Saturday 28 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Man United 3 West Ham 0
Wakiwa nyumbani Old Trafford, Manchester United wameifunga West Ham mabao 3-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu.
Hiki ni kipigo cha tatu mfululizo kwa West Ham na wamefungwa Mechi zote za Ligi Kuu tangu Msimu huu uanze.
Man United walipata bao la kwanza dakika ya 34 baada ya Giggs kuchanja mbuga ndani ya boksi na kuangushwa na Jonathan Spector, Mchezaji wa zamani wa Man United, na Refa Clattenburg akatoa penalti iliyofungwa na Rooney ambalo hilo ni goli lake la kwanza tangu Mwezi Machi.
Licha ya kutawala, hadi mapumziko Man United walikuwa mbele 1-0.
Kipindi cha Pili muvu nzuri kati ya Scholes na Rooney ilitua kwa Nani aliehadaa Mabeki ndani ya boksi na kufunga bao dakika ya 49.
Berbatov aliunganisha krosi ya Nani na kupachika bao la 3 dakika ya 69.
Vikosi vilivyoanza:
Man United: Van der Sar, O'Shea, Vidic, Jonathan Evans, Evra, Nani, Scholes, Fletcher, Giggs, Rooney, Berbatov.
Akiba: Kuszczak, Owen, Smalling, Hernandez, Carrick, Rafael Da Silva, Valencia.
West Ham: Green, Spector, Gabbidon, Upson, Ilunga, Faubert, Noble, Parker, Boa Morte, Dyer, Cole.
Akiba: Stech, Barrera, Kovac, McCarthy, da Costa, Stanislas, Piquionne.
Refa: Mark Clattenburg
CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI KUU: Chelsea yashinda tena, Spurs yatunguliwa kwao!
MATOKEO: Mechi za leo Jumamosi Agosti 28
Blackburn 1 v Arsenal 2
Blackpool 2 v Fulham 2
Chelsea 2 v Stoke 0
Tottenham 0 v Wigan 1
Wolverhampton 1 v Newcastle 1
Baada ya kuchapwa jumla ya mabao 10 katika mechi mbili za kwanza za Ligi Kuu walizocheza kwao Uwanja wa DW, leo Wigan walisafiri hadi Jijini London kucheza na Tottenham katika Uwanja wa White Hart Lane ambao Msimu uliokwisha Wigan walikung’utwa mabao 9-1 lakini leo Straika Hugo Rodallega alliwapa furaha kubwa kwa kufunga bao moja na la ushindi kwenye dakika ya 80.
Mabingwa Chelsea leo wameshinda ila wameshindwa kutoa dozi ya mabao 6 kama walivyofanya katika mechi zao mbili za kwanza na badala yake wameshinda 2-0 kwa mabao ya Malouda na Drogba, aliefunga kwa penalty.
Awali, Lampard alikosa penalti baada ya Kipa Sorensen kuicheza.
Mechi nyingine mbili zilimalizika kwa sare ambapo Wolves na Newcastle iliisha 1-1 na Blackpool v Fulham 2-2.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Blackburn 1 Arsenal 2
Andrey Arshavin ameipa ushindi Arsenal huko ugenini Ewood Park kwa kufunga bao la pili dakika ya 51 dhidi ya Timu ngumu na ya wapiganaji Blackburn Rovers katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa leo.
Arsenal ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao dakika ya 20 baada ya muvu tamu iliyomkuta Theo Walcott aliemalizia vizuri.
Blackburn Rovers walijibu mapigo dakika 7 baadae kwa muvu iliyoanza kwa Samba kumpasia El-Hadji Diouf aliempenyezea Mame Biram Diouf, Mchezaji wa Manchester United aliekopeshwa kwa Rovers, ambae alimalizia wavuni.
Vikosi vilivyoanza:
Blackburn: Robinson, Salgado, Nelsen, Samba, Givet, El-Hadji Diouf, Jones, Pedersen, Grella, Mame Diouf, Kalinic
Akiba: Bunn, Olsson, Emerton, Dunn, Nzonzi, Hoilett, Chimbonda.
Arsenal: Almunia, Sagna, Koscielny, Vermaelen, Clichy, Diaby, Song, Fabregas, Walcott, van Persie, Arshavin
Akiba: Fabianski, Rosicky, Vela, Wilshere, Eboue, Gibbs, Chamakh
Refa: Chris Foy
TEMBELEA: www.sokainbongo.com

CARLING CUP: RAUNDI YA TATU yaanikwa
• Timu vigogo kuanza kucheza!
Timu Vigogo zimepangiwa wapinzani kwenye Raundi ya 3 ya Kombe la Carling na Bingwa Mtetezi Manchester United atacheza ugenini na Timu ya Daraja la chini Scunthorpe United.
Katika mechi za Timu za Ligi Kuu pekee, Chelsea atakuwa nyumbani kucheza na Newcastle United, Stoke City atacheza na Fulham, mechi nyingine za Timu za Ligi Kuu ni Aston Villa v Blackburn, Sunderland v West Ham, West Brom v Manchester City na zile Timu pinzani za London Kaskazini, Tottenham na Arsenal, zitakutana White Hart Lane.
Mechi zote za Raundi hii zitachezwa Wiki ya kuanzia Septemba 20.
RATIBA KAMILI:
Brentford v Everton
Portsmouth v Leicester City
Stoke City v Fulham
Chelsea v Newcastle United
Aston Villa v Blackburn Rovers
Tottenham Hotspur v Arsenal
Millwall v Ipswich Town
Wolverhampton Wanderers v Notts County
Burnley v Bolton Wanderers
Birmingham City v MK Dons
Liverpool v Northampton Town
Scunthorpe United v Manchester United
West Bromwich Albion v Manchester City
Sunderland v West Ham United
Peterborough United v Swansea City
Wigan Athletic v Preston North End
CHEKI: www.sokainbongo.com

UEFA CHAMPIONS LIGI: Mechi za Mwanzo za Makundi
Baada ya kufanyika Droo ya kupanga Makundi, UEFA imetoa Ratiba ya Mechi za Makundi na mechi za kwanza zitachezwa Septemba 14 na 15.
Mechi za Pili zitachezwa Septemba 28 na 29.
RATIBA MECHI ZA KWANZA:
Jumanne, Septemba 14
KUNDI A
FC Twente v FC Internazionale Milano
SV Werder Bremen v Tottenham Hotspur FC
KUNDI B
Olympique Lyonnais v FC Schalke 04
SL Benfica v Hapoel Tel-Aviv FC
KUNDI C
Manchester United FC v Rangers FC
Bursaspor v Valencia CF
KUNDI D
FC Barcelona v Panathinaikos FC
FC København v FC Rubin Kazan
Jumatano, Septemba 15
KUNDI E
FC Bayern München v AS Roma
CFR 1907 Clu v FC Basel 1893
KUNDI F
Olympique de Marseille v FC Spartak Moskva
MŠK Žilina v Chelsea FC
KUNDI G
Real Madrid CF v AFC Ajax
AC Milan v AJ Auxerre
KUNDI H
Arsenal FC v SC Braga
FC Shakhtar Donetsk v FK Partizan
CHEKI: www.sokainbongo.com

