Saturday 21 March 2009

RATIBA LIGI KUU England:
Jumapili, 22 Machi 2009
[saa 10.30 jioni]
Wigan v Hull
[saa 12 jioni]
Man C v Sunderland
[saa 1 usiku]
Liverpool v Aston Villa
Arsenal wainyuka Newcastle 3-1!

Magoli kupitia kwa Niklas Bendtner, Abou Diaby na Samir Nasri yamewapa Arsenal ushindi mnono ugenini wa bao 3-1 dhidi ya Newcastle ambayo ipo hatihati ya kuporomoka daraja.
Ushindi huu wa Arsenal pia unawaongezea nguvu ya kuchukua kiuhakika nafasi ya nne msimamo wa ligi kwani sasa wako pointi 3 mbele ya Aston Villa.
Villa kesho wako ugenini Anfield kumenyena na Liverpool.

Baada ya kipigo cha 2-0 cha Fulham, Ferguson asema: 'Inasikitisha lakini Refa ni Phil Dowd, ulitegemea nini?'
Nae Hodgson wa Fulham akiri bahati na kujituma kumewapa ushindi!

Ferguson amekubali Fulham walicheza vizuri sana kipindi cha kwanza lakini maamuzi ya Refa Phil Dowd yamechangia wao kufungwa.
Ferguson amedai Kadi ya Njano ya pili kwa Rooney haikustahili kabisa kwani alirusha mpira pale frikiki ilipotakiwa kupigwa.
Ferguson alidai: 'Ni Refa Phil Dowd unategemea nini? Lakini si kosa la Refa tu tujilaumu wenyewe pia!'
Meneja wa Fulham, Roy Hodgson, amesema bahati na kujituma kupita kiasi ndio kilichowapa ushindi.
Wakati Mabingwa Man U wapata kipigo cha pili mfululizo LIGI KUU England, Chelsea nao watunguliwa!!

Fulham, wakiwa nyumbani kwao Craven Cottage huku wakipata msaada mkubwa wa Refa Phil Dowd aliewatwanga Wachezaji wa Man U Paul Scholes na Wayne Rooney Kadi Nyekundu, wameifunga Man U bao 2-0 hiki kikiwa kipigo cha pili mfululizo kwa Mabingwa hao.
Wiki iliyokwisha walifungwa 4-1 na Liverpool.

Chelsea, wakiwa nyuma ya Man U kwa pointi 4 ingawa Man U ana mechi moja mkononi, wameshindwa kupunguza tofauti ya pointi baada ya kupigwa na wenzao wa London, Tottenham, bao 1-0.

Matokeo mechi nyingine za LIGI KUU leo:

Blackburn 1 West Ham 1

Stoke 1 Middlesbrough 0

West Brom 1 Bolton 1

Portsmouth 2 Everton 1

Sasa hivi mechi kati ya Newcastle na Arsenal ndio inaanza.

Vikosi ni kama ifuatavyo:

Newcastle: Harper, Steven Taylor, Coloccini, Bassong, Jose Enrique, Ryan Taylor, Butt, Nolan, Duff, Lovenkrands, Martins.

Arsenal: Almunia, Sagna, Gallas, Toure, Clichy, Arshavin, Denilson, Diaby, Nasri, Van Persie, Bendtner.

Masupastaa wa Soka kufunzwa kuendesha Magari!!! Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa kutoa mafunzo hayo!!!!

PFA, Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa England, kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wake, Gordon Taylor, kimetangaza mpango kamambe wa kuwafundisha Mastaa wote wa Soka jinsi ya kuendesha magari kwa ustadi zaidi kufuatia wimbi la ajali na mikasa kadhaa inayowakumba Mastaa hao wakiwa kwenye magari yao ya bei mbaya, yenye nguvu sana na kasi za ajabu.
Hivi majuzi tu, Cristiano Ronaldo alinusurika na kuliteketeza gari lake la bei mbaya sana la aina ya Ferrari pale alipopata ajali akiwa kwenye mwendo wa kasi mjini Manchester.
Nae Mchezaji mwenzake wa Man U, Carlos Tevez, alibambwa na Polisi wa Manchester akiendesha gari huku akiwa hana Leseni ya kuendesha magari ya England.

