Wednesday, 22 September 2010

Spurs 1 Ze Gunners 4
• Redknapp: ‘Nasri alijiangusha kupata penati!’
Meneja wa Tottenham Hotspur Harry Redknapp amemshambulia Mchezaji wa Arsenal Samir Nasri kwa kujiangusha makusudi ili kupata penati ambayo alliifunga mwenyewe dakika za nyongeza na kuifanya Arsenal ipate bao la pili na hivyo kuelekea kwenye ushindi wa mabao 4-1 hapo jana huko White Hart Lane kwenye mechi ya Raundi ya 3 ya Kombe la Carling.
Redknapp ametamka: “Haikuwa penati! Alijiangusha!”
Katika mechi hiyo, hadi dakika 90 ngoma ilikuwa 1-1 na ndipo zikaongezwa dakika 30 na Arsenal kupata penati mbili zilizofungwa na Samir Nasri na bao la 4 kupachikwa na Arshavin.
CARLING CUP: RAUNDI YA TATU
MATOKEO:
Jumanne, Septemba 21
Brentford 1 Everton 1 [penati, Brentford 4 Everton 3]
Portsmouth 1 Leicester City 2
Stoke City 2 Fulham 1
Tottenham Hotspur 1 Arsenal 4
Millwall 1 Ipswich Town 2
Wolverhampton 4 Notts County 2
Burnley 1 Bolton Wanderers 0
Birmingham City 3 MK Dons 1
Sunderland 1 West Ham United 2
Peterborough United 1 Swansea City 3
RATIBA:
Jumatano, Septemba 22
[Zitaanza Saa 3 dak 45 usiku , saa za bongo]
Chelsea v Newcastle United
Aston Villa v Blackburn Rovers
Scunthorpe United v Manchester United
Wigan Athletic v Preston North End
Liverpool v Northampton Town [saa 4 usiku]
West Bromwich Albion v Manchester City [saa 4 usiku]
Bramble abambwa kwa tuhuma za kubaka
Difenda wa Sunderland, Titus Bramble, amekamatwa kwa tuhuma za kubaka Mwanamke kwenye Hoteli huko Jijini Newcastle.
Bramble na Nduguye, Tesfaye Bramble, walikamatwa leo asubuhi na bado wanahojiwa na Polisi.
Klabu ya Sunderland imekataa kuzungumza lolote kuhusu tukio hilo.
Kuszczak atafakari kuhama Man United
Tomasz Kuszczak amekiri kuwa huenda akalazimika kuihama Manchester United ili aende Timu nyingine kupata fursa ya kucheza kila siku.
Kipa huyo kutoka Poland, aliehamia Man United kutoka West Bromwich Mwaka 2006 na kucheza Mechi 52 tu toka wakati huo, ameshindwa kumng’oa Mkongwe Edwin van der Saar kama Kipa nambari wani.
Lakini, wiki iliyopita aliidakia Man United kwenye sare ya 0-0 na Rangers kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI na leo anategemewa kuwa golini kwenye mechi ya Carling Cup na Scunthorpe.
Hivi karibuni, Kuszczak alimshuhudia Kipa mwenzake Ben Foster akiihama Man United kwenda Birmingham City ambako amekuwa Kipa Namba moja na ametamka: “Nimeuelewa uamuzi wa Foster. Alihama kwa sababu anataka kucheza kila siku na kuichezea England. Lakini, hata mie kama sichezeshwi sana nitamwiga Foster. Miaka inaenda na Mwakani natimiza Miaka 29. Nataka kucheza.”

No comments:

Powered By Blogger