UEFA CHAMPIONS LIGI: Jana Chelsea, Arsenal zapeta, Leo ni Man United na Tottenham
Baada ya Chelsea na Arsenal kushinda mechi zao za UEFA CHAMPIONS LIGI hapo jana wakati Chelsea walipoifunga Marseille kwa bao 2-0 na Arsenal kushinda 3-1 dhidi ya Partizan Belgrade, leo ni zamu za wenzao Manchester United ambao wako ugenini Spain kucheza na Valencia na Tottenham watakaokuwa nyumbani White Hart Lane kucheza na FC Twente.
Chelsea walishinda 2-0 dhidi ya Marseille wakiwa kwao Stamford Bridge kwa mabao ya kipindi cha kwanza ya John Terry na Nicolas Anelka aliefunga kwa penati.
Nao Arsenal wakicheza huko Serbia na Partizan Belgrade walishinda 3-1 kwa mabao ya Arshavin, Marouane Chamakh na Sebastien Squillaci.
Bao la Partizan lilifungwa na Cleverson Gabriel Cordova ambae pia baadae alikosa kufunga penati.
Nae Arshavin aliikosesha bao Arsenal baada ya pia kukosa penati.
Nako huko Estadio Mestalla, vinara wa La Liga Valencia watawakaribisha Manchester United ambao watawakosa Mastaa wao Wayne Rooney, Ryan Giggs na Paul Scholes ambao ni majeruhi.
Lakini majeruhi walioopona, Rio Ferdinand na Michael Carrick, huenda wakaingia dimbani.
Nao, Tottenham, baada ya kwenda sare ugenini ya 2-2 na Werder Bremen kwenye mechi ya kwanza ya Kundi lao, leo wapo nyumbani kucheza na FC Twente ya Uholanzi ambao pia walitoka sare ya 2-2 kwenye mechi ya kwanza na Mabingwa Watetezi Inter Milan.
MECHI ZA LEO NI:
Jumatano, 29 Septemba 2010
[Saa 3 dak 45 usiku bongo taimu]
Rubin Kazan v Barcelona [Saa 1 na nusu usiku]
Hapoel Tel-Aviv v Lyon
Inter Milan v Werder Bremen
Panathinaikos v FC Copenhagen
Rangers v Bursaspor
Schalke 04 v Benfica
Tottenham v FC Twente
Valencia v Man Utd
No comments:
Post a Comment