Saturday 25 September 2010

LIGI KUU: Leo siku ya Vigogo kutunguliwa!!
• Baada ya kuchapwa Chelsea nao Ze Gunners, Spurs chaliii!!!
• Liverpool chupuchupu!!!
Baada ya Chelsea kuchapwa 1-0 na Manchester City katika mechi ya Ligi Kuu iliyoanza mapema vikafuata vipigo kwa Vigogo wengine pale Arsenal walipopigwa 3-2 wakiwa nyumbani Emirates na West Bromwich na pia Tottenham kutunguliwa 1-0 huko Upton Park na West Ham.
Bao lililowapa ushindi West Ham dhidi ya Tottenham lilifungwa kwa kichwa na Frederic Piquionne kwenye dakika ya 29.
Nao Liverpool, wakiwa nyumbani Anfield, walitoka sare 2-2 na Sunderland lakini wageni hao watakuwa na kila sababu ya kulalamika bao la kwanza la Liverpool kwani lilifungwa katika utata mkubwa.
Sunderland walipewa frikiki na wakati kila mtu alijua Michael Turner alikuwa akimsogezea Kipa wake ili aipige frikiki hiyo Fernando Torres akaunasa mpira huo na kumpasia Kuyt aliefunga.
Darren Bent aliisawazishia Sunderland kwa penati na pia kufunga tena bao la pili lakini Steven Gerrard akarudisha bao na kuiokoa Liverpool toka kwenye kipigo.
Huko Emirates ndipo kulikuwa na kindumbwendumbwe baada ya wenyeji Arsenal kuendeshwa mchakamchaka kipindi cha pili na West Bromwich Albion kufuatia mechi kuwa 0-0 hadi mapumziko ingawa mambo yangekuwa mabaya kwa Arsenal laiti kama West Brom wangefunga penati kipindi hicho cha kwanza ambayo ilipigwa na Chris Brunt na Kipa Almunia kuiokoa.
Mnigeria Peter Odemwingie ndie alieipatia West Brom bao la kwanza, Gonzalo Jara akapiga la pili na Jerome Thomas akaunga bao la 3 kuwafanya West Brom wawe mbele 3-0.
Samir Nasri akafufua matumaini ya Arsenal alipopachika bao mbili na kufanya magoli yawe 3-2 lakini West Brom walisimama imara na kupata ushindi wao mnono wa pili kwa Wiki hii ambapo Jumatano waliifunga Manchester City 2-1 kwenye Carling Cup.
Vikosi vilivyoanza:
Arsenal: Almunia, Sagna, Squillaci, Koscielny, Clichy, Song, Diaby, Eboue, Nasri, Arshavin, Chamakh.
Akiba: Fabianski, Rosicky, Vela, Denilson, Wilshere, Djourou, Emmanuel-Thomas.
West Brom: Carson, Jara, Pablo, Olsson, Shorey, Mulumbu, Scharner, Brunt, Morrison, Thomas, Odemwingie.
Akiba: Myhill, Tchoyi, Reid, Dorrans, Zuiverloon, Fortune, Cox.
Refa: Michael Oliver
LIGI KUU ENGLAND:
MATOKEO:
Jumamosi, 25 Septemba 2010
Man City 1 Chelsea 0
Arsenal 2 West Brom 3
Birmingham 0 Wigan 0
Blackpool 1 Blackburn 2
Fulham 0 Everton 0
Liverpool 2 Sunderland 2
West Ham 1 Tottenham 0
RATIBA:
Jumapili, 26 Septemba 2010
[saa 8 mchana]
Bolton v Man Utd
[saa 10 dak 5 jioni]
Wolverhampton v Aston Villa
[saa 12 dak 10]
Newcastle v Stoke
Manchester City 1 Chelsea 0
Jana Roberto Mancini alimsifia Mtaliana mwenzake Carlo Ancelotti na Chelsea yake kuwa watachukua Ubingwa wa Ligi Kuu Msimu huu kirahisi mno lakini leo Mancini na Timu yake tajiri, Manchester City, katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu iliyoanza mapema, waliwatungua Chelsea bao 1-0 kwenye mechi iliyochezwa Uwanja wa City of Manchester.
Ni bao la kipindi cha pili la juhudi binafsi za Carlos Tevez ndilo liliwapa ushindi Man City na kuipa kilio cha kwanza Chelsea ambao walikuwa wameshinda mechi zao zote 5 za Ligi Msimu huu tena nyingine kwa lundo la magoli.
CARLING CUP: Droo ya Raundi ya 4 yafanyika!
• Mechi kuchezwa Wiki ya kuanzia Oktoba 20
Ipswich v Northampton
West Ham v Stoke
Man United v Wolves
Leicester v West Brom
Aston Villa v Burnley
Wigan v Swansea
Birmingham v Brentford
Newcastle v Arsenal
Redknapp aishambulia West Ham kumrubuni O’Hara
Leo Tottenham wataingia Uwanja wa Upton Park kucheza na wenyeji wao West Ham kwenye Ligi Kuu na tayari Meneja wa Tottenham Hotspur Harry Redknapp ameshachokoza vita kwa kuishambulia West Ham kwa kutaka kumrubuni Kiungo wao Jamie O'Hara kabla Msimu wa sasa kuanza.
Klabu za Ligi Kuu haziruhusiwi kuongea na Mchezaji wa Timu nyingine moja kwa moja kuhusu uhamisho na zinatakiwa kuongea na Klabu ya Mchezaji inaemtaka.
Redknapp amedai: “Walikuwa wakimpigia simu kila wakati. Lakini hili licha ya kuwa kinyume cha sheria hufanywa na kila mtu.”
Lampard bado sio fiti
Kiungo wa Chelsea Frank Lampard ataendelea kusota nje ya Uwanja baada ya kuchelewa kupona baada ya kufanyiwa opersheni ya ngiri na hivyo leo atalikosa pambano la Ligi Kuu dhidi ya Manchester City huko Uwanjani City of Manchester.
