Saturday, 19 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Rooney awataka radhi Mashabiki England
Straika wa England Wayne Rooney amewaomba radhi Mashabiki wa England kufuatia maneno yake yaliyonaswa kwenye kamera ya pembeni mwa Uwanja aliyoyatoa mara tu baada ya filimbi ya mwisho ya mechi ya Ijumaa Juni 18 ambayo England ilienda sare 0-0 na Algeria.
Rooney alinaswa na kamera hiyo akisema: “Ni vizuri kuwaona Mashabiki wako wakikuzomea…….!”
Katika stetimenti ya FA, Rooney anakaririwa akiomba radhi na kusema alitoa matamshi yake huku akiwa amezongwa na hasira za kucheza vibaya na kutoka sare.
Kiwango cha Rooney katika mechi mbili walizocheza huko Afrika Kusini kwenye Kundi lao kimeonekana kuporomoka na hajaifungia goli England katika mechi 8 sasa. Hali hiyo imempa wasiwasi Kocha wa England Fabio Capello aliekiri uchezaji wa Rooney sio wa yule Rooney wanaemjua.
TEMBELEA: www.sokainbongo.com

Ghana 1 Australia 1
Ghana wameweza kutoka sare 1-1 na Australia ambayo katika mechi yake ya pili mfululizo wamelazimika kucheza wakiwa pungufu baada ya leo Straika wao Harry Kewell kupewa Kadi Nyekundu kwa kuushika mpira uliokuwa ukitinga wavuni yeye akiwa kasimama mstari wa golini.
Katika mechi ya kwanza na Germany Mchezaji Tim Cahill alipewa Kadi Nyekundu.
Australia ndio walioanza kupata bao dakika ya 11 kupitia Holman baada ya Kipa Kingson kuitema frikiki ya Bresciano na mpira kumaliziwa na Holman.
Ghana walipewa penalti dakika ya 25 na Asamoah Gyan akaifungia Ghana bao la kusawazisha hii ikiwa ni penalti yake ya pili kwani katika mechi ya kwanza na Serbia aliipa ushindi wa 1-0 kwa penalti.
Penalti hiyo ya Ghana ilitokea baada ya Harry Kewell kuzuia shuti la Annan kwa mkono akiwa mstari wa goli na Refa Roberto Rosetti kuamua penalti na kumpa Kadi Nyekundu Kewell.
Kwa sare ya leo Ghana wametua kilele cha Kundi D wakiwa na pointi 4, Germany pointi 3, Serbia pointi 3 na Australia 1
Timu:
Ghana: Kingson; Pantsil, Jonathan Mensah, Addy, Sarpei; Annan; Asamoah, Boateng; Ayew, Gyan, Tagoe.
Australia: Schwarzer; Wilkshire, Moore, Neill, Carney; Valeri, Culina; Emerton, Holman, Bresciano; Kewell.
Refa Roberto Rossetti.
Uholanzi waiua Japan
Uholanzi imejiweka nafasi nzuri ya kutinga Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia walipoifunga Japan bao 1-0 katika mechi ya Kundi E huko Mjini Durban Uwanja wa Moses Mabhida iliyochezwa leo Jumamosi Juni 19.
Uholanzi walishinda mechi yao ya kwanza wa bao 2-0 dhidi ya Denmark na Japan walifunga Cameroun 1-0.
Uholanzi watapata uhakika wa kusonga mbele ikiwa katika mechi nyingine ya Kundi E itakayochezwa baadae leo Cameron watashindwa kuifunga Denmark.
Bao la ushindi kwa Uholanzi alifunga Wesley Sneijder dakika ya 52.
Anelka afungishwa virago kurudishwa kwao!!
Straika wa Ufaransa anaechezea Chelsea huko England, Nicolas Anelka, anadaiwa kumtukana Kocha wa Ufaransa, Raymond Domenech, katika tukio ambalo limetokea wakati wa mapumziko kwenye mechi ya juzi Alhamisi Ufaransa waliyofungwa 2-0 na Mexico.
Inasemekana Domenech alimlaumu Anelka kwa kutokuwa makini na pozisheni yake na ndipo Anelka akalipuka na kumtukana Kocha huyo matusi ya nguoni.
Domenech akambadilisha Anelka na kumuingiza Andre-Pierre Gignac
kabla Kipindi cha Pili kuanza.
Kumekuwa na madai ya kuwa kambi ya Timu ya Ufaransa haiko shwari na kumekuwa na mpasuko mkubwa ingawa Viongozi wamekuwa wakikanusha hilo.
Ufaransa wanamaliza mechi zao kwa kucheza na Afrika Kusini siku ya Jumanne Juni 22 na Mexico na Uruguay wanacheza pamoja siku hiyo hiyo na wanahitaji sare tu ile wote wawili wasonge mbele.
CHEKI: www.sokainbongo.com

USA walia: ‘TUMEIBIWA!”
Timu ya USA imepiga kelele za kuibiwa baada ya goli lao la 3 kukataliwa na Refa Koman Coulibaly kutoka Mali kwenye mechi dhidi ya Slovenia hapo Ijumaa Juni 18 ambayo iliisha 2-2 huku USA wakitoka mapumziko wakiwa bao 2-0 nyuma na wakasawazisha na pia kufunga bao ‘safi’ lililokataliwa.
Mchezaji wa USA Landon Donovan alisema: “Tumeibiwa! Sijui kwa nini halikukubaliwa!”
Nae Kocha Bob Bradley, ambae Mtoto wake Michae Bradley ndie aliefunga bao la pili la USA la kusawazisha, alisema: “Mpaka sasa sijui ni kwanini limekataliwa!”
Goli hilo la 3 lilifungwa dakika ya 85 huku ngoma ikiwa 2-2 kufuatia frikiki iliyodondoshwa ndani ya boksi na Maurice Edu akaushindilia mpira wavuni.
Kuna taarifa kuwa FIFA wanachunguza bao hilo na huenda wakamwadhibu Refa Coulibaly endapo atakuwa amekosea kwenye uamuzi wake.

Magazeti England waibatukia England
Kila Gazeti huko England limeishambulia Timu ya England kwa kucheza ovyo katika mechi ya Kundi C ya Kombe la Dunia huko Green Point Ijumaa Juni 18 dhidi ya Algeria na kuambulia sare ya 0-0 na kuwafanya washike nafasi ya 3 Kundi hilo nyuma ya Slovenia na USA.
Magazetio hayo pia yalionyesha wasiwasi wao na fomu ya Straika Wayne Rooney ambae katika mechi mbili za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini ameonyesha kiwango kilichoporomoka.
Sare ya jana ilimfanya hata Kocha wa England Fabio Capello aishangae Timu yake na kusema uchezaji wake ulikuwa ni kama Timu tofauti na ile anayoijua.
Sasa England haina njia ya mkato ni lazima iifunge Slovenia katika mechi yao ya mwisho ili wasonge mbele.
Gazeti la Daily Mirror lilitoka na kichwa cha habari: “Ni upuuzi mtupu!” na Guardian lilisema: “Hamna Moto, Hamna Moyo, Hamna Matumaini!”
Nalo The Sun walichapisha habari zinazosema England haina kisingizio bali ni wabovu.
England watamaliza na Slovenia Jumatano Juni 23.
CHEKI: www.sokainbongo.com

