Thursday 31 December 2009

MECHI YA LIGI KUU ENGLAND JANA YAWEKA HISTORIA: Hakuna hata Mchezaji mmoja wa England aliecheza!!!
  • Waingereza waja juu!!!!
Meneja wa Blackburn Rovers Sam Allardyce ameitabiria Timu ya Taifa ya England kuwa katika hali ngumu hapo baadae baada ya mechi ya Ligi Kuu hapo jana kati ya Portsmouth na Arsenal kuweka historia ya kuwa mechi ya kwanza kabisa katika Ligi hiyo kuchezwa huku hamna hata Mchezaji mmoja Raia wa England aliecheza.
Allardyce alisema: “Kwa Timu ya Taifa, hilo linasikitisha sana! Ligi Kuu na FA lazima walitazame hilo!”
Rais wa FIFA Sepp Blatter amekuwa akipiga kampeni ya kuanzisha Sheria inayoitwa “6 jumlisha 5”, ikimaanisha Timu lazima ziwe na Wachezaji watano Raia wa Nchi yenye Ligi yake au waliolelewa na Klabu za Nchi hiyo katika mechi moja lakini hilo limekuwa likipingana na Sheria za Haki na Uhuru wa Binadamu zilizowekwa na Jumuia ya Nchi za Ulaya.
Katika mechi hiyo iliyochezwa jana Jumatano Desemba 30 ambayo Arsenal iliifunga Portsmouth 4-1, Wachezaji 22 walioanza mechi hiyo walikuwa wanatoka Nchi 15 [hamna hata mmoja toka England] huku Ufaransa ikitoa Wachezaji 7.
Kulikuwa na Wachezaji wawili kutoka Algeria, na mmoja mmoja kutoka Bosnia, Ireland, Israel, Iceland, Afrika Kusini, Scotland, Ujerumani, Spain, Belgium, Wales, Cameroun, Croatia na Urusi.
Katika Wachezaji wa Akiba kulikuwa na wanne kutoka England na wawili kati yao, Craig Esmond wa Arsenal aliingizwa badala ya Mfaransa Samir Nasri, na, Portsmouth wakamuingiza Michael Brown badala ya Richard Hughes kutoka Scotland.
Historia hiyo iliwekwa hapo jana ikiwa ni miaka 10 baada ya Chelsea kuweka historia ya kuichezesha Timu bila Mchezaji hata mmoja toka England katika mechi yao na Southampton iliyochezwa Desemba 26, 1999.
Meneja wa Sunderland Steve Bruce aliunga mkono katika kuponda hali hiyo lakini alisema: “Hatutoi Wachezaji wazuri Chipukizi na ndio maana tunahaha dunia nzima kusaka Wachezaji wenye vipaji! Kila Meneja wa Klabu za England angependa kuwa na Wachezaji wa England lakini hamna vipaji!”
Nae Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane, ambae ni Raia wa Ireland na kwa sasa ni Meneja wa Ipswich Town, alisema: “Hilo, pengine, litamuumiza kichwa Fabio Capello, Meneja wa England lakini kwangu halinikoseshi usingizi!!!”
KOMBE LA FA: Ni wikiendi ya FA, Ligi Kuu ni likizo!!!
Wikiendi hii ni mechi za Raundi ya Tatu ya Mitoano ya Kombe la FA tu na Timu za Ligi Kuu zimeingizwa rasmi na kupangiwa mechi kwenye Kombe hilo.
Timu nyingi za Ligi Kuu zinapambana na Timu za Madaraja ya chini lakini kuna baadhi ya mechi zinazozikutanisha Timu za Ligi Kuu zenyewe kama vile mechi ya Aston Villa v Blackburn, Wigan v Hull na West Ham v Arsenal.
Hivyo, wikiendi hii hamna mechi za Ligi Kuu ila Jumanne ijayo itakuwepo mechi moja ya Stoke v Fulham na Jumatano pia itakuwepo moja ya Arsenal v Bolton.
Wikiendi ya Januari 9 mechi za Ligi Kuu zitachezwa kama kawaida.
RATIBA: MECHI ZA FA CUP RAUNDI YA TATU
Jumamosi, 2 Januari 2010 [saa za bongo]
[saa 9 na nusu mchana]
Bristol City v Cardiff
[saa 12 jioni]
Accrington v Gillingham
Aston Villa v Blackburn
Blackpool v Ipswich
Bolton v Lincoln City
Brentford v Doncaster
Everton v Carlisle
Fulham v Swindon
Huddersfield v West Brom
Leicester v Swansea
MK Dons v Burnsley
Middlesbrough v Man City
Millwall v Derby
Nottingham Forest v Birmingham
Plymouth v Newcastle
Portsmouth v Coventry
Preston v Colchester
Scunthorpe v Barnsley
Sheffield Wednesday v Crystal Palace
Southampton v Luton
Stoke v York
Sunderland v Barrow
Torquay v Brighton
Tottenham v Peterborough
Wigan v Hull
[saa 2 na robo usiku]
Reading v Liverpool
Jumapili, 3 JanuarI 2010
[saa 10 jioni]
Man U v Leeds United
[saa 12 jioni]
Chelsea v Watford
Notts County v Forest Green
Sheffield United v QPR
[saa 1 na robo usiku]
West Ham v Arsenal
[saa 2 na robo usiku]
Tranmere v Wolves
Tembo kutua Bongo Jumamosi
Timu ya Taifa ya Cote D’ivoire, maarufu kama Tembo, watatua Dar es Salaam Jumamosi ili kupiga kambi ya mazoezi kwa matayarisho ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazoanza kuchezwa huko Angola Januari 10.
Tembo watacheza na Timu ya Taifa ya Bongo, Taifa Stars, Uwanja wa Taifa Jumatatu usiku.
Kikosi hicho cha Ivory Coast kitawasili kikiwa na Watu 50.
Viingilio kwenye mechi hiyo ni kuanzia Shilingi 50,000/= hadi 5,000/=.
Tembo hao watakuwa na Mastaa wao kina Didier Drogba, Solomon Kalou, Yaya Toure, Aruna Dindane, Habib Kolo Toure na wengineo.
USHINDI WA 5-0 KWA WIGAN: Fergie aisifia Timu yake:
• Timu yote ilicheza murua!
• Rooney alikuwa kiboko!
Sir Alex Ferguson amesema alikuwa kwenye Xmas mbaya baada ya kufungwa mechi mbili dhidi ya Fulham 3-0 na Villa 1-0 lakini, baada ya kuikung’uta Wigan 5-0 hapo jana, yuko tayari kusherehekea bethdei yake akitimiza miaka 68 leo na pia mkesha wa Mwaka mpya.
Meneja huyo wa Manchester United anaamini Timu yake iko kwenye nafasi nzuri kuiandama Chelsea inayoongoza Ligi kwa vile tu wako pointi mbili nyuma yao.
Ferguson akizungumzia mechi ya jana alisema: “Wachezaji walijua ni lazima kufunga magoli kwani mwishoni mwa Ligi nani anajua pengine tofauti ya magoli itakuwa muhimu!”
Kero kubwa kwa Wigan hapo jana ilikuwa ni Winga wa Man U Antonio Valencia ambae Man U walimnunua kutoka Wigan mwanzoni mwa Msimu huu kwa Pauni Milioni 16. Valencia alifunga bao moja na kutengeneza matatu hapo jana.
Ferguson amesema: “Kwetu, muhimu ni kuwa Valencia alifunga goli moja na hilo ni goli lake la 6. Atafunga mengine zaidi msimu huu!!”
Kuhusu Rooney, ambae alifunga bao lake la 14 katika mechi 19 za Ligi, Ferguson amemsifu na kumwita ni kiboko.
Akizungumzia mechi ijayo ya Jumapili watakapocheza na Leeds United kwenye Kombe la FA, Ferguson amesema Kikosi tofauti kitacheza kikiwa na Chipukizi huku akidokeza Nahodha wake Gary Neville yuko fiti, Jonny Evans sasa yuko mazoezini na Ro Ferdinand tayari ameanza mazoezi.
Man United 5 Wigan 0
Manchester United, wakiwa nyumbani Old Trafford, wameibamiza Wigan mabao 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu England na kujichimbia nafasi ya pili kwenye Ligi hiyo wakiwa na pointi 43 kwa mechi 20 huku vinara Chelsea wakiwa na pointi 45 kwa mechi 20.
Katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi, Man U waliibamiza Wigan 5-0 Uwanja wa DW, nyumbani kwa Wigan, na mabao yote kwenye mechi hiyo yalifungwa kipindi cha pili.
Lakini katika mechi ya leo, hadi mapumziko Man U walikuwa mbele kwa mabao 3-0 Wafungaji wakiwa Wayne Rooney, dakika ya 28, Carrick, dakika ya 31 na Rafael dakika ya 44.
Kipindi cha pili Berbatov akapiga bao la 4 dakika ya 49 na Valencia akapachika la 5 dakika ya 74.
VIKOSI:
Man Utd: Kuszczak, Rafael Da Silva, Brown, Vidic, Evra, Valencia, Carrick, Fletcher, Park, Berbatov, Rooney.
AKIBA: Amos, Neville, Owen, Anderson, Welbeck, Fabio Da Silva, Obertan.
Wigan: Kirkland, Melchiot, Boyce, Bramble, Figueroa, Gomez, Thomas, Cho, Scharner, N'Zogbia, Rodallega.
AKIBA: Pollitt, Edman, Amaya, Scotland, Koumas, Sinclair, McCarthy.
REFA: Lee Mason
Portsmouth 1 Arsenal 4
Timu iliyo mkiani kwenye Ligi Kuu, Portsmouth, leo uwanjani kwao Fratton Park wamezidi kupigiliwa misumari huko chini baada ya kupata kichapo cha mabao 4-1 toka kwa Arsenal kwenye mechi ya Ligi Kuu.
Kwa ushindi huu, Arsenal wamefikisha pointi 41 kwa mechi 19 na wako nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Man U walio nafasi ya pili wakiwa na pointi 43 kwa mechi 20.
Hadi mapumziko Arsenal ilikuwa mbele kwa bao 2 Wafungaji wakiwa Eduardo, dakika ya 27 na Nasri dakika ya 42.
Kipindi cha pili Arsenal wakaongeza bao 2 kupitia Ramsey na Song.
Bao la Portsmouth lilifungwa na Nadir Belhadj.
VIKOSI:
Portsmouth: Begovic, Finnan, Kaboul, Ben-Haim, Hreidarsson, Yebda, Mokoena, Hughes, Belhadj, Boateng, Piquionne.
AKIBA: Ashdown, Diop, Brown, Utaka, Vanden Borre, Kanu, Wilson.
Arsenal: Almunia, Sagna, Gallas, Vermaelen, Traore, Ramsey, Song Billong, Diaby, Nasri, Eduardo, Arshavin.
AKIBA: Fabianski, Rosicky, Vela, Silvestre, Wilshere, Merida, Eastmond.

