Saturday 21 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Wigan 0 Chelsea 6
Leo Chelsea wakicheza ugenini Uwanja wa DW waliendeleza ubabe wao Ligi Kuu kwa kuichapa Wigan kwa mabao 6-0 huu ukiwa ushindi wao wa pili mfululizo baada ya kuwachapa West Bromwich 6-0 wiki iliyopita.
Kwa Wigan hiki ni kipigo chao cha pili mfululizo hapo kwao DW baada ya kupigwa 4-0 na Blackpool Wiki iliyopita.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Malouda, Anelka, bao mbili, Kalou, bao mbili na Benayoun.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Arsenal 6 Blackpool 0
• Walcott ameremeta kwa bao 3!!!
Arsenal wakiwa kwao Emirates leo wametoa somo kwa Timu mpya Blackpool ambayo wiki iliyokwisha iliitandika Wigan bao 4-0 kwa kuibugiza mabao 6-0 huku bao 3 zikifungwa na Winga Theo Walcott ambae leo aling’ara sana.
Blackpool waliijikuta maji shingoni baada ya dakika 32 tu, huku wakiwa nyuma kwa bao 1 la Walcott la dakika ya 13, wakajikuta wakitoa penalti pamoja na Kadi Nyekundu kwa Beki wao Ivan Evatt aliemwangusha Marouane Chamakh ndani ya boksi.
Penalti hiyo ilifungwa na Andre Arshavin.
Mabao mengine ya Arsenal yalifungwa na Walcott, dakika ya 39 na 58, Abou Diaby, dakika ya 49 na Marouane Chamakh dakika ya 83.
Vikosi vilivyoanza:
Arsenal: Almunia, Sagna, Song, Vermaelen, Clichy, Diaby, Wilshere, Walcott, Rosicky, Arshavin, Chamakh.
Akiba: Fabianski, Fabregas, van Persie, Vela, Djourou, Eboue, Gibbs.
Blackpool: Gilks, Baptiste, Evatt, Cathcart, Crainey, Sylvestre, Vaughan, Adam, Grandin, Harewood, Taylor-Fletcher.
Akiba: Halstead, Eardley, Ormerod, Basham, Edwards, Demontagnac, Keinan.
Refa: Michael Jones
KWA UFUPI: Mechi nyingine za Ligi Kuu
Everton 1 Wolverhampton 1
Ingawa walitawala mechi hii na pia wakiwa nyumbani, Everton walijikuta wakitoka sare 1-1 na Wolves waliojitutumua sana.
Everton ndio walipata bao mwanzo kupitia Tim Cahill dakika ya 43 lakini Wolves walisawazisha dakika ya 74 kwa bao la Sylvan Ebanks-Blake.
West Ham 1 Bolton 3
Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa West Ham baada ya Wiki iliyopita kuchapwa 3-0 na Aston Villa ugenini.
Leo wakiwa nyumbani wamepigwa 3-1 na pia kukosa penalti hafifu iliyopigwa na Carlton Cole na Kipa wa Bolton Jussi Jaaskelainen kuicheza.
Mabao ya Bolton yalifungwa na John Elmander, dakika ya 68 na 84, na jingine, la kwanza, West Ham walijifunga wenyewe kwa Beki Mathew Upson kupachika wavuni kwake.
Bao la west Ham lilifungwa na Mark Noble kwa penalty dakika ya 79.
Birmigham 2 Blackburn 1
Blackburn walitangulia kupata bao dakika ya 54 Mfungaji akiwa Steve Nzonzi lakini Birmingham wakazinduka na kufunga bao mbili dakika ya 57 na 71, Mfungaji wa yote akiwa ni Craig Gardner.
Stoke City 1 Tottenham 2
Mabao mawili ya Gareth Bale, dakika ya 20 na 30, yamewapa Tottenham ushindi wa 2-1 ugenini.
Boa la Stoke lilifungwa na Ricardo Fuller dakika ya 25.
West Brom 1 Sunderland 0
Wakiwa wametoka kwenye kichapo cha 6-0 huko Stamford Bridge Wiki iliyopita mikononi mwa Mabingwa Chelsea, WBA leo wamezinduka wakiwa kwao na kuitungua Sunderland bao 1-0 Mfungaji akiwa Mchezaji mpya Mnigeria Peter Odimwingie aliefunga dakika ya 81.
CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI KUU ENGLAND: Matokeo mechi za leo
Jumamosi, 21 Agosti 2010
Arsenal 6 v Blackpool 0
Birmingham 2 v Blackburn 1
Everton 1 v Wolverhampton 1
Stoke 1 v Tottenham 2
West Brom 1 v Sunderland 0
West Ham 1 v Bolton 3
MATOKEO MECHI ZA LEO ZA BUNDESLIGA:
Hannoverscher 1896 2 v Eintracht Frankfurt 1
TSG Hoffenheim 4 v SV Werder Bremen 1
FC Cologne 1 v FC Kaiserslautern 1
Borussia Munchengladbach 1 v FC Nurnberg 1
Freiburg 1 v FC St. Pauli 3
Hamburger SV 2 v Schalke 1
CHEKI: www.sokainbongo.com