MADAI SCHOLES ‘MCHEZA RAFU’, ROVERS ‘WACHEZA RAGA’: Fergie, Big Sam wajibu mapigo kwa Wenger!
• Mourinho nae amkandya!
Kufuatia Arsene Wenger kutoa shutuma kuwa Kiungo Veterani wa Manchester United, Paul Scholes, ni ‘Mcheza Rafu’ na Timu ya Blackburn Rovers ni ‘Wacheza Raga’, Mameneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, na wa Blackburn, Sam Allardyce, Big Sam, wamejibu mapigo.
Big Sam amedai Wenger amechanganyikiwa na sasa hata hajui afanye nini ili kushinda Vikombe.
Ferguson amenena Wenger ameonyesha kutokuwa na heshima kwa kumbandika Scholes sifa ambayo hastahili.
Leo, Arsenal itatinga Ewood Park, nyumbani kwa Blackburn Rovers, Timu ya Big Sam, ambayo Msimu uliokwisha iliwaliza Arsenal kwa bao 2-1 na mechi hiyo imemfanya Wenger aombe hifadhi ya Refa ili kuwanusuru Wachezaji wake wasikumbane na ‘Soka la Raga’.
Kihistoria, Wenger na Big Sam washakutana mara 21 na ni mara 8 tu ndizo Wenger ameshinda.
Big Sam amesema: “Hatustahili kuwafunga Arsenal lakini huwa tunawafunga. Si sababu ya Raga lakini mpaka pale watakaposema kwenye Soka usimguse mwenzio, soka ya ubavu ni muhimu!”
Big Sam akaongeza: “Hebu nimkumbushe Wenger. Timu yake ilikuwa ikuchukua Ubingwa na ndio ilikuwa Timu chafu kwa rafu kupita zote! Walikuwa Mabingwa huku wakiongoza kwa Kadi Nyekundu na Njano kupita Timu yeyote! Patrick Viera, Emmanuel Petit, Sol Campbell na Martin Keown walitumia kila mbinu chafu kushinda!”
Big Sam akachambua zaidi kwa kutamka: “Wenger amebadilisha mbinu. Ametoka kwenye Timu ile ya mibavu na uchafu na sasa Timu yake inatandaza Soka na kumuvu vizuri tu lakini wakati wote tunakubali Soka hilo linafurahisha kulitazama, lakini si Timu nzuri kama ile iliyopita iliyokuwa ikishinda Mataji kwa mibavu.”
Ni Miaka mitano sasa tangu Arsenal ishinde Kikombe pale iliposhinda FA Cup kwa matuta dhidi ya Manchester United.
Ingawa Miaka ya hivi karibuni uhusiano wa Wenger na Ferguson umeonekana poa na hata alipohojiwa Wenger akatania kuwa siku hizi Ferguson anamwona si tishio na ndio maana hawagombani, kauli ya Wenger kumsifia na papo hapo kumponda Scholes ni ‘Mcheza Rafu’ iliibua hisia Ferguson atalipuka.
Hata hivyo Ferguson alijibu tuhuma hizo kistaarabu kwa kusema: “Sijui kwa nini Wenger ametamka hilo. Najua Scholes si mzuri kwa kukaba Watu na mara nyingi hukosea na kuwavaa wenzake lakini hajamuumiza Mtu. Ni rahisi sana kusema ubaya wa Mchezaji yeyote! Naweza kusema hilo kuhusu Mchezaji wake mmoja wa Arsenal lakini sina haja. Inashangaza kumponda Mchezaji ambae ametoa mchango mkubwa kwa Soka ya Uingereza kwa Miaka 18!”
Huko Madrid, Jose Mourinho ameendeleza libeneke la kumponda Arsene Wenger ingawa hakumtaja kwa jina wakati alipohojiwa.
Mourinho alitamka: “Kama huchezi vizuri, hushindi. Ni upumbavu kudai ‘Tulicheza vizuri, lakini hatukushinda!’ Hao huwa wanadai ilikuwa bahati mbaya, tulimiliki mpira asilimia 90 au tumefungwa dakika ya mwisho au kwa frikiki! Mara nyingi nawaona Makocha hao wana akili kupita mie! Mie nikifungwa, siku zote najiuliza kosa liko wapi.”
Alipoulizwa kama majibu yake yanamlenga Wenger, Mourinho alisema: “Kuna Kocha mmoja Timu zake zimekuwa zikicheza Soka safi kwa Miaka 10 na Wachezaji wake siku zote ni Vijana chipukizi. Siku zote ni Timu changa isiyokua na isiyoshinda chochote! Kwangu mie huu ni wehu na upuuzi mkubwa!”
CHEKI: www.sokainbongo.com

UEFA SUPERCUP: Atletico watwaa Kombe!
• Atletico 2 Inter Milan 0
Jana usiku huko Monaco, Mabingwa wa EUROPA LIGI, Atletico Madrid, wametwaa UEFA Supercup kwa kuwafunga Mabingwa wa UEFA CHAMPIONS LIGI, Inter Milan, mabao 2-0.
Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Jose Antonio Reyes, ndie aliefunga bao la kwanza kwenye dakika ya 62 na dakika ya 83 Sergio Aguero akapachika bao la pili.
Mchezaji Bora Ulaya, Diego Milito, alikosa penalti dakika ya 90.
Msimu uliokwisha, Inter Milan chini ya Kocha Jose Mourinho ambae sasa yuko Real Madrid, walitwaa Ubingwa wa Italia, Kombe la Italia na UEFA CHAMPIONS LIGI.
Msimu huu Inter Milan wako chini ya Kocha wa zamani wa Liverpool, Rafael Benitez, na wiki iliyopita walitwaa Italian Supercup kwa kuifunga AS Roma 3-1.
BUNDESLIGA: FC Kaiserslautern 2 Bayern Munich 0
Hapo jana, kwenye mechi ya Ligi ya Bundesliga huko Ujerumani, FC Kaiserslautern iliwafunga Mabingwa Bayern Munich kwa bao 2-0.
Mabao ya dakika ya 36 na 37 ya Ivo Ilicevic na Srdjan Lakic ndio yaliowatoa nishai Mabingwa hao.
Mechi zingine za Bundesliga zitachezwa leo na kesho.

Friday 27 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI KUU ENGLAND: Tathmini Mechi za Wikiendi hii
Jumamosi, 28 Agosti 2010
[saa za bongo]
[saa 8 dak 45 mchana]
Blackburn v Arsenal
[saa 11 jioni]
Blackpool v Fulham
Chelsea v Stoke
Tottenham v Wigan
Wolverhampton v Newcastle
[saa 1 na nusu usiku]
Man Utd v West Ham
Jumapili, 29 Agosti 2010
[saa 9 na nusu mchana]
Bolton v Birmingham
[saa 11 jioni]
Liverpool v West Brom
Sunderland v Man City
[saa 12 jioni]
Aston Villa v Everton
Timu zote 20 za Ligi Kuu zitajimwaga dimbani kucheza Mechi zao za tatu za Ligi hapo kesho na Jumapili.
Mechi ya kwanza ya Wikiendi ni ile ya Saa 8 dakika 45 mchana Jumamosi huko Ewood Park kati ya Wenyeji Blackburn Rovers na Arsenal.
Msimu uliokwisha, Blackburn ilishinda 2-1 na kumfanya Arsene Wenger alalamike mibavu ya Blackburn ambao wamefungwa mechi moja tu kati ya 11 za mwisho za Ligi Kuu kuchezewa Uwanjani kwao.
Tayari Wenger ashaanza kuigwaya mechi hii kwa kumtaka Refa aidhibiti vizuri.
Wigan, baada ya kutandikwa jumla ya mabao 10 kati mechi zao mbili za kwanza za ligi Msimu huu, wanasafiri hadi Jijini London, Uwanjani White Hart Lane, nyumbani kwa Tottenham ambao waliinyuka Wigan mabao 9-1 Msimu uliopita.
Chelsea ndio Timu pekee Msimu huu iliyoshinda mechi zake mbili ilizocheza kwa mabao 6-0 kila moja na kesho wanawakaribisha Stoke City huko Stamford Bridge ambao Msimu uliokwisha walipigwa 7-0 Uwanjani hapo.
Baada ya Meneja wao, Sir Alex Ferguson, kukiri sare ya 2-2 na Fulham huko Craven Cottage wiki iliyopita ilikuwa ni kupoteza pointi kipumbavu, kesho Manchester United wataivaa West Ham, Timu ambayo imepoteza mechi zake zote mbili za Ligi, Uwanjani Old Trafford.
Baada ya kuiwasha Aston Villa 6-0, Newcastle inaenda kucheza na Wolves ambayo, baada ya mechi mbili, imeshinda mechi moja na kutoka sare mechi moja Msimu huu.
Blackpool,Timu iliyopanda Daraja Msimu huu, ilishinda mechi ya kwanza kwa kuichapa Wigan 4-0 lakini ikapewa somo pale ilipopigwa 6-0 na Arsenal, na wikiendi hii wanacheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Uwanjani kwao dhidi ya Fulham.
Huko Reebok Stadium, Siku ya Jumapili, Bolton wanaikaribisha Birmingham City na hii ni mechi kali ukizingatia viwango vinavyofanana vya Timu hizi.
Liverpool, baada ya kupigwa 3-0 na Manchester City, watakuwa nyumbani kucheza na West Bromwich Albion.
Nao wababe wa Liverpool, Timu Tajiri, Manchester City, wanasafiri kwenda kucheza na Sunderland ambao wametoka sare mechi moja na kufungwa moja.
Mechi ya mwisho ya Wikiendi hii itakuwa huko Villa Park kati ya Aston Villa na Everton.
CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI ZA ULAYA: Kunguruma Wikiendi hii
Wakati Bundesliga ilianza wikiendi iliyopita na inaendelea leo kwa Mechi kati ya FC Kaiserslautern v Bayern Munich, Ligi za La Liga ya Spain na Serie A kule Italia, zitaanza rasmi Wikiendi hii.
Ifuatayo ni Ratiba ya Wikiendi hii kwa Ligi hizo:
BUNDESLIGA: 
Ijumaa, Agosti 27
FC Kaiserslautern v Bayern Munich
Jumamosi, Agosti 28
FC Nurnberg v SC Freiburg
Eintracht Frankfurt v Hamburger SV
VfL Wolfsburg v FSV Mainz 05
Schalke 04 v Hannoverscher 1896
SV Werder Bremen v FC Köln
FC St. Pauli v TSG Hoffenheim
Jumapili, Agosti 29
Bayer Leverkusen v Borussia Moenchengladbach
Stuttgart v Borussia Dortmund
LA LIGA
Jumamosi, 28 Agosti 2010
Hercules v Athletic Bilbao
Malaga v Valencia
Levante v Sevilla
Jumapili, 29 Agosti 2010
Atletico Madrid v Sporting Gijon
Deportivo La Coruna v Real Zaragoza
Espanyol v Getafe
Mallorca v Real Madrid
Osasuna v Almeria
Racing Santander v Barcelona
Real Sociedad v Villarreal
SERIE A
Jumamosi, 28 Agosti 2010
Roma v Cesena
Udinese v Genoa
Jumapili, 29 August 2010
AC Milan v Lecce
Bari v Juventus
Bologna v Inter Milan
Chievo v Catania
Fiorentina v Napoli
Palermo v Cagliari
Parma v Brescia
CHEKI: www.sokainbongo.com

