Saturday 18 September 2010

PITIA PITIA TOVUTI ITAKAYOTOKA UPYAAAA HIVI KARIBUNIIII: www.sokainbongo.com

BIGI MECHI: Man United v Liverpool
Jumapili, Septemba 19,
Uwanja: Old Trafford,
Saa: 9.30 mchana Bongo Taimu
TATHMINI:
Vikosi vinatarajiwa:
Manchester United (Fomesheni 4-4-1-1): Van der Sar; Neville, Vidic, Evans, Evra; Nani, Scholes, Fletcher, Park; Berbatov; Rooney
Liverpool (4-2-3-1): Reina; Johnson, Skrtel, Carragher, Konchesky; Poulsen, Meireles; Maxi, Gerrard, Jovanovic; Torres.
Refa: Howard Webb.
Historia:
Katika Mechi 18 za Ligi Kuu za Watani hawa wa Jadi Uwanjani Old Trafford, Manchester United wameshinda 10 na kupoteza 4 huku wakifunga bao 27 na kufungwa 15.
Rekodi hii ni pamoja na ushindi wa Mechi 5 katika 6 za mwisho kati yao Uwanjani Old Trafford.
Katika historia yao kwa Mechi zote 77 za Ligi zilizochezwa Old Trafford, Manchestet United wameshinda Mechi 37 na Liverpool wameshinda 15 tu huku Man United wakishindilia jumla ya mabao 127 na kufungwa 70 katika mechi zote hizo.
Meneja wa Liverpool, Roy Hodgson, awali akiwa Fulham, ashakutana na Sir Alex Ferguson wa Manchester United kwenye Mechi za Ligi Kuu mara 9 na ameweza kushinda mbili tu.
Msimu huu, Liverpool imeshinda Mechi moja tu ya Ligi Kuu, kutoka sare 2 na kufungwa 1 wakati Man United wameshinda 2 na sare 2.
Ingawa Man United walibadilisha Kikosi chao Wachezaji 10 kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI waliyotoka droo 0-0 na Rangers Jumanne iliyopita, kesho wanategemewa kuwarudisha Wachezaji wengi waliocheza kwenye sare ya 3-3 na Everton Jumamosi iliyopita akiwemo Wayne Rooney ambae hakucheza mechi hiyo ingawa alicheza na Rangers.
Lakini, Man United itawakosa Antonio Valencia, Owen Hargreaves na Michael Carrick ambao ni majeruhi.
Liverpool itawakosa Fabio Aurelio na Dirk Kuyt.
Nini wanasema:
Sir Alex Ferguson: “Pengine naonekana kama kasuku lakini hii ni BIGI MECHI! Hamna kipingamizi kuhusu hilo! Hilo halibadiliki!”
Roy Hodgson: “Ni gemu ngumu lakini ni gemu inayovutia Dunia nzima Miaka yote hii na tuombe isiwe tofauti Wikiendi hii!”
Matokeo Msimu uliokwisha:
-Liverpool 2 Man United 0
-Man United 2 Liverpool 1
Takwimu ya Mechi:
Liverpool wameshinda mara moja katika mechi zao 11 za ugenini zilizokwisha na kufunga bao 8 tu katika Mechi 14 za mwisho.
Sunderland 1 Arsenal 1
Darren Bent alifunga dakika ya 94 na kuifanya Timu yake Sunderland watoke droo 1-1 na Arsenal ambao walicheza takriban dakika 30 za mwisho wakiwa Mtu 10 baada ya Alex Song kupewa Kadi ya Njano ya pili na hivyo kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Arsenal walipata bao lao kibahati tu kwenye dakika ya 12 wakati Difenda wa Sunderland Antony Ferdinand, akiwa Mita kama 30 nje ya goli lake, alipopiga mpira mbele na kumgonga Cesc Fabregas mguuni wakati akija kwa kasi kumkaba na mpira huo ukapaa juu na kumpita Kipa Mignolet aliekuwa ametoka golini.
Ukweli ni kuwa hilo goli litaingia kwenye kumbukumbu kama moja ya magoli ya ajabu na bahati kubwa.
Arsenal wangeweza kujihakikishia ushindi kwenye mechi hii lakini walikosa kufunga penalti waliyopewa kwenye dakika ya 73 baada ya Beki Mmisri wa Sunderland Ahmed Almohamady kumchezea rafu Samir Nasri na penalti iliyopigwa na Tomas Rosicky kuota mbawa.
Vikosi vilivyoanza:
Sunderland: Mignolet, Onuoha, Bramble, Ferdinand, Richardson, Elmohamady, Riveros, Meyler, Malbranque, Welbeck, Bent.
Akiba: Carson, Bardsley, Zenden, Da Silva, Reid, Colback, Gyan.
Arsenal: Almunia, Clichy, Squillaci, Koscielny, Sagna, Song, Wilshere, Nasri, Fabregas, Arshavin, Chamakh.
Akiba: Fabianski, Rosicky, Vela, Denilson, Djourou, Eboue, Gibbs.
Refa: Phil Dowd
Spurs, WBA zazinduka Kipindi cha Pili na kushinda bao 3!
• Newcastle yairamba Everton ugenini!
Katika mechi za Ligi Kuu leo, Timu za Tottenham Hotspur na West Bromwich Albion, zikicheza nyumbani kila mmoja, zilijikuta ziko nyuma kwa bao 1-0 hadi mapumziko lakini zikazinduka Kipindi cha Pili na kushinda 3-1 kila mmoja wakati Spurs walipoikung’uta Wolves na WBA kuitwanga Birmingham.
