Saturday 11 September 2010

CHEKI: www.sokainbonbo.com

Neville: ‘Naichukia zaidi Man City kupita Liverpool!’
Beki wa Manchester United, Gary Neville, ameiponda Manchester City na pia kudai kuwa, kwake yeye, Liverpool ni bora kupita Man City.
Msimu uliokwisha, Neville alizua mzozo pale alipomponda Carlos Tevez, Mchezaji aliewahi kuichezea Man United na kisha kuhamia Man City, na pia alipoenda kushangilia ushindi wa Man United mbele ya Mashabiki wa Man City waliokuwepo Old Trafford kuitazama mechi ya Man United v Man City.
Neville ametamka: “Nawaheshimu Liverpool kama Klabu yenye utamaduni mzuri na historia ndefu na si Klabu iliyoibuka hivi karibuni na kutumia mifedha kiwehu!”
Walcott nje Wiki 6
Winga wa Arsenal Theo Walcott atakuwa nje kwa Wiki 6 akiuguza enka yake aliyoumia akiichezea England dhidi ya Uswisi Jumanne iliyopita.
Habari hizi zimethibitishwa na Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema Walcott atakuwa nje Wiki 4 hadi 6.
Msimu huu Walcott ameanza kwa moto mkali na kufunga bao 4 katika mechi 4 alizochezea Arsenal.
Winga huyo atazikosa mechi dhidi ya Bolton, Sunderland, West Bromwich na mechi mbili za UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya Braga na Partizan Belgrade.
Rufaa ya Evra yatupwa!
Nahodha wa Ufaransa, Patrice Evra, ataendelea na kifungo chake cha mechi 5 alichopewa na FFF, Chama cha Soka Ufaransa, kwa kuongoza mgomo wa Wachezaji huko Afrika Kusini Uafarnsa ilipokuwa kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Wachezaji wa Ufaransa waligomea mazoezi baada ya mwenzao Nicolas Anelka kufukuzwa baada ya kugombana na Kocha Raymond Domenech.
Pamoja na Evra, Wachezaji wengine wa Ufaransa waliofungiwa kufuatia sakata hilo la Kombe la Dunia ni Anelka, mechi 18, Franck Ribery, mechi 3 na Jeremy Toulalan, mechi moja.
Evra alikata rufaa kupinga kifungo hicho kwa Kamati ya Rufaa ya FFF lakini kamati hiyo imesema adhabu itabaki pale pale.

Friday 10 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

RATIBA LIGI ZA ULAYA: Kundirima Wikiendi!!!!
BUNDESLIGA:
Ijumaa,10 Septemba
1899 Hoffenheim v Schalke
Jumamosi,11 Septemba
Freiburg v Stuttgart
Borussia Moenchengladbach v Eintracht Frankfurt
Hamburg v Nurnberg
Borussia Dortmund v Wolfsburg
Hannover v Bayer Leverkusen
Bayern Munich v Werder Bremen
Jumapili, 12 Septemba
Mainz 05 v Kaiserslautern
Cologne v St Pauli
LA LIGA:
Jumamosi,11 Septemba
Valencia v Racing Santander
Barcelona v Hercules
Real Madrid v Osasuna
Athletic Bilbao v Atlético Madrid
Jumapili, 12 Septemba
Sporting Gijon v Mallorca
Getafe v Levante
Zaragoza v Malaga
Villarreal v Espanyol
Sevilla v Deportivo
Jumatatu, 13 Septemba
Almeria v Real Sociedad
SERIE A:
Jumamosi, 11 Septemba
Inter Milan v Udinese
Cesena v AC Milan
Cagliari v Roma
Jumapili, 12 Septemba
Brescia v Palermo
Lecce v Fiorentina
Catania v Parma
Lazio v Bologna
Juventus v Sampdoria
Genoa v Chievo
Napoli v Bari

Thursday 9 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI KUU England kurudi dimbani Wikiendi hii!!
Baada ya kuzipisha Mechi za Kimataifa za Nchi za Ulaya kugombea kufuzu Fainali za EURO 2012, patashika za Ligi Kuu zinarudi tena Wikiendi hii kwa Mechi ya kwanza hapo Jumamosi Septemba 11 huko Goodison Park kati ya Wenyeji Everton na Manchester United, mechi ambayo itaanza Saa 8 dakika 45 mchana, bongo taimu.
Mechi hiyo itafuatiwa na mechi 7 ambazo zitaanza Saa 11 jioni zikiwemo za Mabingwa Chelsea wakiwa ugenini kwa West Ham na Arsenal wakiwa nyumbani Emirates kucheza na Bolton Wanderers.
Jumapili kutakuwa na mechi moja tu kati ya Birmingham na Liverpool.
Jumatatu usiku ni mechi kati ya Stoke City na Aston Villa.
RATIBA kamili:
[Saa za Bongo]
Jumamosi, 11 Septemba 2010
[Saa 8 dak 45 mchana]
Everton v Man United
[Saa 11 jioni]
Arsenal v Bolton
Fulham v Wolverhampton
Man City v Blackburn
Newcastle v Blackpool
West Brom v Tottenham
West Ham v Chelsea
Wigan v Sunderland
Jumapili, 12 Septemba 2010
[Saa 12 jioni]
Birmingham v Liverpool
Jumatatu, 13 Septemba 2010
[Saa 4 usiku]
Stoke v Aston Villa
CHEKI: www.sokainbongo.com

