Saturday, 18 October 2008

MABINGWA Man U 4 West Brom 0

Kisago cha kipindi cha pili cha mchezo kimewafanya West Bromwich Albion wabugia mabao manne baada ya kujihami vizuri kipindi chote cha kwanza ingawa Refa Mark Halsey alilikataa bao la wazi la Wayne Rooney kipindi hicho.
Hadi mapumziko 0-0.
Kipindi cha pili Rooney alipata bao la kwanza, Ronaldo la pili, Berbatov la tatu na Nani akashindilia la nne.
MATOKEO:

Arsenal 3 Everton 1

Liverpool 3 Wigan 2

Aston Villa 0 Portsmouth 0

Fulham 0 Sunderland 0

Bolton 0 Blackburn 0
Boro 0 Chelsea 5

Middlesbrough wakiwa nyumbani Uwanja wa Riverside wamecheza mpira mbovu wa chini ya kiwango na kuwafanya wanaoongoza LIGI KUU Chelsea kupata pointi 3 za chee na magoli matano bila ya hata kuonyesha kiwango chochote cha juu.
Ni mechi ambayo inapingana na imani ya wengi kuwa LIGI KUU UINGEREZA ndio bora duniani.
Mpaka timu zinaenda mapumziko Chelsea walikuwa mbele kwa 1-0 kwa bao lililofungwa na Kalou.
Baada ya mapumziko Juliano Belletti wa Chelsea akapachika bao la pili kwa mkwaju mkali. Bao la tatu lilimbabatiza beki wa Boro David Wheater baada ya shuti la Kalou.
Ni Kalou tena aliepiga krosi iliyomaliziwa na Frank Lampard kwa kichwa kufanya 4-0.
Karamu ya magoli ilimaliziwa na Florent Malouda baada ya Kipa wa Boro Ross Turnbull kutema shuti la Anelka.

Middlesbrough: Turnbull, Grounds, Wheater, Riggott, Taylor, Aliadiere, Shawky, O'Neil, Adam Johnson, Downing, Mido. AKIBA: Jones, Digard, Emnes, Alves, Bennett, John Johnson, Walker.
Chelsea: Cudicini, Bosingwa, Terry, Alex, Bridge, Belletti, Lampard, Mikel, Kalou, Anelka, Malouda. AKIBA: Hilario, Ivanovic, Sinclair, Ferreira, Deco, Mancienne, Stoch.
MAN U WAWEKA WAPELELEZI BRAZIL KUVUMBUA VIPAJI

Mabingwa wa Ulaya na Uingereza, Manchester United, wameweka watu wawili wa kudumu huko Brazil ili kuzunguka nchi yote na kutafuta Wachezaji chipukizi wenye vipaji ili wawasajili.
Mpaka sasa Klabu hiyo Man U inao Wachezaji wanne vijana ambao ni Anderson, Mapacha Rafael na Fabio Da Silva na Rodrigo Possebon.
Meneja wa Man U Six Alex Ferguson amethibitisha kuwepo kwa wasakaji hao kwa kusema: ‘Ni nchi ambayo lazima uiangalie kwa umakini kwani siku zote inatoa wachezaji spesho wanaomudu mechi kubwa.’

BALLACK NJE WIKI TATU

Kiungo wa Chelsea, Michael Ballack, atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye miguu yote miwili baada ya kusikia maumivu mara baada ya kuichezea Timu ya Taifa ya Ujerumani walipoifunga Wales bao 1-0 siku ya Jumatano kwenye mechi ya KOMBE LA DUNIA.

