Saturday, 2 October 2010

LIGI KUU England:
Sunderland 0 Man United 0
Huko Stadium of Light, kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyochelewa kuanza kwa dakika 20 baada ya dari la Chumba cha Kubadilishia jezi cha Man United kuporomoka kufuatia kupasuka bomba la maji, Sunderland walicheza vizuri na kuweza kutoka sare 0-0 na Manchester United ambayo, kama kawaida ya Sir Alex Ferguson siku hizi, Kikosi kilipanguliwa na hivyo kushindwa kucheza mpira wenye mtiririko.
Kipindi cha kwanza Sunderland walitawala na walipaswa kuwa mbele kwa nafasi walizozipata.
Kipindi cha pili, Man United walizinduka alipobadilishwa Michael Owen na kuingizwa Dimitar Berbatov na wangeweza kupata bao kwa mabadiliko hayo.
Vikosi vilivyoanza:
Sunderland: Mignolet, Onuoha, Turner, Bramble, Bardsley, Malbranque, Cattermole, Henderson, Zenden, Bent, Elmohamady.
Akiba: Gordon, Mensah, Da Silva, Riveros, Reid, Ferdinand, Gyan.
Man Utd: Van der Sar, Rafael Da Silva, Ferdinand, Vidic, O'Shea, Nani, Scholes, Fletcher, Anderson, Macheda, Owen.
Akiba: Kuszczak, Evra, Berbatov, Smalling, Hernandez, Gibson, Bebe.
Refa: Chris Foy
Birmingham 0 Everton 2
Walikuwa hawajafungwa Mwaka mzima na katika mechi 18 kwenye Uwanja wao wa Mtakatifu Andrew, lakini leo Birmigham wameonja joto ya jiwe baada ya Everton kuwatandika 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu na huu ukiwa ushindi wa kwanza wa Ligi kwao.
Everton waliandika bao la kwanza baada ya krosi ya Leon Osman kumkuta Roger Johnson aliejifunga mwenyewe.
Krosi ya Leighton Barnes ilimkuta Tim Cahill na kufunga kwa kichwa bao la pili.
MATOKEO Mechi nyingine:
Stoke 1 Blackburn 0
Tottenham 2 Aston Villa 1
West Brom 1 Bolton 1
West Ham 1 Fulham 1
RATIBA KESHO:
Jumapili, 3 Octoba 2010
[Saa 9 na nusu mchana]
Man City v Newcastle
[Saa 11 jioni]
Liverpool v Blackpool
[Saa 12 jioni]
Chelsea v Arsenal
Wigan 2 Wolves 0
Katika mechi ya Ligi Kuu iliyoanza mapema leo, Wigan wakiwa nyumbani Uwanja wa DW wameweza kuwatungua Wolves mabao 2-0.
Wolves ilibidi wacheze Mtu 10 kuanzia dakika ya 11 baada ya Karl Henry kutandikwa Kadi Nyekundu na Refa Lee Mason kwa kumchezea rafu mbaya Jordi Gomez.
Hadi mapumziko ngoma ilikuwa 0-0 na ni Jordi Gomez alieipatia Wigan bao la kwanza dakika ya 64 kwa frikiki murua.
Hugo Rodallega alipachika bao la pili dakika ya 85 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Charles N’Zogbia.
Adebayor aililia Juve
Straika wa Manchester City Emmanuel Adebayor ambae namba zimekuwa adimu Msimu huu amedokeza yu tayari kwenda Juventus Mwezi Januari dirisha la uhamisho likifunguliwa.
Kwenye Ligi Kuu Msimu huu Adebayor amecheza mechi 3 tu na hilo limemfanya aangalie maslahi kwingineko ingawa Meneja wa Man City Roberto Mancini amesema Mchezaji huyo bado ana nafasi hapo.
Adebayor alihamia Man City kwa Pauni Milioni 25 mwaka jana akitokea Arsenal.
Spurs na West Ham wautaka Uwanja wa Olimpiki London
Klabu za London, Tottenham na West Ham, zimewasilisha maombi yao ya kuuchukua Uwanja wa Olimpiki 2012 wa London wenye uwezo wa kuchukua Watazamaji 80,000.
Siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya kuumiliki Uwanja huo ilikuwa Jumanne na uamuzi wa nani apewe utatolewa ifikapo Machi Mwakani.
Hivi karibuni Tottenham walipewa kibali cha kuupanua na kuuendeleza Uwanja wao White Hart Lane na Manispaa ya eneo lao hatua ambayo ilisifiwa na Mbunge wa eneo hilo, David Lammy, ambae pia ameuponda uongozi wa Tottenham kwa kuutaka Uwanja wa Olimpiki.
Mbunge huyo alisema: “Kuendeleza White Hart Lane ni hatua bora lakini kuhamia Uwanja ulio mbali na hapa ni makosa makubwa. Klabu za Soka zinatakiwa zibaki kwenye jamii yake eneo lile lile. Mashabiki hawataisamehe Spurs ikihama!”
Holloway aomba radhi kumkashifu Refa
Meneja wa Blackpool Ian Holloway ameomba radhi kwa kumtukana Refa Mike Dean baada ya Timu yake kufungwa 2-1 na Blackburn wiki iliyokwisha.
FA ilimshitaki Holloway kwa utovu wa nidhamu.
Holloway ametamka: “Nakiri nilimtukana na hilo ni kosa. Inabidi nijufunze kwani sielewi maamuzi mengine ya Marefa lakini natakiwa niwe mtulivu na kuwaachia Marefa wafanye kazi yao.”
Holloway amesema ameongea na Marefa na Mkuu wao atakuja kumwelekeza nini rafu na nini si rafu.
Rooney atoboa kuumia roho
Wayne Rooney ametoboa kuwa matukio yaliyomwandama Miezi ya hivi karibuni yamemwumiza sana na kufanya kiwango chake kiporomoke.
Tangu kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwezi Juni na tangu Msimu mpya wa Ligi Kuu uanze, Rooney ameonekana kupwaya mno.
Nje ya uwanja, Rooney amekumbwa na kashfa ya kutembea na changudoa wakati mkewe yuko mja mzito.
Rooney ametamka: “Ni wazi ni wakati mgumu kwangu lakini ni bora niendelee kucheza soka tu na kila kitu kitanyooka. Mie ni binadamu na naumia roho, ni lazima niyashinde haya nirudishe kiwango changu!”
Tangu Msimu huu uanze Rooney amefunga bao moja tu kwa njia ya penati dhidi ya West Ham na Man United ilimuacha kwenye mechi na Valencia Siku ya Jumatano baada ya kuwa na maumivu ya enka aliyoumia wikiendi iliyopita lakini sasa amepona na huenda leo akacheza mechi ya Ligi na Sunderland.

