Friday 17 October 2008

ARSENAL NA LIVERPOOL WAKUMBWA NA MAJERUHI WA NYOTA WAO!!!

Baada ya Wachezaji Mastaa kwenda kutetea Nchi zao kwa zaidi ya siku 10 ili kuwania nafasi za kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI Klabu kadhaa za LIGI KUU UINGEREZA zimewapokea tena nyota wake kwa masikitiko makubwa baada ya baadhi kurudi wakiwa na majeruhi waliyopata kwenye mechi hizo za KOMBE LA DUNIA.
Klabu ya Liverpool imetangaza nyota wao Fernando Torres atakuwa nje kwa wiki 2 baada ya kuumia kwenye mechi ya Nchi yake Spain ilipocheza na Belgium na kushinda 2-1.
Torres alitolewa dakika ya 16 tu ya mchezo.
Hii inamaanisha Torres atakosa mechi dhidi ya Wigan wikiendi hii, ile na Atletico Madrid Jumatano na ya Chelsea wiki ijayo.

Nao Arsenal wametangaza Wachezaji wao watatu wamerudi majeruhi Klabuni hapo. Wachezaji hao ni Nahodha William Gallas, Bacary Sagna na Nicklas Bendtner.
Lakini Meneja Arsene Wenger amesema Mikael Silvestre aliehamia hapo toka Man U huenda akacheza mechi yake ya kwanza na pia Robin van Persie, Johan Djourou na Cesc Fabregas wamo kikosini ingawa taarifa za awali ziliripoti nao ni majeruhi.
Wikiendi hii Arsenal wako kwao Emirates Stadium kucheza na Everton kwenye LIGI KUU.

No comments:

Powered By Blogger