Wednesday 7 May 2008


SCOLARI KWENDA MAN CITY,
ERIKSSON KUMWAGA UNGA!!!
Kuna habari zimezagaa huko Uingereza kuwa Meneja wa sasa MAN CITY, Sven-Goran Eriksson, atatimuliwa mwishoni mwa msimu huu na mmiliki wa timu hiyo Bwana Thaksin Shinawatra ambae ni Waziri Mkuu wa zamani wa nchi ya Thailand na badala yake atachukuliwa Mbrazil Luiz Felipe Scolari ambae kwa sasa ni Meneja wa Timu ya Taifa ya Ureno.
Eriksson hajazungumza chochote kuhusu uvumi wa kumwaga unga uliozagaa takriban wiki mbili sasa ingawa inasemekana ashawaambia wachezaji wake kuwa hatokuwepo msimu ujao.

No comments:

Powered By Blogger