Thursday 23 September 2010

Bebe acheza, Fergie hakuwepo!!
BEBE
Jana kwenye Uwanja wa Glanford, Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana ya Chini ya Miaka 21 ya Ureno Bebe, alianza rasmi kuichezea Manchester United alipoingizwa dakika 15 za mwisho katika mechi dhidi ya Scunthorpe ya Raundi ya 3 ya Kombe la Carling ambayo Man United walishinda 5-2.
Licha ya Bebe kuwa mvuto, Wadau walishtushwa na kutokuwepo Uwanjani kwa Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambae alikuwa ameruka hadi Hispania kwenda kuitazama Valencia, wapinzani wa Man United Wiki ijayo kwenye mechi ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI itakayochezwa huko Spain, walipokuwa wakicheza nyumbani Estadio Mestalla mechi ya La Liga dhidi ya Atletico Madrid iliyoisha 1-1.
Bebe, Miaka 20, alionyesha cheche zake na wengi walisifia na kuridhika kuwa yapo matumaini makubwa katika uchezaji wake.
Meneja Msaidizi Mike Phelan alisema ameridhika na Bebe na hiyo ilikuwa nafasi muhimu kwake kupata uzoefu zaidi.
Nae Difenda Chipukizi, Chris Smalling aliecheza dabo Sentahafu na Rio Ferdinand katika mechi hiyo ya jana, alitamka: “Bebe amekuwa akijituma sana mazoezini. Amewatesa sana Mabeki wa Scunthorpe na natumaini atang’ara zaidi hapo mbele.”

No comments:

Powered By Blogger