Wednesday 30 December 2009

Meneja Bolton apigwa Shoka!!
Bolton Wanderers imethibitisha kuwa Meneja wao Gary Megson amefukuzwa kazi.
Megson alichukua Umeneja hapo Bolton Oktoba 2007 na katika msimu wake wa kwanza aliinusuru Klabu hiyo kushushwa Daraja na msimu uliokwisha aliinyanyua Timu na kumaliza nafasi ya 13 kwenye Ligi.
Lakini msimu huu, Timu hiyo imekuwa ikiyumba na katika mechi ya jana, wakiwa nyumbani, waliupoteza uongozi wa bao 2-0 na kuwaruhusu Hull City kupata sare ya 2-2.
Kimsimamo, Bolton wako nafasi ya 18 na wana pointi 18 kwenye Ligi ikiwa ni nafasi ya kushushwa Daraja ingawa wamecheza mechi chache (mechi 18) ukilinganisha na Timu nyingi zilizocheza mechi 20.
Wadau wengi wa Bolton wamekuwa hawampendi Megson na hata jana mara baada ya mechi na Hull kumalizika mwenyewe Megson alikiri Mashabiki wa Bolton hawamtaki.
Bolton imetangaza kuwa Timu itasimamiwa na Meneja Msaidizi Chris Evans ambae atasaidiwa na Kocha wa Timu ya Kwanza Steve Wegley.
Fergie: Ubingwa ni mbio za mtu 2!!!
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson anategemea kinyang’anyiro cha Ubingwa wa Ligi Kuu ni kupiganiwa na Timu mbili tu ambazo ni Man U na Chelsea huku Timu nyingine zinazoweka ngumu wakati huu kupukutika kadri Ligi inavyosonga mbele.
Ferguson amesema: “Kwa sasa haionekani hivyo lakini historia inatuambia ni Timu mbili tu ndizo zitakuwa wababe wa kugombea taji!! Chelsea ni hatari kubwa kwa sababu wana uzoefu mkubwa!”
Ferguson alitamka mwanzoni mwa msimu kuwa Chelsea ndie atakuwa mshindani wao mkubwa, na, licha ya upinzani mkubwa unaoonyeshwa na Timu mbalimbali kwa sasa, Ferguson bado anaamini Chelsea ndio tishio.
Ferguson amesisitiza: “Mwanzoni mwa msimu niliwaona Chelsea ndio tishio kubwa na bado sijabadili mawazo!”
Ukichukulia majeruhi yaliyowakumba Manchester United, na sasa Kipa Edwin van der Sar kwenda likizo ya muda usiojulikana kumuuguza mkewe ambae ni mgojwa sana, Man U kuwa nyuma ya vinara Chelsea kwa pointi chache kwenye Ligi ni kitu kinachowatia imani kubwa Wadau wa Mabingwa hao Watetezi.
Vilevile, kuweza kufunga mabao 40 katika mechi 19 za Ligi ni kitu cha mvuto hasa ukizingatia pengo la Mfungaji wao bora msimu uliopita, Cristiano Ronaldo, alietimkia Real Madrid.
Ferguson ametamka: “Watu wamechukulia kumpoteza Ronaldo kama pigo kubwa! Wamehisi hatuwezi kuwa wazuri kama alivyokuwepo! Ronaldo ni Mchezaji Bora sana! Lakini sisi tumebadilika na ukweli ni kuwa msimu uliokwisha baada ya mechi 19 tulikuwa na pointi 41, msimu huu kwa mechi 19 tuna pointi 40!!”
Kigoli cha ‘babu’ chaipa ushindi Liverpool, Bolton v Hull ngoma ngumu!!!
Kigoli cha dakika za majeruhi, dakika ya 93, lilolifumaniwa na Fernando Torres limewapa ushindi Liverpool wa bao 1-0 huko Villa Park dhidi ya Wenyeji Aston Villa ambao hiki ni kipigo chao cha pili mfululizo kwenye Ligi Kuu baada ya kudundwa 3-0 na Arsenal mechi iliyopita.
Kwa ushindi huo, Liverpool sasa imeipiku Birmingham na kuchukua nafasi ya 7 kwenye msimamo wa Ligi.
Katika mechi nyingine ya Ligi Kuu iliyochezwa jana, Bolton na Hull City zilitoka sare 2-2.
Hull City walikuwa nyuma 2-0 kwa mabao ya Ivan Klasnic dakika ya 20 na dakika ya 61 Kevin Davies alifunga kwa kichwa bao la pili lakini mabao mawili ya Stephen Hunt yaliiwezesha Hull kupata droo.
MECHI ZA LIGI LEO: Jumatano, 30 Desemba 2009
[saa za bongo]
[saa 4 dak 45 usiku]
Portsmouth v Arsenal
[saa 5 usiku]
Man U v Wigan

Tuesday 29 December 2009

LEO NI:
• Aston Villa v Liverpool
• Bolton v Hull City
Leo usiku kutakuwa na mechi mbili za Ligi Kuu England kati ya Aston Villa v Liverpool na nyingine ni Bolton v Hull.
Kwa Mashabiki wengi mechi yenye mvuto zaidi ni ile kati ya Villa v Liverpool itakayochezwa Villa Park kwa sababu tu Villa Msimu huu imechachamaa kuwania kumaliza Ligi ikiwa kwenye Timu Bora nne ili wafuzu kucheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE Msimu ujao na Liverpool awali iliota kutwaa Ubingwa Msimu huu lakini baada ya mwendo mbovu, ikiwemo kufungwa mechi 7 za Ligi na sare nyingi, sasa wako nafasi ya 8 kwenye Ligi na, bila shaka, wanaombea tu kumaliza wakiwa kwenye Timu Bora nne.
Villa katika mechi yake ya mwisho ilitandikwa mabao 3-0 na Arsenal Uwanjani Emirates na leo itashuka kwao ikitaka kufuta matokeo hayo mabaya.
Liverpool walishinda mechi yao ya mwisho kwa bao 2-0 dhidi ya Wolves walipokuwa nyumbani Anfield.
Katika mechi ya leo, Villa watamkosa Winga wao machachari Ashley Young ambae ana adhabu ya kufungiwa mechi moja baada ya kupata jumla ya Kadi 5 za Njano.
Liverpool watamkosa Kiungo wao mahiri kutoka Argentina Javier Mascherano ambae ana adhabu ya kufungiwa mechi.
Refa katika mechi hiyo ni Peter Walton.
Van der Sar kapewa likizo, Nani kuuzwa?
Edwin van der Sar amepewa likizo ya dharura na Manchester United baada ya mkewe kuugua ghafla huko kwao Uholanzi na inasemekana hali yake si nzuri.
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amemruhusu Van der Sar kumuuguza mkewe hadi hali yake itakapotengamaa.
Van der Sar hajaichezea Man U tangu November 21 walipoifunga Everton 3-0 kwenye Ligi Kuu alipoumia goti.
Inategemewa Makipa Tomasz Kuszczak au Ben Foster ndio watakaokaa golini kwenye mechi ya kesho ya Ligi Kuu na Wigan huko Old Trafford.
Lakini katika siku za hivi kribuni Tomasz Kuszczak ndio amekuwa akidaka kila mechi.
Wakati huohuo, kuna uvumi mkubwa kuwa huenda Winga wa Man U Nani akatimkia Spain au Italy mwezi Januari dirisha la uhamisho likifunguliwa na inasemekana pia huenda akarudi kwao Ureno na kuchezea Benfica ili Man U wamchukue Nyota Chipukizi toka Argentina Angel di Maria toka Klabu hiyo.
Wakala wa Nani, Jorge Mendez, amedokeza kuwa yupo mbioni kushughulikia suala la Nani.
Kuwafunga “Vibonde” wawili, Mancini aota Ubingwa Man City!!
Roberto Mancini, Meneja mpya wa Manchester City, ambaye alianza himaya yake kwa kuwafunga ‘Vibonde’ Stoke City 2-0 Desemba 26 na kisha jana kuibwaga Wolves 3-0, ameanza majigambo na kudai Timu yake ni nzuri sana kuliko alivyofikiria mwanzo na wana uwezo wa kutwaa Ubingwa wa England.
Awali, alipoingia tu Man City wiki moja iliyopita, Mancini alitangaza lengo lake ni kumaliza miongoni mwa Timu Bora nne Msimu huu na kisha kutwaa Ubingwa Msimu ujao.
Mancini ametamba: “Tumebakiza mechi 19 za Ligi na uwezo tunao wa kuwa Mabingwa! Tuna Timu nzuri!”
Mancini aliongeza kwa kusema wiki yake ya kwanza hapo Man City imekuwa nzuri ingawa ana listi ya majeruhi kibao wakiwemo Wachezaji kina Stephen Ireland, Roque Santa Cruz, Joleon Lescott, Wayne Bridge, Shaun Wright-Phillips na Nedum Onuoha.
Vilevile, atawakosa Kolo Toure na Emmanuel Adebayor kwa mwezi Januari watakaposafiri kwenda kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko Angola.
LIGI KUU England: Chelsea kileleni!!!
• Goli la kujifunga wenyewe laipa ushindi Chelsea!!!
• Man City ushindi wa pili kwa Mancini!!!!
Kwenye mechi za jana za Ligi Kuu, Chelsea wakiwa ngomeni kwao Stamford Bridge walikuwa nyuma kwa bao 1-0 hadi mapumziko lakini kipindi cha pili wakapata mabao mawili moja likiwa la kujifunga wenyewe na kuilaza Timu ngumu Fulham 2-1.
Fulham walipata bao lao kupitia Gera dakika ya 4 na Drogba akaisawzishia Chelsea dakika ya 73.
Lakini dakika ya 75, Chris Smalling wa Fulham akajifunga mwenyewe na kuipa Chelsea ushindi wasiostahili.
Kwa ushindi huo, Chelsea wako mbele kwenye Ligi wakiwa na pointi 45 kwa mechi 20 wakifuatiwa na Manchester United, wanaocheza kesho na Wigan, wakiwa na pointi 40 kwa mechi 19. Timu ya 3 ni Arsenal, pia wanacheza kesho na ugenini na Portsmouth, na wana pointi 38 kwa mechi 18.
Nao Manchester City, wakicheza mechi yao ya pili chini ya Meneja mpya Roberto Mancini, wameshinda mechi yao ya pili baada ya kuikung’uta Wolves 3-0 ugenini.
Mabao ya Man City yalifungwa na Tevez, dakika ya 33 na 86, na Garrido dakika ya 69.
Tottenham Hotspurs, baada ya kuwafunga West Ham 2-0, sasa wameikwaa nafasi ya 4 kwenye Ligi wakiwa na pointi 37 kwa mechi 20.
MSIMAMO kileleni mwa LIGI KUU England: [Timu zimecheza mechi 20 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea pointi 45
2 Man Utd pointi 40 [mechi 19]
3 Arsenal pointi 38 [mechi 18]
4 Tottenham pointi 37
5 Aston Villa pointi 35 [mechi 19]
6 Man City pointi 35 [mechi 19]
7 Birmingham pointi 32
8 Liverpool pointi 30 [mechi 19]
9 Fulham pointi 27 [mechi 19]
10 Sunderland pointi 23
MECHI ZA LIGI KUU LEO: Jumanne, 29 Desemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
Aston Villa v Liverpool
[saa 5 usiku]
Bolton v Hull