Jagielka adai Mashabiki Everton watamzomea Rooney
Phil Jagielka amedai Wayne Rooney atapata wakati mgumu mno kutoka kwa Mashabiki wa Everton wakati Manchester United watakapoenda kucheza mechi ya Ligi Kuu huko Goodison Park siku ya Jumamosi.
Rooney aliihama Everton Mwaka 2004 kwenda kucheza Manchester United na amekuwa akizomewa kila anaporudi kucheza Uwanja wa Goodison Park na Timu yake Man United lakini safari hii Mashabiki hao wa Everton wamepata sababu ya kumzomea zaidi baada ya Staa huyo kulipuliwa na baadhi ya Magazeti kuwa alitembea na Changudoa wakati Mkewe akiwa mja mzito.
Jagielka ana hamu ya kucheza dhidi ya Rooney baada ya Jumanne kucheza Timu moja wakati wote wawili walipokuwepo kwenye Kikosi cha England kilichoifunga Uswisi 3-1 kwenye mechi ya EURO 2012.
Jagielka amesema: “Atapata shida toka kwa Mashabiki lakini Rooney ni kichwa ngumu hivyo hatasumbuka. Mie ntafurahia kushindana nae.”
Rio ategemea kuendelea Unahodha England
Rio Ferdinand anategemea kuendelea kuwa Nahodha wa England ingawa kumekuwa na mbiu kutoka baadhi ya Magazeti kuwa Unahodha apewe Steven Gerrard ambae amejizolea sifa toka Magazeti hayo kwa kile kinachodaiwa kuiongoza vyema Timu katika ushindi wa mechi mbili za EURO 2012 dhidi ya Bulgaria na Uswisi hivi majuzi.
Kocha wa England, Fabio Capello, amelipanchi suala hilo kwa kutamka: “Kwangu uchezaji wa Mchezaji ni muhimu sana kupita nani ni Nahodha.”
Hata hivyo, Ferdinand, ambae yuko fiti baada ya kuumia goti lilimkosesha Kombe la Dunia, amedokeza kuwa ana uhakika kubaki Nahodha kwenye mechi ya EURO 2012 hapo Oktoba 12 dhidi ya Montenegro.
CHEKI: www.sokainbongo.com
Capello kula pensheni 2012
Fabio Capello amethibitisha ataendelea kuwa Kocha wa England hadi Mkataba wake utakapomalizika Mwaka 2012.
Mtaliana huyo aliingia madarakani Mwaka 2008 kwa Mkataba wa Miaka miwili na nusu lakini Mkataba huo ukaongezwa kabla ya kuanza kwa Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni.
Baada ya kubwagwa nje Raundi ya Pili huko Afrika Kusini kwa kichapo cha 4-1 toka kwa Ujerumani, kumekuwa na manung’uniko kuwa iikuwa makosa kumwongezea Mkataba kabla ya Mashindano makubwa.
England kwa sasa imeanza kampeni ya kuingia Fainali za EURO 2012 zitakazochezwa huko Poland na Ukraine kwa pamoja Mwaka 2012 na tayari Capello, Miaka 64, ameshaiongoza England katika ushindi wa mechi mbili zao za kwanza za Kundi lao walipozichapa Bulgaria na Uswisi kwa mabao 4-0 na 3-1 kila mmoja hivi juzi.
Mechi inayofuata ya England kwenye Kundi lao ni Oktoba 12 watakapokuwa Wembley kucheza na Montenegro.
Capello ameahidi kuhakikisha England inafika Fainali za EURO 2012 lakini hataendelea kuwa Kocha baada ya hapo kwa kuwa umri wake utakuwa mkubwa na angependelea kula pensheni yake kwa raha.
Balotelli kula kisu gotini
Fowadi wa Manchester City Mario Balotelli atafanyiwa operesheni ya goti na atakuwa nje kwa Wiki 6.
Supa Mario aliumia goti kwenye mechi na FC Tmisoara ya EUROPA LIGI hapo Agosti 19 na ingawa alipumzishwa ili apate nafuu alijitonesha mazoezini Wiki iliyopita na sasa imelazimu apasuliwe.
Balotelli, Miaka 20, alihamia Man City kutoka Inter Milan kwa kitita cha Pauni Milioni 21 Mwezi uliokwisha na amechezea Man City dakika 33 tu katika mechi na FC Timisoara ambayo Man City walishinda 1-0.
Supa Mario atazikosa mechi za Klabu yake dhidi ya Chelsea kwenye Ligi Kuu na ile ya EUROPA LIGI na Juventus.
Inategemewa atarudi uwanjani kabla ya pambano la Ligi Kuu na Arsenal hapo Oktoba 24.