Manchester City kuikwaa Hamburg ya Ujerumani Robo Fainali UEFA CUP

Klabu pekee ya England iliyobaki kwenye Kombe la UEFA, Manchester Ciy, imepangiwa kukutana na Hamburg ya Ujerumani kwenye Robo Fainali Kombe la UEFA.
Ikishinda mechi hiyo itapambana na Mshindi kati ya Werder Bremen au Udinese kwenye Nusu Fainali.
Ratiba kamili ya UEFA CUP ni:
ROBO FAINALI [mechi kuchezwa Aprili 9 na marudiano Aprili 16]
Hamburg v Manchester City
Paris St Germain [PSG] v Dynamo Kiev
Shakhtar Donetsk v Marseille
Werder Bremen v Udinese
NUSU FAINALI [kuchezwa Aprili 30 na marudio Mei 7]
Werder Bremen/Udinese v Hamburg/Man City
PSG/Dynamo Kiev v Shakhtar Donetsk/Marseille

Drogba aonywa na Polisi!!!

Mchezaji wa Chelsea anaetoka Ivory Coast, Didier Drogba, ameepuka kuburuzwa Mahakamani na badala yake kupewa onyo kali baada ya kuwarushia Mashabiki wa Burnley sarafu mara baada ya kufunga goli kwenye mechi kati ya Chelsea na Burnley kugombea Kombe la Carling iliyochezwa Novemba mwaka jana na kumalizika 1-1 lakini Chelsea wakatolewa kwa penalti tano tano.
FA ilimfungia Drogba mechi 3 kwa kitendo hicho.
Polisi baada ya uchunguzi na kushauriana na Waendesha Mashtaka waliamua kumwita Makao Makuu na kumpa onyo kali badala ya kumshtaki Mahakamani.

Nae Steven Gerrard afutiwa shtaka moja Mahakamani lakini kesi kuendelea kwa shtaka moja jingine!!!

Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, amefutiwa Shtaka la kushambulia kwa kutumia nguvu lakini bado anakabiliwa na shtaka jingine la kuvunja amani na kusababisha vurugu hadharani.
Gerrard yuko kwenye kesi hiyo inaowahusisha wenzake watano kufuatia ugomvi na vurugu zilizotokea ndani ya Naiti Klabu moja huko Liverpool mnamo Desemba 29 ambako DJ wa Klabu hiyo aliumizwa usoni.
Kesi hiyo itaendelea tena Aprili 3.

Friday 20 March 2009



DROO YA ROBO FAINALI UEFA CHAMPIONS LEAGUE!!!!



Mjini Nyon, Switzerland, kura ya kuchagua Timu zipi zitakutana Robo Fainali na Nusu Fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya ilifanyika na matokeo yake ni kama ifuatavyo.

Villarreal v Arsenal
Manchester United v FC Porto
Liverpool v Chelsea
Barcelona v Bayern Munich
Mechi kuchezwa tarehe 7/8 April na marudiano 14/15 April
NUSU FAINALI

Mshindi wa Villareal/Arsenal v Man U/Porto
Mshindi wa Liverpool/Chelsea v Barcelona/Bayern Munich

Thursday 19 March 2009

Droo ya Robo Fainali na Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kesho!!!!