Wenger: ‘Scholes ni Mchezaji mzuri lakini Mcheza rafu!’
Bila shaka Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, huenda atamkera rafiki yake wa siku hizi Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United, kwani alipohojiwa na Wanahabari Wenger alimsifia Veterani wa Man United Paul Scholes lakini pia akamponda kuwa ni Mchezaji anaecheza rafu nyingi.
Wenger, akihojiwa, alijibu: “Unaniuliza kama Scholes anacheza mchezo mzuri uwanjani, nitajibu hapana! Hucheza rafu sana!”
Mwaka jana, Wenger aliwahi kumsema Kiungo wa Man United, Darren Fletcher, kuwa katika mechi iliyochezwa Old Trafford na Man United kuichapa Arsenal alichezeshwa tu ili kucheza rafu tu na kuwasimamisha Arsenal.
Alipotajiwa kuwa Mchezaji wake wa zamani Patrick Viera alikuwa na rekodi mbovu ya kucheza rafu kupita Scholes, Wenger akang’ang’ania kuwa ingawa Scholes ni Mchezaji mzuri lakini ni mcheza rafu.
Mchina abwaga manyanga kuinunua Liverpool
Tajiri wa Hong Kong, Kenny Huang, amejitoa katika ununuzi wa Klabu ya Liverpool baada kuona ofa yake inazungushwa tu na kuwekewa mizengwe.
Mara baada ya Huang kutoa ofa ya kuinunua Liverpool kutoka kwa wenye mali Wamarekani wawili, Tom Hicks na George Gilleet, akaingia mnunuzi wa pili kutoka Syria Yahya Kirdi.
Liverpool ina madeni zaidi ya Pauni Milioni 350.
Wakati huo huo, Meneja wa Liverpool, Roy Hodgson, amesema huenda akamtoa kwa mkopo Alberto Aquilani ili arudi kwao Italia.
Aquilani alinunuliwa Mwaka jana kwa Pauni Milioni 20 ili kuchukua nafasi ya Xabi Alonso aliehama lakini ameshindwa kujizatiti Klabuni hapo na amekuwa akikumbwa na majeruhi mara kwa mara.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Vidic asaini Mkataba mpya Man United
Nemanja Vidic amesaini Mkataba mpya wa Miaka minne na Klabu yake Manchester United na hivyo kuondoa kabisa uvumi kuwa anahama.
Vidic alikuwa akiunganishwa na kuhamia AC Milan na Real Madrid.
Mara baada ya Vidic kusaini  Mkataba huo huku mbele ya Mkurugenzi Mtendaji, David Gill, na Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, Ferguson aliamka: “Hii inaua uvumi wote. Vidic ni sentahafi bora Ulaya na tumefurahi tutakuwa nae kwa Miaka mingi ijayo.”
Vidic alijiunga na Manchester United Januari 2006 kutoka Spartak Moscow na kuiwezesha Klabu yake, akiwa patna na Rio Ferdinand kwenye difensi, kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 3 pamoja na Ubingwa wa Ulaya Mwaka 2008.
Ireland aiponda Klabu yake ya zamani Man City!
Stephen Ireland ameishambulia vikali Manchester City, kuanzia Meneja wake Roberto Mancini na baadhi ya Wachezaji wa Timu hiyo ambao amesema wameheuka kwa fedha na hatua yake hiyo inafuatia kukasirishwa kwake kwa kulazimika kuhamia Aston Villa.
Ireland alilazimika kuondoka Man City kwenda Aston Villa ikiwa ni makubaliano ya Klabu hizo mbili ili kukamilisha uhamisho wa James Milner kutoka Aston Villa kwenda Man City.
Miongoni mwa maneno ya Ireland, Miaka 24, ambae alianzia Soka lake hapo Man City tangu akiwa na Miaka 15, ni pamoja na kudai:
• James Milner atapata mstuko akitua Man City kwani huko si kuzuri kama anavyotarajia.
• Amedai Meneja Mancini hana uhusiano mzuri na Wachezaji wake.
• Ireland amejigamba yeye ni sawa au mzuri zaidi ya Wachezaji wapya waliosainiwa na Man City Msimu huu.
• Wachezaji wapya wa Man City wanaheuka kwa fedha na kuvaa Saa za mkononi za bei mbaya za zaidi ya Pauni 10,000.
• Wachezaji wa Man City hawatambui tena uaminifu na utiifu kwa Klabu hiyo.
• Alimponda Mancini kwa kumbeza na kwamba amesahau yeye siku zote alikuwa Mchezaji bora mazoezini.
Ireland pia alisema: “Nimefika Villa na nimeshangazwa. Ni Klabu ya kifamilia, kila Mtu ni mstaarabu. Ni tofauti na Man City.”
PAULO ZE PWEZA: Aunga mkono Nchi yake England!!
Ingawa imeelezwa amestaafu kutabiri matokeo ya mechi za Soka baada kujijengea Usupastaa alipokuwa akitabiri kwa usahihi wakati wa Fainali za Kombe la Dunia zilizochezwa huko Afrika Kusini, Pweza Paulo ameibuka na kuiunga mkono Nchi yake aliyozaliwa England kuwa ndio itashinda kinyang’anyiro cha kuwa Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 ambazo England ni mmoja wa Wagombea.
Paulo Ze Pweza kwa sasa anaishi kwenye bwawa lake kwenye Kituo cha Viumbe wa Baharini kiitwacho Sea Life huko Oberhausen, Ujerumani lakini alizaliwa huko Weymouth, England Mwaka 2008.
CHEKI: www.sokainbongo.com

BUNDESLIGA Yaanza!
• Bayern yashinda dakika za majeruhi!
Mabingwa Watetezi wa Bundesliga, Bayern Munich, jana walihitaji goli la dakika za majeruhi ili waifunge VfL Wolfsburg 2-1 katika mechi ya kwanza ya Msimu mpya wa Ligi hiyo ya Ujerumani.
Mabao ya Bayern Munich yalifungwa na Thomas Mueller na Bastian Schweinsteiger.
Bao la Wolfsburg lilifungwa na Edin Dzeko.
MECHI ZA LEO ZA BUNDESLIGA:
Hannoverscher 1896 v Eintracht Frankfurt
TSG Hoffenheim v SV Werder Bremen
FC Köln v FC Kaiserslautern
Borussia Mönchengladbach v FC Nurnberg Week
SC Freiburg v FC St. Pauli
Hamburger SV v Schalke 04
SPAIN SUPER CUP: Leo marudio FC Barcelona v Sevilla
Baada ya kuchapwa 3-1, leo wakiwa kwao Nou Camp, FC Barcelona wanahitaji ushindi mnono ili waibwage Sevilla na kutwaa Taji la Supercup ambalo huashiria mwanzo mwa Msimu mpya huko Spain.
Ligi ya Spain, La Liga, inategemewa kuanza Agosti 28.
Fergie: ‘Hamna tena Mchezaji mpya Msimu huu!’
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesisitiza kuwa Kikosi chake cha sasa kinaridhisha hivyo hataongeza Mchezaji yeyote kabla Dirisha la Uhamisho kufunga Agosti 31.
Tayari Ferguson alishatamka kuwa haongezi Mchezaji hasa kwa vile soko lenyewe limepotoshwa na ununuzi wa Wachezaji kwa bei mbaya hasa unaofanywa na Manchester City na kuifanya thamani ya Wachezaji wenye majina makubwa kupandishwa mno kupita thamani yao halisi.
Hata hivyo, Vyombo vya Habari vimeendelea kuwahusisha baadhi ya Wachezaji na kuhamia Man United na sasa anavumishwa Kiungo wa Real Madrid kutoka Uholanzi, Rafael van der Vaart, kuwa yuko mbioni kutua Old Trafford.
Msimu huu, Ferguson amewanunua Wachezaji watatu tu Chipukizi kwa bei poa na nao ni Bebe, Javier Hernandez, aka Chicharito, na Chris Smalling.
Akihojiwa kuhusu kikosi chake, Ferguson alitamka: “Hatuna tatizo. Kila pozisheni uwanjani ipo poa.”
Wakati huo huo, Kiungo Chipukizi wa Man United kutoka Brazil, Rodrigo Possebon, atajiunga na Santos ya Brazil kwa Mkataba wa Miaka minne.
Possebon alijiunga na Man United Mwaka 2008 akitokea Klabu ya Brazil Internacional lakini alishindwa kujikita Kikosi cha Kwanza cha Man United.