Monday 28 December 2009

MATOKEO ZA LIGI KUU England: Jumatatu, 28 Desemba 2009
Tottenham 2 v West Ham 0
Blackburn 2 v Sunderland 2
Chelsea 2 v Fulham 1
Everton 2 v Burnley 0
Stoke 0 v Birmingham 1
MECHI INAYOFUATA [saa 4 dak 45 usiku saa za bongo]
Wolves v Man City
MECHI ZA LIGI KUU ZIJAZO:
[saa za bongo]
Jumanne, 29 Desemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
Aston Villa v Liverpool
[saa 5 usiku]
Bolton v Hull
Jumatano, 30 Desemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
Portsmouth v Arsenal
[saa 5 usiku]
Man U v Wigan
MECHI MFULULIZO ENGLAND!!
Wiki yote hii kutakuwa na uhondo mfululizo wa mechi za Ligi Kuu England kisha Jumamosi tarehe 2 Januari 2010 Timu za Ligi Kuu England zitajimwaga kwa mara ya kwanza ndani ya viwanja mbalimbali kugombea Kombe la FA hiyo ikiwa ni Raundi ya 3 ya Kombe hilo maarufu.
Hivyo, kwa sababu ya Kombe hilo la FA, wikiendi ijayo kutakuwa hamna mapambano ya Ligi Kuu na mechi za Ligi zitachezwa Jumanne tarehe 5 Januari na Jumatano tarehe 6 Januari na kisha kuendelea kama kawaida wikiendi ya tarehe 9 Januari.
Vilevile, Jumanne Januari 5 kutakuwa na mechi ya Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Carling kati ya Blackburn na Aston Villa na Jumatano Januari 6 ni Nusu Fainali ya pili ya Kombe la Carling kati ya Mahasimu Manchester City na Manchester United.
Mechi hizo za Nusu Fainali za Kombe la Carling zinachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini na marudiano yake ni Januari 19 na 20.
Ratiba kamili kuanzia kesho ni:
Jumanne, 29 Decemba 2009
LIGI KUU England
Aston Villa v Liverpool
Bolton v Hull
Jumatano, 30 Decemba 2009
LIGI KUU England
Man Utd v Wigan
Portsmouth v Arsenal
Jumamosi, 2 Januari 2010
KOMBE LA FA
Accrington Stanley v Gillingham
Aston Villa v Blackburn
Blackpool v Ipswich
Bolton v Lincoln City
Brentford v Doncaster
Bristol City v Cardiff
Everton v Carlisle
Fulham v Swindon
Huddersfield v West Brom
Leicester v Swansea
Middlesbrough v Man City
Millwall v Derby
MK Dons v Burnley
Nottm Forest v Birmingham
Plymouth v Newcastle
Portsmouth v Coventry
Preston v Colchester
Reading v Liverpool
Scunthorpe v Barnsley
Sheff Wed v Crystal Palace
Southampton v Luton
Stoke v York
Sunderland v Barrow
Torquay v Brighton
Tottenham v Peterborough
Wigan v Hull
Jumanne, 5 Januari 2010
KOMBE LA CARLING, NUSU FAINALI, MECHI YA KWANZA
Blackburn v Aston Villa
LIGI KUU England
Stoke v Fulham
Jumatano, 6 Januari 2010
KOMBE LA CARLING, NUSU FAINALI, MECHI YA KWANZA
Man City v Man U
LIGI KUU England
Arsenal v Bolton
Jumamosi, 9 Januari 2010
LIGI KUU England
Arsenal v Everton
Birmingham v Man U
Burnley v Stoke
Fulham v Portsmouth
Hull v Chelsea
Sunderland v Bolton
Wigan vAston Villa
Jumapili, 10 Januari 2010
LIGI KUU England
Liverpool v Tottenham
West Ham v Wolves
Jumatatu, 11 Januari 2010
LIGI KUU England
Man City v Blackburn
Tottenham 2 West Ham 0
Kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa leo White Hart Lane nyumbani kwa Tottenham Hotspurs na kumalizika punde tu, wenyeji walimudu kuifunga West Ham mabao 2-0 na kujikita nafasi ya 4 kwenye msimamo wa Ligi huku wakiwa na pointi 37.
Luka Modric ambae hajaichezea Tottenham tangu mwezi Agosti alipovunjika mguu aliifungia Timu yake bao la kwanza baada ya kupokea pasi nzuri toka kwa Winga Aaron Lennon kwenye dakika ya 11.
Hadi mapumziko Tottenham 1 West Ham 0.
Kipindi cha pili dakika ya 81, Jermaine Defoe alipachika bao la pili kufuatia kaunta ataki murua ya Tottenham.
VIKOSI:
Tottenham: Gomes, Corluka, Dawson, King, Assou-Ekotto, Lennon, Palacios, Huddlestone, Modric, Crouch, Defoe.
AKIBA: Alnwick, Hutton, Bale, Jenas, Keane, Bassong, Kranjcar.
West Ham: Green, Faubert, Tomkins, Upson, Ilunga, Collison, Behrami, Kovac, Parker, Diamanti, Franco.
AKIBA: Stech, Jimenez, Spector, Da Costa, Nouble, Payne, Stanislas.
REFA: Chris Foy
Mechi za LIGI KUU England zinazofuata na zitakazoanza muda si mrefu ni:
Blackburn v Sunderland
Chelsea v Fulham
Everton v Burnley
Stoke v Birmingham
[saa 4 dak 45 usiku]
Wolves v Man City
Ancelotti akiri Chelsea taabani!!!
Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti amekubali kuwa Timu yake Chelsea kwa sasa ipo hoi bin taabani kufuatia matokeo yasiyoridhisha katika mechi za hivi karibuni na kudorora kwao kumefuatia mara baada ya kuikung’uta Arsenal 3-0 kwenye Ligi Kuu mwezi uliopita.
Tangu ushindi huo wa kishindo Chelsea wameshinda mechi moja tu katika 5 walizocheza na sasa wapinzani wao Manchester United na Arsenal wameikaribia mno kwenye msimamo wa Ligi.
Chelsea bado wanaongoza Ligi Kuu wakiwa na pointi 42 wakifuatiwa na Man Uwenye pointi 40 na Arsenal pointi 38.
Ancelotti amekiri kupwaya kwao na amesema: “Ni kweli tumepoteza mwelekeo lakini bado tuna uwezo wa kutwaa Ubingwa! Ni mbio ndefu na sasa tuko Nusu tu!”
Leo jioni Chelsea watakuwa nyumbani Stamford Bridge kuikwaa Timu ngumu Fulham kwenye mechi ya Ligi Kuu.
Rooney apona kuzivaa hasira za Fergie!!!
Wayne Rooney amepona kukumbana na hasira za Meneja wake Sir Alex Ferguson hapo jana baada ya kufanya kosa kubwa lililoisaidia Hull City kupata bao la kusawazisha kwenye mechi ya Ligi Kuu ambayo hatimaye Manchester United walishinda mabao 3-1.
Rooney ndie aliewafungia Man U bao la kwanza dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili Rooney alifanya kosa kubwa pale pasi yake aliyotaka kumrudishia Kipa wake Kuszczak kunaswa na Craig Fagan aliemtilia pasi mwenzake Altidore lakini aliangushwa na Beki wa Man U Rafael kwenye boksi na ndipo Fagan akasawazisha kwa penalti.
Rooney amesema: “Goli lao la kusawazisha ni kosa langu! Meneja wangu asingefurahishwa lakini bahati tumeshinda!”
Baada ya kosa lake, Rooney alicheza kufa na kupona na kusababisha bao la pili pale krosi yake ilipombabaisha Beki wa Hull Andy Dawson na kujifunga mwenyewe.
Kisha Rooney akatengeneza bao la 3 na kumpa pasi Berbatov aliepachika bao hilo.
Ferguson alimsifia Rooney kwa kusema: “Ni mpiganaji! Alifanya kosa moja lakini yeye ni mshindi! Alijisahihisha na kuutengeneza ushindi wetu!”
Kwa goli lake la jana sasa Rooney ana magoli 13 kwenye Ligi Kuu na amefungana na Defoe pamoja na Drogba katika Ufungaji goli nyingi.

Sunday 27 December 2009

Man U yaidunda Hull na kurudi nafasi ya 2!!!
Kwa mara ya kwanza katika mechi karibu 5, Manchester United leo walishuka ugenini uwanja wa KC kupambana na Hull City kwenye mechi ya Ligi Kuu huku wakiwa na Difensi ambayo inatambulika na si ile ya kuungaunga iliyowafanya wachapwe na Villa na Fulham.

