Tuesday 14 September 2010

UEFA CHAMPIONS LIGI:
TATHMINI: Mechi za Leo za Timu za England
Werder Bremen v Tottenham
Katika Uwanja wa Weserstadion huko Ujerumani, Werder Bremen wanaikaribisha Tottenham ya England katika mechi ya KUNDI A ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Mechi nyingine ya KUNDI A ambayo pia inachezwa leo ni kati ya FC Twente na Mabingwa Watetezi Inter Milan.
Tottenham wanakabiliwa na majeruhi na watawakosa Jermaine Defoe na Michael Dawson ambao wote waliumia wakiichezea England wiki iliyopita.
Lakini, Tottenham watakuwa nae Luka Modric ambae ilidhaniwa hatacheza baada ya kuumia na kutolewa kwenye mechi ya Ligi Kuu Jumamosi Tottenham walipotoka sare 1-1 na West Bromwich.
Werder Bremen nao wanakabiliwa kuwakosa Wachezaji muhimu ambao wana maumivu na Wachezaji hao ni Mertesacker, Naldo na Claudio Pizarro. Hivyo, huenda Werder Bremen wakalazimika kumchezesha Veterani wa zamani wa Manchester United na Arsenal, Mikael Silvestre.
Katika mechi ya Bundesliga hapo majuzi Jumamosi, Werder ya kuungaunga ilitoka sare 0-0 na Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tottenham kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI na huenda wakamchezesha Mchezaji wao mpya Rafael van der Vaart waliemnunua kutoka Real Madrid.
Manchester United v Rangers
Ni mechi yenye ushindani wa jadi kwani siku zote mechi za England na Scotland huamsha hisia hizo na hali leo haitakuwa tofauti wakati Manchester United watakapoikaribisha Rangers ya Scotland Uwanjani Old Trafford katika mechi ya kwanza ya KUNDI C ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Mechi nyingine ya Kundi hili ni kati ya Bursapor ya Uturuki na Valencia ya Spain.
Manchester United leo inategemewa kuwachezesha Nyota wake Wayne Rooney na Rio Ferdinand.
Rooney hakucheza mechi ya Ligi Kuu ya Jumamosi dhidi ya Everton na Meneja wa Man United Sir Alex Ferguson alisema Mchezaji huyo aliachwa ili kumwepusha kuandamwa na Mashabiki wa Timu yake ya zamani Everton Uwanjani Goodison Park.
Rooney amelipuliwa na baadhi ya Magazeti na kuhusishwa kutembea na changudoa wakati mkewe akiwa mja mzito.
Ferdinand alikuwa nje ya uwanja tangu Mwezi Juni alipoumia goti mazoezini akiwa na England huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Rangers wanategemea Difenda wao Steven Whittaker atacheza baada ya kupona musuli lakini huenda wakamkosa Kirk Broadfoot alieumia enka.
Kiungo wa Man United, Michael Carrick, atakuwa nje ya mechi hii akiendelea kuuguza enka.
Mara ya mwisho kwa Man United na Rangers kucheza kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI ilikuwa Mwaka 2003 na Man United ilishinda mechi zote mbili za Makundi kwa bao 1-0 huko Ibrox, nyumbani kwa Rangers, na 3-0 Uwanjani Old Trafford.
Msimu uliokwisha, Rangers ilishindwa kushinda mechi zao zote 6 za Makundi za UEFA CHAMPIONS LIGI.
Msimu uliokwisha, Man United walitolewa kwenye Robo Fainali ya michuano hii na Bayern Munich.
Meneja mwenye msiba aipa ushindi Stoke!
Hakuwepo Uwanjani Britannia kipindi cha kwanza akiwa kwenye msiba wa Mama yake mzazi na Timu yake Stoke City ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 walipokuwa wakicheza na Aston Villa kwenye mechi ya Ligi Kuu hapo jana, lakini Tony Pulis alifika Chumba cha Kubadili Jezi wakati wa mapumziko na kuihutubia Timu yake na kuifanya ipande morali na kushinda 2-1 kwenye mechi hiyo.
Meneja Msaidizi wa Stoke, Dave Kemp, amenena: “Alikuja wakati wa mapumziko na kuwaamsha Wachezaji!”
Hata Meneja wa Muda wa Aston Villa, Kevin MacDonald, amemsifia Pulis na kumwita ‘Mtu mwema’.

No comments:

Powered By Blogger