Saturday, 23 August 2008
Arsenal kiwango chasikitisha!!
Timu ya Arsenal ambayo ni moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa kwenye LIGI KUU UINGEREZA ilicheza mchezo mbovu na kujikuta wanakung'utwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Craven Cottage walipocheza na Fulham.
Bao la ushindi la Fulham lilipachikwa dakika ya 21 na Brede Hangeland.
Hii ni mechi ya pili kwa Arsenal na ya kwanza walishinda kwa mbinde bao 1-0 nyumbani kwao Uwanja wa Emirates walipocheza na timu iliyopanda daraja msimu huu West Brom.
TIMU ZILIKUWA:
Fulham: Schwarzer, Pantsil, Hughes, Hangeland, Kallio, Davies, Bullard, Murphy, Gera, Zamora, Ki-Hyeon.Subs Not Used: Stockdale, Teymourian, Nevland, Stoor, Dempsey, Milsom, Baird.
Arsenal: Almunia, Sagna, Toure, Gallas, Clichy, Walcott, Eboue, Denilson, Nasri, Adebayor, Van Persie.Subs Not Used: Fabianski, Ramsey, Song Billong, Wilshere, Djourou, Bendtner, Gibbs.
WATAZAMAJI: 25,276
Refa: Martin Atkinson (W Yorkshire).
BLACKBURN 1 v HULL CITY 1
LIVERPOOL 2 v MIDDLESBROUGH 1
NEWCASTLE 1 v BOLTON 0
STOKE CITY 3 v ASTON VILLA 2
TOTTENHAM 1 v SUNDERLAND 2
WEST BROM 1 v EVERTON 2
RIPOTI ZA MECHI KWA UFUPI:
West Brom 1-2 Everton
Magoli ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Leon Osman na Ayegbeni Yakubu yaliwapa ushindi Everton waliocheza ugenini dhidi ya West Brom.
Bao la West Brom lilifungwa dakika ya 89 na Bednar kwa njia ya penalti.
Blackburn 1-1 Hull
Timu iliyopanda daraja msimu huu Hull City wamezidi kugangamara na kutoka suluhu ugenini ya bao 1-1 na Blackburn.
Jason Roberts wa Blackburn aliua mtego wa kuotea na kufunga bao dakika ya 39 lakini Hull City wakasawazisha muda mfupi baadae kupitia Richard Garcia aliefunga kwa kichwa.
Katika mechi yao ya kwanza LIGI KUU Hull City waliwafunga Fulham 2-1.
Liverpool 2-1 Middlesbrough
Steven Gerrard alipiga mkwaju mkali katika dakika za majeruhi na kufunga bao la ushindi kwa Liverpool ambao wengi walitegemea wamekufa nyumbani kwao baada ya Mido kuwapa bao la kuongoza Middlesbrough katika dakika ya 70 lililodumu hadi dakika ya 86 wakati shuti la Jamie Carragher lilipombabatiza Nahodha wa Boro Emmanuel Pogatetz na kuwasawazishia Liverpool.
Huu ni ushindi wa pili kwa Liverpool kwani wiki iliyopita walishinda ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Sunderland.
Newcastle 1-0 Bolton
Michael Owen alitokea benchi la akiba na kuingizwa uwanjani kwenye dakika ya 53 alifunga bao la ushindi dakika ya 71 na kufanya mechi Newcastle 1 Bolton 0.
Katika mechi yao ya kwanza ya LIGI KUU Newcastle walilazimisha sare ya 1-1 na Man U walipocheza Old Trafford nyumbani kwa Mabingwa hao wa LIGI KUU.
Stoke City 3-2 Aston Villa
Mamady Sidibe aliwapatia Stoke City bao la tatu na la ushindi katika dakika za majeruhi kwenye vuta nikuvute walipocheza na Aston Villa.
MAGOLI YA STOKE CITY: Lawrence dakika ya 30 kwa penalti, Fuller 80, Sidibe 90.
MAGOLI YA ASTON VILLAs: Carew 63, Laursen 84.
JUMAMOSI, 23 August 2008
[saa 11 jioni bongo time]
BLACKBURN v HULL CITY
[ITAONYESHWA LAIVU DSTV SUPERSPORT3]
[LAIVU GTV GS2]
[LAIVU GTV GS1]
[saa 1 na nusu usiku bongo time]
FULHAM v ARSENAL
[LAIVU GTV GS1]
Friday, 22 August 2008
Tmu ya Brazil ikiongozwa na Nahodha Ronaldinho imefanikiwa kuifunga Belgium 3-0 na kutwaa Medali ya Shaba kwenye mashindano ya soka upande wa wanaume.
Magoli ya Brazil yalifungwa na Diego Rafes dakika ya 28 na Jo dakika ya 45 na 92.