Wednesday 8 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Vilabu Ulaya vyaishukia FIFA
Chama cha Klabu za Ulaya, ECA [European Clubs Association], kimeitaka FIFA ifikirie upya katika upanganji wake wa Kalenda ya Mechi za Kimataifa za Kirafiki.
ECA, yenye Vilabu Wanachama 200 huko Ulaya zikiwemo Timu zote Vigogo, wametaka mazungumzo ya haraka na FIFA baada ya Mameneja wengi wa Klabu hizo kulalamika kuwepo kwa Mechi za Kimataifa za kirafiki Mwezi Agosti wakati wakiwa wanajitayarisha kwa Msimu mpya wa Ligi.
Mwenyekiti wa ECA, Karl-Heinz Rummenigge, ameziponda Mechi hizo na kuziita upuuzi mtupu.
Rummenigge ameitaka FIFA ielewe kuwa Klabu ndizo Waajiri wa Wachezaji na hivyo wana kila haki kuitaka FIFA ikubaliane nao.
ECA pia imeitaka FIFA na UEFA kuwakatia Bima Wachezaji ili Klabu zilipwe wakiumia wakati wanachezea Timu za Taifa.
Rufaa ya Evra kusikilizwa kesho
Rufaa ya Nahodha wa Ufaransa kupinga kifungo cha mechi 5 itasikilizwa kesho na Kamisheni ya Rufaa ya FFF, Shirikisho la Soka Ufaransa.
Patrice Evra alifungiwa mechi 5 baada ya Timu yao kugoma kufanya mazoezi hapo Juni 20 walipokuwa Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia wakipinga kufukuzwa kwa Mchezaji mwenzao Nicolas Anelka aliekuwa amegombana na Kocha wa Ufaransa wakati huo, Raymond Domenech.
Pamoja na Evra, Wachezaji wengine wa Ufaransa waliofungiwa kufuatia sakata hilo la Kombe la Dunia ni Anelka, mechi 18, Franck Ribery, mechi 3 na Jeremy Toulalan, mechi moja.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Wakaguzi wa FIFA wapo USA
Timu ya Wakaguzi wa FIFA ya Wagombea Uenyeji wa Kombe la Dunia ipo Marekani na tayari imeshatembelea New York, Ikulu ya Marekani huko Washington na inategemewa kupitia jumla ya Miji mingine mitatu katika ukaguzi wao wa Siku 3.
Wakaguzi hao sita wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka la Chile, Harold Mayne-Nicholls, pia watatembelea Miji ya Miami, Dallas na Houston.
Timuhiyo ya Wakaguzi tayari washapitia Nchi Waombaji 8 kati ya 9 na watamalizia ukaguzi wao huko Qatar kati ya Septemba 13 hadi 17.
Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, ndie Mwenyekiti wa Kamati ya Marekani ya Kugombea Uenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia.
Inategemewa Nchi ya Ulaya itapewa Uenyeji wa Fainali za 2018 na Wagombea ni England, Russia, Spain na Ureno kwa pamoja na Ubelgiji na Uholanzi kwa pamoja.
Fainali za Mwaka 2022 zinashindaniwa na USA, Australia, Japan, Korea Kusini na Qatar.
Uamuzi wa nani atapewa Uenyaji wa Fainali hizo za Kombe la Dunia utafanyika Desemba 2 na Kamati Kuu ya FIFA yenye Watu 24.
Fainali zijazo za Mwaka 2014 zitafanyika Nchini Brazil.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Capello afurahishwa na Rooney
Fabio Capello alikuwa na furaha kubwa hapo jana baada ya ushindi wa England wa ugenini wa mabao 3-1 dhidi ya Uswisi kwenye mechi ya Makundi ya EURO 2012 lakini furahi hiyo ilizidi kifani jinsi Wayne Rooney alivyokabiliana na presha ya skandali yake kwa kufunga bao la kwanza.
Capello alitamka baada ya mechi: “Alicheza vizuri. Daima alikuwa ndio kiungo wa mashambulizi yote. Alikuwa na presha kubwa lakini alimudu vyema!”
Ufaransa yazinduka, yashinda ugenini!
Ufaransa, jana ikiwa ugenini, ilizinduka toka lindi la kufungwa na balaa ya migogoro, na kuichapa Bosnia & Herzegovina mabao 2-0 katika mechi ya Makundi ya EURO 2012.
Mabao ya Karim Benzema, dakika ya 72, na Frank Malouda, dakika ya 77, yaliwafufua Vigogo hao wa Ulaya.
EURO 2012
MATOKEO:
Jumanne, 7 Septemba 2010
Turkey 3 Belgium 2
Austria 2 Kazakhstan 0
Germany 6 Azerbaijan 1
Russia 0 Slovakia 1
FYR Macedonia 2 Armenia 2
Republic of Ireland 3 Andorra 1
Serbia 1 Slovenia 1
Italy 5 Faroe Islands 0
Belarus 0 Romania 0
Albania 1 Luxembourg 0
Bosnia & Herzegovina 0 France 2
Sweden 6 San Marino 0
Netherlands 2 Finland 1
Hungary 2 Moldova 1
Georgia 0 Israel 0
Malta 0 Latvia 2
Croatia 0 Greece 0
Bulgaria 0 Montenegro 1
Switzerland 1 England 3
Denmark 1 Iceland 0
Norway 1 Portugal 0
Czech Republic 0 Lithuania 1
Scotland 2 Liechtenstein 1
Mabingwa wa Dunia Spain wapondwa na Argentina
Katika mechi ya kirafiki, Mabingwa wa Dunia, Spain, walichapwa mabao 4-1 na Wenyeji wao Argentina huko Buenos Aires.
Mabao ya Argentina yalifungwa na Lionel Messi na Gonzalo Higuan mapema kisha Kipa wa Liverpool, Pepe Reina, akaipa ‘zawadi’ Argentina pale alipoanguka na kuuruhusu mpira umpite tobo na ndipo Carlos Tevez alipouwahi na kufunga bao la 3.
Baada ya hapo, Spain wakapata bao lao Mfungaji akiwa Fernando Llorente lakini Sergio Aguero akaifungia Argentina bao la 4 dakika za majeruhi.