Friday 20 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI KUU ENGLAND: Mechi za Wikiendi hii
[Saa za Bongo]
Jumamosi, 21 Agosti 2010
[Saa 11 jioni]
Arsenal v Blackpool
Birmingham v Blackburn
Everton v Wolverhampton
Stoke v Tottenham
West Brom v Sunderland
West Ham v Bolton
[Saa 1 na robo usiku]
Wigan v Chelsea
Jumapili, 22 Agosti 2010
[Saa 9 na nusu mchana]
Newcastle v Aston Villa
[Saa 12 jioni]
Fulham v Man Utd
Jumatatu, 23 Agosti 2010
[Saa 4 usiku]
Manchester City v Liverpool
TATHMINI:
Timu iliyopanda Daraja, Blackpool, itatua Uwanja wa Emirates wakitafuta ushindi wao wa pili katika mechi mbili za Ligi Kuu baada ya kuichapa Wigan 4-0 lakini kazi hiyo itakuwa ngumu kwa vile Wenyeji wao ni Arsenal ambao wanatafuta ushindi wao wa kwanza baada ya kwenda sare 1-1 na Liverpool katika mechi ya kwanza.
Katika mechi hii, huenda Nahodha wa Arsenal, Cesc Fabregas, akaonekana Uwanjani baada ya kuwa majeruhi.
Baada ya kipigo cha 3-2 ugenini kwenye mechi ya kwanza ya UEFA CHAMPIONS LIGI walichokipata huko Uswisi toka kwa Young Boys siku ya Jumanne, Tottenham wataingia tena ugenini kucheza na Stoke City waliofungwa na Wolves kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu.
Kwenye mechi ya kwanza ya Ligi, Wigan walinyukwa 4-0 na Blackpool na kesho wapo nyumbani Uwanja wa DW kucheza na Mabingwa wa Ligi Kuu Chelsea ambao waliwatandika West Bromwich Albion mabao 6-0.
Msimu uliokwisha, kwenye mechi kama hii, Wigan waliifunga Chelsea.
West Bromwich Albion, baada ya kipigo cha 6-0 huko Stamford Bridge, watakuwa nyumbani kuwakaribisha Sunderland ambao katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Birmingham waliongoza 2-0 lakini wakawaruhusu Birmingham kusawazisha na mechi kwisha 2-2.
West Ham watakuwa kwao Upton Park kucheza na Bolton Wanderers na safari hii wataombea ushindi baada ya kufungwa 3-0 na Aston Villa kwenye mechi ya kwanza.
Bolton walitoka sare 0-0 na Fulham kwenye mechi ya ufunguzi.
Baada ya kuchapwa 1-0 na Blackburn huko Ewood Park, Everton watakuwa nyumbani Goodison Park kucheza na Wolves ambao walishinda mechi ya kwanza 2-1 dhidi ya Stoke City.
Katika Uwanja wa Mtakatifu Andrew, Birmingham watawakaribisha Blackburn Rovers na pambano hili litakuwa gumu hasa kwa vile Birmingham wana rekodi nzuri Uwanjani kwao ya kutofungwa katika mechi zao 15 za mwisho za Ligi Kuu.
Mechi ya kwanza ya Jumapili ni kati ya Newcastle United v Aston Villa Uwanjani St James.
Hii ni mechi ya kwanza ya Uwanja wa nyumbani kwa Newcastle tangu wapande Daraja kurudi tena Ligi Kuu na ni muhimu hasa baada ya kupigwa 3-0 na Manchester United wiki iliyokwisha.
Aston Villa wanaingia kwenye mechi hii wakitoka kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya West Ham.
Mechi ya pili ya Jumapili ni huko Craven Cottage ambako Fulham watacheza na Manchester United ambao katika Misimu miwili iliyopita wamekuwa wakifungwa kila wanapotua Craven Cottage.
Jumatatu usiku, Uwanjani City of Manchester, Timu Tajiri iliyonunua Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu huu kwa jumla ya Pauni Milioni 126, Manchester City wataivaa Liverpol kwenye mechi inayongojewa kwa hamu na Wadau wengi.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Cole ataka radhi kwa kukosa Penalti
Joe Cole amebeba lawama zote kwa kukosa kufunga penalti katika mechi ya jana ya EUROPA LIGI dhidi ya Trabzonspor ya Uturuki ambayo Liverpool walishinda 1-0.
Goli la Liverpool lilifungwa na Ryan Babel baada ya pande la Joe Cole.
Cole ametamka: “Ni bahati mbaya lakini ilikuwa penalti mbovu! Sijawahi kupiga penalti Miaka 15 sasa na itabidi ningoje Miaka 15 ili nipige nyingine!”
Mpiga penalti wa kawaida wa Liverpool kawaida ni Nahodha wao Steven Gerrard lakini jana alipumzishwa.
Kwa Joe Cole, hiyo ni mechi yake ya pili kuichezea Klabu yake mpya Liverpool na katika mechi ya kwanza walipotoka sare 1-1 na Arsenal Jumapili iliyopita alitwangwa Kadi Nyekundu.
Alhamisi ijayo Liverpool itakwenda Uturuki kurudiana na Trabzonspor.
CHEKI: www.sokainbongo.com

EUROPA LIGI: Matokeo
• Rapid Vienna 1 v Aston Villa 1
• FC Timisoara 0 v Man City 1
• Liverpool 1 v Trabzonspor 0
Bao la dakika 45 la Ryan Babel limewapa ushindi Liverpool kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza na Trabzonspor ya Uturuki Uwanjani Anfield huku balaa likiendelea kumkumba Mchezaji wao mpya Joe Cole ambae Jumapili alitwangwa Kadi Nyekundu kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Arsenal na leo akakosa kufunga penalti.
Manchester City wakicheza ugenini huko Romania na Wenyeji wao FC Timisoara waliweza kushinda kwa bao 1-0 Mfungaji akiwa ‘Super Mario’, Bario Balotelli, kwenye dakika ya 72, na hii ikiwa ni mechi yake ya kwanza kwa Klabu yake mpya.
Nao Aston Villa, walitoka sare ugenini na Rapid Vienna kwa bao 1-1.
Marudio ya mechi hizi ni Alhamisi ijayo.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Kocha Ureno, Queiroz afungiwa Siku 30
Kocha wa Timu ya Taifa ya Ureno, Carlos Queiroz, amefungiwa Siku 30 na Chama cha Soka cha Ureno kwa kuwatukana Wakaguzi wa Madawa yaliyopigwa marufuku kwa Wachezaji ambao walikwenda Kambini Nchini Ureno kuwakagua Wachezaji wa Ureno wakati wakijitayarisha kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Queiroz atakosa kuisimamia Timu yake kwa mechi za Makundi kugombea kuingia Fainali za EURO 2012 ambazo Ureno watacheza na Cyprus Septemba 3 na Norway siku nne baadae.
Pia, Kocha huyo amepigwa Faini ya Dola 1280.
Kamati ya Nidhamu ya Chama cha Soka cha Ureno, FPF, ilimwona ana hatia ya kutoa matusi lakini haikumkuta na hatia na kosa la kutaka kuwazuia Wakaguzi hao kufanya kazi yao ambalo ni kosa kubwa zaidi na, pengine, lingemfanya amwage unga.
Katika utetezi wake, Queiroz aliita Mashahidi kadhaa, akiwemo Sir Alex Ferguson, alieruka hadi Lisbon, Ureno kutetea tabia njema ya Msaidizi wake wa zamani wa huko Old Trafford.

Thursday 19 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com


Gallas kutua Spurs
Nahodha wa zamani wa Arsenal, William Gallas, anatarajiwa kupimwa afya yake Tottenham Hotspurs kesho Ijumaa huku Klabu kadhaa zikiwa zinamwinda zikiwemo Juventus ya Italia na Panathinaikos ya Ugiriki.
Gallas, Miaka 33, alimaliza Mkataba wake na Arsenal mwishoni mwa Msimu uliopita na Meneja wa Tottenham, Harry Redknapp akatangaza nia yake kumchukua.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Ze Gunners wamng’ang’ania Schwarzer, Fulham wagomea ofa!
Ofa ya pili ya kumnunua Kipa Veterani wa Fulham, Mark Schwarzer, imekataliwa na Klabu hiyo na Meneja wa Fulham, Mark Hughes, amewataka Arsenal wapandishe dau lao.
Mwezi Mei, Arsenal walitoa ofa ya Pauni Milioni 2 kwa Schwarzer, Miaka 37, na hivi juzi wamerudia tena lakini Fulham wanataka fedha zaidi.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, yuko sokoni kutafuta Kipa mwingine baada ya Makipa wake, Manuel Almunia na Lukasz Fabiasnky, kuonekana kulegalega, kupwaya na kuwa uchochoro.
Kufuatia kugoma kwa Fulham, taarifa za ndani ya Arsenal zinadai kuwa macho ya Wenger sasa yako kwa Kipa Shay Given wa Manchester City ambae amepigwa benchi na Chipukizi Joe Hart na hivyo kutaka kuhama.
Kipa mwingine mlengwa wa Wenger ni Maarten Stekelenburg wa Ajax ambae pia aliichezea Kombe la Dunia Uholanzi huko Afrika Kusini.
CHEKI: www.sokainbongo.com