Friday, 17 October 2008

LIGI KUU: DONDOO ZA MECHI ZA VIGOGO ZA JUMAMOSI

Arsenal v Everton [Emirates Stadium, London, saa 11 jioni]

Arsenal wakiwa uwanja wa nyumbani huenda wakawakosa nyota wao William Gallas, Bacary Sagna na Nicklas Bendtner ambao wamerudi klabuni majeruhi baada ya kutoka kwenye Timu zao za Taifa zilizoshiriki michuano ya kuwania nafasi za kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010.
Arsenal ambao wako nafasi ya 4 wakiwa na pointi 13 wameshapoteza mechi mbili kwenye LIGI KUU msimu huu wakati msimu mzima uliopita walipoteza mechi 3 tu!
Tangu wahamie hapo Emirates Stadium wamepoteza mechi 2 za LIGI KUU ya kwanza ikiwa dhidi ya West Ham Agosti 2006 na ile ya juzi tu Septemba 27 walipofungwa na timu mpya LIGI KUU Hull City.
Everton wanashikilia nafasi ya 15 na wana pointi 8 ingawa hawajafungwa hata mechi moja ugenini tangu ligi ianze.
Refa kwenye mechi hii ni Peter Walton.

Liverpool v Wigan [Anfield, Liverpool saa 11 jioni]

Nyota na mfungaji wa Liverpool Fernando Torres ataikosa mechi baada ya kuumizwa kwenye mechi ya Nchi yake Spain ilipoifunga Belgium 2-1 kwenye KOMBE LA DUNIA.
Wigan hawajawahi kuwafunga vigogo wa LIGI KUU ingawa msimu uliopita kwenye mechi kama hii walitoka sare ya 1-1 baada ya Emile Heskey kuisawazishia dakika ya mwisho ya mchezo.
Refa: Alan Wiley

Middlesbrough v Chelsea [Riverside Stadium, saa 8 dak 45 mchana]

Chelsea ambao wanaongoza LIGI KUU watakuwa wanatetea rekodi yao ya kutofungwa mechi hata moja ya ligi tangu Mbrazil Luis Felipe Scolari ashuke Chelsea.
Middlesbrough ambao walianza ligi vizuri mwezi Agosti kwa kushinda mechi 4 lakini wakapoteza mechi zote walizocheza Septemba ingawa mwezi huu Oktoba wameanza kwa ushindi baada ya kuwafunga Wigan.
Refa: Phil Dowd

Manchester United v West Brom [Old Trafford saa 1 na nusu usiku]

Mabingwa watetezi Man U wataingia uwanjani kucheza na West Brom ambayo haijawahi hata siku moja kuifunga Man U kwenye historia ya LIGI KUU.
Refa: Mark Halsey
BAADA YA KIPIGO CHA CHILE, MENEJA WA ARGENTINA AMWAGA UNGA!!!!!

Meneja wa Timu ya Taifa ya Argentina, Alfio Basile, amejiuzulu wadhifa wake huo mara baada ya Argentina kupigwa bao 1-0 na Chile katika mechi ya Kundi la Nchi za Marekani Kusini la kuwania kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010.
Rais wa Chama cha Soka cha Argentina, Julio Grondona, amesema licha ya kumbembeleza Basile asijiuzulu Kocha huyo aligoma.
Alfio Basile ashawahi kuwa Meneja wa Argentina katika kipindi cha nyuma kati ya mwaka 1990 hadi 1994.
Katika Kundi la Nchi hizo za Marekani ya Kusini, Argentina inashikilia nafasi ya 3 ikiwa nyuma ya Paraguay inayoongoza na Brazil ni ya pili. Timu nne za juu za Kundi hili ndizo zinaingia FAINALI KOMBE LA DUNIA moja kwa moja.
Inasemekana nafasi ya Alfio Basile huenda ikachukuliwa na mmoja kati ya Kocha wa Timu ya Vijana wa Argentina Sergio Batista au Kocha wa Klabu ya River Plate Diego Simeone ama Miguel Angel Russo.
RIO: 'Kiwango cha Rooney kimepanda kwa sababu ya kutua Berbatov Man U!'