Leo Beki ilichezwa na Rafael pembeni kulia, Evra pembeni kushoto na Dabo Sentahafu ilichezwa na Wes Brown na Nemanja Vidic.
Carrick na Fletcher ambao ndio walikuwa wakicheza kama Masentahafu katika mechi za hivi karibuni, kwenye mechi hii walirudi kwenye nafasi zao za kawaida za Kiungo.
Na Kikosi hicho kilichokuwa na uwiano hakikuwaangusha Washabiki wa Man U kwani waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 na hivyo kuipiku Arsenal na kutinga nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi huku Chelsea bado wakiongoza wakiwa na pointi 42, Man U 40, Arsenal 38 na Aston Villa 35. 
Wayne Rooney alifunga bao la kwanza Kipindi cha Kwanza kwenye dakika za majeruhi baada ya kazi nzuri kwenye wingi ya kulia ya Darren Fletcher alietia krosi iliyoguswa na Giggs na kumkuta Rooney alieidokoa hadi wavuni.
Kipindi cha pili Hull walisawazisha kwa penalti iliyofungwa na Craig Fagan dakika ya 14 baada ya pasi ya Rooney kunaswa na Fagan aliempasia Jozy Altidore ambae aliangushwa na Rafael wa Man U na Refa Alan Wiley kuamua ni penalti.
Katika dakika ya 28 ya Kipindi hicho cha Pili, Man U walifunga bao la pili baada ya Giggs kumpenyezea Rooney aliepiga krosi ili imfikie Park [alieingizwa badala ya Valencia] lakini Beki wa Hull Andy Dawson akajifunga mwenyewe.
Dimitar Berbatov akaweka wavuni bao dakika ya 82 baada ya pande tamu kutoka kwa Wayne Rooney.
VIKOSI:
Hull: Myhill, Mendy, Gardner, Zayatte, Dawson, Garcia, Boateng, Olofinjana, Hunt, Altidore, Fagan.
AKIBA: Duke, Barmby, Geovanni, Kilbane, Ghilas, Vennegoor of Hesselink, Cairney.
Man Utd: Kuszczak, Rafael Da Silva, Vidic, Brown, Evra, Valencia, Carrick, Fletcher, Giggs, Berbatov, Rooney.
AKIBA: Foster, Owen, Park, Welbeck, Fabio Da Silva, Obertan, De Laet.
REFA: Alan Wiley
MECHI ZINAZOKUJA ZA LIGI KUU England: [saa za bongo]
Jumatatu, 28 Desemba 2009
[saa 9 dak 45 mchana]
Tottenham v West Ham
[saa 12 jioni]
Blackburn v Sunderland
Chelsea v Fulham
Everton v Burnley
Stoke v Birmingham
[saa 4 dak 45 usiku]
Wolves v Man City
Jumanne, 29 Desemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
Aston Villa v Liverpool
[saa 5 usiku]
Bolton v Hull
Jumatano, 30 Desemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
Portsmouth v Arsenal
[saa 5 usiku]
Man U v Wigan
Fabregas aipa ushindi Arsenal lakini...........!!!!!!!
Nahodha wa Arsenal Cesc Fabregas ambae leo ndie alieipa ushindi Timu yake baada ya kuingizwa Kipindi cha Pili na kufunga bao 2 zilizoipa ushindi Arsenal wa bao 3-0 dhidi ya Aston Villa kwenye Ligi Kuu Uwanjani Emirates alilazimika kutolewa huku zikiwa zimebaki dakika 6 mpira kumalizika baada ya kujitonesha sehemu aliyoumia hivi karibuni na ambayo ndio iliyomfanya asianze mechi hii tangu mwanzo.
Taarifa zinasema kuna hatari Fabregas akawa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja baada ya kujiumiza tena musuli ule ule wa mguu uliomfanya akose mechi hivi karibuni.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amethibitisha habari za kuumia Nahodha wake ingawa amesema bado hawajajua atakuwa nje kwa muda gani. 
Wenger vilivile alidokeza kuwa mwezi Januari wanaweza kuingia sokoni dirisha la uhamisho litakapofunguka kununua Mshambuliaji mmoja ili kuziba pengo la Robin van Persie ambae atakuwa nje mpaka Aprili au Mei kuuguza enka yake.
Mitutu ikiongozwa na Fabregas yaiua Villa!!
Katika mechi ya Ligi Kuu leo Arsenal wakiwa nyumbani Uwanjani Emirates wameipiga Aston Villa mabao 3-0 na mabao mawili ya kwanza yakifungwa na Nahodha wao Cesc Fabregas alieanza mechi hii akiwa benchi na kuingizwa mara baada ya Kipindi cha Pili kuanza.
Fabregas alifunga bao la kwanza kwa frikiki murua kwenye dakika ya 65 na kuongeza bao la pili baada ya pasi tamu ya Theo Walcott dakika ya 80.
Abou Diaby akaongeza bao la 3 dakika ya 90.
Kwa ushindi huo, Arsenal sasa wako nafasi ya pili na wamecheza mechi 18 na wana pointi 38 na wako nyuma ya Chelsea wanaoongoza kwa kuwa na pointi 42 kwa mechi 19.
Mabingwa Watetezi Manchester United, wanaocheza na Hull City muda si mrefu kuanzia sasa, wako nafasi ya 3 wakiwa wamecheza mechi 18 na wana pointi 37.
Aston Villa wako nafasi ya 4, wamecheza mechi 19 na wana pointi 35.
VIKOSI:
Arsenal: Almunia, Sagna, Gallas, Vermaelen, Traore, Song Billong, Denilson, Nasri, Diaby, Eduardo, Arshavin.
AKIBA: Fabianski, Fabregas, Vela, Walcott, Ramsey, Silvestre, Eboue.
Aston Villa: Friedel, Luke Young, Dunne, Cuellar, Warnock, Ashley Young, Petrov, Milner, Downing, Agbonlahor, Heskey.
AKIBA: Guzan, Sidwell, Carew, Delph, Reo-Coker, Beye, Collins.
DAVID JAMES ataka kuhamia Spurs!
Kipa wa Portsmouth David James, miaka 39, ambae pia hudakia Timu ya England, ameonyesha dhamira yake ya kuungana tena na aliekuwa Meneja wa Portsmouth ambae sasa yupo Tottenham, Harry Redknapp, ili fufue matumaini yake ya kuitwa Kikosi cha England kitachokwenda Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani.
James amesema: “Ni bora kuchezea Spurs, huko nafasi yangu ya kuchezea England itaongezeka! Harry ni Kocha bora na ndio maana Spurs wana mafanikio!”
Huko Tottenham, Kipa wao wa akiba, Carlo Cudicini, yupo nje baada ya kuumia kwenye ajali ya pikipiki na hilo litamfanya James awe Kipa Msaidizi chini ya Kipa kutoka Brazil Heurelho Gomes ambae siku za nyuma alionekana kupwaya.
Hata hivyo, Meneja wa sasa wa Portsmouth, Avram Grant, hayuko tayari kumwachia David James kuondoka ingawa anaweza kulazimika kumwachia kwa vile Portsmouth ina matatizo makubwa ya fedha.
LIVERPOOL yashinda kwa “msaada wa Refa!”
Jana Liverpool iliweza kuwafunga Wolves 2-0 kwenye Ligi Kuu baada ya Wolves kucheza mtu 10 mara baada ya Refa Andre Marriner kumtoa Stepen Ward kwa Kadi Nyekundu baada ya kumpa kadi ya pili ya Njano katika mazingira ya utatanisha.
Refa Marriner kwanza alimpa Kadi ya Njano Berra kwa rafu ambayo Ward alimchezea Lucas Leiva wa Liverpool lakini baada ya Wachezaji wa Liverpool kulalamika, Refa huyo aliongea na Msaidizi wake na ndipo alipompa Kadi ya Pili ya Njano Ward na kisha kumwonyesha Nyekundu na kumtoa.
Uamuzi huo uliwapa mwanya Liverpool waliofunga bao la kwanza kupitia Steven Gerrard na la pili akafunga Yossi Benayoun.
WOLVES walalamikia Refa kuibeba Liverpool!!!
Bosi wa Wolves Mick McCarthy amepinga vikali kutolewa Mchezaji wake Stephen Ward na Refa Andre Marriner ambae alimpa Kadi 2 za Njano na kisha Nyekundu na hivyo kuwapa mwanya Liverpool kupata bao 2 baada ya Wolves kubaki mtu 10.
Refa Marriner kwanza alimpa Kadi ya Njano Berra kwa rafu ambayo Ward alimchezea Lucas Leiva wa Liverpool lakini baada ya Wachezaji wa Liverpool kulalamika, Refa huyo aliongea na Msaidizi wake na ndipo alipompa Kadi ya Pili ya Njano Ward na kisha kumwonyesha Nyekundu na kumtoa.
McCarthy amedai: “Nimeona marudiao ya video! Sidhani alistahili kutolewa nje! Refa hakupata msaada wowote toka kwa Mwamuzi wa akiba Phil Dowd! Na pale alipompa KadI Berra na kulalamikiwa na Wachezaji wa Liverpool alilazimika kumpa Kadi Ward!! Hayo ni makosa kwa Refa kukubalisha presha ya Wachezaji!”
MANCINI aanza kibarua kwa ushindi!!
Meneja mpya wa Manchester CityRoberto Mancini ameanza kibarua kwa mguu mzuri baada ya kuwafunga Stoke City 2-0 hapo jana kwenye Ligi Kuu lakini amekiri kuwa Timu yake inabidi iongeze juhudi na kukaza uzi.
Mancini amembadili Meneja Mark Hughes Jumamosi iliyopita na mechi ya jana ilikuwa ndio mechi yake ya kwanza ambapo Martin Petrov na Carlos Tevez ndio waliomfungia mabao ya ushindi yaliyopatikana kipindi cha kwanza.
Wenger haitaki mipira ya kurusha!!
Arsene Wenger wa Arsenal amependekeza kuwa badala ya mipira kurushwa ikitoka pembeni mwa uwanja ziwe zinapigwa frikiki ili kuharakisha mchezo.
Mfaransa huyo pia amedai kuwa baadhi ya Timu kwenye Ligi kuu hunufaiki zaidi kwa vile tu wanao Wachezaji wenye nguvu ya kurusha mipira mbali na akatoa mfano wa Mchezaji wa Stoke City Rory Delap ambae akirusha mpira ni kama kaupiga kwa mguu na mara nyingi huipa ushindi Stoke kwa mipira ya kurusha.
Wenger amedai: “ Sheria ibadilishwe! Soka ni mpira wa miguu na si mikono!”