Wolves walipata bao lao Kipindi cha kwanza mfungaji akiwa Steven Fletcher. Bao hilo lilidumu hadi dakika ya 77 wakati Rafael van der Vaart aliposawazisha kwa penalti na dakika 3 kabla mpira kwisha Roman Pavlyuchenko alifunga la pili na kwenye dakika za majeruhi Beki Allan Hutton akapachika la 3.
West Bromwich walikuwa nyuma kwa bao moja hadi haftaimu lakini mabao ya Kipindi cha pili yaliyofungwa na Dann [alijifunga mwenyewe] dakika ya 51, Peter Odemwingie, dakika ya 59 na Olsson dakika ya 69 yaliwapa ushindi wa 3-1 dhidi ya Birmingham.
Nao Newcastle, wakiwa ugenini Goodison Park, walipewa ushindi na Mchezaji mpya kutoka Ufaransa, Hatem Ben Arfa baada ya shuti lake la Mita 25 la dakika ya 45 kwenda juu pembeni na kumpita Kipa wa Everton Tim Howard.
Huko Villa Park, Aston Villa walishindwa kumuaga kwa raha Meneja wa muda Kevin MacDonald anaeachia ngazi Jumatatu kumpisha Meneja mpya Gerrard Houllier anaeshika wadhifa, baada ya kuongoza kwa bao la frikiki ya Ashley Young, dakika ya 13, na kushindwa kulilinda na ndipo Bolton wakasawazisha kupitia Kevin Davies kwenye dakika ya 35.
Nako huko Ewood Park, Wenyeji Blackburn Rovers walitoka sare na Fulham ya 1-1 na kuwafanya Fulham wawe hawajafungwa katika mechi 5 zao za Ligi Kuu Msimu huu.
Blackburn walifunga mwanzo kwa kichwa cha Chris Samba kwenye dakika ya 36 na Fulham, ambao wako chini ya Meneja wa zamani wa Blackburn Mark Hughes, kusawazisha kwa kichwa cha Clint Dempsey kwenye dakika ya 56.
Stoke City 1 West Ham 1
Katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England leo, West Ham, wakicheza ugenini, wamepata pointi yao ya kwanza kwa Msimu huu baada ya kwenda sare 1-1 na Stoke City.
Scott Parker ndie alieifungia West Ham bao kwenye dakika ya 32 na bao hilo lilidumu hadi mapumziko.
Dakika 3 tu baada ya Kipindi cha Pili kuanza, Kenwyne Jones aliisawazishia Stoke City.
Matokeo hayo yameichimbia West Ham mkiani wakiwa na pointi moja katika mechi 5 wakati Stoke wapo nafasi ya 16 na wana pointi 4 kwa mechi 5.
BIGI MECHI: Man United v Liverpool
• Hodgson ahofia urafiki wake na Fergie!
Meneja wa Liverpool Roy Hodgson amekiri urafiki wake na Sir Alex Ferguson kesho utakuwa majaribuni wakati Manchester United itakapowakaribisha Watani zao wa Jadi Liverpool Uwanjani Old Trafford kwenye mechi ya Ligi Kuu.
Hodgson amekuwa na urafiki wa muda mrefu na Ferguson lakini Meneja huyo wa Man United hakuwa na uhusiano mzuri na Meneja wa Liverpool aliepita, Rafael Benitez, ambae mara kadhaa alisimama mbele ya Wanahabari kumshambulia Ferguson.
Hodgson ametamka: “Ni rafiki yangu wa dhati. Lakini sijui yeye kama ananchukulia mimi kama rafiki wa dhati, hilo mwulizeni mwenyewe. Tunaongea vizuri tu na kutaniani.”
Hodgson akaongeza: “Siku moja nilimuuliza: ‘Sasa nimeingia Liverpool ina maana hatuongei tena?’ Hakukata simu ila hilo jibu alonipa!”
Hata hivyo, Hodgson, Miaka 62, amedai kuwa urafiki wao haujaathirika kwa yeye kutua Liverpool na ana uhakika atapewa glasi ya mvinyo wakikutana hiyo kesho huko Old Trafford.
Hodgson alimalizia kwa kusema: “Hamna urafiki wakati wa mechi. Lakini Washabiki hawaji uwanjani kuniangalia mimi au Fergie. Wao wanakuja kuwatazama Wachezaji 22. Lakini, Sir Alex ni Meneja bora katika historia ya Uingereza!”
Bifu la Pulis na Wenger laendelea!
Meneja wa Stoke City, Tony Pulis, amepeleka malamiko yake kwa Wasimamizi wa Ligi Kuu kumripoti Meneja wa Arsenal Arsene Wenger kwa kumshambulia Difenda wao Ryan Shawcross na kumwita ‘Mcheza Raga’.
Imeripotiwa kuwa Stoike City waliiandikia Arsenal barua mara mbili wakitaka kuombwa radhi lakini hawakupewa jibu lolote na sasa wameamua kupeleka malamiko kwa Ligi Kuu baada ya FA kutamka haitamchukulia hatua yeyote.
Mapema Mwaka huu, Ryan Shawcross alimvunja mguu Chipukizi wa Arsenal Aaron Ramsey na tangu wakati huo Wenger amekuwa akimwandama Mchezaji huyo kwa vijembe.