Rio Ferdinand, beki mahiri wa Mabingwa Manchester United, ambae pia alikuwa Nahodha wa England kwenye mechi mbili za England za kuwania kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010 ambazo zote walishinda dhidi ya Kazakhstan kwa mabao 5-1 na Belarus bao 3-1, amesema anaamini kuibuka upya kwa kiwango cha juu kwa Wayne Rooney kinatokana na Manchester United kumununua Dimitar Berbatov.
Katika mechi tatu zilizopita za England, Wayne Rooney amefunga mabao 5 baada ya kuichezea England kwa mwaka mmoja bila ya kufunga bao lolote.
Rio anasema: 'Nadhani Berbatov ametusaidia na amemsaidia Rooney kuinua kiwango chake. Kila mchezaji daima hutaka kumuonyesha mchezaji mpya ubora wake. Sasa huu ushindani uliopo Man U unazaa matunda.!'
Rio aliongeza: 'Rooney ni mchezaji hodari na ni jinamizi kwa beki yeyote anaepambana nae. Ni mpiganaji na daima huhangaika kutafuta ushindi kwa timu yake na hata mazoezini yuko hivyohivyo-ni mshindani mahiri!'
Nae Muargentina Carlos Tevez amekanusha vikali taarifa zilizogaa na zilizomnukuu yeye akitamka kuwa kiwango chake msimu huu kimeshuka kwani Klabu ya Manchester United inamchezesha tofauti na alivyozoea na hivyo kusababisha kuwa butu msimu huu kwani mpaka sasa amefunga goli moja tu.
Carlos Tevez amezikana taarifa hizo kwa kutamka: 'Sijafanya mahojiano na Mwandishi yeyote na kwa kweli nina furaha kuwa Manchester United. Mie nikiwa uwanjani nataka timu ishinde tu na sijali nacheza wapi na vipi.'
ARSENAL NA LIVERPOOL WAKUMBWA NA MAJERUHI WA NYOTA WAO!!!

Baada ya Wachezaji Mastaa kwenda kutetea Nchi zao kwa zaidi ya siku 10 ili kuwania nafasi za kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI Klabu kadhaa za LIGI KUU UINGEREZA zimewapokea tena nyota wake kwa masikitiko makubwa baada ya baadhi kurudi wakiwa na majeruhi waliyopata kwenye mechi hizo za KOMBE LA DUNIA.
Klabu ya Liverpool imetangaza nyota wao Fernando Torres atakuwa nje kwa wiki 2 baada ya kuumia kwenye mechi ya Nchi yake Spain ilipocheza na Belgium na kushinda 2-1.
Torres alitolewa dakika ya 16 tu ya mchezo.
Hii inamaanisha Torres atakosa mechi dhidi ya Wigan wikiendi hii, ile na Atletico Madrid Jumatano na ya Chelsea wiki ijayo.

Nao Arsenal wametangaza Wachezaji wao watatu wamerudi majeruhi Klabuni hapo. Wachezaji hao ni Nahodha William Gallas, Bacary Sagna na Nicklas Bendtner.
Lakini Meneja Arsene Wenger amesema Mikael Silvestre aliehamia hapo toka Man U huenda akacheza mechi yake ya kwanza na pia Robin van Persie, Johan Djourou na Cesc Fabregas wamo kikosini ingawa taarifa za awali ziliripoti nao ni majeruhi.
Wikiendi hii Arsenal wako kwao Emirates Stadium kucheza na Everton kwenye LIGI KUU.
UEFA WASIMAMISHA KWA MUDA ADHABU YA KUTOKUCHEZA UWANJA WA ATLETICO MADRID: Mechi ya Atletico Madrid v Liverpool kuchezwa uwanjani hapo!!

Chama cha Soka Ulaya, UEFA, kimesimamisha kwa muda ile adhabu ya kuufungia Uwanja wa Atletico Madrid ya Spain, Vicente Calderon Stadium, mjini Madrid, ya kutochezewa mechi 3 kwa sababu ya vurugu za Mashabiki wa Klabu hiyo zilizoambatana na vituko vya ubaguzi wa rangi walizofanyiwa Marseille ya Ufaransa kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwanzoni mwa mwezi huu.
Hatua hii ya kusimamisha adhabu hii kwa muda kufuatia rufaa ya Atletico Madrid inamaanisha mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ya Jumatano ijayo tarehe 22 Oktoba 2008 itachezewa hapohapo Uwanja wa Vicente Calderon.
Mbali ya Atletico Madrid kukata rufaa, Liverpool nao walilalamika kuwa adhabu hiyo ya kuufungia uwanja huo pia inawaadhibu Mashabiki wao na kuwatia hasara kwani walishafanya mipango siku nyingi kwenda mjini Madrid kuishangilia Liverpool na hivyo kufanya mechi kuchezwa nje ya Madrid ni usumbufu na hasara kwao.