Friday, 1 October 2010

Wenger: ‘Arsenal ya kuungaunga ina uwezo kuifunga Chelsea!’
Arsene Wenger ana imani kubwa Timu yake Arsenal inao uwezo mkubwa kuwafunga Mabingwa Watetezi na vinara wa Ligi Kuu, Chelsea, watakapokutana Jumapili huko Stamford Bridge licha ya kuwakosa Wachezaji kadhaa wa Timu ya kwanza.
Siku hiyo, Arsenal itabidi icheze bila Nahodha Cesc Fabregas na Mastaa wengine kama vile Kipa Manuel Almunia, Kieran Gibbs, Thomas Vermaelen, Theo Walcott na Robin van Persie ambao wote ni majeruhi.
Arsenal walifungwa 3-2 na West Brom kwenye mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu wikiendi iliyopita Uwanjani Emirates lakini juzi walishinda kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI huko Serbia kwa kuilaza Partizan Belgrade 3-1.
Wenger amedai: “Naamini tuna uwezo wa kushinda. Tukicheza vizuri tutashinda. Uwezo upo licha ya Chelsea kuwa Timu nzuri.”
Spurs yahofia Huddlestone kufungiwa na UEFA!
Klabu ya Tottenham Hotspur inasubiri kwa wasiwasi mkubwa uchunguzi wa UEFA kuhusu Mchezaji wao Tom Huddlestone ambae alionekana akimpiga kiwiko Mchezaji wa FC Twente Marc Janko kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Jumatano huko White Hart Lane ambayo Spurs walishinda bao 4-1.
Janko amedai Huddlestone alikusudia kumpiga kipepsi wakati Wachezaji hao walipovaana katika tukio ambalo Refa alipiga filimbi kuashiria ni Janko ndie aliecheza faulo.
UEFA imethibitisha kuchunguza mikanda ya tukio hilo na endapo Huddlestone atapatikana na hatia atafungiwa mechi zijazo za Tottenham za UEFA CHAMPIONS LIGI ambazo ni pamoja na mechi mbili mfululizo na Inter Milan.
LIGI KUU England: Mechi za Wikiendi hii
Jumamosi, 2 Octoba 2010
[Saa za Bongo]
[Saa 8 dak 45 mchana]
Wigan v Wolverhampton
[Saa 11 jioni]
Birmingham v Everton
Stoke v Blackburn
Sunderland v Man United
Tottenham v Aston Villa
West Brom v Bolton
West Ham v Fulham
Jumapili, 3 Octoba 2010
[Saa 9 na nusu mchana]
Man City v Newcastle
[Saa 11 jioni]
Liverpool v Blackpool
[Saa 12 jioni]
Chelsea v Arsenal
TATHMINI:
Chelsea v Arsenal
Ni mechi kubwa na yenye mvuto mkubwa na ipo Jumapili huko Stamford Bridge ambako Chelsea watawakaribisha wenzao wa London Arsenal huku timu zote mbili zikiwa zimetoka kwenye vipigo vyao vya kwanza vya Ligi katika mechi zao za mwisho wikiendi iliyopita.
Arsenal walifungwa nyumbani 3-2 na West Bromwich Albion.
Chelsea walipigwa 1-0 na Manchester City.
Arsenal wamekuwa wakipata wakati mgumu kila wanapocheza na Chelsea katika miaka ya hivi karibuni huku Didier Drogba akiwa ndie mwiba mkubwa kwao akiwa amewafunga goli 10 katika mechi 12 kati yao.
Katika mechi 17 za mwisho kati ya Chelsea na Arsenal, Arsenal wameshinda mara mbili tu.
Sunderland v Manchester United
Baada ya ushindi mtamu ugenini huko Uwanja wa Mestall walipoifunga Valencia bao 1-0 kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI, Man United wanasafiri tena kwenda kucheza na Sunderland.
Msimu huu Man United wametoka sare 3 katika mechi zao zote za ugenini huku wakiruhusu lundo ya magoli lakini kupona kwa Rio Ferdinand, ambae alicheza na Valencia akishirikiana na patna wake wa siku zote Nemanja Vidic, kutaleta ahueni kwa Mashabiki wa Mashetani hao Wekundu.
Tottenham v Aston Villa
Aston Villa, chini ya Meneja mpya Gerard Houllier, watakuwa White Hart Lane kuivaa Tottenham ambayo wiki iliyopita ilipigwa na West Ham.
Villa walishinda 2-1 dhidi ya Wolves wiki iliyopita.
Wigan v Wolves
Uwanjani DW, Wigan wanaikaribisha Wolves na timu hizi zimetenganishwa kwa pointi moja tu kati yao.
West Ham v Fulham
West Ham, baada ya kuifunga Tottenham, watataka kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Fulham ambayo bado haijafungwa kwenye Ligi Msimu huu kwa kutoka sare mechi 5 kati ya 6 walizocheza.
Birmingham v Everton
Everton wapo mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu na wana pointi 3 na mechi hii dhidi ya Birmingham Uwanjani kwao kwa Mtakatifu Andrew ni ngumu mno kwani Birmingham hawafungiki hapo na hawajafungwa katika mechi 18 za Ligi uwanjani hapo.
West Brom v Bolton
West Brom watakuwa nyumbani Uwanjani Hawthorns na bado wana moto wa kuiadhibu Arsenal bao 3-2 huko Emirates wikiendi iliyokwisha.
Nao Bolton wana furaha ya kutoka sare 2-2 na Manchester United.
Hivyo pambano hili litakuwa la vuta ni kuvute.
Stoke City v Blackburn Rovers
Hili pambano lipo Uwanja wa Britannia na linazikutanisha Timu zinazocheza staili ya aina moja tu ya ile ‘vita mbele’ na hivyo moto utawaka uwanjani.
Katika mechi zao 3 za mwisho za Ligi Stoke wamevuna pointi 7 kati ya 9 na Blackburn hawajafungwa katika mechi zao 3 za mwisho.
Manchester City v Newcastle
Ndio kwanza wametoika kuiua Chelsea, hivyo Man City bado wana moto na wanapambana na Newcastle ambayo hivi karibuni imeonyesha kuteleza kwani baada ya kushinda mechi mbili wakafungwa mechi 3 zilizofuata.
Liverpool v Blackpool
Ushindi kwa Liverpool ni kitu muhimu mno kwani Msimu huu kwenye Ligi wameonyesha ugoigoi mkubwa.
Blackpool nao hawapo katika hali nzuri na katika mechi ya wikiendi iliyopita walifungwa nyumbani na Blackburn
Rooney yuko fiti
Straika wa Manchester United Wayne Rooney yuko fiti kuichezea England kwenye mechi ya Makundi ya EURO 2012 na Montenegro hapo Oktoba 12 baada ya kupona enka yake lakini Meneja wake Sir Alex Ferguson amesema ni mapema mno kumchezesha hapo kesho na Sunderland kwenye Ligi Kuu.