Lampard alifanyiwa upasuaji huo mwishoni mwa Agosti na ilitegemewa atakuwa nje kwa Wiki mbili lakini uponaji wake umekuwa wa pole pole na bado hata mazoezi hajaanza hivyo pia atazikosa mechi zijazo za UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya Marseille Jumanne Setemba 28 na lile la Ligi Kuu Oktoba 3 na Arsenal.
Katika mechi ya leo huko Manchester, Chelsea pia iatawakosa Salomon Kalou na Yossi Benayoun ambao ni majeruhi.
LIGI ZA ULAYA leo:
Jumamosi, Septemba 25
Calcio League A
AC Milan v Genoa
AS Roma v Inter Milan
La Liga
Sporting Gijon v Valencia
Levante v Real Madrid
Athletic de Bilbao v FC
Bundesliga
VfB Stuttgart v Bayer 04 Leverkusen
Schalke 04 v Borussia Mönchengladbach
Eintracht Frankfurt v FC Nurnberg
FC St. Pauli v BV Borussia Dortmund
Bayern Munich v FSV Mainz
Werder Bremen v Hamburger SV
Ufaransa Ligi 1
Nice v Stade Rennais FC
Montpellier HSC v Arles
Olympique de Marseille v FC Sochaux
Lorient v AS Monaco
Caen v FC Girondins de Bordeaux
Auxerre v AS Nancy Lorraine
Olympique Lyonnais v St.Etienne
CAS yamfungulia kwa muda Queiroz
• Rufaa yake kusikilizwa Novemba
Carlos Queiroz, Kocha wa Ureno alietimuliwa na kufungiwa Miezi 6 kwa kuwatukana Maafisa wa Kuthibiti Madawa yasiyo halali, amefunguliwa kwa muda na Mahamaka ya Usuluhisho kwenye Michezo, CAS [Court for Arbitration in Sports] na Mahakama hiyo itasikiliza Rufaa yake Mwezi Novemba.
Queiroz, ambae aliwahi kuwa Kocha wa Real Madrid na pia Msaidizi wa Sir Alex Ferguson Klabuni Manchester United, amefukuzwa Ukocha wa Ureno Mwezi huu na pia kufungiwa kuwa Kocha ndani na nje ya Ureno kwa Miezi 6 kuanzia Agosti.
Jumanne iliyopita Chama cha Soka cha Ureno, FPF, kilimteua Paulo Bento, aliekuwa Kocha wa zamani wa Sporting Lisbon, kuichukua Timu ya Taifa ya Ureno.
Licha ya kukata Rufaa kwa CAS, Queiroz pia amepeleka malalamiko yake kwa FIFA akidai Serikali ya Ureno iliipa presha FPF imfukuze Ukocha wa Ureno na endapo hilo litathibitishwa basi FPF itakuwa imekiuka taratibu za FIFA za kutoingiliwa na Serikali.

Friday 24 September 2010

LIGI KUU ENGLAND: RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi, 25 Septemba 2010
[saa 8 dak 45 mchana]
Man City v Chelsea
[saa 11 jioni]
Arsenal v West Brom
Birmingham v Wigan
Blackpool v Blackburn
Fulham v Everton
Liverpool v Sunderland
West Ham v Tottenham
Jumapili, 26 Septemba 2010
[saa 8 mchana]
Bolton v Man Utd
[saa 10 dak 5 jioni]
Wolverhampton v Aston Villa
[saa 12 dak 10]
Newcastle v Stoke
TATHMINI:
Man City v Chelsea
Vinara wa Ligi Kuu ambao pia ni Mabingwa Watetezi Chelsea wanasafiri hadi Uwanja wa City of Manchester kuikwaa ‘Timu Tajiri’ Manchester City, pambano ambalo wengi wanahisi huu ndio mtihani wa kwanza mgumu wa Chelsea baada ya kuanza na Timu ubwete kwenye Ligi Msimu huu.
Timu zote hizi mbili zilifungwa na kutupwa nje ya Carling Cup katika mechi zilizochezwa majuzi huku Chelsea wakibwagwa 4-3 na Newcastle na Man City kuchapwa 2-1 na West Bromwich.
Liverpool v Sunderland
Hii imekuwa Wiki ngumu kwa Liverpool kwani Jumapili iliyopita walichapwa 3-2 na Mahasimu wao Manchester United kwenye mechi ya Ligi Kuu na juzi wakatolewa nje ya Carling Cup na Timu ndogo ya Daraja la Ligi 2, Northampton, iliyowashinda kwa penati 4-2 baada ya mechi kwisha 2-2.
Sunderland, wiki iliyopita, walitoka sare 1-1 na Arsenal.
Arsenal v West Brom
Wakiwa kwao Uwanja wa Emirates, Arsenal wanaikaribisha West Brom Timu ambayo imepanda Daraja Msimu huu na inayojikongoja vizuri tu.
Wiki iliyopita Arsenal walipokwa tonge mdomoni pale Sunderland waliposawazisha dakika za majeruhi na kumfanya Bosi wao Arsene Wenger kuwaka na hatimaye kupigwa Faini na FA na kufungiwa mechi moja baada ya kumvaa Refa wa Akiba akilalamikia muda.
Wenger ameshatumikia adhabu yake ya mechi moja hapo juzi kwenye mechi ya Carling Cup walipoipiga Tottenham 4-1 baada ya muda wa nyongeza.
Mara ya mwisho kwa West Bromwich kutua Jijini London Msimu huu ilikuwa ni huko Stamford Bridge ambako walichapwa 6-0 na Timu yake ya zamani ya Bosi wao Robert Di Matteo, Chelsea.
West Ham v Tottenham
Hii ni dabi ya Timu za London Uwanjani Upton Park na West Ham, chini ya Meneja Avram Grant, bado wanasuasua kwenye Ligi Kuu wakiwa mkiani na wana pointi 1 tu baada ya mechi 5.
Tottenham wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi 8.
Fulham v Everton
Jumanne iliyopita, Everton walitolewa nje ya Carling Cup na Timu ya chini Brentford na kwenye Ligi Kuu Msimu huu, hawajashinda hata mechi moja na mechi hii itakayochezwa Craven Cottage, nyumbani kwa Fulham, ni ngumu kwao.
