Thursday 21 August 2008

SOKA OLIMPIKI:
WANAWAKE: USA WATWAA DHAHABU, BRAZIL FEDHA NA UJERUMANI SHABA!
Timu ya Wanawake ya Brazil ikiongozwa na Mchezaji Bora wa Dunia Marta licha ya kutawala dakika zote za mchezo na kukosa lukuki ya magoli ilifungwa bao 1-0 na USA na hivyo kukosa Medali ya Dhahabu ambayo wameitwaa USA.
Bao la USA lilifungwa dakika ya 97 na Carli Lloyd wakati mechi ilipoingia kwenye nusu saa ya muda wa ziada.
Awali Ujerumani iliwafunga Japan 2-0 kwa mabao yaliyofungwa na Fatmire Bajramaj na kuwa washindi wa tatu na kutwaa Medali ya Shaba.

WANAUME: FAINALI JUMAMOSI!
NIGERIA v ARGENTINA!
Ijumaa Agosti 22 saa nane mchana Timu ya Wanaume ya Brazil inapambana na Belgium kutafuta mshindi wa Medali ya Shaba.
Nigeria watajimwaga na Argentina kwenye FAINALI kupata Bingwa wa Olimpiki kuanzia saa kumi jioni saa za bongo siku ya Jumamosi.
Katika Nusu Fainali, Argentina waliwabamiza wapwa zao Brazil mabao 3-0 na Nigeria waliwashindilia Belgium 4-2.

No comments:

Powered By Blogger