Saturday 7 November 2009

RATIBA LIGI KUU England:
Jumamosi, Novemba 7
Aston Villa v Bolton
Blackburn v Portsmouth
Tottenham v Sunderland
Wolves v Arsenal
Jumapili, Novemba 8
Chelsea v Man U
Hull City v Stoke
West Ham v Everton
Wigan v Fulham
ZE BIGI MECHI: Chelsea v Man U
Stamford Bridge, Jumapili Novemba 8, Saa 1 usiku [Bongo Taimu]
Chesea, anaeongoza Ligi, atakuwa nyumbani Stamford Bridge, kupambana na Mabingwa Watetezi Manchester United ambao wako nafasi ya pili.
Msimu uliokwisha, mechi kama hii iltoka sare 1-1 huku Ji-Sung Park akiifungia goli Man U na Salomon Kalou kusawazisha dakika ya 80.
Nini wanasema:
Sir Alex Ferguson: "Chelsea ni mechi kubwana rekodi yetu uwanjani kwao si nzuri kwa miaka ya hivi karibuni. Wachezaji wanajua umuhimu wa mechi hii na wataishughulikia kwa ubora zaidi kuliko ile mechi ya Anfield.”
Gary Neville: "Kwa sasa Chelsea wako juu. Ni mechi ngumu.”
Vikosi:
Chelsea (Pengine, 4-4-2): Cech; Ivanovic, Carvalho, Terry, A Cole; Essien, Ballack, Lampard, J Cole; Anelka, Drogba.
Manchester United (Pengine, 4-4-2): Van der Sar; O'Shea, Brown, Evans, Evra; Valencia, Scholes, Carrick, Nani; Berbatov, Rooney.
Refa: Martin Atkinson.
Msimu uliokwisha: Chelsea 1 Man United 1; Man United 3 Chelsea 0.
Ferdinand kuwa nje kwa muda mrefu!!
Beki mahiri wa Manchester United, Rio Ferdinand, anategemewa kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kushindwa kupona musuli ya mguuni.
Meneja wake Sir Alex Ferguson amesema: “Hajapona. Na atakuwa nje muda mrefu!”
Hivyo, Ferdinand ataikosa mechi ya kesho ya Ligi Kuu na Chelsea na pia kuichezea England huko Doha, Qatar Novemba 14 ambapo England itacheza na Brazil.
Jumamosi hii, Ferdinand anatimiza miaka 31 na msimu huu amekuwa akikumbwa na majeruhi ya mara kwa mara kwani aliukosa mwezi mzima wa kwanza wa msimu huu baada ya kuchanika musuli pajani akiwa mazoezini.
Kifungo cha kusajili Wachezaji Chelsea chasimamishwa!!
CAS [Court of Arbitration for Sport] imesimamisha kifungo walichopewa Chelsea na FIFA cha kutosajili Wachezaji hadi 2011 baada ya kukiuka sheria na kumchukua Mchezaji Gael Kakuta kutoka Lens ya Ufaransa.
CAS imetamka kuwa kifungo hicho kitasimama hadi rufaa ya Chelsea itakaposikilizwa na uamuzi kutoka.
Rufaa hiyo inategemewa kusikilizwa mwakani.
Uamuzi huo unamaanisha Chelsea wanaweza kusajili Wachezaji mwezi Januari 2010 wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa lakini Meneja wa Chelsea, Carlo Ancelotti, amesema hana nia ya kusajili mtu.
Hata hivyo, mwezi huo wa Januari, Chelsea itawapoteza Wachezaji Michael Essien, Didier Drogba, Salomon Kalou na John Mikel Obi ambao wote watakuwa na Timu zao za Taifa kwenye Mashindano ya Kombe la Afrika kwa Mataifa ya Afrika yatakayochezwa Januari huko Angola.
Viera akasirika kuachwa Ufaransa!
Patrick Viera amesema Kocha wa Ufaransa Raymond Domenech amefanya makosa makubwa kutomchagua Kikosi cha Ufaransa ambacho kitacheza na Republic of Ireland kwenye mechi ya mtoano kuwania kuingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani wiki ijayo.
Viera ameshaichezea Ufaransa mara 107 na msimu huu huko Klabuni kwake Inter ya Italia hana namba.
Viera, mwenye miaka 33, ametamka: "Mie najijua mwenyewe na Ufaransa hamna bora kama mie!”