Wenger ahofia wacheza ‘Raga’ Blackburn!
Jumamosi, Arsenal watatua Ewood Park nyumbani kwa Blackburn Rovers, walio chini ya Meneja Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, na tayari Meneja wa Arsenal ameanza kuigwaya mechi hiyo ya Ligi Kuu kwa kumtaka Refa wa mechi hiyo, Chris Foy, awe makini pengine akiikumbuka mechi ya Msimu uliokwisha walipochapwa 2-1 na Blackburn na Wenger kuulalamikia uchezaji wa nguvu wa Blackburn bila Refa kuwalinda.
Wenger amesema kuwa ni uhuru wa kila Timu kucheza staili wanayoona bora kwao ili mradi inafuata sheria za Soka na Refa anahakikisha sheria za Soka zinafuatwa.
Wenger ametamka: “Timu ikicheza mipira mirefu, ya juu na kutumia ubavu ni sahihi tu lakini wafuate Sheria za Soka na sio kucheza Raga na Refa anatizama tu!”
CHEKI: www.sokainbongo.com

EUROPA LIGI: Makundi yapangwa!
Makundi ya Mashindano ya EUROPA LIGI yamepangwa katika Droo iliyofanyika leo huko Monaco na Timu za England, Manchester City na Liverpool, zipo kwenye Makundi magumu.
Kila Kundi lina Timu 4 na Timu mbili za juu ndizo zinazosonga mbele.
Manchester City wako pamoja na Vigogo wa Italia Juventus na Liverpool wako na Timu ngumu za Steau Bucharest ya Romania, Napoli ya Italia na Utrecht ya Uholanzi.
Mechi za kwanza zitaanza Septemba 16.
MAKUNDI:
KUNDI A:
Juventus
Manchester City
Salzburg
Lech Posnan
KUNDI B:
Atletico Madrid
Bayer Leverkusen
Rosenburg
Thessaloniki
KUNDI C
Sporting
Lille
Levski Sofia
Gent
KUNDI D
Villarreal
Club Brugge
Dinamo Zagreb
PAOK
KUNDI E
Alkmaar
Dinamo Kiev
BATE Borisov
FC Sheriff
KUNDI F
CSKA Moscow
Palermo
Sparta Prague
Lausanne
KUNDI G
Zenit St Petersburg
Anderlecht
AEK Athens
Hajduk Split
KUNDI H
Stuttgart
Getafe
Odense
Young Boys
KUNDI I
PSV Eindhoven
Sampdoria
FC Metalist Kharkiv
Debreceni
KUNDI J
Sevilla
PSG
Borussia Dortmund
Karpaty Lviv
KUNDI K
Liverpool
Steaua Bucharest
Napoli
Utrecht
KUNDI L
Porto
Besiktas
CSKA Sofia
Rapid Vienna
Barca wampata Mascherano
Liverpool imemuuza Kiungo Javier Mascherano kwa Barcelona kwa dau linalosadikiwa kuwa Pauni Milioni 17 na habari hizi zimethibitishwa na taarifa katika tovuti ya Barcelona ingawa tamko hilo limesema taarifa zaidi zitatolewa baada ya Mchezaji huyo kufuzu upimaji afya yake.
Mascherano alijunga na Liverpool Mwaka 2007 akitokea West Ham lakini tangu Msimu uliokwisha alionyesha nia yake kutaka kuihama Liverpool.
CHEKI: www.sokainbongo.com

UEFA SUPERCUP: Inter Milan v Atletico Madrid
Leo huko Monaco, ndani ya Stade Louis II, Msimu mpya wa Ulaya wa 2010/11 utaanuliwa rasmi kwa pambano la kugombea UEFA SUPERCUP kati ya Mabingwa wa UEFA CHAMPIONS LIGI, Inter Milan ya Italia na Atletico Madrid ya Spain, ambao ndio Mabingwa wa EUROPA LIGI.
Mechi hii, itakayoanza Saa 3 dakika 45 usiku, saa za bongo, itakuwa chini ya usimamizi wa Refa Massimo Busacca wa Uswisi.
CHEKI: www.sokainbongo.com

EUROPA LIGI: Droo ya Makundi leo
Baada ya matokeo ya hapo jana kufuatia mechi za marudiano za Raundi ya Mchujo, jumla ya Timu 48 zimepangwa kwenye Makapu Manne kwa ajili ya Droo ya kupanga Makundi.
Kati ya Timu hizo 48, Timu 10 ni zile zilizobwagwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwenye Hatua ya Mchujo ambazo mechi zake za marudio zilichezwa juzi Jumanne na Jumatano.
Droo hiyo itafanyika leo Saa 8, saa za bongo, huko Monaco.
Timu hizo 48 zimepangwa katika Makapu manne, kufuatia Ubora wao, na zitapangwa katika Makundi 12 ya Timu 4 kila moja.
Kila Kapu litatoa Timu moja ili kukamilisha Kundi la Timu 4 na Timu za Nchi moja haziwezi kupangwa Kundi moja.
Timu za Kapu la 1, ambazo ndizo zimepewa Ubora wa juu, ni pamoja na Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo, Atletico Madrid na pia wamo Liverpool FC.
Mechi za kwanza za Makundi zitachezwa Septemba 16.
Washindi wawili wa juu wa Kila Kundi watasonga Hatu ya Mtoano ya Timu 32 na idadi hiyo itafikiwa baada ya kujumuika Timu zitakazoshika nafasi ya 3 kutoka Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
MGAWANYO WA MAKAPU:
KAPU LA 1
1 Club Atlético de Madrid (Mabingwa Watetezi)
2 Liverpool FC (England)
3 Sevilla FC (Spain)
4 FC Porto (Ureno)
5 Villarreal CF (Spain)
6 PFC CSKA Moskva (Urusi)
7 PSV Eindhoven (Uholanzi)
8 FC Zenit St. Petersburg (Urusi)
9 Juventus (Italy)
10 Sporting Clube de Portugal (Ureno)
11 VfB Stuttgart (Ujerumani)
12 AZ Alkmaar (Uholanzi)
KAPU LA 2
13 FC Steaua Bucureşti (Roumania)
14 LOSC Lille Métropole (Ufaransa)
15 FC Dynamo Kyiv (Ukraine)
16 RSC Anderlecht (Ubelgiji)
17 Bayer 04 Leverkusen (Ujerumani)
18 Paris Saint-Germain FC (Ufaransa)
19 Club Brugge KV (Ubelgiji)
20 US Città di Palermo (Italia)
21 Getafe CF (Spain)
22 Beşiktaş JK (Uturuki)
23 Manchester City FC (England)
24 UC Sampdoria (Italia)
KAPU LA 3
25 AC Sparta Praha (Czech)
26 AEK Athens FC (Ugiriki)
27 FC Metalist Kharkiv (Ukraine)
28 PFC Levski Sofia (Bulgaria)
29 Rosenborg BK (Norway)
30 FC Salzburg (Austria)
31 PFC CSKA Sofia (Bulgaria)
32 Odense BK (Denmark)
33 SSC Napoli (Italia)
34 BV Borussia Dortmund (Ujerumani)
35 NK Dinamo Zagreb (Croatia)
36 FC BATE Borisov (Belarus)
KAPU LA 4
37 Aris Thessaloniki FC (Ugiriki)
38 SK Rapid Wien (Austria)
39 PAOK FC (Ugiriki)
40 KKS Lech Poznań (Poland)
41 FC Karpaty Lviv (Ukrania)
42 BSC Young Boys (Uswisi)
43 FC Utrecht (Uholanzi)
44 KAA Gent (Ubelgiji)
45 FC Lausanne-Sport (Uswisi)
46 FC Sheriff (Moldova)
47 Debreceni VSC (Hungary)
48 HNK Hajduk Split (Croatia)
CHEKI: www.sokainbongo.com

EUROPA LIGI: Villa nje, Liverpool & Man City zapeta!
  •  Celtic yabwagwa!
Aston Villa, ikiwa kwao Villa Park, ilichapwa 3-2 na Rapid Vienna na kubwagwa nje ya EUROPA LIGI baada ya kutoka sare 1-1 mechi ya kwanza.
Wenzao wa Ligi Kuu Liverpool na Manchester City walishinda mechi zao za marudiano na kujihakikishia leo kuwemo kwenye Droo ya kupanga Makundi ya EUROPA LIGI.
Man City, wakicheza nyumbani City of Manchester Stadium, waliichapa FC Timisoara 2-0 na hivyo kuwatoa nje Timu hiyo ya Roumania kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya kushinda mechi ya kwanza ugenini kwa bao 1-0.
Mabao ya Man City yalifungwa Kipindi cha Pili na Shaun Wright-Phillips na Boyata.
Liverpool, wakicheza ugenini huko Uturuki, walijikuta wako nyuma dakika ya 3 tu, lakini walikaza mshipi na kufunga bao mbili kupitia Kacar, aliejifunga mwenyewe, dakika ya 84 na Kuyt dakika ya 88.
Nayo, Timu kongwe ya Scotland, Celtic, imebwagwa nje ya EUROPA LIGI na FC Utrecht ya Uholanzi baada ya kuchapwa 4-0 kwenye mechi ya marudiano.
Celtic ilishinda mechi ya kwanza 2-0.