Saturday 26 December 2009

LIGI KUU England: MATOKEO MECHI ZA LEO Jumamosi, 26 Desemba 2009:
Birmingham 0 v Chelsea 0
Fulham 0 v Tottenham 0
West Ham 2 v Portsmouth 0
Burnley 1 v Bolton 1
Man City 2 v Stoke 0
Sunderland 1 v Everton 1
Wigan 1 v Blackburn 1
[MECHI INAANZA saa 2 na nusu usiku saa za bongo]
Liverpool v Wolves
MECHI ZA KESHO Jumapili, 27 Desemba 2009
[saa 10 na nusu jioni]
Arsenal v Aston Villa
[saa 1 usiku]
Hull v Man U
Chelsea wakwaa kisiki kwa Mtakatifu Andrews!!!
Timu vinara wa Ligi Kuu, Chelsea, leo Boksingi Dei Desemba 26, wameambulia pointi moja tu ugenini uwanja wa Mtakatifu Andrews walipotoka suluhu 0-0 na Wenyeji Birmigham.
Mchezaji wa Chelsea, Florent Malouda, alipewa Kadi Nyekundu na Mwamuzi Peter Walton baada ya kupewa Kadi 2 za Njano.
Kwa matokeo hayo Chelsea sasa wamecheza mechi 19 na wana pointi 42, Man U wakifuatia kwa mechi 18 pointi 37, Arsenal ni wa 3 mechi 17 pointi 35 na Aston Villa ni wa 4 mechi 18 pointi 35. 
Zote, Man U, Arsenal na Aston Villa zitacheza kesho huku Man U akiwa mgeni wa Hull City na Arsenal na Aston Villa zikipambana zenyewe huko Emirates Stadium.
VIKOSI:
Birmingham: Hart, Carr, Roger Johnson, Dann, Ridgewell, Larsson, Ferguson, Bowyer, McFadden, Jerome, Benitez.
AKIBA: Maik Taylor, Phillips, Fahey, McSheffrey, Damien Johnson, Carsley, Vignal.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Terry, Alex, Ashley Cole, Belletti, Mikel, Malouda, Lampard, Drogba, Sturridge.
AKIBA: Hilario, Carvalho, Joe Cole, Ballack, Zhirkov, Paulo Ferreira, Kalou.
Katika mechi nyingine za leo zilizoanza mapema MATOKEO NI:
Fulham 0 Tottenham 0
West Ham 2 Portsmouth 0
Benitez aungama: “Torres hayuko fiti!!!!”
Meneja wa Liverpool Rafa Benitez amekubali kuwa Mshambuliaji wake nyota Fernando Torres hayuko fiti kucheza kila mechi na wanalazimika kumchunguza kwanza na halafu waamue kama acheze au la.
Msimu huu, Torres amekuwa nje mara kwa mara na kuna uvumi kuwa inabidi afanyiwe operesheni ya kutibu ngiri [hernia].
Katika mechi ya mwisho waliyocheza Liverpool na kufungwa 2-0 na Portsmouth kwenye Ligi Kuu, Torres alicheza chini ya kiwango lakini katika mechi ya leo ya Desemba 26 watakapocheza na Wolves kwenye Ligi Kuu, Mchezaji huyo anategemewa kuanza.
Liverpool, ambao wako pointi 8 nyuma ya Timu 4 za juu, wanakabiliwa na mechi ngumu 3 mfululizo baada ya mechi ya leo, kwenye Ligi Kuu, watacheza na Aston Villa, iliyo nafasi ya 4 kwenye Ligi, kisha watacheza na Reading kwenye Kombe la FA na baada ya hapo watapambana kwenye Ligi Kuu na Timu ya 5 kwenye Ligi, Tottenham.
Benitez anahaha kuhakikisha Straika wake yuko fiti lakini amekiri: “Ni lazima tumwangalie na kuhakikisha anacheza akiwa fiti tu!
Wakati huohuo, Benitez amekanusha taarifa kuwa alifanya mazungumzo na Nahodha wake Steven Gerrard ili kujadili kushuka kwa kiwango chake na kutojiamini kwake.
Mwenyekiti Arsenal aishambulia Barca!!!
Mwenyekiti wa Arsenal Peter Hill-Wood ameishambulia vikali Barcelona kwa kuwandama Nahodha wao Cesc Fabrega, miaka 22, na kujaribu kumrubuni ajiunge na Barcelona.
Mara kwa mara Barcelona imekuwa ikihusishwa na kumnunua Fabregas ambae alianza mpira akiwa kwenye Timu ya Vijana ya Barcelona na kisha kujiunga Arsenal.
Ingawa Real Madrid nao wanatajwa kutaka kumnunua Fabregas lakini ni Barcelona wakiongozwa na Rais wao Joan Laporta ndio vinara wa kumrubuni Kiungo huyo wa Arsenal mwenye asili ya Spain.
Na kauli za hivi karibuni za Joan Laporta zimemkera mno Mwenyekiti wa Arsenal, Peter Hill-Wood, aliefoka: “Nimechoka na uhuni huu wa Barcelona na upumbavu wao! Cesc ana Mkataba wa muda mrefu na mzuri na sisi! Yuko na sisi miaka 7 sasa na hana nia ya kuondoka! Hatuwezi kuwazuia kuongea ovyo lakini huu ni upuuzi uliokithiri!!”
LIGI KUU England: Yafikia Nusu, Uhamisho kufunguliwa Januari, je nini kitegemewe?
Ligi Kuu England wikiendi hii inafikia hatua muhimu ya Timu kufikia kucheza mechi 19 ambazo ni nusu ya mechi zote na vita kileleni iko wazi huku kuna Timu 8 zikigombea Ubingwa na nafasi 4 za kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao na huko mkiani, ukitoa Timu hizo 8 zilizo fungu la kugombea Ubingwa, Timu zote zilizobaki, kimahesabu, zipo kwenye vita ya kukwepa kushuka Daraja.
Mwezi Januari dirisha la uhamisho litafunguliwa na kufungwa Januari 31 na kila Timu, pengine, itakuwa ikifikiria kuingia sokoni na kuimarisha Vikosi vyao. Lakini, kikawaida, biashara ya Wachezaji mwezi Januari ni ngumu na vile vile Klabu nyingi kwa sasa zinakabiliwa na matatizo ya kifedha.
Ifuatayo ni tathmini ya kila Klabu ie, nini kinahitajika, uwezo kifedha na Wachezaji gani walengwa:
ARSENAL
WANAHITAJI: Sentafowadi mwenye nguvu hasa baada ya kuumia kwa Robin van Persie na Nicklas Bendtner ambao wako nje kwa muda mrefu.
FEDHA: Arsenal wanasisitiza pesa wanazo ila tatizo ni kumlazimisha Arsene Wenger jinsi ya kuzitumia.
WALENGWA: Straika wa Wolfsburg Edin Dzeko ambae thamani yake ni Pauni Milioni 20 na mwingine ni Mchezaji wa Bordeaux Marouane Chamakh ambae Wenger amesita kumsaka kwa ajili ya bei yake.
ZIADA: Beki kutokaUswisi Philippe Senderos huenda akahamia Atletico Madrid.
ASTON VILLA
WANAHITAJI: Meneja Martin O'Neill anafurahishwa na mwenendo wa Klabu yake lakini anataka kusajili Straika mmoja.
FEDHA: Villa haijafuja pesa kama Klabu nyingine, hivyo, bila shaka, mfuko wao wa ununuzi wa Wachezaji bado umetuna.
WALENGWA:Kuna tetesi kuwa endapo Spurs wataamua kumuuza Nahodha wao Robbie Keane, Villa watamdaka.
ZIADA: Nicky Shorey na Nigel Reo-Coker ndio wanaohusishwa na uhamisho.
BIRMINGHAM
WANAHITAJI: Wachezaji zaidi wa viwango vya juu huku Straika akiwa juu ya listi yao.
FEDHA: Mmiliki wao Carson Yeung ameahidi kutoa Pauni Milioni 40 ili kununua Wachezaji.
WALENGWA: Listi yao ya ununuzi wamo Mchezaji wa Sporting Gijon Michel na Mchezaji wa Rangers Kris Boyd.
ZIADA: Huenda Kevin Phillips, Franck Queudrue na Teemu Tainio wakauzwa.
BLACKBURN
WANAHITAJI: Mfungaji magoli kwani wana uhaba mkubwa wa magoli. Vilevile, wameonyesha nia ya kuongeza Mkataba kwa Franco Di Santo ambae wamemkopa kutoka Chelsea.
FEDHA: Meneja Sam Allardyce aliufilisi mfuko wa kununua Wachezaji kabala Msimu kuanza hivyo atalazimika kuuza Wachezaji kabla ya kununua.
WALENGWA: Straika wa Stoke James Beattie na Beki kutoka Portsmouth Nadir Belhadj.
ZIADA: Winga Morten Gamst Pedersen na Mshambuliaji Benni McCarthy huenda wakauzwa.
BOLTON
WANAHITAJI: Kiungo mlinzi na Mshambuliaji.
FEDHA: Meneja Gary Megson ndie alietumia fedha kidogo kupita yeyote kwenye Ligi Kuu katika ununuzi wa Wachezaji.
WALENGWA: Kiungo wa Celtic Scott Brown, Mchezaji wa Blackpool Charlie Adam na Straika wa Stoke James Beattie.
ZIADA: Danny Shittu yumo kwenye listi hii.
BURNLEY
WANAHITAJI: Sentafowadi na labda Mshambuliaji.
FEDHA: Meneja Owen Coyle huenda akalazimika kuomba pesa itakazolipwa Klabu hivi karibuni kama mgao wao wa malipo toka Kampuni za TV, zinazokadiriwa kuwa Pauni Milioni 7, ili kunua Wachezaji kwa sababu hana na hawezi kuuza Mchezaji hata mmoja ili kupata pesa.
WALENGWA: Beki wa Celtic Gary Caldwell au Beki wa Sheffield United Matt Kilgallon.
ZIADA: Hamna.
CHELSEA
WANAHITAJI: Washambuliaji kuziba mapengo ya Didier Drogba na Salomon Kalou watakaokuwa Afrika mwezi Januari kucheza kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika. Huenda wakamrudisha Franco Di Santo ambae yuko Blackburn kwa mkopo.
FEDHA: Meneja Carlo Ancelotti ametamka hanunui mtu mwezi Januari lakini hakuna anaemwamini na kwa Chelsea fedha si tatizo.
WALENGWA: Sergio Aguero, kwa Pauni Milioni30, anategemewa kuhama kutoka Atletico Madrid kwenda Stamford Bridge.
ZIADA: Chelsea hawathubutu kuuza Mchezaji yeyote kwa vile wanakabiliwa na adhabu ya FIFA ya kutosajili Mchezaji yeyote hadi 2011 baada ya kumsajili Mchezaji Gael Kakuta kinyume cha sheria. Adhabu hii imesitishwa na CAS [Mahakama ya Usuluhishi katika Michezo] hadi itakapotoa uamuzi.
EVERTON
WANAHITAJI: Lundo la Wachezaji majeruhi kupona na Louis Saha kusaini Mkataba mpya kabla hajakuwa Mchezaji huru mwishoni mwa msimu.
FEDHA: Kitita walichopata baada ya kumuuza Joleon Lescott Manchester City kimeshatumiwa na Meneja David Moyes hana hata senti moja ya kununua mtu Januari.
WALENGWA: Mchezaji anaecheza Timu moja na David Beckham huko LA Galaxy, Landon Donovan, atatua Januari kucheza kwa mkopo.
ZIADA: Wakati karibu Timu nzima ni majeruhi, hakuna atakaeondoka Goodison Park.
FULHAM
WANAHITAJI: Meneja Roy Hodgson amesuka Timu nzuri yenye Kikosi kidogo lakini kwa vile pia wanacheza Ulaya kwenye EUROPA LIGI, watakabiliwa na mechi nyingi zaidi na wanahitaji kuimarisha Kikosi chao.
FEDHA: Ni lazima wauze kabla ya kununua.
WALENGWA: Wanataka kumfanya Jonathan Greening, waliemchukua kwa mkopo toka West Brom, awe Mchezaji wao wa kudumu.
ZIADA: Seol Ki-Hyeon, Eddie Johnson na Diomansy Kamara hawana namba za kudumu.
HULL CITY
WANAHITAJI: Mchezaji yeyote mfungaji magoli na Kiungo wa kucheza badala ya Jimmy Bullard anaeumia mara kwa mara.
FEDHA: Meneja Phil Brown ameamrishwa na Mwenyekiti Adam Pearson apunguze Kikosi chake chenye Wachezaji 41.
WALENGWA: Hana.
ZIADA: Ni upunguzwaji wa Wachezaji hao 41.
LIVERPOOL
WANAHITAJI: Straika kumpunguzia mzigo Fernando Torres.
FEDHA: Meneja Rafa Benitez amepoteza pesa nyingi kwa kusaini Wachezaji wasio na manufaa. Ni lazima auze ndio anunue.
WALENGWA: Kiungo wa West Ham Scott Parker na Straika wa Bayern Munich Luca Toni ndio wanaowindwa.
MANCHESTER CITY
WANAHITAJI: Meneja aliefukuzwa, Mark Hughes, alitumia zaidi ya Pauni Milioni 50 kuwanunua Walinzi Kolo Toure, Joleon Lescott na Wayne Bridge na wote hawajang’ara. Sasa Meneja mpya Roberto Mancini inabidi aanze upya.
FEDHA: Klabu inamilikiwa na Koo ya Kifalme ya Abu Dhabi ambao ni Matajiri wakubwa! Bila shaka, vijisenti si tatizo!!
WALENGWA: Senta Hafu wa Juventus Giorgio Chiellini na Fulbeki wa Inter Milan Maicon ndio walengwa wakubwa. Lakini, nani anajua kama Man City hawatamzonga tena Nahodha wa Chelsea, John Terry?
ZIADA: ni ngumu kujua Meneja mpya Roberto Mancini hamtaki nani kwa vile yupo Klabuni kwa muda mfupi sana [wiki tu].
MANCHESTER UNITED
WANAHITAJI: Madifenda hasa baada ya wimbi la kuumia Madifenda wote na kutokujulikana lini Rio Ferdinand atapona na kurudi uwanjani.
FEDHA: Zipo hasa baada ya kutumia Pauni Milioni 20 tu kati ya Pauni Milioni 80 walizopata kwa kumuuza Cristiano Ronaldo.
WALENGWA: Kiraka wa Ajax Gregory van der Wiel, Beki wa West Ham Matthew Upson na Kiungo wa Everton Jack Rodwell.
ZIADA: Haitegemewi kuondoka mtu.
PORTSMOUTH
WANAHITAJI: Kuondolewa kwa kufungiwa kwao kutosajili Mchezaji hadi watakapolipa madeni yanayowakabili kwa kutokumalizia kulipa ada za uhamisho za Wachezaji waliowanunua.
FEDHA: Hawana. Klabu inatakiwa ilipe Pauni Milioni 8 kama deni la ada za uhamisho wa Wachezaji. Njia yao ya kupata Wachezaji ni kwa njia ya mkopo tu.
WALENGWA: Kuongeza mkataba wa mkopo wa Jamie O’Hara kutoka Tottenham.
ZIADA: Inabidi wauze ili walipe madeni na Wachezaji wanaoweza kutolewa kafara ni Nadir Belhadj, John Utaka na pengine Kipa David James.
STOKE CITY
WANAHITAJI: Mshambuliaji wa bei poa.
FEDHA: Meneja Tony Pulis alizilipua pesa zake zote za kununulia Wachezaji kabla Msimu huu haujanza alipotumia Pauni Milioni 20 kuwanunua Tuncay, Robert Huth, Dean Whitehead na Danny Collins.
WALENGWA: Mshambuliaji wa Leeds Jermaine Beckford
ZIADA: Baada ya kugombana na Meneja Tony Pulis, Mshambuliaji James Beattie atauzwa na pia Mshambuliaji mwingine, Dave Kitson, kiwango kimeporomoka hivyo yumo mbioni kuuzwa.
SUNDERLAND
WANAHITAJI: Bosi wa Sunderland Steve Bruce anakerwa sana na udhaifu wa Difensi yake.
FEDHA: Zipo.
WALENGWA: Beki wa pembeni Maynor Figueroa toka Wigan, Sentahafu wa Middlesbrough David Whetaer.
ZIADA: Anton Ferdinand na David Healy hawampendizi Steve Bruce hivyo huenda wakauzwa.
TOTTENHAM
WANAHITAJI: Meneja Harry Redknapp anaridhika na Kikosi chake lakini yeye daima huwa macho wazi kukiimarisha.
FEDHA: Bodi ya Klabu imesisitiza lazima wauzwe Wachezaji ndio wanunuliwe wengine.
WALENGWA: Wachezaji wa West Ham Scott Parker na Matthew Upson wanatajwa sana.
ZIADA: David Bentley na Roman Pavlyuchenko watauzwa. Uvumi umezagaa Robbie Keane nae yuko
njiani kuuzwa.
WEST HAM
WANAHITAJI: Wafungaji kubeba mzigo wa Dean Ashton [amestaafu baada ya kuumia] na Carlton Cole.
FEDHA: Inabidi wauze ndio wanunue.
WALENGWA: Robbie Keane kutoka Tottenham ambae watabadilishana na Mchezaji wao.
ZIADA: Ili kutatua uhaba wa fedha Klabuni, itabidi Scott Parker na Matthew Upson wauzwe.
WIGAN
WANAHITAJI: Walinzi na pengine Viungo wapiganaji.
FEDHA: Zipo baada ya kuuza Wachezaji kadhaa msimu huu.
WALENGWA: Wachezaji wa Portsmouth Younes Kaboul na Kevin-Prince Boateng. Pia mazungumzo yanaendelea ili kumchukua kutoka Chile Mlinzi Waldo Ponce.
ZIADA: Maynor Figueroa yuko njiani kwenda Sunderland na Paul Scharner amedokeza anahama.
WOLVES
WANAHITAJI: Meneja Mick McCarthy anaridhishwa na Kikosi chake.
FEDHA: Hawana.
WALENGWA: Labda wambebe Dave Kitson kwa mkopo kutoka Stoke.
Ziada: Hamna.
Kitendawili cha Rio kurudi uwanjani!!!
Rio Ferdinand anasumbuliwa na tatizo la mgongo ambalo husababisha hata kuumwa kwa misuli ya miguu yake na ugonjwa huu umemweka nje ya uwanja tangu mwishoni mwa Oktoba na kusababisha kuzikosa mechi za Klabu yake Manchester United 13 na mpaka sasa Klabu yake haijui lini atarudi uwanjani.
Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man U, amesema Rio ataonekana muda si mrefu ingawa hakusema lini ila aligusia tu kuwa wiki mbili zilizopita alipigwa sindano na baada ya wiki moja akaanza mazoezi kweye jim na bado wanamwangalia maendeleo yake.
Siku chache zilizopita, mwenyewe Rio alitamka, wakati wa ufunguzi wa Mfuko wake wa Hisani, kuwa nafasi yake kwenye Kikosi cha England kitakachoenda Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni haiko mashakani.
Lakini, wakati Ligi Kuu leo inatimiza kufikia hatua ya Nusu yake kwa Timu kucheza mechi 19 kati ya 38 wanazotakiwa kucheza, Wadau wanajiuliza kuhusu Rio na Ferguson akazungumza: “Rio yuko imara. Hajaonyesha athari zozote kisaikolojia kuhusu kuumia kwake. Lakini nina hakika yeye kama Mchezaji ana usongo mkubwa wa kutaka kucheza mechi hasa wakati huu kwenye mvutano mkubwa kuelekea Ubingwa!”