Thursday, 16 October 2008

RATIBA YA WIKIENDI HII NA WIKI IJAYO
Baada ya hekaheka zilizotanda dunia nzima za mitoano ya kutafuta Nchi zitakazoingia FAINALI KOMBE LA DUNIA huko AFRIKA KUSINI mwaka 2010, sasa tunarudi kwenye michuano ya Vilabu na macho yetu yako kwenye LIGI KUU UINGEREZA kwa mechi zitakazochezwa wikiendi hii pamoja na mechi za UEFA CHAMPIONS LEAGUE za Jumanne na Jumatano ijayo:
Ratiba ni kama ifuatavywo:

LIGI KUU UINGEREZA

JUMAMOSI, 18 Oktoba 2008

Middlesbrough v Chelsea [saa 8 dak 45 mchana saa za bongo]

Arsenal v Everton [saa 11 jioni]

Aston Villa v Portsmouth

Bolton v Blackburn

Liverpool v Wigan

Fulham v Sunderland

Man United v West Brom [saa 1 na nusu usiku]

JUMAPILI, 19 Oktoba 2008

Hull City v West Ham [saa 12 jioni]

Stoke City v Tottenham [saa 1 usiku]

JUMATATU, 20 Oktoba 2008

Newcastle v Man City [saa 5 usiku]

UEFA CHAMPIONS LEAGUE

JUMANNE, 21 October 2008


[Saa 4 dak 45 usiku]

Bayern Munich v Fiorentina,

FC Porto v Dynamo Kiev,

Fenerbahce v Arsenal,

Juventus v Real Madrid,

Man United v Celtic,

Steaua Bucuresti v Lyon,

Villarreal v AaB, Gp E,

Zenit St Petersburg v BATE, Gp H, [Saa 2 na nusu usiku]

JUMATANO, 22 October 2008

[Saa 4 dak 45 usiku]

Atletico Madrid v Liverpool,

Basle v Barcelona,

Bordeaux v CFR Cluj-Napoca,

Chelsea v Roma,

Inter Milan v Anorthosis Famagusta,

Panathinaikos v Werder Bremen,

PSV v Marseille,

Shakhtar Donetsk v Sporting,




KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010: ROONEY AIPA USHINDI ENGLAND!
Belarus 1 England 3

Wayne Rooney alipachika mabao 2-0 katika ushindi wa mabao 3-1 England walioupata mjini Minsk, Belarus katika mechi ya mitoano ya kutafuta Nchi zitakazoingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI mwaka 2010.
Huu ni ushindi wa nne kwa England katika Kundi lake la 6 baada ya kuzifunga Andorra 2-0, Croatia 4-1, Kzakhstan 5-1.
England ilipata bao la kwanza kupitia Kiungo anaepondwa sana akichezea England, Steven Gerrard, katika dakika ya 11 baada ya pasi safi ya Wayne Rooney.
Belarus walisawazisha kabala ya hafutaimu.
Kipindi cha pili Wayne Rooney akapachika mabao mawili dakika za 50 na 74.