Thursday 26 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

WACHEZAJI BORA WA MWAKA UEFA watajwa: Wachezaji wa Mabingwa Inter Milan wakwapua zawadi zote 5!!!
• Diego Milito MCHEZAJI BORA ULAYA!!!
Sambamba na kupangwa kwa Droo ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI, pia kulikuwa na kinyang’anyiro cha Tuzo za Wachezaji Bora wa Ulaya kwa Msimu wa 2009/10 na Wachezaji wa Mabingwa wa Ulaya Inter Milan ndio walionyakuwa Tuzo zote 5.
Diego Milito ndio aliibuka Mchezaji Bora wa Mwaka pamoja na kutwaa pia Tuzo ya Straika Bora wa Mwaka.
Diego Milito, atokae Argentina, ndie alifunga bao zote mbili zilizoiua FC Barcelona kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI na kuipa Inter Milan Ubingwa.
MCHEZAJI BORA: Diego Milito (Inter Milan)
KIPA BORA: Julio Cesar (Inter Milan)
DIFENDA BORA: Maicon (Inter Milan)
KIUNGO BORA: Wesley Sneijder (Inter Milan)
FOWADI BORA: Diego Milito [Inter Milan]
CHEKI: www.sokainbongo.com

UEFA CHAMPIONS LIGI: Droo ya Makundi tayari!!!!
Leo huko Monaco, imefanyika Droo ya kupanga Makundi ya kugombea UEFA CHAMPIONS LIGI na mechi za Makundi hayo zitaanza kuchezwa Septemba 14 na 15.
Mgawanyo ni kama ufuatavyo:
KUNDI A:
-Inter Milan
-Werder Bremen
-Tottenham
-FC Twente
KUNDI B:
-Lyon
-Benfica
-Schalke
-Hapoel Tel Aviv
KUNDI C:
-Manchester United
-Valencia
-Rangers
-Bursaspor
KUNDI D:
-FC Barcelona
-Panathinaikos
-FC Copenhagen
-Rubin Kazan
KUNDI E:
-Bayern Munich
-AS Roma
-FC Basel
-CFR Cluj
KUNDI F:
-Chelsea
-Marseille
-Spartak Moscow
-MSK Zilina
KUNDI G:
-AC Milan
-Real Madrid
-Ajax
-Auxerre
KUNDI H:
-Arsenal
-Shakhtar Donetsk
-SC Braga
-Partizan Belgrade
CHEKI: www.sokainbongo.com

Klabu Ulaya zasubiri Droo ya UEFA CHAMPIONS LIGI
Leo Saa 1 usiku Droo ya kupanga Makundi ya Mashindano ya UEFA CHAMPIONS LIGI itafanyika na Klabu za England, Chelsea, Manchester United, Arsenal na Tottenham, zinasubiri kwa hamu kujua Wapinzani wao.
Timu zote zimepangwa katika Makapu manne tofauti na Timu zilizomo kwenye Kapu moja haziwezi kukutana na pia Timu zinazotoka Nchi moja haziwezi kukutana.
Timu za Nchi moja zinaweza kukutana kwenye Mashindano haya yakifika Hatua ya Robo Fainali na kuendelea.
Droo inafanyika huko Monaco kwa kupanga Makundi manane ya Timu 4 kila moja.
Kila Kundi litakuwa na Timu moja toka Kapu la 1, la 2, la 3 na la 4 ila Timu za Nchi moja haziwezi kupangwa Kundi moja.
Mechi za Makundi zitaanza Septemba 14 na 15.
Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI itachezwa Uwanja wa Wembley tarehe 28 Mei 2011.
Timu na Makapu yao:
Kapu la 1: Inter Milan, Barcelona, Manchester United, Chelsea, Arsenal, Bayern Munich, AC Milan, Lyon.
Kapu la 2: Werder Bremen, Real Madrid, Roma, Shakhtar Donetsk, Benfica, Valencia, Marseille, Panathinaikos.
Kapu la 3: Tottenham, Rangers, Ajax, Schalke, Basle, Braga, FC Copenhagen, Spartak Moscow.
Kapu la 4: Hapoel Tel Aviv, FC Twente, Rubin Kazan, Auxerre, CFR Cluj, Partizan Belgrade, MSK Zilina, Bursaspor.
France yatangaza Kikosi chao kwa EURO 2012
• Wamo 9 wa Kombe la Dunia!
Ufaransa imewarudisha kundini Wachezaji 9 waliokuwa huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia na ambao waliadhibiwa kwa kutochukuliwa kwenye mechi ya kirafiki na Norway mwanzoni mwa Mwezi kwa kushiriki mgomo huko Afrika Kusini baada ya kufukuzwa mwenzao Nicolas Anelka.
Miongoni mwa Kikosi hicho yupo Straika wa Everton, Louis Saha, ambae hajachezea Ufaransa tangu 2006 ingawa aliwahi kuitwa Mwezi Februari lakini alijitoa baada ya kuumia.
France itacheza mechi za kuwania kuingia Fainali za EURO 2012 hapo Septemba 3 Mjini Paris dhidi ya Belarus na huko Sarajevo Septemba 7 dhidi ya Bosnia.
Katika Kikosi cha wachezaji 21 kilichotangazwa na Kocha Laurent Blanc wapo Wachezaji wanne walioitwa kwa mara ya kwanza.
Wachezaji hao ni Straika wa Lorient Kevin Gameiro, Kipa Cédric Carrasso , Walinzi Mamadou Sakho na Benoît Trémoulinas.
Wachezaji wazoefu waliotemwa ni Éric Abidal, Anthony Réveillère, William Gallas, Marc Planus, Djibril Cissé, Sidney Govou, André-Pierre Gignac, Thierry Henry, na Sébastien Squillaci.
Kikosi kamili:
Makipa: Cédric Carrasso (Girondins Bordeaux), Hugo Lloris (Olympique Lyon), Steve Mandanda (Olympique Marseille).
Mabeki: Gaël Clichy (Arsenal), Philippe Mexes (AS Roma), Adil Rami (Lille), Mamadou Sakho (Paris St Germain), Bacary Sagna (Arsenal), Benoît Trémoulinas (Girondins Bordeaux).
Viungo: Abou Diaby (Arsenal), Alou Diarra (Girondins Bordeaux), Lassana Diarra (Real Madrid), Yann M'Vila (Stade Rennes), Florent Malouda (Chelsea), Jeremy Menez (AS Roma), Mathieu Valbuena (Olympique Marseille).
Mafowadi: Karim Benzema (Real Madrid), Kevin Gameiro (Lorient), Guillaume Hoarau (Paris St Germain), Loic Remy (Olympique Marseille), Louis Saha (Everton).
CHEKI: www.sokainbongo.com

UEFA CHAMPIONS LIGI: Droo ya Makundi leo!!!
Washindi 10 wa Hatua ya Mchujo wameshapatikana kwa matokeo ya Mechi za jana Jumatano na juzi Jumanne na wataungana na Timu 22 Vigogo ambao wameingizwa moja kwa moja katika Hatua ya Makundi ili kupangwa Makundi manane ya Timu nne nne kila Kundi katika Droo itakayofanyika leo jioni.
Mechi za Makundi zitachezwa kuanzia Septemba hadi Desemba na washindi wawili wa kila Kundi watasonga Hatua ya Kwanza ya Mtoano.
Timu zitakazoshika nafasi ya tatu katika Makundi zitatupwa kwenye EUROPA LIGI Hatua ya Mtoano ya Timu 32.
TIMU 32 ZA KWENYE DROO:
ZILIZOINGIA MOJA KWA MOJA:
-Arsenal
-Barcelona
-Bayern Munich
-Benfica
-Bursaspor
-CFR Cluj
-Chelsea
-Inter Milan
-Lyon
-Man United
-Marseille
-AC Milan
-Panathinaikos
-Rangers
-Real Madrid
-AS Roma
-Rubin Kazan
-Schalke
-Shakhtar Donetsk
-Spartak Moscow
-FC Twente
-Valencia
TIMU 10 TOKA MCHUJO:
-Partizan Belgrade
-Basle
-Hapoel Tel-Aviv
-Werder Bremen
-Braga
-Tottenham
-Ajax Amsterdam
-Auxerre
-FC Copenhagen
-MSK Zilina