Thursday 5 November 2009

Benni McCarthy kuhama Blackburn Januari ili apate namba!!
Mshambuliaji toka Bondeni, Benni McCarthy, ambae kwa sasa anapigwa benchi na Timu yake Blackburn Rovers anataka kuihama Timu hiyo ili aende kwingine ambapo atapata namba na hivyo kupata nafasi kubwa ya kuchukuliwa Kikosi cha Timu ya Taifa ya Afrika Kusini kitakachocheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika huko huko kwao kuanzia Juni 11, 2010 hadi Julai 11, 2010.
Habari hizi za kuhama zimethibitishwa na Meneja wa Blackburn Sam Alladyce ambae amesema: “Namwelewa nia yake ni kutaka kucheza kila siku. Lakini kwa sasa hapati namba kwa vile David Dunn amepona na amerudi kwenye fomu. Ikitokea ofa nzuri kwa Benni ntaruhusu ahame!”
Tangu msimu huu uanze, Benni McCarthy ameanza mechi moja tu na ni ile ya ufunguzi Blackburn na Manchester City na mechi nyingine zote amecheza akitokea benchi.
MAN CITY kwenda Abu Dhabi kwa Tajiri wao!!
Mmiliki wa Manchester City Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan anategemewa kuiona Timu yake ikicheza kwa mara ya kwanza tangu alipoinunua kwa Pauni Milioni 210 Septemba mwaka jana wakati itakapozuru Abu Dhabi na kucheza na Timu ya Taifa ya Falme za Nchi za Kiarabu, UAE, Novemba 12.
Mark Hughes, Meneja wa Man City, anatagemewa kuongoza Kikosi pungufu kwa vile Wachezaji wao Nyota wengi watakuwa kwenye Timu zao za Taifa ambazo zitakuwa kwenye mechi za mwisho za kuwania kuingia Fainali Kombe la Dunia.
Kikosi hicho kitaruka kwenda Abu Dhabi Jumatatu ijayo.
Wiki ya kuanzia Jumatatu hiyo ni wiki ya Timu za Taifa kufuatana na Kalenda ya FIFA.
Sheikh Mansour ni mmoja wa Koo ya Kifalme huko UAE na mwakilishi wake hapo Man City ambae amemteua Mwenyekiti ni Khaldoon al-Mubarak.
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
Wenyeji Nigeria, Spain na Korea Robo Fainali!
MATOKEO MECHI ZA LEO Alhamisi, Novemba 5:
Nigeria 5 New Zealand 0
Spain 4 Burkina Faso 1
Mexico 3 South Korea 5
Iran 1 v Uruguay 2
RATIBA ROBO FAINALI:
Novemba 8:
Colombia v Turkey
Uswisi v Italy
Novemba 9:
Spain v Uruguay
Nigeria v South Korea
BONGO YANYUKWA 5-1 NA MISRI MECHI YA KIRAFIKI!
Katika mechi ya Kirafiki iliyochezwa Misri kuanzia saa 2 na nusu Bongo Taimu, Timu ya Taifa ya Tanzania leo imefungwa mabao 5-1 na Misri inayojitayarisha kucheza mechi yake ya mwisho na Algeria ili kuingia Fainali Kombe la Dunia mwakani huko Afrika Kusini mechi itakayochezwa Novemba 14.
Misri wanahitaji ushindi wa 3-0 ili waingie Fainali na ikiwa mechi hiyo itaisha huku Misri kashinda 2-0 basi itachezwa Uwanja wa Nchi baki [sio Misri wala Algeria] ili apatikane Mshindi kwenda Fainali Kombe la Dunia.
Magoli ya Misri yalifungwa na Imad Mutab, dakika ya 8 na 34, Amr Zaki, dakika ya 34, Mohamed Barakat, dakika ya 41 na Ahmad Raof dakika ya 86.
Bao la Bongo lilifungwa dakika ya 45 na Mfungaji hatukumjua.
ZE BIGI MECHI Jumapili: Chelsea v Man U!!!!
Refa aliewahi ‘kuiua’ Man U kuchezesha!!!!
Martin Atkinson [pichani] ameteuliwa kuchezesha mechi ya Ligi Kuu Jumapili Novemba 8 Uwanjani Stamford Bridge kati ya vinara wa Ligi Kuu Chelsea na Mabingwa Watetezi Manchester United ambao wako nafasi ya pili.
Uteuzi huu wa Refa Atkinson utapokewa kwa kugwaya kwa kambi ya Man U kwani huko nyuma alishawahi kupondwa na Ferguson na hali ya hewa ya hivi karibuni, hasa tangu Ferguson aingie matatani alipotoa kauli kuwa Refa Alan Wiley hayuko fiti na kushitakiwa na FA, katika kila mechi waliyocheza Man U wamekuwa wakiandamwa na maamuzi tata kutoka kwa Marefa hao wa England ambao pia wamekuwa wakiwapa Wachezaji wa Man U Kadi Nyekundu.
Mwezi Machi 2008, Sir Alex Ferguson alipewa onyo kali na FA baada ya kumlaumu sana Refa Martin Atkinson pamoja na Kiongozi Mkuu wa Marefa, Keith Hackett, baada ya Man U kufungwa 1-0 na Portsmouth kwenye mechi ya Nusu Fainali Kombe la FA.
Katika mechi hiyo Refa Atkinson aliwanyima Man U penalti ya wazi kisha kuwapa Portsmouth penalti waliyopatia bao lao la ushindi na papo hapo kumtoa Kipa wa Man U Tomasz Kuszczak kwa Kadi Nyekundu.
Kwa wakati huu, kwa kauli yake kuhusu Refa Alan Wiley, Sir Alex Ferguson anakabiliwa na kesi huko FA.
Kroenke anyemelea kuichukua Arsenal!!
Bilionea Mmarekani, Stan Kroenke, ambae pia ni Mkurugenzi kwenye Bodi ya Arsenal, amezidi kunyemelea kuiteka Arsenal baada ya kuongeza Hisa zake kufikia asilimia 29.9 toka 29.6 alizokuwa nazo majuzi.