England yabanwa mbavu
Inabidi England waifunge Slovenia katika mechi yao ya mwisho ikiwa watataka kusonga Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia baada ya kutoka sare 0-0 na Algeria Uwanja wa Green Point huko Cape Town.
England walicheza chini ya kiwango na kushindwa kufunga bao.
Baada ya mechi Timu hiyo ilizomewa na Mashabiki wao wenyewe na hata Kocha wao, Fabio Capello, alilalamika: “Haikuwa Timu ninayoijua mimi, Timu ninayoiona mazoezini.”
Katika Kundi C, Slovenia wanaongoza wakiwa na Pointi 4, USA 2, England 2 na Algeria 1.
Mechi za mwisho hapo Juni 23 ni Slovenia v England na Algeria v USA.
Timu:
England: James, Johnson, Carragher, Terry, Ashley Cole, Lennon,
Barry, Lampard, Gerrard, Rooney, Heskey.
Akiba: Green, Dawson, Crouch, Joe Cole, Warnock, Upson, Milner, Wright-Phillips, Defoe, King, Carrick, Hart.
Algeria: M'Bohli, Bougherra, Belhadj, Yahia, Kadir, Yebda,
Lacen, Halliche, Boudebouz, Ziani, Matmour.
Akiba: Gaouaoui, Mansouri, Ghezzal, Saifi, Djebbour, Bellaid, Laifaoui,
Guedioura, Medjani, Mesbah, Abdoun, Chaouchi.
Refa: Ravshan Irmatov (Uzbekistan)
TOSIC: ‘MKOPO UNGEFAA!’
Zoran Tosic amedai Sir Alex Ferguson hakumpa nafasi ya kutosha alipokuwepo Manchester United na ndio maana akashindwa kuonyesha makeke yake.
Winga huyo kutoka Serbia ameuzwa kwa CSKA Moscow ya Urusi baada ya kukaa Old Trafford Miezi 18 tu na kucheza mechi 5 ambazo zote alitokea benchi.
Msimu uliokwisha Tosic alipelekwa Bundesliga kucheza kwa mkopo Klabu ya Cologne.
Tosic amelalamika kuwa bora angpelekwa CSKA kwa mkopo na si kuuzwa moja kwa moja

Friday, 18 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

USA 2 Slovenia 2
USA ilitoka nyuma wakiwa bao 2-0 hadi haftaimu leo Ijumaa Juni 18 huko Uwanja wa Ellis Park, Johannesburg na kusawazisha na pengine wangeshinda mechi hii lakini Refa Koman Coulibaly toka Mali kulikataa bao la 3 ‘safi’.
Slovenia walipata bao lao la kwanza dakika ya 13 kupitia Birsa aliefumua mkwaju toka Mita 25 na bao la pili walifunga dakika ya 41 kupitia Ljubijankic baada ya uzembe wa Difensi ya USA kumruhusu Novakovic kupokea pasi akiwa peke yake na kumpenyezea Ljubijankic aliefunga.
Hadi mapumziko Slovenia 2 USA 0.
Dakika ya 48 Cesar alifanya makosa katika kuokoa na Donovan akaingia haraka ndani ya boksi na kufunga toka engo mbaya.
Ndipo ilipowadia dakika ya 82 wakati Mtoto wa Kocha Bob Bradley wa USA, Bradley aliposawazisha baada ya pasi ya Altidore.
USA walifunga goli zuri baada ya hapo lakini likakataliwa.
Timu:
Slovenia: Samir Handanovic; Miso Brecko, Marko Suler, Bostjan Cesar, Bojan Jokic, Valter Birsa, Robert Koren, Aleksandar Radosavljevic, Andraz Kirm, Zlatan Ljubijankic, Milivoje Novakovic
USA: Tim Howard; Steve Cherundolo, Jay DeMerit, Oguchi Onyewu, Carlos Bocanegra; Landon Donovan, Michael Bradley, Jose Torres, Clint Dempsey; Jozy Altidore, Robbie Findley.
RefA: Koman Coulibaly (Mali)
Serbia 1 Germany 0
Serbia wamefufua matumaini yao baada ya kufungwa nechi yao ya kwanza na Ghana 1-0 walipowatungua vigogo Ujerumani 1-0 huko Uwanja wa Nelson Mandela, Port Elizabeth leo Ijumaa Juni 18 na staa mkubwa wa mechi hii alikuwa Refa toka Spain alietoa Kadi kama njugu.
Ujerumani ilicheza mechi hii ikiwa pungufu baada ya Miroslav Klose kutolewa kwa Kadi Nyekundu dakika ya 37 kufuatia Kadi za Njano mbili za papo kwa papo.
Dakika moja baada ya Klose kutolewa Milan Jovanovic akafunga alipopewa pasi na Nikola Zigic.
Ujeruamani walipoteza nafasi ya kurudisha dakika ya 60 walipokosa penalti iliyopigwa na Lukas Podolski kuokolewa na Kipa Vladimir.
Adhabu hiyo ilitolewa Beki Nemanja Vidic alipounawa mpira.
Serbia walikosa chansi mbili za kuongeza bao walipogonga mwamba mara mili kupitia Jovanovic na Zigic.
Ujerumani walishinda mechi yao ya kwanza walipoikung’uta Australia 4-0.
CHEKI: www.sokainbongo.com


Ufaransa......inasikitisha!!!
Wengi walijua Ufaransa, wakiongozwa na Meneja Raymond Domenech ambae huko kwao hawezi hata siku moja kuwa Bingwa wa Mtu anaependwa, ni bomu  na jana Alhamisi Juni 17 imetandikwa 2-0 na Mexico.
Kipigo hiki kimewaacha Ufaransa kukosa kabisa matumaini ya kusonga Raundi ya Pili kwani wamecheza mechi mbili na wana pointi moja tu na Timu za juu Kundi lao ni Mexico na Uruguay zenye pointi 4 kila moja na zinamaliza kwa kucheza pamoja.
Ufaransa watamaliza na Mwenyeji Afrika Kusini na wote wana pointi moja kila mmoja.
Ni Mchezaji mpya wa Manchester United, Hernandez aka Chicharito, aliefunga bao la kwanza dakika ya 64 alipopenyezewa ndefu na Marquez na akakontroli kifuani na kumzunguka Kipa Lloris.
Goli la pili la Mexico ni kazi ya Pablo Barrero aliemtambuka Kepteni wa Ufaransa, Patrice Evra, na kuangushwa na Eric Abidal na kuzaa penalti iliyofungwa na Mkongwe Blanco, umri Miaka 37, alietoka umbali wa Mita kama 15 toka mpira wa penalti ulikowekwa.
Les Bleus walia na El Tri furaha.
Timu:
France: Lloris, Sagna, Gallas, Abidal, Evra, Govou, Toulalan,
Diaby, Malouda, Ribery, Anelka.
Akiba: Mandanda, Reveillere, Planus, Gourcuff, Cisse, Gignac, Henry, Squillaci, Diarra, Valbuena, Clichy.
Mexico: Perez, Osorio, Moreno, Rodriguez, Salcido, Marquez,
Giovani, Juarez, Torrado, Vela, Franco.
Akiba: Ochoa, Barrera, Castro, Blanco, Aguilar, Hernandez, Guardado, Magallon, Torres, Bautista, Medina, Michel.
Refa: Khalil Al Ghamdi (Saudi Arabia)

