Tuesday 3 November 2009

REFA KUJICHANGANYA NA MAPACHA WA MAN U: FA yaamua Kadi ihamishwe apewe Rafael!!!

Chama cha Soka cha England,FA, katika hatua inayoendeleza utata, imeamua kuishughulikia rufaa ya Manchester United kuhusu kosa la Refa
Chris Foy kumpa kimakosa Fabio da Silva Kadi ya Njano kwa kusema Kadi hiyo atabandikwa Nduguye Pacha mwenzake Rafael da Silva ambae ndie alicheza rafu.
Utata huo ulitokea kwenye mechi ya Kombe la Carling kati ya Barnsley na Manchester United ambayo Man U walishinda 2-0 na Mapacha hao wawili kuonekana wakimkabili Jamal Campbell-Ryce wa Barnsley kwenye dakika ya 83 na Rafael kucheza faulo ambayo Refa Chris Foy alimpa Kadi ya Njano Fabio.
Mapacha hao, Rafael na Fabio wenye umri wa miaka 19, wamefanana mno kiasi ambacho hata Meneja wao wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amekiri kuwa hata yeye anaweza kuwatenganisha tu kwa sababu Fabio huvaa pete ya ndoa kidoleni mwake.
Uamuzi huu wa FA umewashangaza Wadau kwani sheria na taratibu za Soka zinasema endapo Refa atakosea na kumpa Kadi Mchezaji kimakosa basi Kadi hiyo hufutwa.
Lakini uamuzi huo wa FA ambao umeenda mbele na kuihamisha Kadi hiyo kwa Mchezaji mwingine unaonekana ni kitu kipya.
Manchester United bado haijasema lolote kuhusu uamuzi huu wa kushangaza wa FA.

No comments:

Powered By Blogger