Tuesday 7 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Uswisi 1 England 3
• Rooney afunga bao la kwanza
Wayne Rooney, alieandamwa na skandali, aliipatia England bao la kwanza katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uswisi huko Uwanja wa St Jakob Park, Basle katika mechi ya Kundi G kuwania kuingia Fainali za EURO 2012.
Bao la pili la England lilifungwa na Adam Johnson na Uswisi, wakicheza Watu 10 wakati huo baada ya Stefan Lichsteiner kutolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya kupata Kadi Njano mbili, walipata bao lao kufuatia shuti la mbali la Kijana wa Miaka 18 Shaqiri.
Ndipo Darren Bent, aleingia badala ya Rooney, akapachika bao la 3 na kuivusha England salama.
Vikosi vilivyoanza:
Switzerland: Benaglio, Lichtsteiner, Grichting, Von Bergen, Ziegler, Margairaz, Inler, Schwegler, Degen, Derdiyok, Frei.
Akiba: Wolfli, Affolter, Streller, Padalino, Fernandes, Costanzo, Shaqiri.
England: Hart, Glen Johnson, Jagielka, Lescott, Ashley Cole, Walcott, Gerrard, Barry, Milner, Defoe, Rooney.
Akiba: Foster, Gibbs, Cahill, Carrick, Adam Johnson, Wright-Phillips, Bent.
Refa: Nicola Rizzoli (Italy)
Van Persie nje Wiki 6
Straika wa Arsenal Robin van Persie atakuwa nje ya uwanja kwa Wiki 6 baada ya kugundulika kuwa enka aliyoumia Agosti 28 kwenye mechi ya Ligi Kuu ambayo Arsenal iliwafunga Blackburm mabao 2-1 ipo kwenye hali mbaya kupita ilivyodhaniwa.
Msimu uliokwisha, Van Persie alikuwa nje kwa Miezi mitano baada ya pia kuumia enka.
Straika huyo kutoka Uholanzi sasa atazikosa mechi mbili za kwanza za Arsenal za UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya Braga Uwanja wa Emirates Septemba 15 na ile ya ugenini na Partizan Belgrade Septemba 28.
Pia hatacheza mechi 5 za Ligi Kuu zikiwemo dabi na Tottenham Septemba 21 huko White Hart Lane na ile dhidi ya Mabingwa Chelsea hapo Oktoba 3.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Houllier Meneja mpya Villa
Aliekuwa Meneja wa zamani wa Liverpool, Gerrard Houllier, amesaini Mkataba wa Miaka miwili wa kuwa Meneja mpya wa Aston Villa kuchukua nafasi ya Martin O’Neill alieondoka mwenyewe.
Houllier, Miaka 63, amekuwa kwenye majadiliano na Villa kwa wiki moja na kesho anategemewa kutangazwa rasmi.
Houllier anategemewa kumchukua Msaidizi wake wa zamani wa Liverpool, Phil Thompson, awe tena Msaidizi wake huko Aston Villa.
Sare na Algeria yazua ndoto Bongo!
Baada ya kutoka sare na Algeria ya 1-1 Siku ya Ijumaa kwenye mechi ya Makundi kuwania kuingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika iliyochezwa huko Algiers, ndoto za Wadau wa Bongo za kucheza Fainali kwa mara ya kwanza tangu 1980 zimefufuka hasa baada ya Vigogo wengine, Morocco, ambao wapo Kundi moja na Tanzania, kutoka sare 0-0 na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mechi inayofuata kwa Taifa Stars ni ya ugenini tena huko Morocco Novemba 9 na kufuatiwa na mechi ya nyumbani kucheza na Jamhuri ya Afrika ya Kati Machi Mwakani.
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitachezwa Mwaka 2012 huko Equatorial Guinea na Gabon, kwa pamoja.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Vermaelen adai Fabregas ni Barca damu!
Beki wa Arsenal, Thomas Vermaelen, amekiri kuwa Mchezaji mwenzake hapo Arsenal Cesc Fabregas ana damu ya FC Barcelona.
Fabregas amekuwa akihusishwa na kurudi tena Barca kwa muda mrefu sasa, Klabu ambayo alianza nayo Soka akiwa mtoto.
Ingawa alitegemewa kuhamia huko Barca kabla Msimu huu haujanza lakini Arsenal wakamng’ang’ania na kuikataa ofa rasmi ya Barcelona.
Vermaelen ametoboa kwa kusema: “Cesc anaibeba Barca moyoni mwake, ipo kwenye damu yake…hivyo ni ngumu yeye kuisahau Barca!”
Hivi juzi, Fabregas alikaririwa akisema kuwa Arsenal ilikataa yeye kwenda Barcelona lakini hawezi kusema nini walichoongea yeye na Meneja wake wa Arsenal Arsene Wenger.
Gibson akerwa na Kocha wa kwao Ireland
Kiungo Chipukizi wa Manchester United Darron Gibson amechukizwa na Kocha wa Timu ya Jamhuri ya Ireland, Giovanni Trapattoni, kwa kumtaka aondoke Man United ili aende Timu nyingine kupata namba ya kudumu na hivyo kuweza kuchaguliwa Kikosi cha Kwanza cha Ireland.
Gibson, Miaka 22, amekuwa hachezeshwi kwenye Timu ya Ireland na
Trapattoni na kama kawaida Ijumaa iliyopita alipigwa benchi kwenye mechi ya EURO 2012 dhidi ya Armenia waliyoshinda 1-0 na leo anategemewa tena kuwa nje kwenye mechi na Andorra ya EURO 2012.
Gibson amesema: “Kama Trapattoni anataka nihame Klabu kama Manchester United niende Timu kama Stoke ili nicheze mechi nyingi lakini nikose nafasi ya kushinda Vikombe, simuelewi! Wapi unaweza kwenda ukitoka Man United? Kwenye Klabu ipi, kama si Man United, nnakoweza kukuza kiwango?”
CHEKI: www.sokainbongo.com