Kroenke, ambae ni Mmilikiwa wa Timu ya Vikapu ya NBA huko Marekani ya Denver Nuggets na ile ya Soka inayocheza Ligi ya MLS, Colorado Rapids, atalazimika kutoa ofa ya kununua Hisa zote hapo Arsenal akifikisha Hisa asilimia 29.99.
Mpaka sasa Kroenke hajasema lolote nini anakitaka hapo Arsenal na amebatizwa jina ‘Silent Stan” yaani ‘Stan Mkimya’.
LIGI KUU: West Ham 2 Aston Villa 1
Katika mechi pekee ya Ligi Kuu iliyochezwa Jumatano Novemba 4, West Ham waliibuka washindi kwa mabao 2-1 nyumbani Uptown Park dhidi ya Timu ngumu Aston Villa.
Mchezaji alieingizwa kutoka benchi la akiba, Zavon Hines, ndie aliewafungia West Ham bao la pili na la ushindi dakika ya 90.
Mark Noble aliipatia West Ham bao la kwanza kwa penalti dakika ya 45 baada ya Habib Beye kucheza rafu iliyoonekana na Refa Steve Bennett.
Kipindi cha pili dakika ya 49 Refa Steve Bennett aliwapa penalti Aston Villa alipoamua Manual Da Costa wa West Ham alicheza faulo lakini penalti hiyo iliyopigwa na Ashley Young iliokolewa na Kipa Robert Green.
Ashley Young alirekebisha makosa yake kwa kuisawazishia Villa dakika ya 52.
Beye alipewa Kadi ya Pili ya Njano na hivyo kupata Nyekundu dakika ya 84 na kuwaacha Villa wakiwa mtu 10.
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
Colombia, Italy, Turkey na Uswisi zipo ROBO FAINALI!!!
MATOKEO Novemba 4:
Argentina 2 Colombia 3
Italy 2 USA 1
Turkey 2 UAE 0
Uswisi 4 Germany 3
Baada ya kuwatoa Argentina 3-2, Colombia wameingia Robo Fainali na watakutana na Turkey waliowafunga UAE 2-0.
Nao Uswisi watacheza na Italy Robo Fainali baada ya Uswisi kuitoa Ujerumani 4-3 na Italy kuibwaga USA 2-1
Ratiba ya mechi za leo za RAUNDI YA PILI:
Novemba 5:
Spain v Burkina Faso
Iran v Uruguay
Mexico v South Korea
Nigeria v New Zealand
UEFA CHAMPIONS LIGI: Taarifa ya Mechi za Jumatano Novemba 4
Liverpool njia panda!!! Arsenal kidedea!!!
Lyon na Sevilla zasonga mbele Raundi ya Mtoano!!
Liverpool wamejiweka kwenye hali ngumu mno kwa kutoka sare 1-1 na Lyon hapo jana na sasa ili wasonge mbele kwenye Mashindano hayo ni lazima washinde mechi zao mbili zilizobaki na pia waombe Fiorentina wafungwe.
Wakati Liverpool wapo mashakani kwa Arsenal mambo ni mdundo baada ya kuichapa AZ Alkmaar mabao 4-1 na kwa kila hali wanategemewa kuingia Raundi ijayo.
Ripoti kwa kila Kundi:
KUNDI F:
Msimamo:
-Inter Milan pointi 6
-Rubin Kazan pointi 5
-Barcelona pointi 5
-Dynamo Kiev pointi 4
Inter Milan walifunga goli mbili katika dakika 4 za mwisho na kuibuka washindi kwa bao 2-1 dhidi ya Dynamo Kiev na hivyo kuchukua uongozi wa Kundi hili.
Katika mechi nyingine ya Kundi hili iliyochezwa mapema, Rubin Kazan walitoka sare 0-0 na Mabingwa Watetezi Barcelona.
KUNDI E:
Msimamo:
-Lyon pointi 10
-Fiorentina pointi 9
-Liverpool pointi 4
-Debrecen 0
Lyon walisawazisha dakika ya 90 kupitia Lisandro baada ya Liverpool kupata bao la uongozi kupitia Babel na hivyo kuifanya Liverpool iwe mashakani kusonga mbele kwani Fiorentina waliichapa Debrecen mabao 5-2.
Endapo katika mechi ijayo Liverpool atashindwa kuwafunga Debrcen, Liverpool watakuwa nje ya Mashindano.
Na hata wakiwafunga Debrecen na huku Fiorentina wawafunge Lyon, basi Leverpool nje!
KUNDI H:
Msimao:
-Arsenal pointi 10
-Olympiacos pointi 6
-Standard Liege pointi 4
-AZ Alkmaara pointi 2
Licha ya Arsenal kuifunga AZ Alkmaar mabao 4-1 bado uhakika wa kusonga mbele haujathibitika baada ya Standard Liege kuifunga Olympiacos 2-0.
KUNDI G:
Msimamo:
-Sevilla pointi 10
-Unirea Urziceni pointi 5
-Stuttgart pointi 3
-Rangers pointi 2
Sevilla walitoka suluhu 1-1 na Stuttgart na kutinga Raundi inayofuata ya Timu 16 ya Mtoano.
Katika mechi nyingine, Rangers ya Scotland na Unirea Urziceni zilitoka sare 1-1.
MECHI ZIJAZO ZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
Jumanne, Novemba 24:
KUNDI E
Debrecen v Liverpool
Fiorentina v Lyon
KUNDI F
Barcelona v Inter Milan
Rubin Kazan v Dynamo Kiev
KUNDI G
Rangers v Stuttgart
Unirea Urziceni v Sevilla
KUNDI H
AZ Alkmaar v Olympiacos
Arsenal v Standard Liege
Jumatano, Novemba 25:
KUNDI B
Manchester United v Besiktas
CSKA MOSCOW V Wolfsburg
KUNDI A
Bordeaux v Juventus
Bayern Munich v Maccabi Haifa
KUNDI C
Real Madrid v FC Zurich
AC Milan v Marseille
KUNDI D
FC Porto v Chelsea
Apoel Cyprus v Atletico Madrid