Thursday, 17 June 2010

TEMBELEA: www.sokainbongo.com

Spain na Mchawi nani!!!!
Siku moja baada ya kuchapwa 1-0 bila kutegemea na Uswisi kwenye mechi yao ya kwanza ya Kundi H Fainali za Kombe la Dunia, Spain nzima imekuwa ikihaha kutafuta mchawi nani huku Magazeti na Vyombo vingine vya Habari vikilenga lawama zao kwa Timu kwa ujumla, Wachezaji kibinafsi na hata Refa Howard Webb kutoka England aliebebeshwa lawama za kufungwa Mabingwa hao watarajiwa wa Dunia kwa goli walilodai ni ofsaidi.
Gazeti kubwa na maarufu huko Spain na shabiki mkubwa wa Real Madrid, Marca, lilmetamka: "Spain haiwezi tena kuota ndoto ya kuwaza nani mpinzani wao Raundi inayofuata! Sasa ni kujinusuru tu!”
Marca waliendelea kwa kumnukuu Meneja wa zamani wa Spain, Luis Aragones, ambae alisema: “Spain ilicheza bila kujiamini.”
Aragones akaongeza kuwa kufungwa na Uswisi ni pigo kubwa na yeye angekuwa bado Kocha asingetumia Viungo wawili wa kuzuia mipira kama walivyochezeshwa Xabi Alonso na Sergio Busquets kwa pamoja.
Nae Kipa wa Spain Iker Casillas alitoa masikitiko yake kwa kusema wao hawakutegemea kipigo hicho na wamesikitishwa mno.
Beki Gerard Pique akazungumza: “Sasa huu ujinga kuwa sisi ni Mabingwa watarajiwa na kwamba tutatwaa Kombe la Dunia kirahisi tuusahau!”
Lakini Magazeti mengine ya Spain yamemtoa Refa Howard Webb kama mbuzi wa kafara kwa kudai goli la Uswisi lilikuwa ofsaidi na pia Mchezaji wa Uswisi Stephane Grichting alipaswa kuwashwa Kadi Nyekundu kwa kumchezea rafu Andres Iniesta wakati akiwa ndie Beki wa mwisho.
Gazeti la Marca lilizidi kumlaumu Refa Howard Webb kwa vilevile kuinyima Spain penalti kwa madai David Silva alichezewa madhambi.
Gazeti jingine kigogo lilishambulia Timu na baadhi ya Wachezaji kwa kudai Timu ilikuwa ikiremba kupindukia na Mabeki Pique na Puyol ndio wakosaji kwa kuruhusu Uswisi kufunga na kosa hilo wamekuwa wakilifanya mara kwa mara Klabuni kwao FC Barcelona.
Ni Gazeti moja tu lililojaribu kuinua mioyo ya Watu kwa kuandika Bango kubwa: ‘Bado inawezekana!’ pengine wameisahau historia kwamba hakuna hata Timu moja ilitwaa Kombe la Dunia baada ya kufungwa mechi yake ya kwanza kwenye Fainali.
ANGALIA: www.sokainbongo.com

Nigeria wajinyonga!!
Ugiriki leo wameifunga Nigeria bao 2-1 baada ya kutoka nyuma kwa bao 1-0 lakini ni Nigeria wenyewe ndio waliosababisha hali hiyo baada ya wenyewe kujitia kitanzi pale Mchezaji wao Sani Kaita alipotwangwa Kadi Nyekundu dakika ya 33 kwa kumrushia teke Katsouranis ambae licha ya teke hilo kutokumgusa vilivyo alijidondosha chini mithili amelipuliwa na bomu.
Ushindi huu wa Ugiriki umewaweka Nigeria kwenye hali ngumu mno na pengine ni miujiza mikubwa itakayowafanya waingie Raundi ya Pili kwani wameshafungwa mechi mbili na wamebakisha moja tu na Korea Kusini huku Ugiriki na Korea Kusini kila moja zina pointi 3 na vinara ni Argentina wana pointi 6 baada ya kushinda mechi zao mbili.
Ugiriki watamaliza na Argentina.
Katika mechi hii Nigeria walipata bao dakika ya 16 kupitia Uche ambae frikiki yake ilienda moja kwa moja wavuni huku Kipa Tzorvas akidaivu mbovu.
Ndipo wehu wa Kaita kwenye dakika ya 33 wa kurusha teke kumfanya atolewe nje na kuiacha Nigeria iwe Mtu 10.
Hapo ndipo Kocha wa Ugiriki akapata mwanya na kumtoa Beki mmoja na kumuingiza Straika na Ugiriki ikaanza wimbi baada ya wimbi kutafuta bao la kusawazisha na dakika ya 44 shuti la Salpingidis likamgonga Haruna na Kipa Enyeama akapangua lakini mpira ukarudi tena kwa Salpingidis aliefumua shuti wavuni.
Bao la ushindi kwa Ugiriki lilipatikana kufuatia Kipa Enyeama kutema shuti la Karagounis na mpira kumdondokea Torosidis aliefunga.
Timu:
Greece: 12-Alexandros Tzorvas; 11-Loukas Vyntra, 16-Sotiris Kyrgiakos, 15-Vassilis Torosidis, 6-Alexandros Tziolis, 8-Avraam Papadopoulos, 19-Socratis Papastathopoulos, 10-Giorgos Karagounis, 21-Kostas Katsouranis; 14-Dimitris Salpingidis, 17-Fanis Gekas.
Nigeria: 1-Vincent Enyeama; 17-Chidi Odiah, 6-Danny Shittu, 2-Joseph Yobo, 3-Taye Taiwo, 12-Kalu Uche, 20-Dickson Etuhu, 15-Haruna Lukman, 14-Sani Kaita, 8-Yakubu Aiyegbeni, 11-Peter Odemwingie.
Refa: Oscar Ruiz (Colombia)
PITIA: www.sokainbongo.com


Argentina 4 Korea Kusini 1
Leo Argentina wamijasafishia njia ya kutinga Raundi ijayo ya Kombe la Dunia walipoichapa Korea Kusini mabao 4-1 huko Soka City, Soweto na kuwafanya wawe wanaongoza Kundi B wakiwa na pointi 6 baada ya pia kushinda mechi yao ya kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya Nigeria.
Mechi ya mwisho Argentina watacheza na Ugiriki.
Shujaa kwa Argentina alikuwa ni Straika wa Real Madrid, Gonzalo Higuain, aliepachika bao 3 na bao moja Korea walijifunga wenyewe.
Argentina ndio waliotangulia kupata bao dakika ya 16 baada ya frikiki ya Lionel Messi kumbabatiza Park Chu-young.
Bao la pili lifungwa na Gonzalo Higuain dakika ya 33.
Korea Kusini walipata bao la sekunde chache kabla ya haftaimu baada ya Difenda Demichelis kuporwa mpira na Lee Chung-yong na kwenda kufunga.
Huku wakijikakamua, Korea Kusini walijikuta wakipigwa bao mbili toka kwa Higuain ndani ya dakika 4, dakika ya 76 na 80, na hivyo kumalizwa kabisa.
Timu:
Argentina: 22-Sergio Romero; 2-Martin Demichelis, 13-Walter Samuel, 6-Gabriel Heinze, 17-Jonas Gutierrez; 14-Javier Mascherano, 20-Maxi Rodriguez, 7-Angel Di Maria; 10-Lionel Messi, 11-Carlos Tevez, 9-Gonzalo Higuain.
South Korea: 18-Jung Sung-ryong; 2-Oh Beom-seok, 12-Lee Young-pyo, 4-Cho Yong-hyung, 14-Lee Jung-soo, 8-Kim Jung-woo, 16-Ki Sung-yong, 7-Park Ji-sung, 17-Lee Chung-yong, 10-Park Chu-young, 19-Yeom Ki-hun.
Refa: Frank De Bleeckere (Belgium)
CHEKI: www.sokainbongo.com

