Sunday 15 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Wenger aota Ubingwa Msimu huu
Meneja wa Asernal, Arsene Wenger, amekitaka Kikosi chake kigangamale na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu huu.
Arsenal, ambao wanaanza kampeni yao ya Ligi Kuu kwa kucheza ugenini huko Anfield dhidi ya Liverpool leo jioni, hawajachukua Kombe lolote tangu Mwaka 2005 waliposhinda FA Cup na sasa imepita Misimu 6 tangu watwae Ubingwa wa Ligi Kuu.
Pia, tangu Msimu wa 2005/5, hawajamaliza wakiwa nafasi mbili za juu.
Wenger, ambae tayari ameongeza Mkataba wake na atabaki Arsenal hadi 2014, amesema: “Tusipotwaa Ubingwa, Watu wataanza kuuliza! Ni sahihi kwani tusipotwaa Ubingwa ni fedheha kubwa kwetu!”
Wenger ameongeza kuwa siku za nyuma walishindwa kutwaa Ubingwa kwa vile Kikosi chao kilikuwa kichanga lakini sasa kimekomaa.
Wenger ametamka: “Sasa tumekomaa na ikiwa tutashindwa ni lazima tubadili msimamo. Kwangu mimi Kombe ni Ubingwa wa Ligi Kuu au wa Ulaya!”
Rio nje muda mrefu zaidi
Sir Alex Ferguson amesema Beki wake Rio Ferdinand huenda akarudi tena Uwanjani baada ya Mwezi mmoja kutokana na kuchelewa kupona goti aliloumia akiwa huko Afrika Kusini akiwa mazoezini na England walipokuwa wakisubiri kucheza Kombe la Dunia.
Hivyo, Ferdinand atazikosa Mechi 4 za Manchester United za Ligi Kuu na pia Mechi za England za Makundi kuwania kuingia Fainali za EURO 2012 itakapocheza na Bulgaria Septemba 3 na Uswisi Septemba 7.

No comments:

Powered By Blogger