Wednesday 4 November 2009

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Rubin Kazan 0 Barcelona 0
Katika mechi iliyochezwa Urusi na kuanza mapema kupita nyingine zote za leo za UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Mabingwa Watetezi wa Kombe hili Barcelona wamejikuta wakitoka 0-0 na Mabingwa wa Urusi Rubin Kazan ambao waliwanyuka Barcelona 2-1 huko kwao Nou Camp wiki mbili zilizokwisha.
Matokeo haya yanamaanisha Kundi hili liko wazi na Inter Milan ambao wako mkiani wakiwafunga Dynamo Kiev katika mechi inayoanza dakika chache zijazo watachupa hadi kileleni kwenye Kundi hili F.
UEFA EUROPA LIGI
RATIBA Alhamisi, 5 Novemba 2009
AEK Athens v BATE,
Anderlecht v Politehnica Timisoara,
Basle v CSKA Sofia,
CFR 1907 Cluj-Napoca v Sparta Prague,
Dinamo Bucharest v Galatasaray,
Dinamo Zagreb v Ajax,
Everton v Benfica,
FC Copenhagen v PSV,
FC Twente v FC Sheriff Tiraspol,
Fenerbahce v Steaua Bucharest,
Genoa v Lille,
Hamburg vCeltic
Heerenveen v Hertha Berlin,
Levski Sofia v SV Red Bull Salzburg,
Nacional v Athletic Bilbao,
Partizan Belgrade v Club Brugge,
Rapid Vienna v Hapoel Tel-Aviv,
Roma v Fulham
SK Sturm Graz v Panathinaikos,
Slavia Prague v Valencia,
Sporting v FK Ventspils,
Toulouse v Shakhtar Donetsk,
Villarreal v Lazio,
Werder Bremen v FK Austria Vienna,
Wenger hajui la Kroenke lipi!!!
Arsene Wenger amesema hasumbuliwa na taarifa kuwa Mmarekani Stan Kroenke ameendeleza kwa kasi ununuzi na ulimbikizaji wa Hisa za Arsenal.
Mpaka sasa Bilionea huyo ambae pia ni Mmiliki wa Klabu ya NBA, Denver Nuggets, ndie mwenye Hisa nyingi Arsenal aliehodhi Hisa asilimia 29.6 na akifikisha Hisa aslimia 29.99 sheria zinamlazimisha kutoa ofa ya kununua Hisa zote zilobaki Klabuni hapo.
Wenger amebainisha: “Hainisumbia ili mradi wasiniingilie na kuniambia nibadili msimamo na falsafa yangu kuhusu Soka ya Timu hii! Sijui nia ya Kroenke ni nini! Sijawahi kuongea nae!”
FA yaitupa Rufaa ya Liverpool ya Kadi Nyekundu kwa Degen, ya Carragher uamuzi bado!!!
Chama cha Soka England, FA, wameitupilia mbali Rufaa ya Liverpool waliyokata kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Mchezaji wao Philipp Degen katika mechi ya Ligi Kuu Jumamosi iliyopita ambayo walichapwa 3-1 na Fulham.
Degen alipewa moja kwa moja Kadi Nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya Clint Dempsey na sasa atatumikia kifungo cha mechi 3 za huko England.
Liverpool pia wamekata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Mchezaji wao Jamie Carragher katika mechi hiyo hiyo ya Jumamosi waliyofungwa na Fulham ambayo Carragher akiwa ndie mtu wa mwisho kwenye ulinzi alimkamata Fowadi wa Fulham Bobby Zamora na hivyo kulambwa Nyekundu.
FA haijatoa uamuzi kuhusu rufaa ya Carragher.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Tathmini Mechi za Leo!
Arsenal bado wamo, Liverpool hatihati!!!
RATIBA:
Jumatano, 4 Novemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
KUNDI E
Fiorentina v Debrecen,
Lyon v Liverpool,
KUNDI F
Rubin Kazan v Barcelona,
Dynamo Kiev v Inter Milan,
KUNDI G
Sevilla v VfB Stuttgart,
Unirea Urziceni v Rangers
KUNDI H
Arsenal v AZ Alkmaar,
Standard Liege v Olympiakos


Arsenal v AZ Alkmaar
Arsenal wakiwa nyumbani Emirates Stadium watamkosa fulbeki Gael Clichy ambae amegundulika amevunjika kimfupa cha mgongo na atakuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili.
Lakini Kiungo toka Czech Tomas Rosicky amerudi kundini baada ya kupona goti ila Mafowadi Nicklas Bendtner na Theo Walcott, Kipa Lukas Fabianski (paja) na Kiungo Denilson (mgongo) bado ni majeruhi.
Arsenal wakiwafunga AZ Alkmaar na Standard Liege washindwe kuifunga Olympiakos Arsenal watasonga mbele na kuungana na Chelsea na Manchester United Raundi inayofuata ya Mtoano ya Timu 16.
Mpaka sasa Arsenal wako kileleni Kundi H wakiwa na pointi 7 kutoka mechi 3 baada ya kushinda 2 na kutoka 1-1 na AZ Alkmaar mechi iliyokwisha.
Lyon v Liverpool
Liverpool leo wako ugenini huko Ufaransa kucheza na Lyon Timu ambayo iliifunga Liverpool mechi iliyokwisha iliyochezwa Anfield kwa bao 2-1 na leo lazima Liverpool washinde ili kufufua uhai wao wa kusonga mbele.
Endapo Liverpool watafungwa basi atabaki na matumaini finyu mno ya kufuzu kuingia Raundi inayofuata.
Mpaka sasa Liverpool wanaweweseka baada ya kufungwa mechi 6 katika 7 za mwisho walizocheza na hali hiyo haiwapi matumaini hasa kwa vile pia wanakabiliwa na majeruhi kibao.
Majeruhi hao ni Nahodha Steven Gerrard (nyonga), Albert Riera (paja), Martin Kelly (enka), Martin Skrtel (musuli na kuugua maradhi), Glen Johnson (musuli) na Fabio Aurelio (musuli).
Fernando Torres yupo Kikosini ingawa inasemekana hayuko fiti kabisa lakini atacheza.
Pia Mchezaji mpya, Alberto Aquilani huenda akachezeshwa baada ya kupona.
Katika Kundi lao Liverpool wako nafasi ya 3 huku Lyon wakiongoza wakiwa na pointi 9, Fiorentina wa pili pointi 6 na Liverpool pointi 3.
Leo Fiorentina wako nyumbani wanacheza na Vibonde wa Kundi hili Timu ambayo waliifunga mechi iliyopita kwao, Debrecen ya Hungary.
Chelsea na Man U zatinga Raundi ya Mtoano UEFA CHAMPIONS LEAGUE!!
Baada ya Chelsea kutoka sare 2-2 na Atletico Madrid huko Spain na Manchester United kutoka suluhu 3-3 na CSKA Moscow, Timu hizi mbili zimesonga mbele kuingia Raundi inayofuata ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ya Mtoano itakayokuwa na Timu 16 huku zikiwa zimebakiza mechi 2 katika Makundi yao.
Timu nyingine zilizofuzu jana kusonga mbele ni FC Porto ambayo ipo Kundi la Chelsea na Bordeaux iliyo Kundi A.
Ferguson awataka UEFA wafute Kadi ya Fletcher!!!
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amewataka UEFA waifute Kadi ya Njano aliyopewa Darren Fletcher kwa kile Refa alichodhani kajiangusha ndani ya boksi ili apate penalti katika mechi ya jana ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE iliyochezwa Old Trafford na CSKA Moscow na kumalizika 3-3.
Huku mechi ikiwa 3-1 kwa CSKA kuwa mbele, Aleksei Berezutski alimkwatua Fletcher aliekuwa anaenda kufunga na Refa Olegário Benquerença kutoka Ureno akampa Fletcher Kadi ya Njano kitendo ambacho Ferguson amekiita kibovu katika miaka yake 50 ya soka.
UEFA hawaruhusu Timu kukata rufaa kuhusu Kadi za Njano labda Refa ampe Mchezaji Kadi kwa makosa yaani Mchezaji ambae hana hatia apewe Kadi badala ya mwingine aliecheza rafu.
Msimu uliokwisha Fletcher alikosa kucheza Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Barcelona baada ya kupewa Kadi kwenye Nusu Fainali Man U walipocheza na Arsenal.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
MATOKEO: Jumanne, 3 Novemba 2009