Friday 17 September 2010

LIGI KUU England: BIGI MECHI Jumapili!!
Kufuatia michuano ya UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI kuanza kuchezwa hatua ya Makundi katikati ya Wiki hii, Jumanne, Jumatano na jana Alhamisi, macho ya Wadau sasa yanarejea kwenye Ligi Kuu na pambano litakalokodolewa macho sana ni lile la Jumapili la BIGI MECHI huko Old Trafford ambako Manchester United watawakaribisha Watani zao wa Jadi, Liverpool.
Vigogo wengine wa Ligi Kuu, Mabingwa Chelsea, pia wanacheza Jumapili nyumbani Stamford Bridge kuwakaribisha Blackpool na Arsenal wanacheza Jumamosi ugenini na Sunderland.
RATIBA MECHI ZA WIKIENDI:
Jumamosi, 18 Septemba 2010
[Saa 8 dak 45 mchana]
Stoke v West Ham
[Saa 11 jioni]
Aston Villa v Bolton
Blackburn v Fulham
Everton v Newcastle
Tottenham v Wolverhampton
West Brom v Birmingham
[Saa 1 na nusu usiku]
Sunderland v Arsenal
Jumapili, 19 Septemba 2010
[Saa 9 na nusu mchana]
Man Utd v Liverpool
[Saa 11 jioni]
Wigan v Man City
[Saa 12 jioni]
Chelsea v Blackpool
EUROPA LIGI: Liverpool & Man City zapeta, Juve droo!
Hapo jana, kwenye mechi za kwanza za Makundi yao, Manchester City, ikicheza ugenini huko Austria, iliichapa Red Bull Salzburg 2-0 na Liverpool ikiwa nyumbani Anfield iliichapa Steau Bucharest 4-1.
Juventus, Vigogo wa Italia, walishikwa koo na na Timu ‘ndogo’ kutoka Poland Lech Poznan kwa bao 3-3.
‘Timu Tajiri’ Man City ilifunga mabao yake kupitia David Silva, likiwa bao lake la kwanza kwa Klabu hiyo tangu ahamie kutoka Valencia na la pili lilifungwa na Mbrazil Jo.
Nae Joe Cole, aliifungia Liverpool bao la kwanza, na hilo likiwa bao lake la kwanza tangu ajiunge nayo, tena liliweka historia kwa kufungwa haraka mno pale lilipotinga sekunde 25 tu tangu mpira uanze.
Cristian Tanase wa Steau Bucharest alisawazisha lakini Liverpool, waliocheza bila Nyota Steven Gerrard na Fernando Torres, wakaongeza bao 3 zaidi zikifungwa na David Ngog , bao mbili, na Lucas.

Thursday 16 September 2010

Allardyce amshukia Wenger!
• Adai anachota akili za Marefa waisaidie Arsenal
Sam Allardyce amemjia juu Arsene Wenger na kudai Meneja huyo wa Arsenal ni mwerevu na anatumia Vyombo vya Habari ili kuwarubuni Marefa na kuwafanya Wachezaji wake wasiguswe kwenye mechi.
Jumamosi, kwenye mechi ya Ligi Kuu, Abou Diaby wa Arsenal aliumia baada ya kugongana na Kipa wa Bolton, Adam Bogdan, na Wenger alidai kuwa Kipa huyo alikusudia na angepewa Kadi Nyekundu.
Wenger alitoa madai hayo kwenye program ya Arsenal ya kabla ya mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya Braga ya Ureno ambayo Washabiki huinunua kabla ya mechi.
Lakini Meneja wa zamani wa Bolton ambae sasa yupo Blackburn Rovers, Sam Allardyce maarufu kama Big Sam, ametamka: “Wenger ni Mtu mjanja! Anataka kuwarubuni na kuwachota akili Marefa ili Wachezaji wake wasiguswe kwenye mechi!
Wiki za nyuma Big Sam aliwahi kumpa vipande vyake Wenger pale alipotamka: “Hebu nimkumbushe Wenger. Timu yake ilikuwa ikuchukua Ubingwa na ndio ilikuwa Timu chafu kwa rafu kupita zote! Walikuwa Mabingwa huku wakiongoza kwa Kadi Nyekundu na Njano kupita Timu yeyote! Patrick Viera, Emmanuel Petit, Sol Campbell na Martin Keown walitumia kila mbinu chafu kushinda!”
Big Sam amesema hivi leo: “Wenger anatumia Vyombo vya Habari ili Marefa waisaidie. Ameleta dhana kuwa kila Timu inakusudia kuwaumiza Wachezaji wa Arsenal. Na nadhani Marefa wamechotwa akili na hilo na tunaona matokeo yake kwenye mechi!”
Allardyce aliongeza kwa kusema zile zama za Wachezaji kuingia Uwanjani ili kuwaumiza wenzao makusudi zimepitwa na wakati.
Arsenal, Chelsea zachakaza Ulaya!!
Klabu za Arsenal na Chelsea zimeanza kampeni zao za UEFA CHAMPIONS LIGI kwa kupata ushindi mnono kwenye mechi zao za kwanza za Makundi yao kwa Arsenal kuibamiza Braga ya Ureno 6-0 Uwanjani Emirates na Chelsea kushinda ugenini kwa bao 4-1 dhidi ya MSK Zilina.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Cesc Fagregas na Carlos Vela, bao mbili mbili, Andre Arshavin na Marouane Chamakh.
Wafungaji wa Chelsea walikuwa Nicolas Anelka, mabao mawili, Michael Essien na Daniel Sturridge.
UEFA CHAMPIONS LIGI:
MATOKEO:
Jumatano, Septemba 15
KUNDI E
FC Bayern Munchen 2 AS Roma O
CFR 1907 Clu 2 FC Basel 1
KUNDI F
Olympique de Marseille 0 FC Spartak Moskva 1
MSK Zilina 1 Chelsea FC 4
KUNDI G
Real Madrid CF 2 AFC Ajax 0
AC Milan 2 AJ Auxerre 0
KUNDI H
Arsenal FC 6 SC Braga 0
FC Shakhtar Donetsk 1 FK Partizan 0

