Thursday, 8 May 2008


EL CLASICO DERBY

MABINGWA WAPYA LA LIGA YA SPAIN REAL MADRID JANA WALIWABAMIZA WAPINZANI WAO WA JADI BARCELONA 4 - 1!!!!!!


REAL washeherekea kuchukua ubingwa wa Spain kwa kuitandika BARCELONA 4-1 hapo jana katika uwanja wao wa nyumbani BERNABEU.

Raul alipachika bao la kwanza, Arjen Robben la pili, Gonzalo Higuan la tatu na Ruud van Nistelrooy la nne kwa njia ya penalti. Bao la Barcelona lilifungwa na Thierry Henry.




ERIKSSON AZUNGUMZA NA BENFICA!!



Meneja wa MAN CITY, Sven-Goran Eriksson inasemekana amefanya mazungumzo na Klabu ya nchini Ureno BENFICA ila aende kuiongoza klabu hiyo akitimuliwa MAN CITY.
########################################



Wednesday, 7 May 2008


SCOLARI KWENDA MAN CITY,
ERIKSSON KUMWAGA UNGA!!!
Kuna habari zimezagaa huko Uingereza kuwa Meneja wa sasa MAN CITY, Sven-Goran Eriksson, atatimuliwa mwishoni mwa msimu huu na mmiliki wa timu hiyo Bwana Thaksin Shinawatra ambae ni Waziri Mkuu wa zamani wa nchi ya Thailand na badala yake atachukuliwa Mbrazil Luiz Felipe Scolari ambae kwa sasa ni Meneja wa Timu ya Taifa ya Ureno.
Eriksson hajazungumza chochote kuhusu uvumi wa kumwaga unga uliozagaa takriban wiki mbili sasa ingawa inasemekana ashawaambia wachezaji wake kuwa hatokuwepo msimu ujao.

WIGAN ITAPATA DONGE NONO IKIIFUNGA MAN U!!!!


WAKATI LIGI KUU UINGEREZA INATEGEMEWA KUFIKA MWISHO JUMAPILI HII HUKU CHELSEA WAKIOMBA MUNGU MAN UNITED WATELEZE KATIKA MECHI YAO NA WIGAN, WACHEZAJI NA MENEJA WA CHELSEA WAMEONEKA 'WAKIIBEMBELEZA WIGAN IIWEKEE NGUMU MAN U.

ENDAPO MAN U ATAIFUNGA TU WIGAN BASI UBINGWA UNAENDA OLD TRAFFORD!!!

NAE MENEJA WA WIGAN, STEVE BRUCE [ALIEKUWA MCHEZAJI WA ZAMANI WA MAN U] AMEJARIBU KUONDOA UTATA KWAMBA WIGAN 'ITAACHIA' KWA KUSEMA KUWA WIGAN WANACHANGAMOTO KUBWA KATIKA KUSHINDA MECHI HIYO INGAWA KWA SASA WAMESHAPONA BALAA LA KUSHUKA DARAJA.

STEVE BRUCE ALISEMA: 'SISI TUPO NAFASI YA 13 KATIKA MSIMAMO WA LIGI NA ENDAPO TUTAIFUNGA MAN U NA EVERTON WATAIFUNGA NEWCASTLE BASI TUTAMALIZA KATIKA NAFASI YA 12 NA HIVYO KUSHINDA PAUNI ZA UINGEREZA MILIONI 6 LAKI 4 LAKINI TUKIFUNGWA NA MAN U TUTAMALIZA TUKIWA NAFASI YA 15 NA HIVYO KUPATA MILIONI 4 LAKI 3 TU, HASARA YA PAUNI MILIONI 2 LAKI 1!!! SASA NANI ANADAI HATUNA SABABU YA KUSHINDA?'

Tuesday, 6 May 2008


ARSENAL MABINGWA UINGEREZA!!!!!!!!!!


WANYAKUA LIGI KUU NA KOMBE LA F.A!!!
Timu ya Wanawake ya ARSENAL HIVI JUZI ILINYAKUA KOMBE
LA F.A. LA WANAWAKE KWA KUIBAMIZA LEEDS 4-1 KATIKA FAINALI!!
KINA MAMA HAO WA ARSENAL WAMEHITIMISHA MSIMU MZURI KWAO KWANI MAPEMA WALINYAKUA UBINGWA WA UINGEREZA BAADA KUWA WA KWANZA KATIKA LIGI KUU YA KINAMAA!!!