Msimu huu, katika mechi zao 5 za Ligi Kuu, Fulham hawajafungwa baada ya kushinda moja na kutoka sare 4 lakini kesho watakuwa na ubutu mbele baada ya Mafowadi wao wawili wa kutumainiwa, Moussa Dembele na Bobby Zamora, kuwa majeruhi.
Blackpool v Blackburn
Hii ni mechi ya pili ya nyumbani kwa Blackpool waliopanda Daraja Msimu huu na ambao wako nafasi ya 9 wakiwa na pointi 7 huku Blackburn wakiwa nafasi ya 14 wakiwa na pointi 5.
Birmingham v Wigan Athletic
Wigan, ambao wameonyesha udhaifu mkubwa kwenye difensi, wapo nafasi ya 18 wakiwa na pointi 4 na watakuwa wageni wa Birmigham ambao hawafungiki wakiwa nyumbani Uwanja wa Mtakatifu Andrew.
Bolton v Man United
Kawaida Manchester United hupata wakati mgumu wakiwa Uwanja wa Reebok, nyumbani kwa Bolton, lakini safari hii ndio kwanza wametoka kuwabonda Mahasimu wao Liverpool kwa bao 3-2 Jumapili iliyopita na Jumatano, Kikosi chao cha pili, kiliichapa Scunthorpe 5-2 kwenye Carling Cup.
Hivyo, Manchester United watakaza uzi ili washinde kabla hawajasafiri kwenda Spain kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI na Valencia siku ya Jumatano Septemba 29.
Wolves v Aston Villa
Hii ni dabi ya Timu za Katikati ya England, eneo la Midlands, na mechi ya kwanza kwa Meneja mpya wa Aston Villa, Gerard Houllier, ambae siku za nyuma alikuwa Liverpool.
Newcastle v Stoke City
Newcastle wapo nyumbani Uwanja wa St James Park na bado wana furaha ya kuichapa Chelsea 4-3 huko Stamford Bridge na kuitupa nje ya Carling Cup hivi juzi.
Newcastle wapo nafasi ya 6 kwenye Ligi na Stoke wapo nafasi ya 17.
Hargreaves aanza mazoezi na Man United
Owen Hargreaves, Miaka 29, ameanza tena mazoezi na Kikosi cha kwanza cha Manchester United baada ya kutoka matibabu huko Marekani ambako alifanyiwa operesheni ya magoti yake yote mawili Miaka miwili iliyopita lakini ikabidi Mwezi Julai arudishwe tena kwa Madaktari baada ya kusikia maumivu tena.
Meneja wa Man United, Sir Alex Ferguson, amethibitisha kurudi kwa Hargreaves na amesema: “Ameanza mazoezi na Kikosi cha Kwanza na alionekana safi sana. Hii ni silaha mpya kwangu.”
Fergie: ‘Rooney ameelemewa!’
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amekiri Wayne Rooney anaandamwa mno na Vyombo vya Habari na hilo limearhiri uchezaji wake.
Hivi karibuni Rooney alilipuliwa Magazetini kuwa alitembea na changudoa wakati mkewe akiwa mja mzito.
Msimu huu, Rooney amefunga bao moja tu kwa Timu yake na Ferguson hakumpanga kwenye mechi ya huko Goodison Park dhidi ya Tinu ya Rooney ya zamani Everton akihofia kusakamwa na Mashabiki.
Ferguson amesema Rooney amekuwa kwenye presha na hilo limemchosha akili.
Wakati huo huo, Ferguson amedai ratiba ya Msimu huu imeibeba Chelsea kwa kuanza na Timu ubwete.
Ferguson ametamka: “Wameanza vizuri mno. Pengine ratiba hiyo wameipanga wenyewe. Msimu uliokwisha walimaliza ratiba yao kwa kucheza na Timu dhaifu na kuzifunga lundo ya magoli na Msimu huu wameendelea hivyo hivyo!”
Arsenal yapata Faida
Klabu ya Arsenal imetangaza kuwa imepata faida ya Pauni Milioni 56 kwa Mwaka wa Fedha uliomalizika Mei 2010 na faida hiyo ina ongezeko la Pauni Milioni 10.5 toka ya Mwaka uliopita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Arsenal, Ivan Gazidis, amesema deni la Klabu hiyo limeshuka kutoka Pauni Milioni 297.7 hadi 135.6 kwa sababu waliuza Fleti zao 362 zilizokuwa Uwanja wao wa zamani wa Highbury na kulipa deni.

Thursday 23 September 2010

Wenger: ‘Ntaendelea Ukocha labda afya igome!’
• Adai Klabu Tajiri zinamkosesha Ubingwa!
WENGER ndani ya OLD TRAFFORD
Akiwa na umri wa Miaka 61 na tayari amesaini Mkataba mpya hadi Mwaka 2014, Arsene Wenger, ambae alitua Arsenal Septemba 1996, amesema ataendelea kuwa Kocha na kukuza vipaji vya Vijana hadi afya yake itakapogoma.
Wenger amebainisha kwamba bado yuko Arsenal kwa miaka mingi sasa si kwamba hatakiwi kwingine ila tu ni kwa sababu Arsenal imempa uhuru na haingiliwi chochote kwenye kazi yake.
Lakini amekiri kuwa siku moja atarudi kwao Ufaransa na ipo Klabu moja ambayo iko moyoni mwake na hiyo ni Strasbourg.
Kwa sasa, Wenger ana kibarua kikubwa cha kuifanya Arsenal ishinde Kombe lake la kwanza tangu 2005 waliponyakua FA Cup na pia kutwaa tena Ubingwa wa England tangu Msimu wa 2003/4 walipoutwaa Ubingwa bila kufungwa hata mechi moja.
Licha ya kutopata mafanikio yeyote kwa Miaka mitano, Wenger amejitetea: “Watu wanasema hatujashinda kitu kwa Miaka mitano sasa. Ni kweli, lakini siku zote tupo juu licha ya Klabu kuwa na matatizo. Arsenal wamejenga Uwanja mpya inabidi tulipe hilo, na tumejenga Kikosi kipya! Utasema nini ikiwa Manchester City iliyotumia Pauni Milioni 200 Msimu huu haishindi Kombe lolote?”