Wednesday 25 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Tottenham wawabonda Young Boys 4-0
Kwa mara ya kwanza tangu 1961, Tottenham wamefuzu kuingia Mashindano makubwa ya Ulaya walipowabonda Young Boys ya Uswisi kwa mabao 4-0 Uwanjani White Hart Lane kwenye mechi ya marudiano Hatua ya Mchujo kuingia kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Kwenye mechi ya kwanza huko Uswisi, Tottenham walichapwa kwa bao 3-2 hivyo wamefuzu kwa jumla ya mabao 6-3.
Mabao ya Tottenham yalifungwa na defoe, dakika ya 5 na Peter Crouch mabao matatu, dakika ya 32, 61 na 77 kwa penalti.
Droo ya kugawa Makundi itafanyika Alhamisi Agosti 26.
MATOKEO KAMILI:
UEFA CHAMPIONS LIGI: Hatua ya Mchujo kuingia Makundi-Mechi za Marudiano
Jumatano, 25 Agosti 2010
Ajax 2 v Dynamo Kiev 1, (Mechi ya kwanza 3-2)
Auxerre 2 v Zenit St Petersburg 0, (2-1)
FC Copenhagen 1 v Rosenborg 0, (2-2, FC Copenhagen yapeta goli la ugenini)
MSK Zilina 1 v Sparta Prague 0, (3-0)
Tottenham 4 v Young Boys 0, (6-3)
PITIA: www.sokainbongo.com

Gerrard na Torres kuikosa Ulaya kesho!
Liverpool wamesafiri hadi Uturuki kwa ajili ya Mechi ya Marudiano ya EUROPA LIGI na Trabzonspor bila ya Mastaa wao wakubwa Nahodha Steven Gerrard na Fernando Torres.
Liverpool walishinda mechi ya kwanza nyumbani Anfield kwa bao 1-0.
Gerrard inasemekana anaumwa mgongo na Torres amepumzishwa na Meneja Roy Hodgson ili kumnusuru kucheza Mechi tatu mfululizo hasa ukizingatia matatizo yake ya kuumia mara kwa mara yaliyokuwa yakimkumba.
Nae Javier Mascherano pia hayumo kwenye msafara huku habari za kuhamia kwake FC Barcelona zikipeperushwa angani.
CHEKI: www.sokainbongo.com

‘Mtu Spesheli’ anena: ‘England itashindwa chini ya Capello!’
• Mourinho aifutia mafanikio chini ya Mtaliana huyo!
Jose Mourinho amedai England haiwezi kufanikiwa ikiwa chini ya Kocha kutoka Italia Fabio Capello kwa vile hana uhusiano mzuri na Wachezaji wake.
Huko England, Magazeti mengi, hasa yale ya Mitaani, yameanza wimbi la kumponda Capello huku moja likimwita Capello ‘punda’.
Mourinho, ambae jana aliwakandya Rafael Benitez, Arsene Wenger na Liverpool, ametamka: “Tatizo ni Capello, Capello hawezi kuifanikisha England!”
Capello aliwahi kuwa Kocha wa Real Madrid ambayo ndiyo Klabu ya sasa ya Mourinho na ‘Mtu Spesheli’ amesema: “Muulize yeyote hapa Real na watakwambia Capello hawezi kubadilika! Huwezi kuwapigia kelele Wachezaji wako! Wachezaji hao wanataka waonekane ni Watu spesheli!”
Mourinho akaongeza: “Ni wazi Capello hataisaidia England. Hawajui Wachezaji na Wachezaji wanamwogopa. Ni vurugu tu! Wachezaji wanahitaji mbinu za wazi na si kuchanganywa. Ni tatizo la Meneja. Ni aibu hii!”
Minong’ono: Man United kumnasa Defour kabla Dirisha kufungwa!
Kuna taarifa nzito zimeibuka kuwa Manchester United huenda wakamchota Kiungo anaesifika kutoka Standard Liege ya Ubelgiji, Steven Defour, ambae amekuwa kwenye rada za Klabu hiyo kwa muda mrefu kabla Dirisha la uhamisho halijafungwa hapo Agosti 31.
Bosi wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, aliwahi kumtumia barua Mchezaji huyo hapo Mwaka jana kumpa pole na kumtakia apone haraka baada ya kuumia vibaya mguu wake.
Wakati Klabu kadhaa za Ulaya zikimkodolea macho kuna dalili Man United itamnyakua Defour, ambae ni Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji, ili kuziba pengo la Owen Hargreaves ambae kurudi kwake Uwanjani ni kitendawili baada ya magoti yake kushindwa kutengemaa.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Bongo yapepea Ligi Kuu England!!
Bodi ya Utalii Tanzania, TTB, imesema Wizara ya Maliasili na Utalii ikishirikiana na Mamlaka zake tanzu TTB, TANAPA [Mamlaka ya Hifadhi za Wanyama] na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, zimeingia Mkataba na Lantech Service Agency ya Uingereza ili kutoa matangazo kwenye Mechi 114 za Ligi Kuu England kwa Msimu wa 2010/11.
Matangazo hayo yanayohusu Mbuga za Wanyama, Mlima Kilimanjaro na Bichi za Zanzibar yatakuwa yakionyeshwa wakati wa Mechi kwenye Matangazo ya Dijito yaliyo pembezoni na yanayozunguka Uwanja mzima katika Viwanja vya Timu 6 za Ligi Kuu.
Viwanja hivyo ni Ewood Park, Uwanja wa Blackburn Rovers, St James Park, Uwanja wa Newcastle, Stadium of Light wa Sunderland, Molineux wa Wolves, Britannia wa Stoke City na The Hawthorns wa West Bromwich Albion.
Matangazo hayo yatadumu sekunde 30 kwenye bodi za Matangazo kuzunguka Viwanja hivyo na yataonekana mara 6 kila Mechi.
Matangazo hayo yalianza kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye Mechi za Blackburn v Everton, Sunderland v Birmingham and Wolves v Stoke City hapo Agosti 14.
Robinho aigomea Fenerbahce
Fowadi wa Manchester City Robinho amekataa kuhamia Klabu ya Uturuki Fenerbahce na ameng’ang’ania kuhamia Italy au Spain kabla ya Jumanne ijayo Agosti 31 ambayo ndio Siku ya mwisho kwa uhamisho.
Robinho amelazimika kurudi Manchester City baada ya kukaa huko kwao Brazil na Klabu ya Santos kwa mkopo wa Miezi 6.
Robinho alisajiliwa kwa pauni Milioni 32.5 Mwaka 2008 ikiwa ni rekodi kwa Uingereza akitokea Real Madrid lakini amekuwa hapataki Man City.
Man City imewagomea Santos kuongeza mkopo wake na badala yake wanataka kumuuza moja kwa moja ili warudishe fedha zao.
Ingawa Meneja wa Man City, Roberto Mancini, amekiri Robinho anataka kuondoka, yeye ameacha milango wazi kwake kwa kusema ikiwa atafanya mazoezi kwa bidii anaweza kucheza Man City.
Fergie aiunga mkono England Kombe la Dunia 2018
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameyapa uzito maombi ya England kuwa Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia la Mwaka 2018 kwa kuipamba England kabla hajakutana na Wakaguzi wa FIFA ambao wako England kwa ziara ya Siku 4 kukagua Maombi hayo pamoja na Viwanja mbalimbali, ukiwemo Old Trafford ambako Sir Alex Ferguson na Sir Bobby Charlton watawakaribisha Wakaguzi hao 6 wa FIFA.
Ferguson, akitoa sapoti yake kwa England, alitamka: “Viwanja kwa Wachezaji na Mashabiki ni vizuri sana! Na mapenzi ya Waingereza kwa Soka yatahakikisha kila Mtu anakaribishwa na kupata wakati mzuri.”
CHEKI: www.sokainbongo.com

MATOKEO:
UEFA CHAMPIONS LIGI: Hatua ya Mchujo kuingia Makundi-Mechi za Marudiano
Timu za Partizan Belgrade, Basle, Hapoel Tel-Aviv, Werder Bremen na Braga zimefuzu kuingia kwenye Kapu la Droo ya kupanga Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI baada ya kushinda Mechi zao hapo jana.
Timu hizo 5 zitaungana na Washindi wa tano wa Mechi za leo kwenye Droo hiyo itakayojumuisha Vigogo wengine wa Ulaya kama vile Mabingwa Watetezi Inter Milan, Barcelona, Real Madrid, Chelsea, Manchester United, Arsenal na kadhalika.
MATOKEO KAMILI:
Anderlecht 2 v Partizan Belgrade 2, (Jumla ya Magoli kwa mechi mbili 4-2, Penalti 2-3)
FC Sheriff Tiraspol 0 v Basle 3, (0-4)
Hapoel Tel-Aviv 1 v Red Bull Salzburg 1, (4-3)
Sampdoria 3 v Werder Bremen 2, (4-5)
Sevilla 3 v Braga 4, (3-5)
EUROPA LIGI: Hatua ya Mchujo kuingia Makundi-Mechi za Marudiano
Anorthosis Famagusta 1 v CSKA Moscow 2, (1-6)
MECHI ZA LEO:
Jumatano, 25 Agosti 2010
UEFA CHAMPIONS LIGI:Hatua ya Mchujo kuingia Makundi-Mechi za Marudiano
Ajax v Dynamo Kiev, (Mechi ya kwanza 1-1)
Auxerre v Zenit St Petersburg, (0-1)
FC Copenhagen v Rosenborg, (1-2)
MSK Zilina v Sparta Prague, (2-0)
Tottenham v Young Boys, (2-3)