Wednesday 15 September 2010

Valencia kuukosa Msimu wote!
Winga wa Manchester United Antonio Valencia kutoka Ecuador atakuwa nje kwa Msimu mzima baada ya kuumia enka jana katika mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI kati ya Man United na Rangers. Ilitegemewa leo atafanyiwa upasuaji wa enka baada ya kuthibitika enka hiyo imevunjika.
Man United ilitoka sare 0-0 na Rangers Uwanjani Old Trafford.
UEFA CHAMPIONS LIGI:
RATIBA MECHI ZA LEO:
Jumatano, Septemba 15
KUNDI E
FC Bayern Munchen v AS Roma
CFR 1907 Clu v FC Basel 1893
KUNDI F
Olympique de Marseille v FC Spartak Moskva
MSK Zilina v Chelsea FC
KUNDI G
Real Madrid CF v AFC Ajax
AC Milan v AJ Auxerre
KUNDI H
Arsenal FC v SC Braga
FC Shakhtar Donetsk v FK Partizan
MATOKEO MECHI ZA JANA:
Jumanne, Septemba 14
KUNDI A
FC Twente FC 2 Inter Milan 2
SV Werder Bremen 2 Tottenham Hotspur FC 2
KUNDI B
Olympique Lyonnais 1 FC Schalke 0
SL Benfica 2 Hapoel Tel-Aviv FC 0
KUNDI C
Manchester United FC 0 Rangers FC 0
Bursaspor 0 Valencia CF 4
KUNDI D
FC Barcelona 5 Panathinaikos FC 1
FC Kobenhavn 1 FC Rubin Kazan 0