Wenger alisisitiza: “Sababu kubwa hatujashinda Kombe lolote kwa Miaka mitano ni kuwa tupo kwenye Ligi bora Duniani na tunacheza na Klabu tajiri!”
Bebe acheza, Fergie hakuwepo!!
BEBE
Jana kwenye Uwanja wa Glanford, Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana ya Chini ya Miaka 21 ya Ureno Bebe, alianza rasmi kuichezea Manchester United alipoingizwa dakika 15 za mwisho katika mechi dhidi ya Scunthorpe ya Raundi ya 3 ya Kombe la Carling ambayo Man United walishinda 5-2.
Licha ya Bebe kuwa mvuto, Wadau walishtushwa na kutokuwepo Uwanjani kwa Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambae alikuwa ameruka hadi Hispania kwenda kuitazama Valencia, wapinzani wa Man United Wiki ijayo kwenye mechi ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI itakayochezwa huko Spain, walipokuwa wakicheza nyumbani Estadio Mestalla mechi ya La Liga dhidi ya Atletico Madrid iliyoisha 1-1.
Bebe, Miaka 20, alionyesha cheche zake na wengi walisifia na kuridhika kuwa yapo matumaini makubwa katika uchezaji wake.
Meneja Msaidizi Mike Phelan alisema ameridhika na Bebe na hiyo ilikuwa nafasi muhimu kwake kupata uzoefu zaidi.
Nae Difenda Chipukizi, Chris Smalling aliecheza dabo Sentahafu na Rio Ferdinand katika mechi hiyo ya jana, alitamka: “Bebe amekuwa akijituma sana mazoezini. Amewatesa sana Mabeki wa Scunthorpe na natumaini atang’ara zaidi hapo mbele.”
FERGIE: 'Kuchagua Mchezaji Bora Utata!'
Andersson, Giggs & Rooney
Alex Ferguson amekiri ni vigumu kwake kuchagua nani ni Mchezaji Bora wa Manchester United katika kipindi chake cha Miaka 24 Klabuni hapo.
Ferguson, alieanza utawala wake Man United Mwaka 1986, allikuwa akihojiwa na Stesheni ya TV CNN, na alikiri ugumu wa swali hilo ingawa aliwataja Wachezaji 7 kuwa ni wazuri.
FERGIE
Ferguson aliiambia CNN kuwa Bryan Robson aliekuwa Nahodha wake na pia wa England alikuwa kipenzi cha Wachezaji wenzake na pia makini kwenye mbinu.
Pia alimtaja Roy Keane kama kiongozi bora na ni mpiganaji.
Ferguson alisema: “Paul Scholes ni Mchezaji wa kushangaza, siku zote ataonekana kama Mchezaji bora katika historia ya Man United. Alikuwepo Cantona, pia Giggs na Ronaldo, Rooney na wote hawa ni Wachezaji mahiri na ni ngumu sana kusema nani bora!”
FIFA yaonya dili za kura za Uenyeji Kombe la Dunia
FIFA imezionya Nchi zinazogombea Uenyeji wa Kombe la Dunia kwa Mwaka 2018 na 2022 kuwa ni marufuku kuingia dili na Nchi nyingine ili wapigiwe kura.
Onyo hilo la FIFA limekuja baada ya kuibuka fununu kuwa kuna Nchi moja huko Ulaya inayogombea Uenyeji wa Mwaka 2018 imefikia makubaliano na nyingine inayogombea 2022 ili wapigiane kura kusaidiana.
Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valcke amesema FIFA wana njia zao za kuchunguza mambo na kufuatilia nini kinafanywa na Wagombea Uenyeji wote.
Nchi za Ulaya zinazogombea Uenyeji wa Mwaka 2018 na 2022 ni England, Russia, Spain/Portugal, kwa pamoja, Netherlands/Belgium, kwa pamoja, na pia ipo USA inayowania nafasi hiyo.
Qatar, Australia, Japan na Korea Kusini zinagombea 2022 lakini ikiwa Nchi ya Ulaya itashinda Uenyeji wa 2018 Nchi nyingine za Ulaya zitaondolewa kwenye kinyang’anyiro cha 2022.
Kamati Kuu ya FIFA itatoa uamuzi wa nani watakuwa Wenyeji hapo Desemba 2.
Vela afungiwa Miezi 6
CARLOS VELA
Straika wa Mexico na pia Arsenal, Carlos Vela, pamoja na mwenzake Efrain Juárez wamefungiwa Miezi 6 na Chama cha Soka cha Mexico kwa kukiuka kanuni baada ya kuangusha bonge la Pati kwenye Hoteli iliyopiga kambi Timu ya Taifa ya Mexico mara baada ya kucheza mechi ya kirafiki na Colombia Mwezi uliopita.
Wachezaji wengine wa Mexico 11 waliadhibiwa kwa kupigwa Faini ya Pauni 2500 kila mmoja na hao ni Giovani dos Santos, Javier Hernández, Guillermo Ochoa, Francisco Rodriguez, Carlos Salcido, Andrés Guardado, Gerardo Torrado, Pablo Barrera, Rafael Márquez, Enrique Esqueda na Héctor Moreno.
Chelsea, Liverpool, Man City nje Carling!!!
• Hodgson aomba radhi!
Meneja wa Liverpool Roy Hodgson amelazimika kuomba radhi kufuatia Timu yake kuadhiriwa Uwanjani kwao Anfield na Timu ya Daraja la chini Northampton kwa kutolewa nje ya Carling Cup ilipopigwa na 4-2 kwa mikwaju ya penati baada ya kwenda sare 2-2 katika muda wa kawaida.
Northampton wapo Daraja la Ligi 2 ambayo ni Madaraja matatu chini ya Ligi Kuu.
Hodgson amesema: “Tumecheza na Timu ya chini na usiposhinda hilo ni jambo baya.”
Hodgson, ambae ametokea Fulham kumbadili Rafa Benitez alietimkia Inter Milan, amekiri kazi yake hapo Anfield ni ngumu na ameanza kwa mguu mbaya.
