa: Iker Casillas (Real Madrid), Victor Valdes (Barcelona), Pepe Reina (Liverpool)
Mabeki : Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Carles Puyol (Barcelona), Gerard Pique (Barcelona), Carlos Marchena (Villarreal), Joan Capdevila (Villarreal), Nacho Monreal (Osasuna)
Viungo : Xabi Alonso (Real Madrid), Sergio Busquets (Barcelona), Santi Cazorla (Villarreal), Andres Iniesta (Barcelona), Pablo Hernandez (Valencia), Borja Valero (Villarreal), Bruno Soriano (Villarreal)
Mafowadi : David Villa (Barcelona), David Silva (Manchester City), Fernando Llorente (Athletic Bilbao), Aritz Aduriz (Valencia)
KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA
RATIBA:
Ijumaa, 8 Oktoba 2010
Libya v Zambia
Mali v Liberia
Senega lv Mauritius
Zimbabwe v Cape Verde
Namibia v Mauritania
Central African Republic v Algeria
Togo v Tunisia
Comoros v Mozambique
Jumamosi, 9 Oktoba 2010
Malawi v Chad
Kenya v Uganda
Tanzania v Morocco
Burundi v Ivory Coast
Rwanda v Benin
Cameroon v Congo DR
Angola v Guinea-Bissau
Burkina Faso v Gambia
Jumapili, 10 Oktoba 2010
Sierra Leone v South Africa
Ghana v Sudan
Madagascar v Ethiopia
Niger v Egypt
Congo v Swaziland
Guinea v Nigeria

Monday, 4 October 2010

Yanga, Simba zafukuzana Ligi Kuu Vodacom
Yanga ipo kileleni na Simba wako nyuma yao kwa pointi moja baada ya mechi 6 za Ligi Kuu Vodacom.
Wakongwe hao wataumana huko CCM Kirumba Mwanza Oktoba 16 huo ukiwa Uwanja wa nyumbani wa Simba.
Uwanja wa Jamhuri huko Morogoro ndio 'homu graundi' ya Yanga baada ya Timu hizo mbili kutimuliwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ambao uko matengenezoni.
Mpaka sasa Yanga wana pointi 16 baada ya kushinda mechi 5 na sare moja huku Simba wana pointi 15 kwa kushinda mechi 5 na kufungwa moja.
FIFA yaifungia Nigeria
FIFA imeifungia Nigeria kutocheza mashindano yeyote ya Kimataifa baada ya Chama cha Soka cha Nigeria, NFF, kuingiliwa katika uendeshwaji wake na Serikali.
Hatua ya FIFA imefuatia kuburutwa Mahakamani Viongozi kadhaa wa NFF na Kikundi kimoja kinachodai uchaguzi wa Viongozi wa NFF haukuwa halali.
Vilevile, Kamisheni ya Michezo ya Nchi hiyo ilitaka kulazimisha Ligi ya huko ianze Msimu mpya bila ya Timu yeyote kuteremshwa Daraja.
Hatua hizo zimeifanya FIFA itoe amri ya kuisimamisha Nchi hiyo na hivyo kuleta kizaazaa juu ya hatma ya mechi ya Wikiendi hii ya Makundi ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Guinea na Nigeria huko Conakry, Guinea.
Capello ataja Kikosi cha England
Kocha wa England Fabio Capello ametangaza Kikosi chake kitakachocheza mechi ya Makundi ya EURO 2012 huko Wembley na Montenegro Oktoba 12 na miongoni mwa Wachezaji hao yupo Straika wa Bolton Simon Davies, Miaka 33, ambae hajawahi kuichezea England.
Mastraika wengine kwenye Kikosi hicho ni Wayne Rooney, Darren Bent na Peter Crouch.
Wachezaji wengine maarufu ambao wametajwa ni John Terry, Rio Ferdinand, Joe Cole, Aaron Lennon na Kipa Rob Green.
Chipukizi wa Arsenal Jack Wilshere nae yumo kundini.
Kwenye Kundi lao, England tayari wameshacheza mechi mbili na kuzishinda Bulgaria na Uswisi.