EUROPA LIGI: Ulaya kuwaka moto leo!
• Rapid Vienna v Aston Villa
• FC Timisoara v Man City
• Liverpool v Trabzonspor
Timu 3 za Ligi Kuu England, Aston Villa, Liverpool na Man City, leo ni miongoni mwa lundo la Timu za Ulaya zitakazocheza mechi ya kwanza ya Raundi ya Mchujo ili kuwania kuingia Hatua ya Makundi ya EUROPA LIGI.
Marudio ya mechi za leo ni Wiki ijayo Alhamisi, Agosti 26.
Liverpool wataanza mechi ya leo wakiwa nyumbani Anfield dhidi ya Trabonspor ya Uturuki lakini watacheza bila ya Javier Mascherano ambae aliumia siku ya Jumapili walipotoka sare na Arsenal ya 1-1 kwenye Ligi Kuu.
Lakini, pengine, sababu kubwa ya kutomchezesha Mascherano ni kumlinda thamani yake isipungue kwani inajulikana Mascherano anataka kuhama Liverpool na akicheza leo, Klabu yake mpya haItaruhusiwa kuMchezesha Mashindano ya Ulaya.
Aston Villa na Manchester City zitakuwa ugenini huku Villa wakiwa Austria Uwanja wa Gerhard Happi dhidi ya Rapid Vienna na watacheza bila ya Richard Dunne, aliefungiwa, John Carew, Gabriel Agbonlahor, Carlos Cuellar na James Collins ambao ni majeruhi.
Man City wao wapo Uwanja wa Dan Paltisanu huko Romania kucheza na FC Timisoara na Mchezaji mpya, Supa Mario, Mario Balotelli, huenda akacheza mechi yake ya kwanza.
Ze Gunners mbioni kumnasa Beki Squillaci
Klabu ya Sevilla ya Spain imethibitisha Arsenal na wao wapo mazungumzoni ili Senta hafu wao kutoka Ufaransa, Sebastien Squillaci, ahamie Emirates.
Squillaci aliachwa na Sevilla kwenye Kikosi chao kilichocheza na Braga kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI ili kumfanya asizuiwe kuichezea Arsenal akihamia huko.
Arsenal wapo sokoni kutafuta Beki ili kuziba mapengo yaliyoachwa na William Gallas, Sol Campbell, Mikel Silvestre na Philippe Senderos ambao wote walimaliza Mikataba yao.
Tayari Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ameshanunua Senta Hafu mmoja kutoka Ufaransa ambae ni Laurent Koscielny aliecheza mechi ya Ligi Kuu Jumapili na Liverpool na kutwangwa Kadi Nyekundu.
Squillaci alihamia Sevilla Mwaka 2008 akitokea Lyon.
Liverpool wadai Mascherano atang’oka kwa dau nono!
Kocha wa Liverpool, Roy Hodgson, amesisitiza Kiungo wao kutoka Argentina ataruhusiwa kuondoka Liverpool ikiwa Timu inayomtaka itatoa dau zuri na linalostahili kwa thamani yake.
Mascherano, Miaka 26, ambae ndie Nahodha wa Timu ya Taifa ya Argentina, bado amebakiza Miaka miwili kwenye Mkataba wake na Liverpool lakini mwenyewe amekuwa akitaka kwenda Inter Milan kuungana tena na aliekuwa Meneja wa Liverpool, Rafa Benitez, ambae yuko huko.
Mascherano ameichezea Liverpool mara 138 tangu ahamie hapo kutoka West Ham Mwaka 2007.

Wednesday 18 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

BEBE: ‘Toto la Mtaani’ lapanda chati hadi Old Trafford!!!!
Mwaka mmoja uliopita, Bebe, Miaka 20, jina kamili Tiago Manuel Dias Correja, alishiriki huko Bosnia Sherehe za Soka la Ulaya la Mtaani kwa Watu Wasio na Makazi akitokea kwenye Kituo cha Hifadhi ya Casa do Gaiato ambayo huwekwa Watu wasio na Makazi.
Mara baada ya kuwika huko Bosnia kwa kufunga mabao 40 katika Mechi 6 alizoichezea Timu ya Ureno ya Watu Wasio na Makazi, Bebe akachukuliwa na Timu ya Daraja la 3 Estrela Amadora na hapo akang’ara zaidi na kununuliwa na Vitoria Guimaraes, Timu ya Daraja la Juu.
Ndipo Sir Alex Ferguson akaletewa taarifa Bebe ni ‘lulu’ na Maskaunti wa Manchester United walio Ureno na taarifa hizo zilipigwa dole na aliekuwa Msaidizi wa Ferguson, Carlos Quieroz, ambae sasa ndie Kocha wa Ureno.
Baada ya Miezi mitatu tu kuwa na Vitoria Guimaraes, Bebe akatua Manchester United kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 7.4.
Bebe ametamka: “Kutua Man United ni kutimia kwa ndoto! Kuwa na Wareno hapa ni motisha! Ronaldo aliwahi kucheza hapa. Nani na Anderson wapo hapa. Nataka kuwa kama wao!”
Anderson ni Mbrazil lakini wao huongea Kireno na pia amekulia Kisoka huko Ureno.
Nae Kocha wa Man United, Ferguson, ametamka: “Bebe ni kichocheo kwa Vijana wote ambao hawakujaliwa kuwa na mwanzo mzuri maishani. Ipo mifano mizuri ya Vijana wasiobarikiwa kuanza vizuri maisha yao na kisha wakafanikiwa. Wanachotakiwa ni kuwa na juhudi.”
Boateng anunuliwa na Genoa, aangukia AC Milan
Mchezaji wa Portsmouth, Kevin-Prince Boateng, ameuzwa kwa Klabu ya Italia Genoa wa ada ya Pauni Milioni 5 na mara tu baada ya kukamilika uhamisho huo akakopeshwa kwa AC Milan ambako atakaa kwa Msimu mmoja.
Boateng, miaka 23, aliiwezesha Ghana kufika Robo Fainali ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na alijiunga na Portsmouth Mwaka jana Mwezi Agosti akitokea Tottenham.
CHEKI: www.sokainbongo.com

