CHEKI: www.sokainbongo.com
Lipende au Lichukie, Vuvuzela Daima!!!
Vuvuzela safarini Mtoni!!!
Usishangae Msimu ujao wa Ligi Kuu England utakaoanza Agosti 14 ukianza kuziona Vuvuzela za Rangi nyekundu zikiwa Old Trafford, za rangi ya bluu zikiwa Stamford Bridge, nyeusi na nyeupe zikiwa St James Park na za rangi ya Ze Gunners zikiwa Emirates kwani Waandaaji wa Kombe la Dunia huko Afrika Kusini wamewahimiza Washabiki toka kila kona ya Dunia waliopo Afrika Kusini kushuhudia Kombe la Dunia kuzinunua Vuvuzela za rangi za Klabu zao wanazoshabikia, kuingia nazo Viwanjani huko Bondeni na kuzipuliza watakavyo na Kombe la Dunia likiisha waende na Vuvuzela zao kuzipuliza kwenye Viwanja vya Klabu zao.
Kauli hiyo ya Waandaaji hao imekuja kufuatia baadhi ya Wadau, na hasa Watangazaji na baadhi ya Timu, kudai zinaleta usumbufu na huwafanya kupoteza malengo Uwanjani na hivyo Vuvuzela zipigwe marufuku kwenye Kombe la Dunia.
Malalamiko hayo yalimfanya Danny Jordaan, Mkuu wa Kamati ya Maandalizi, kuwataka Washabiki wawe wanaimba badala ya kuzipuliza Vuvuzela mfululizo.
Nae Msemaji wa Ligi Kuu England amesema wao hawana pingamizi Vuvuzela kuvamia huko kwa sababu hamna kanuni inayopinga hilo na ni juu ya Wasimamizi wa Viwanja binafsi kuamua kama hawazitaki.
Hivi sasa kuna mjadala mkubwa unaendelea huko Bondeni huku Kombe la Dunia likiendelea kuhusu Vuvuzela lakini Waandaaji wameng’ang’ania Vuvuzela ni sehemu ya utamaduni wa Soka huko Afrika Kusini na chimbuko lake ni sehemu ya Historia yao kwani Vuvuzela zilitumika wakati wa jadi kupigisha mbiu za mgambo.
Mmoja wa Waandaaji alisema: “Hivi sasa Vuvuzela si zana ya Afrika Kusini pekee! Wageni waliopo wamezinunua kwa wingi na wataondoka nazo mara baada ya Mashindano na bila shaka utaziona Old Trafford, Stamford Bridge, Emirates, Anfield, Nou Camp, Santiago Bernabeau na huko Munich kwa Bayern!!”
Lakini kuna baadhi ya Raia wa Afrika Kusini wamedai kuna ‘Washamba’ wa Vuvuzela ndio wanaharibu matumizi yake kwani hulipuliza bila taimingi kwani wenyewe huko Bondeni hulizibua kwa pamoja Uwanja mzima pale tu kuna tukio kubwa.
Nae Msemaje wa Waandaaji alimalizia: “Mashindano haya Wenyeji ni Afrika Kusini. Nyinyi kama Wageni wetu lazima mkumbatie utamaduni wetu na jinsi tunavyoshangilia. Tufunge mjadala huu ulioendelea Mwaka mzima tangu Mashindano ya Kombe la Mabara! Ama lipende Vuvuzela au lichukie tu! Sisi Afrka Kusini tunalipenda!”
No comments:
Post a Comment