KUNDI A
Bayern Munich 0 v Bordeaux 2,
Maccabi Haifa 0 v Juventus 1,
KUNDI B
Manchester United 3 v CSKA Moscow 3,
Besiktas 0 v Wolfsburg 3,
KUNDI C
AC Milan 1 v Real Madrid 1,
Marseille 6 v FC Zurich 1,
KUNDI D
Apoel Nicosia 0 v FC Porto 1,
Atletico Madrid 2 v Chelsea 2

Tuesday 3 November 2009

REFA KUJICHANGANYA NA MAPACHA WA MAN U: FA yaamua Kadi ihamishwe apewe Rafael!!!

Chama cha Soka cha England,FA, katika hatua inayoendeleza utata, imeamua kuishughulikia rufaa ya Manchester United kuhusu kosa la Refa
Chris Foy kumpa kimakosa Fabio da Silva Kadi ya Njano kwa kusema Kadi hiyo atabandikwa Nduguye Pacha mwenzake Rafael da Silva ambae ndie alicheza rafu.
Utata huo ulitokea kwenye mechi ya Kombe la Carling kati ya Barnsley na Manchester United ambayo Man U walishinda 2-0 na Mapacha hao wawili kuonekana wakimkabili Jamal Campbell-Ryce wa Barnsley kwenye dakika ya 83 na Rafael kucheza faulo ambayo Refa Chris Foy alimpa Kadi ya Njano Fabio.
Mapacha hao, Rafael na Fabio wenye umri wa miaka 19, wamefanana mno kiasi ambacho hata Meneja wao wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amekiri kuwa hata yeye anaweza kuwatenganisha tu kwa sababu Fabio huvaa pete ya ndoa kidoleni mwake.
Uamuzi huu wa FA umewashangaza Wadau kwani sheria na taratibu za Soka zinasema endapo Refa atakosea na kumpa Kadi Mchezaji kimakosa basi Kadi hiyo hufutwa.
Lakini uamuzi huo wa FA ambao umeenda mbele na kuihamisha Kadi hiyo kwa Mchezaji mwingine unaonekana ni kitu kipya.
Manchester United bado haijasema lolote kuhusu uamuzi huu wa kushangaza wa FA.