Friday 25 December 2009

Wachezaji kutimkia Afrika: Chelsea bila Drogba na wenzake, Portsmouth kuathirika sana!!
Huku Klabu zikiminyana kutafuta Ubingwa na nyingine zikipigania uhai wao wa kubaki Ligi Kuu England, Wachezaji karibu 27 wanaondoka muda wowote kuanzia sasa kujiunga na Timu zao za Taifa zinazojitayarisha kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazochezwa Nchini Angola kuanzia Januari 10 hadi 31.
Klabu zitakazopata pigo la kuondokewa Wachezaji ambalo linatofautiana kwa idadi ya Wachezaji ni pamoja na Chelsea, Arsenal, Manchester City na Portsmouth.
Klabu ambazo haziathiriki hata kidogo na wimbi la kuondokewa Wachezaji ni Manchester United, Liverpool na West Ham.
Wachezaji walio njiani kuelekea Angola:
Arsenal: Emmanuel Eboué (Ivory Coast), Alex Song (Cameroon)
Aston Villa: Moustapha Salifou (Togo)
Bolton Wanderers: Danny Shittu (Nigeria)
Burnley: André Bikey (Cameroon)
Chelsea: Didier Drogba (Ivory Coast), Michael Essien (Ghana), Salomon Kalou (Ivory Coast), John Obi Mikel (Nigeria)
Everton: Aiyegbeni Yakubu, Joseph Yobo (both Nigeria)
Fulham: John Pantsil (Ghana), Dickson Etuhu (Nigeria)
Hull: Daniel Cousin (Gabon), Seyi Olofinjana (Nigeria)
Manchester City: Kolo Touré (Ivory Coast), Emmanuel Adebayor (Togo)
Portsmouth: Nadir Belhadj, Hassan Yebda (both Algeria), John Utaka, Nwankwo Kanu (both Nigeria), Aruna Dindane (Ivory Coast)
Stoke City: Mamady Sidibe (Mali)
Sunderland: John Mensah (Ghana)
Tottenham Hotspur: Benoît Assou-Ekotto (roon)
Wigan Athletic: Richard Kingson (Ghana
LIGI KUU England: Tathmini Mechi za Boksingi Dei na za Jumapili
Timu za Ligi Kuu England, baada ya kusheherekea Xmas, hawana nafasi ya kufungua zawadi zao Siku ya Boksingi Dei kwani Klabu 16 zitakuwa kazini siku hiyo na siku inayofuatia Klabu 4 zilizobaki nazo pia zinaingia mtamboni.
RATIBA:
Jumamosi, 26 Desemba 2009
[saa 9 dak 45 mchana]
Birmingham v Chelsea
[saa 10 jioni]
Fulham v Tottenham
West Ham v Portsmouth
[saa 11 jioni]
Burnley v Bolton
[saa 12 jioni]
Man City v Stoke
Sunderland v Everton
Wigan v Blackburn
[saa 2 na nusu usiku]
Liverpool v Wolves
Jumapili, 27 Desemba 2009
[saa 10 na nusu jioni]
Arsenal v Aston Villa
[saa 1 usiku]
Hull v Man U
Baada ya malamiko na kukerwa kwa kutimuliwa kwa Mark Hughes huko Manchester City, Meneja mpya wa Klabu hiyo Mtaliana Roberto Mancini ataanza kibarua chake kwa kuikaribisha Stoke City Uwanja wa City of Manchester hapo kesho.
Mechi nyingine ya kesho ambayo italeta ushindani wa nguvu ni ile itakayozikutanisha Timu za mkiani West Ham ambayo itaikaribisha Portsmouth Uwanjani Upton Park. Katika mechi zao za mwisho Timu hizi zilizo mashakani zilijitutumua na kupata mafanikio mazuri pale Portsmouth walipoitandika Liverpool 2-0 na West Ham kwenda sare na vinara wa Ligi Chelsea kwa bao 1-1.
Birmingham City, walio nafasi ya 7 kwenye Ligi baada ya kutofungwa katika mechi 9 za mwisho, wanawakaribisha Chelsea ambao siku hizi za hivi karibuni wameonyesha kupwaya mno baada ya kushinda mechi moja tu katika 6 walizocheza mwisho. Chelsea huenda wakalazimika kumchezesha Chipukizi Daniel Sturridge baada ya Anelka kuumia na pia kumpa uzoefu kwani hii ni mechi ya mwisho kwa Didier Drogba kucheza kabla hajaenda kwao kujiunga na Timu ya Taifa ya Ivory Coast inayojitayarisha kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Liverpool ambao wako kwenye wakati mgumu kufuatia matokeo mabaya wanawakaribisha Wolves Uwanjani Anfield huku Benitez akisakamwa na kutetewa na Wachezaji wake asifukuzwe. Benitez mwenyewe ameshatangaza ni lazima washinde mechi hii.
Kimbembe kipo kwenye Dabi ya Timu za London huko Craven Cottage wakati Fulham watakapowakaribisha Tottenham, Timu iliyo nafasi ya 5. Kwa sasa Fulham wana matumaini makubwa hasa baada ya kuwaangushia Mabingwa Watetezi Manchester United kipigo cha 3-0 kwenye mechi yao ya mwisho.
Mechi ya Sunderland v Everton ni mechi muhimu mno kwa Klabu hizo kwa vile zote zinasuasua huku Sunderland wakiwa wameshinda mechi 2 tu-dhidi ya Arsenal na Liverpool- katika mechi zao 11 za mwisho na Everton hawajashinda mechi yeyote katika 6 walizocheza mwisho na sasa wako pointi 2 tu juu ya Timu zilizo eneo la kuporomoka Daraja.
Bolton watafanya safari fupi kuelekea East Lancashire Uwanjani Turf Moor kukumbana na Timu ambayo ni ngumu Uwanjani hapo, Burnley, waliofungwa mechi moja tu kati ya 9 za Ligi Kuu Uwanjani hapo. Hata hivyo, bila shaka, Bolton watakuwa wanajiamini hasa baada ya kuifunga West Ham kwenye mechi yao ya mwisho na pia kupata mapumziko ya siku 11 baada ya mechi yao ya Jumatatu iliyokwisha waliyokuwa wacheze na Wigan kuahirishwa kwa sababu ya hali ya hewa ya baridi kali na barafu.
Wigan v Blackburn ni mechi nyingine ngumu inayozikutanisha Timu zenye tofauti ya pointi moja tu kati yao.
Jumapili itaanza kwa mechi kubwa kati ya Arsenal v Aston Villa.
Kimsimamo Arsenal wako nafasi ya 3 na Villa wako nafasi ya 4. Villa hawajawahi kufungwa Uwanja wa Emirates na katika mechi kama hii msimu uliokwisha, Villa waliifunga Arsenal.
Mechi hii itaikutanisha Fowadi ya Arsenal inayofunga Magoli kemkem, Magoli 44 katika mechi 17, na Difensi ngumu ya Aston Villa, iliyofungwa Goli 14 tu katika mechi 18.
Mechi ya pili na ya mwisho siku ya Jumapili ni kati ya Hull City na Manchester United Uwanjani KC. Mabingwa Watetezi, Man U wanaokabiliwa na matatizo ya Difensi kufuatia kujeruhiwa Madifenda wao wote [isipokuwa Evra], wanatoka kwenye kipigo cha 3-0 walichopewa ugenini na Fulham. Hull City nao wana hali mbaya huku wakiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi.
Mvuto kwenye mechi hii ni Refa Alan Wiley [pichani] kupangiwa kuichezesha ikiwa ni mechi yake ya kwanza kwa Man U tangu Meneja wa Man U, Sir Alex Ferguson, kumbatukia hayuko fiti kuchezesha, kauli aliyoitoa mara baada ya sare ya 2-2 kati ya Man U na Sunderland mwezi Oktoba.
Kauli hiyo ilimfanya Ferguson afungiwe mechi 2 na FA licha ya kumwomba msamaha Refa Alan Wiley.
Fergie ashutumu kufukuzwa Hughes Man City!!
Sir Alex Ferguson amefoka na kulaumu jinsi Manchester City walivyomfukuza aliekuwa Meneja wao Mark Hughes na kumteua Roberto Mancini kuchukua nafasi yake na kukiita kitendo hicho kuwa ‘hakikubaliki”.
Ingawa Mark Hughes ameiongoza vizuri Manchester City msimu huu ikiwa imefungwa mechi 2 tu kwenye Ligi Kuu, ikiwa ni idadi ndogo kupita Timu yeyote kwenye Ligi Kuu, na pia kuipeleka Timu hiyo kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Carling ambako watakutana mwezi Januari na Mahasimu wao Manchester United, hayo yote hayakutosha kumnusuru kwenye kibarua chake.
Mameneja wengi, akiwemo Mchezaji mwenzake wa zamani Steve Bruce ambae alicheza pamoja na Hughes Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson, wamejitokeza kumtetea Mark Hughes na kuponda kwa sauti kali jinsi alivyofukuzwa.
Manchester City, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wao Garry Cook, wametetea uamuzi wao wa kumtimua Hughes lakini Ferguson amesema: “Ni vitendo visivyokubalika! Hatujali kama umepoteza mechi 2 au 20, kuna njia ya kuwathamini na kuwatendea binadamu! Nashangaa, Naona Xmas huwafanya Wamiliki wa Klabu kuonyesha tabia zao mbovu! Sijui kwa nini! Asubuhi yote ya Jumamosi, mashine za uvumi zilizagaa kufukuzwa kwa Mark Hughes na bila shaka Mark alisikia hilo! Ni hali mbaya mno kuwa kwenye mazingara hayo huku ukijua mechi ya Jumamosi ni ya mwisho kwako!”
Meneja wa Hull Brown aponda mashitaka ya FA na kusema ni kashfa!!!
Meneja wa Hull City Phil Brown amelaumu Klabu yake kushitakiwa, ikijumuishwa na Arsenal, kwa kushindwa kudhibiti Wachezaji wake kufuatia zogo lililotokea kwenye mechi ya Ligi Kuu wiki iliyopita huko Emirates Stadium ambayo Arsenal walishinda 3-0.
Zogo hilo lilizuka baada ya Samir Nasri wa Arsenal kumkanyaga Richard Garcia wa Hull na ndipo Wachezaji wa pande zote kuzongana na Refa Steve Bennett akawapa Kadi za Njano Nasri na Stephen Hunt wa Hull kwa tukio hilo.
Lakini baadae, wakati Timu zikienda Vyumba vya Kubadilisha jezi, Wachezaji wakavaana tena na kuleta kitimtim.
FA imezipa hadi Januari 13 Klabu hizo kuwasilisha utetezi wao wa mashitaka yao.
Phil Brown amedai Klabu yake isingehusishwa kwenye mashitaka hayo na ni Nasri ndie chanzo cha fujo hizo ambazo alizianzisha alipoona Refa Steve Bennett haoni.
Brown amedai Klabu yake itapinga tuhuma za kuleta fujo.
Keane haondoki Spurs!!!
Harry Redknapp amesema hataki kumuuza Nahodha wake Robbie Keane licha ya kukumbwa na mzozo wa kuongoza Wachezaji wa Tottenham kwenda Dublin, Ireland wiki iliyopita kwenye Pati ya Xmas bila ya ridhaa ya Klabu.
Uvumi ulikuwa umezagaa kuwa Harry Redknapp atamuuza Keane na kumnunua Craig Bellamy kutoka Manchester City lakini Meneja huyo wa Tottenham amekanusha habari hizo.
Uvumi huo uliota mizizi kwa Wadau wengi wakizingatia kuwa katika mechi nyingi za hivi karibuni Redknapp amekuwa akiwachezesha kwa pamoja Jermain Defoe na Peter Crouch na kumtupa benchi Keane lakini Redknapp amesema: “Sitaki kumuuza Keane. Hamna Keane wengi kwenye Soka!”
Hata hivyo Redknapp alidokeza huenda akaingia sokoni dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari kwani Wachezaji wake Roman Pavlyuchenko na David Bentley wanang’ang’ania kuhama kwa sababu hawapati namba za kudumu hapo Spurs na hivyo huenda akalazimika kuwauza na pesa zao zikasaidia kununua Wachezaji wengine.
Vilevile, Redknapp alizungumzia kuhusu Mchezaji wao Jamie O’Hara ambae yuko Portsmouth kwa mkopo na kusema kuwa ataongea na Mwenyekiti wake ili waamue kama aendelee kubaki Portsmouth au wamrudishe Tottenham.

