Thursday 30 September 2010

EUROPA LIGI Leo:
Man City 1 Juve 1
Manchester City wakiwa kwao na kuwa nyuma bao moja walijitutumua na kurudisha na kufanya ngoma iwe 1-1 na Vigogo wa Italia Juventus katika mechi ya Kundi A.
Juventus walifunga bao lao kupitia Iaquinta dakika ya 10 na Adam Johnson kusawazisha dakika ya 37.
FC Utrecht 0 Liverpool 0
Liverpool, wakicheza bila Nahodha wao Steven Gerrard, wametoka sare 0-0 na FC Utrecht huko Uholanzi katika mechi iliyopooza ingawa ilitawaliwa na Ultrecht.
MATOKEO MECHI NYINGINE:
Alhamisi, 30 Septemba 2010
Borussia Dortmund 0 Sevilla 1
CSKA Moscow 3 Sparta Prague 0
CSKA Sofia 0 FC Porto 1
FC Metalist Kharkiv 0 PSV Eindhoven 2
FC UTRECHT 0 LIVERPOOL 0
Hajduk Split 1 Anderlecht 0
Odense BK 1 VfB Stuttgart 2
Paris SG 2 Karpaty Lviv 0
Rapid Vienna 1 Besiktas 2
Sampdoria 1 Debrecen 0
Steaua Bucharest 3 Napoli 3
Young Boys 2 Getafe 0
Zenit St Petersburg 4 AEK Athens 2
AA Gent 1 Lille 1
Atletico Madrid 1 Bayer Leverkusen 1
BATE Borisov 4 AZ Alkmaar 1
FC Sheriff Tiraspol 2 Dynamo Kiev 0
Lech Poznan 2 Red Bull Salzburg 0
MAN CITY 1 JUVENTUS 1
PAOK Salonika 1 Dinamo Zagreb 0
Palermo 1 Lausanne Sports 0
Rosenborg 2 Aris Salonika 1
Sporting 5 Levski Sofia 0
Villarreal 2 Club Bruges 1
Bruce ahofu kuumia Rooney ni geresha!
Bosi wa Sunderland Steve Bruce, ambae alikuwa Mchezaji wa Manchester United enzi za uchezaji wake, haamini kama Wayne Rooney ni majeruhi kweli na ana hisia atacheza mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu wakati Manchester United itakapotembelea Stadium of Light kuikwaa Sunderland.
Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United, alitangaza kuwa Rooney atakuwa nje kwa wiki tatu baada ya kuumia enka kwenye mechi ya Ligi Jumamosi iliyopita walipocheza na Bolton na jana hakuwemo kwenye Kikosi kilichocheza na Valencia kwenye ushindi wa 1-0 wa UEFA CHAMPIONS LIGI.
Lakini Msimu huu Rooney ameporomoka kiwango kufuatia uchezaji mbovu huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia na hivi karibuni amejikuta akinangwa na Magazeti kuwa alitembea na changudoa wakati mkewe yuko mja mzito.
Steve Bruce, ambae anamjua fika Ferguson tangu alipokuwa Mchezaji wake huko Manchester United, amehoji: “Ni kweli Rooney yuko nje wiki 3? Sijui hilo lakini sishangai akicheza kwani siku zote hutajua kama Sir Alex anatumia mbinu zake!”
Bruce amekiri huu ni wakati mgumu kwa Rooney lakini amebainisha kuwa Staa huyo yupo kwenye himaya nzuri chini ya Ferguson ambae huwaangalia vizuri Wachezaji wake.
Sunderland wataingia mechi ya Jumamosi dhidi ya Manchester United huku tayari wameshawafunga Manchester City na kutoka sare na Arsenal na Liverpool.
Rio yu tayari!
Beki mahiri wa Manchester United Rio Ferdinand amesema yuko fiti kucheza mechi zote baada ya kupona goti aliloumia huko Afrika Kusini mwezi Juni wakati England ilipokuwa kambini kwa ajili ya Kombe la Dunia lakini uamuzi wa mechi zipi atacheza upo kwa Meneja wake Sir Alex Ferguson.
Tangu apone Rio amekuwa akicheza mechi moja kwa wiki na alianza kucheza mechi na Rangers ya UEFA CHAMPIONS LIGI lakini aliachwa mechi ya Ligi na Liverpool kisha akacheza mechi na Scunthorpe ya Carling Cup lakini hakucheza na Bolton na jana alicheza dhidi ya Valencia kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.
Kuhusu hali hiyo, Rio amesema: “Nahitaji kucheza lakini hilo ni juu ya Meneja wangu na yeye ana uzoefu mkubwa kupita mtu yeyote duniani.”
Wenger: ‘Fabregas fifte fifte kucheza na Chelsea’
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa kuna hatihati kama Cesc Fabregas atakuwa fiti kucheza na Chelsea huko Stamford Bridge Jumapili kwenye BIGI MECHI ya Ligi Kuu.
Fabregas aliumia musuli ya mguu wiki mbili zilizopita Arsenal walipotoka sare na Sunderland.
Wenger amesema watajua Jumamosi asubuhi kama Nahodha wao atacheza au la.
Wiki iliyopita Arsenal walichapwa 3-2 na West Brom Uwanja wa Emirates kwenye Ligi Kuu lakini Jumanne walipata ushindi wa 3-1 ugenini walipoichapa Partizan Belgrade kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.

No comments:

Powered By Blogger