Jana Brazil ya wanawake ilikosa Medali ya Dhahabu baada ya kufungwa na USA bao 1-0.
Kesho ni Fainali ya wanaume kati ya Nigeria na Argentina.
Thursday, 21 August 2008
Manchester City wameafikiana na Klabu ya Hamburg ya Ujerumani kumnunua Mlinzi wa Kibelgiji Vincent Kompany [22] ambae ameshaichezea Timu ya Taifa ya Ubelgiji mara 23.
Mpaka sasa Meneja wa Man City Mark Hughes ameshawasaini Mbrazil Jo kutoka CSKA Moscow na Tal Ben Haim kutoka Chelsea.
SUNDERLAND WAPATA WA PILI SIKU MOJA!!!
Sunderland wamemnunua David Healy kutoka Fulham kwa mkataba wa miaka mitatu na anakua Mchezaji wa pili kuchukuliwa na Klabu hiyo kwa leo baada ya Djibril Cisse kusaini leo kwa mkopo.
Meneja wa Sunderland amesema anamfahamu David Healy tangu alipoanza kucheza Man U na anaamini atasaidia sana Sunderland.
WANAWAKE: USA WATWAA DHAHABU, BRAZIL FEDHA NA UJERUMANI SHABA!
England 2-2 Czech Rep.
Wembley Stadium, London
Scotland 0-0 Northern Ireland
Hampden Park, Glasgow
Norway 1-1 Rep. Ireland
Ulleval Stadium, Oslo
France 3-2 Sweden
Ullevi Stadium, Gothenburg
Portugal 5-0 Faroe Islands
Estadio Municipal, Aveiro
Belarus 0-0 Argentina
Dinamo Stadium, Minsk
Cisse alichezea timu ya Liverpool iliyochukua Ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2006 na ashawahi kuvunjika miguu yote miwili alipokuwa na Liverpool na hivyo kukosa kuichezea Ufaransa kwenye Kombe la Dunia mwaka 2006.
Sunderland inayoongozwa na Meneja Roy Keane, Nahodha wa zamani wa Man U, ishawasajili msimu huu Wachezaji wapya watatu kutoka Tottenham yaani Teemu Tainio, Steed Malbranque na Pascal Chimbonda na vilevile El Hadji Diouf kutoka Bolton.
[saa 11 jioni bongo time]
LIVERPOOL v MIDDLESBROUGH
NEWCASTLE v BOLTON
STOKE CITY v ASTON VILLA
TOTTENHAM v SUNDERLAND
WEST BROMWICH ALBION v EVERTON
[saa 1 na nusu usiku bongo time]
JUMAPILI, 24 August 2008
[saa 9 na nusu mchana bongo time]
[saa 12 jioni bongo time]
[saa 4 usiku bongo time]
Goli la kwanza lilifungwa na Milan Baros wa Czech dakika ya 22 na Wes Brown akasawazisha dakika ya 45. Dakika ya 48 Czech wakapata bao la pili lililodumu hadi dakika ya 90 Joe Cole aliposawazisha.
Uingereza ambayo iliwakatisha Washabiki wake hiyo jana kwa mchezo mbovu itaanza kampeni yake ya kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi ujao kwa mechi dhidi ya Andorra tarehe 6 Septemba na tarehe 10 Septemba wanacheza na Croatia.
UINGEREZA: James, Brown, Ferdinand (Woodgate 57), Terry, Ashley Cole, Beckham (Jenas 79), Barry, Lampard (Bentley 79), Gerrard (Joe Cole 57), Defoe (Heskey 46), Rooney (Downing 69).AKIBA: Robinson, Hart, Johnson, Bridge, Upson, Walcott.
MAGOLI: Brown 45, Joe Cole 90.
Czech Republic: Cech, Grygera (Pospech 46), Ujfalusi, Rozehnal, Jankulovski, Vlcek (Jarolim 46), Kovac (Rajnoch 75), Polak, Plasil (Papadopulos 90), Sirl (Kadlec 75), Baros (Sverkos 46).AKIBA: Zitka.
MAGOLI: Baros 22, Jankulovski 48.
WATAZAMAJI: 69,738
REFA: Terje Hauge (Norway).
Mikael Silvestre wa MAN U anunuliwa ARSENAL
Silvestre [31] alijiunga na Man U Septemba 1999 na alikuwa amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Man U ingawa ilikuwa dhahiri asingeongezewa muda na klabu hiyo.
Tangu Patrice Evra ajiunge Man U kutoka Monaco mwaka 2006 Silvestre amekuwa akikosa namba timu hiyo.
Silvestre amechezea mechi 249 za LIGI KUU kwa timu ya Man U na ni mchezaji wa kwanza kuuzwa kwa Arsenal tangu alipouzwa Brian Kid mwaka 1974.
