Timu 8 zilizobaki kwenye kinyang'anyiro cha kuwania Kombe la Mabingwa wa Ligi Ulaya, UEFA CHAMPIONS LEAGUE, kesho mchana zitajua wapinzani watakaopambana nao kwenye Robo Fainali na Nusu Fainali.
Timu zilizoingia Robo Fainali ni nne kutoka England ambazo ni Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo, Manchester United, Chelsea, Liverpool na Arsenal, kutoka Hispania ni Barcelona na Villareal na nyingine ni Bayern Munich [Ujerumani] na FC Porto [Ureno].
Kwenye droo hiyo kura inakuwa huru na timu yeyote inaweza kupangwa na nyingine yeyote hata kama wanatoka nchi moja.
Tutawaletea matokeo ya droo hiyo kesho mchana kwenye saa 8 na nusu mchana saa za kibongo.
Habari nyingine:
-FA England kuchunguza tuhuma za Fabregas kumtemea mate Meneja Msaidizi wa Hull City.
FA imeingilia kati na kuwataka Mameneja wa Hull City, Phil Brown, na Msaidizi wake, Brian Horton, kuelezea kimaandishi mkasa huo wa Nahodha wa Arsenal, Cesc Fabregas, kumtemea mate Brian Horton.
Fabregas hakucheza mechi ya siku ya tukio kati ya Arsenal na Hull kwani ni majeruhi.
-Van der Sar aigomea Holland!
Kipa wa Manchester United, Edwin Van der Sar [38], ameukataa wito wa kuchezea Timu ya Taifa ya Holland uliofanywa na Meneja wa Timu ya Holland, Bert van Marwijk, ambae alimwomba Kipa huyo afute kustaafu kwake Timu ya Taifa.
Van der Sar alistaafu kuchezea Timu ya Holland mara tu baada ya EURO 2008 lakini alikubali kuidakia Holland mwezi Oktoba 2008 kwenye mechi dhidi ya Iceland na Norway wakati nchi yake ilipokabiliwa na upungufu wa Makipa baada ya wanaotumainiwa kuumia.
Meneja Bert van Marwijk alimwomba Van der Sar aidakie Holland kwenye mechi zijazo za Mchujo wa Kombe la Dunia dhidi ya Scotland Machi 28 na ile ya Macedonia Aprili 1.
No comments:
Post a Comment