Thursday 24 December 2009

Liverpool yadidimia, Nahodha Gerrard kiwango chini!!
Wakati kuna dhana kubwa Meneja wa Liverpool Rafa Benitez atatimuliwa wakati wowote, pia kuna imani kubwa Nahodha wao Steven Gerrard kiwango chake kimeporomoka mno.
Gerrard, miaka29, ndie alikuwa injini ya mafanikio waliyopata Liverpool miaka ya hivi karibuni ikiwemo kutwaa Ubingwa wa Klabu za Ulaya mwaka 2005 huko Instanbul na kuichachafya Manchester United katika kinyang’anyiro cha Ligi Kuu msimu uliopita.
Lakini msimu huu huku Liverpool ikisuasua na kupoteza mechi nyingi Ligi Kuu na pia kubwagwa nje ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, kiwango cha Gerrard kimeonekana kushuka wazi wazi na kumfanya hata Benitez kumtaka Nahodha wake abadilike na asijipe presha bali acheze mpira wake wa kawaida.
Angalia nini Steven Gerrard alichovuna katika historia yake ya Soka ukulinganisha na Ryan Giggs:
Steven Gerrard [Ameshinda jumla ya Mataji/Tuzo 12:
FA Cup [2], Kombe la Ligi [2], UEFA CHAMPIONS LEAGUE [1], UEFA Cup [1], UEFA Super Cup [2], Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka, toka kwa Waandishi, [1], Mchezaji Bora wa PFA [Chama cha Wachezaji wa Kulipwa [1], Mchezaji Bora Chipukizi wa PFA [1], Mchezaji Bora wa UEFA [1]
Ryan Giggs [Ameshinda Mtaji/Tuzo 27]:
LIGI KUU [11], FA Cup [4], Kombe la Ligi [3], UEFA CHAMPIONS LEAGUE [2], UEFA Super Cup [1], Klabu Bingwa Duniani [2], Mchezaji Bora wa BBC [1], Mchezaji Bora wa PFA [1], Mchezaji Bora Chipukizi wa PFA [2]]
Wenger: “Giggs ni chaguo langu la Mchezaji Bora katika miaka 10!!”
Hivi karibuni Ryan Giggs alipewa Tuzo ya BBC [Shirika la Utangazaji Uingereza] ya kuwa Mwanamichezo Bora wa Mwaka 2009 na Klabu yake Manchester United ikamwongezea Mkataba ambao utamweka Old Trafford hadi 2011.
Akiwa na umri wa miaka 36, Giggs ndie Mchezaji pekee wa LIGI KUU England aliepata mafanikio makubwa. Giggs ameshashinda Mataji 11 ya Ubingwa wa Ligi Kuu, ametwaa Vikombe vitatu vya Kombe la FA, Vikombe vitatu vya Kombe la Ligi, ameshinda Klabu Bingwa Ulaya mara 2, UEFA Super Cup mara moja na Klabu Bingwa ya Dunia mara 2.
Mafanikio yote ameyapata akiwa na Klabu yake Manchester United ambayo alianza kuichezea tangu akiwa na miaka 14.
Mafanikio yake ni listi ndefu inayozidi kuongezeka.
Giggs ni Mchezaji pekee wa Manchester United kucheza Misimu yote 11 ambayo Man U alitwaa Ubingwa wa Ligi Kuu. Ni Mchezaji pekee wa Man U aliefunga magoli katika Misimu 11 ya kucheza katika Mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Ni Mchezaji pekee kwenye Ligi Kuu kucheza kila Msimu na kufunga katika kila Msimu tangu Ligi Kuu ilipoanza.
Ni Mchezaji wa Pili wa Kiungo katika Ligi Kuu aliefunga zaidi ya Magoli 100 wa kwanza akiwa ni Matt Le Tissier aliekuwa akichezea Southampton.
Arsene Wenger amebaini: “Ryan Giggs ni Mchezaji Bora Ligi Kuu katika kipindi cha Miaka 10 iliyopita! Yeye ana staili na ni Mshindi! Lakini lile goli alilotufunga kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA mwaka 1999 bado linaniumiza roho!!”
LIVERPOOL: Hofu ya kutimuliwa Benitez, Wachezaji waaanza kumtetea!!
Rafa Benitez amekalia kuti kavu hasa baada ya Liverpool kubwagwa nje ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na pia kufanya vibaya kwenye LIGI KUU England wakiwa wameshinda mechi 3 tu kati ya 12 walizocheza mwisho na hivyo kuwa nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi.
Ingawa inaaminika kibarua chake kiko salama kwa sababu tu Liverpool hawana uwezo kifedha kumfukuza na kuteua Meneja mpya kwa kuwa wanakabiliwa na lundo la madeni, hali ni mbaya Klabuni kiasi cha kufanya Wachezaji kujitokeza na kuanza kunadi utetezi wake.
Nyota wa Liverpool, Fernando Torres, amesema: “Kumfukuza Meneja si jawabu! Meneja hachezi, ni sisi inabidi tucheze vizuri pamoja!”
Nae Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, akiunga mkono hoja hiyo, amesema: “Sisi ni timu! Ni sisi wa kulaumiwa kwa hali tuliyonayo!”
Liverpool, inayomilikiwa na Matajiri wa Kimarekani George Gillet na Tom Hicks, inadaiwa Pauni Milioni 240 na endapo watashindwa kufuzu kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu ujao watakosa mapato ya zaidi ya Pauni Milioni 20.
Hali ya Rafa Benitez imezidishwa ugumu kwa vile hana pesa za kununua Wachezaji ili kuimarisha Kikosi na ili afanye hivyo ni lazima auze baadhi ya Wachezaji ingawa Fernando Torres na Steven Gerrard hawauzwi.
Wachezaji ambao wanadhaniwa watapelekwa sokoni ni Ryan Babel, Andrea Dossena, Andry Voronin na Philipp Degen.
Na endapo watafaulu kuuza Wachezaji, inasemekana Liverpool wanawawinda Luca Toni kutoka Bayern Munich na Ruud van Nistelrooy toka Real Madrid.
Wakati huo huo, Mlinzi wa Liverpool, Glen Johnson, huenda akahojiwa na Polisi baada ya Mwanafunzi mmoja kudai alishambuliwa nje ya Naitiklabu moja Jijini London.
Arsenal na Hull City kitanzini FA!!!
Klabu za Arsenal na Hull City zimeshitakiwa na FA, Chama cha Soka England, kwa kushindwa kuwadhibiti Wachezaji wao kufuatia mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Uwanja wa Emirates wikiendi iliyopita ambayo Arsenal walishinda 3-0.
Shitaka hilo linafuatia mzozo uliotokea baada ya Mchezaji wa Arsenal Samir Nasri kumkanyaga Kiungo wa Hull Richard Garcia na kundi la Wachezaji wa pande zote mbili kuvaana baada ya tukio hilo.
Refa Steve Bennett aliwapa Kadi za Njano Nasri na Stephen Hunt wa Hull kufuatia mzozo huo lakini vurugu ziliendelea wakati Wachezaji walipokuwa wakitoka Uwanjani kuelekea Vyumba vya kubadilishia jezi.
Msimu uliokwisha Timu hizi pia ziligubikwa na mzozo baada ya Hull City kudai Nahodha wa Arsenal, Cesc Fabregas, ambae hakucheza siku hiyo ya tukio kwenye mechi ya Kombe la FA, alimtemea mate Meneja Msaidizi wa Hull lakini uchunguzi wa FA ulishindwa kuthibitisha tukio hilo na hivyo Fabregas hakuchukuliwa hatua yeyote.
Arsena na Hull City zimepewa hadi Januari 13 kujibu mashitaka hayo.

