Sunday 5 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Carragher afunga mabao Mechi yake ya kumuenzi!
Katika mechi iliyochezwa jana Jumamosi Uwanjani Anfield kumuenzi Jamie Carragher kwa utumishi wake bora kwa Klabu ya Liverpol wa Miaka 16, kati ya Liverpool na Kombaini ya Mahasimu wao wakubwa Jijini Liverpool, Everton, Carragher aliweza kufunga bao mbili, bao moja kwa kila upande lakini mwishowe Liverpool walishinda 4-1.
Nyota wa Liverpool wa sasa, Steven Gerrard na Joe Cole, walicheza pamoja na wa zamani Luis Garcia, Emile Heskey na Michael Owen.
Carragher aliifungia bao Liverpool kwa njia ya penalti Kipindi cha Kwanza na Kipindi cha Pili alifunga penalti nyingine kwa Everton, Timu ambayo alikuwa Shabiki wao alipokuwa mtoto.
Michael Owen, ambae sasa ni Mchezaji wa Wapinzani wakubwa wa Liverpool, Manchester United, alianza kwa kuzomewa na baadhi ya Mashabiki wa Liverpool humo Anfield lakini baadae waligeuka na kumshangilia.
Marefa washindwa kufika Mechi ya Zambia v Comoros
• Wakwama Dubai!!!
Mechi ya kugombea kuingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Zambia na Comoro iliyokuwa ichezwe jana huko Lusaka ilibidi iahirishwe hadi leo kwa sababu Marefa waliopangwa na CAF kutoka Eritrea walikuwa wamekwama huko Dubai walikoenda kuunganisha Ndege ili wafike Lusaka.
CAF iliamrisha Mechi hiyo ichezwe leo na pia kuwaweka Marefa toka Afrika Kusini kuwa kwenye tahadhari ili waende Lusaka mara moja endapo Marefa hao wa Eritrea watachelewa zaidi kufika.

No comments:

Powered By Blogger