Thursday 5 November 2009

Kroenke anyemelea kuichukua Arsenal!!
Bilionea Mmarekani, Stan Kroenke, ambae pia ni Mkurugenzi kwenye Bodi ya Arsenal, amezidi kunyemelea kuiteka Arsenal baada ya kuongeza Hisa zake kufikia asilimia 29.9 toka 29.6 alizokuwa nazo majuzi.
Kroenke, ambae ni Mmilikiwa wa Timu ya Vikapu ya NBA huko Marekani ya Denver Nuggets na ile ya Soka inayocheza Ligi ya MLS, Colorado Rapids, atalazimika kutoa ofa ya kununua Hisa zote hapo Arsenal akifikisha Hisa asilimia 29.99.
Mpaka sasa Kroenke hajasema lolote nini anakitaka hapo Arsenal na amebatizwa jina ‘Silent Stan” yaani ‘Stan Mkimya’.
LIGI KUU: West Ham 2 Aston Villa 1
Katika mechi pekee ya Ligi Kuu iliyochezwa Jumatano Novemba 4, West Ham waliibuka washindi kwa mabao 2-1 nyumbani Uptown Park dhidi ya Timu ngumu Aston Villa.
Mchezaji alieingizwa kutoka benchi la akiba, Zavon Hines, ndie aliewafungia West Ham bao la pili na la ushindi dakika ya 90.
Mark Noble aliipatia West Ham bao la kwanza kwa penalti dakika ya 45 baada ya Habib Beye kucheza rafu iliyoonekana na Refa Steve Bennett.
Kipindi cha pili dakika ya 49 Refa Steve Bennett aliwapa penalti Aston Villa alipoamua Manual Da Costa wa West Ham alicheza faulo lakini penalti hiyo iliyopigwa na Ashley Young iliokolewa na Kipa Robert Green.
Ashley Young alirekebisha makosa yake kwa kuisawazishia Villa dakika ya 52.
Beye alipewa Kadi ya Pili ya Njano na hivyo kupata Nyekundu dakika ya 84 na kuwaacha Villa wakiwa mtu 10.
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
Colombia, Italy, Turkey na Uswisi zipo ROBO FAINALI!!!
MATOKEO Novemba 4:
Argentina 2 Colombia 3
Italy 2 USA 1
Turkey 2 UAE 0
Uswisi 4 Germany 3
Baada ya kuwatoa Argentina 3-2, Colombia wameingia Robo Fainali na watakutana na Turkey waliowafunga UAE 2-0.
Nao Uswisi watacheza na Italy Robo Fainali baada ya Uswisi kuitoa Ujerumani 4-3 na Italy kuibwaga USA 2-1
Ratiba ya mechi za leo za RAUNDI YA PILI:
Novemba 5:
Spain v Burkina Faso
Iran v Uruguay
Mexico v South Korea
Nigeria v New Zealand
UEFA CHAMPIONS LIGI: Taarifa ya Mechi za Jumatano Novemba 4
Liverpool njia panda!!! Arsenal kidedea!!!
Lyon na Sevilla zasonga mbele Raundi ya Mtoano!!
Liverpool wamejiweka kwenye hali ngumu mno kwa kutoka sare 1-1 na Lyon hapo jana na sasa ili wasonge mbele kwenye Mashindano hayo ni lazima washinde mechi zao mbili zilizobaki na pia waombe Fiorentina wafungwe.
Wakati Liverpool wapo mashakani kwa Arsenal mambo ni mdundo baada ya kuichapa AZ Alkmaar mabao 4-1 na kwa kila hali wanategemewa kuingia Raundi ijayo.
Ripoti kwa kila Kundi:
KUNDI F:
Msimamo:
-Inter Milan pointi 6
-Rubin Kazan pointi 5
-Barcelona pointi 5
-Dynamo Kiev pointi 4
Inter Milan walifunga goli mbili katika dakika 4 za mwisho na kuibuka washindi kwa bao 2-1 dhidi ya Dynamo Kiev na hivyo kuchukua uongozi wa Kundi hili.
Katika mechi nyingine ya Kundi hili iliyochezwa mapema, Rubin Kazan walitoka sare 0-0 na Mabingwa Watetezi Barcelona.
KUNDI E:
Msimamo:
-Lyon pointi 10
-Fiorentina pointi 9
-Liverpool pointi 4
-Debrecen 0
Lyon walisawazisha dakika ya 90 kupitia Lisandro baada ya Liverpool kupata bao la uongozi kupitia Babel na hivyo kuifanya Liverpool iwe mashakani kusonga mbele kwani Fiorentina waliichapa Debrecen mabao 5-2.
Endapo katika mechi ijayo Liverpool atashindwa kuwafunga Debrcen, Liverpool watakuwa nje ya Mashindano.
Na hata wakiwafunga Debrecen na huku Fiorentina wawafunge Lyon, basi Leverpool nje!
KUNDI H:
Msimao:
-Arsenal pointi 10
-Olympiacos pointi 6
-Standard Liege pointi 4
-AZ Alkmaara pointi 2
Licha ya Arsenal kuifunga AZ Alkmaar mabao 4-1 bado uhakika wa kusonga mbele haujathibitika baada ya Standard Liege kuifunga Olympiacos 2-0.
KUNDI G:
Msimamo:
-Sevilla pointi 10
-Unirea Urziceni pointi 5
-Stuttgart pointi 3
-Rangers pointi 2
Sevilla walitoka suluhu 1-1 na Stuttgart na kutinga Raundi inayofuata ya Timu 16 ya Mtoano.
Katika mechi nyingine, Rangers ya Scotland na Unirea Urziceni zilitoka sare 1-1.
MECHI ZIJAZO ZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
Jumanne, Novemba 24:
KUNDI E
Debrecen v Liverpool
Fiorentina v Lyon
KUNDI F
Barcelona v Inter Milan
Rubin Kazan v Dynamo Kiev
KUNDI G
Rangers v Stuttgart
Unirea Urziceni v Sevilla
KUNDI H
AZ Alkmaar v Olympiacos
Arsenal v Standard Liege
Jumatano, Novemba 25:
KUNDI B
Manchester United v Besiktas
CSKA MOSCOW V Wolfsburg
KUNDI A
Bordeaux v Juventus
Bayern Munich v Maccabi Haifa
KUNDI C
Real Madrid v FC Zurich
AC Milan v Marseille
KUNDI D
FC Porto v Chelsea
Apoel Cyprus v Atletico Madrid

No comments:

Powered By Blogger