Tuesday, 19 August 2008
Argentina 3 Brazil 0 !!!!!
Ni mechi ambayo wapenzi wengi wa Brazil wanaamini Refa kutoka Uruguay hawakuwatendea haki pale aliporuhusu bao la kwanza lililofungwa kwa mkono, la pili la kuotea na la tatu la penalti tata na vilevile kuwanyima bao lao safi!!
Lakini juu ya yote ni pale Refa huyo wa Uruguay kuwapa wachezaji wawili wa Brazil kadi nyekundu huku watani wa jadi Argentina wakicheza rafu ambazo Refa alizipeta tu!
Hii ina maana Nigeria watakutana na Argentina kugombea Medali ya Dhahabu kwenye Fainali na atakaefungwa mechi hii atapata Medali ya Fedha.
Brazil watamenyana na Belgium kwenye patashika ya Medali ya Shaba.
LIGI KUU UINGEREZA imetangaza kwamba tarehe ya mwisho ya kipindi cha uhamisho wa Wachezaji itakuwa Septemba 1 badala ya 31 Agosti 2008 kwa sababu tarehe hiyo Agosti 31 imeangukia Jumapili.
Baada ya tarehe hiyo Klabu haziruhusiwi kuhamisha tena Wachezaji hadi kipindi kingine cha uhamisho kinachoanza tarehe 1 Januari, 2009.
Nigeria wamewabamiza Belgium mabao 4-1 na kuingia Fainali ya Soka ya Olimpiki kwa Wanaume na hivyo kujihakikishia angalau Medali ya Fedha ikiwa watashidwa hiyo fainali ambayo watakutana na mshindi kati ya watani wa jadi Brazil au Argentina ambao watapambana katika Nusu Fainali inayoanza muda si mrefu.
Katika Olympic za 1996 huko Atalanta, Marekani Nigeria walitwaa Medali ya Dhahabu baada kushinda Fainali ikiwa na akina Kanu.
Mpaka mapumziko Nigeria ilikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Olubayo Adefemi.
Mchezaji wa Everton Victor Anichebe alitoa pande zuri kwa Chinedu Ogbuke Obasi aliepachika goli la pili, Obasi akafunga la tatu na Chibuzor Okonkwo akapachika la nne.
Laurent Ciman akapata bao la kufuta machozi kwa Belgium ambao bado wana nafasi ya kupata Medali ya Shaba kwani watakutana na timu itakayofungwa kati ya Brazil na Argentina kugombea medali hiyo.
Monday, 18 August 2008
Wakati kesho ni mechi za Nusu Fainali za Soka upande wa Wanaume leo timu za Soka za Wanawake za Brazil na USA zimetinga Fainali.
Timu ya Wanawake ya Brazil ikiongozwa na Mchezaji Bora wa Dunia kwa Wanawake Marta [pichani] leo iliwabamiza Mabingwa wa Dunia wa Wanawake Ujerumani kwa mabao 4-1. Nao Mabingwa watetetezi wa Olympic upande wa Wanawake USA waliwafunga Japan 4-2 katika Nusu Fainali nyingine.
Kesho saa 7 mchana saa za bongo Nusu Fainali ya kwanza upande wa Wanaume itachezwa kati ya Nigeria na Belgium.
Saa 10 jioni watani wa jadi Brazil na Argentina watashuka dimbani.
Kiungo wa Manchester United Michael Carrick atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu baada ya kuumia enka kwenye mechi ya jana dhidi ya Newcastle ambayo iliisha kwa bao 1-1.
Carrick alitoka nje ya kiwanja kwenye dakika ya 25 ya mechi.
Hii ina maana mchezaji huyu atazikosa mechi za Man U mbili ya kwanza ni ya LIGI KUU tarehe 25 Agosti dhidi ya Portsmouth.
Ya pili ni ya tarehe 29 Agosti 2008 itakayochezwa huko Monaco kugombea European Super Cup dhidi ya Klabu ya Kirusi Zenit St Petersburg ambao ni Mabingwa wa Kombe la UEFA. Super hushindaniwa kati ya Bingwa wa LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA na Bingwa wa Kombe la UEFA.
Carrick sasa anajumuika kwenye listi ndefu ya Wachezaji wa Man U ambao hawataonekana uwanjani kwa muda kutokana na sababu mbalimbali.
Kwenye mechi hiyo hiyo ya jana Ryan Giggs na chipukizi Frazier Campbell waliumia na ilibidi watolewe.
Wengine ambao hawakuwepo na hawatakuwepo ni Cristiano Ronaldo, Louis Saha, Park Ji-Sung and Owen Hargreaves ambao wote ni majeruhi, Nani amefungiwa mechi mbili, Anderson yuko na Timu ya Brazil kwenye michuano ya Olympic na Carlos Tevez yuko Argentina kwenye msiba wa familia.
