Saturday 19 June 2010


Magazeti England waibatukia England
Kila Gazeti huko England limeishambulia Timu ya England kwa kucheza ovyo katika mechi ya Kundi C ya Kombe la Dunia huko Green Point Ijumaa Juni 18 dhidi ya Algeria na kuambulia sare ya 0-0 na kuwafanya washike nafasi ya 3 Kundi hilo nyuma ya Slovenia na USA.
Magazetio hayo pia yalionyesha wasiwasi wao na fomu ya Straika Wayne Rooney ambae katika mechi mbili za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini ameonyesha kiwango kilichoporomoka.
Sare ya jana ilimfanya hata Kocha wa England Fabio Capello aishangae Timu yake na kusema uchezaji wake ulikuwa ni kama Timu tofauti na ile anayoijua.
Sasa England haina njia ya mkato ni lazima iifunge Slovenia katika mechi yao ya mwisho ili wasonge mbele.
Gazeti la Daily Mirror lilitoka na kichwa cha habari: “Ni upuuzi mtupu!” na Guardian lilisema: “Hamna Moto, Hamna Moyo, Hamna Matumaini!”
Nalo The Sun walichapisha habari zinazosema England haina kisingizio bali ni wabovu.
England watamaliza na Slovenia Jumatano Juni 23.

No comments:

Powered By Blogger