Tuesday 24 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Evra kukatia Rufaa kifungo!
Patrice Evra ameamua kukata Rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa Mechi 5 za Timu ya Taifa ya Ufaransa kwa ushiriki wake katika mgomo wa Wachezaji wa Ufaransa huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia.
Evra ndie alikuwa Nahodha wa Ufaransa huko Afrika Kusini na mgomo wa Wachezaji ulitokea baada ya mwenzao Nicolas Anelka kufukuzwa kwenye Timu baada ya kugombana na aliekuwa Kocha wa Ufaransa Raymond Domenech.
Pamoja na Evra, Wachezaji wengine waliofungiwa ni Anelka, mechi 18, Franck Ribery, mechi 3 na Jeremy Toulalan, mechi moja.
Kocha mpya wa Ufaransa, Laurent Blanc, ambae tayari aliwaadhibu Wachezaji wote 23 waliokuwa Afrika Kusini kwa kutowaita kwenye mechi ya kirafiki na Norway mwanzoni mwa Mwezi huu, ameshangazwa na ukali wa adhabu zilizotolewa pamoja na kutofautiana kwa urefu wake kwa kosa ambalo aliliita ni moja na la Wachezaji wote kwa pamoja.
‘Mtu Spesheli’ anena: ‘Ni Chelsea, Man United na Man City! Ze Gunners na Liverpool hawana lao!’
Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho ametamka kuwa Arsenal na Liverpool hawana chao Msimu huu kwa kuwa hawana ubavu wa kutwaa Ubingwa.
Mourinho, maarufu kama ‘Mtu Spesheli’, ambae aliwahi kuwa na Chelsea kwa Miaka mitatu, ametabiri kuwa vita ya Ubingwa ni ya Chelsea, Manchester United na Manchester City.
Mourinho alitamka: ‘Naamini ni Chelsea, Manchester United na Manchester City ndizo Timu zinaweza kuwa Bingwa. Ni ngumu kumuona Roy Hodgson akileta mafanikio Liverpool ambayo imezidi kuwa mbovu Mwaka hadi Mwaka. Liverpool ya 2004 ilikuwa bora kupita ya 2005! Ile ya 2005 ilikuwa bora kupita ya 2006 na kadhalika!”
Kuhusu Arsenal, Mourinho ametoa mawazo yake kuwa Meneja wao, Arsene Wenger, siku zote amekuwa akitoa kisingizio Kikosi chake ni kichanga.
Mourinho alieleza: “Kila Mwaka Arsenal huonekana wanakaribia Ubingwa lakini hamna kitu! Siku zote wanasema ni Timu changa, mwakani itakuwa bora! Lakini Timu ya Chipukizi ya jana si leo tena ni chipukizi! Sasa wamefika Miaka 25, 26 na 27 na ni lazima washinde! Fabregas, Walcott, Clichy, Song na Sagna si watoto tena! Wako kwenye umri wa kuwa Mabingwa! Lakini sidhani kama wana uwezo, nadhani ni Chelsea au Manchester United na Manchester City ambao wana Kikosi kizuri!”
CHEKI: www.sokainbongo.com

MSIMU MPYA WA UEFA ULAYA KUPAMBWA WIKI HII!!!
Ingawa mechi za Mtoano na Mchujo za Makombe ya UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI zimekuwa zikindirima ili kuzipata Timu zitakazoingia Droo ya Makundi ya Mashindano hayo, UEFA watazindua rasmi Msimu wao mpya wa 2010/11 huko Monaco wiki hii kwa kutangazwa kwa Wachezaji Bora wa Ulaya wa Mwaka, kugombewa kwa kwa Kombe la UEFA SUPERCUP kati ya Bingwa wa UEFA CHAMPIONS LIGI, Inter Milan, na Club Atletico de Madrid, Bingwa wa EUROPA LIGI, hapo Alhamisi, na pia kufanyika Droo ya Makundi kwa Mashindano ya Ulaya.
Ratiba ya UEFA inaonyesha Tuzo za Wachezaji Bora zitafanyika Alhamisi Agosti 26 pamoja na Droo ya kupanga Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI huku Mechi za Makundi hayo kuanza kuchezwa Septemba 14 na 15.
Droo ya Makundi ya EUROPA LIGI itafanyika Ijumaa Agosti 27 na kufuatiwa na pambano la kugombea UEFA SUPERCUP kati ya Inter Milan na Atletico Madrid Uwanjani Stade Loius II.
LEO NA KESHO NI SOKOMOKO ULAYA!!
• Timu kugombea Dola Milioni 19!!!!
Jumanne, Agosti 24
UEFA CHAMPIONS LIGI: Hatua ya Mchujo kuingia Makundi-Mechi za Marudiano
Anderlecht v Partizan Belgrade, (Mechi ya kwanza 2-2)
FC Sheriff Tiraspol v Basle, (0-1)
Hapoel Tel-Aviv v Red Bull Salzburg, (3-2)
Sampdoria v Werder Bremen, (1-3)
Sevilla v Braga, (0-1)
EUROPA LIGI: Hatua ya Mchujo kuingia Makundi-Mechi ya Marudiano
Anorthosis Famagusta v CSKA Moscow, (0-4)
Jumatano, 25 Agosti 2010
UEFA CHAMPIONS LIGI:Hatua ya Mchujo kuingia Makundi-Mechi za Marudiano
Ajax v Dynamo Kiev, (Mechi ya kwanza 1-1)
Auxerre v Zenit St Petersburg, (0-1)
FC Copenhagen v Rosenborg, (1-2)
MSK Zilina v Sparta Prague, (2-0)
Tottenham v Young Boys, (2-3)
Timu zinazocheza hatua ya Makundi kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI huwa na uhakika wa kupata angalau Dola Milioni 19 kila moja na leo na kesho Timu 20 zipo kwenye kinyang’anyiro cha Mechi za Marudiano za Hatua ya Mchujo ili kupata Timu 10 ambazo Alhamisi Agosti 26 jioni zitaingia kwenye Kapu la Droo ya kupanga Makundi ya Mashindano hayo wakijumuika na Timu Mabingwa, kama vile Inter Milan, Real Madrid, Manchester United, Barcelona, Arsenal na Chelsea, ambao wameingizwa moja kwa moja Hatua ya Makundi.
Timu hizo 20 zitakazocheza Mechi za Marudiano leo na kesho zilikutana kwenye Mechi ya Kwanza Wiki iliyopita na kati ya hizo ni Timu mbili tu ndizo zimelekea kushika hatamu ya kujihakikishia kuingia Hatua ya Makundi.
Timu hizo ni Zilina ya Slovakia ambayo iliifunga Spart Prague 2-0 ugenini na, pengine, Hapoel Tel Aviv ambayo iliifunga Red Bull Salzburg 3-2 ugenini.
Timu ya Ligi Kuu England, Tottenham, ilicheza ugenini huko Uswisi na Young Boys na kujikuta iko nyuma kwa bao 3-0 hadi dakika ya 28 ya mchezo lakini ikajitutumua na kupata matokeo ya 3-2 ambayo yatawapa matumaini makubwa kuwatungua Young Boys watakapowaalika Uwanjani kwao, White Hart Lane, Jijini London hapo kesho.
Pia leo kutakuwa na Mechi moja ya Hatua ya Mchujo ya EUROPA LIGI kati ya Anorthosis Famagusta v CSKA Moscow, (Matokeo Mechi ya kwanza 0-4) na mechi zote nyingine kuchezwa Alhamisi Agosti 26.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Man City waifumua Liverpool 3-0
Goli mbili toka kwa Carlos Tevez na moja la Gareth Barry zilishusha kipondo cha 3-0 toka Kwa Manchester City dhidi ya Liverpool Uwanjani City of Manchester mbele ya Watazamaji 47,087 mmoja wao akiwa Mmiliki Tajiri wa Man City Sheikh Mansour ambae ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika Uwanjani hapo.
Klabu Tajiri kwenye Ligi Kuu, Man City, iliyotumia zaidi ya Pauni Milioni 125 kununua Wachezaji Msimu huu, ilifunga bao la kwanza toka kwa Gareth Barry dakika ya 13 na hadi mapumziko matokeo yalikuwa 1-0.
Kipindi cha pili Carlos Tevez alipachika bao mbili, dakika ya 52 na 67.
Liverpool, wakitumia mfumo wa 4-4-2 bila ya Kiungo nanga Javier Mascherano ambae habari zimepamba moto kuwa mguu nje kwenda FC Barcelona, walizidiwa musuli kila idara huku Man City ikitawala kiungo kupitia Wachezaji wao Yaya Toure, Gareth Barry, Nigel de Jong, wakisaidiwa na James Milner na Winga Adam Johnson.
Vikosi vilivyoanza:
Manchester City (4-3-3): Hart; Richards, Kolo Toure, Kompany, Lescott; Yaya Toure, De Jong, Barry; Johnson, Tevez, Milner.
Akiba: Given, Zabaleta, Wright-Phillips, Adebayor, Silva, Vieira, Jo.
Liverpool (4-4-2): Reina; Johnson, Skrtel, Carragher, Agger; Jovanovic, Gerrard, Lucas, Kuyt; Torres, Ngog.
Akiba: Jones, Aurelio, Pacheco, Kyrgiakos, Maxi, Babel, Poulsen.
Refa: Phil Dowd