FUNGUA PAZIA MSIMU MPYA 2010/11: NGAO YA HISANI
Yanga 3 Simba 1
Leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Wapinzani wa Jadi, Yanga na Simba, walijimwaga dimbani katika pambano maalum la kufungua pazia ya Msimu mpya wa 2010/11 kugombea Ngao ya Hisani na Yanga walibuka kidedea kwa kuitwanga Simba kwa mikwaju ya penalti 3-1 baada ya Timu hizo kwenda sare 0-0 hadi mwishoni mwa dakika 90.
Simba walikosa penalti 3 kati ya 4 zilizopigwa na kufunga moja tu.
Yanga walifunga penalti 3 na kukosa moja.
Fulham yamsaini Dembele
Fulham imekamilisha usajili wa Fowadi wa Kimataifa wa Ubelgiji Moussa Dembele ambae anachezea Klabu ya AZ Alkmaar kwa Mkataba wa Miaka mitatu.
Dembele, umri Miaka 23, amechukuliwa kwa ada ya Pauni Milioni 5 na amekuwa akiichezea Klabu ya Uholanzi AZ Alkmaar kwa Miaka mitatu.
Meneja wa Fulham, Mark Hughes, amefurahishwa kwa usajili huo kwani Birmingham pia ilikuwa ikimwania Mchezaji huyo.
UEFA CHAMPIONS LIGI: Tottenham yachapwa 3-2
Klabu Ya Uswisi, Young Boys Berne, imewafunga Tottenham mabao 3-2 katika mechi ya kwanza ya Hatua ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONS LIGI mjini Berne, Uswisi.
Timu hizo zitarudiana White Hart Lane, Jijini London, nyumbani kwa Tottenham, Jumatano ijayo.
Katika mechi nyingine za UEFA CHAMPIONS LIGI hapo jana, Zilina ya Slovakia ilifunga Slavia Prague 2-0, Ajax Amsterdam na Dynamo Kiev zilitoka sare 1-1 huko Kiev.
Rosenborg iliifunga FC Copenhagen 2-1 na Zenit St Petersburg iliishinda Auxerre 1-0.
Huko Uswisi, Young Boys walikuwa mbele kwa ba0 3-0 hadi dakika ya 28 kwa magoli kupitia Senad Lulic, Henri Bienvenu kutoka Cameroun na Xavier Hochstrasser.
Mabao ya Tottenham yalifungwa na Sebastien Bassong na Roman Pavlyuchenko.
Leo kutakuwa na mechi 5 za UEFA CHAMPIONS LIGI na marudio yake ni Jumanne ijayo.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Anelka acheka kufungiwa
Nicolas Anelka, ambae jana alifungiwa mechi 18 na FFF, Chama cha Soka Ufaransa, amekidhihaki kifungo hicho na kuuita ni upuuzi na kichekesho.
Kamati ya Nidhamu ya FFF hapo jana iliamua kuwapa adhabu Wachezaji wanne kati ya watano waliofikishwa mbele yao kujibu tuhuma za kuongoza mgomo wa Wachezaji huko Afrika Kusini kufuatia kufukuzwa kwa Nicolas Anelka baada ya kugombana na Kocha Raymond Domenech.
Anelka alipewa kifungo cha mechi 18 kutoichezea France na Evra amefungiwa mechi 5.
Ribery amepewa adhabu ya mechi 3 na Jeremy Toulalan mechi moja.
Eric Abidal amenusurika adhabu.
France haikushinda hata mechi moja huko Afrika Kusini na ilimaliza Kundi lake ikiwa mkiani na Timu nzima iligoma kufanya mazoezi baada ya mwenzao Nicolas Anelka kufukuzwa kufuatia kugombana na aliekuwa Kocha wao Raymond Domenech.
Wachezaji wote 23 walisimamishwa kucheza mechi ya kirafiki na Norway iliyochezwa Oslo Agosti 11 na France kufungwa na Norway 2-1 na hatua hiyo ilipendekewa na Kocha mpya Laurent Blanc.
Anelka amesema: ‘Hawa watu ni wachekeshaji. Nakufa kwa kicheko! Upuuzi huo haunihusu kwa vile nilishtaafu Soka ya Kimataifa tangu Juni 19 siku niliyoondolewa Timu ya Ufaransa.”
Nasri kuwa nje Mwezi mzima
Samir Nasri atafanyiwa upasuaji wa goti lake na ataluwa nje ya Uwanja kwa Mwezi mzima.
Nasri aliumia juzi kwenye mechi ya huko Anfield ya Ligi Kuu ambayo Timu yake Arsenal ilitoka sare 1-1 na Liverpool.
Kiungo huyo mwenye Miaka 23 alimaliza dakika 90 za mechi hiyo ya juzi lakini Klabu yake imethibitisha ni lazima afanyiwe operesheni ndogo.
Jumamosi Arsenal ipo nyumbani kwenye Ligi Kuu na itacheza na Timu iliyopanda Daraja Msimu huu Blackpool lakini kukosekana kwa Nasri ni pigo kwani kunaleta udhaifu kwenye Kiungo hasa kwa vile haijulikani kama Nahodha wao Cesc Fabregas ataweza kucheza mechi hiyo.
Anderson arudi mazoezini
Anderson ambae aliumia vibaya goti lake kwenye mechi na West Ham Mwezi Februari Mwaka huu yupo kwenye mazoezi makali na inategemewa ataonekana tena dimbani akiwa na Timu yake Manchester United Mwezi Septemba.
Maumivu hayo ya goti yalimfanya akose kuichezea Nchi yake Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.
Anderson, akiongea kwenye tovuti ya Man United, amesema: “Nina furaha kurudi baada ya Miezi 6 bila Soka. Najiskia vizuri na nipo kwenye mazoezi makali sasa. Sina tatizo tena na goti, nakimbia na kufanya mazoezi magumu sasa.”

Tuesday 17 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Man United yaanua rasmi Vifaa Vitatu
Sir Alex Ferguson leo amewatambulisha rasmi Wachezaji watatu wapya huku akiwashambulia Wapinzani wao kwao kujiingiza kwenye matumizi ya ‘kamikaze’ katika kununua Wachezaji wapya kwa bei mbaya.
‘Kamikaze’ ni staili ya kujitoa muhanga waliotumia Askari wa Japan kwenye Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Ferguson hakuitaja Klabu yeyote kwa jina ambayo inatumia ‘kamikaze’ lakini, bila shaka, ni jirani zao Manchester City ambao tayari washatumia zaidi ya Pauni Milioni 125 kununua Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu huu mpya wakiwa pamoja na Mario Balotelli, ambae ndio kwanza amesaini, na James Milner, anaetegemewa kukamilisha uhamisho wake hapo kesho.
Ferguson alipiga picha ya pamoja na Wachezaji hao wapya Javier Hernandez aka Chicharito, Chris Smalling na Bebe.
Wakati wa utambulisho, Fergie alizungumza: “Katika Miaka mitatu au miwili iliyopita, tumeona Matajiri wakinunua Klabu na kufanya matumizi ya ‘kamikaze’. Inashangaza! Sioni kama kasi hiyo itapungua. Itachukua Miaka miwili au mitatu ndipo watagundua huwezi ukafanikiwa kwa matumizi kama hayo!”
Ferguson akasisitiza msimamo wa Man United kuendeleza Vijana: “Ukiwatunza vizuri, Vijana wanaendelea. Tena wanakuwa watiifu na waaminifu kwa Klabu kwa kuwa wanataka kulipa fadhila za malezi mazuri.”