Ferguson amesema Rooney alianza mazoezi Alhamisi na mwenyewe yuko tayari kucheza Jumamosi lakini itabidi afikirie sana kwa vile hata kumharakisha.
Kupona kwa Rooney kutamsaidia sana Meneja wa England Fabio Capello kwani Wachezaji wake wengi wa mbele ni majeruhi. Listi ya majeruhi wapo Frank Lampard, Theo Walcott, Jermain Defoe na Bobby Zamora.

Thursday, 30 September 2010

EUROPA LIGI Leo:
Man City 1 Juve 1
Manchester City wakiwa kwao na kuwa nyuma bao moja walijitutumua na kurudisha na kufanya ngoma iwe 1-1 na Vigogo wa Italia Juventus katika mechi ya Kundi A.
Juventus walifunga bao lao kupitia Iaquinta dakika ya 10 na Adam Johnson kusawazisha dakika ya 37.
FC Utrecht 0 Liverpool 0
Liverpool, wakicheza bila Nahodha wao Steven Gerrard, wametoka sare 0-0 na FC Utrecht huko Uholanzi katika mechi iliyopooza ingawa ilitawaliwa na Ultrecht.
MATOKEO MECHI NYINGINE:
Alhamisi, 30 Septemba 2010
Borussia Dortmund 0 Sevilla 1
CSKA Moscow 3 Sparta Prague 0
CSKA Sofia 0 FC Porto 1
FC Metalist Kharkiv 0 PSV Eindhoven 2
FC UTRECHT 0 LIVERPOOL 0
Hajduk Split 1 Anderlecht 0
Odense BK 1 VfB Stuttgart 2
Paris SG 2 Karpaty Lviv 0
Rapid Vienna 1 Besiktas 2
Sampdoria 1 Debrecen 0
Steaua Bucharest 3 Napoli 3
Young Boys 2 Getafe 0
Zenit St Petersburg 4 AEK Athens 2
AA Gent 1 Lille 1
Atletico Madrid 1 Bayer Leverkusen 1
BATE Borisov 4 AZ Alkmaar 1
FC Sheriff Tiraspol 2 Dynamo Kiev 0
Lech Poznan 2 Red Bull Salzburg 0
MAN CITY 1 JUVENTUS 1
PAOK Salonika 1 Dinamo Zagreb 0
Palermo 1 Lausanne Sports 0
Rosenborg 2 Aris Salonika 1
Sporting 5 Levski Sofia 0
Villarreal 2 Club Bruges 1
Bruce ahofu kuumia Rooney ni geresha!
Bosi wa Sunderland Steve Bruce, ambae alikuwa Mchezaji wa Manchester United enzi za uchezaji wake, haamini kama Wayne Rooney ni majeruhi kweli na ana hisia atacheza mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu wakati Manchester United itakapotembelea Stadium of Light kuikwaa Sunderland.
Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United, alitangaza kuwa Rooney atakuwa nje kwa wiki tatu baada ya kuumia enka kwenye mechi ya Ligi Jumamosi iliyopita walipocheza na Bolton na jana hakuwemo kwenye Kikosi kilichocheza na Valencia kwenye ushindi wa 1-0 wa UEFA CHAMPIONS LIGI.
Lakini Msimu huu Rooney ameporomoka kiwango kufuatia uchezaji mbovu huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia na hivi karibuni amejikuta akinangwa na Magazeti kuwa alitembea na changudoa wakati mkewe yuko mja mzito.
Steve Bruce, ambae anamjua fika Ferguson tangu alipokuwa Mchezaji wake huko Manchester United, amehoji: “Ni kweli Rooney yuko nje wiki 3? Sijui hilo lakini sishangai akicheza kwani siku zote hutajua kama Sir Alex anatumia mbinu zake!”
Bruce amekiri huu ni wakati mgumu kwa Rooney lakini amebainisha kuwa Staa huyo yupo kwenye himaya nzuri chini ya Ferguson ambae huwaangalia vizuri Wachezaji wake.
Sunderland wataingia mechi ya Jumamosi dhidi ya Manchester United huku tayari wameshawafunga Manchester City na kutoka sare na Arsenal na Liverpool.
Rio yu tayari!
Beki mahiri wa Manchester United Rio Ferdinand amesema yuko fiti kucheza mechi zote baada ya kupona goti aliloumia huko Afrika Kusini mwezi Juni wakati England ilipokuwa kambini kwa ajili ya Kombe la Dunia lakini uamuzi wa mechi zipi atacheza upo kwa Meneja wake Sir Alex Ferguson.
Tangu apone Rio amekuwa akicheza mechi moja kwa wiki na alianza kucheza mechi na Rangers ya UEFA CHAMPIONS LIGI lakini aliachwa mechi ya Ligi na Liverpool kisha akacheza mechi na Scunthorpe ya Carling Cup lakini hakucheza na Bolton na jana alicheza dhidi ya Valencia kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.
Kuhusu hali hiyo, Rio amesema: “Nahitaji kucheza lakini hilo ni juu ya Meneja wangu na yeye ana uzoefu mkubwa kupita mtu yeyote duniani.”
Wenger: ‘Fabregas fifte fifte kucheza na Chelsea’
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa kuna hatihati kama Cesc Fabregas atakuwa fiti kucheza na Chelsea huko Stamford Bridge Jumapili kwenye BIGI MECHI ya Ligi Kuu.
Fabregas aliumia musuli ya mguu wiki mbili zilizopita Arsenal walipotoka sare na Sunderland.
Wenger amesema watajua Jumamosi asubuhi kama Nahodha wao atacheza au la.
Wiki iliyopita Arsenal walichapwa 3-2 na West Brom Uwanja wa Emirates kwenye Ligi Kuu lakini Jumanne walipata ushindi wa 3-1 ugenini walipoichapa Partizan Belgrade kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.
Chelsea wajitayarisha kwa Ze Gunners bila Ancelotti
Chelsea wapo kwenye maandalizi ya BIGI MECHI ya Ligi Kuu ya Jumapili watakapoikaribisha Arsenal Stamford Bridge bila ya Meneja wao Carlo Ancelotti ambae amefiwa na Baba yake mzazi huko kwao Italia.
Giuseppe Ancelotti, Miaka 87, alifariki hapo jana Jumatano na anazikwa Jumamosi.
Carlo Ancelotti yupo huko Italia kwenye msiba lakini Klabu yake Chelsea imethibitisha atakuwepo Stamford Bridge Jumapili kwenye mechi na Arsenal.