Monday 23 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Squillaci kupimwa afya Ze Gunners
Beki kutoka Ufaransa Sebastien Squillaci anategemewa kupimwa afya yake Klabuni Arsenal ili kukamilisha uhamisho wake kutoka Klabu ya Hispania, Sevilla.
Sevilla imethibitisha kuwa Squillaci, Miaka 30, yupo njiani kwenda London kukamilisha taratibu za uhamisho wake.
Arsenal inakabiliwa na uhaba wa Masentahafu baada ya William Gallas, Sol Campbell na Mikael Silvestre kung’oka Klabuni hapo.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameshamsaini Sentahafu Laurent Koscielny na pia Johan Djourou anategemewa kurudi Uwanjani baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Squillaci alikuwemo kwenye Kikosi cha Ufaransa huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia na alicheza mechi moja.
Mido yupo Ajax
Straika kutoka Misri Mido amehamia Ajax huko Uholanzi kutoka Klabu yake Middlesbrough katika uhamisho wa bure.
Middlesbrough na Mido wamekuwa na mvutano na hatimaye Meneja wa Boro, Gordon Strachan, akaamua kumtema Kikosini na hivyo kumruhusu aondoke kama Mchezaji huru.
Mido, Miaka 27, alianzia kucheza Soka lake huko Ulaya na Ajax na alikaa Miaka miwili na kuondoka Ajax Mwaka 2003 na kuzunguka Klabu kadhaa huko Ulaya zikiwemo Celta Vigo, Marseille, Roma, Tottenham, Wigan, kisha kurudi kwao kuchezea Zamalek na baadae kwenda West Ham.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Fergie kutwangwa Faini?
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, anaweza akakabiliwa na Faini za mfululizo ikiwa hatabadili msimamo wake wa kukataa kuhojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, mara baada ya mechi za Ligi Kuu England kama kanuni mpya za Ligi hiyo zinavyowataka kila Meneja wa Timu awepo kuhojiwa na BBC baada ya mechi za Timu zao.
Ferguson amekuwa na ugomvi na BBC tangu Mwaka 2004 wakati BBC waliporusha kipindi kilichoitwa Baba na Mwana ambacho kilikuwa kinamuelezea Ferguson na Mwanawe Jason ambae wakati huo alikuwa Wakala wa Wachezaji.
Ferguson alidai kipindi hicho kilizungumza upuuzi mtupu na akawataka BBC wamuombe radhi lakini BBC hawakufanya hivyo na yeye tangu wakati huo amegoma kuhojiwa na BBC.
Mara baada ya mechi ya Ligi Kuu hapo jana kati ya Fulham na Manchester United Ferguson alikataa kuhojiwa na BBC.
Kufuatana na kanuni mpya za Ligi Kuu, suala hilo sasa limepelekwa kwenye Bodi ya Ligi Kuu ili lijadiliwe na huenda akatwangwa Faini ya Pauni 1,000.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Blatter awapa matumaini England!
Rais wa FIFA, Sepp Blatter, ametamka itakuwa rahisi kwa Fainali za Kombe la Dunia kufanyika England kwa vile kila kitu kipo yaani Mashabiki, Viwanja na Miundombinu.
Wakati Blatter akiwapa matumaini, Wakaguzi wa FIFA wa Nchi zinazogombea kuwa Wenyeji wa Fainali za Mwaka 2018 na zile za 2022 wametua England kwa ukaguzi wa Maombi ya England ya kuwa Mwenyeji wa Fainali za Mwaka 2018.
Fainali za Kombe hilo Mwaka huu zilifanyika huko Afrika Kusini Mwezi Juni na Julai na Spain kuibuka Bingwa wa Dunia na zile zinazofuata ni Mwaka 2014 na zitafanyika Brazil.
Wakaguzi hao wamekuwa wakitembelea kila Nchi ya muombaji kwa Siku 4.
Ziara hiyo ilianzia Japan, Korea Kusini, Australia na kisha kwa waombaji wa pamoja Uholanzi na Ubelgiji, halafu Urusi na sasa England, na baadae wataendelea kwa waombaji wengine wa pamoja Spain na Ureno, kisha USA na kumalizia Qatar.
Timu hiyo ya Wakaguzi inaongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka la huko Chile, Harold Mayne-Nicholls.
FIFA itatoa uamuzi wa nani watakuwa Wenyeji Mwaka 2018 na 2022 baada ya mkutano wao huko Zurich, Uswisi Desemba 2, Mwaka huu.
Hata hivyo, Blatter ameonya Urusi ni Wapinzani wakubwa wa England katika maombi hayo kwani na wao wanazitaka Fainali za Mwaka 2018.
CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI KUU ENGLAND: Leo ni Man City v Liverpool
Vigogo wawili wa Ligi Kuu leo wanakwaana Uwanja wa City of Manchester hili likiwa pambano la tatu mfululizo kwa Vigogo kuvaana.
Wiki iliyokwisha Tottenham na Manchester City zilikutana katika mechi zao za kwanza za Ligi Kuu na kutoka sare 0-0 na pia Liverpool iliivaa Arsenal na kutoka sare 1-1.
Leo ni Man City na Liverpool.
Man City, wakitumia musuli yao ya kifedha, wamelundika Wachezaji wapya Msimu huu ambao ni David Silva, Aleksandr Kolarov na Yaya Toure ambao wote walicheza mechi na Tottenham lakini kwa leo wanaweza wakaongezeka Wachezaji wapya wengine James Milner na Mario Balotelli na wale wa zamani kina Jo na Robinho ambao walikuwa nje kwa mkopo Msimu uliopita.
Kwa Meneja wa Man City, Roberto Mancini, ugumu ni kupanga Timu hasa ukizingatia lundo la Wachezaji hao Mastaa na nini utakuwa uamuzi wake wa nani kucheza Kiungo kati ya Yaya Toure, Nigel de Jong, Gareth Barry na Patrick Viera, unangojewa kwa hamu na wadau.
Msimu uliokwisha, Timu hizi zilitoka sare katika mechi zao mbili za Ligi Kuu.
Liverpool wataingia Uwanjani bila ya mchezaji mpya Joe Cole ambae aliwashwa Kadi Nyekundu katika mechi ya Wikiendi iliyopita dhidi ya Arsenal na hivyo sasa anatumikia kifungo cha mechi tatu baada ya kuamua kutokata rufaa.
Lakini Mchezaji wao mpya mwingine, Christian Poulsen, kuenda akawemo dimbani kwenye Kiungo pamoja na Javier Mascherano ambae amepona maumivu yaliyomfanya atolewe kwenye mechi na Arsenal.
Vikosi vinategemewa kuwa:
Man City: Hart, Bridge, K.Toure, Kompany, Richards, Barry, Yaya Toure, De Jong, Milner, Silva, Tevez.
Liverpool: Reina, Aurelio, Carragher, Skrtel, Johnson, Poulsen, Mascherano, Kuyt, Jovanovic, Gerrard, Torres.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Gallas aweka historia kuhamia Spurs
Beki kutoka Ufaransa, William Gallas, atakuwa Mchezaji wa kwanza kuzichezea Klabu tatu pinzani za Jijini London, Chelsea, Arsenal na Tottenham, baada ya kusaini Mkataba wa Mwaka mmoja na Tottenham hivi juzi.
Gallas, Miaka 33, amekuwa Mchezaji wa 14 kuhamia kutoka Arsenal kwenda Tottenham katika historia ya Karne moja lakini atakuwa Mchezaji wa kwanza kucheza Klabu zote 3 zenye upinzani mkubwa huko London.
George Graham aliwahi kuzichezea Chelsea na Arsenal Miaka ya 1960 na katika Miaka ya 1970 alikuwa Meneja wa Arsenal na Tottenham.
Clive Allen alizichezea Tottenham na Chelsea na akasaini kucheza Arsenal Juni 1980 lakini baada ya Miezi miwili, bila ya kucheza mechi hata moja hapo Arsenal, akahamia Crystal Palace.
Mashabiki wengi wa Tottenham mpaka leo wanamshutumu aliekuwa Nahodha wao Sol Campbell alieondoka Tottenham kuhamia Arsenal Miaka 9 iliyopita.
Katika Miaka 10 iliyopita, Gallas ni Mchezaji wa nne tu kuhamia Spurs akitokea Arsenal wengine wakiwa Rohan Ricketts, Jamie O’Hara na David Bentley.
UENYEJI KOMBE LA DUNIA 2018: Wakaguzi FIFA watua England
Leo FA ya England watakuwa wenyeji wa Wakaguzi wa FIFA wanaotembelea Nchi zinazogombea kuwa Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 ili kukagua maombi hayo ikiwemo miundombinu.
Fainali za Kombe hilo Mwaka huu zilifanyika huko Afrika Kusini Mwezi Juni na Julai na Spain kuibuka Bingwa wa Dunia na zile zinazofuata ni Mwaka 2014 na zitafanyika Brazil.
Wakaguzi hao wamekuwa wakitembelea kila Nchi ya muombaji kwa Siku 3.
Ziara hiyo ilianzia Japan, Korea Kusini, Australia na kisha kwa waombaji wa pamoja Uholanzi na Ubelgiji, halafu Urusi na sasa England, na baadae wataendelea kwa waombaji wengine wa pamoja Spain na Ureno, kisha USA na kumalizia Qatar.
Timu hiyo ya Wakaguzi inaongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka la huko Chile, Harold Mayne-Nicholls.
FIFA itatoa amuse wa nani watakuwa Wenyeji Mwaka 2018 na 2022 baada ya mkutano wao huko Zurich, Uswisi Desemba 2, Mwaka huu.
RATIBA YA UKAGUZI:
-Julai 19-22: Japan [Wameomba 2022]
-Julai 22-25: Korea Kusini [Wameomba 2022]
-Agosti 9-12: Uholanzi & Ubelgiji [Waombaji wa pamoja]
-Agosti 16-19: Urusi
-Agosti 23-26: England
-Agosti 30-Septemba 2: Spain & Ureno [Waombaji wa pamoja]
-Septemba 6-9: USA
-Septemba 13-17: Qatar [Wameomba 2022]
Fergie: ‘Fulham walistahili!’
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amekiri kuwa matokeo ya sare ya 2-2 waliyopata jana huko Craven Cottage kwenye mechi ya Ligi Kuu yalistahili hasa kwa vile Fulham walicheza vyema Kipindi cha Pili.
Mara mbili Man United walikuwa mbele na mara mbili Fulham wakasawazisha.
Pia Man United, kwenye dakika ya 87, walikosa penalti iliyopigwa na Nani na kuokolewa na Kipa Stockdale na kama wangeifunga wangekuwa mbele 3-1 lakini dakika mbili baadae Fulham wakasawazisha na mechi kwisha 2-2.
Ferguson alisema: “Ukweli ni kuwa Fulham walistahili sare. Walicheza vizuri sana Kipindi cha Pili.”
Katika mechi hiyo, Nyota wa Man United Wayne Rooney hakucheza kwa kile kilichosemwa ni mgonjwa.

