Friday 29 August 2008

LEO NI UEFA SUPER CUP:
MAN U vs Zenit St Petersburg
UWANJA: STADE LOUIS II, MONACO
Leo saa 3 dakika 45 usiku [bongo time] MABINGWA WA ULAYA, Manchester United, watapambana na MABINGWA WA KOMBE LA UEFA, Zenit St Petrsburg ya Urusi kuwania UEFA SUPER CUP huko Monaco.
Watu wa bongo mechi wataiona moja kwa moja kupitia DSTV Supersport 3.

MAN U KUWA NA UZI MPYA MECHI ZA UGENINI UEFA!!!

Wakati huohuo, Man U msimu huu kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE wakicheza mechi za ugenini watatumia uzi mpya [pichani] uliotengenezwa na NIKE mahsusi kusheherekea miaka 40 tangu Man U walipokuwa Klabu ya kwanza Uingereza kutwaa UBINGWA WA ULAYA.

Katika mechi ya Fainali iliyochezwa mjini London Uwanja wa Wembley tarehe 29 Mei 1968 Man U waliwafunga Benfica mabao 4-1 na kutwaa UBINGWA WA ULAYA.

Benfica wakati huo ilikuwa ikiongozwa na Eusebio fowadi hatari mzaliwa wa Msumbiji. Nao Man U walikuwemo kina Sir Bobby Charlton, Dennis Law, George Best nk.

Siku hiyo Man U walivaa jezi za bluu tupu.

No comments:

Powered By Blogger