Mpaka sasa Liverpool wapo chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu na wana pointi 5 tu kwa mechi 5 na walifungwa mechi yao ya mwisho ya Ligi na Manchester United kwa bao 3-2.
Wikiendi ijayo watakumbana na Sunderland kwenye Ligi Uwanjani Anfield.
Si Liverpool pekee waliokiona cha mtema kuni kwenye mechi za Raundi ya 3 ya Carling hapo jana kwani Chelsea na Manchester City nao wamebwagwa nje.
Chelsea wamefungwa 4-3 na Newcastle Uwanjani kwao Stamford Bridge na Manchester City walichapwa 2-1 na West Bromwich.
Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo la Carling, Manchester United, waliangusha kichapo kwa Scunthorpe cha mabao 5-2.
CARLING CUP: Chelsea, Man City, Rovers  NJEEEEEE!!!!!!!
Jumatano, Septemba 22
Chelsea 3 Newcastle United 4
Aston Villa 3 Blackburn Rovers 1
Scunthorpe United 2 Manchester United 5
Wigan Athletic 2 Preston North End 1
Liverpool 1 Northampton Town 1] [ZIMEONGEZWA DAKIKA 30 NYONGEZA
West Bromwich Albion 2 Manchester City 1

Wednesday 22 September 2010

Spurs 1 Ze Gunners 4
• Redknapp: ‘Nasri alijiangusha kupata penati!’
Meneja wa Tottenham Hotspur Harry Redknapp amemshambulia Mchezaji wa Arsenal Samir Nasri kwa kujiangusha makusudi ili kupata penati ambayo alliifunga mwenyewe dakika za nyongeza na kuifanya Arsenal ipate bao la pili na hivyo kuelekea kwenye ushindi wa mabao 4-1 hapo jana huko White Hart Lane kwenye mechi ya Raundi ya 3 ya Kombe la Carling.
Redknapp ametamka: “Haikuwa penati! Alijiangusha!”
Katika mechi hiyo, hadi dakika 90 ngoma ilikuwa 1-1 na ndipo zikaongezwa dakika 30 na Arsenal kupata penati mbili zilizofungwa na Samir Nasri na bao la 4 kupachikwa na Arshavin.
CARLING CUP: RAUNDI YA TATU
MATOKEO:
Jumanne, Septemba 21
Brentford 1 Everton 1 [penati, Brentford 4 Everton 3]
Portsmouth 1 Leicester City 2
Stoke City 2 Fulham 1
Tottenham Hotspur 1 Arsenal 4
Millwall 1 Ipswich Town 2
Wolverhampton 4 Notts County 2
Burnley 1 Bolton Wanderers 0
Birmingham City 3 MK Dons 1
Sunderland 1 West Ham United 2
Peterborough United 1 Swansea City 3
RATIBA:
Jumatano, Septemba 22
[Zitaanza Saa 3 dak 45 usiku , saa za bongo]
Chelsea v Newcastle United
Aston Villa v Blackburn Rovers
Scunthorpe United v Manchester United
Wigan Athletic v Preston North End
Liverpool v Northampton Town [saa 4 usiku]
West Bromwich Albion v Manchester City [saa 4 usiku]
Bramble abambwa kwa tuhuma za kubaka
Difenda wa Sunderland, Titus Bramble, amekamatwa kwa tuhuma za kubaka Mwanamke kwenye Hoteli huko Jijini Newcastle.
Bramble na Nduguye, Tesfaye Bramble, walikamatwa leo asubuhi na bado wanahojiwa na Polisi.
Klabu ya Sunderland imekataa kuzungumza lolote kuhusu tukio hilo.
Kuszczak atafakari kuhama Man United
Tomasz Kuszczak amekiri kuwa huenda akalazimika kuihama Manchester United ili aende Timu nyingine kupata fursa ya kucheza kila siku.
Kipa huyo kutoka Poland, aliehamia Man United kutoka West Bromwich Mwaka 2006 na kucheza Mechi 52 tu toka wakati huo, ameshindwa kumng’oa Mkongwe Edwin van der Saar kama Kipa nambari wani.
Lakini, wiki iliyopita aliidakia Man United kwenye sare ya 0-0 na Rangers kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI na leo anategemewa kuwa golini kwenye mechi ya Carling Cup na Scunthorpe.
Hivi karibuni, Kuszczak alimshuhudia Kipa mwenzake Ben Foster akiihama Man United kwenda Birmingham City ambako amekuwa Kipa Namba moja na ametamka: “Nimeuelewa uamuzi wa Foster. Alihama kwa sababu anataka kucheza kila siku na kuichezea England. Lakini, hata mie kama sichezeshwi sana nitamwiga Foster. Miaka inaenda na Mwakani natimiza Miaka 29. Nataka kucheza.”

Tuesday 21 September 2010

Agger aruka hana bifu na Meneja wake!
• Kuyt kurejea mapema baada ya kupona!
Beki wa Liverpool Daniel Agger amezikana taarifa kuwa alimpinga Meneja wake Roy Hodgson kuhusu mbinu anazotumia ambazo huwataka Mabeki kutotuliza mipira nyuma na kupiga mbele ndefu haraka.
Habari za kumpinga Hodgson ziliibuka Nchini kwa Agger huko Denmark lakini Beki huyo wa Kimataifa mwenye Miaka 25 amezikana na kusema si za kwake.
Ilidaiwa kuwa Agger alisema yeye ni Mchezaji aliezoea kutuliza mpira chini na kuanza kwa pasi na si kuosha mipira kwa kubutua mipira mirefu mbele kama wanavyolazimishwa na Meneja wao Hodgson.
Wakati huo huo, Liverpool wamepata habari za faraja kubwa kwao baada ya Fowadi wao mpiganaji mkubwa uwanjani Dirk Kuyt kuanza tena mazoezi baada ya kuumia bega akiwa na Timu ya Taifa ya Uholanzi.
Kuyt amekuwa nje ya uwanja kwa Wiki mbili sasa na ilihofiwa atakuwa nje kwa muda mrefu uliokadiriwa kuwa hadi Wiki 5.