Ray Wilkins, ambae ndie Msaidizi wa Ancelotti, ndie anaitayarisha Timu kwa pambano hilo la Jumapili.
Wiki iliyokwisha, Chelsea walipata kipigo chao cha kwanza kwenye Ligi Kuu Msimu huu walipofungwa 1-0 na Manchester City lakini bado wanaongoza Ligi hiyo huku wakiwa pointi 3 mbele ya Manchester United na pointi 4 mbele ya Arsenal.
Wiki iliyopita, Arsenal nao walitandikwa 3-2 na West Bromwich Albion kwenye Ligi.
Ferguson amsifia Hernandez
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amemsifia Javier Hernandez, aka Chicharito, baada ya bao lake la dakika ya 85 kuipa ushindi Manchester United wa 1-0 dhidi ya Valencia huko Spain kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI hapo jana.
Hernandez, maarufu kama Chicharito ikimaanisha njegere ndogo, aliingizwa kipindi cha pili, na Ferguson mwenye furaha alitamka: “Jinsi alivyofunga lile goli ni kama kuchambua njegere! Ana kipaji halisi ingawa inabidi ajenge mwili wake. Ni mmaliziaji mahiri!”
Mwenyewe Chicharito alitamka: “Ni usiku mzuri kwangu. Nina furaha kufunga goli zuri na muhimu. Nlipokuwa nyumbani Mexico tulikuwa tunaangalia UEFA CHAMPIONS LIGI. Ni mashindano makubwa duniani. Ndio kwanza nimeanza kuichezea Man United hivyo kufunga goli UEFA kutanipa imani kubwa. Ni fahari na sifa kubwa kuchezea Man United na nataka hili liendelee muda mrefu.”
Ferguson pia alimsifia Rio Ferdinand ambae jana alicheza dabo Sentahafu na Nemanja Vidic kwa kuleta utulivu kwenye ngome ya Man United ambayo hivi karibuni ilikuwa ikivuja mno.

Wednesday, 29 September 2010

UEFA CHAMPIONS LIGI:
MATOKEO:
Jumatano, 29 Septemba 2010
Rubin Kazan 1 Barcelona 1
Hapoel Tel-Aviv 1 Lyon 2
Inter Milan 4 Werder Bremen 0
Panathinaikos 0 FC Copenhagen 2
Rangers 1 Bursaspor 0
Schalke 2 Benfica 0
Tottenham 4 FC Twente 1
Valencia 0 Man Utd 1
UEFA CHAMPIONS LIGI: Rubin Kazan 1 Barca 1
Katika mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI iliyoanza mapema leo kupita zote huko Urusi, FC Rubin Kazan walitoka sare na Magwiji wa Ulaya FC Barcelona kwa bao 1-1.
Ni Rubin Kazan ndio walitangulia kupata bao dakika ya 30 kwa penati iliyofungwa na Cristian Noboa na Barca kusawazisha kwa penati dakika ya 60 mfungaji akiwa ni David Villa.
Katika mechi ya leo, Staa Lionel Messi ambae alikuwa majeruhi hivi karibuni, alianzia benchi na kuingizwa kipindi cha pili.
Mtandao wa Uhamisho Wachezaji wa FIFA rasmi Ijumaa
Kuanzia Ijumaa Wiki hii, Uhamisho wa Kimataifa wa Wachezaji Soka lazima upitie kwenye Mtandao wa Uhamisho wa FIFA ujulikanao kama TMS [Transfer Matching System].
Mwanzoni mwa Mwaka huu wakati FIFA ilipoutambulisha mfumo huo mpya wa Uhamisho ilisema njia hiyo mpya itadhibiti uhamisho wa Kimataifa wa Wachezaji na kuondoa kasoro nyingi zikiwemo zile za Wachezaji kumilikiwa na Kampuni badala ya Klabu wanazochezea na ununuzi wa Wachezaji hao unaohusishwa kuhodhi pesa kinyume cha sheria.
Meneja Mkuu wa TMS, Mark Goddard, alisema: “Mpaka sasa mtindo uliokuwa ukitumiwa ni wa makaratasi kama ilivyokuwa miaka 100 nyuma! Ilikuwa ngumu kufuatilia Wachezaji gani wamehamishwa. Kulikuwa na uhamisho feki, kulikuwa na uuzwaji wa Wachezaji ambao hawapo ili mradi Watu mafisadi wahamishe pesa zao toka Nchi moja hadi nyingine kinyume cha sheria!”
Katika mfumo wa TMS uanaotumia mtandao, ili kukamilisha uhamisho wa Mchezaji inabidi Klabu zinazouza na kununua Mchezaji ziingize kwenye mtandao taarifa zote zinazotakiwa kuhusiana na Mchezaji anaehamishwa zikiwemo ada ya uhamisho, mshahara wa Mchezaji huyo, Wakala wake au Mwanasheria wake na muda wa mkataba wake.
Pia, ada ya uhamisho ni lazima itoke Benki moja kwenda nyingine.
Goddard alisema: “Huu ni mradi mkubwa wa FIFA. Haujabadilisha sheria za uhamisho bali unadhibiti uhamisho na kuondoa kasoro na dosari nyingi.”
Moja ya kasoro hizo ni ile ya Wachezaji kumilikiwa na ‘Watu baki” badala ya Klabu. Mtindo huo ni kitu cha kawaida huko Marekani ya Kusini ambako baadhi ya Wachezaji humilikiwa na Makampuni, Mawakala na hata Mifuko ya Pensheni.
Mfano maarufu ni umiliki wa Mchezaji Carlos Tevez aliechukuliwa na West Ham kutoka Corinthians lakini ikabainika baadae kuwa Corinthians haikuwa ikimmiliki.
West Ham ilipigwa faini ya Pauni Milioni 5.5 Aprili 2007 kwa kukiuka sheria za Ligi Kuu zinazokataza Mchezaji kumilikiwa na Kampuni binafsi badala ya Klabu.
Vilevile, mtindo huu wa TMS utaondoa kesi za madai zinazohusiana na kutolipwa au kutokamilishwa ada ya uhamisho wa Mchezaji kwa vile vitu vyote vitakuwa wazi mtandaoni.
Goddard ameongeza kuwa mtindo huo mpya unarahisisha mno uhamisho wa Mchezaji na akatoa mfano wa Mchezaji mmoja aliehama Klabu moja kutoka England na kwenda Scotland na uhamisho wote ikiwemo kupata kibali cha Kimataifa vilichukua dakika 7 tu na Mchezaji huyo akafanikiwa kuichezea Klabu yake mpya siku hiyo hiyo.