Sunday 22 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Fulham 2 Man United 2
Leo uwanjani Craven Cottage, Fulham wameweza kuisimamisha Manchester United na kutoka nao sare 2-2 katika mchezo mkali wa vuta nikuvute.
Pengine matokeo hayo ni mazuri kwa Man United hasa ukichukulia katika Misimu miwili iliyopita wamekuwa wakifungwa Uwanjani hapo.
Man United ndio waliopata bao kwanza dakika ya 11 Mfungaji akiwa Mkongwe Paul Scholes.
Kipindi cha Pili Simon Davies alisawazisha dakika ya 57.
Beki wa Fulham Brede Hangeland alijifunga mwenyewe kwenye dakika ya 84 na kuwapa Man United bao la pili.
Kwenye dakika ya 85, Nani aliikosesha Man United ushindi pale aliposhindwa kufunga penalti iliyookolewa na Kipa Stockdale.
Ndipo kwenye dakika ya 89 Hangeland akafuta makosa yake alipofunga bao la kichwa kufuatia kona na kufanya mechi iwe 2-2.
Vikosi vilivyoanza:
Fulham: Stockdale, Pantsil, Hughes, Hangeland, Konchesky, Duff, Murphy, Etuhu, Davies, Dempsey, Zamora.
Akiba: Zuberbuhler, Kelly, Baird, Gera, Riise, Greening, Dembele.
Man Utd: Van der Sar, O'Shea, Vidic, Jonathan Evans, Evra, Valencia, Fletcher, Scholes, Park, Hernandez, Berbatov.
Akiba: Kuszczak, Owen, Giggs, Smalling, Carrick, Nani, Rafael Da Silva.
Refa: Peter Walton
CHEKI: www.sokainbongo.com


Newcastle 6 Aston Villa 0
Wakiwa nyumbani, St James Park, wakicheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu tangu wapande Daraja, Newcastle leo imewapa furaha kubwa baada ya kuinyuka Timu ngumu Aston Villa bao 6-0.
Wakati mechi iko 0-0, John Carew aliikosesha Villa bao pale penalti yake ilipoota mbawa.
Hadi mapumziko Newcastle walikuwa mbele kwa bao 3-0 zilizofungwa na Viungo Joey Barton na Kevin Nolan, na la tatu na Straika Andy Carroll.
Kipindi cha pili, Carroll akafunga bao mbili na Kevin Nolan akapata bao lake la pili na la 6 kwa Newcastle.
Vikosi vilivyoanza:
Newcastle: Harper, Perch, Coloccini, Williamson, Jose Enrique, Routledge, Smith, Barton, Gutierrez, Nolan, Carroll.
Akiba: Krul, Lovenkrands, Ryan Taylor, Xisco, Ameobi, Vuckic, Tavernier.
Aston Villa: Friedel, Luke Young, Clark, Dunne, Warnock, Albrighton, Petrov, Ireland, Downing, Ashley Young, Carew.
Akiba: Guzan, Delfouneso, Heskey, Reo-Coker, Beye, Lichaj, Bannan.
Refa: Martin Atkinson
Scholes kudumu Man United
Paul Scholes amesema ataendelea kucheza Manchester United kwa muda mrefu zaidi ikiwa Klabu itamuona bado anahitajika.
Scholes, Miaka 35, anatimiza Miaka 18 akiwa yupo Manchester United na ameanza Msimu huu mpya kwa kung’ara sana hasa katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu walipoifunga Newcastle bao 3-0 na yeye kuwa ndio Mchezaji Bora wa Mechi hiyo.
Scholes ametamka: “Nimebaki hapa kwani ni Klabu Bora! Mie Mzawa wa Manchester sina sababu kuondoka. Meneja akiendelea kunihitaji, ntaendelea kucheza. Huwezi kuchoshwa na kushinda Vikombe! Huchoki kushinda kila wiki! Nani atachoka hilo?”
Lyon wamwania Robinho
Lyon ya Ufaransa imeingia kwenye mbio za kutaka kumchukua Robinho ambae amekuwa hataki kubaki Manchester City baada ya kumaliza Mkataba wa mkopo na Klabu ya kwao Brazil Santos.
Inasadikiwa Man City washanyosha mikono kwa Robinho na sasa wana nia tu ya kujaribu kurudisha Pauni Milioni 32.5 walizomnunulia Septemba 2008.
Ingawa Robinho yumo mwenye Kikosi cha Man City walichokisajili kwa ajili ya EUROPA LIGI hakuwemo kwenye mechi na FC Timisoara Alhamisi iliyopita kwa vile Man City hawataki kutibua soko lake kwani akiichezea Man City kwenye mashindano hayo hataruhusiwa kuichezea Klabu nyingine Ulaya Msimu huu.
Inasemekana Lyon wametoa ofa ya kumchukua Robinho kwa mkopo lakini Man City wanataka kumuuza moja kwa moja.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Inter yainyuka Roma, yatwaa Supercup
Jana Samuel Eto’o alipachika bao mbili za Kipindi cha Pili na kuiwezesha Inter Milan kuichapa Roma bao 3-1 na kutwaa Supercup Kombe linaloashiria mwanzo wa Msimu mpya.
John Riise ndie alifunga bao kwa Roma lakini Goran Pandev akaisawazishia Inter na kisha Eto’o akapachika mbili na kumpa Meneja mpya wa Inter Milan, Rafa Benitez, Kombe lake la kwanza.
Msimu uliokwisha chini ya Jose Mourinho, aliekwenda Real Madrid, Inter walitwaa Mataji matatu yakiwa ni Ubingwa wa Ulaya, Ubingwa wa Italia na Kombe la Italia.
Barca 4 Sevilla 0
• Yatwaa Spanish Supercup kwa jumla ya bao 5-3
Barcelona, wakiwa kwao Nou Camp, wameweza kuupindua ushindi wa 3-1 wa Sevilla katika mechi ya kwanza na kuichapa Sevilla 4-0 na hivyo kutwaa Supercup kwa jumla ya mabao 5-3.
Lionel Messi wa Barca alipachika mabao matatu na bao pamoja Abdoulay Konko wa Sevilla alijifunga mwenyewe.
Kuyt kwenda Inter Milan?
Straika wa Liverpool kutoka Uholanzi, Dirk Kuyt, ameambiwa na Bodi yao kuwa Inter Milan imetoa ofa ya kumnunua Mchezaji huyo mpiganaji mzuri kiwanjani.
Inter Milan kwa sasa ipo chini ya Meneja wa zamani wa Liverpool, Rafa Benitez, ambae inadaiwa anawataka pia Wachezaji wengine wa Liverpool.
Hata hivyo, Liverpool haijasema nini uamuzi wao kuhusu ofa hiyo ambayo inakadiriwa kuwa Pauni Milioni 15.
Kuyt alijiunga na Liverpool Mwaka 2006 na ni Mchezaji muhimu wa Holland ambayo aliichezea pia kwenye Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na mpaka sasa ameshaichezea Nchi hiyo mechi 70.
Powered By Blogger