Wamiliki wa Liverpool ambao ni Wamarekani wawili Tom Hicks na George Gillett wamekwama katika mikakati yao ya kujenga uwanja mpya wa Klabu ya Liverpool katika eneo jingine liitwalo Stanley Park baada ya kushindwa kupata kibali cha plani za kupanua uwanja huo mpya ili kufikia uwezo wa kuchukua watazamaji 73,000 kwani vibali vya mwanzo walivyopata vya ujenzi wa kiwanja kipya vilikuwa vya plani ya ujenzi wa uwanja wenye chini ya uwezo huo.
Uwanja wao wa sasa uitwao Anfield una uwezo wa kuingiza watazamaji 45,362 tu.
Vilevile wamiliki hao wameshindwa kupata uwezo wa kifedha ili kuendeleza mradi huo ingawa hili limekuja baada ya wao kuwa na mfarakano mkubwa kati yao.
Wamiliki hao wa Kimarekani wakati wanainunua Klabu ahadi yao kubwa ilikuwa ni kujenga uwanja mkubwa ili kushindana na Manchester United na vilevile kuitangaza Liverpool vyema katika soko la dunia.