Timu 8 zilizobaki kwenye kinyang'anyiro cha kuwania Kombe la Mabingwa wa Ligi Ulaya, UEFA CHAMPIONS LEAGUE, kesho mchana zitajua wapinzani watakaopambana nao kwenye Robo Fainali na Nusu Fainali.
Timu zilizoingia Robo Fainali ni nne kutoka England ambazo ni Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo, Manchester United, Chelsea, Liverpool na Arsenal, kutoka Hispania ni Barcelona na Villareal na nyingine ni Bayern Munich [Ujerumani] na FC Porto [Ureno].
Kwenye droo hiyo kura inakuwa huru na timu yeyote inaweza kupangwa na nyingine yeyote hata kama wanatoka nchi moja.
Tutawaletea matokeo ya droo hiyo kesho mchana kwenye saa 8 na nusu mchana saa za kibongo.

Habari nyingine:

-FA England kuchunguza tuhuma za Fabregas kumtemea mate Meneja Msaidizi wa Hull City.

FA imeingilia kati na kuwataka Mameneja wa Hull City, Phil Brown, na Msaidizi wake, Brian Horton, kuelezea kimaandishi mkasa huo wa Nahodha wa Arsenal, Cesc Fabregas, kumtemea mate Brian Horton.
Fabregas hakucheza mechi ya siku ya tukio kati ya Arsenal na Hull kwani ni majeruhi.

-Van der Sar aigomea Holland!

Kipa wa Manchester United, Edwin Van der Sar [38], ameukataa wito wa kuchezea Timu ya Taifa ya Holland uliofanywa na Meneja wa Timu ya Holland, Bert van Marwijk, ambae alimwomba Kipa huyo afute kustaafu kwake Timu ya Taifa.
Van der Sar alistaafu kuchezea Timu ya Holland mara tu baada ya EURO 2008 lakini alikubali kuidakia Holland mwezi Oktoba 2008 kwenye mechi dhidi ya Iceland na Norway wakati nchi yake ilipokabiliwa na upungufu wa Makipa baada ya wanaotumainiwa kuumia.
Meneja Bert van Marwijk alimwomba Van der Sar aidakie Holland kwenye mechi zijazo za Mchujo wa Kombe la Dunia dhidi ya Scotland Machi 28 na ile ya Macedonia Aprili 1.

Wednesday 18 March 2009

Arsenal watinga NUSU FAINALI FA CUP kwa utata! Goli la ofsaidi lawabeba, sasa kukutana na Chelsea!! Fabregas amtemea mate Meneja Msaidizi wa Hull City!!

Jana usiku, Arsenal waliokuwa wakicheza kwao Emirates na kujikuta wako nyuma kwa bao 1-0 hadi zikibaki dakika 16, waliibuka kidedea baada ya Robin van Persie kusawazisha na William Gallas kupachika bao la pili na la ushindi huku akiwa dhahiri ameotea.
Baada ya mechi, Meneja wa Hull City, Phil Brown, alidai Mchezaji wa Arsenal, Cesc Fabregas, ambae hakucheza kwani ni majeruhi wa muda mrefu na alieingia uwanjani mara baada ya mechi kwisha ili kuwapongeza wenzake, alimtemea mate Meneja Msaidizi wa Hull City, Brian Horton, wakati timu zikitoka uwanjani mwishoni mwa mechi kuelekea vyumba vya kubadilisha nguo.
Fabregas mwenyewe amekanusha tuhuma hizo.
Sasa Arsenal watacheza Nusu Fainali ya Kombe la FA hapo Aprili 18, 2009 na kupambana na Chelsea Uwanjani Wembley.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya Manchester United na Everton itayochezwa Aprili 19, 2009 pia Wembley.
Fainali itakuwa mwezi Mei.

LIGI KUU WIKIENDI HII:
[SAA BONGO TAIMU]
Jumamosi, 21 Machi 2009
[saa 9.45 mchana]
Portsmouth v Everton
[saa 12 jioni]
Blackburn v West Ham
Fulham v Man U
Stoke v Middlesbrough
Tottenham v Chelsea
West Bromwich v Bolton
Jumapili, 22 Machi 2009
[saa 10.30 jioni]
Wigan v Hull
[saa 12 jioni]
Man C v Sunderland
[saa 1 usiku]
Liverpool v Aston Villa
Powered By Blogger