Kikosi kamili cha England ni:
Ben Foster (Birmingham City), Robert Green (West Ham United), Joe Hart (Manchester City) , Ashley Cole (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Rio Ferdinand (Manchester United), Joleon Lescott (Manchester City), John Terry (Chelsea), Stephen Warnock (Aston Villa), Gareth Barry (Manchester City), Joe Cole (Liverpool), Steven Gerrard (Liverpool), Tom Huddlestone (Tottenham Hotspur), Adam Johnson (Manchester City), Aaron Lennon (Tottenham Hotspur), Jack Wilshere (Arsenal), Shaun Wright-Phillips (Manchester City), Ashley Young (Aston Villa), Darren Bent (Sunderland), Peter Crouch (Tottenham Hotspur), Kevin Davies (Bolton Wanderers), Wayne Rooney (Manchester United)
De Jong atemwa Holland kwa uchezaji rafu!
Kiungo wa Manchester City Nigel de Jong ametupwa nje ya Timu ya Uholanzi kwa mechi za EURO 2012 dhidi ya Moldova na Sweden kwa kile Kocha wa Timu hiyo ya Taifa, Bert Van Marwijk, kukiita uchezaji wa mabavu kupindukia.
Jumapili kwenye mechi ya Ligi Kuu kati ya Manchester City na Newcastle De Jong alimvunja mguu Hatem Ben Arfa na Kocha Marwijk ametamka: “Ni mbaya na ilikuwa si lazima! Nina matatizo na uchezaji wa De Jong anaecheza kwa nguvu kupindukia.”
Hiyo si mara ya kwanza kwa De Jong kumvunja mtu mguu kwani Mwezi Machi alimvunja Mchezaji wa USA Stuart Holden, ambae pia huchezea Bolton.
Lakini Dunia inamkumbuka vizuri De Jong kwenye Fainali ya Kombe la Dunia Spain ilipocheza na Holland huko Afrika Kusini na De Jong kumshindilia Xabi Alonso wa Spain guu la kifuani lakini akaepuka kutolewa.
Ben Arfa avunjwa mguu
Kiungo wa Newcastle Hatem Ben Arfa amevunjika mguu katika mechi ya Ligi Kuu waliyofungwa 2-1 na Manchester City Jumapili.
Ben Arfa, Miaka 23, aliumizwa na Nigel De Jong dakika ya 4 tu ya mchezo na kukimbizwa hospitalini.
Bosi wa Necastle, Chris Hughton, amethibitisha kwa kusema: “Aliumizwa katika rafu isiyostahili.”
Ben Arfa yupo Newcastle kwa mkopo akitokea Marseille ya Ufaransa na hiyo ilikuwa mechi yake ya tatu.
Hodgson: ‘Huu ni mwanzo usiokubalika!’
Bosi wa Liverpool, Roy Hodgson, amesema matokeo wanayopata Liverpool kwa sasa ni mwanzo mbaya wa Msimu na hayakubaliki.
Jumapili, Liverpool wakiwa nyumbani Anfield, walipigwa 2-1 na Blackpool kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyowafanya wawe nafasi ya tatu toka mkiani kwenye eneo la kuporomoka Daraja.
Hodgson ametamka: “Ni mwanzo mbaya wa Msimu. Hatufurahii na lazima tubadilike. Tuna kazi ngumu.”
Real Madrid 6 Deportivo 1
Huko kwenye La Liga Nchini Spain Jumapili Vigogo Real Madrid wameinyuka Deportivo la Coruna mabao 6-1 na kushika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi.
Awali, FC Barcelona walitoka sare 1-1 na Mallorca.
Baada ya mechi 6, Valencia ndie kinara akiwa na pointi 16, Viillareal ni wa pili akiwa na pointi 15, Real Madrid pointi 14 na Barcelona pointi 13.
Katika mechi hiyo ya Real, Wafungaji wao walikuwa Cristiano Ronaldo mabao mawili na wengine ni Mesut Oezil, Angel Di Maria na Gonzalo Higuain.
Bao jingine lilifungwa na Ze Castro wa Deportivo aliejifunga mwenyewe.

