Tuesday 7 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Uswisi 1 England 3
• Rooney afunga bao la kwanza
Wayne Rooney, alieandamwa na skandali, aliipatia England bao la kwanza katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uswisi huko Uwanja wa St Jakob Park, Basle katika mechi ya Kundi G kuwania kuingia Fainali za EURO 2012.
Bao la pili la England lilifungwa na Adam Johnson na Uswisi, wakicheza Watu 10 wakati huo baada ya Stefan Lichsteiner kutolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya kupata Kadi Njano mbili, walipata bao lao kufuatia shuti la mbali la Kijana wa Miaka 18 Shaqiri.
Ndipo Darren Bent, aleingia badala ya Rooney, akapachika bao la 3 na kuivusha England salama.
Vikosi vilivyoanza:
Switzerland: Benaglio, Lichtsteiner, Grichting, Von Bergen, Ziegler, Margairaz, Inler, Schwegler, Degen, Derdiyok, Frei.
Akiba: Wolfli, Affolter, Streller, Padalino, Fernandes, Costanzo, Shaqiri.
England: Hart, Glen Johnson, Jagielka, Lescott, Ashley Cole, Walcott, Gerrard, Barry, Milner, Defoe, Rooney.
Akiba: Foster, Gibbs, Cahill, Carrick, Adam Johnson, Wright-Phillips, Bent.
Refa: Nicola Rizzoli (Italy)
Van Persie nje Wiki 6
Straika wa Arsenal Robin van Persie atakuwa nje ya uwanja kwa Wiki 6 baada ya kugundulika kuwa enka aliyoumia Agosti 28 kwenye mechi ya Ligi Kuu ambayo Arsenal iliwafunga Blackburm mabao 2-1 ipo kwenye hali mbaya kupita ilivyodhaniwa.
Msimu uliokwisha, Van Persie alikuwa nje kwa Miezi mitano baada ya pia kuumia enka.
Straika huyo kutoka Uholanzi sasa atazikosa mechi mbili za kwanza za Arsenal za UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya Braga Uwanja wa Emirates Septemba 15 na ile ya ugenini na Partizan Belgrade Septemba 28.
Pia hatacheza mechi 5 za Ligi Kuu zikiwemo dabi na Tottenham Septemba 21 huko White Hart Lane na ile dhidi ya Mabingwa Chelsea hapo Oktoba 3.

No comments:

Powered By Blogger