Kroenke aendelea kununua hisa zaidi Arsenal
Mkurugenzi wa Arsenal, Stan Kroenke, ambae ni Mmarekani, ameendelea kununua na kulimbikiza hisa za Klabu ya Arsenal na sasa anamiliki hisa asilimia 29.6 na kisheria akizidisha zaidi ya hisa asilimia 29.99 basi atalazimika kutoa ofa ya kununua hisa za Klabu zote zilizobaki.
Siku za hivi karibuni, Mmarekani huyo ambae ni Bilionea na ni Mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Vikapu huko Marekani, yaani NBA, Denver Nuggets, amenunua hisa 427 kwa bei ya Pauni 8,500 kila moja kwa jumla ya Pauni Milioni 3.6.
Stan Kroenke, aliebatizwa jina ‘Stan Mkimya’ [‘Silent Stan’] kwa vile amekataa kuelezea lolote kuhusu dhamira yake kuhusu kulimbikiza hisa za Arsenal, ndie kwa sasa Mmiliki wa hisa nyingi hapo Arsenal.
Wamiliki wengine wa hisa za Arsenal ni Tajiri wa Uzbekistan, Alisher Usmanov, mwenye asilimia 24, na wengine ni Danny Fiszman na Bibi Bracewell-Smith.
Beckham kutua AC Milan Januari 2010
Klabu ya David Beckham Los Angeles Galaxy ya Marekani na AC Milan zimethibitisha kufikia makubaliano kumruhusu Mchezaji huyo wa England kwenda kucheza kwa mkopo AC Milan mwezi Januari 2010 kwa miezi 6 wakati ambapo msimu wa Ligi ya MLS huko Marekani utakaposimama.
Lengo la Beckham kwenda kucheza huko Italia ni kukidhi matakwa ya Kocha wa England Fabio Capello ambae amemtaka Mchezaji huyo wa England, anaeshikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi kwa Wachezaji wa mbele huko England, acheze Ligi yenye ushindani ili afikiriwe kuchukuliwa kuichezea England na hasa Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini zitakazoanza Juni 11, 2010.
Mwezi Januari, 2009, David Beckham alisaini mkataba wa miezi mitatu kuichezea AC Milan kwa mkopo na mkataba huo ukaongezwa hadi Ligi ya Serie A Italia ilipomalizika mwezi Mei, 2009 baada ya Beckham kuonyesha soka ya hali ya juu.
Kwa kuichezea AC Milan kwa kipindi hicho, Kocha Fabio Capello, ameendelea kumchukua Beckham kucheza Timu ya England.
LEO UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Tathmini ya Mechi
RATIBA: Jumanne, 3 Novemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
KUNDI A
Bayern Munich v Bordeaux,
Maccabi Haifa v Juventus,
KUNDI B
Manchester United v CSKA Moscow,
Besiktas v Wolfsburg,
KUNDI C
AC Milan v Real Madrid,
Marseille v FC Zurich,
KUNDI D
Apoel Nicosia v FC Porto,
Atletico Madrid v Chelsea
Kimbembe kwa Real Madrid!!!!!
Klabu za England, Chelsea na Manchester United, leo zinaweza kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele Raundi ifuatayo ya Mtoano wakishinda mechi zao za leo.
Chelsea wanasafiri hadi Spain kucheza na Atletico Madrid wakiwa tayari wameshashinda mechi zao zote 3 za kwanza za Kundi D na mechi ya mwisho waliyocheza kwao waliibamiza Atletico Madrid bao 4-0.
Kipigo hicho kiliifanya Atletico Madrid, ambayo imeanza vibaya mno msimu huu hata kwenye Ligi ya kwao, kumtimua Kocha Abel Resino na wakamteua Quique Sanchez Flores kuchukua nafasi yake.
Mpaka sasa Atletico Madrid wana pointi moja tu katika Kundi D.
Katika Kundi hilo, FC Porto ndio wenye nafasi nzuri kuungana na Chelsea kuingia Raundi ifuatayo baada ya kuifunga APOEL Nicosia 2-1 mechi iliyokwisha na leo wanarudiana huko Visiwa vya Cyprus.
Katika Kundi B, Manchester United, ambao walikuwa Mabingwa wa Ulaya mwaka 2008 na kutolewa Fainali 2009, wako kileleni kwa kushinda mechi zao zote 3, ya mwisho ikiwa ushindi wa 1-0 huko Moscow walipoidonyoa CSKA Moscow wanaokutana nao leo Old Trafford.
Nafasi ya Pili kwenye Kundi hili B bado haijapata ufumbuzi na inagombewa na Wolfsburg, CSKA na hata Besiktas.
Leo, Besiktas inaikaribisha Wolsburg na Timu hizi zilitoka suluhu 0-0 mechi ya mwisho.
Gumzo na macho ya wengi leo ni mechi ya Kundi C ya marudiano kati ya AC Milan na Real Madrid baada ya AC Milan kuifunga Real mechi ya mwisho huko Spain Uwanja wa nyumbani wa Real wa Santiago Bernabeu 3-2 huku Pato akifunga bao la ushindi dakika 2 kabla mpira kumalizika.
Real leo itamkosa Mchezaji wa bei mbaya Ronaldo alieumia lakini Kaka yupo na leo itakuwa mechi yake ya kwanza kurudi kucheza Uwanjani San Siro tangu aihame AC Milan na kujiunga Real msimu huu.
Katika mechi nyingine ya Kundi hili C ni kati ya Marseille na FC Zurich huku Timu zote mbili zikiwa na matumaini ya kusonga mbele endapo kigogo mmoja kati ya Real na AC Milan akitetereka.
Marseille walliishinda FC Zurich 1-0 mechi ya kwanza.
Leo, katika Kundi A, Bordeaux wakimudu kuwafunga Bayern Munich watatinga Raundi ya Pili. Katika mechi yao ya kwanza ambayo Bordeaux walikosa penalti mbili na Bayern kulambwa Kadi 2 Nyekundu, Bordeaux walishinda 2-1.
Juventus wako nafasi ya pili Kundi hili na leo wapo Israel kucheza na Maccabi Haifa ambao wamefungwa mechi zote kwenye Kundi lao.
Fergie ampa ‘Mzazi’ Rooney ofu!!!
Mkewe Coleen ajifungua Mtoto wa Kiume, apewa jina Kai!!!
Mshambuliaji Nyota wa Manchester United, Wayne Rooney, alipewa ofu ya kutofanya mazoezi hapo jana Jumatatu baada ya Mkewe, Coleen, kujifungua Mtoto wao kwanza wa Kiume aliepewa jina Kai.
Inasemekana Sir Alex Ferguson alikuwa na nia ya kumpumzisha Rooney mechi ya leo ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na CSKA Moscow ichezwayo Old Trafford ili awe freshi kwa mechi kali ya Ligi Kuu ya Jumapili watakayocheza huko Stamford Bridge na Chelsea lakini baadae akajumuishwa tena Kikosini baada ya Dimitar Berbatov kupata maumivu.
Hata hivyo baada ya Rooney kuwa Mzazi na Berbatov kupata afueni, Ferguson ameamua kumpumzisha Rooney na kumwacha aiangalie Familia yake iliyopata memba mpya.
Hivyo, Mafowadi Michael Owen, Berbatov na Chipukizi Federico huenda wawili kati yao wakacheza mechi ya leo na CSKA Moscow.
Kwa Owen hii ni mechi muhimu kwake kwani Meneja wa England Fabio Capello atakuwepo Old Trafford kuitazama na siku chache zijazo anatarajiwa kutangaza Kikosi cha England kitachocheza mechi ya kirafiki hapo Novemba 14 na Brazil huko Doha, Qatar.
Lakini mwenyewe Owen ameuponda umuhimu huo kwake kwa kutamka: “Nimechezea England mara 89 na ningependa kuichezea tena. Naweza kujiongezea nafasi ya kuchaguliwa England nikicheza vizuri Man U lakini sikosi usingizi kwa kutokuchaguliwa England! Ninachowaza tu ni kucheza vizuri Man U na yote mengine yatafuata baada ya hapo!”
Mechi ya KOMBE LA CARLING: Man City v Arsenal, Van Persie ataka kisasi!!!
Ingawa kawaida Meneja Arsene Wenger hutumia Vijana Chipukizi ili kuwapa uzoefu kwenye mechi za Kombe la Carling, mara baada ya kugundua kuwa Arsenal wamepangiwa Manchester City Robin Van Persie ameonyesha shauku kubwa ya kutaka kucheza mechi hiyo ili alipe kisasi.
Van Persie aligundua Arsenal wamepangiwa Man City mara baada ya mechi ya Arsenal na Tottenham ya Ligi Kuu siku ya Jumamosi ambayo Arsenal walishinda 3-0 na yeye Van Persie kufunga bao 2.
Mara baada ya mechi hiyo, Van Persie aliuliza: “Droo ya Carling vipi? Ni Man City? Nataka kucheza!”
Usongo wa Van Persie na mechi hiyo na Man City umekuja hasa baada ya Arsenal kufungwa 4-2 na Timu hiyo kwenye mechi ya Ligi Kuu ambayo Mchezaji mwenzake wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Adebayor, ambae sasa anachezea Man City kumtimba kwa makusudi, kosa ambalo lilimfanya afungiwe mechi 3 na FA ingawa Refa hakuona kitendo hicho.
Adebayor vilevile alipigwa faini kwa kitendo chake cha kuwakebehi Mashabiki wa Arsenal alipokwenda kushangilia mbele yao mara baada ya kuifungia Man City bao katika mechi hiyo hiyo.
Van Persie amekuwa akidai kitendo cha Adebayor kilikuwa cha makusudi na kibaya sana.
Fergie awaomba Mashabiki wa Man U waache nyimbo za kashfa kwa Wenger
Arsene Wenger hukumbwa na nyimbo za Mashabiki za kumkejeli kila Uwanja wa ugenini anaoenda kucheza na Timu yake Arsenal lakini aendapo Old Trafford, nyumbani kwa Manchester United, hukumbana na nyimbo za kashfa na mojawapo ikiwa ile inayomtuhumu kubaka watoto wadogo.
Hali hiyo imemkera Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, na sasa ameamua kuandika barua ya wazi kwa Mashabiki hao wanaoimba nyimbo hizo ili waache tabia hiyo.
Ferguson pia amewataka Walinzi wa Uwanjani wa Old Trafford pamoja na Polisi kuchunguza ili kuwabaini viongozi wanaohamasisha nyimbo hizo ili wapigwe marufuku kuingia uwanjani na vile vile kushitakiwa.

