Monday 6 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Capello: ‘Rooney atacheza kesho!’
• Gerrard: ‘Kesho Rooney atawika!’
Fabio Capello amesistiza Wayne Rooney atacheza mechi ya England na Uswisi itayochezwa hapo kesho Uwanja wa St Jakob Park, Basle, Uswisi ya kugombea kuingia Fainali za EURO 2012 licha ya kulipuliwa na kumulikwa kupindukia na Magazeti kufuatia kutangazwa kutembea na Changudoa wakati Mkewe akiwa Mja Mzito.
Capello amesema: “Aliniambia anataka kucheza na atacheza. Nategemea uchezaji wake utakuwa mzuri kama alivyocheza Wembley Ijumaa. Mkazo wetu ni gemu ya kesho na si maisha binafsi ya Wachezaji.”
Kocha huyo wa England aliongeza mara baada ya Rooney kukazania kucheza yeye hakusita kuamua atacheza na tatizo dogo kwake ni kuamua nani atakuwa Sentahafu pacha wa Phil Jagielka kati ya Matthew Upson na Gary Cahill.
Nae Steven Gerrad, Nahodha wa England, amesema anategemea Rooney atakuwa na gemu spesheli kesho kwa vile sehemu bora kwa Mchezaji mwenye matatizo ya kibinafsi ni kuwa uwanjani.

No comments:

Powered By Blogger