CHEKI: www.sokainbongo.com

KIFUNGO: Anelka, mechi 18; Evra, mechi 5 & Ribery,  3!!!!!!
Kamati ya Nidhamu ya FFF, Chama cha Soka France, leo imeamua kuwapa adhabu Wachezaji wanne kati ya watano waliofikishwa mbele yao kujibu tuhuma za kuongoza mgomo wa Wachezaji huko Afrika Kusini kufuatia kufukuzwa kwa Nicolas Anelka baada ya kugombana na Kocha Raymond Domenech.
Anelka amepewa kifungo cha mechi 18 kutoichezea France na Evra amefungiwa mechi 5.
Ribery amepewa adhabu ya mechi 3 na Jeremy Toulalan mechi moja.
Eric Abidal amenusurika adhabu.
Ozil aenda Real
Real Madrid imemnyakua Kiungo wa Ujerumani, Mesut Ozil, alieng’ara na Nchi yake huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia, kwa ada ya Pauni Milioni 12.4.
Ozit, Miaka 21, anachezea Werder Bremen huko Ujerumani na amebakiza Mwaka mmoja tu kumaliza Mkataba wake hivyo imekuwa ni busara kwa Bremen kumuuza sasa la sivyo Mwakani isingepata hata senti.
Ozit anategemewa kupimwa afya yake hapo kesho Jumatano.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Wachezaji watano wa Ufaransa wako kiti moto!!!
Wachezaji watano waliokuwa Timu ya Ufaransa iliyocheza Kombe la Dunia huko Afrika Kusini leo watashuka mbele ya Kamati ya Nidhamu ya FFF, Chama cha Soka France, kujibu shutuma za kuwa vinara wa mgomo wa Wachezaji huko Afrika Kusini.
Wachezaji hao ni Nahodha Patrice Evra, Nicolas Anelka, Eric Abidal, Franck Ribery na Jeremy Toulalan.
France haikushinda hata mechi moja huko Afrika Kusini na ilimaliza Kundi lake ikiwa mkiani na Timu nzima iligoma kufanya mazoezi baada ya mwenzao Nicolas Anelka kufukuzwa kufuatia kugombana na aliekuwa Kocha wao Raymond Domenech.
Wachezaji wote 23 walisimamishwa kucheza mechi ya kirafiki na Norway iliyochezwa Oslo Agosti 11 na France kufungwa na Norway 2-1 na hatua hiyo ilipendekewa na Kocha mpya Laurent Blanc.
Hata hivyo huenda Franck Ribery asiwepo kwenye kiti moto hicho baada ya Klabu yake Bayern Munich kukataa kumruhusu kwa vile wito huo uko nje ya Kalenda ya Kimataifa ya FIFA.
Ferguson ampa Tano Scholes!!!
Sir Alex Ferguson amemmiminia sifa Kiungo wake Veterani Paul Scholes baada ya kuwa ndio injini iliyoleta ushindi wa bao 3-0 hapo jana kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Newcastle Uwanjani Old Trafford.
Ferguson ametamka: “Ni mtoa pasi mzuri na ana akili ya mpira! Mtu yeyote anaecheza kiwango hicho kwa umri wake ni Mchezaji spesho!”
Scholes yupo Manchester United kwa Miaka 17 sasa na amechezea mechi 400 na kutwaa Ubingwa mara 9.
CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI KUU BARCLAYS: Man United 3 Newcastle 0
Manchester United, wakiwa nyumbani Old Trafford, wameanza kampeni yao ya kurudisha taji, kwa kuichapa ‘Timu mpya’ Newcastle mabao 3-0.
Katika Msimu wao wa mwisho Ligi Kuu Mwaka 2008/9 kabla kushushwa Daraja, Newcastle waliweza kutoka sare 1-1 na Man United hapo Old Trafford lakini leo Jumatatu usiku Agosti 16, katika mechi yao ya kwanza tangu wapande Daraja, walikuta habari mpya.
Wakicheza huku wakiwa na Mtu 9 nyuma na kumwacha Straika wao Carroll ahahe peke yake mbele, Newcastle walidumu hadi dakika ya 33 na ndipo Dimitar Berbatov alipowatoboa kwa bao la kwanza.
Bao la pili la Man United lilifungwa na Darren Fletcher baada ya ujanja wa Rooney.
Wakongwe Scholes na Giggs walishirikiana vyema na kusababisha bao la tatu kupitia Giggs dakika ya 85.
Mechi inayofuata kwa Man United ni Jumapili ijayo ugenini dhidi ya Fulham.
Vikosi vilivyoanza:
Man Utd: Van der Sar, O'Shea, Vidic, Jonathan Evans, Evra, Valencia, Fletcher, Scholes, Nani, Berbatov, Rooney.
Akiba: Kuszczak, Rafael Da Silva, Smalling, Carrick, Giggs, Macheda, Hernandez.
Newcastle: Harper, Perch, Coloccini, Williamson, Jose Enrique, Routledge, Smith, Nolan, Barton, Gutierrez, Carroll.
Akiba: Krul, Ryan Taylor, Xisco, Ameobi, Vuckic, Ranger, Tavernier.
Refa: Chris Foy
Almunia kuondoka Ze Gunners!!
Manuel Almunia amekiri kuwa itamlazimu aondoke Arsenal ikiwa Klabu hiyo itamleta Kipa mwingine.
Kumekuwa na taarifa kuwa Arsenal iko mbioni kumchota Kipa wa Fulham Mark Shwarzer au Shay Given toka Manchester City kwa vile Makipa wa Arsenal Almunia na mwenzake Fabianski hawaaminiki.
Almunia ndie aliecheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya sare 1-1 na Liverpool hapo Jumapili na Wadau kumlaumu kwa bao la Liverpool.
Almunia ameungama kuwa ni ngumu kwake kuwa makini huku kuna taarifa kila kona kuwa Kipa mpya atatua Emirates.

Monday 16 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Blatter ataka mabadiliko Kombe la Dunia
Sepp Blatter amesema FIFA inatafakari kuondoa matokeo ya sare kwenye Mechi za Makundi katika Fainali za Kombe la Dunia kwa Timu kupigiana penalti baada ya dakika 90 ikiwa ziko sare.
Rais huyo wa FIFA ametamka: “Penalti kwenye hatua za Makundi zitazimaliza Timu zinazocheza defensi tu. Pia tunafikiria kuondoa muda wa nyongeza wa Dakika 30 kwa Mechi za Raundi ya Pili na kuendelea kwa kurudisha lile goli la dhahabu. Hivyo Timu zikiwa sare Dakika 90 zitaongezwa muda na itayofunga bao ndio Mshindi na Mechi itasimama hapohapo!”
Sheria hiyo ya goli la dhahabu ilitumika kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Ufaransa Mwaka 1998 lakini Fainali iliyofuata ya Mwaka 2002 huko Japan na Korea Kusini ilifutwa.
Blatter anaamini mabadiliko hayo yataleta msisimko zaidi kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa kuziwekea ngumu Timu zinazotaka suluhu tu.
Fainali zinazofuata za Kombe la Dunia ni Mwaka 2014 huko Brazil.
Pia, Blatter alisistiza FIFA iko kwenye jitihadi ya kulipatia ufumbuzi suala la kutumia teknlojia ya kisasa ya kusaidia Marefa kutoa uamuzi sahihi na wa haraka juu ya mpira kuvuka mstari wa goli au la.
Blatter ametamka: “Pale tu tutakapopata mfumo salama, wa haraka na usio na utata, tutautumia!”
Suala hilo la kutumia teknolojia litajadiliwa Mwezi Oktoba kwenye Mkutano wa IFAB [International Football Association Board], chombo ambacho kinaijumuisha FIFA na Vyama vya Soka vya England, Wales, Scotland na Ireland ambavyo ndivyo vinachukuliwa kama Waanzilishi wa Soka na hivyo ndio wenye mamlaka ya kubadili Sheria za Soka Duniani.