Belarus: Zhevnov, Verkhovtsov, Filipenko, Omelyanchuk, Molosh, Kulchy, Sitko, Putsilo (Rodionov 67), Stasevich (Viacheslav Hleb 90), Kutuzov (Strakhanovich 77), Bulyga. AKIBA: Veremko, Korytko, Pavlov, Sosnovskiy.
KADI: Putsilo.
GOLI: Sitko 28.
England: James, Brown, Ferdinand, Upson, Bridge, Barry, Lampard, Gerrard, Walcott (Wright-Phillips 68), Rooney (Beckham 87), Heskey (Crouch 70). AKIBA: Carson, Johnson, Lescott, Defoe.
MAGOLIs: Gerrard 11, Rooney 50, 74.
WATAZAMAJI: 32,000.
REFA: Terje Hauge (Norway).
MATOKEO MENGINE:
ULAYA
Russia 3 Finland 0
Czech 1 Slovenia 0
Norway 0 Holland 1
Croatia 4 Andorra 0
Germany 1 Wales 0
Italy 2 Montenegro 0
Portugal 0 Albania 0
MAREKANI YA KUSINI
Paraguay 1 Peru 0
Chile 1 Argentina 0
Brazil 0 Colombia 0
Venezuela 3 Ecuador 0

Tuesday, 14 October 2008

KOMBE LA DUNIA: BELARUS v ENGLAND= Nani kucheza kiungo?
GERRARD AU LAMPARD?

Mjadala, mabishano, malumbano na sasa yamefika kwa Meneja wa England, Fabio Capello, na hata wahusika wenyewe wakuu- Steven Gerrard na Frank Lampard.
Uingereza nzima kuanzia kwa Washabiki, Waandishi, Wataalam wa Soka na hata Meneja wa England sasa wamekumbwa kwenye utata wa je Steven Gerrard na Frank Lampard wanaweza kucheza timu moja?
Wengi, hasa Waandishi na Wataalam wa Soka, wametoa takwimu na vithibitisho kadhaa vya mechi walizocheza pamoja wakiwa Timu ya Taifa ya England na kila kitu kimethibitisha kwamba nyota hao wawili wanaotamba kwenye Klabu zao za Chelsea na Liverpool hawawezi kucheza timu moja kwa wakati mmoja.
Waliobobea kwenye soka wanadai wote wawili wanacheza staili ya aina moja na kwa mfumo unaotumiwa na England haiwezekani wakacheza pamoja.
Lakini, Meneja wa England, Fabio Capello amedai: 'Hivi watu kwa nini wanauliza kuhusu Gerrard na Lampard? Nasema wanaweza kucheza pamoja! Ni mastaa, wachezaji mahiri hawa!'
Kitu cha kushangaza ni kuwa mwenyewe Steven Gerrard ambae ni Nahodha wa Liverpool amekiri: 'Ntakuwa mkweli sijawahi kuichezea England vizuri kama nnavyoichezea Liverpool. Nadhani tatizo langu ni kwamba nataka kufanya kila kitu peke yangu uwanjani, kuzunguka uwanja mzima kama vile hakuna wengine wanaoweza kuiendesha timu! Hili Capello ameligundua na tumeongea na hata Meneja wa Liverpool Rafael Benitez ametaka nitulize boli.'
Gerrard anaendelea kukiri hata akiachwa mechi ya kesho hasikitiki kwani kwake ushindi kwa England ndio kitu muhimu zaidi.
KOMBE LA DUNIA: MECHI ZA MITOANO KUINGIA FAINALI AFRIKA KUSINI 2010

ULAYA:

Timu za Mataifa ya Ulaya baada ya mikikimikiki ya mechi za Jumamosi kesho tena wanajimwaga dimbani katika mechi za Makundi ya Nchi za Ulaya kuwania nafasi za kuingia Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Nchi hizi za Ulaya zimegawanywa Makundi 9 na bingwa wa kila Kundi anaingia moja kwa moja Fainali hizo.
Nchi zitakazoshika nafasi ya pili katika Makundi hayo 9 zitakachukuliwa Timu Nane Bora kugawanywa timu mbili mbili zitakazoshindana mechi za mtoano za nyumbani na ugenini ili kupata timu nyingine nne zitakazoenda Fainali.
Uingereza ambayo ipo Kundi la 6 pamoja na Croatia, Ukraine, Belarus, Kazakhstan na Andorra inaongoza Kundi hilo ikiwa na pointi 9 baada ya kushinda mechi zake tatu za kwanza ilipozifunga Andorra 2-0, Croatia 4-1 na Kazakhstan 5-1.
Uingereza kesho Jumatano watakuwa ugenini kupambana na Belarus huko mjini Minsk.

