Tuesday 7 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

EURO 2012: Uswisi v England
Leo huko Basle, Uwanjani St Jakob Park, Wenyeji Uswisi watashuka dimbani kupambana na England kwenye mechi ya Kundi G kutafuta Timu zitakazoingia Fainali za EURO 2012 huku macho ya kila Mtu yatakuwa kwa Wayne Rooney ambae amelipuliwa na Magazeti ya Uingereza kwa kutembea na Changudoa wakati Mkewe akiwa mja mzito.
Ingawa Magazeti hayo yaliendelea kudai Rooney ataachwa kutoka Kikosi cha England, Kocha Fabio Capello amesisitiza Straika huyo atacheza leo.
Pambano la leo ni gumu kupita lile la Ijumaa ambalo England waliifunga kirahisi Bulgaria kwa bao 4-0 huku Rooney akizitengeneza bao zote hizo.
Kundi G lina Timu 5 ambazo ni England, Uswisi, Bulgaria, Wales na Montenegro.
Hii ni mechi ya kwanza kwa Uswisi na ndio inahesabiwa mechi ngumu kupita zote katika Kundi G.
Mechi nyingine ya Kundi hili iliyochezwa Ijumaa ilikuwa kati ya Montenegro na Wales ambayo Montenegro walishinda 1-0.
Uswisi ipo chini ya Kocha Mjerumani Ottmar Hitzfeld na huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia Mwezi Juni, Uswisi iliwafunga Mabingwa wa Dunia Spain.
Katika mechi 20 zilizochezwa kati ya Uswisi na England, Uswisi imeshinda mechi 3 tu na ya mwisho kushinda ilikuwa 1982.
England imeifunga Uswisi mara 12 kikiwemo kipigo cha 8-1 Mwaka 1963.
Vikosi vinategemewa kuwa:
England: Hart, G Johnson, Jagielka, Cahill, A Cole, Barry, Gerrard, Milner, Walcott, Rooney, Defoe
Switzerland: Wolfli, Lichsteiner, Grichting, Von Bergen, Ziegler, Fernandes, Degen, Barnetta, Inler, Frei, Derdiyok

No comments:

Powered By Blogger