Sunday, 17 August 2008
Mabingwa wa LIGI KUU UINGEREZA Manchester United wameanza kampeni ya kutetea ubingwa wao kwa suluhu ya 1-1 na timu ya Newcastle kwenye uwanja wao wa Old Trafford.
Ingawa Man U walitawala dakika 20 za mwanzo na kukosa mabao kadhaa ya wazi Newcastle ndio waliopata bao kwanza wakati Mnigeria Obafemi Martins alipofunga kwa kichwa kufuatia mpira wa kona.
Bao hili lilidumu dakika moja tu na Darren Flrtcher akarudisha baada ya muvu nzuri ya Mabingwa hao.
Baada ya hapo Man U walipata pigo pale kiungo Michael Carrick alipoumia na kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na John O’Shea.
Kipindi cha pili Man U iliwaingiza chipukizi wawili kutoka Brazil ambao ni Rodrigo Possebon na Rafael Da Silva. Vijana hao. Mbali ya Man U kutoshinda, walionyesha ni wachezaji wenye vipaji.
Mchezaji tegemeo Carlos Tevez hakuwepo kwenye timu kwa sababu amerudi kwao Argentina baada ya kupata msiba kwenye familia.
Man Utd: Van der Sar, Brown, Vidic, Ferdinand, Evra, Fletcher, Carrick, Scholes, Giggs, Campbell, Rooney. AKIBA: Kuszczak, Neville, Rafael Da Silva, O'Shea, Evans, Gibson, Possebon.
Newcastle: Given, Beye, Taylor, Coloccini, N'Zogbia, Milner, Butt, Guthrie, Gutierrez, Duff, Martins. AKIBA: Harper, Jose Enrique, Bassong, Smith, Geremi, Edgar, Donaldson.
Aston Villa wamewafunga Manchester City 4-2 katika mechi ambayo imechezwa Villa Park nyumbani kwa Aston Villa.
Goli la kwanza la Villa lilifungwa na John Carew na Elano akarudisha kwa Man City kwa penalti.
Gabriel Agbonlahor akapachika mabao matatu kwa Villa na Vedran Corluka akafunga la pili kwa Man City.
Timu zilikuwa:
Aston Villa: Friedel, Luke Young, Davies, Laursen, Shorey, Reo-Coker, Petrov, Barry, Ashley Young, Agbonlahor, Carew. AKIBA: Taylor, Harewood, Knight, Salifou, Routledge, Gardner, Osbourne.Man City: Hart, Corluka, Richards, Ben-Haim, Garrido, Etuhu, Gelson, Johnson, Petrov, Elano, Evans. AKIBA: Schmeichel, Michael Ball, Onuoha, Ireland, Hamann, Sturridge, Caicedo.
Wawashindilia Portsmouth 4-0!
Katika mechi yao ya kwanza ya msimu huu wa LIGI KUU na pia mechi ya kwanza kwa Meneja mpya Mbrazil Scolari Chelsea wametoa onyo kali pale walipowabamiza Mabingwa wa FA Portsmouth kwa mabao 4-0.
Mpaka haftaimu, Chelsea walikuwa mbele kwa bao 3-0 mabao yaliyofungwa na Joe Cole, Anelka na Frank Lampard.
Mreno Deco akicheza mechi yake ya kwanza ya LIGI KUU alifunga bao la nne.
Beki wa Arsenal Justin Hoyte ameuzwa kwa klabu ya Middlebrough kwa Pauni milioni 3.
Beki huyu Mwingereza mwenye umri wa miaka 23 alianza kuchezea Arsenal tangu timu ya watoto na amecheza jumla ya mechi 68 kwenye kikosi cha kwanza tangu msimu wa 2002/3 ingawa hakuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi hicho.
Wachezaji wengine waliouzwa msimu huu na klabu walizoenda pamoja na dau lao kwenye mabano ni Gilberto Silva (Panathinaikos, £1m), Alexander Hleb (Barcelona, £11.8m), Jens Lehmann (Stuttgart, bure-mkataba uliiisha) na Mathieu Flamini (AC Milan, bure-mkataba uliisha)
Nusu Fainali za Soka kwenye Olimpiki zitachezwa siku ya Jumanne kwa mechi baina ya Nigeria na Belgium na mechi nyingine ni ya watani wa jadi Brazil na Argentina.
Kwenye Robo Fainali jana Nigeria iliifunga Ivory Coast 2-0, Belgium ikaitoa Italy 3-2, Brazil iliifunga Cameroun 2-0 na Argentina waliwatoa Holland 2-1.
Fainali ni tarehe 23 Agosti 2008.