EURO 2012: Uswisi v England
Leo huko Basle, Uwanjani St Jakob Park, Wenyeji Uswisi watashuka dimbani kupambana na England kwenye mechi ya Kundi G kutafuta Timu zitakazoingia Fainali za EURO 2012 huku macho ya kila Mtu yatakuwa kwa Wayne Rooney ambae amelipuliwa na Magazeti ya Uingereza kwa kutembea na Changudoa wakati Mkewe akiwa mja mzito.
Ingawa Magazeti hayo yaliendelea kudai Rooney ataachwa kutoka Kikosi cha England, Kocha Fabio Capello amesisitiza Straika huyo atacheza leo.
Pambano la leo ni gumu kupita lile la Ijumaa ambalo England waliifunga kirahisi Bulgaria kwa bao 4-0 huku Rooney akizitengeneza bao zote hizo.
Kundi G lina Timu 5 ambazo ni England, Uswisi, Bulgaria, Wales na Montenegro.
Hii ni mechi ya kwanza kwa Uswisi na ndio inahesabiwa mechi ngumu kupita zote katika Kundi G.
Mechi nyingine ya Kundi hili iliyochezwa Ijumaa ilikuwa kati ya Montenegro na Wales ambayo Montenegro walishinda 1-0.
Uswisi ipo chini ya Kocha Mjerumani Ottmar Hitzfeld na huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia Mwezi Juni, Uswisi iliwafunga Mabingwa wa Dunia Spain.
Katika mechi 20 zilizochezwa kati ya Uswisi na England, Uswisi imeshinda mechi 3 tu na ya mwisho kushinda ilikuwa 1982.
England imeifunga Uswisi mara 12 kikiwemo kipigo cha 8-1 Mwaka 1963.
Vikosi vinategemewa kuwa:
England: Hart, G Johnson, Jagielka, Cahill, A Cole, Barry, Gerrard, Milner, Walcott, Rooney, Defoe
Switzerland: Wolfli, Lichsteiner, Grichting, Von Bergen, Ziegler, Fernandes, Degen, Barnetta, Inler, Frei, Derdiyok
CHEKI: www.sokainbongo.com

Kuyt nje wiki kadhaa
Liverpool itamkosa Mshambuliaji wake mpiganaji uwanjani Dirk Kuyt alieumia bega akiwa mazoezini na Timu ya Taifa ya Uholanzi na taarifa za awali zimesema atakuwa nje ya uwanja kwa Wiki kadhaa.
Kuyt, Miaka 30, akiwa kambini na Uholanzi ambao leo wanacheza na Finland kwenye EURO 2012, alianguka vibaya na kufikia bega wakati akijaribu kuunganisha krosi.
Kuumia kwa Kuyt ni pigo kubwa kwa Liverpool ambayo itamkosa katika mechi zijazo dhidi ya Birmingham kwenye Ligi Kuu, Steau Bucharest kwenye EUROPA LIGI na ile BIGI MECHI ya Ligi Kuu dhidi ya Manchester United September 19 huko Old Trafford.

