Sunday 1 November 2009

Sasa Benitez alia na Refa!!!
Ni kipigo cha 5 katika mechi 11 za Ligi, kipigo cha 6 katika mechi zao 7 za mwisho!!!
Kipigo cha 3-1 kutoka kwa Fulham walichokipata Liverpool jana ni kipigo chao cha 5 katika mechi 11 za Ligi Kuu walizocheza msimu huu na katika mechi zao zote 7 za mwisho walizocheza wamefungwa mechi 6 katika hizo 7.
Mbali ya kipigo cha jana, Liverpool pia walimaliza mechi hiyo wakiwa mtu 9 tu baada ya Wachezaji wao Philipp Degen na Jamie Carragher kupewa Kadi Nyekundu na Refa Lee Mason aliechezesha jana.
Sasa Meneja wa Liverpool, Rafa Benitez, amemjia juu Refa Lee Mason na kudai Refa huyo hakupaswa kuwapa Wachezaji wake Kadi Nyekundu.
Benitez amesema: “ Degen alipaswa kupewa Kadi ya Njano na si Nyekundu! Na Carragher aliucheza mpira kwa hiyo tutakata rufaa kwa hilo!”
Hata hivyo, baadhi ya Mashabiki wa Liverpool wamekerwa na Benitez kwa uamuzi wa kuwatoa na kuwabadilisha Wachezaji wao Nyota Fernando Torres, Yossi Benayoun na Dirk Kuyt huku mechi ikiwa 1-1.
Jumatano Liverpool wanakabiliwa na mechi ngumu ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ya ugenini na Lyon ambayo iliifunga Liverpool kwake Anfield na sasa inabidi Liverpool ashinde mechi hiyo ili afufue matumaini ya kuendelea kwenye Mashindano hayo.
Endapo Liverpool atafungwa mechi hiyo bila shaka atatupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

No comments:

Powered By Blogger