Wenger amfurahia Fabianski
Arsène Wenger amemtaka Kipa wake nambari mbili Lukasz Fabianski kutumia nafasi ya kuumia kwa Manuel Almunia ili adhihirishe yeye ni Kipa bora na anastahili kupewa namba.
Jana Fabianski ndie alikuwa langoni katika ushindi wa ugenini wa 3-1 dhidi ya Partizan Belgrade na aling’ara na pia kuukoa penati.
Mtihani mkubwa kwa Fabianski ni Jumapili ijayo wakati Arsenal watakapotua Stamford Bridge kucheza na Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Chelsea ambao pia ni vinara wa Ligi.
Wenger alitamka: “ Fabianski alicheza vizuri. Tumemwona Mchezaji yuleyule tunaemwona mazoezini. Nina hakika atakuwa Kipa bora, anataka uzoefu tu!"
EUROPA LIGI: Kesho ni lundo la mechi!
• FC Utrecht v Liverpool: Gerrard apumzishwa!
• Man City v Juventus
Kesho Liverpool watakuwa huko Uholanzi kucheza mechi yao ya pili ya Kundi lao la EUROPA LIGI watakapokutana na FC Utrecht lakini Nahodha wao Steven Gerrard hatasafiri nao baada ya Meneja Roy Hodgson kuamua kumpumzisha.
Pia Mlinzi Daniel Agger ameachwa katika Kikosi hicho lakini Staa Fernando Torres yumo katika Kikosi cha Wachezaji 20 waliosafiri.
Mmoja wa Wachezaji ambae yumo Kikosini ni Dirk Kuyt ambae ni Mchezaji wa zamani wa FC Utrecht.
Hapo Septemba 16, Liverpool iliifunga Steaua Bucharest 4-1 katika mechi yao ya kwanza ya Kundi lao.
Kikosi kamili kilichosafiri:
Reina, Jones, Johnson, Kelly, Kyrgiakos, Skrtel, Carragher, Shelvey, Poulsen, Lucas, Rodriguez, Spearing, Babel, Meireles, Jovanovic, Cole, Kuyt, Eccleston, Ngog, Torres.
Nao Manchester City, baada ya ushindi wa 2-0 ugenini huko Austria walipowachapa Red Bull Salzburg, kesho watakuwa nyumbani kuwakwaa Wakongwe wa Italia Juventus ambao walitoka sare 3-3 na ‘vibonde’ Lech Poznan kutoka Poland katika mechi yao ya kwanza ya Kundi hili.
RATIBA YA MECHI:
Alhamisi, 30 Septemba 2010
Borussia Dortmund v Sevilla
CSKA Moscow v Sparta Prague
CSKA Sofia v FC Porto
FC Metalist Kharkiv v PSV Eindhoven
FC UTRECHT V LIVERPOOL
Hajduk Split v Anderlecht
Odense BK v VfB Stuttgart
Paris SG v Karpaty Lviv
Rapid Vienna v Besiktas
Sampdoria v Debrecen
Steaua Bucharest v Napoli
Young Boys v Getafe
Zenit St Petersburg v AEK Athens
AA Gent v Lille
Atletico Madrid v Bayer Leverkusen
BATE Borisov v AZ Alkmaar
FC Sheriff Tiraspol v Dynamo Kiev
Lech Poznan v Red Bull Salzburg
MAN CITY V JUVENTUS
PAOK Salonika v Dinamo Zagreb
Palermo v Lausanne Sports
Rosenborg v Aris Salonika
Sporting v Levski Sofia
Villarreal v Club Bruges
UEFA CHAMPIONS LIGI: Jana Chelsea, Arsenal zapeta, Leo ni Man United na Tottenham
Baada ya Chelsea na Arsenal kushinda mechi zao za UEFA CHAMPIONS LIGI hapo jana wakati Chelsea walipoifunga Marseille kwa bao 2-0 na Arsenal kushinda 3-1 dhidi ya Partizan Belgrade, leo ni zamu za wenzao Manchester United ambao wako ugenini Spain kucheza na Valencia na Tottenham watakaokuwa nyumbani White Hart Lane kucheza na FC Twente.
Chelsea walishinda 2-0 dhidi ya Marseille wakiwa kwao Stamford Bridge kwa mabao ya kipindi cha kwanza ya John Terry na Nicolas Anelka aliefunga kwa penati.
Nao Arsenal wakicheza huko Serbia na Partizan Belgrade walishinda 3-1 kwa mabao ya Arshavin, Marouane Chamakh na Sebastien Squillaci.
Bao la Partizan lilifungwa na Cleverson Gabriel Cordova ambae pia baadae alikosa kufunga penati.
Nae Arshavin aliikosesha bao Arsenal baada ya pia kukosa penati.
Nako huko Estadio Mestalla, vinara wa La Liga Valencia watawakaribisha Manchester United ambao watawakosa Mastaa wao Wayne Rooney, Ryan Giggs na Paul Scholes ambao ni majeruhi.
Lakini majeruhi walioopona, Rio Ferdinand na Michael Carrick, huenda wakaingia dimbani.
Nao, Tottenham, baada ya kwenda sare ugenini ya 2-2 na Werder Bremen kwenye mechi ya kwanza ya Kundi lao, leo wapo nyumbani kucheza na FC Twente ya Uholanzi ambao pia walitoka sare ya 2-2 kwenye mechi ya kwanza na Mabingwa Watetezi Inter Milan.
MECHI ZA LEO NI:
Jumatano, 29 Septemba 2010
[Saa 3 dak 45 usiku bongo taimu]
Rubin Kazan v Barcelona [Saa 1 na nusu usiku]
Hapoel Tel-Aviv v Lyon
Inter Milan v Werder Bremen
Panathinaikos v FC Copenhagen
Rangers v Bursaspor
Schalke 04 v Benfica
Tottenham v FC Twente
Valencia v Man Utd

Tuesday, 28 September 2010

UEFA CHAMPIONS LIGI:
MATOKEO:
Jumanne, 28 Septemba 2010
Spartak Moscow 3 MSK Zilina 0
Auxerre 0 Real Madrid 1
Basle 1 Bayern Munich 2
Braga 0 Shakhtar Donetsk 3
Chelsea 2 Marseille 0
Partizan Belgrade 1 Arsenal 3
Roma 2 CFR Cluj-Napoca 1
Ajax 1 AC Milan 1
RATIBA:
Jumatano, 29 Septemba 2010
[Saa 3 dak 45 usiku bongo taimu]
Rubin Kazan v Barcelona [Saa 1 na nusu usiku]
Hapoel Tel-Aviv v Lyon
Inter Milan v Werder Bremen
Panathinaikos v FC Copenhagen
Rangers v Bursaspor
Schalke 04 v Benfica
Tottenham v FC Twente
Valencia v Manchester United
Rooney nje Wiki 3
Manchester United imetangaza kuwa Wayne Rooney hatacheza kwa wiki 3 ili kuuguza enka yake aliyoumia Jumamosi kwenye mechi ya Ligi Kuu walipocheza na Bolton na kutoka sare 2-2.