RATIBA 2010/11 LIGI KUUENGLAND yaanikwa!!
Ratiba ya Msimu mpya wa Ligi Kuu England itakayoanza Agosti 14 leo imetangazwa na Mabingwa Watetezi Chelsea wataanza wakiwa nyumbani Uwanja wa Stamford Bridge kucheza na Timu iliyopanda Daraja West Bromwich Albion.
Timu ya pili Ligi Kuu, Manchester United, wataanza nyumbani Old Trafford kwa kucheza na Newcastle United ambao pia wamepanda Daraja.
Siku hiyo ya ufunguzi, Agosti 14, kutakuwa na Bigi Mechi pale Liverpool watakapoikaribisha Arsenal huko Anfield.
BIGI MECHI:
-Agosti 14: Liverpool v Arsenal
-Septemba 18: Man United v Liverpol
-Oktoba 2: Chelsea v Arsenal
-Desemba 18: Chelsea v Man United.
-Desemba 25: Arsenal v Chelsea
SIKU YA UFUNGUZI Agosti 14:
Aston Villa v West Ham
Blackburn v Everton
Blackpool v Wigan
Bolton v Fulham
Chelsea v West Brom
Liverpool v Arsenal
Man United v Newcastle
Sunderland v Birmingham
Tottenham v Man City
Wolverhampton v Stoke City
Parreira amlaumu Refa kipigo cha Bafana Bafana
Baada ya kufungwa bao 3-0 na Uruguay hapo jana Jumatano Juni 16 na kufanya wawe njia panda kusonga Raundi ya Pili ya Fainali za Kombe la Dunia toka Kundi A, Kocha wa Afrika Kusini Mbrazil Carlos Alberto Parreira amemvaa na Refa Massimo Busacca toka Uswisina kusema : “ Wachezaji wamechukizwa na kila Mtu anasema huyu ndio Refa mbovu kupita wote hapa! Alikuwa akitoa Kadi zisizostahili!”
Refa huyo alimtoa Kipa wa Bafana Bafana, Khune, kwa Kadi Nyekundu na kuipa penalti Uruguay ambayo ilifungwa na Diego Forlan na kuandika bao la pili dakika ya 80.
Bao la kwanza la Uruguay lilifungwa na Forlan dakika ya 24 baada ya kumparaza Mchezaji wa Bafana.
Goli la 3 liliingizwa dakika za majeruhi na Alvaro Pereira.
Afrika Kusini sasa ni lazima washinde mechi yao ya mwisho na Ufaransa ikiwa watataka kufuzu kuingia Raundi ya Pili.
Alhamisi kwenye Kundi hili, Ufaransa inacheza na Mexico.
Timu:
South Africa: Khune, Gaxa, Mokoena, Khumalo, Masilela, Tshabalala, Dikgacoi, Letsholonyane, Modise, Pienaar, Mphela.
Akiba: Josephs, Ngcongca, Sibaya, Davids, Booth, Thwala, Parker, Nomvethe, Moriri, Sangweni, Khuboni, Walters.
Uruguay: Muslera, Maxi Pereira, Lugano, Godin, Fucile, Arevalo Rios, Perez, Pereira, Suarez, Forlan, Cavani.
Akiba: Castillo, Gargano, Victorino, Eguren, Abreu, Gonzalez, Scotti, Alvaro Fernandez, Sebastian Fernandez, Caceres, Silva.
Refa: Massimo Busacca (Switzerland)

Wednesday, 16 June 2010

TEMBELEA: www.sokainbongo.com

FIFA yatupa ombi la Ufaransa la Kipa mpya
FIFA imeikatalia Ufaransa kumwita Kipa mpya baada ya mmoja wa Makipa wao watatu kuumia juzi Jumatatu na maumivu hayo yatamweka nje kwa Mwezi mmoja.
Kipa Cedric Carrasso, Miaka 28, ameumia musuli pajani na Ufaransa ilitaka kumwita Stephane Ruffier lakini FIFA imegoma na kusema kanuni zinaeleza wazi Timu haziruhusiwi kumbadili Mchezaji baada ya kucheza mechi zao za kwanza.
Kanuni za FIFA za Fainali za Kombe la Dunia zinaruhusu Timu kubadili Mchezaji alieumia mpaka Masaa 24 kabla ya Mechi yao ya kwanza.
Hata hivyo kuumia kwa Carrasso hakutaiathiri sana Ufaransa kwani Kipa Nambari wani ni Hugo Lloris wa Lyon na msaidizi wake ni Steve Mandanda wa Marseille na wote wako fiti.
Maradona ashambulia tena!!
Katika Mkutano na Wanahabari leo Alhamisi Juni 16 huko Afrika Kusini, Kocha wa Argentina Diego Maradona amerudia tena kumshambulia Pele na pia safari hii amemwingiza Rais wa UEFA, Michel Platini, ambae alikuwa Mchezaji Staa wa Ufaransa Miaka ya nyuma.
Hivi majuzi Pele aliripotiwa akijibu shutuma za Maradona za awali kwa kusema Maradona amechukua kazi ya Ukocha wa Argentina kwa vile alikuwa hana kazi na anahitaji pesa.
Maradona sasa amemtaka Pele arudi Makumbusho akimaanisha abaki tu awe kumbukumbu.
Akimgeukia Platini ambae aliwahi kuuhoji uwezo wa Maradona kama Kocha, Maradona alidai: “Platini? Sishangai kuhusu yeye kwani nimekuwa na uhusiano wa ‘habari nzuri na kwa heri tu’ na yeye! Tunajua Wafaransa walivyo na Platini ni Mfaransa na anaamini yeye ni bora kuliko mtu yeyote!”
Kisha Maradona akauvaa Jabulani, mpira rasmi wa Fainali hizi, na akatamka: “Sitaki kuzungumza kuhusu mpira huu kwa sababu kila mtu anauzungumza lakini ni muhimu! Nawataka Pele na Platini waende uwanjani waucheze huu Jabulani na wauangalie kama mzuri au mbaya na waache kuzungumza upuuzi kuhusu mimi!”
PITIA: www.sokainbongo.com

Ndugu kina Palacios wa Honduras waweka Historia
Honduras imekuwa Nchi ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kuweza kuwa na Ndugu watatu katika Kikosi chao baada ya kumwita kujiunga na Timu Jerry Palacios kumbadilisha Julio Cesar de Leon alieumia.
Kabla kuitwa kwa Jerry Palacios, Honduras ilikuwa na Kaka zake wawili, Wilson Palacios anaechezea Tottenham na Johnny Palacios wa Olimpia ya huko Honduras.
Jerry Palacios ni Straika toka Klabu ya China Hangzhou Greentown.
Honduras iliruhusiwa kumbadili Mchezaji huyo alieumia kwa vile FIFA inakubali hilo ikiwa tu litafanyika Masaa 24 kabla ya mechi ya kwanza ya Timu.
Familia hiyo ya kina Palacious ilipata balaa Miaka mitatu iliyopita pale mdogo wao Edwin alipotekwa nyara huko Honduras lakini licha ya kulipwa Dola 150,000 ili aachiwe, maiti ya Edwin iliokotwa porini.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Spain chaliiii!!
Hawajafungwa muda mrefu na wengi walikuwa tayari wamewakubali kuwa Spain ndio Mabingwa wa Dunia watarajiwa lakini leo Jumatano Juni 16 katika mechi yao ya kwanza ya Kundi H katika Fainali za Kombe la Dunia iliyochezwa Uwanja wa Moses Mabhida, Durban, Spain wamepigwa bao 1-0 na Uswisi.
Matokeo haya ndio makubwa ya kustua yaliyotokea tangu kuanza Fainali hizi kwani Spain, mbali ya kushabikiwa kuwa Bingwa wa Dunia, katika mechi 48 za mwisho alizocheza kabla ya leo ameshinda 45 kati ya hizo.
Ilikuwa ni dakika ya 52 ndio iliyowaliza Spain pale goli kiki ndefu ya Uswisi ilipomkuta Derdiyok aliepiga kwa kichwa kwa Nkufo na kuchomoka kuomba tena mpira akiwa katikati ya Madifenda wa Spain Pique na Puyol na ndipo Kipa Casillas akaruka miguu mbele na kumwangusha Derdiyok lakini Refa hakusimamisha mpira na mpira huo ukamgonga Pique na kutiririka kwa Fernandez aliupachika wavuni.
Timu:
Spain: 1-Iker Casillas; 15-Sergio Ramos, 3-Gerard Pique, 5-Carles Puyol, 11-Joan Capdevila; 16-Sergio Busquets; 8-Xavi, 14-Xabi Alonso; 21-David Silva, 7-David Villa, 6-Andres Iniesta.
Switzerland: 1-Diego Benaglio; 13-Stephane Grichting, 2-Stephan Lichtsteiner, 4-Philippe Senderos, 17-Reto Ziegler; 7-Tranquillo Barnetta, 8-Gokhan Inler, 6-Benjamin Huggel, 16-Gelson Fernandes; 19-Eren Derdiyok, 10-Blaise Nkufo.
Refa: Howard Webb (England)
Ratiba 2010/11 Ligi Kuu England kesho!!!
Klabu za Ligi Kuu England kesho Alhamisi Juni 17 zitajua ratiba zao kwa Msimu mpya wa 2010/11 utakaoanza Agosti 14.
Kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu kutakuwa na lile pambano la fungua pazia la Ngao ya Hisani litakalochezwa Uwanja wa Wembley hapo Agosti 8 kati ya Mabingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA, Chelsea, dhidi ya Manchester United ambao walishika nafasi ya pili kwenye Ligi.
Capello anatafakari mabadiliko
Kocha wa England Fabio Capello amedokeza Kiungo Gareth Barry ataanza mechi na Algeria Siku ya Ijumaa baada ya kupona enka lakini bado hajaamua nani atakuwa patna wa Wayne Rooney kwenye mashambulizi.
Pia baada ya kufanya kosa kubwa kwenye mechi ya kwanza na USA na kufungisha bao lililowapa sare ya 1-1 USA, Kipa Robert Green hana uhakika kama atacheza mechi hiyo na Algeria.
Rooney bado ana matumaini
Mshambuliaji wa England, Wayne Rooney, bado ana matumaini ya kufanya vizuri kwenye Kombe la Dunia licha ya kwenda sare na USA ya 1-1 katika mechi ya kwanza ya Kundi C.
Kuhusu yeye fomu yake ya ufungaji kudidimia ambayo amefunga bao moja tu katika mechi 8 za mwisho za  Kimataifa za England, Rooney amesema hilo halimtii hofu mradi tu wengine wanafunga na England inashinda.
Rooney pia amemponda Mkongwe wa Ujerumani Franz Beckenbauer aliedai England inacheza butua na kukimbiza mpira tu kwa kusema: “Hayo ni maoni yake! Sisi hatuko hivyo na hatusikiliza vitu hivyo.”

