CHEKI: www.sokainbongo.com
BUNDESLIGA Yaanza!
• Bayern yashinda dakika za majeruhi!
Mabingwa Watetezi wa Bundesliga, Bayern Munich, jana walihitaji goli la dakika za majeruhi ili waifunge VfL Wolfsburg 2-1 katika mechi ya kwanza ya Msimu mpya wa Ligi hiyo ya Ujerumani.
Mabao ya Bayern Munich yalifungwa na Thomas Mueller na Bastian Schweinsteiger.
Bao la Wolfsburg lilifungwa na Edin Dzeko.
MECHI ZA LEO ZA BUNDESLIGA:
Hannoverscher 1896 v Eintracht Frankfurt
TSG Hoffenheim v SV Werder Bremen
FC Köln v FC Kaiserslautern
Borussia Mönchengladbach v FC Nurnberg Week
SC Freiburg v FC St. Pauli
Hamburger SV v Schalke 04
SPAIN SUPER CUP: Leo marudio FC Barcelona v Sevilla
Baada ya kuchapwa 3-1, leo wakiwa kwao Nou Camp, FC Barcelona wanahitaji ushindi mnono ili waibwage Sevilla na kutwaa Taji la Supercup ambalo huashiria mwanzo mwa Msimu mpya huko Spain.
Ligi ya Spain, La Liga, inategemewa kuanza Agosti 28.
Fergie: ‘Hamna tena Mchezaji mpya Msimu huu!’
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesisitiza kuwa Kikosi chake cha sasa kinaridhisha hivyo hataongeza Mchezaji yeyote kabla Dirisha la Uhamisho kufunga Agosti 31.
Tayari Ferguson alishatamka kuwa haongezi Mchezaji hasa kwa vile soko lenyewe limepotoshwa na ununuzi wa Wachezaji kwa bei mbaya hasa unaofanywa na Manchester City na kuifanya thamani ya Wachezaji wenye majina makubwa kupandishwa mno kupita thamani yao halisi.
Hata hivyo, Vyombo vya Habari vimeendelea kuwahusisha baadhi ya Wachezaji na kuhamia Man United na sasa anavumishwa Kiungo wa Real Madrid kutoka Uholanzi, Rafael van der Vaart, kuwa yuko mbioni kutua Old Trafford.
Msimu huu, Ferguson amewanunua Wachezaji watatu tu Chipukizi kwa bei poa na nao ni Bebe, Javier Hernandez, aka Chicharito, na Chris Smalling.
Akihojiwa kuhusu kikosi chake, Ferguson alitamka: “Hatuna tatizo. Kila pozisheni uwanjani ipo poa.”
Wakati huo huo, Kiungo Chipukizi wa Man United kutoka Brazil, Rodrigo Possebon, atajiunga na Santos ya Brazil kwa Mkataba wa Miaka minne.
Possebon alijiunga na Man United Mwaka 2008 akitokea Klabu ya Brazil Internacional lakini alishindwa kujikita Kikosi cha Kwanza cha Man United.
No comments:
Post a Comment