Friday 1 October 2010

LIGI KUU England: Mechi za Wikiendi hii
Jumamosi, 2 Octoba 2010
[Saa za Bongo]
[Saa 8 dak 45 mchana]
Wigan v Wolverhampton
[Saa 11 jioni]
Birmingham v Everton
Stoke v Blackburn
Sunderland v Man United
Tottenham v Aston Villa
West Brom v Bolton
West Ham v Fulham
Jumapili, 3 Octoba 2010
[Saa 9 na nusu mchana]
Man City v Newcastle
[Saa 11 jioni]
Liverpool v Blackpool
[Saa 12 jioni]
Chelsea v Arsenal
TATHMINI:
Chelsea v Arsenal
Ni mechi kubwa na yenye mvuto mkubwa na ipo Jumapili huko Stamford Bridge ambako Chelsea watawakaribisha wenzao wa London Arsenal huku timu zote mbili zikiwa zimetoka kwenye vipigo vyao vya kwanza vya Ligi katika mechi zao za mwisho wikiendi iliyopita.
Arsenal walifungwa nyumbani 3-2 na West Bromwich Albion.
Chelsea walipigwa 1-0 na Manchester City.
Arsenal wamekuwa wakipata wakati mgumu kila wanapocheza na Chelsea katika miaka ya hivi karibuni huku Didier Drogba akiwa ndie mwiba mkubwa kwao akiwa amewafunga goli 10 katika mechi 12 kati yao.
Katika mechi 17 za mwisho kati ya Chelsea na Arsenal, Arsenal wameshinda mara mbili tu.
Sunderland v Manchester United
Baada ya ushindi mtamu ugenini huko Uwanja wa Mestall walipoifunga Valencia bao 1-0 kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI, Man United wanasafiri tena kwenda kucheza na Sunderland.
Msimu huu Man United wametoka sare 3 katika mechi zao zote za ugenini huku wakiruhusu lundo ya magoli lakini kupona kwa Rio Ferdinand, ambae alicheza na Valencia akishirikiana na patna wake wa siku zote Nemanja Vidic, kutaleta ahueni kwa Mashabiki wa Mashetani hao Wekundu.
Tottenham v Aston Villa
Aston Villa, chini ya Meneja mpya Gerard Houllier, watakuwa White Hart Lane kuivaa Tottenham ambayo wiki iliyopita ilipigwa na West Ham.
Villa walishinda 2-1 dhidi ya Wolves wiki iliyopita.
Wigan v Wolves
Uwanjani DW, Wigan wanaikaribisha Wolves na timu hizi zimetenganishwa kwa pointi moja tu kati yao.
West Ham v Fulham
West Ham, baada ya kuifunga Tottenham, watataka kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Fulham ambayo bado haijafungwa kwenye Ligi Msimu huu kwa kutoka sare mechi 5 kati ya 6 walizocheza.
Birmingham v Everton
Everton wapo mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu na wana pointi 3 na mechi hii dhidi ya Birmingham Uwanjani kwao kwa Mtakatifu Andrew ni ngumu mno kwani Birmingham hawafungiki hapo na hawajafungwa katika mechi 18 za Ligi uwanjani hapo.
West Brom v Bolton
West Brom watakuwa nyumbani Uwanjani Hawthorns na bado wana moto wa kuiadhibu Arsenal bao 3-2 huko Emirates wikiendi iliyokwisha.
Nao Bolton wana furaha ya kutoka sare 2-2 na Manchester United.
Hivyo pambano hili litakuwa la vuta ni kuvute.
Stoke City v Blackburn Rovers
Hili pambano lipo Uwanja wa Britannia na linazikutanisha Timu zinazocheza staili ya aina moja tu ya ile ‘vita mbele’ na hivyo moto utawaka uwanjani.
Katika mechi zao 3 za mwisho za Ligi Stoke wamevuna pointi 7 kati ya 9 na Blackburn hawajafungwa katika mechi zao 3 za mwisho.
Manchester City v Newcastle
Ndio kwanza wametoika kuiua Chelsea, hivyo Man City bado wana moto na wanapambana na Newcastle ambayo hivi karibuni imeonyesha kuteleza kwani baada ya kushinda mechi mbili wakafungwa mechi 3 zilizofuata.
Liverpool v Blackpool
Ushindi kwa Liverpool ni kitu muhimu mno kwani Msimu huu kwenye Ligi wameonyesha ugoigoi mkubwa.
Blackpool nao hawapo katika hali nzuri na katika mechi ya wikiendi iliyopita walifungwa nyumbani na Blackburn

No comments:

Powered By Blogger