Saturday, 2 October 2010

Adebayor aililia Juve
Straika wa Manchester City Emmanuel Adebayor ambae namba zimekuwa adimu Msimu huu amedokeza yu tayari kwenda Juventus Mwezi Januari dirisha la uhamisho likifunguliwa.
Kwenye Ligi Kuu Msimu huu Adebayor amecheza mechi 3 tu na hilo limemfanya aangalie maslahi kwingineko ingawa Meneja wa Man City Roberto Mancini amesema Mchezaji huyo bado ana nafasi hapo.
Adebayor alihamia Man City kwa Pauni Milioni 25 mwaka jana akitokea Arsenal.
Spurs na West Ham wautaka Uwanja wa Olimpiki London
Klabu za London, Tottenham na West Ham, zimewasilisha maombi yao ya kuuchukua Uwanja wa Olimpiki 2012 wa London wenye uwezo wa kuchukua Watazamaji 80,000.
Siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya kuumiliki Uwanja huo ilikuwa Jumanne na uamuzi wa nani apewe utatolewa ifikapo Machi Mwakani.
Hivi karibuni Tottenham walipewa kibali cha kuupanua na kuuendeleza Uwanja wao White Hart Lane na Manispaa ya eneo lao hatua ambayo ilisifiwa na Mbunge wa eneo hilo, David Lammy, ambae pia ameuponda uongozi wa Tottenham kwa kuutaka Uwanja wa Olimpiki.
Mbunge huyo alisema: “Kuendeleza White Hart Lane ni hatua bora lakini kuhamia Uwanja ulio mbali na hapa ni makosa makubwa. Klabu za Soka zinatakiwa zibaki kwenye jamii yake eneo lile lile. Mashabiki hawataisamehe Spurs ikihama!”

No comments:

Powered By Blogger