Monday 6 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Capello: ‘Rooney atacheza kesho!’
• Gerrard: ‘Kesho Rooney atawika!’
Fabio Capello amesistiza Wayne Rooney atacheza mechi ya England na Uswisi itayochezwa hapo kesho Uwanja wa St Jakob Park, Basle, Uswisi ya kugombea kuingia Fainali za EURO 2012 licha ya kulipuliwa na kumulikwa kupindukia na Magazeti kufuatia kutangazwa kutembea na Changudoa wakati Mkewe akiwa Mja Mzito.
Capello amesema: “Aliniambia anataka kucheza na atacheza. Nategemea uchezaji wake utakuwa mzuri kama alivyocheza Wembley Ijumaa. Mkazo wetu ni gemu ya kesho na si maisha binafsi ya Wachezaji.”
Kocha huyo wa England aliongeza mara baada ya Rooney kukazania kucheza yeye hakusita kuamua atacheza na tatizo dogo kwake ni kuamua nani atakuwa Sentahafu pacha wa Phil Jagielka kati ya Matthew Upson na Gary Cahill.
Nae Steven Gerrad, Nahodha wa England, amesema anategemea Rooney atakuwa na gemu spesheli kesho kwa vile sehemu bora kwa Mchezaji mwenye matatizo ya kibinafsi ni kuwa uwanjani.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Hodgson aomba Liverpool iuzwe
Meneja wa Liverpool Roy Hodgson amesema kazi yake ya sasa ni kuhakikisha Kikosi cha Wachezaji wake wa sasa wanabaki pamoja hadi Wamiliki wapya wa Klabu watakapoingia na kumpa mtaji wa kukiimarisha.
Hadi sasa Liverpool imekuwa haiuziki ingawa Wamiliki wa sasa, Wamarekani wawili Tom Hicks na George Gillet, wamekuwa wakihaha kuiuza ili kuyakimbia madeni yanayoikaba Klabu hiyo.
Ingawa Hodgson, alierithi Umeneja kutoka kwa Rafael Benitez aliehamia Inter Milan, amekuwa akijitahidi kuwabakisha Wachezaji hivi karibuni alilazimika kumuacha Kiungo Javier Mascherano aende Barcelona.
Hodgson amesema: “Klabu inauzwa lakini hakuna anaejua mwelekeo wake mpya Wanunuzi wakiingia. Hali ikibadilika huenda tukapata fungu la kununua Wachezaji na kujiimarisha.”
Hata hivyo Hodgson amesisitiza Liverpool iliyopo itapigana kupata ushindi.
Shawcross wa Stoke amponda Wenger
Beki wa Stoke City, Ryan Shawcross, ambae hivi karibuni alishambuliwa na Meneja wa Arsenal Wenger kwa kuitwa Mcheza Raga, amejibu mapigo na kumshambulia Mfaransa huyo.
Stoke City ilipeleka malamiko rasmi kwa FA kuhusu Wenger lakini FA ilisema Meneja huyo hana kesi ya kujibu.
Hasira za Wenger kwa Shawcross zilianza mwanzoni mwa Mwaka huu pale Beki huyo wa Stoke alipomvunja mguu Chipukizi wake Aaron Ramsey.
Hivi karibuni, Wenger alimwita Shawcross Mcheza Raga na kuitaja mechi kati ya Stoke na Tottenham.
Shawcross amehoji: “Kila Mtu ana maoni yake lakini mechi ile haikuhusu Timu yake, kwa nini aizungumzie? Huyu Bwana ana lake kuhusu mimi. Inashangaza kuniingiza mimi. Siku zote ana matatizo na Stoke, Meneja wetu na baadhi ya Wachezaji wetu.”
CHEKI: www.sokainbongo.com

Rooney yuko Uswisi na England
Licha ya kulipuliwa kwenye baadhi ya Magazeti huko Uingereza na skandali la kutembea na Changudoa na pia kudaiwa atatupwa nje ya Timu ya Taifa ya England, Wayne Rooney aliondoka na Wachezaji wenzake kwenda Uswisi ili kucheza mechi ya Kundi lao kwenye EURO 2012 ambapo kesho watacheza na Uswisi.
Magazeti hayo yamemwandama Staa huyo wa Manchester United na pia tegemeo kubwa la England huku mengine yakidai Wadhamini wake, Makampuni ya Nike, EA Sports na Coca Cola, yanafikiria kumtema.
Lakini, Kampuni ya Nike tayari imeshatangaza kuwa wataendelea kubakia na Rooney na kuwa sakata lililomkumba ni suala binafsi la Rooney na Familia yake.
Kampuni ya Nike ilikuwa na msimamo kama huo baada ya Mcheza Gofu maarufu Tiger Woods kukumbwa na skandali la ngono nje ya ndoa.
Nao Coca Cola wamefuata nyayo za Nike na kudai hilo ni suala binafsi la Rooney na Familia yake.
Nayo Magazeti mengine, pengine yakigundua kuwa kutokuwepo kwa Rooney kwenye Timu ya England ni pigo kubwa, yamemwomba Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, aingilie na kumnyoosha Rooney ili aepuke maisha mabovu na hivyo kuisaidia England ifanye vyema kwenye michuano ya Kimataifa kwa vile Mchezaji huyo ndie mkombozi wao.
Bebe yumo Kikosi cha UEFA
UEFA imethibitisha kuwa Mchezaji mpya wa Manchester United, Bebe, kutoka Ureno yumo miongoni mwa Kikosi kilichosajiliwa kwao kwa ajili ya michuano ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Kulikuwa na taarifa kwenye Vyombo vya Habari kuwa Bebe na Owen Hargreaves ndio Wachezaji ambao hakusajiliwa lakini UEFA imethibitisha ni Hargreaves tu ndie ambae hayumo kwenye Kikosi hicho cha Wachezaji 25.
Hivyo Bebe yuko huru kuichezea Man United Jumanne ijayo dhidi ya Rangers ya Scotland katika mechi ya kwanza ya Kundi lao ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
CHEKI: www.sokainbongo.com