Rooney hakuwemo kwenye Kikosi cha Man United kilichoenda Spain kucheza na Valencia hapo kesho kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI .
Pia Nyota huyo atazikosa mechi ya Ligi Kuu ya Jumamosi Man United watakapoenda ugenini kucheza na Sunderland na pia mechi ya England ya EURO 2012 dhidi ya Montenegro Oktoba 12.
Mbali ya kuumia, fomu ya Rooney Msimu huu imeporomoka na hata Meneja wake wa Man United Sir Alex Ferguson amekiri hilo na kusema ni kwa sababu ya kusakamwa mno na Magazeti.
Hivi karibuni, Rooney alilipuliwa na Magazeti na skandali la kudaiwa kutembea na changudoa wakati mkewe akiwa mja mzito.
FA yamshitaki Meneja wa Blackpool
Meneja wa Blackpool Ian Holloway ameshitakiwa kwa utovu wa nidhamu na vitendo vyake kwa Marefa.
Jumamosi, Blackpool, wakiwa nyumbani, walifungwa 2-1 na Blackburn kwenye mechi ya Ligi Kuu na Holloway alichukizwa na goli la pili kufungwa kwenye dakika za majeruhi.
Baada ya mechi, Holloway alitamka: “Refa [Mike Dean] alichezesha vibaya na najua ataniripoti kwa kumpa maneno yake baada ya mechi wakati tukitoka uwanjani. Nadhani kulikuwa na maamuzi ya kushangaza.”
Blackpool waliudhiwa na goli la ushindi la Blackburn kufungwa dakika za majeruhi huku Mfungaji Brett Emerton akiwa ofsaidi na pia wakati linaenda kufungwa Mchezaji wa Blackpool, Gary Taylor-Fletcher, alifanyiwa madhambi.
Kufuatia na kanuni mpya za FA za kuharakisha kesi, Holloway anatakiwa ajibu mashitaka hayo ifikapo Ijumaa na akikiri kabla ya hapo atapigwa Faini ya Pauni 8000 na kufungiwa mechi moja.
Ikiwa atapinga mashitaka yake kesi itapelekwa kwenye Kamati ya Sheria na huko anaweza kupewa adhabu kali zaidi akipatikana na hatia.
Scholes & Rooney nje tripu ya Spain
Manchester United imeelekea Spain ambako kesho itacheza na Vinara wa La Liga Valencia kwenye mechi ya Kundi lao ya UEFA CHAMPIONS LIGI bila ya Wachezaji mahiri kadhaa kwenye Kikosi cha Wachezaji 22.
Paul Scholes, Wayne Rooney na Ryan Giggs hawakwenda Spain na wakati Scholes amepumzishwa tu, Rooney na Giggs ni majeruhi.
Lakini Kiungo Michael Carrick ambae hajacheza tangu mechi ya ufunguzi ya Msimu huu ya Ngao ya Hisani dhidi ya Chelsea yumo baada ya kupona maumivu na huenda kesho akacheza.
Katika mechi za ufunguzi za Kundi C, Man United walitoka sare 0-0 na Rangers wakati Valencia waliichapa ugenini Bursapor ya Uturuki kwa bao 4-0.
Licha ya kuondokewa na Mastaa wao David Villa na David Silva, Valencia ndio wametwaa uongozi wa La Liga Msimu huu na Kiungo wa Man United Darren Fletcher amekiri: “Ni mechi ngumu. Wao wameanza vizuri Ligi yao lakini sisi wazoefu wa mechi za Ulaya.”
Fletcher ameongeza pia kwa kusema kitu muhimu ukicheza na Timu za Spain ni kumiliki mpira kwani ukiupoteza utachukua muda mrefu kuunasa tena na hilo litakutesa.
Kikosi kilichosafiri ni:
Van der Sar, Kuszczak, Amos, Rafael, O'Shea, Brown, Ferdinand, Vidic, Evans, Smalling, Evra, Nani, Fletcher, Anderson, Carrick, Gibson, Park, Bebe, Berbatov, Owen, Hernandez, Macheda.

Monday, 27 September 2010

FIFA yamsaidia Kipa wa Togo aliepigwa risasi Angola
Kipa wa Togo Kodjovi Obilale, ambae alijeruhiwa kwa risasi na Waasi wa Cabinda wakati Basi la Timu yao lilipokuwa likiingia Angola toka Congo kwenda kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na tukio hilo kuwaua Watu wawili kwenye msafara, amesema FIFA imempa msaada wa Dola 25,000.
Obilale, Miaka 25, alipigwa risasi mgongoni na hadi sasa ikiwa Miezi minane imepita hawezi kutembea.
Obilale, aliepokea barua kutoka kwa Rais wa FIFA Sepp Blatter, amesema: “Huu ni wema!”
Kipa huyo wa Togo alikerwa na CAF kwa kutomsaidia na ndipo alipomwandikia barua Sepp Blatter.
Katika barua yake, Blatter ameahidi kulichunguza jalada la Kipa huyo na kumtakia moyo wa kishujaa kukabiliana na matatizo yake.
Obilale alikuwa akichezea Timu ya Daraja la chini huko Ufaransa na hadi sasa hawezi kuusogeza mguu wake wa kulia chini ya goti ambao pia umekufa ganzi.
UEFA CHAMPIONS LIGI: Vumbi Ulaya kesho na Jumatano
Ratiba
Jumanne, 28 Septemba 2010
[Saa 3 dak 45 usiku bongo taimu]
Spartak Moscow v MSK Zilina [Saa 1 na nusu usiku]
Ajax v AC Milan
Auxerre v Real Madrid
Basle v Bayern Munich
Braga v Shakhtar Donetsk
Chelsea v Marseille
Partizan Belgrade v Arsenal
Roma v CFR 1907 Cluj-Napoca
________________________________________
Jumatano, 29 Septemba 2010
[Saa 3 dak 45 usiku bongo taimu]
Rubin Kazan v Barcelona [Saa 1 na nusu usiku]
Hapoel Tel-Aviv v Lyon
Inter Milan v Werder Bremen
Panathinaikos v FC Copenhagen
Rangers v Bursaspor
Schalke 04 v Benfica
Tottenham v FC Twente
Valencia v Man Utd
Tathmini:
Mabingwa Inter Milan, Washindi wa Pili Bayern Munich, wanaoshikilia rekodi ya Ubingwa Ulaya mara nyingi Real Madrid na Klabu za England nne, Chelsea, Manchester United, Tottenham na Arsenal, zote zilipata matokeo yasiyoridhisha kwenye Ligi za nyumbani kwao Wikiendi hii.