Tuesday 14 September 2010

Fergie: ‘Sijutii kumtema Rooney!’
• Pia, atafuta Nahodha mpya!
Licha ya kuiona na kukasirishwa na Manchester United kuutupa uongozi wa mabao 3-1 hadi dakika za majeruhi na kuruhusu Everton kusawazisha na kuifanya mechi ya Ligi Kuu Jumamosi kumalizika 3-3, Sir Alex Ferguson ameng’ang’ania kuwa uamuzi wake wa kumwacha Wayne Rooney ulikuwa ni sahihi.
Rooney hakucheza mechi ya Ligi Kuu ya Jumamosi dhidi ya Everton na Meneja wa Man United Sir Alex Ferguson alisema Mchezaji huyo aliachwa ili kumwepusha kuandamwa na Mashabiki wa Timu yake ya zamani Everton Uwanjani Goodison Park. Rooney amelipuliwa na baadhi ya Magazeti na kuhusishwa kutembea na changudoa wakati mkewe akiwa mja mzito.
Ferguson ametamka: “Sijutii. Sielezei zaidi. Sikutaka kuruhusu upuuzi wa kumshambulia na kumkebehi huko Goodison Park. Sina tatizo na yeye kucheza na Rangers.”
Ferguson alisistiza Rooney ni Mchezaji bora na hamna haja kwa ya kuelezea chochote kuhusu hilo.
Lakini Ferguson alitoa fununu kuwa yuko mbioni kumtafuta Nahodha wa kudumu wa Timu yake kwa vile Gary Neville amekuwa hachezi mfululizo kutokana na kuumia mara kwa mara.
Ikiwa Neville atacheza mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI na Rangers leo Jumanne Septemba 14 hiyo itakuwa mechi yake ya 600 kwa Man United lakini Ferguson amethibitisha hatavaa utepe wa Unahodha.
Jumamosi kwenye mechi na Everton licha ya Neville kucheza, Nahodha alikuwa Nemanja Vidic.
Ferguson ameelezea: "Gary bado ni Nahodha lakini natafuta mtu anaecheza kila wiki. Katika Miaka miwili mitatu iliyopita Gary amekuwa akiandamwa na majeruhi mfululizo. Mwenyewe Gary anajua kuwa kwa sasa hawezi kuchezeshwa kila mechi.”
Alipoulizwa ikiwa Ferdinand atapewa tena Unahodha endapo atacheza mechi na Rangers, Ferguson alijibu: “Sina la kusema. Wala sijafikiria hilo!”
UEFA CHAMPIONS LIGI:
TATHMINI: Mechi za Leo za Timu za England
Werder Bremen v Tottenham
Katika Uwanja wa Weserstadion huko Ujerumani, Werder Bremen wanaikaribisha Tottenham ya England katika mechi ya KUNDI A ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Mechi nyingine ya KUNDI A ambayo pia inachezwa leo ni kati ya FC Twente na Mabingwa Watetezi Inter Milan.
Tottenham wanakabiliwa na majeruhi na watawakosa Jermaine Defoe na Michael Dawson ambao wote waliumia wakiichezea England wiki iliyopita.
Lakini, Tottenham watakuwa nae Luka Modric ambae ilidhaniwa hatacheza baada ya kuumia na kutolewa kwenye mechi ya Ligi Kuu Jumamosi Tottenham walipotoka sare 1-1 na West Bromwich.
Werder Bremen nao wanakabiliwa kuwakosa Wachezaji muhimu ambao wana maumivu na Wachezaji hao ni Mertesacker, Naldo na Claudio Pizarro. Hivyo, huenda Werder Bremen wakalazimika kumchezesha Veterani wa zamani wa Manchester United na Arsenal, Mikael Silvestre.
Katika mechi ya Bundesliga hapo majuzi Jumamosi, Werder ya kuungaunga ilitoka sare 0-0 na Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tottenham kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI na huenda wakamchezesha Mchezaji wao mpya Rafael van der Vaart waliemnunua kutoka Real Madrid.
Manchester United v Rangers
Ni mechi yenye ushindani wa jadi kwani siku zote mechi za England na Scotland huamsha hisia hizo na hali leo haitakuwa tofauti wakati Manchester United watakapoikaribisha Rangers ya Scotland Uwanjani Old Trafford katika mechi ya kwanza ya KUNDI C ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Mechi nyingine ya Kundi hili ni kati ya Bursapor ya Uturuki na Valencia ya Spain.
Manchester United leo inategemewa kuwachezesha Nyota wake Wayne Rooney na Rio Ferdinand.
Rooney hakucheza mechi ya Ligi Kuu ya Jumamosi dhidi ya Everton na Meneja wa Man United Sir Alex Ferguson alisema Mchezaji huyo aliachwa ili kumwepusha kuandamwa na Mashabiki wa Timu yake ya zamani Everton Uwanjani Goodison Park.
Rooney amelipuliwa na baadhi ya Magazeti na kuhusishwa kutembea na changudoa wakati mkewe akiwa mja mzito.
Ferdinand alikuwa nje ya uwanja tangu Mwezi Juni alipoumia goti mazoezini akiwa na England huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Rangers wanategemea Difenda wao Steven Whittaker atacheza baada ya kupona musuli lakini huenda wakamkosa Kirk Broadfoot alieumia enka.
Kiungo wa Man United, Michael Carrick, atakuwa nje ya mechi hii akiendelea kuuguza enka.
Mara ya mwisho kwa Man United na Rangers kucheza kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI ilikuwa Mwaka 2003 na Man United ilishinda mechi zote mbili za Makundi kwa bao 1-0 huko Ibrox, nyumbani kwa Rangers, na 3-0 Uwanjani Old Trafford.
Msimu uliokwisha, Rangers ilishindwa kushinda mechi zao zote 6 za Makundi za UEFA CHAMPIONS LIGI.
Msimu uliokwisha, Man United walitolewa kwenye Robo Fainali ya michuano hii na Bayern Munich.
Meneja mwenye msiba aipa ushindi Stoke!
Hakuwepo Uwanjani Britannia kipindi cha kwanza akiwa kwenye msiba wa Mama yake mzazi na Timu yake Stoke City ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 walipokuwa wakicheza na Aston Villa kwenye mechi ya Ligi Kuu hapo jana, lakini Tony Pulis alifika Chumba cha Kubadili Jezi wakati wa mapumziko na kuihutubia Timu yake na kuifanya ipande morali na kushinda 2-1 kwenye mechi hiyo.
Meneja Msaidizi wa Stoke, Dave Kemp, amenena: “Alikuja wakati wa mapumziko na kuwaamsha Wachezaji!”
Hata Meneja wa Muda wa Aston Villa, Kevin MacDonald, amemsifia Pulis na kumwita ‘Mtu mwema’.
UEFA CHAMPIONS LIGI:
RATIBA MECHI ZA LEO:
Jumanne, Septemba 14
KUNDI A
FC Twente v FC Internazionale Milano
SV Werder Bremen v Tottenham Hotspur FC
KUNDI B
Olympique Lyonnais v FC Schalke 04
SL Benfica v Hapoel Tel-Aviv FC
KUNDI C
Manchester United FC v Rangers FC
Bursaspor v Valencia CF
KUNDI D
FC Barcelona v Panathinaikos FC
FC Kobenhavn v FC Rubin Kazan
LIGI KUU ENGLAND: Stoke yatoka nyuma kuibwaga Villa
Jana, Stoke City wakiwa nyumbani, walikuwa nyuma kwa bao 1-0 hadi mapumziko lakini walifufuka kipindi cha pili na kuipiga Aston Villa mabao 2-1.
Villa walipata bao lao dakika ya 35 Downing akifunga kwa kichwa cha kudaivu kufuatia krosi ya Gabriel Agbonlahor.
Kwenye dakika ya 80, Kenwyne Jones alisawazisha kwa kichwa na hilo ni bao lake la kwanza kwa Stoke tangu ahamie kutoka Sunderland.
Kwenye dakika za majeruhi, dakika ya pili ya muda huo, piga ni kupiga golini kwa Villa, ilitua kwa Difenda Robert Huth aliemalizia wavuni na kuipa Stoke ushindi wake wa kwanza tangu Ligi ianze Msimu huu.