Tuesday, 15 June 2010

PITIA: http://www.sokainbongo.com/


Bifu la Pele v Maradona!!
Edison Arantes do Nascimento, aka Pele, na Diego Armando Maradona ndio wanaosifika kuwa Wachezaji Bora kabisa katika historia ya Soka lakini Pele ndie anasifika kama ‘Mfalme wa Soka’ na mara nyingi Magwiji hawa wamekuwa na ‘Bifu la Mdomo’.
Huko Afrika Kusini limezuka ‘zozo’ jipya kati yao baada ya kudaiwa Maradona ametamka kuwa kuna ‘Muungwana Mweusi’ [ikatafsiriwa kuwa ni Pele] amehoji uwezo wa wa Afrika Kusini kuwa Nchi ya kwanza Afrika kuwa Mwenyeji wa Kombe la Dunia.
Alipohojiwa na Wanahabari, Pele alijibu mapigo: “Simwelewi huyu! Alipohitaji msaada kwangu alipoanzisha Programu za TV huko Argentina nilikwenda kumsaidia! Nikacheza nae mpira na nilimsaidia kila kitu! Baadae nilijaribu kumsaidia kutengeneza matangazo ya Progrmu zake za TV na akawa ama anachelewa kuja au haji kabisaa!”
Pele akaongeza kwa dhihaka: “Sasa kanikumbuka huku Afrika Kusini! Bila shaka ananipenda!”
Pele, aliewahi kuwa Waziri wa Michezo Brazil, alizungumza zaidi na kusema hawezi kuwa Kocha wa Brazil kwa sababu hataki kuteseka kama anavyoteseka Dunga, Kocha wa sasa wa Brazil.
Kisha Pele akamgeukia Maradona na kutamka: “Maradona alichukua Ukocha Argentina kwa sababu alikuwa hana kazi na alihitaji kazi na alikuwa anahitaji pesa pia! Najua Argentina imefuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia kwa matatizo! Lakini hilo si kosa la Maradona, hilo ni kosa la wale waliomchagua Kocha!”
Kocha Ureno akerwa na Drogba kucheza na gamba mkononi!
Kocha wa Ureno Carlos Queiroz amedokeza kukerwa kwake na uamuzi wa FIFA kumruhusu Nahodha wa Ivory Coast Didier Drogba kucheza huku akiwa na gamba gumu mkononi kulinda sehemu aliyovunjika Juni 4 na kufanyiwa upasuaji huko Uswisi baada ya kuumia katika mechi ya kujipima nguvu na Japan.
Drogba aliruhusiwa kucheza mechi ya Kundi G ya leo Juni 15 na Ureno iliyoisha 0-0 baada ya Kikao cha Jumatatu kati ya FIFA pamoja na Refa wa mechi hiyo Jorge Larrionda toka Uruguay pamoja na Timu hizo mbili Ivory Coast na Ureno
Lakini Queiroz, aliewahi kuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson Manchester United, alihoji na kushangaa uamuzi huo kwa kusema: “ Si kazi yetu sisi kusema acheze au la ni FIFA! Jana FIFA wamesema ni juu ya Refa! Inashangaza, Wachezaji wanakatazwa kuvaa bangili, herini na plasta na huyu kavunjika mkono na kavaa gamba gumu karuhusiwa kucheza! Je angeumiza Wachezaji na hilo gamba? Labda watabadili sheria!”
CHEKI: www.sokainbongo.com


Lipende au Lichukie, Vuvuzela Daima!!!
Vuvuzela safarini Mtoni!!!
Usishangae Msimu ujao wa Ligi Kuu England utakaoanza Agosti 14 ukianza kuziona Vuvuzela za Rangi nyekundu zikiwa Old Trafford, za rangi ya bluu zikiwa Stamford Bridge, nyeusi na nyeupe zikiwa St James Park na za rangi ya Ze Gunners zikiwa Emirates kwani Waandaaji wa Kombe la Dunia huko Afrika Kusini wamewahimiza Washabiki toka kila kona ya Dunia waliopo Afrika Kusini kushuhudia Kombe la Dunia kuzinunua Vuvuzela za rangi za Klabu zao wanazoshabikia, kuingia nazo Viwanjani huko Bondeni na kuzipuliza watakavyo na Kombe la Dunia likiisha waende na Vuvuzela zao kuzipuliza kwenye Viwanja vya Klabu zao.
Kauli hiyo ya Waandaaji hao imekuja kufuatia baadhi ya Wadau, na hasa Watangazaji na baadhi ya Timu, kudai zinaleta usumbufu na huwafanya kupoteza malengo Uwanjani na hivyo Vuvuzela zipigwe marufuku kwenye Kombe la Dunia.
Malalamiko hayo yalimfanya Danny Jordaan, Mkuu wa Kamati ya Maandalizi, kuwataka Washabiki wawe wanaimba badala ya kuzipuliza Vuvuzela mfululizo.
Nae Msemaji wa Ligi Kuu England amesema wao hawana pingamizi Vuvuzela kuvamia huko kwa sababu hamna kanuni inayopinga hilo na ni juu ya Wasimamizi wa Viwanja binafsi kuamua kama hawazitaki.
Hivi sasa kuna mjadala mkubwa unaendelea huko Bondeni huku Kombe la Dunia likiendelea kuhusu Vuvuzela lakini Waandaaji wameng’ang’ania Vuvuzela ni sehemu ya utamaduni wa Soka huko Afrika Kusini na chimbuko lake ni sehemu ya Historia yao kwani Vuvuzela zilitumika wakati wa jadi kupigisha mbiu za mgambo.
Mmoja wa Waandaaji alisema: “Hivi sasa Vuvuzela si zana ya Afrika Kusini pekee! Wageni waliopo wamezinunua kwa wingi na wataondoka nazo mara baada ya Mashindano na bila shaka utaziona Old Trafford, Stamford Bridge, Emirates, Anfield, Nou Camp, Santiago Bernabeau na huko Munich kwa Bayern!!”
Lakini kuna baadhi ya Raia wa Afrika Kusini wamedai kuna ‘Washamba’ wa Vuvuzela ndio wanaharibu matumizi yake kwani hulipuliza bila taimingi kwani wenyewe huko Bondeni hulizibua kwa pamoja Uwanja mzima pale tu kuna tukio kubwa.
Nae Msemaje wa Waandaaji alimalizia: “Mashindano haya Wenyeji ni Afrika Kusini. Nyinyi kama Wageni wetu lazima mkumbatie utamaduni wetu na jinsi tunavyoshangilia. Tufunge mjadala huu ulioendelea Mwaka mzima tangu Mashindano ya Kombe la Mabara! Ama lipende Vuvuzela au lichukie tu! Sisi Afrka Kusini tunalipenda!”
CHEKI: www.sokainbongo.com