Kati ya Vigogo hao 7 wa Ulaya, hakuna alieshinda mechi zao za Ligi huku Inter, Bayern, Chelsea, Arsenal na Tottenham Hotspur wakifungwa na Real Madrid na Manchester United wakipata sare.
Sasa Vigogo hao 7 watalenga makucha yao huko Ulaya kesho Jumanne na kesho kutwa Jumatano kuwania ushindi katika mechi za pili za Makundi yao katika kinyang’anyiro cha UEFA CHAMPIONS LIGI.
Katika Kundi H, Arsenal wanasafiri kwenda kuikumba Partizan Belgrade wakitokea kwenye ushindi wa 6-0 dhidi ya Sporting Braga katika mechi yao ya kwanza ya Kundi lao.
Kwenye mechi hii ya kesho, Arsenal inakabiliwa na majeruhi wakiwemo Kipa Manuel Almunia, Cesc Fabregas, Abou Diaby, Robin van Persie, Theo Walcott, Nicklas Bendtner, Kieran Gibbs na Thomas Vermaelen.
Mabingwa wa England Chelsea, waliopigwa 1-0 na Manchester City Jumamosi kwenye Ligi Kuu, wanawakaribisha Wafaransa Olympique Marseille Uwanjani Stamford Bridge Siku ya Jumanne.
Chelsea inao majeruhi kwa Mastaa wao wakiwemo Frank Lampard, Salomon Kalou na Yossi Benayoun na huku Didier Drogba akiwa amesimamishwa kwa mechi hii.
Chelsea walishinda mechi yao ya kwanza huko Slovakia kwa kuifunga MSK Zilina 4-1.
Jumanne, Bayern Munich watakuwa Uswisi kucheza na Basel huku wakitokea kwenye kipigo cha 2-1 kwenye Bundesliga dhidi ya Mainz.
Kocha wa Basel ni Thorsten Fink ambae aliwahi kutwaa Ubingwa wa Ulaya wakati akiwa Mchezaji wa Bayern Munich Mwaka 2001.
Kundi G ni mechi kati ya Auxerre na Real Madrid na Ajax Amsterdam v AC Milan.
Mabingwa Watetezi Inter Milan watakuwa nyumbani kucheza na Werder Bremen na hii ni mechi muhimu kwao baada ya kuanza utetezi wa taji lao kwa sare ya 2-2 na Mabingwa wa Uholanzi FC Twente Enschede.
Katika mechi nyingine ya Kundi hili la Inter Milan, Tottenham watacheza na FC Twente.
Manchester United, waliotoka sare 0-0 na Rangers, watatua Metsalla Stadium kucheza na vinara wa La Liga Valencia bila Nyota wao Wayne Rooney, Mkongwe Ryan Giggs na Winga Luis Antonio Valencia kwani wote ni majeruhi.
Rangers watakuwa nyumbani kucheza na Waturuki Bursapor.
Rooney kuikosa mechi na Valencia
Manchester United imethibitisha kuwa Nyota wao Wayne Rooney hatasafiri na Kikosi chao kwenda Spain kucheza na Valencia Siku ya Jumatano kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwa sababu ana maumivu ya enka.
Rooney aliumia enka na kutolewa mapema Kipindi cha Pili katika mechi ya jana ya Ligi Kuu Man United ilipotoka sare 2-2 na Bolton Uwanja wa Reebok.
Rooney sasa anaungana na Mkongwe Ryan Giggs kuwa kwenye listi ya majeruhi.
Man United walianza mechi kwenye Kundi C la UEFA CHAMPIONS LIGI kwa kutoka sare 0-0 na Rangers Uwanjani Old Trafford na Valencia walianza kwa kishindo huko ugenini Uturuki kwa kuibamiza Bursapor mabao 4-0.
Kwenye Ligi huko Spain, Valencia ndio vinara wa La Liga.
Lampard kuzikosa mechi muhimu
Frank Lampard atazikosa mechi muhimu za Klabu yake Chelsea na pia za England kwa sababu hajapona vizuri baada kufanyiwa upasuaji kutibu ngiri.
Lampard, Miaka 32, alifanyiwa operesheni mwishoni mwa Agosti na awali ilitegemewa atakaa nje kwa Wiki mbili lakini sasa, baada ya kuwa nje kwa mwezi mzima, Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti amethibitisha atakuwa nje kwa Wiki mbili zaidi.
Kwa kuwa nje kipindi hicho atazikosa mechi za Chelsea dhidi ya Marseille hapo kesho, ile ya Arsenal Oktoba 3 na mechi ya England ya Euro 2012 na Montenegro hapo Oktoba 12.
MATOKEO LIGI ZA ULAYA:
Jumapili, Septemba 26
Serie A
Cesena 1 Napoli 4
Fiorentina 2 Parma 0
Catania 1 Bologna 1
Chievo Verona 0 SS Lazio 1
Sampdoria 0 Udinese 0
Palermo 2 US Lecce 2
As Bari 2 Brescia 1
Juventus 4Cagliari 2
La Liga
Real Mallorca 2 Real Socieda 0
Espanyol 1 Osasuna 0
Deportivo La Coruna 0 Almeria 2
Real Racing Santander 0 Getafe CF 1
Hercules CF 2 Sevilla FC 0
Atletico de Madrid 1 Real Zaragoza 0
German Bundesliga
VfL Wolfsburg 2 SC Freiburg 1
FC Kaiserslautern 0 Hannoverscher 1
French Ligi 1
Brest 1 Valenciennes 0
Toulouse FC 1 Lille OSC 1
Racing Club de Lens 0 Paris Saint-Germain 2
Kipa Almunia nje UEFA CHAMPIONS LIGI
Manuel Almunia ataikosa tripu ya mechi ya UEFA Champions Ligi kwenda kucheza na Partizan Belgrade Siku ya Jumanne baada ya kuumia kiwiko cha mkono kwenye mechi ya Ligi Kuu Jumamosi Arsenal walipofungwa 3-2 na West Bromwich Albion Uwanjani Emirates.
Almunia aliumia wakati alipomwangusha Mshambuliaji wa West Bromwich Peter Odemwingie na kusababisha penati ambayo ilipigwa na Chris Brunt lakini aliikoa.
Hata hivyo Almunia aliingia lawamani kwa kushindwa kuzuia bao rahisi la pili baada ya shuti la Gonzalo Jara kumpenya lakini Meneja wake Arsene Wenger amekataa kumnyooshea kidole.
Kipa wa akiba Lukasz Fabianski anategemewa kudaka katika mechi hiyo na Partizan Belgrade.
