Sunday 3 October 2010

Man City 2 Newcastle 1
Manchester City wakiwa uwanja wa nyumbani, City of Manchester, walishinda mabao 2-1 dhidi ya Newcastle katika mechi ya kwanza kati ya 3 za leo za Ligi Kuu England na kufikisha pointi 14 na sasa wako pointi moja mbele ya wapwa zao Manchester United.
Ni Man City ndio walitangulia kupata bao kwa penati ya Carlos Tevez dakika ya 18 baada ya Tevez kufanyiwa faulo na Mike Williamson.
Newcastle walisawazisha kwa mkwaju wa Jonas Gutierrez dakika ya 24.
Lakini Mchezaji Adam Johnson alietoka benchi ndie aliwapa ushindi Man City kwa kufunga bao la pili dakika ya 75.
Newcastle watahisi wameonewa pale Straika wao Shola Ameobi alipoangushwa waziwazi ndani ya boksi na Joleon Lescott lakini Refa Martin Atkinson akageuka kipofu na kupeta kelele za penati.

No comments:

Powered By Blogger