Tuesday 3 November 2009

Fergie ampa ‘Mzazi’ Rooney ofu!!!
Mkewe Coleen ajifungua Mtoto wa Kiume, apewa jina Kai!!!
Mshambuliaji Nyota wa Manchester United, Wayne Rooney, alipewa ofu ya kutofanya mazoezi hapo jana Jumatatu baada ya Mkewe, Coleen, kujifungua Mtoto wao kwanza wa Kiume aliepewa jina Kai.
Inasemekana Sir Alex Ferguson alikuwa na nia ya kumpumzisha Rooney mechi ya leo ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na CSKA Moscow ichezwayo Old Trafford ili awe freshi kwa mechi kali ya Ligi Kuu ya Jumapili watakayocheza huko Stamford Bridge na Chelsea lakini baadae akajumuishwa tena Kikosini baada ya Dimitar Berbatov kupata maumivu.
Hata hivyo baada ya Rooney kuwa Mzazi na Berbatov kupata afueni, Ferguson ameamua kumpumzisha Rooney na kumwacha aiangalie Familia yake iliyopata memba mpya.
Hivyo, Mafowadi Michael Owen, Berbatov na Chipukizi Federico huenda wawili kati yao wakacheza mechi ya leo na CSKA Moscow.
Kwa Owen hii ni mechi muhimu kwake kwani Meneja wa England Fabio Capello atakuwepo Old Trafford kuitazama na siku chache zijazo anatarajiwa kutangaza Kikosi cha England kitachocheza mechi ya kirafiki hapo Novemba 14 na Brazil huko Doha, Qatar.
Lakini mwenyewe Owen ameuponda umuhimu huo kwake kwa kutamka: “Nimechezea England mara 89 na ningependa kuichezea tena. Naweza kujiongezea nafasi ya kuchaguliwa England nikicheza vizuri Man U lakini sikosi usingizi kwa kutokuchaguliwa England! Ninachowaza tu ni kucheza vizuri Man U na yote mengine yatafuata baada ya hapo!”

No comments:

Powered By Blogger