Beckenbauer aikandya England!
Franz Beckenbauer ameiponda England kwa kucheza ‘butua butua’ na amedai hilo linatokana na kutokuwa na vipaji vya nyumbani kwenye Ligi Kuu na badala yake kutegemea Wageni.
Wakati kwenye Fainali za Kombe la Dunia huo Afrika Kusini Nchi ya Beckenbauer imeanza vizuri kwa kuiwasha Australia 4-0, England imeanza kwa kusuasua kwa kuambua sare ya 1-1 na USA huku Kipa wa England Robert Green akiipa goli la zawadi USA.
Beckenbauer, Miaka 64, alikuwa Kepteni wa Germany iliyonyakua Kombe la Dunia Mwaka 1974.
Mkongwe huyo ametamka: “Niliiona England ikicheza na USA na hio haikuwa Soka na inaelekea wamerudi nyuma Kisoka kwani wanacheza mpira wa kizamani wa kubutua na kukimbiza tu!”
Beckenabauer aliongeza kwa kudai haoni kama Kocha wa England Fabio Capello anaweza kuibadili Timu.
Adidas imewanufaisha Ujerumani kwa Jabulani!!!
Beki wa England, Jamie Carragher, amedai Ujerumani imenufaika sana na kuucheza mpira wa Jabulani kwa muda mrefu kwa vile Watengenezaji wake, Adidas, ni Kampuni ya Kijerumani na vilivile ni Wadhamini wa Bundesliga na hivyo Ligi hiyo ilianza kuutumia mpira huo tangu Msimu uliopita.
Timu nyingi pamoja na Wachezaji wengi sana walio Fainali za Kombe la Dunia wameulaumu mpira huo Jabulani kwamba ni mgumu kuumiliki, kuucheza na pia huwababaisha sana Makipa kwa vile hupinda na kubadilisha mwelekeo ukishapigwa.
Carragher amedai: “Wamenufaika kwa kuutumia muda mrefu kwani mpira huu ni tofauti mno!”
Hata hivyo, Carragher amekiri Ujerumani ilicheza vizuri mno ilipowabamiza Australia 4-0.


Ivory Coast 0 Ureno 0
Huku mvua ikianguka Uwanjani Nelson Mandela Mjini Port Elizabeth, Ivory Coast na Ureno zilitoka sare ya 0-0 kwenye mechi ambayo nafasi zilikuwa adimu sana.
Supastaa Cristiano Ronaldo alikaribia kufunga pale shuti lake lilipogonga mwamba lakini baada ya hapo alifunikwa kabisa.
Ivory Coast walianza mechi hii bila ya Nahodha na Supastaa wao Didier Drogba ambae ndie Mchezaji Bora Afrika na Mfungaji Bora Ligi Kuu England ambae alivunjika mfupa mkononi kwenye mechi ya kirafiki na Japan huko Uswisi takriban siku 10 zilizopita na kulazimika kufanyiwa operesheni.
Ilibidi Drogba aombewe kibali maalum toka FIFA ili acheze mechi hii huku akiwa amevaa gamba gumu mkononi kuulinda na aliingizwa Kipindi cha Pili kuchukua nafasi ya Mchezaji mwenzake wa Chelsea Kalou na nusura afunge goli lakini shuti lake halikulenga
Mechi inayofuata kwa Ivory Coast ni dhidi ya Brazil Juni 20 na Ureno wataikumba Korea Kaskazini Juni 21.
Timu:
Ivory Coast: Barry, Demel, Toure, Zokora, Tiene, Eboue, Toure Yaya, Tiote, Gervinho, Dindane, Kalou.
Portugal: Eduardo, Ferreira, Bruno Alves, Carvalho, Fabio Coentrao, Deco, Mendes, Raul Meireles, Ronaldo, Liedson, Danny.
Refa: Jorge Larrionda (Uruguay)
CHEKI: www.sokainbongo.com


KOMBE LA DUNIA:
RATIBA: Juni 16
Saa 8.30 mchana: Honduras v Chile [Mbombela, Nelspruit]
Saa 11 jioni: Spain v Uswisi [Moses, Mabhida, Durban]
Saa 3.30 usiku: Afrika Kusini v Uruguay [Loftus, Versfed, Pretoria]
New Zealand 1 Slovakia 1
New Zealand leo wametoka sare 1-1 na Slovakia huko Uwanja wa Royal Bafokeng, Rustenburg baada ya kusawazisha bao dakika ya 92 kwa kichwa cha Reid.
Slovakia walipata bao lao dakika ya 50 Mfungaji akiwa Vittek.
Timu:
New Zealand: Paston, Reid, Nelsen, Vicelich, Smith, Bertos, Elliott, Lochhead, Fallon, Smeltz, Killen.
Akiba: Moss, Sigmund, Brown, Barron, McGlinchey, Clapham, Mulligan, Boyens, Wood, Christie, Brockie, Bannatyne.
Slovakia: Mucha, Zabavnik, Durica, Skrtel, Cech, Strba, Weiss, Sestak, Hamsik, Vittek, Jendrisek.
Akiba: Pernis, Pekarik, Kozak, Sapara, Holosko, Jakubko, Stoch, Kucka, Kopunek, Salata, Petras, Kuciak.
Refa: Jerome Damon (South Africa)
Italia 1 Paraguay 1
Mchezaji mpya wa Wigan, Antolin Alcaraz, ambae amechukuliwa toka Club Brugge na atakaeonekana na Timu yake hiyo mpya Msimu ujao unaoanza Agosti 14, jana nusura awatoe nishai Mabingwa Watetezi wa Kombe la Dunia Italy alipoifungia Nchi yake Paraguay bao kwenye dakika ya 39.
Lakini Italia wakagangamara na kusawazisha dakika ya 63 kwa bao la De Rossi dakika ya 63 na hivyo kuwaokoa Italia na kuifanya mechi imalizike 1-1.
Timu:
Italy: Buffon, Zambrotta, Cannavaro, Chiellini, Criscito, De Rossi, Marchisio, Montolivo, Pepe, Gilardino, Iaquinta.
Paraguay: Villar, Bonet, Alcaraz, Da Silva, Morel Rodriguez, Vera, Victor Caceres, Riveros, Torres, Haedo Valdez, Barrios.
Refa: Benito Archundia Tellez (Mexico)
PITIA: www.sokainbongo.com