‘Les Bleus’ piga ua kesho!!!
Huku jahazi likiendelea kutota kufuatia aibu ya Fainali za Kombe la Dunia iliyozaa kufungiwa baadhi ya Nyota wao na kufungwa nyumbani katika mechi ya kwanza tu ya EURO 2012, kesho Ufaransa ipo ugenini kucheza na Bosnia-Herzegovina katika mechi ya pili ya Kundi lao kuwania kuingia Fainali za EURO 2012.
Siku ya Ijumaa, Les Bleus walichapwa 1-0 na Belarus na kipigo hicho kilimfanya Beki wa Ufaransa anaecheza Arsenal akiite ni ‘kupigwa kibao usoni’.
Sagna ametamka: “Tumepigwa kibao usoni lakini kesho ni siku nyingine na lazima tufanye kazi ya ziada.”
Ufaransa kwa sasa ipo chini ya Kocha mpya, Gwiji la zamani, Laurent Blanc na inawakosa Wachezaji Nyota kama Nahodha wao Patrice Evra na Franck Ribery ambao wako kifungoni kufuatia sakata la huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
………..Anelka bado MSTAAFU!!!!!!!!!!!!!
Staa wa Chelsea, Nicolas Anelka, amesisitiza msimamo wake kuwa yeye alistaafu kuichezea Ufaransa tangu Juni 19 siku aliyofukuzwa kwenye Timu hiyo ya Ufaransa huko Afrika Kusini ilipokuwa kwenye Kombe la Dunia.
Anelka, Miaka 31, amedai hamna uwezekano wowote wa kurudi kuichezea Les Bleus [maana yake Timu ya Bluu] baada ya kifungo chake cha mechi 18 alichopewa kufuatia sakata lake la huko Afrika Kusini.
Mchezaji huyo wa Chelsea ametamka: “Sina haja kuchezea Les Bleus kwani kila Wikiendi naichezea Bluu ya Chelsea!”

Sunday 5 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Adebayor: ‘Man City ni Timu Kubwa kupita Ze Gunners!’
Robinho: ‘Man City ni Cha Mtoto kwa Man United!’
Wakati Emmanuel Adebayor anaikandya Timu yake ya zamani Arsenal kwa kudai Timu yake ya sasa, Manchester City, ni ‘Timu Kubwa’ kupita Arsenal, Robinho ameiponda Timu yake ya zamani, Man City, na kusema haijaipita kwa ukubwa Manchester United ambao ni Mahasimu wao wakubwa.
Adebayor amedai kuwa kwa Kikosi walichonacho Man City kwa sasa ni wazi wao watawapiku Arsenal na kuonekana ni ‘Timu Kubwa’.
Adebayor ametamka: “Kama tutashinda mechi 10 mfululizo ni wazi Watu watasema sasa Man City ni Timu Kubwa!”
Nae Supastaa kutoka Brazil, Robinho, ambae hivi juzi tu amehamia AC Milan kwa ada ya Pauni Milioni 18 akitokea Manchester City, amedai alipokuwa Klabu hiyo ya Jijini Manchester chini ya Mameneja Mark Hughes na mrithi wake Roberto Mancini, ilikuwa ni kama yuko ofisini badala ya Klabu ya Soka.
Robinho, aliehamia Man City kutoka Real Madrid kwa Pauni Milioni 32.5, amesema: “Wote, Hughes na Mancini, hawakunielewa. Kulikuwa hamna uhusiano kati ya Wachezaji na Klabu. Ilikuwa ni kama Ofisi, unaenda mazoezini kisha kwa heri, unaenda kwenye mechi, kwa heri! Mimi ni Mbrazil na ni lazima niwe na furaha na kila kitu ndipo ntacheza Soka bora! “
Robinho akaongeza kuwa alipotua Man City, Wakurugenzi walimwahidi kuwa Man City itaipiku Man United baada ya Miaka michache na kuwa Klabu kubwa lakini sasa muda umepita na hamna kilichobadilika.
Pia Robinho aliponda mandhari ya Jiji la Manchester na kudai ni sehemu ngumu kwa Kijana wa Kibrazil kuishi hasa ukizingatia kijiwinta chake, baridi kali na usiku wa kiza totoro.
CHEKI: www.sokainbongo.com