Monday 2 November 2009

Shabiki alievaa kama Kondoo apigwa kibiriti, wenzake wammwagia Bia kuuzima moto huo!!!
Shabiki mwenye umri wa miaka 24 ambae alivaa mavazi kama Kondoo alichomwa moto na kuunguzwa vibaya mikononi na miguuni ndani ya Treni wakati yeye na wenzake wakitoka kuishangilia Timu yao Aberdeen iliyokuwa ikicheza na Hibs mjini Edinburgh huko Scotland.
Baada ya mtu huyo kulipuliwa moto na huku akikimbia ndani ya Treni hiyo iliyokuwa ikisafiri kati ya Edinburgh na Aberdeen, Mashabiki wenzake walimmwagia Bia ili kujaribu kuuzima moto huo.
Polisi inamshikilia mtu mmoja kwa tukio hilo.
Carragher: “Inauma!!!”
Jamie Carragher amekiri kuwa Liverpool wanaumia sana kwa vipigo mfululizo lakini amewataka Wachezaji wenzake wasife moyo.
Carragher Jumamosi alipewa Kadi Nyekundu katika kipigo cha bao 3-1 walichopewa na Fulham kwenye Ligi Kuu na kuwafanya wawe wamefungwa mechi 6 katika 7 walizocheza mwisho.
Liverpool sasa wako pointi 9 nyuma ya vinara Chelsea na pointi 7 nyuma ya Mahasimu wao Manchester United ambao wako nafasi ya pili.
Mbali ya kuwa nafasi mbaya kwenye Ligi na kupokea vipigo vitano kati mechi 11 za Ligi walizocheza, Liverpool Jumatano iliyopita walibwagwa nje ya Kombe la Ligi baada ya kufungwa 2-1 na Arsenal na hali hii imemfanya Meneja wao Rafa Benitez kukalia kuti kavu.
Jumatano hii Liverpool wana kibarua kikubwa huko Ufaransa watakapokutana na Lyon kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE, timu ambayo iliifunga Liverpool 2-1 nyumbani kwake Anfield.
Kipigo kingine toka kwa Lyon kutaifanya Liverpool iwe nje ya Kombe hilo la Ulaya na pengine kuwa ndio msumari wa mwisho kwa Benitez.
Faraja pekee kwa Liverpool ni ule ushindi wa 2-0 walioupata baada ya kuwafunga Manchester United lakini hilo pia halimpi moyo Jamie Carragher ambae amesema: “Ni wakati mgumu kwetu na tunaumia sana! Tuliibuka tulipoifunga Man U lakini sasa tumepigwa mechi 2 mfululizo!! Ni sisi Wachezaji pekee ndio tunaweza kuibadili hali hii!”
Birmingham 0 Manchester City 0
Manchester City inabidi impe pongezi Kipa wao Shay Given kwa kuokoa penalti na kuwafanya watoke suluhu 0-0 na Birmingham Uwanjani Mtakatifu Andrea Mjini Birmingham katika mechi pekee ya Ligi Kuu England iliyochezwa jana.
Hii ni mechi ya 4 mfululizo kwa Man City kutoka suluhu kwenye Ligi Kuu.
Birmingham walitawala mechi hii lakini walishindwa kutumia nafasi zao na mwisho walimaliza wakiwa Wachezaji 10 baada ya Barry Ferguson kupewa Kadi mbili za Njano na hivyo kuonyeshwa Nyekundu.
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
Timu zilizoingia Raundi ya Pili zakamilika!!
MATOKEO MECHI ZA JANA Novemba 1:
KUNDI E
Malawi 1 Spain 4
USA 1 United Arab Emirates 0
KUNDI F
Korea Republic 2 Algeria 0
Italy 0 Uruguay 0
Spain na USA zimeshika nafasi za juu za KUNDI E na hivyo kuingia Raundi ya Pili na katika KUNDI F ni Italy na Korea ndizo zimesonga mbele.
Timu zilizofuzu kuingia Raundi ya Pili kwa tiketi ya kuwa nafasi ya 3 bora ni Uruguay, UAE, Germany na New Zealand.
Lakini UAE ndio wenye bahati kubwa sana kwani walikuwa wamefungana kila kitu, pointi na magoli, na Brazil na Uholanzi hivyo wakapata nafasi tu ya kusonga mbele kwa sababu tu walipata Kadi moja chache kupita Brazil na Uholanzi.
RATIBA RAUNDI YA PILI:
Novemba 4:
Argentina v Colombia
Turkey v UAE
Switzerland v Germany
Italy v USA
Novemba 5:
Spain v Burkina Faso
Iran v Uruguay
Mexico v South Korea
Nigeria v New Zealand