RATIBA: Jumatano, 15 Oktoba 2008

Austria v Serbia,

Belarus v England, [saa 3 na nusu usiku bongo taimu]

Belgium v Spain,

Bosnia-Herzegovina v Armenia,

Croatia v Andorra,

Czech Republic v Slovenia,

Estonia v Turkey,

Georgia v Bulgaria,

Germany v Wales,

Greece v Switzerland,

Iceland v FYR Macedonia,

Italy v Montenegro,

Latvia v Israel,

Lithuania v Faroe Islands,

Luxembourg v Moldova,

Malta v Hungary,

Northern Ireland v San Marino,

Norway v Holland,

Portugal v Albania,

Rep of Ireland v Cyprus,

Russia v Finland,

Slovakia v Poland,

MAREKANI YA KUSINI:

Timu nne za juu za Kundi hili lenye jumla ya Nchi 10 zitaingia moja kwa moja FAINALI huko AFRiKA KUSINI mwaka 2010.
Timu ya 5 itakwenda kupambana na Mshindi wa Nne Kundi la Oceania ili kupata timu moja kati ya hizo itakayoingia FAINALI.
Mpaka sasa Paraguay ndie anaeongoza akiwa na pointi 20, wa pili ni Brazil pointi 16 , watatu ni Argentina nae ana pointi 16 [kazidiwa magoli na Brazil] na wanne ni Chile pointi 13.
Timu zote zimecheza mechi 9.

RATIBA:

Jumanne 14 Oktoba 2008

Bolivia v Uruguay

Jumatano 15 Oktoba 2008

Paraguay v Peru

Chile v Argentina

Venezuela v Ecuador

Brazil v Colombia
INJINI YA MANCHESTER UNITED KUANZA KUNGURUMA TENA: Hargreaves na Carrick kuonekana uwanjani wikiendi hii!!

Bosi wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amethibitisha kwamba Wachezaji wake wawili ambao ndio injini ya Klabu yake, Michael Carrick na Owen Hargreaves sasa wamepona na watashuka tena uwanjani wikiendi hii wakati Mabingwa hao wa LIGI KUU watakapowakaribisha West Bromwich Old Trafford kwenye mechi ya LIGI KUU UINGEREZA siku ya Jumamosi tarehe 18 Oktoba 2008. Baada ya Kiungo mwingine mahiri, Paul Scholes, kuumia na inaaminika atakuwa nje ya uwanja hadi Desemba, Man U walikuwa na uhaba mkubwa wa viungo na taarifa za kupona kwa Hargreaves na Carrick ni habari njema kwa mashabiki wa timu hiyo.
Carrick ameshakosa mechi 6 tangu avunjike mfupa mguuni kwenye mechi waliyocheza Anfield na Liverpool mwezi Septemba na Hrgreaves ana tatizo la muda mrefu la goti ambalo hutulia na kurudi tena tangu ajiunge na Man U akitokea Bayern Munich mwezi Agosti mwaka jana.
Sir Alex Ferguson amesema Wachezaji wote wako kwenye mazoezi kamili na bila shaka watakuwemo kwenye kikosi cha mechi ya Jumamosi watakapocheza na West Bromwich.
UEFA WAPIGA MARUFUKU UWANJA WA ATLETICO MADRID: Mechi ya Atletico Madrid na Liverpool kuchezwa kwingine!!