CHELSEA 2
NEWCASTLE 0!
UBINGWA KUAMULIWA JUMAPILI!
NI MAN U
AU
CHELSEA?
Jana Chelsea waliwafunga Newcastle bao 2-0 na hivyo kuweka uhai matumaini yao kuwa wanaweza kutwaa ubingwa Jumapili, 11 MEI 2008 iwapo MAN U watateleza [wakitoka droo au wakifungwa] na huku Chelsea akishinda mechi yake na Bolton ambao nafasi yao kushuka daraja ni finyu ingawa kimahesabu wanaweza kushuka.
MAN U ANAMALIZA LIGI AKICHEZA UGENINI NYUMBANI KWA WIGAN TIMU AMBAYO JUZI WALIPOSHINDA 2-0 ZIDI YA ASTON VILLA WALIJIHAKIKISHIA KUBAKI LIGI KUU!
MAN U na WIGAN zimeshawahi kukutana mara 8 kabla huku MAN U AKISHINDA MECHI ZOTE KWA JUMLA YA MABAO 20-3!!!
******************************************************************************************************************************************
NANI ANASHUKA DARAJA?
MSIMAMO WA TIMU ZA CHINI NI:
15. SUNDERLAND POINTI 39.................. AMEPONA!!!
16. BOLTON POINTI 36........................... INAWEZAKANA KUSHUKA INGAWA...!!!
17. FULHAM POINTI 33........................... KIMBEMBE CHA KUSHUKA KIPO!!!
18. READING6 POINTI 33....................... KIMBEMBE CHA KUSHUKA KIPO!!!
19. BIRMINGHAM POINTI 32................ KIMBEMBE CHA KUSHUKA KIPO!!!
20. DERBY POINTI 11.............................. AMESHUKA DARAJA!!!!!
MECHI ZAO ZILIZOBAKI:
CHELSEA VS BOLTON
PORTSMOUTH VS FULHAM
DERBY VS READING
BIRMINGHAM VS BLACKBURN
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Monday, 5 May 2008


WEST BROMWICH ALBION NA STOKE CITY ZAPANDA DARAJA KUINGIA LIGI KUU UINGEREZA!!!!


TIMU ZA WEST BROMWICH ALBION NA STOKE CITY ZIMEINGIA LIGI KUU UINGEREZA BAADA YA KUSHIKA NAFASI MBILI ZA KWANZA KATIKA LIGI IITWAYO COCA COLA FOOTBALL LEAGUE CHAMPIONSHIP SIKU YA JUMAPILI.


West Bromwich wamechukua UBINGWA na STOKE CITY ilishika nafasi ya pili.


Timu ya tatu itakayoungana nao kupanda daraja itaamuliwa katika mtoano utaohusisha timu za HULL, BRISTOL CITY, CRYSTAL PALACE na WATFORD.

==============================================================


HUKO SPAIN, TIMU YA REAL MADRID IMETWAA UBINGWA WA LA LIGA SPAIN HUKU ZIKIWA ZIMEBAKI MECHI TATU.

REAL waliwafunga OSASUNA 2-1 na walicheza watu 10 katika mechi hiyo baada ya mchezaji wao, FABIO CANNAVARO, kutolewa kwa kadi nyekundu.


==============================================================


LIGI KUU UINGEREZA KUFIKA TAMATI JUMAPILI TAREHE 11 MEI 2008!!!


Timu zote [isipokuwa CHELSEA na NEWCASTLE wanaocheza leo JUMATATU saa 12 jioni] zimebakiza mechi moja ambazo zitachezwa JUMAPILI HII SAA 11 jioni.

Wakati Ubingwa utakuwa wa MAN U au CHELSEA, na tayari DERBY imeshashuka daraja [kuzipisha WEST BROMWICH na STOKE CITY zilizopanda daraja], timu nyingine mbili zitakazoungana na DERBY zitakuwa ama BIRMINGHAM au READING au FULHAM au BOLTON [ingawa BOLTON nafasi yake kushuka ni finyu sana!].


MATOKEO YA MECHI ZA JUMAMOSI NA JUMAPILI NI:

JUMAPILI

ARSENAL 1 EVERTON O [BENDTNER 77]

LIVERPOOL 1 MAN CITY 0 [TORRES]


JUMAMOSI

ASTON VILLA 0 WIGAN 2

BLACKBURN 3 DERBY 1

BOLTON 2 SUNDERLAND 0

FULHAM 2 BIRMINGHAM 0

MAN U 4 WEST HAM 1

BORO 2 PORTSMOUTH 0

READING 0 SPURS 1



Powered By Blogger