Wednesday 18 March 2009

Arsenal watinga NUSU FAINALI FA CUP kwa utata! Goli la ofsaidi lawabeba, sasa kukutana na Chelsea!! Fabregas amtemea mate Meneja Msaidizi wa Hull City!!

Jana usiku, Arsenal waliokuwa wakicheza kwao Emirates na kujikuta wako nyuma kwa bao 1-0 hadi zikibaki dakika 16, waliibuka kidedea baada ya Robin van Persie kusawazisha na William Gallas kupachika bao la pili na la ushindi huku akiwa dhahiri ameotea.
Baada ya mechi, Meneja wa Hull City, Phil Brown, alidai Mchezaji wa Arsenal, Cesc Fabregas, ambae hakucheza kwani ni majeruhi wa muda mrefu na alieingia uwanjani mara baada ya mechi kwisha ili kuwapongeza wenzake, alimtemea mate Meneja Msaidizi wa Hull City, Brian Horton, wakati timu zikitoka uwanjani mwishoni mwa mechi kuelekea vyumba vya kubadilisha nguo.
Fabregas mwenyewe amekanusha tuhuma hizo.
Sasa Arsenal watacheza Nusu Fainali ya Kombe la FA hapo Aprili 18, 2009 na kupambana na Chelsea Uwanjani Wembley.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya Manchester United na Everton itayochezwa Aprili 19, 2009 pia Wembley.
Fainali itakuwa mwezi Mei.

LIGI KUU WIKIENDI HII:
[SAA BONGO TAIMU]
Jumamosi, 21 Machi 2009
[saa 9.45 mchana]
Portsmouth v Everton
[saa 12 jioni]
Blackburn v West Ham
Fulham v Man U
Stoke v Middlesbrough
Tottenham v Chelsea
West Bromwich v Bolton
Jumapili, 22 Machi 2009
[saa 10.30 jioni]
Wigan v Hull
[saa 12 jioni]
Man C v Sunderland
[saa 1 usiku]
Liverpool v Aston Villa

No comments:

Powered By Blogger