Fergie aitwa kama Shahidi!!
Bosi wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, aliruka hadi Ureno kwenda kumtetea Msaidizi wake wa zamani ambae sasa ni Kocha wa Ureno, Carlos Queiroz, anaepigania kunusuru kibarua chake baada ya kushitakiwa na Chama cha Soka cha Ureno kwa kuwa mkali na kuwatukana Maafisa waliotumwa kuwapima Wachezaji wa Ureno kama wanatumia madawa marufuku au la kabla ya kuanza kwa Fainali za Kombe la Dunia.
Ferguson aliitwa kama shahidi wa upande wa utetezi wa Queiroz ili kuthibitisha tabia nzuri ya Kocha huyo.
Queiroz, ambae alikuwa Msaidizi wa Ferguson kwa Miaka mitano huko Old Trafford, amekana shutuma hizo ambazo akipatikana na hatia nazo huenda akafukuzwa kama Kocha wa Ureno.
Katika utetezi huo, Ferguson alitamka: “Ni Kocha Bora na Mwalimu mzuri na lengo lake maishani ni kuwaendeleza Vijana, kuwapa msukumo na kuhakikisha wanakuwa Watu wema na ndio maana nipo hapa kumtetea kwa vile pia namjua vyema na ni Mtu mwenye utiifu na heshima kubwa! Carlos ni mmoja wa Watu wema!”
CHEKI: www.sokainbongo.com

UEFA yataja Majina 12 ya Wagombea Uchezaji Bora Ulaya
• Rooney ndie Mchezaji pekee LIGI KUU!!!
UEFA imetaja majina ya Wachezaji 12 watakaogombea Tuzo za Wachezaji Bora katika pozisheni na pia Mchezaji Bora wa Ulaya wa Mwaka.
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Alhamisi Agosti 26 kwenye Droo ya UEFA CHAMPIONS LIGI ya kupanga Makundi.
Wagombea waliotajwa wanagombea Uchezaji Bora kwenye pozisheni za Kipa, Beki, Kiungo na Fowadi.
Pia, Mchezaji mmoja atachaguliwa kuwa ndie Mchezaji Bora Ulaya wa Mwaka.
Wachezaji hao Bora watachaguliwa na Makocha wa Timu 16 zilizocheza hatua ya Mtoano ya Msimu uliopita wa 2009/10 wa UEFA CHAMPIONS LIGI.
Listi ya Wagombea:
• KIPA BORA:
Júlio César (FC Internazionale Milano)
Hugo Lloris (Olympique Lyonnais)
Víctor Valdés (FC Barcelona)
• BEKI BORA:
Lúcio (FC Internazionale Milano)
Maicon (FC Internazionale Milano)
Gerard Piqué (FC Barcelona)
• KIUNGO BORA:
Xavi Hernández (FC Barcelona)
Arjen Robben (FC Bayern München)
Wesley Sneijder (FC Internazionale Milano)
• FOWADI BORA:
Lionel Messi (FC Barcelona)
Diego Milito (FC Internazionale Milano)
Wayne Rooney (Manchester United FC)
CHEKI: www.sokainbongo.com

Bellamy apigwa marufuku Man City!!!
Straika wa Manchester City, Craig Bellamy, amepigwa marufuku asikanyage mazoezini mwa Manchester City hadi atakapotafutiwa mahala pa kwenda kufuatia amri aliyotoa Meneja wao Roberto Mancini.
Bellamy amekuwa na bifu la muda mrefu na Mancini na siku za hivi karibuni limelipuka baada ya jina lake kutokuwemo kwenye Listi ya Wachezaji 25 waliosajiliwa na Klabu hiyo kwa ajili ya michuano ya EUROPA LIGI.
Bellamy alitamka wazi kuwa hawezi kubaki hapo ikiwa hatakuwemo kwenye Kikosi hicho na inaelekea jina lake limekatwa dakika za mwisho ili kuliongeza jina la Robinho anaelazimika kurudi Klabuni hapo baada ya Mkataba wake wa mkopo huko Santos kumalizika na Man City kugoma kumwongezea.
Inadaiwa kuwa Bellamy alipandwa na hasira na kuzirushia kwa Meneja na Wachezaji wenzake kadhaa na ndipo alipozuiwa kufanya mazoezi na Timu ya Kwanza na kupelekwa kucheza na Timu ya Rezevu lakini akaendeleza hasira zake.
Bellamy tayari amerudi kwao Wales na anategemewa kufanya mazoezi na Klabu ya nyumbani kwao Jijini Cardiff, Timu ya Cardiff City, ambayo pia imeonyesha nia ya kumchukua kwa mkopo Mchezaji huyo machachari lakini inaelekea wanashindana bei na Man City.
Awali Tottenham ilionyesha nia ya kumnunua Bellamy lakini Man City imegoma kwa vile wanaichukulia Timu hiyo kama mpinzani wao kwenye kinyang’anyiro cha kugombea nafasi za kucheza Ulaya.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Gerrard amtetea Reina kwa kuipa zawadi Arsenal
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, amemtetea Kipa wake Jose Reina kwa kosa lake kuipa Arsenal zawadi ya bao la kusawazisha dakika za mwisho za majeruhi hapo jana Uwanjani Anfield kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu kwa Timu hizo mbili.
Mechi hiyo ilikwisha kwa bao 1-1.
Gerrard ametamka: “Huyu ni Kipa mzuri na anatupa pointi nyingi. Ile ilikuwa bahati mbaya!”
Nahodha huyo wa Liverpool pia amedai Joe Cole alietolewa nje kwa Kadi Nyekundu na Refa Martin Atkinson kwa kumchezea rafu Beki wa Arsenal Laurent Koscielny, alikuwa na bahati mbaya kupewa Kadi hiyo na alidhani alistahili Njano badala yake.
Nae Beki wa Arsenal, Laurent Koscielny, alitolewa kwa Kadi Nyekundu mwishoni baada ya kupata Kadi za Njano mbili ndani ya dakika moja.
CAPELLO: Mwanzo wa mwisho umefika!
• FA yatangaza Meneja ataefuatia ni Mwingereza!
Mrithi wa Mtaliana Fabio Capello kama Kocha wa England atakuwa Mwingereza FA imetamka.
Mkataba wa Capello unamalizika 2012 ingawa kwa sasa yuko kwenye presha kubwa baada ya kutofanya vizuri kama wadau walivyotarajia huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
FA imesema wao wanategemea Capello atatumikia muda wake wote wa Mkataba na hivyo kuondoa dhana kuwa huenda akang’oka mapema.
England inategemewa kuanza kampeni za kufuzu kuingia Fainali za EURO 2012 Mwezi ujao watakapoanza mechi zao za Makundi.
CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI KUU ENGLAND: Mechi za kwanza kwa kila Timu kwisha Jumatatu!
• Ni OLD TRAFFORD: Man United v Newcastle United!
Jumatatu, Agosti 16 usiku saa 4, saa za bongo, Manchester United itatinga Uwanja wa nyumbani Old Trafford kuikaribisha Timu mpya Ligi Kuu, Newcastle, walioshushwa Daraja Msimu wa 2008/9 lakini wakaibuka tena Ligi Kuu baada ya Msimu mmoja tu Daraja la chini.
Timu hizi zilipambana katika mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu Msimu wa 2008/9 kama hii ya kesho Uwanjani Old Trafford na kutoka sare 1-1.
Man United huenda ikamkosa Patrice Evra ambae ana maumivu kidogo ya mguu na ni wazi itawakosa Anderson, Ferdinand na Hargreaves ambao wote hawajapona maumivu yao.
Newcastle ina mlolongo wa majeruhi ambao ni Sol Campbell, Smith, Simpson, S Taylor, Gosling, na Best.
Vikosi vinategemewa:
Man United: Van der Sar, O’Shea, Vidic, Evans, Evra, Valencia, Carrick, Scholes, Giggs, Rooney, Nani
Akiba: Kuszczak, Brown, Rafael, Gibson, Obertan, Fabio, Park, Neville, Hernández, Smalling, Bébé, Fletcher, Owen, Berbatov, C Evans, De Laet
Newcastle: Harper, Williamson, Coloccini, Taylor, Enrique, Smith, Barton, Gutierrez, Carroll, Lovenkrands, Nolan.
Akiba: Forster, Krul, Campbell, Routledge, Perch, Xisco, Ameobi, Guthrie, Kadar, Ranger
Refa: C Foy.