Hodgson amesema Kuyt huenda akacheza Wikiendi hii kwenye mechi na Sunderland ya Ligi Kuu au ile inayofuata ya EUROPA LIGI Wiki ijayo huko Uholanzi dhidi ya Klabu ya zamani ya Kuyt Utrecht.
Bebe kuwemo Kikosi cha Man United Carling Cup

Bebe, Chicharito, Sir Alex na Smalling
 Mchezaji mpya wa Manchester United Bebe ameingizwa kwenye Kikosi kitakachocheza na Scunthorpe hapo kesho kwenye Raundi ya 3 ya Carling Cup.
Bebe, Miaka 20, amehamia Man United kutoka Vitoria Guimaraes ya Ureno lakini tangu atue hapo hajacheza mechi yeyote ya Kikosi cha Kwanza mbali ya kucheza mechi moja tu ya Kikosi cha Rizevu.
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amethibitisha Kikosi kitakachocheza kesho kitakuwa mchanganyiko wa Chipukizi na wale wazoefu.
Ferguson amesema: “Tuna Wachezaji wengi na wengi wanahitaji mechi. Bebe na Macheda kesho watashiriki.”
Mwenyewe Bebe, akijibu tuhuma za baadhi ya Magazeti kuwa hastahili kuwemo Man United, ameomba Wadau kuwa wavumilivu na wataona cheche zake.
Bebe ametamka: “Nitakuwa moto kwa Man United. Lazima niwe fiti kwani soka la England ni tofauti. Sir Alex amesema anaridhishwa na mimi lakini nifanye mazoezi zaidi.”
Bebe pia ametoa shukran zake kwa Wachezaji wenzake kwa kumsaidia kuizoea Man United hasa Mapacha, Rafael na Fabio, Nani na Anderson kwa vile wanaongea nae Kireno.
Wenger akiri makosa, apigwa Faini na Kifungo mechi 1
Arsene Wenger amekubali makosa yake aliyoshitakiwa na FA baada ya kumvaa Refa wa Akiba Siku ya Jumamosi kwenye mechi ya Ligi Kuu mara baada ya Sunderland kusawazisha bao dakika za majeruhi na Wenger kulalamikia muda umekwisha.
Kufuatia kukiri makosa hayo, Wenger sasa atalipa Faini ya Pauni 8,000 na kuikosa mechi ya leo ya Carling Cup ambapo Arsenal watakuwa wageni wa Tottenham huko White Hart Lane.
Kwa kukiri haraka kosa lake, Wenger amepata ile adhabu ya kawaida ambayo hupewa kila Mtu anaekiri mara baada ya kushitakiwa na hivyo kukwepa kesi kwenda kwenye Kamisheni Huru ya Sheria ambayo isingekaa haraka na kungekuwapo uwezekano wa Wenger kuadhibiwa na kuikosa BIGI MECHI hapo Oktoba 3 huko Stamford Bridge ambako Arsenal wataenda kuivaa Chelsea.
Hii ni mara ya kwanza kwa Wenger kufungiwa mechi tangu ahamie Arsenal Mwaka 1996 ingawa 2001alifungiwa Mechi 12 baada ya kumvaa Refa Msaidizi walipofungwa na Sunderland lakini adhabu hiyo ilifutwa baada ya kukata rufaa.

Monday 20 September 2010

Fabregas nje Wiki 2
Arsenal watafurahi baada ya taarifa kuwa Nahodha wao Cesc Fabregas hakuumia vibaya kama ilivyoogopwa alipotolewa baada ya nusu saa ya mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu walipotoka sare 1-1 na Sunderland.
Fabregas ndie aliewapatia Arsenal bao kwenye mechi hiyo na baada ya hapo akaonekana kuchechemea lakini ripoti za Madaktari zimesema atakuwa nje kwa Wiki mbili akiuguza musuli za paja na hivyo kuna uwezekano mkubwa akacheza BIGI MECHI hapo Oktoba 3 dhidi ya Chelsea huko Stamford Bridge.
Wenger afunguliwa mashitaka na FA
Arsene Wenger amefunguliwa mashitaka na FA kwa kutumia lugha chafu na utovu wa nidhamu kufuatia vitendo vyake kwa Marefa wa mechi ya Ligi Kuu Jumamosi iliyopita walipotoka sare 1-1 na Sunderland.
Wenger alionekana akimvaa Refa wa Akiba Martin Atkinson mara baada ya Darren Bent wa Sunderland kufunga goli la kusawazisha dakika za majeruhi.
Lakini, Wenger baadae alikana kumsakama Atkinson na kusema: “Sikulalamika kwa Mtu. Katika zile dakika 4 za nyongeza kulikuwa hamna kitu cha kufanya muda uongezwe zaidi ya hapo. Lakini najua Refa anaweza kuongeza muda zaidi ya dakika 4.”
Kufuatana na kanuni mpya za FA za kuharakisha kesi, Wenger amepewa hadi Alhamisi ili kujibu mashitaka hayo na atapewa Faini ya Pauni 8,000 na kufungiwa mechi moja ikiwa atakubali makosa lakini akikana shauri lake litapelekwa kwa Kamati ya Sheria ambayo inaweza ikatoa adhabu kali zaidi.
Mancini kumruhusu Given kung’oka
Bosi wa Manchester City Roberto Mancini amesema atamruhusu Kipa Shay Given kuhama Dirisha la uhamisho likifunguliwa Mwezi Januari Mwakani.
Given amepoteza nafasi yake kama Kipa nambari wani na imechukuliwa na Joe Hart ambae ndie amedaka mechi zote 8 za Man City Msimu huu.
Mancini amesema: “Nimemwambia anaweza kubaki lakini naheshimu amuse wake akiamua kuondoka.”
Shay Given ameshatamka hawezi kubaki Man City ikiwa hatapangwa.
Gerrard ajutia kukosa pointi Old Trafford
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, anahisi walistahili kuondoka Old Trafford hapo jana angalau na pointi moja baada ya kutoka nyuma wakiwa bao 2-0 na kuifanya mechi iwe sare 2-2 lakini Shujaa wa Manchester United Dimitar Berbatov akawaua kwa bao lake la 3.