Sunday 1 November 2009

UHONDO WA KANDANDA WIKI INAYOKUJA!!!
RATIBA: [saa za bongo]
LIGI KUU ENGLAND:
Jumatano, 4 Novemba 2009
[saa 5 usiku]
West Ham v Aston Villa
Jumamosi, 7 Novemba 2009
[saa 12 jioni]
Aston Villa v Bolton
Blackburn v Portsmouth
Man City v Burnley
Tottenham v Sunderland
Wolverhampton v Arsenal
[saa 1 na nusu usiku]
Jumapili, 8 Novemba 2009
[saa 10 na nusu jioni]
Hull v Stoke
[saa 12 jioni]
West Ham v Everton
Wigan v Fulham
[saa 1 usiku]
Chelsea v Man U
Jumatatu, 9 Novemba 2009
[saa 5 usiku]
Liverpool v Birmingham
UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
Jumanne, 3 Novemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
AC Milan v Real Madrid,
Apoel Nicosia v FC Porto,
Atletico Madrid v Chelsea
Bayern Munich v Bordeaux,
Besiktas v Wolfsburg,
Maccabi Haifa v Juventus,
Manchester United v CSKA Moscow,
Marseille v FC Zurich,
Jumatano, 4 Novemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
Arsenal v AZ Alkmaar,
Dynamo Kiev v Inter Milan,
Fiorentina v Debrecen,
Lyon v Liverpool,
Rubin Kazan v Barcelona,
Sevilla v VfB Stuttgart,
Standard Liege v Olympiakos,
Unirea Urziceni v Rangers
EUROPA LIGI:
Alhamisi, 5 Novemba 2009
RATIBA TUTAILETA BAADAE
Sasa Benitez alia na Refa!!!
Ni kipigo cha 5 katika mechi 11 za Ligi, kipigo cha 6 katika mechi zao 7 za mwisho!!!
Kipigo cha 3-1 kutoka kwa Fulham walichokipata Liverpool jana ni kipigo chao cha 5 katika mechi 11 za Ligi Kuu walizocheza msimu huu na katika mechi zao zote 7 za mwisho walizocheza wamefungwa mechi 6 katika hizo 7.
Mbali ya kipigo cha jana, Liverpool pia walimaliza mechi hiyo wakiwa mtu 9 tu baada ya Wachezaji wao Philipp Degen na Jamie Carragher kupewa Kadi Nyekundu na Refa Lee Mason aliechezesha jana.
Sasa Meneja wa Liverpool, Rafa Benitez, amemjia juu Refa Lee Mason na kudai Refa huyo hakupaswa kuwapa Wachezaji wake Kadi Nyekundu.
Benitez amesema: “ Degen alipaswa kupewa Kadi ya Njano na si Nyekundu! Na Carragher aliucheza mpira kwa hiyo tutakata rufaa kwa hilo!”
Hata hivyo, baadhi ya Mashabiki wa Liverpool wamekerwa na Benitez kwa uamuzi wa kuwatoa na kuwabadilisha Wachezaji wao Nyota Fernando Torres, Yossi Benayoun na Dirk Kuyt huku mechi ikiwa 1-1.
Jumatano Liverpool wanakabiliwa na mechi ngumu ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ya ugenini na Lyon ambayo iliifunga Liverpool kwake Anfield na sasa inabidi Liverpool ashinde mechi hiyo ili afufue matumaini ya kuendelea kwenye Mashindano hayo.
Endapo Liverpool atafungwa mechi hiyo bila shaka atatupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
Iran, Colombia, Turkey na Burkina Faso zaingia Raundi ya Pili
Katika KUNDI C, Iran na Colombia zimemaliza nafasi ya kwanza na ya pili na zimeingia Raundi ya Pili huku Uholanzi ikisubiri kujua kama iatapata nafasi hiyo kama Mshindi wa 3.
Kwenye KUNDI D ni Turkey na Burkina Faso ndizo zimefuzu huku New Zealand ikusubiria nafasi ya 3.
MATOKEO MECHI Jumamosi, Oktoba 31:
KUNDI C
Gambia 2 v Colombia 2
Netherlands 0 v Iran 1
KUNDI D
Burkina Faso 4 v Costa Rica 1
New Zealand 1 v Turkey 1
RATIBA MECHI ZA LEO Novemba 1:
KUNDI E
Malawi v Spain
UAE v USA
KUNDI F
Korea Republic v Algeria
Italy v Uruguay
Powered By Blogger