Monday 13 September 2010

FA yamfungulia mashitaka Moyes
David Moyes huenda akalikwaa rungu la FA kwa kuvamia uwanja na kumvaa Refa Martin Atkinson kwa maneno mara baada ya mechi kati ya Everton na Manchester United kwisha akidai Refa huyo alipaswa
kuongeza muda katika mechi ambayo Timu yake Everton ilipata bao mbili kwenye dakika za majeruhi na kutoka sare 3-3 hapo Jumamosi katika mechi ya hiyo Ligi Kuu.
FA imeamua kumfungulia mashitaka Meneja huyo pamoja na Msaidizi wake Steve Round.
Mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa na Refa Martin Atkinson, Moyes alivamia uwanja na kwenda kumpa maneno yake Refa huyo kwa kile alichodai Refa hakuongeza muda ilivyopaswa.
Moyes anadai wakati Everton wanafunga mabao yao mawili dakika za majeruhi huku tayari bango lilikwisha onyesha dakika 3 za nyongeza, Refa huyo alipaswa kuongeza muda zaidi kufidia muda uliopotezwa baada ya magoli kufungwa na mpira kuanza tena.
Rooney kilingeni tena!
Straika Wayne Rooney ameendelea na mazoezi na Timu yake Manchester United hivi leo licha ya Magazeti huko Uingereza kuchapisha kila ya aina ya stori huku mengine yakidai Meneja wake amemwadhibu na ndio maana aliachwa kwenye Kikosi kilichocheza na Everton kwenye mechi ya Ligi Kuu hapo Jumamosi.
Rooney amekuwa akikabiliwa na skandali baada ya kulipuliwa kwenye baadhi ya Magazeti akidaiwa kutembea na Changudoa wakati Mkewe akiwa na mimba.
Lakini, leo Rooney alionekana mazoezini na Timu yake akiwa na wenzake huku akiwa mwenye furaha kubwa na Sir Alex Ferguson amethibitisha Rooney atacheza kesho katika mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Old Trafford dhidi ya Rangers.
Torres apondwa, Hodgson amtetea!
Kiungo wa zamani wa Liverpool, Jamie Redknapp, ambae sasa ni mtoa tathmini kwenye Kituo cha TV cha SKY wakati wa mechi za Ligi Kuu, amemponda Fowadi wa Liverpool, Fernando Torres, kwa kuwa chini ya kiwango na pia kutoonyesha ari yoyote katika mechi ya jana ya Ligi Kuu ambayo Liverpool ilitoka sare 0-0 na Birmingham Uwanjani Mtakatifu Andrew.
Torres amekuwa na wakati mgumu baada ya kuandamwa na maumivu ya nyonga na goti yaliyomfanya aukose Msimu uliopita kwa muda mrefu na pia kutong’ara kwenye Kombe la Dunia akiwa na Nchi yake Spain huko Afrika Kusini.
Jamie Redknapp amesema: “Kwa dakika 45, alikuwa ovyo. Alishindwa kumiliki mpira, alishindwa kufukuza mpira, akakata tamaa na angweza kupewa Kadi ya Njano kwa kucheza rafu.”
Lakini Meneja wa Liverpool, Roy Hodgson, amepinga na kutamka: “Sikubaliani na maoni ya Redknapp. Torres atarejea kiwango chake.”
Hodgson pia ameonyeshwa kushangazwa na baadhi ya wadau kutangaza Ubingwa kwa baadhi ya Timu huku Ligi ikiwa imechezwa mechi 4 tu.
Hadi sasa Liverpool wamecheza mechi 4 na wana pointi 5 wakiwa pointi 7 nyuma ya vinara Chelsea.
UEFA CHAMPIONS LIGI: Tathmini ya Timu za England kwenye Makundi yao.

