Saturday 25 September 2010

Redknapp aishambulia West Ham kumrubuni O’Hara
Leo Tottenham wataingia Uwanja wa Upton Park kucheza na wenyeji wao West Ham kwenye Ligi Kuu na tayari Meneja wa Tottenham Hotspur Harry Redknapp ameshachokoza vita kwa kuishambulia West Ham kwa kutaka kumrubuni Kiungo wao Jamie O'Hara kabla Msimu wa sasa kuanza.
Klabu za Ligi Kuu haziruhusiwi kuongea na Mchezaji wa Timu nyingine moja kwa moja kuhusu uhamisho na zinatakiwa kuongea na Klabu ya Mchezaji inaemtaka.
Redknapp amedai: “Walikuwa wakimpigia simu kila wakati. Lakini hili licha ya kuwa kinyume cha sheria hufanywa na kila mtu.”
Lampard bado sio fiti
Kiungo wa Chelsea Frank Lampard ataendelea kusota nje ya Uwanja baada ya kuchelewa kupona baada ya kufanyiwa opersheni ya ngiri na hivyo leo atalikosa pambano la Ligi Kuu dhidi ya Manchester City huko Uwanjani City of Manchester.
Lampard alifanyiwa upasuaji huo mwishoni mwa Agosti na ilitegemewa atakuwa nje kwa Wiki mbili lakini uponaji wake umekuwa wa pole pole na bado hata mazoezi hajaanza hivyo pia atazikosa mechi zijazo za UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya Marseille Jumanne Setemba 28 na lile la Ligi Kuu Oktoba 3 na Arsenal.
Katika mechi ya leo huko Manchester, Chelsea pia iatawakosa Salomon Kalou na Yossi Benayoun ambao ni majeruhi.

No comments:

Powered By Blogger