Dalkurd ya Sweden yatoa ofa ya Tegete Mtandaoni!
Klabu ya Daraja la Kwanza ya huko Sweden, Dalkurd FF, imetoa ofa rasmi kwa Yanga kupitia mtandaoni kwa kutumia mtindo mpya wa uhamisho wa FIFA ili imchukue kwa mkopo wa Mwaka mmoja straika wa Yanga Jerry Tegete.
Ili kuondoa utata na ubabaishaji Dalkurd FF imetumia mtindo mpya wa FIFA wa kumuombea Uhamisho Tegete na utaratibu huo unatumia njia za elektroniki kupitia mtandaoni na unaitwa ‘Transfer Matching System’ [TMS] na hivyo kuondoa utaratibu wa sasa wa kutumia faksi na makaratasi ili kuhamisha Wachezaji na hivyo kuondoa dosari nyingi.
Katika mfumo wa TMS uanaotumia mtandao, ili kukamilisha uhamisho wa Mchezaji inabidi Klabu zinazouza na kununua Mchezaji ziingize kwenye mtandao taarifa zote zinazotakiwa kuhusiana na Mchezaji anaehamishwa zikiwemo Ada ya Uhamisho, Mshahara wa Mchezaji huyo, Wakala wake au Mwanasheria wake na muda wa Mkataba wake.
Pia, ada ya uhamisho ni lazima itoke Benki moja kwenda nyingine na Benki zote ziwe zinatambulika halali kisheria.
Habari za kutoa ofa hiyo rasmi zimethibitishwa na Wakala wa Tegete, Damas Ndumbaro.
Wakati wa uzinduzi wa Mradi huo mpya wa FIFA wa Uhamisho Miezi kadhaa iliyopita, Meneja Mkuu wa TMS, Mark Goddard, alisema: “Mpaka sasa mtindo uliokuwa ukitumiwa ni wa makaratasi kama ilivyokuwa miaka 100 nyuma! Ilikuwa ngumu kufuatilia Wachezaji gani wamehamishwa. Kulikuwa na uhamisho feki, kulikuwa na uuzwaji wa Wachezaji ambao hawapo ili mradi Watu mafisadi wahamishe pesa zao toka Nchi moja hadi nyingine kinyume cha sheria!”
Goddard aliongeza: “Huu ni mradi mkubwa wa FIFA. Haujabadilisha sheria za uhamisho bali unadhibiti uhamisho na kuondoa kasoro na dosari nyingi.”
Mdau mmoja wa Bongo aliunga mkono TMS kwa kuamini mtindo huo utawakata maini Mafisadi wa Soka waliokuwa wakidhulumu Wachezaji na Klabu za Bongo.

Monday, 14 June 2010

PITIA: www.sokainbongo.com

Honda ni shujaa Japan!!!!
Bao la dakika ya 39 la Honda limeipiga chini Cameroun kwa bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Free State huko Bloemfontein leo Juni 14 mechi ya Kundi E ambalo awali leo Uholanzi ilishinda 2-0 dhidi ya Denmark.
Kipindi cha pili Cameroun walijitutumua ili warudishe bila mafanikio.
Cameroun inaungana na Algeria na Nigeria kwa kuwa Timu za Afrika zilizofungwa mechi zao za kwanza za Makundi yao kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Timu pakee ya Afrika iliyoshinda ni Ghana iliyoichapa Serbia 1-0 na Afrika Kusini ilitoka sare 1-1 na Mexico.
Nyingine ni Ivory Coast wanaocheza kesho na Ureno.
Mechi inayofuata kwa Cameroun ni Juni 19 dhidi ya Denmark.
Timu:
Cameroon: Hamidou, M'bia Etoundi, N'Koulou, Bassong, Assou-Ekotto, Matip, Makoun, Enoh, Eto'o, Webo, Choupo-Moting.
Akiba: Kameni, Rigobert Song, Alex Song, N'Guemo, Njitap, Emana, Bong, Chedjou, Idrissou, Mandjeck, Ndy Assembe, Aboubakar.
Japan: Kawashima, Nagatomo, Nakazawa, Tanaka, Komano, Matsui,
Honda, Abe, Hasebe, Endo, Okubo.
Akiba: Narazaki, Uchida, Okazaki, Shunsuke Nakamura, Tamada, Yano, Iwamasa, Kengo Nakamura, Konno, Morimoto, Inamoto, Kawaguchi. Referee: Olegario Benquerenca (Portugal)
TEMBELEA: www.sokainbongo.com

Rufaa ya Mutu yatupwa, kuilipa Pauni Milioni 14 Ze Bluzi!!
Adrian Mutu ameamriwa kuilipa Chelsea fidia ya Pauni Milioni 14.3 baada ya rufaa yake kutupwa na Mahakama ya Juu huko Uswisi.
Chelsea walimfukuza Mutu Mwaka 2004 alipofungiwa kucheza Soka baada ya kugundulika akitumia kokeni na pia kumdai fidia kwa kukiuka Mkataba wake.
FIFA walimwamuru Mutu ailipe fidia Chelsea lakini Mutu akagoma na kukata rufaa CAS [Court of Arbitration for Sports], yaani Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, lakini huko nako Mutu akagonga mwamba na ndipo akakata rufaa Mahakama ya Juu ya Uswisi.
Kwa sasa Mutu yupo kwenye kifungo kingine cha Miezi 9 baada ya kugundulika anatumai dawa aina ya ‘Sibutramine’ wakati akiichezea Fiorentina Mwezi Februari na dawa hiyo ipo kwenye listi ya madawa marufuku.
Cahill alizwa na Kadi Nyekundu
Kiungo wa Australia Tim Cahill alidondokwa machozi wakati akielezea kupewa Kadi Nyekundu na hivyo kutolewa nje katika mechi ya jana ambayo Ujerumani iliichabanga Australia 4-0 katika Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia.
Cahill, Mchezaji wa Everton huko England, alionyeshwa Kadi hiyo baada ya kuvaana na Bastian Schweinsteiger lakini Watu wengi wanadai Refa Marco Rodriguez kutoka Mexico alikosea kwa kumpa Kadi hiyo na sana sana angepewa Kadi ya Njano.
Cahil amenung’unika: “Ndoto huwepo na zinateketezwa kwa muda mchache tu! Lakini nimefarijika kumsikia Schweinsteiger akisema ile si Kadi Nyekundu!”
Cahill ataikosa mechi ijayo na Ghana Siku ya Jumamosi.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Holland 2 Denmark 0
Huko Soccer City, Soweto, leo Holland imeanza vyema kampeni zake za Kombe la Dunia walipoichapa Timu ngumu Denmark kwa bao 2-0.
Hadi mapumziko mabao yalikuwa 0-0.
Holland walipata bao lao la kwanza dakika ya 46 baada ya krosi ya Van Persie kumkuta Difenda wa Denmark Poulsen ambae badala ya kuokoa alipiga kichwa kilichomgonga mwenzake Agger na kutinga wavuni.
Dirk Kuyt, Mchezaji wa Liverpool, alimalizia mpira wa Elia aliemhadaa Kipa Sorensen hiyo ikiwa ni dakika ya 85.
Mechi zinazofuata kwa Kundi hili E ni Juni 19 wakati Holland atakapocheza na Japan na Denmark kuivaa Camerou.
Timu:
Holland: 1-Maarten Stekelenburg; 2-Gregory van der Wiel, 3-John Heitinga, 4-Joris Mathijsen, 5-Giovanni van Bronckhorst, 7-Dirk Kuyt, 6-Mark van Bommel, 10-Wesley Sneijder, 8-Nigel de Jong, 23-Rafael van der Vaart, 9-Robin van Persie.
Denmark: 1-Thomas Sorensen; 4-Daniel Agger, 3-Simon Kjaer, 6-Lars Jacobsen, 15-Simon Poulsen, 10-Martin Jorgensen, 2-Christian Poulsen, 20-Thomas Enevoldsen, 12-Thomas Kahlenberg, 19-Dennis Rommedahl, 11-Nicklas Bendtner.
Refa: Stephane Lannoy (France)