Gerrard amesema: “Ukiwa Old Trafford na uko nyuma 2-0 kisha ukasawazisha na kuifanya mechi iwe 2-2 ni wazi unapata moyo mpya na unastahili kupata angalau pointi moja!”
Gerrard alisikitika na kipigo cha 3-2 toka kwa Mahasimu wao wakubwa lakini alitamka: “Ni Berbatov ndie aliekuwa tofauti hapo jana. Na goli lake la pili ni la Kimataifa!”
Gerrard ndie alieifungia Liverpool bao zao mbili, moja kwa penati na la pili kwa frikiki.
CARLING CUP: Kunguruma kesho na Jumatano
Timu Vigogo zinajimwaga Uwanjani hapo kesho na Jumatano kwenye Raundi ya 3 ya Kombe la Carling na Bingwa Mtetezi Manchester United atacheza ugenini na Timu ya Daraja la chini Scunthorpe United.
Katika mechi za Timu za Ligi Kuu pekee, Chelsea atakuwa nyumbani kucheza na Newcastle United, Stoke City na Fulham, Aston Villa v Blackburn, Sunderland v West Ham, West Brom v Manchester City na Timu pinzani za Kaskazini ya London, Tottenham na Arsenal zitakutana White Hart Lane kwenye dabi yao.
Jumanne, Septemba 21
[Saa 3 dak 45 usiku, saa za bongo labda itajwe tofauti]
Brentford v Everton
Portsmouth v Leicester City
Stoke City v Fulham
Tottenham Hotspur v Arsenal
Millwall v Ipswich Town
Wolverhampton Wanderers v Notts County
Burnley v Bolton Wanderers
Birmingham City v MK Dons
Sunderland v West Ham United
Peterborough United v Swansea City
Jumatano, Septemba 22
Chelsea v Newcastle United
Aston Villa v Blackburn Rovers
Scunthorpe United v Manchester United
Wigan Athletic v Preston North End
Liverpool v Northampton Town [saa 4 usiku]
West Bromwich Albion v Manchester City [saa 4 usiku]

Sunday 19 September 2010

LIGI KUU ENGLAND: Mechi zijazo
Jumamosi, 25 Septemba 2010
[saa 8 dak 45 mchana]
Man City v Chelsea
[saa 11 jioni]
Arsenal v West Brom
Birmingham v Wigan
Blackpool v Blackburn
Fulham v Everton
Liverpool v Sunderland
West Ham v Tottenham
Jumapili, 26 Septemba 2010
[saa 8 mchana]
Bolton v Man Utd
[saa 10 dak 5 jioni]
Wolverhampton v Aston Villa
[saa 12 dak 10]
Newcastle v Stoke
Fergie: ‘Siku zote sikuwa na wasiwasi na Berbatov!’
SIR ALEX FERGUSON
Sir Alex Ferguson amesisitiza hakuwa na wasiwasi na Dimitar Berbatov na alijua fika Mchezaji huyo ni kipaji na hatari mno na leo ameifikisha patamu baada ya kuwaua wapinzani wao wakubwa Liverpool kwa kufunga bao zote 3 katika ushindi wa 3-2 kwenye mechi ya Ligi Kuu Uwanjani Old Trafford.
Tangu ahamie Manchester United kutoka Tottenham Mwaka 2008 kwa dau kubwa, Berbatov amekuwa akipondwa kwa uchezaji wake lakini Msimu huu ameanza kwa moto mkali kwa kufunga bao 6 katika mechi 5 za Ligi Kuu za Msimu huu.
Ferguson ametamka: “Magazeti yalimshambulia sana Msimu uliopita na hilo hutokea sisi tukinunua Mchezaji kwa bei mbaya na hafungi hetitriki kila mechi! Sikuwa na wasiwasi na yeye, na leo mmeona tena kipaji chake!”
Ferguson akiizungumzia gemu ya leo alisema walipokuwa 2-0 mbele alijiambia mwenyewe hii leo goli 10 na mara ikawa 2-2 lakini mwishowe ulikuwa ushindi mtamu.
Ferguson alitamka: “Hawakucheza lolote Liverpool na walimtegemea Mshika Kibendera awaokoe [akimaanisha goli la kwanza la penalti ambalo Refa Howard Webb alipewa ishara na Mshika Kibendera kutoa penalti]. Van der Sar hakuokoa hata mpira mmoja na Scholes alitawala Kiungo! Tulikuwa moto mbele hasa Berbatov na Nani, hatukustahili kutoshinda mechi hii!”
Chelsea 4 Blackpool 0
Mabingwa Watetezi Chelsea leo tena wameendeleza wimbi lao la ushindi kwa kuifunga Blackpool mabao 4-0 Uwanjani Stamford Bridge huu ukiwa ushindi wao wa 5 mfululizo tangu Msimu mpya wa Ligi Kuu uanze na kuwafanya wabaki kileleni kwa pointi 4 mbele dhidi ya Arsenal na Man United zinazofungana pointi kwa kuwa na pointi 11.
Leo mabao yote ya Chelsea yalifungwa Kipindi cha Kwanza wafungaji wakiwa Kalou, Malouda, bao mbili, na Drogba.
Mechi inayofuata kwa Chelsea kwenye Ligi Kuu ni ile ya ugenini Jumamosi ijayo huko City of Manchester Stadium watakapokumbana na ‘Timu Tajiri’ Manchester City na safari hii mechi hii ikiwa tofauti kwa Mabingwa hao kwa kuonekana kidogo ngumu baada ya kuanza Ligi Kuu na kuziponda Timu ubwete kama vile West Bromwich Albion, Wigan Athletic, Stoke City, West Ham United na leo Blackpool.
Vikosi vilivyoanza:
Chelsea: Cech, Ferreira, Ivanovic, Alex, Cole, Essien, Mikel, Ramires, Kalou, Drogba, Malouda.
Akiba: Turnbull, Benayoun, Zhirkov, Sturridge, Anelka, Bruma, Kakuta.
Blackpool: Gilks, Eardley, Evatt, Baptiste, Keinan, Crainey, Grandin, Adam, Vaughan, Varney, Campbell.
Akiba: Halstead, Southern, Harewood, Ormerod, Taylor-Fletcher, Cathcart, Carney.
