Saturday 2 October 2010

Holloway aomba radhi kumkashifu Refa
Meneja wa Blackpool Ian Holloway ameomba radhi kwa kumtukana Refa Mike Dean baada ya Timu yake kufungwa 2-1 na Blackburn wiki iliyokwisha.
FA ilimshitaki Holloway kwa utovu wa nidhamu.
Holloway ametamka: “Nakiri nilimtukana na hilo ni kosa. Inabidi nijufunze kwani sielewi maamuzi mengine ya Marefa lakini natakiwa niwe mtulivu na kuwaachia Marefa wafanye kazi yao.”
Holloway amesema ameongea na Marefa na Mkuu wao atakuja kumwelekeza nini rafu na nini si rafu.
Rooney atoboa kuumia roho
Wayne Rooney ametoboa kuwa matukio yaliyomwandama Miezi ya hivi karibuni yamemwumiza sana na kufanya kiwango chake kiporomoke.
Tangu kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwezi Juni na tangu Msimu mpya wa Ligi Kuu uanze, Rooney ameonekana kupwaya mno.
Nje ya uwanja, Rooney amekumbwa na kashfa ya kutembea na changudoa wakati mkewe yuko mja mzito.
Rooney ametamka: “Ni wazi ni wakati mgumu kwangu lakini ni bora niendelee kucheza soka tu na kila kitu kitanyooka. Mie ni binadamu na naumia roho, ni lazima niyashinde haya nirudishe kiwango changu!”
Tangu Msimu huu uanze Rooney amefunga bao moja tu kwa njia ya penati dhidi ya West Ham na Man United ilimuacha kwenye mechi na Valencia Siku ya Jumatano baada ya kuwa na maumivu ya enka aliyoumia wikiendi iliyopita lakini sasa amepona na huenda leo akacheza mechi ya Ligi na Sunderland.

No comments:

Powered By Blogger