Sunday, 3 October 2010

LIGI KUU ENGLAND: Kwenda ‘vakesheni’ kwa Wiki 2 kupisha EURO 2012 na Kalenda ya Kimataifa ya FIFA
Baada ya mechi za Jumapili Oktoba 3, LIGI KUU inakwenda ‘holidei’ kupisha michuano ya Kimataifa kwa mujibu wa Kalenda ya FIFA ambayo imeweka Oktoba 8 na wikiendi yake pamoja na Oktoba 12 mahsusi kwa mechi za Kimataifa kama vile za Ulaya, EURO 2012, Kombe la Mataifa ya Afrika, na ya Mabara mengine Duniani.
Ligi Kuu itarudi tena dimbani wikiendi ya Oktoba 16.
RATIBA
Jumamosi, 16 Oktoba 2010
[Saa za Bongo]
[Saa 11 Jioni]
Arsenal v Birmingham
Bolton v Stoke
Fulham v Tottenham
Man Utd v West Brom
Newcastle v Wigan
Wolverhampton v West Ham
[Saa 1 na nusu usiku]
Aston Villa v Chelsea, 17:30
Jumapili, 17 Oktoba 2010
Everton v Liverpool, 13:30
Blackpool v Man City, 16:00
Jumatatu, 18 Oktoba 2010
Blackburn v Sunderland, 20:00
Chelsea wajikita kileleni!
• Chelsea 2 Ze Gunners 0
Bao moja kila kipindi yamewapa Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Chelsea ushindi wa mabao 2-0 juu ya Arsenal Uwanjani Stamford Bridge katika mechi ya tatu ya leo ya Ligi na kuwafanya wajikite uongozini kwa pointi 4 mbele ya Manchester City walio nafasi ya pili, pointi 5 mbele ya Man United na pointi 7 mbele ya Arsenal huku Timu zote zikiwa zimecheza mechi 7.
Kama kawaida yao, Arsenal ndio walikuwa na umiliki bora wa mpira lakini ni Chelsea ndio walioleta mpasuko kwenye ngome ya Arsenal.
Alikuwa Didier Drogba aliefunga bao la kwanza dakika ya 39 alipoiwahi krosi ya Ashley Cole na kumhadaa Kipa Lukasz Fabianski.
Na bunduki kali ya Alex kutoka friki ya mita kama 30 hivi kwenye dakika ya 85 ilizaa bao la pili na kuifanya Stamford Bridge yote indirime kwa furaha.
Vikosi vilivyoanza:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Alex, Terry, Cole, Mikel, Essien, Ramires, Malouda, Anelka, Drogba.
Akiba: Turnbull, Zhirkov, Ferreira, Sturridge, Van Aanholt, Kakuta, McEachran.
Arsenal: Fabianski, Sagna, Koscielny, Squillaci, Clichy, Diaby, Nasri, Wilshere, Song, Arshavin, Chamakh.
Akiba: Szczesny, Rosicky, Vela, Denilson, Djourou, Eboue, Emmanuel-Thomas.
Refa: Mike Dean
MATOKEO MECHI ZA LEO:
Manchester City 2 Newcastle 1
Liverpool 1 Blackpool 2
Chelsea 2 Arsenal 0
Baada ya matokeo ya leo, Msimamo kwa Timu za juu ni:
1 Chelsea pointi 18
2 Man City pointi 14
3 Man United pointi 13
4 Arsenal pointi 11
5 Tottenham pointi 11
6 West Brom pointi 10
7 Stoke pointi 10
8 Villa pointi 10
9 Blackpool pointi 10
10 Fulham pointi 9
Liverpool wapigwa kwao Anfield!
• Liverpool 1 Blackpool 2
Liverpool leo wamedidimizwa mkiani na kupelekwa nafasi ya 3 toka chini baada ya kutandikwa bao 2-1 na Blackpool uwanjani kwao Anfield.
Licha ya kufungwa, Liverpool pia wameingizwa kwenye wasiwasi baada ya Straika wao Nyota Fernando Torres kucheza dakika 9 tu na kisha kutolewa akiwa majeruhi.
Ni mabao ya kipindi cha kwanza ya Blackpool yaliyofungwa na Charlie Adam kwa penati baada ya Beki wa Liverpool Glen Johnson kumchezea rafu Luke Varney na la pili kufungwa na Luke Varney ndio yaliyowaibua Blackpool kidedea katika mechi yao ya kwanza hapo Anfield tangu Mwaka 1971.