FIFA yawafungia Wacongo
FIFA imewafungia Wachezaji wawili wa TP Mazembe ya Congo DR kwa kuleta fujo kwenye mechi ya Kombe la Kagame huko Rwanda Mwezi Mei na kusababisha pambano kati ya APR ya Rwanda na TP Mazembe livunjike.
FIFA inalitambua rasmi Kombe la Kagame ambalo ndio hutoa Klabu Bingwa ya Nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Wachezaji hao wawili wa TP Mazembe ni Nahodha wao Tresor Mputu Mabi, aliefungiwa Miezi 12, na Guy Lusadisu aliefungiwa Miezi 11.
CECAFA ililipeleka suala Wachezaji hao kwa CAF ambayo iliamua kuwafungia na sasa FIFA imepitisha rasmi Kifungo hicho ambacho kinahusu mechi za ndani na za Kimataifa.
Mputu na Lisadisu pia huichezea Timu ya Taifa ya Congo.
Polisi walimbamba Supa Mario na Bulungutu!
Wiki kadhaa baada ya kusajiliwa na ‘Timu Tajiri’ Manchester City kwa dau la Pauni Milioni 22, Mchezaji kutoka Italia, Mario Balotelli, maarufu kama Supa Mario, wakati akienda mazoezini asubuhi, Gari alilokuwa akiliendesha aina ya Audi R8 liligongana na Gari jingine.
Mara tu baada ya ajali hiyo iliyotokea Siku 8 zilizopita, Polisi wakatinga kwenye tukio na kama desturi ya huko Ulaya wakampima papo hapo ili kujua kama alikuwa njwii lakini akaonekana safi na ndipo walipompekua wakakuta kwenye mfuko wake wa nyuma wa suruali ana Pauni 5,000.
Polisi wakastuka kumwona Kijana wa Miaka 20, anaeongea Kiingereza kibovu, akiwa na pesa nyingi kama hizo na walipomhoji amepata wapi pesa nyingi kama hizo, Supa Mario, bila kusita wala kutetereka, akajibu: “Ni kwa sababu ni tajiri!”
Kitu kingine cha kushangaza katika tukio hilo la ajali ni pale ilipodhihirika Dereva wa Gari iliyogongana na la Supa Mario alikuwa ni Shabiki la kutupwa la Manchester City ambae alikuwa ana Tiketi ya Msimu kuingia mpirani kwenye mechi za Man City kwa Miaka 25 sasa.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Carragher afunga mabao Mechi yake ya kumuenzi!
Katika mechi iliyochezwa jana Jumamosi Uwanjani Anfield kumuenzi Jamie Carragher kwa utumishi wake bora kwa Klabu ya Liverpol wa Miaka 16, kati ya Liverpool na Kombaini ya Mahasimu wao wakubwa Jijini Liverpool, Everton, Carragher aliweza kufunga bao mbili, bao moja kwa kila upande lakini mwishowe Liverpool walishinda 4-1.
Nyota wa Liverpool wa sasa, Steven Gerrard na Joe Cole, walicheza pamoja na wa zamani Luis Garcia, Emile Heskey na Michael Owen.
Carragher aliifungia bao Liverpool kwa njia ya penalti Kipindi cha Kwanza na Kipindi cha Pili alifunga penalti nyingine kwa Everton, Timu ambayo alikuwa Shabiki wao alipokuwa mtoto.
Michael Owen, ambae sasa ni Mchezaji wa Wapinzani wakubwa wa Liverpool, Manchester United, alianza kwa kuzomewa na baadhi ya Mashabiki wa Liverpool humo Anfield lakini baadae waligeuka na kumshangilia.
Marefa washindwa kufika Mechi ya Zambia v Comoros
• Wakwama Dubai!!!
Mechi ya kugombea kuingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Zambia na Comoro iliyokuwa ichezwe jana huko Lusaka ilibidi iahirishwe hadi leo kwa sababu Marefa waliopangwa na CAF kutoka Eritrea walikuwa wamekwama huko Dubai walikoenda kuunganisha Ndege ili wafike Lusaka.
CAF iliamrisha Mechi hiyo ichezwe leo na pia kuwaweka Marefa toka Afrika Kusini kuwa kwenye tahadhari ili waende Lusaka mara moja endapo Marefa hao wa Eritrea watachelewa zaidi kufika.
PITIA: www.sokainbongo.com

Magazeti England yamvaa Rooney na skandali!!!
Magazeti mawili ya huko England yametoa ripoti kuwa ndoa ya Wayne Rooney ipo majaribuni baada ya kugundulika alitembea na changudoa wakati Mkewe alipokuwa mja mzito.
Imedaiwa Rooney alimjulisha Mkewe jana kuhusu kuvuja kwa Skandali hiyo.
Imedaiwa kuwa Rooney alitembea na Jennifer Thompson, Miaka 21, ambae hutoza Pauni 1,200 kwa usiku mmoja, mara 7 katika kipindi cha Miezi minne.
Licha ya habari hizo kuandikwa kwenye Magazeti, FA imethibitisha Rooney atakuwemo kwenye msafara wa England unaokwenda Uswisi kucheza Mechi ya Makundi ya EURO 2012 dhidi ya Uswisi hapo Jumanne.
Man United yatoa Kikosi cha UEFA CHAMPIONS LIGI
Kikosi cha Wachezaji 30 watakaoiwakilisha Manchester United kwenye Mechi za Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI kimetangazwa na hawamo Owen Hargreaves na Bebe.
Mchezaji mwingine alieachwa ni Beki Ritchie De Laet.
Wachezaji wapya, Javier Hernandez na Chris Smalling, wamo pamoja na Chipukizi 6 ambao huingizwa kwenye Listi kama Listi B ambao ni Kipa Ben Amos, Mapacha Rafael na Fabio, Oliver Gill, Corry Evans na Federico Macheda.
Kikosi kamili ni:
Van der Sar, Kuszczak, Amos*; Neville, Evra, J.Evans, Ferdinand, W.Brown, Smalling, Vidic, O'Shea, Fabio*, Rafael*, Gill*; Nani, Anderson, Giggs, Park, Carrick, Scholes, Fletcher, Valencia, Gibson, C.Evans*; Berbatov, Rooney, Hernandez, Owen, Obertan, Macheda*.


*Inamaanisha kutoka Listi B ya Chipukizi.
PITIA: www.sokainbongo.com


KOMBE LA MATAIFA YA AFRICA:
MECHI ZA MAKUNDI
MATOKEO
Ijumaa, 3 Septemba 2010
Algeria 1 v Tanzania 1
Jumamosi, 4 Septemba 2010
Mauritius 1 v Cameroun 3
Morocco 0 v Central African Republic 0
South Africa 2 v Niger 0
Tunisia 2 v Malawi 2
Botswana 2 v Togo 1
Mauritania v Burkina Faso [IMEAHIRISHWA]
Sudan 2 v Congo 0
Cape Verde 1 v Mali 0
Guinea-Bissau 1 v Kenya 0
Gambia 3 v Namibia 1
Uganda 3 v Angola 0
Ivory Coast 3 v Rwanda 0
RATIBA
Jumapili, 5 Septemba 2010
Nigeria v Madagascar
Congo DR v Senegal
Swaziland v Ghana
Mozambique v Libya
Ethiopia v Guinea
Benin v Burundi
Liberia v Zimbabwe
Egypt v Sierra Leone
Zambia v Comoros
Powered By Blogger