Chama cha Soka Ulaya, UEFA, kimeupiga marufuku Uwanja wa Klabu ya Atletico Madrid ya Spain uitwao Calderon Stadium kuchezewa mechi za UEFA CHAMPIONS LEAGUE kufuatia vurugu za mashabiki wa Klabu hiyo zilizoambatana na vitendo vya ubaguzi wa rangi kwenye mechi dhidi ya Marseille ya Ufaransa katika michuano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE iliyochezwa tarehe 1 Oktoba ambayo Atletico Madrid walishinda 1-0.
Katika mechi hiyo Wachezaji wa Marseille ambao wengi ni weusi walipigiwa kelele za milio ya nyani na baada ya mechi basi lao lilishambuliwa. Vilevile Mashabiki wa Marseille waliokuwemo humo uwanjani walipigwa na hata Polisi waliingilia na kuwasulubu zaidi [tizama picha Mashabiki wa Marseille wakishambuliwa na Polisi].
Mbali ya Klabu ya Atletico Madrid kufungiwa uwanja wao vilevile wamekung'utwa faini nzito ya Euro 150,000 [takriban Sh milioni 225] na Meneja wao Javier Aguirre nae amepigwa marufuku asikae kwenye benchi la akiba, asiwepo kwenye vyumba vya Wachezaji kubadilishia nguo hapo uwanjani na pia asifanye mawasiliano yeyote na timu yake wakati wa mechi.
Adhabu hizi zinamaanisha mechi za Atletico Madrid na Liverpool hapo tarehe 22 Oktoba na ile na PSV Eindhoven ya tarehe 26 Novemba itabidi zichezwe kwenye uwanja mwingine ulio umbali usiopungua maili 200 toka jiji la Madrid.
Atletico Madrid wamepewa mpaka saa 7 mchana tarehe 17 Oktoba 2008 kukata rufaa kama hawakuridhika na adhabu.
ENGLAND: Nahodha John Terry na Ashley Cole kukosa mechi ya Jumatano na Belarus!

Nahodha wa Timu ya Taifa John Terry na Mlinzi Ashley Cole hawatacheza mechi ya Jumatano huko Minsk, Belarus dhidi ya Belarus katika mitoano ya kutafuta timu zitazocheza FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010 kwa kuwa wote ni majeruhi.
John Terry aliikosa mechi ya Jumamosi England walipoifunga Kazhakstan mabao 5-1 kwenye Uwanja wao wa Wembley katika mechi ya Kombe la Dunia.
Ashley Cole alicheza mechi hiyo ingawa alipata wakati mgumu sana pale alipozomewa na mashabiki wa England kwa kufanya kosa kubwa lililowazawadia Kazakhstan bao lao moja. Kitendo hicho cha kumzomea Cole kimelaumiwa vikali na wachezaji wa England.

MAREKANI KUSINI: Venezuela 0 Brazil 4; Ecuador 1 Chile o

Katika Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini la KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI 2010, Brazil ilipata ushindi mnono ugenini Venezuela pale waliposhinda mabao 4-0 huku nyota wao Kaka akicheza kwa mara ya kwanza tangu Novemba mwaka jana na kufunga bao moja.
Mabao mengine ya Brazil yalifungwa na Robinho aliefunga bao 2 na Adriano 1.
Brazil wako nafasi ya pili katika Kundi hili linaloongozwa na Paraguay. Argentina ni wa tatu.

Nao Ecuador waliwafunga Chile 1-0 katika mechi ambayo Wachezaji watatu walipewa kadi nyekundu, wawili wa Ecuador na mmoja wa Chile

Sunday, 12 October 2008

MATOKEO: ULAYA

Bulgaria 0 v Italy 0,

England 5 v Kazakhstan 1,

Germany 2 v Russia 1,

Romania 2 v France 2,

Scotland 0 v Norway 0,

Sweden 0 v Portugal 0,

MAREKANI KUSINI:

Bolivia 3 v Peru 0,

Argentina 2 v Uruguay 1,

Colombia 0 v Paraguay 1,

AFRIKA:

Tanzania 3 v Cape Verde 1

Malawi 2 v Congo DRC 1

Namibia 4 v Zimbabwe 2

Ivory Coast 3 v Madagascar 0

Botswana 0 v Mozambique 1

Ghana 3 v Lesotho 0

Cameroon 5 v Mauritius 0

Tunisia 5 v Seychelles 0

Nigeria 4 v Sierra Leone 1

Senegal 1 v Gambia 1

Morocco 4 v Mauritania 1
Powered By Blogger