MAKUNDI:
KUNDI A: Inter Milan, Werder Bremen, TOTTENHAM, FC Twente.
KUNDI B: Lyon, Benfica, Schalke, Hapoel Tel-Aviv.
KUNDI C: MANCHESTER UNITED,Valencia, Rangers, Bursaspor.
KUNDI D: Barcelona, Panathinaikos, FC Copenhagen, Rubin Kazan.
KUNDI E: Bayern Munich, Roma, FC Basle, Cluj.
KUNDI F: CHELSEA, Marseille, Spartak Moscow, MSK Zilina.
KUNDI G: AC Milan, Real Madrid, Ajax, Auxerre.
KUNDI H: ARSENAL, Shakhtar Donetsk, FC Braga, FK Partizan
TATHMINI: 
Msimu wa 2010/11 wa UEFA CHAMPIONS LIGI unaanza rasmi kesho Jumanne Septemba 14 na ifuatayo ni tathmini ya Makundi ambazo zimo Timu za England Chelsea, Tottenham, Manchester United na Arsenal.
KUNDI A:
Inter Milan: Hawa ni Mabingwa Watetezi wa Kombe hili na Kikosi chao kilichotwaa Ubingwa Msimu uliokwisha bado kiko vilevile ila Msimu huu wako chini ya Meneja mpya Rafael Benitez.
Katika Kundi hili Inter Milan wanategemewa kuchukua nafasi ya kwanza.
Werder Bremen: Wamempoteza Staa wao mkubwa, Mesut Ozil, ambae amehamia Real Madrid na Timu hii ndio itakuwa ikapigania nafasi ya pili ya Kundi hili na Tottenham.
Tottenham: Ni lazima wapata pointi wakienda kucheza huko Ujerumani ili wapate nafasi ya kufuzu kuingia Raundi inayofuata.
FC Twente: Ipo chini ya Kocha Steve McClaren aliewahi kuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson huko Manchester United na pia kuwa Kocha wa England.
RATIBA:
Septemba 14
Twente v Inter Milan
Werder Bremen v TOTTENHAM
Septemba 29
TOTTENHAM v Twente
Inter Milan v Werder Bremen
Oktoba 20
Inter Milan v TOTTENHAM
Twente v Werder Bremen
Novemba 2
TOTTENHAM v Inter Milan
Werder Bremen v Twente
Novemba 24
Inter Milan v Twente
TOTTENHAM v Werder Bremen
Desemba 7
Twente v TOTTENHAM
Werder Bremen v Inter Milan
KUNDI C:
Manchester United: Kwa Manchester United na Meneja wake Sir Alex Ferguson kutwaa uongozi wa Kundi hili ni kitu kinachotegemewa na wadau wengi.
Valencia: Timu hii ya Spain inategemewa kuchukua nafasi ya pili ya Kundi hili.
Rangers: Wadau hawawapi nafasi yeyote Timu hii kutoka Scotland.
Bursaspor: Hii ni Timu toka Uturuki na haipewi matumaini yeyote katika KUNDI C.
RATIBA:
Septemba 14
MAN UNITED v Rangers
Bursaspor v Valencia
Septemba 29
Valencia v MAN UNITED
Rangers v Bursaspor
Oktoba 20
Rangers v Valencia
MAN UNITED v Bursaspor
Novemba 2
Valencia v Rangers
Bursaspor v MAN UNITED
Novemba 24
Rangers v MAN UNITED
Valencia v Bursaspor
Desemba 7
MAN UNITED v Valencia
Bursaspor v Rangers
KUNDI F
Chelsea: Wababe hawa wa Stamford Bridge wanategemewa watafuzu kwa kuchukua nafasi ya kwanza ya KUNDI F.
Marseilles: Chini ya Gwiji la zamani la Timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, Marseille inatumainiwa kuchukua nafasi ya pili.
Spartak Moscow: Ni wagumu mno wakiwa nyumbani lakini hawategemiwa kufua dafu kwenye Kundi hili.
Zilina: Ingawa Slovakia ilifanya vizuri kidogo huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia lakini Zilina haiwezi kuambulia kitu kwenye michuano hii.
RATIBA:
Septemba 15
Marseilles v Spartak Moscow
Zilina v CHELSEA
Septemba 28
CHELSEA v Marseilles
Spartak Moscow v Zilina
Oktoba 19
Spartak Moscow v CHELSEA
Marseilles v Zilina
Novemba 3
CHELSEA v Spartak Moscow
Zilina v Marseilles
Novemba 23
Spartak Moscow v Marseilles
CHELSEA v Zilina
Desemba 8
Marseilles v CHELSEA
Zilina v Spartak Moscow
KUNDI H
Arsenal: Arsène Wenger na Arsenal yake watatwaa uongozi wa Kundi hili.
Shakhtar Donetsk: Ni timu hatari lakini haina uimara wa kushinda mechi mfululizo. Watatwaa nafasi ya pili nyuma ya Arsenal.
Braga: Timu nzuri lakini si ngumu hivyo wao na Partisan Belgrade watagombea nafasi za chini za Kundi hili.
Partisan Belgrade: Si tishio wakicheza Ulaya lakini ni wagumu nyumbani.
RATIBA:
Septemba 15
ARSENAL v Braga
Shakhtar Donetsk v Partisan
Septemba 28
Partisan v ARSENAL
Braga v Shakhtar Donetsk
Oktoba 19
Braga v Partisan
ARSENAL v Shakhtar Donetsk
Novemba 3
Partisan v Braga
Shakhtar Donetsk v ARSENAL
Novemba 23
Braga v ARSENAL
Partizan v Shakhtar Donetsk
Desemba 8
ARSENAL v Partisan
Shakhtar Donetsk v Braga
Zamora avunjika mguu
Straika wa Fulham Bobby Zamora amefanyiwa operesheni ya dharura baada ya kuvunjika mguu katika mechi ya Ligi Kuu Jumamosi ambayo Fulham waliifunga Wolves 2-1.
Zamora, Miaka 29, alichaguliwa kuichezea England Mwezi Agosti kwa mara ya kwanza na Ijumaa iliyopita alisani Mkataba mpya wa Miaka minne na Klabu yake Fulham.
Inategemewa Straika huyo atakuwa nje ya uwanja hadi Januari mwakani.
Wenger ang’ang’ania kushambulia tu!
Arsene Wenger, baada ya kuiona Arsenal yake, ikifikisha magoli 1000 ya Ligi Kuu chini ya himaya yake walipoifunga Bolton Wanderers 4-1 Jumamosi kwenye mechi ya Ligi Kuu, ameshikilia msimamo wake wa kushambulia tu.
Wenger ametamka: “Watu wanakuja hapa kuona tukishambulia na kufunga magoli. Hilo ni muhimu. Tutaendelea na falsafa hiyo kwani tunao Wachezaji wenye vipaji vya kushambulia.”
Hata hivyo, Wenger amekiri Msimu huu ni mgumu mno kwani upinzani kwao utatoka Klabu za Manchester City, Manchester United, Tottenham na Chelsea.