Sunday 15 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Liverpool, Arsenal ngoma ngumu 1-1!
• Wachezaji wapya waona Nyekundu!
Ni Bigi Mechi iliyojaa kila aina ya vimbwanga vikiwemo vya Wachezaji wapya wa kila upande kulambwa Kadi Nyekundu katika Mechi yao ya kwanza tu ya Ligi Kuu kutoka kwa Refa Martin Atkinson.
Joe Cole, akiichezea Liverpool mechi yake ya kwanza kwenye Ligi Kuu alipigwa Nyekundu kwa mchezo mbaya dhidi ya Beki mpya wa Arsenal kutoka Ufaransa, Koscielny, kwenye dakika za majeruhi za Kipindi cha kwanza lakini nae Koscielny akatwangwa Nyekundu dakika za lala salama baada ya kupewa Kadi za Njano mbili.
Wakicheza Mtu 10, Liverpool ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 46 kupitia Ngog baada ya pande la Mascherano.
Arsenal walisawazisha bao hilo dakika ya 91 kufuatia kosa la Kipa Reina alieutema wavuni mpira uliogonga mwamba wa Chamakh wa Arsenal baada ya krosi ya Rosicky.
Vikosi vilivyoanza:
Liverpool: Reina, Johnson, Carragher, Agger, Skrtel, Gerrard, Jovanovic, Mascherano, Kuyt, Cole, Ngog.
Akiba: Cavalieri, Aurelio, Torres, Maxi, Babel, Lucas, Kelly.
Arsenal: Almunia, Clichy, Vermaelen, Koscielny, Diaby, Nasri, Eboue, Sagna, Wilshere, Arshavin, Chamakh.
Akiba: Fabianski, Rosicky, van Persie, Vela, Walcott, Song, Gibbs.
Refa: Martin Atkinson
CHEKI: www.sokainbongo.com

MAN UNITED yatangaza Namba za Jezi za Wachezaji
Manchester United imetangaza Namba za Jezi za Wachezaji wake kwa ajili ya Msimu wa 2010/11 wa Ligi Kuu lakini bado haijateua Kikosi chake cha Wachezaji 25 wanaotakiwa kusajiliwa kwa Ligi ili kukidhi Sheria mpya ya kuwa na Wachezaji wa nane kati ya hao 25 ‘waliolelewa’ nyumbani kwa Miaka Mitatu kabla hawajatimiza Umri wa Miaka 21.
‘Kulelewa nyumbani’ kunamaanisha kuwemo kwenye Klabu za England au Wales kwa Miaka mitatu kabla hawajatimiza umri wa Miaka 21.
Man United imesema Kikosi hicho cha Wachezaji 25 kitatangazwa Septemba Mosi ambayo ndio Siku ya mwisho kuwasilisha usajili huo.
Wachezaji wapya, Chris Smalling na Chicharito, wamepewa Jezi Namba 12 kwa Smalling na 14 kwa Chicharito.
Mchezaji mwingine mpya ni Bebe kutoka Ureno lakini bado hajapewa Namba ya Jezi kwa vile usajili wake bado haujakamilika.
Kikosi kamili na Namba za Jezi:
1. Van der Sar, 2. Neville, 3. Evra, 4. Hargreaves, 5. Ferdinand, 6. Brown, 7. Owen, 8. Anderson, 9. Berbatov, 10. Rooney, 11. Giggs, 12. Smalling, 13. Park, 14. Chicharito, 15. Vidic, 16. Carrick, 17. Nani, 18. Scholes, 20. Fabio, 21. Rafael, 22. O'Shea, 23. J Evans, 24. Fletcher, 25. Valencia, 26. Obertan, 27. Macheda, 28. Gibson, 29. Kuszczak, 30. De Laet, 31. C Evans, 35. Cleverley, 40. Amos, 42. Eikrem, 44. Dudgeon, 45. Gill.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Wenger aota Ubingwa Msimu huu
Meneja wa Asernal, Arsene Wenger, amekitaka Kikosi chake kigangamale na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu huu.
Arsenal, ambao wanaanza kampeni yao ya Ligi Kuu kwa kucheza ugenini huko Anfield dhidi ya Liverpool leo jioni, hawajachukua Kombe lolote tangu Mwaka 2005 waliposhinda FA Cup na sasa imepita Misimu 6 tangu watwae Ubingwa wa Ligi Kuu.
Pia, tangu Msimu wa 2005/5, hawajamaliza wakiwa nafasi mbili za juu.
Wenger, ambae tayari ameongeza Mkataba wake na atabaki Arsenal hadi 2014, amesema: “Tusipotwaa Ubingwa, Watu wataanza kuuliza! Ni sahihi kwani tusipotwaa Ubingwa ni fedheha kubwa kwetu!”
Wenger ameongeza kuwa siku za nyuma walishindwa kutwaa Ubingwa kwa vile Kikosi chao kilikuwa kichanga lakini sasa kimekomaa.
Wenger ametamka: “Sasa tumekomaa na ikiwa tutashindwa ni lazima tubadili msimamo. Kwangu mimi Kombe ni Ubingwa wa Ligi Kuu au wa Ulaya!”
Rio nje muda mrefu zaidi
Sir Alex Ferguson amesema Beki wake Rio Ferdinand huenda akarudi tena Uwanjani baada ya Mwezi mmoja kutokana na kuchelewa kupona goti aliloumia akiwa huko Afrika Kusini akiwa mazoezini na England walipokuwa wakisubiri kucheza Kombe la Dunia.
Hivyo, Ferdinand atazikosa Mechi 4 za Manchester United za Ligi Kuu na pia Mechi za England za Makundi kuwania kuingia Fainali za EURO 2012 itakapocheza na Bulgaria Septemba 3 na Uswisi Septemba 7.
Barca yatwangwa!!
Sevilla, ikiwa nyuma kwa bao 1-0 hapo jana, ilizinduka na kuibamiza FC Barcelona mabao 3-1 katika mechi ya kwanza ya Supercup, Kombe linaloshindaniwa na Bingwa wa La Liga na yule alienyakua Kombe la Mfalme huko Spain ikiwa Mechi za ufunguzi wa Msimu mpya.
Mechi ya marudiano itakuwa Nou Camp, Barcelona hapo Agosti 21.
Zlatan Ibrahimovic aliwapa Barca bao la kuongoza lakini Kipindi cha pili Sevilla walizinduka na Frederic Kanoute akapachika bao mbili na Luis Fabiano akafunga la tatu.
LIGI KUU: Leo ni Liverpool v Arsenal
Ni Bigi Mechi ambayo imeshangaza wengi kupangwa kuwa ndio Mechi ya kwanza kwa Msimu mpya wa Ligi Kuu England kwa Timu za Liverpool na Arsenal zitakapokutana huko Anfield leo saa 12 jioni, bongo taimu.
Katika Mechi kama hii Msimu uliokwisha, Arsenal ilishinda bao 2-1.
Kwa jumla, Timu hizi zimeshacheza mara 173 na Liverpool wameshinda mara 68, Arsenal mara 60 na sare 44.
Lakini kwenye makutano yao kwenye historia ya Ligi Kuu, Liverpool wameshinda Mechi 3 kati ya 18 walizocheza.
Katika Mechi ya leo, Mastaa watakaokosekana ni Van Persie na Fabregas kwa Arsenal na Liverpool watamkosa Fernando Torres kwa vile wote bado sio fiti.
Refa katika Mechi ya leo atakuwa Martin Atkinson
Powered By Blogger