Sunday, 13 June 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

MASHINE YA KIJERUMANI YATOA ONYO KALI!!!
Germany 4 Australia 0
Mjini Durban, Uwanjani Moses Mabhida, Mashine ya Kijerumani ilianza kusaga kwa ufanisi wa hali ya juu kabisa na ilichukua dakika 8 tu kuwatawanya Australia na kupata bao la kwanza kupitia fataki ya Podolski baada ya pande la Muller.
Miroslav Klose akafunga bao la pili kwa Ujerumani dakika ya 26 baada ya krosi ya Kepteni Phillip Lahm kumvuta Kipa Schwarzer na kupotea na kumkuta Klose aliefunga.
Kipindi cha Pili Mchezaji wa Everton Tim Cahill wa Australia alitolewa kwa Kadi Nyekundu na Refa Marco Rodriguez wa Mexico kwa kosa ambalo wengi watahisi halikustahili kabisa.
Kutolewa kwa Mpiganaji huyo wa Australia kuliwapa pengo kubwa na kuruhusu Ujerumani kupachika bao mbili zaidi kupitia Muller na Cacau.
Timu:
Australia: Schwarzer, Wilkshire, Moore, Neill, Chipperfield, Valeri, Grella, Emerton, Culina, Garcia, Cahill.
Akiba: Federici, Beauchamp, Kennedy, Kewell, Holman, Jedinak, Rukavytsya, Milligan, Carney, Vidosic, Bresciano, Galekovic.
Germany; Neuer, Lahm, Friedrich, Mertesacker, Badstuber, Schweinsteiger, Khedira, Muller, Ozil, Podolski, Klose.
Akiba: Wiese, Jansen, Aogo, Tasci, Kiessling, Trochowski, Kroos, Cacau, Boateng, Marin, Gomez, Butt.
Refa: Marco Rodriguez [Mexico]
CHEKI: www.sokainbongo.com

Capello na utata wa Kipa!!!
Meneja wa England Fabio Capello ana mtihani mkubwa wa kuchagua nani Kipa wake katika mechi ijayo ya Kombe la Dunia England v Algeria Ijumaa Juni 18 baada ya Kipa aliekuwa akimtegemea Robert Green kuiangusha vibaya kwa kutoa goli la zawadi kwa USA na kufanya mechi imalizike 1-1.
Makipa wengine wa England ni Mkongwe David James na Chipukizi Joe Harta mbao wote hao ni mahiri na kwa baadhi ya Wadau ni, pengine, bora kupita Robert Green.
Capello amekataa kumlaumu Green lakini ameweka bayana hajaamua nani atakuwa Kipa kwenye mechi na Algeria.
Capello amesema: “Makosa ni makosa, nitaongea na Green na baada ya hapo nitaamua.”
Argentina v Nigeria walengwa na Mionzi ya Leza kwenye mechi
FIFA imeamuru ufanyike uchunguzi wa kina baada ya Wachezaji kwenye mechi kati ya Argentina na Nigeria kulengwa na Mionzi ya Kijani toka kwenye Leza Uwanjani Ellis Park, Johannesburg hapo jana.
Ingawa hamna Timu iliyolalamikia tukio hilo, FIFA imeamua kulichunguza ili kujua Mtu huyo alipitapita vipi na chombo cha kulengesha Mionzi ya Leza na kuingia ndani ya Uwanja.
Mara baada ya kugundulika Mionzi hiyo Walinzi walifuatilia na haikurudiwa tena.
Hii si mara ya kwanza kwa Mionzi ya aina hiyo kutumika Uwanjani kwani Februari 2008 Cristiano Ronaldo alipokuwa akiichezea Manchester United dhidi ya Lyon huko Ufaransa alilengwa nayo kwenye mechi hiyo.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Ghana 1 Serbia 0
Ghana leo imekuwa Timu ya kwanza toka Afrika kuonja ushindi katika Fainali za Kombe la Dunia huko Uwanja wa Loftus, Pretoria walipoifunga Serbia kwa bao 1-0, bao la penalti ya dakika 85 Mfungaji akiwa Asamoah Gyan.
Timu nyingine za Afrika ambazo tayari zimeshacheza mecho moja moja ni Wenyeji Afrika Kusini waliotoka sare ya 1-1 na Mexico na Nigeria waliofungwa 1-0 na Argentina.
Hadi mapumziko, Serbia na Ghana zilikuwa hazijafungana na matukio yote makuu yalitokea Kipindi cha Pili.
Kwenye dakika ya 74 Serbia walibakia Mtu 10 baada ya Alexander Lukovic kupewa Kadi ya Njano ya pili na hivyo kuwashwa Nyekundu na kutolewa baada ya kumshika Asamoah Gyan aliekuwa anachoropoka.
Licha ya kucheza pungufu Serbia bado kidogo wapate bao dakika ya 79 kupitia Krasic lakini Kipa Kingston aliokoa vizuri sana.
Ndipo ilipotimu dakika ya 83 na Ghana kupewa penalti baada ya Beki Kuzmanovic kuunawa mpira wa juu.
Asamoah Gyan akapiga penalti hiyo na kumpeleka mbovu Kipa Stojkoviv na kuipa Ghana bao muhimu na la ushindi.
Katika dakika ya 92, Gyan tena angepata bao la pili lakini bomba yake ikagonga mwamba.
Mechi inayofuata Ghana wataivaa Australia Juni 19 na Serbia watapambana na Ujerumani Juni 18.
Timu:
Serbia: Stojkovic; Ivanovic, Vidic, Lukovic Kolarov; Krasic, Stankovic, Milijas, Jovanovic; Zigic, Pantelic.
Ghana: Kingson; Pantsil, Mensah, Vorsah, Sarpei; Annan, Asamoah, Ayew, Boateng; Asamoah Gyan, Tagoe.
Refa: Hector Baldassi (Argentina)
CHEKI: www.sokainbongo.com

Slovenia 1 Algeria 0
Inaelekea Kundi C ni la balaa kwa Makipa kwani baada ya jana Kipa wa England kufanya kosa kubwa na kuwazawadia USA bao la kusawzisha leo Kipa wa Algeria, Faouzi Chaouchi, katika dakika ya 79 alifanya kosa kama la Kipa wa England, Robert Green, na kuwapa ushindi wasiotegemea Slovenia.
Shuti la mbali la Koren ambalo lilielekea halina madhara lilimponyoka Kipa huyo wa Algeria na kutinga wavuni.
Dakika mbili kabla ya bao hilo, Kipa wa Slovenia, Samir Handanovic, nusura awape zawadi Algeria pale pasi yake kwa Beki Suler ilinaswa na Karim Ziani lakini Mchezaji huyo itabidi ajilaumu kwani alishindwa kuukontroli mpira wakati akiwa pekee na Kipa.
Algeria ilimaliza mechi hii ikiwa Mtu 10 baada ya Ghezzal kupewa Kadi Nyekundu dakika ya 74 kufuatia Kadi za Njano mbili, ya kwanza aliyoipata dakika moja tu tangu aingizwe toka benchi dakika ya 60 na dakika ya 74 akalambwa Kadi ya pili ya Njano baada ya kuushika mpira kwa makusudi.
Mechi zinazofuata kwa Timu hizi ni Algeria v England na USA v Slovenia.
Timu:
Algeria: Chaouchi, Yahia, Bougherra, Halliche, Belhadj, Kadir, Lacen, Ziani, Yebda, Djebbour, Matmour.
Akiba: Gaouaoui, Mansouri, Boudebouz, Ghezzal, Saifi, Bellaid, Laifaoui, Guedioura, Medjani, Mesbah, Abdoun, M'Bohli.
Slovenia: Samir Handanovic, Brecko, Suler, Cesar, Jokic, Kirm, Koren, Radosavljevic, Birsa, Novakovic, Dedic.
Akiba: Jasmin Handanovic, Dzinic, Ilic, Pecnik, Ljubijankic, Krhin, Filekovic, Komac, Stevanovic, Mavric, Matavz, Seliga.
Refa: Carlos Batres (Guatemala).
Powered By Blogger