Wednesday 23 December 2009

Anelka kuzikosa mechi za Ligi Kuu Xmas!!
Mshambuliaji wa Chelsea Nicolas Anelka atazikosa mechi za Chelsea za Ligi Kuu za Desemba 26 watakapocheza ugenini na Birmingham na ile ya Desemba 28 watakapoivaa Fulham katika dabi ya Timu za Magharibi ya London kwa sababu ni majeruhi.
Anelka hakucheza mechi ya Jumapili iliyopita ya Ligi Kuu Chelsea walipotoka sare na West Ham kwa vile ameumia mguu na sasa tatizo hilohilo limemfanya aendelee kuwa nje.
Sasa Chelsea wamesema wanategemea Anelka kuanza kucheza kwenye mechi ya Kombe la FA hapo Januari 3 watakapocheza na Watford.
Chelsea pia watamkosa Mshambuliaji wao mkubwa Didier Drogba ambae anatakiwa ajiunge na Timu ya Taifa ya Ivory Coast kabla ya mwisho wa Desemba kwa ajili ya matayarisho ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazochezwa huko Angola kuanzia Januari 10.
Ivory Coast inategemewa kupiga Kambi yake ya mazoezi Nchini Tanzania mwanzoni mwa Januari ambako itakutana na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, katika mechi mbili za kujipima nguvu.
Diouf apata kibali kuchezea Man U!!!
Mchezaji kutoka Senegal, Mame Biram Diouf, miaka 22, amepewa kibali cha kazi na hivyo kuruhusiwa kuichezea Manchester United kuanzia Januari.
Diouf alisajiliwa na Manchester United kabla msimu huu kuanza kutoka Klabu ya Molde ya Norway lakini ikabidi aendelee kuichezea Molde kwa mkopo kwa sababu ya kukosa kibali cha kazi.
Tangu wakati huo, ameshaichezea Molde mechi 12 na kufunga mabao manne na kufanya idadi yake ya magoli kwa Klabu ya Molde kuwa ni 33 katika mechi 75 alizoichezea.
Bosi wa Man U, Sir Alex Ferguson, amemsifia Diouf ambae ameshaichezea Senegal mara moja, kwa kutamka: “Anafanya mazoezi na sisi na anafurahisha na kuvutia! Klabu yetu ni bora kwa kuvumbua vipaji na kuvikuza! Yeye ana miaka 22 tu na anaonekana ni bora!”
KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA lamtia kinyaa Grant!!!
Meneja wa Portsmouth, Avram Grant, anashangazwa mno na FIFA kuruhusu Kombe la Mataifa ya Afrika kuchezwa Januari na kulazimisha Wachezaji Mastaa wanaocheza Ligi kubwa Ulaya kuziacha Klabu zao zinazowalipa pesa nyingi na kwenda Afrika kwa mwezi mzima.
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitachezwa huko Angola kuanzia Januari 10 hadi 31 na Klabu kadhaa za Ligi Kuu England zitawakosa Mastaa wao wanaotoka Afrika.
Portsmouth, Klabu iliyomo mashakani kwani ipo mkiani kwenye Ligi Kuu na pia hairuhusiwi kusajili Mchezaji yeyote kwa vile inakabiliwa na madeni yanayotokana na kushindwa kumalizia kulipia ada za uhamisho za Wachezaji kadhaa iliyowanunua, itawakosa Wachezaji wake kina Aruna Dindane toka Ivory Coast, Kanu toka Nigeria, Nadir Belhadj na Hassan Yebda toka Algeria.
Grant ametamka: “Sijui kwa nini FIFA wanaruhusu hili! Sisi tunawalipa Wachezaji hao pesa nyingi, wao wanakaa nao miezi miwili bure! Wachezaji hao wanatakiwa kujiunga na Timu zao za Taifa wiki 2 kabla! “
Grant amesema ataongea na Timu za Taifa za Wachezaji wake ili kuwaombea wachelewe kujiunga ili angalau wawepo kwenye mechi ya Desemba 30 watakapocheza na Arsenal.
Wenger akata tamaa kuhusu Van Persie!!
Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger, amekiri kuwa itakuwa ni bahati kubwa kama Staa wake Robin van Persie atapona enka aliyoumia na kurudi uwanjani kabla msimu haujaisha hapo Mei mwakani.
Wenger amesema: “Ikiwa wewe ni mtu wa matumaini, unaweza ukasema atacheza Aprili lakini ukweli ni kuwa ni pengine ni Mei ndio atarudi! Sitaki kujipa matumaini ya uongo! Bora nisubiri tu na ikitokea akirudi mapema hilo litakuwa kama zawadi!”
Van Persie aliumizwa na Difenda wa Italia Giorgio Chiellini Novemba 14 katika mechi ya kirafiki kati ya Uholanzi na Italia na ikabidi afanyiwe upasuaji kwenye enka yake ili kuunga kamba za musuli zilizokatika.
Arsenal imekitaka Chama cha Soka cha Uholanzi kuwalipa fidia kwa kuumizwa Mchezaji huyo lakini inawezekana malipo hayo yasitolewe kwani kuna makubaliano kati ya FIFA na UEFA kulipa fidia tu kwa Wachezaji wanaoumia kwenye Fainali za Kombe la Dunia na Fainali za EURO Cup na si mechi nyingine zozote.
LIGI KUU England yaingia patamu!!! Mechi za Xmas, Boksingi Dei na Nyuu Iya kutoa fununu nani mbivu, nani mbichi!!!!
Wakati Chelsea bado kinara, Mabingwa Watetezi Manchester United wakisuasua na Difensi ya kuunga baada ya wote [isipokuwa Evra] kuumia, Arsenal akijikongoja licha ya Majeruhi ya Mastaa wao na Liverpool akipigwa nje ndani huku Timu 'zisizotegemewa' kama Villa, Spurs na Man City, kwa mnyato, zikileta upinzani usiotarajiwa, Ligi Kuu sasa inaingia kipindi cha Sikukuu za Xmas na Nyuu Iya ambacho kihistoria ndio hutoa fununu nani mwenye nafasi kubwa ya kuwa Bingwa na nani yumo hatarini kushushwa Daraja.
Miongoni mwa mechi kali zinazotarajiwa kuchezwa kipindi hiki ni zile kati ya Arsenal v Aston Villa [Desemba 27] na ile ya Aston Villa v Liverpool [Desemba 29].
MSIMAMO LIGI KUU England: [Timu zimecheza mechi 18 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea pointi 41
2 Man Utd pointi 37
3 Arsenal pointi 35 [mechi 17]
4 Aston Villa pointi 35
5 Tottenham pointi 33
6 Man City pointi 29 [mechi 17]
7 Birmingham pointi 28
8 Liverpool pointi 27
9 Fulham pointi 26 [mechi 17]
10 Sunderland pointi 21
11 Stoke pointi 21 [mechi 17]
12 Wolves pointi 19
13 Blackburn pointi 19
14 Burnley pointi 19
15 Everton pointi 18 [mechi 17]
16 Wigan pointi 18 [mechi 17]
17 Hull pointi 17
18 Bolton pointi 16 [mechi 16]
19 West Ham pointi 15
20 Portsmouth pointi 14
RATIBA: [saa za bongo]
Jumamosi, 26 Desemba 2009
[saa 9 dak 45 mchana]
Birmingham v Chelsea
[saa 10 jioni]
Fulham v Tottenham
West Ham v Portsmouth
[saa 11 jioni]
Burnley v Bolton
[saa 12 jioni]
Man City v Stoke
Sunderland v Everton
Wigan v Blackburn
[saa 2 na nusu usiku]
Liverpool v Wolves
Jumapili, 27 Desemba 2009
[saa 10 na nusu jioni]
Arsenal v Aston Villa
[saa 1 usiku]
Hull v Man U
Jumatatu, 28 Desemba 2009
[saa 9 dak 45 mchana]
Tottenham v West Ham
[saa 12 jioni]
Blackburn v Sunderland
Chelsea v Fulham
Everton v Burnley
Stoke v Birmingham
[saa 4 dak 45 usiku]
Wolves v Man City
Jumanne, 29 Desemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
Aston Villa v Liverpool
[saa 5 usiku]
Bolton v Hull
Jumatano, 30 Desemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
Portsmouth v Arsenal
[saa 5 usiku]
Man U v Wigan
Jumanne, 5 Januari 2010
[saa 4 dak 45 usiku]
Stoke v Fulham
Jumatano, 6 Januari 2010
[saa 4 dak 45 usiku]
Arsenal v Bolton
Jumamosi, 9 Januari 2010
[saa 9 dak 45 mchana]
Hull v Chelsea
[saa 12 jioni]
Arsenal v Everton
Burnley v Stoke
Fulham v Portsmouth
Sunderland v Bolton
Wigan v Aston Villa
[saa 2 na nusu usiku]
Birmingham v Man U
Powered By Blogger