Kipindi cha pili Liverpool waliibuka na kujipa matumaini pale Beki Kyrgiakos alipofunga kwa kichwa baada ya friki ya Steven Gerrard lakini Blackpool walisimama imara na kumaliza gemu washindi.
Vikosi vilivyoanza:
Liverpool: Reina, Johnson, Kyrgiakos, Skrtel, Carragher, Poulsen, Meireles, Kuyt, Gerrard, Cole, Torres.
Akiba: Jones, Jovanovic, Maxi, Lucas, Ngog, Spearing, Kelly.
Blackpool: Gilks, Eardley, Evatt, Cathcart, Crainey, Vaughan, Adam, Campbell, Grandin, Varney, Taylor-Fletcher.
Akiba: Halstead, Southern, Harewood, Ormerod, Sylvestre, Phillips, Keinan.
Refa: Michael Jones
Man City 2 Newcastle 1
Manchester City wakiwa uwanja wa nyumbani, City of Manchester, walishinda mabao 2-1 dhidi ya Newcastle katika mechi ya kwanza kati ya 3 za leo za Ligi Kuu England na kufikisha pointi 14 na sasa wako pointi moja mbele ya wapwa zao Manchester United.
Ni Man City ndio walitangulia kupata bao kwa penati ya Carlos Tevez dakika ya 18 baada ya Tevez kufanyiwa faulo na Mike Williamson.
Newcastle walisawazisha kwa mkwaju wa Jonas Gutierrez dakika ya 24.
Lakini Mchezaji Adam Johnson alietoka benchi ndie aliwapa ushindi Man City kwa kufunga bao la pili dakika ya 75.
Newcastle watahisi wameonewa pale Straika wao Shola Ameobi alipoangushwa waziwazi ndani ya boksi na Joleon Lescott lakini Refa Martin Atkinson akageuka kipofu na kupeta kelele za penati.
Ferguson aridhika na pointi ya Sunderland
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema sare ya 0-0 waliyoipata huko Sunderland ni sawa yao kwa vile Sunderland walicheza vizuri sana.
Sare hiyo imewafanya Man United wawe wametoka droo mechi zao zote 4 za Msimu huu walizocheza ugenini na kuwafanya wawe nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 13 kwa mechi 7 huku Chelsea wakiwa mbele yao wakiwa na pointi 15 kwa mechi 6.
Leo, Chelsea wanaivaa Arsenal na Manchester City wanacheza na Newcastle na hizi ni mechi ambazo zitageuza msimao wa Timu 4 za juu kama inavyoonyeshwa hapa:
1 Chelsea mechi 6, pointi 15
2 Man United mechi 7 pointi 13
3 Arsenal mechi 6 pointi 11
4 Man City mechi 6 pointi 11
Ferguson amesema ameridhika kwa kutofungwa goli hata moja hasa kwa vile Msimu huu difensi yake imekuwa ikivuja lakini kwa mechi mbili sasa tangu Rio Ferdinand kupona na kurudi uwanjani kuwa patna wa Nemanja Vidic, Man United haijafungwa bao.
Juzi Jumatano waliifunga Valencia bao 1-0 kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.
Katika mechi hiyo ya jana, Man United walimpumzisha Nyota wao Wayne Rooney ambae alikuwa akiuguza enka.
Eriksson ni Bosi mpya Leicester City
Sven-Goran Eriksson ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa Leicester City ambayo iko Daraja la Coca Cola Championship, chini tu ya Ligi Kuu, kuchukua nafasi ya Paulo Sousa alietimuliwa juzi Ijumaa.
Eriksson, Miaka 62, na aliewahi kuwa Kocha wa England na pia Manchester City, amesaini Mkataba wa Miaka miwili na Klabu hiyo ambayo iko mkiani kwenye Ligi ya Daraja lake.
Mwenyewe Eriksson ametamka: “Nina furaha kuwa hapa. Klabu inataka kupanda Ligi Kuu na hilo pia ni lengo langu.”
Eriksson amekuwa hana kibarua tangu alipoiongoza Ivory Coast kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwezi Juni na kabla ya hapo alikuwa ni Mkurugenzi wa Soka huko Notts County kazi ambayo aliichukua mara baada ya kutupwa nje kama Kocha wa Mexico ambako alidumu kuanzia Juni 2008 hadi Aprili 2009.