Wednesday 4 November 2009

Chelsea na Man U zatinga Raundi ya Mtoano UEFA CHAMPIONS LEAGUE!!
Baada ya Chelsea kutoka sare 2-2 na Atletico Madrid huko Spain na Manchester United kutoka suluhu 3-3 na CSKA Moscow, Timu hizi mbili zimesonga mbele kuingia Raundi inayofuata ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ya Mtoano itakayokuwa na Timu 16 huku zikiwa zimebakiza mechi 2 katika Makundi yao.
Timu nyingine zilizofuzu jana kusonga mbele ni FC Porto ambayo ipo Kundi la Chelsea na Bordeaux iliyo Kundi A.
Ferguson awataka UEFA wafute Kadi ya Fletcher!!!
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amewataka UEFA waifute Kadi ya Njano aliyopewa Darren Fletcher kwa kile Refa alichodhani kajiangusha ndani ya boksi ili apate penalti katika mechi ya jana ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE iliyochezwa Old Trafford na CSKA Moscow na kumalizika 3-3.
Huku mechi ikiwa 3-1 kwa CSKA kuwa mbele, Aleksei Berezutski alimkwatua Fletcher aliekuwa anaenda kufunga na Refa Olegário Benquerença kutoka Ureno akampa Fletcher Kadi ya Njano kitendo ambacho Ferguson amekiita kibovu katika miaka yake 50 ya soka.
UEFA hawaruhusu Timu kukata rufaa kuhusu Kadi za Njano labda Refa ampe Mchezaji Kadi kwa makosa yaani Mchezaji ambae hana hatia apewe Kadi badala ya mwingine aliecheza rafu.
Msimu uliokwisha Fletcher alikosa kucheza Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Barcelona baada ya kupewa Kadi kwenye Nusu Fainali Man U walipocheza na Arsenal.

No comments:

Powered By Blogger