Sunday 12 September 2010

Birmingham 0 Liverpool 0
Liverpool inabidi wamshukuru Kipa Pepe Reina kwa kufuta mabao ya wazi kadhaa wa kadha na kuwafanya waibuke na sare ya 0-0 ugenini na Birmingham.
Hii ni mechi ya 17 ya Ligi Kuu kwa Birmingham kutoipoteza kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Mtakatifu Andrew.
Inaelekea leo Reina alikuwa na kazi moja tu ya kuwafanya Washabiki wasahau makosa yake ya mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu alipowapa Arsenal bao la zawadi kwenye dakika za majeruhi na kuifanya mechi iwe 1-1.
Pia Reina hivi majuzi alifanya kosa la kibwege alipoidakia Nchi yake Spain na kupigwa 4-1 na Argentina.
Jumapili ijayo Septemba 19 Liverpool watatembelea Old Trafford kucheza na watani wao wa jadi Manchester United kwenye mechi ya Ligi Kuu.
Moyes achukizwa na Refa Atkinson, Fergie akasirishwa na kutupa pointi!
Wakati Kocha wa Everton, David Moyes, akimponda Refa Martin Atkinson, Sir Alex Ferguson wa Manchester United amekasirishwa na Timu yake kuumwaga ‘ushindi’ wa 3-1 walipokuwa wakiongoza hadi kwenye dakika za majeruhi na kuwaruhusu Everton kusawazisha na mechi kwisha 3-3.
Mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa na Refa Martin Atkinson, Moyes alivamia uwanja na kwenda kumpa maneno yake Refa huyo kwa kile alichodai Refa hakuongeza muda ilivyopaswa.
Moyes anadai wakati Everton wanafunga mabao yao mawili dakika za majeruhi huku tayari bango lilikwisha onyesha dakika 3 za nyongeza, Refa huyo alipaswa kuongeza muda zaidi kufidia muda uliopotezwa baada ya magoli kufungwa na mpira kuanza tena.
Sir Alex Ferguson nae alikasirishwa na Wachezaji wake kukosa mabao kadhaa na alisema: “Tumetupa pointi hizi! Naomba mwishoni mwa Msimu tusije tukazijutia hizi pointi. Tulikuwa na nafasi kadhaa za kuongeza mabao na hatukuzitumia.”
LIGI KUU England
MATOKEO:
Jumamosi, 11 Septemba 2010
Everton 3 Man United 3
Arsenal 4 Bolton 1
Fulham 2 Wolverhampton 1
Man City 1 Blackburn 1
Newcastle 0 Blackpool 2
West Brom 1 Tottenham 1
West Ham 1 Chelsea 3
Wigan v Sunderland
RATIBA:
Jumapili, 12 Septemba 2010
[Saa 12 jioni]
Birmingham v Liverpool
Jumatatu, 13 Septemba 2010
[Saa 4 usiku]
Stoke v Aston Villa
RATIBA LIGI ZA ULAYA: MATOKEO/RATIBA
BUNDESLIGA:
Ijumaa,10 Septemba
1899 Hoffenheim 2 Schalke 0
Jumamosi,11 Septemba
Freiburg 2 Stuttgart 1
Borussia Moenchengladbach 0 Eintracht Frankfurt 4
Hamburg 1 Nurnberg 1
Borussia Dortmund 2 Wolfsburg 0
Hannover 2 Bayer Leverkusen 2
Bayern Munich 0 Werder Bremen 0
Jumapili, 12 Septemba
Mainz 05 v Kaiserslautern
Cologne v St Pauli
LA LIGA:
Jumamosi,11 Septemba
Valencia 1 Racing Santander 0
Barcelona 0 Hercules 2
Real Madrid 1 Osasuna 0
Athletic Bilbao 1 Atlético Madrid 2
Jumapili, 12 Septemba
Sporting Gijon v Mallorca
Getafe v Levante
Zaragoza v Malaga
Villarreal v Espanyol
Sevilla v Deportivo
Jumatatu, 13 Septemba
Almeria v Real Sociedad
SERIE A:
Jumamosi, 11 Septemba
Inter Milan 2 Udinese 1
Cesena 2 AC Milan 0
Cagliari 5 Roma 1
Jumapili, 12 Septemba
Brescia v Palermo
Lecce v Fiorentina
Catania v Parma
Lazio v Bologna
Juventus v Sampdoria
Genoa v Chievo
Napoli v Bari
Powered By Blogger