Sunday 12 September 2010

Moyes achukizwa na Refa Atkinson, Fergie akasirishwa na kutupa pointi!
Wakati Kocha wa Everton, David Moyes, akimponda Refa Martin Atkinson, Sir Alex Ferguson wa Manchester United amekasirishwa na Timu yake kuumwaga ‘ushindi’ wa 3-1 walipokuwa wakiongoza hadi kwenye dakika za majeruhi na kuwaruhusu Everton kusawazisha na mechi kwisha 3-3.
Mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa na Refa Martin Atkinson, Moyes alivamia uwanja na kwenda kumpa maneno yake Refa huyo kwa kile alichodai Refa hakuongeza muda ilivyopaswa.
Moyes anadai wakati Everton wanafunga mabao yao mawili dakika za majeruhi huku tayari bango lilikwisha onyesha dakika 3 za nyongeza, Refa huyo alipaswa kuongeza muda zaidi kufidia muda uliopotezwa baada ya magoli kufungwa na mpira kuanza tena.
Sir Alex Ferguson nae alikasirishwa na Wachezaji wake kukosa mabao kadhaa na alisema: “Tumetupa pointi hizi! Naomba mwishoni mwa Msimu tusije tukazijutia hizi pointi. Tulikuwa na nafasi kadhaa za kuongeza mabao na hatukuzitumia.”

No comments:

Powered By Blogger