Ruud amtaka Rooney ajali Soka lake tu
Ruud van Nistelrooy amemtaka Wayne Rooney kupuuza Magazeti yanayomsakama na badala yake atilie mkazo Soka tu.
Hivi karibuni Magazeti yalimlipua Rooney kwa kutembea na changudoa na hata Meneja wake wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amesema kuandamwa huko kumechangia kushuka kwa kiwango chake.
Lakini Ruud van Nistelrooy, Mchezaji wa zamani wa Manchester United, amemtaka Rooney kupuuza Magazeti hayo na amesema: “Ni England pekee Magazeti yanakusama kuhusu maisha yako ya faragha.”

Sunday, 26 September 2010

Newcastle 1 Stoke 2
Bao la kujifunga mwenyewe la Beki James Perch la dakika ya 85 leo limewapa ushindi Stoke City wa 2-1 dhidi ya Newcastle wakiwa ugenini St James Park kwenye mechi ya Ligi Kuu.
Newcastle walitangulia kupata bao dakika ya 45 kwa penati ya Kevin Nolan lakini Stoke wakarudisha KIpindi cha Pili dakika ya 67 Mfungaji akiwa Kenwyne Jones.
Wolves 1 Aston Villa 2
Bao la kichwa la Emile Heskey dakika ya 88 limempa Meneja mpya wa Aston Villa Gerard Houllier ushindi wake wa kwanza walipocheza Ligi Kuu Uwanja wa Molineux leo na wenyeji Wolves.
Stewart Downing ndie aliwapa Villa bao la kwanza dakika ya 25 na Kipindi cha Pili Wolves walisawazisha dakika ya 62 kupitia Mathew Jarvis.
Ushindi huu umewafanya Villa wafikishe pointi 10 na kudandia nafasi ya 5.
LIGI KUU ENGLAND: Mechi zijazo
Jumamosi, 2 Octoba 2010
[Saa za Bongo]
[Saa 8 dak 45 mchana]
Wigan v Wolverhampton
[Saa 11 jioni]
Birmingham v Everton
Stoke v Blackburn
Sunderland v Man United
Tottenham v Aston Villa
West Brom v Bolton
West Ham v Fulham
Jumapili, 3 Octoba 2010
[Saa 9 na nusu mchana]
Man City v Newcastle
[Saa 11 jioni]
Liverpool v Blackpool
[Saa 12 jioni]
Chelsea v Arsenal
Wenger alalama na Ze Gunners yake!!
Arsene Wenger ameiponda Timu yake Arsenal kufuatia kubondwa jana kwenye mechi ya Ligi Kuu na West Bromwich Albion ambao walijikuta wapo 3-0 mbele kwa mabao ya Peter Odemwingie, Gonzalo Jara na Jerome Thomas lakini Samir Nasri akaifungia Arsenal bao mbili na kufanya mechi imalizike 3-2.
Wenger ametamka” “Ni uchezaji mbovu kwenye difensi na mbele. Hakuna hata Mchezaji mmoja aliecheza kiwango!”
Jumapili ijayo Oktoba 3 kwenye mechi ya Ligi Kuu, Arsenal wataitembelea Stamford Bridge kupambana na Chelsea ambao pia hapo jana walichapwa 1-0 na Manchester City.
Wenger alikataa kumnyooshea kidole Kipa Manuel Almunia ingawa alikuwa mmoja wa Wachezaji waliocheza ovyo kwa kusababisha penati ingawa aliiokoa lakini baadae akafungwa bao mbili ambazo Wataalam wanadai ni makosa yake.
Wakati Wenger ananung’unika, Bosi wa West Brom, Roberto Di Matteo, ameipongeza Timu yake na kudai ilistahili kushinda.
Bolton 2 Man United 2
Leo huko Uwanja wa Reebok nusura Manchester United yawakute yale yaliyowakuta Chelsea na Arsenal hapo jana baada ya Vigogo hao wawili kufungwa lakini Manchester United walibahatika kwa kusawazisha mara mbili baada ya Bolton kuchukua uongozi mara mbili.
Zat Knight ndie alieipatia Bolton bao la kwanza dakika ya 6 baada ya kuunganisha kona lakini Nani akasawazisha kwa bao la juhudi binafsi alipoukokota mpira toka mstari wa kati na kutambuka Mabeki wa Bolton kadhaa kisha kufunga kwenye dakika ya 23.
Bolton tena walipata bao la pili dakika ya 67 kufuatia kaunta ataki baada ya kuunasa mpira baada ya kona ya Manchester United kuokolewa na Martin Petrov akamalizia kwa shuti lililombabatiza Darren Fletcher na kutinga.
Ndipo dakika ya 74 frikiki ya Nani ilipounganishwa na Michael Owen wavuni alieingizwa Kipindi cha Pili na kuwaokoa Man United.
Sare ya leo imewafanya Man United washike nafasi ya pili wakiwa na pointi 12 huku Chelsea wakiwa mbele kwa pointi 3 na nyuma ya Man United ni Arsenal na Man City zenye pointi 11 kila mmoja.
Vikosi vilivyoanza:
Bolton: Jaaskelainen, Steinsson, Knight, Ricketts, Robinson, Lee, Holden, Muamba, Petrov, Elmander, Kevin Davies.
Akiba: Bogdan, Taylor, Mark Davies, Klasnic, Moreno, Blake, Alonso.
Man Utd: Van der Sar, O'Shea, Vidic, Jonathan Evans, Evra, Nani, Fletcher, Scholes, Giggs, Rooney, Berbatov.
Akiba: Kuszczak, Owen, Anderson, Smalling, Park, Rafael Da Silva, Macheda.
Refa: Phil Dowd
LIGI ZA ULAYA:

Matokeo Mechi za Jumamosi, Septemba 25
Calcio League A
AC Milan 1 Genoa 0
AS Roma 1 Inter Milan 0
La Liga
Sporting Gijon 0 Valencia 2
Levante 0 Real Madrid 0
Athletic de Bilbao 1 FC Barcelona 3
Bundesliga
VfB Stuttgart 1 Bayer 04 Leverkusen 4
Schalke 04 2 Borussia Monchengladbach 2
Eintracht Frankfurt 2 FC Nurnberg 0
FC St. Pauli 1 BV Borussia Dortmund 3
Bayern Munich 1 FSV Mainz 2
Werder Bremen 3 Hamburger SV 2
Ufaransa Ligi 1
Nice 1 Stade Rennais FC 2
Montpellier HSC 3 Arles 0
Olympique de Marseille 2 FC Sochaux 1
Lorient 2 AS Monaco 1
Caen 0 FC Girondins de Bordeaux 0
Auxerre 2 AS Nancy Lorraine 2
Olympique Lyonnais 0 St.Etienne 1
Powered By Blogger