Refa: Mark Clattenburg
Wigan 0 Man City 2
Carlos Tevez na Yaya Toure leo wamewapa ushindi Manchester City walipofunga bao mbili katika mechi ya Ligi Kuu ambayo Man City walishinda 2-0 ugenini.
Ushindi huu umeiweka Man City nafasi ya 4 wakiwa na pointi 8 kwa mechi 5.
Juu yao wako, jirani zao Man United wenye pointi 11 sawa na Arsenal.
Chelsea ndie wanaongoza wakiwa na pointi 15 kwa kushinda mechi zao zote 5 za Ligi Kuu.
Vikosi vilivyoanza:
Wigan: Al Habsi, Boyce, Gohouri, Alcaraz, Figueroa, N'Zogbia, Thomas, McCarthy, Diame, Rodallega, Di Santo.
Akiba: Kirkland, Watson, Boselli, Moses, Steven Caldwell, Gomez, Stam.
Man City: Hart, Richards, Kompany, Toure, Zabaleta, De Jong, Toure Yaya, Barry, Silva, Milner, Tevez.
Akiba: Given, Wright-Phillips, Adam Johnson, Santa Cruz, Vieira, Jo, Boyata.
Refa: Lee Probert
Berbatov Shujaa Old Trafford!!!
• Apiga Hetitriki!!!!!
• Man United 3 Liverpool 2
SHUJAA BERBATOV
Dimitar Berbatov amekuwa akiandamwa na wengi tangu atue Old Trafford akitokea Tottenham Hotspurs kwa uchezaji wake wa kupooza na kuua mipira ya kasi, ingawa siku zote Meneja wake Sir Alex Ferguson amekuwa akisistiza huyo ni kipaji cha hali ya juu, na leo kwenye BIGI MECHI ya Uingereza kati ya Mahasimu wa karne na karne, Manchester United na Liverpool, Berbatov amethibitisha yeye ni kiboko pale alipowapa raha Mashetani Wekundu kwa kupachika bao zote 3 huku bao zote zikiwa ni tamu na za ufundi wa hali ya juu.
Hii ni mechi ambayo Manchester United waliitawala na walistahili ushindi lakini nusura waimwage kama walivyofanya kwenye mechi zao mbili za Ligi Kuu zilizopita walipotoka sare na Fulham na Everton kwani leo waliongoza 2-0 na kuwaruhusu Liverpool kurudisha na kufanya mechi iwe 2-2 lakini leo Shujaa ni Berbatov ambae alifunga bao lake la 3 na la ushindi kwa Man United.
Berbatov alifunga bao la kwanza dakika ya 42 kwa kichwa kufuatia kona ya Ryan Giggs na hadi mapumziko Man United 1 Liverpool 0.
Ndipo kwenye dakika ya 52 pande refu la Darren Fletcher kumlenga Nani kwenye winga ya kulia na krosi ya Nani golini ilimkuta Berbatov kwenye boksi huku akiwa amelipa mgongo goli, akaukontroli mpira kwa paja la mguu mmoja na kuachia tiktaka iliyogonga posti ya juu na kujikita wavuni.
Hakika hilo ni miongoni mwa Magoli ya Msimu kama si Goli la Msimu.
Lakini Liverpool wakafufuka na ndani ya dakika 6, wakafunga bao la kwanza kwa penalti baada ya Torres kuangushwa na Johny Evans na la pili kwa frikiki, zote zikipigwa na Nahodha wao Steven Gerrard.
Hizo zilikuwa ni dakika ya 64 na 70.
Lakini Shujaa ni Dimitar Berbatov.
Zikiwa zimebaki dakika 6 mechi kwisha, krosi ya John O’Shea iliunganishwa kwa kichwa na Berbatov na kuwainua Manchester United kwa furaha.
Vikosi vilivyoanza:
Man United: Van der Sar, O'Shea, Vidic, Jonny Evans, Evra, Nani, Fletcher, Scholes, Giggs, Berbatov, Rooney.
Akiba: Kuszczak, Brown, Owen, Anderson, Smalling, Macheda, Gibson.
Liverpool: Reina, Johnson, Carragher, Skrtel, Konchesky, Meireles, Poulsen, Maxi, Gerrard, Cole, Torres.
Akiba: Jones, Agger, Jovanovic, Kyrgiakos, Babel, Lucas, Ngog.
Refa: Howard Webb
Wenger awaka, pengine kupigwa Rungu na FA!!
Arsene Wenger alilipuka mara baada ya Darren Bent kusawazisha bao kwenye dakika za majeruhi na kuifanya mechi ya Ligi Kuu hapo jana kati ya Sunderland na Arsenal kwisha 1-1.
Goli la Bent liliingia kwenye dakika ya 95 baada ya bango la muda wa nyongeza kuonyeshwa dakika 4 na Wenger amedai: “Ukiwa na saa unaikontroli! Ni kitu rahisi.”
Wenger alionekana akimvaa Refa wa Akiba Martin Atkinson mara baada ya Bent kufunga goli hilo na huenda hilo likamtia matatani na FA.
Lakini, Wenger baadae alikana kumsakama Atkinson na kusema: “Sikulalamika kwa Mtu. Katika zile dakika 4 za nyongeza kulikuwa hamna kitu cha kufanya muda uongezwe zaidi ya hapo. Lakini najua Refa anaweza kuongeza muda zaidi ya dakika 4.”
Katika mechi ya jana, Arsenal walipata bao la bahati baada ya shuti la kuosha mbele la Anton Ferdinand kuzuiwa na Cesc Fabregas na mpira kurudi golini na kutinga.
Arsenal wangeweza kufunga bao la pili lakini penalti iliyopigwa na Tomas Rosicky ilipaa juu na hilo lilimkera Wenger ambae alitamka: “Sikudhani kama Rosicky angepiga, nilijua ni Samir Nasri.”
Vile vile, Wenger alilalamika kuhusu kupewa Kadi Nyekundu Mchezaji wake Song na amedai Kadi ya Njano ya kwanza aliyopewa ilikuwa kali mno na ya Pili ilikuwa pia haistahili.
Powered By Blogger