CHEKI: www.sokainbongo.com
Adebayor: ‘Man City ni Timu Kubwa kupita Ze Gunners!’
Robinho: ‘Man City ni Cha Mtoto kwa Man United!’
Wakati Emmanuel Adebayor anaikandya Timu yake ya zamani Arsenal kwa kudai Timu yake ya sasa, Manchester City, ni ‘Timu Kubwa’ kupita Arsenal, Robinho ameiponda Timu yake ya zamani, Man City, na kusema haijaipita kwa ukubwa Manchester United ambao ni Mahasimu wao wakubwa.
Adebayor amedai kuwa kwa Kikosi walichonacho Man City kwa sasa ni wazi wao watawapiku Arsenal na kuonekana ni ‘Timu Kubwa’.
Adebayor ametamka: “Kama tutashinda mechi 10 mfululizo ni wazi Watu watasema sasa Man City ni Timu Kubwa!”
Nae Supastaa kutoka Brazil, Robinho, ambae hivi juzi tu amehamia AC Milan kwa ada ya Pauni Milioni 18 akitokea Manchester City, amedai alipokuwa Klabu hiyo ya Jijini Manchester chini ya Mameneja Mark Hughes na mrithi wake Roberto Mancini, ilikuwa ni kama yuko ofisini badala ya Klabu ya Soka.
Robinho, aliehamia Man City kutoka Real Madrid kwa Pauni Milioni 32.5, amesema: “Wote, Hughes na Mancini, hawakunielewa. Kulikuwa hamna uhusiano kati ya Wachezaji na Klabu. Ilikuwa ni kama Ofisi, unaenda mazoezini kisha kwa heri, unaenda kwenye mechi, kwa heri! Mimi ni Mbrazil na ni lazima niwe na furaha na kila kitu ndipo ntacheza Soka bora! “
Robinho akaongeza kuwa alipotua Man City, Wakurugenzi walimwahidi kuwa Man City itaipiku Man United baada ya Miaka michache na kuwa Klabu kubwa lakini sasa muda umepita na hamna kilichobadilika.
Pia Robinho aliponda mandhari ya Jiji la Manchester na kudai ni sehemu ngumu kwa Kijana wa Kibrazil kuishi hasa ukizingatia kijiwinta chake, baridi kali na usiku wa kiza totoro.
No comments:
Post a Comment